Haki za Wazazi Wawili
Haki za wazazi wawili (Kiarabu: حق الوالدين) Ni zile haki wanazostahiki kupewa baba na mama kutoka kwa watoto wao. Kuzingatia na kuchunga haki hizi kumetajwa kuwa ni miongoni mwa maagizo muhimu ya Mwenye Ezi Mungu, na kwamba baada ya haki ya Mwenye Ezi Mungu kwa waja wake, haki za wazazi ndiyo haki zinazo chukuliwa katika nafasi ya pili juu ya shingo za watoto.
Miongoni mwa haki za baba na mama kwa watoto wao zilizotajwa katika vyanzo vya kidini, ni; kuwafanyia hisani, kuwaheshimu na kuwatii wazazi na kukidhi mahitaji yao ya kifedha. Katika Qur'ani, baada ya Mwenye Ezi Mungu kutoa amri ya kuwafanyia hisani wazazi wawili, pia watoto wanahimizwa si tu kuepuka ukosefu wa adabu na kuto watolea ukali baba na mama hata kwa kiwango kidogo kabisa, bali pia wanahimizwa kuwa wanyenyekevu kwao katika uhai wao, na kuwaombea dua baada ya kufariki kwao. Katika hadithi za Maimamu watoharifu, imeelezwa kwamba; kuwa mwema kitabia mbele ya baba na mama, ni moja wapo ya vitendo bora zaidi na vinavyo pendwa zaidi mbele ya Mwenye Ezi Mungu, na miongoni mwa sifa muhimu za Mashia.
Mafaqihi wanalichukulia suala hili la kuwatii baba na mama, kuwa ni wajibu katika hali ambayo kutotii kwao kutaweza kuwasababishia dhara au maudhi; isipokuwa katika hali ambayo wazazi hao watawaamuru watoto wao kutenda dhambi. Pia, kulingana na fatwa zao, ni wajibu wa mtoto kuhakikisha kuwa anatoa mahitaji ya baba na mama yaliyohitajika katika maisha yao ya kila siku, ikiwa atakuwa na uwezo kufanya hivyo.
Umuhimu na Nafasi ya Haki za Wazazi Wawili
Kuheshimu na kuchunga haki za wazazi ni mojawapo ya amri muhimu za kiungu zilizotajwa ndani ya vyanzo mbali mbali,[1] na baada ya haki ya Mwenyezi Mungu, haki hizo zimekuwa zikichukuliwa kama ndio haki kubwa zaidi zinazo wakabili mtoto kutoka kwa Mola wao.[2] Kutenda wema na kuwa na hisani mbele ya wazazi, ni miongoni mwa haki za baba na mama zilizzoko juu ya shingo za watoto,[3] ambazo zimekuwa zikisisitizwa mara kwa mara ndani ya Qur'ani.[4] Ukariri wa maagizo haya, hasa baada ya amri ya kumuabudu Mwenye Ezi Mungu na kuachana na ushirikina[5], ni ishara ya umuhimu maalum yaliopewa mafundisho na maadili haya ya kidini.[6]
Hadhi ya wazazi wawili, ni suala lililosisitizwa mno kwenye vyanzo vya Hadithi vya Kishia pamoja na Kisunni, na limetengwa milango katika kulijadili suala hilo.[7] Na kutokuheshimu au kutotii wazazi kumeharamishwa na kukahesabiwa kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa vyanzoni humo.[8] Pia umuhimu wa kuheshimu wazazi umetajwa katika vitabu vyengine kadhaa vya dini, kikiwemo kitabu cha Wakiristo kiitwacho Agano la Kale.[9]
Wazazi Wawili Wana Haki Mbele ya Watoto Wao?
Kuna haki kadhaa katika vyanzo vya kidini kuhusiana na wazazi wawili, zikiwemo; kuwanyia hisani, kuheshimu,[10] kuwatii[11] na kuwapatia mahitaji yao ya kifedha.</ref> kuwatii[12]
Hisani na Heshima
- Makala Asili: Kuwatendea Wema Wazazi Wawili
Miongoni mwa haki za wazazi ni kuwapa heshima na kuwa na pendo juu ya wazazi wawili.[13] Sheikh Hurru Amili katika kitabu chake kinachoitwa Wasa’ilu al-Shi’a, ametenga mlango maalumu kuhusiana na haki za wazazi wawili, mlango ambao ndani yake kuna Hadithi kadhaa zinazohusiana na wena na hisani kwa wazazi wawili.[14]
Katika hadithi za Maimamu wa Kishia imeelezwa kwamba; tabia njema kwa baba na mama ni miongoni mwa vitendo bora zaidi[15] vinavyopendwa na Mwenye Ezi Mungu,[16] na ni moja ya sifa kuu za Mashia.[17] Pia, ridhaa na ghadhabu za Mwenye Ezi Mungu zinafungamana na ridhaa na kutokuridhika kwao juu ya matendo au tabia za watoto wao,[18] na hakuna udhuru wowote unaokubalika mbele ya Allah katika kutowapa fadhila baba na mama.[19]
Kuhusiana na maisha ya bwana Mtume (s.a.w.w), imeelezwa kwamba; yeye alikuwa akimheshimu sana mama yake aliye mnyonyesha,[20] na aliwaheshimu wale waot waliokuwa wakiwafanyia wema wazazi wao.[21] Kwa msingi huu, Waislamu wameamrishwa kuwatendea wema wazazi wao, na kuvumilia ugumu wa kuwahudumia,[22] hata kama wazazi hao ni washirikina[23] au ni watenda dhambi.[24]
Mifano Hai ya Utendaji Hisani
Katika Aya za 23 na 24 za Suratu Al-Israa, baada ya kutolewa amri ya kuwafanyia wema wazazi wawili, Mwenye Ezi Mungu ametoa baadhi ya mifano ya suala hilo, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kuwatamkia neno “uf” (kuwagutia) na kutowaonyesha au kuwakabili kwa sura ya ghadhabu.[25] Katika Aya inayofuata, watoto wanahimizwa kuwa waungwana mbele ya wazazi wao hali wakiwa katika kipindi cha maisha ya uzeeni, na si tu kuepuka tabia mbaya dhidi yao, bali pia kuwa wanyenyekevu kwao na kuwaombea dua katika maisha yao ya hapa duniani na baada ya kifo chao, kutokana na shida walizopitia wazazi hao katika kuwalea na kuwatunza watoto wao.[26]
Pia Katika Hadithi kuna orodha ya mifano kuhusiana na haki za wazazi; ikiwemo; kutowaita wazazi kwa kutumia majina yao halisi, kuto watangulia katika matembezi ya njiani, na kutokaa kwa mfumo ambao mgongo wako uakuwa umekabiliana na nyaso zao (kuto wapa mgongo).[27] Aidha, iwapo wazai watamuelekezwa wito, basi anatakiwa ajibu kwa haraka bila kuchelewa, hata kama atakuwa yuko katika sala,[28] na ikiwa tabia na maneno yao yanapingana na awapendayo, basi anatakiwa ajiepushe na kukasirika au kuwatusi wazazi wake.[29] Kuhifadhi faragha ya baba na mama[30] na kuwashukuru wazazi hao,[31] ni mifano mingine ya ukarimu na hisani kwa wazazi.
Kuwatii na Kuwahudumia Kimaisha
Kuwatii wazazi wawili ni moja wapo ya haki za wazee,[32] isipokuwa tu iwapo wao watamtaka mtoto wao kutenda matendo ya kumshirikisha Mwenye Ezi Mungu au kutenda dhambi.[33] Katika Hadithi za Maimamu watoharifu, imeelezwa kwamba; kuwatii wazazi wawili ni miongoni mwa ishara za imani[34] na ishara ya mtu kuwa na busara na nyenendo za kihekima.[35]
Kwa mujibu wa maelezo ya Mirza Qummi ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa Kishia, sulala la kuwatii wazazi -katika baadhi ya mambo- ni jambo lenye mawafikiano baina ya wanazuoni.[36] Yeye anapinga na hajuzishi mtoto fulani kutenda vitendo vya mubahu (vilivyo nyamaziwa na sheria), ambavyo wazazi wake hawakubaliani navyo, isipokuwa tu kama kutofanya hivyo kutamdhuru mtoto huyo.[37] Baadhi ya wanazuoni kama vile Sahibu al-Jawahiri, Sayyid Muhsin Hakim, na Nasir Makarim Shirazi pia no wanaamini kuwa utii kwa wazazi wiwili unahusiana na hali ambapo uasi wa mtoto unaweza kuwasababishia madhara kwa wazazi wake.[38]
Miongoni mwa haki nyingine za wazazi ni kuhakikisha mahitaji yao ya kifedha yanazingatiwa.[39] Kulingana na wanazuoni ni kwamba; ikiwa baba na mama wanahitaji msaada, basi ni wajibu wa mtoto kuwatimizia mahitaji yao, ikiwa mtoto huyo atakuwa ana uwezo wa kusaidia katika kugharamia mahitaji yao.[40] Aidha, katika baadhi ya Aya za Qur'ani,[41] watoto wanashauriwa kuzingatia sehemu ya wazazi wao katika usia wautoao kuhusiana na urithi wa mali watakazo acha watoto hao, iwapo watafariki kabla ya wazazi wao, na wanausiwa kutumia mali zao katika kuwasaidia baba na mama.[42]
Haki za Wazazi Baada ya Kufariki Kwao
Katika vyanzo vya kidini, kuna maagizo kadhaa yanayo waagiza watoto kuwatendea wema wazazi wao baada ya kufariki kwao;[43] miongoni mwa mambo hayo ni kusoma Qur'ani kwa niaba yao, kuwaombea msamaha, kuwaombea dua wazazi wao wawili, kuwatolea sadaka, kulipa madeni yao ya kifedha pamoja na madeni yanayo husiana na majukumu mengine (kama vile sala na saumu), kuwaheshimu marafiki wa wazazi wao na kuendeleza mahusiano mema na jamaa zao,[44] pamoja na kutekelezea ibada, kama vile kusali, kufunga na kuhiji kwa niaba ya yao.[45]
Katika vitabu vya fiqhi, imeelezwa kwamba; ni wajibu kwa mwana mkubwa kutekeleza ibada za sala na saumu zilizo achwa na baba yake.[46] Baadhi ya mafaqihi, kama vile Khamenei, Makarim Shirazi, na Noori Hamedani, wameona kuwa hata mama pia ni miongoni mwa wanaostahiki hukumu hii.[47] Katika Sahifa Sajjadiyya, kuna dua maalumu liyo orodhesha majukumu ya mtoto kwa wazazi wake.[48]
Sababu ya Kusisitizwa Suala la Kuchunga Haki za Wazazi Wawili
Allama Tabataba’i akielezea sababu ya Qur’ani kusisitiza juu ya wema kwa wazazi wawili anasema kwamba; uhusiano wa kihisia kati ya wazazi na watoto husababisha kuunganisha vizazi vipya na vizazi vilivyopita na hivyo kuimarisha familia. Uimara wa familia pia ni moja ya mambo muhimu katika mahusiano ya kijamii, na husababisha uthabiti wa jamii ya wanadamu.[49]
Ibn Maskawayhi (aliye ishi kati ya mwaka 320 na 420 Hijiria) alikuwa mwanazuoni wa Shia ambaye alichunguza kwa nini katika mafundisho ya kidini, watu wanahimizwa kuwafanyia wema wazazi wao na kuheshimu haki zao, lakini hakuna agizo kama hilo kwa wazazi kuhusu watoto wao? Aliibuba na imani ya kwamba; sababu ya hilo, inatokana na wazazi kutowaona mtoto wao kua ni kitu tofauti na wao wenyewe. Jambao ambalo linawapelekea wao kuwapenda watoto wao kama wanavyojipenda wao wenyewe, huku wakihisi kwamba maendeleo ya watoto wao ni sawa na maendeleo yao wenyewe; lakini watoto wao huwa hawana hisia kama hizo kwa wazazi wao.[50]
Mazingatio Makubwa Zaidi Juu ya Haki za Mama
Katika Hadithi, mama ameangaliwa kwa uangalizi wenye masisitizo maalumu kabisa[51] naye anahisabiwa kuwa mzazi mwenye haki kubwa zaidi mbele ya wanawe;[52] kwa kadiri ya kwamba hakuna mtu awezaye kutimiza haki ya mama yake.[53] Katika moja ya Hadithi, zilizopokewa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) imeelezwa kwamba; kumtendea mema yako ni kafara ya madhambi zako ulizozitanguliza.[54]
Katika Aya ya 15 ya Surat Al-Ahqaf, baada ya kusisitiza juu ya wema kwa wazazi wawili na kueleza falsafa yake, ni tu juhudi za mama zilizotajwa ndani ya hitimisho la Aya hiyo. Kulingana na wanazuoni wa Kiislamu, hii inasisitiza nafsi ya mama na kutoa maagizo zaidi katika juu ya haki zake kwa wanawe.[55] Imamu Sajjad (a.s) katika Risalat al-Huquq ameelezea ugumu anaopata mama na uvumilivu katika wakati wa ujauzito wake, na uvumilivu wake juu ya ugumu wa shida za wakati wa utotoni mwa watoto wake, na akawahimiza watoto kutambua thamani ya juhudi za mama zao.[56]
Masuala Yanayofungamana
Rejea
- ↑ Sepah-e Pasdaran, Ma'arif Quran, juz. 2, uk. 78.
- ↑ Rashid Ridha, Tafsir al-Manar, juz. 8, uk. 186; Fadhlullah, Min Wahyi al-Qur'an, juz. 7, uk. 259.
- ↑ Abu al-Sa'ud, Tafsir Abi al-Sa'ud, 1983, juz. 3, uk. 198.
- ↑ Tazama: Qur'an: Surat al-Ankabut: Aya ya 8; Surat al-Ahqaf: Aya ya 15.
- ↑ Qur'an: Surat al-Baqarah: Aya ya 83; Surat An-Nisa: Aya ya 36; Surat al-An'am: Aya ya 151; Surat al-Isra: Aya ya 23.
- ↑ Sheikh Abdul al-adhmi, Tafsir Ithna 'Ashari, juz. 7, uk. 355.
- ↑ Rejea: Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 157; Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 71, uk. 22; Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 8, uk. 2; Muslim bin Hajjaj, Sahih Muslim, juz. 8, uk. 1.
- ↑ Rejea: Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 278; Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 8, uk. 4.
- ↑ Rejea: Biblia Takatifu, Mambo ya Walawi, sura ya 19, mstari wa 3; Kutoka, sura ya 20, mstari wa 12; Kumbukumbu ya Torati, sura ya 5, mstari wa 16.
- ↑ Abu al-Sa'ud, Tafsir Abi al-Sa'ud, juz. 3, uk. 198.
- ↑ Abbas Nejad, Ravansyenasi va Ulum-e Tarbiyati, uk. 81.
- ↑ Abbas Nejad, Ravansyenasi va Ulum-e Tarbiyati, uk. 81.
- ↑ Abu al-Sa'ud, Tafsir Abi al-Sa'ud, 1983 juz. 3, uk. 198; Abbas Nejad, Ravansyenasi va Ulum-e Tarbiyati, 1384 S, uk. 81.
- ↑ Shiekh Hurri 'Amili, Wasail al-Shiah, juz. 21, uk. 505.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 158.
- ↑ Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 8, uk. 2.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 74.
- ↑ Tirmidzi, Sunan Tirmidzi, juz. 3, uk. 207; Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 428.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 162.
- ↑ Abu Daoud, Sunan Abu Daoud, juz. 2, uk. 507-508.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 161.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 162; Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 4, uk. 407 & 408.
- ↑ Bukhari, Sahih al-Bukhari, juz. 8, uk. 4.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 162.
- ↑ Fakhr Razi, Mafatih al-Ghaib, juz. 20, uk. 324.
- ↑ Qur'an: Surat al-Isra: Aya ya 23-34.
- ↑ Rejea: Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 158-159; Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 4, uk. 372; Bukhari, al-Adab al-Mufrad, uk. 30.
- ↑ Majlisi, Bihar al-Anuwar, juz. 71, uk. 37.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 349; Sheikh Tusi, al-Tibyan, juz. 6, uk. 467.
- ↑ Rejea: Kulaini, al-Kafi, juz. 6, uk. 503; Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 4, uk. 372.
- ↑ Sheikh Saduq, Uyun Akhbar al-Ridha, juz. 1, uk. 259.
- ↑ Abbas Nejad, Ravanshenasi va Ulum-e Tarbiyati, uk. 81.
- ↑ Qur'an: Surat al-Ankabut: Aya ya 8; Surat Luqman: Aya ya 13-14; Abbas Nejad, Ravanshenasi va Ulum-e Tarbiyati, uk. 81.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 158.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 22.
- ↑ Mirza-e Qummi, Jami' al-Shattat, juz. 1, uk. 240.
- ↑ Mirza-e Qummi, Jami' al-Shattat, juz. 1, uk. 240.
- ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 21, uk. 23; Hakim, Mustamsik al-Urwah al-Wuthqa, juz. 7, uk. 169; Makarim Shirazi, Istifta'at Jadid, juz. 1, uk. 494.
- ↑ Abbas Nejad, Ravanshenasi va Ulum-e Tarbiyati, uk. 81.
- ↑ Tazama: Imam Khomeini, Najat al-Ibad, uk. 382; Shafi Golpeighani, Jami' al-Ahkam, juz. 2, uk. 104.
- ↑ Qur'an: Surat al-Baqarah: Aya ya 180 & 215.
- ↑ Sheikh Tusi, al-Tibyan, juz. 2, uk. 108.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 159 & 163.
- ↑ Rejea: Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 159 & 163; Tabrasi, Majma' al-Bayan, juz. 6, uk. 632.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 159, hadith nambari 7.
- ↑ Muhaqiq Hilli, Shara'i al-Islam, juz. 4, uk. 19.
- ↑ Rejea: Bani Hashimi, Taudhih al-Masail Maraji', juz. 1, uk. 162 & 761; Khamenei, Ajwibah al-Istifta'at, uk. 110.
- ↑ Imam Sajjad, Sahifah Sajjadiyah, uk. 116-118.
- ↑ Tabatabai, al-Mizan, juz. 7, uk. 374 & juz. 13, uk. 80.
- ↑ Maskawaih, Tahdhib al-Akhlak, uk. 233.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 159-160.
- ↑ Hakim Neishaburi, Dar al-Ma'rifah, juz. 4, uk. 150.
- ↑ Ibnu Abi Jumhur, 'Awali al-La'ali, juz. 1, uk. 269.
- ↑ Kulaini, al-Kafi, juz. 2, uk. 269.
- ↑ Makarim Shirazi, Tafsir Nemuneh, juz. 17, uk. 400; Ibnu Muflih, al-Adab al-Shar'iyyah wa al-Minah al-Mar'iyyah, juz. 1, uk. 338.
- ↑ Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 2, uk. 621.
Vyanzo
- Qur'an al-Kareem
- Biblia Takatifu
- Abbas Nejad, Muhsin. Qur'an, Ravanshenasi va Ulum Tarbiati. Mashhad: Bunyad Pazuheshhayi Qur'an Hauzah na Universitas, Chapa ya kwanza, 1384 S.
- Abu al-Sa'ud, Muhammad bin Muhammad. Tafsir Abi al-Sa'ud. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, Chapa ya kwanza, 1983 M.
- Abu Dawud, Sulaiman bin Ash'ath. Sunan Abu Daoud. Beirut: Chapa ya Sa'id Muhammad Liham, 1410 HS.
- Bani Hashimi Khomeini, Sayyid Muhammad Hussein. Taudhih al-Masail Maraji'. Qom: Kantor penerbit Islami, Chapa ya nane, 1424 HS.
- Bukhari, Muhammad bin Ismail. al-Adab al-Mufrad. Mhakiki: Muhammad Fuad Abdul Baqi. Beirut: Dar al-Bashair al-Islamiah, Chapa ya tatu, 1409 HS.
- Fadhlullah, Muhammad Hussein. Min Wahyi al-Quran. Beirut: Dar al-Milak, Chapa ya kwanza, 1419 HS.
- Fakhr Razi, Muhammad bin Umar. Mafatih al-Ghaib (al-Tafsir al-Kabir). Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, Chapa ya tatu, 1420 HS.
- Hakim Neishaburi, Muhammad bin Abdullah. al-Mustadrak ala al-Sahihain. Beirut: Dar al-Ma'rifah.
- Hakim, Sayyid Muhsin. Mustamsik al-Urwah al-Wuthqa. Qom: Muasasat Dar al-Tafsir, Chapa ya kwanza, 1416 HS.
- Ibnu Abi Jumhur, Muhammad bin Zainuddin. 'Awali al-La'ali al-'Aziziah fi al-Ahadith al-Diniyah. Mhakiki na mhariri: Mujtaba Iraqi. Qom: Dar Sayyidu al-Shuhada lin-Nashr, Chapa ya kwanza, 1405 HS.
- Ibnu Shu'bah Harrani, Hassan bin Ali. Tuhaf al-'Uqul 'an Āli al-Rasul (s.a.w.w). Mhakiki na mhariri: Ali Akbar, Ghafari. Qom: Daftar Intishar Islami, Chapa ya pili, 1404 HS.
- Imam Khomeini, Ruhullah. Najat al-Ibad. Muasasat Tandhim va Nashr Asar-e Imam Khomeini. Teheran: Chapa ya kwanza, 1422 HS.
- Imam Sajjad (a.s), Ali bin al-Hussein. Sahifah Sajjadiyah. Qom: Daftar Intisharat al-Hadi, Chapa ya kwanza, 1376 S.
- Khamenei, Sayyid Ali. Ajwibah al-Istifta'at. Qom: Daftar Imam Ali Kahamenei, Chapa ya kwanza, 1424 HS.
- Kufi Ahwazi, Hussein bin Sa'id. al-Zuhd. Mhakiki: Ghulam Ridha Irfaniyan. Qom: Al-Mat-buat al-Ilmiyah, 1399 HS.
- Kulaini, Muhammad bin Ya'qub. al-Kafi. Mhakiki: Ali Akbar Ghafari. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiah, Chapa ya nne, 1401 HS.
- Majlisi, Muhammad Baqir. Bihar al-Anwar. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, Chapa ya pili, 1403 HS.
- Makarim Shirazi, Nashir. Istifta'at Jadid. Mhakiki na mhariri: Aliyan Nejad, Abu al-Qasim. Qom: Intisharat Madrasat Imam Ali bin Abi Talib (a.s), Chapa ya pili, 1427 HS.
- Maskawaih, Ahmad bin Muhammad. Tahdhib al-Akhlak wa Tathir al-A'laq. Tali'ah al-Nour, Chapa ya kwanza, 1426 HS.
- Mirza-e Qummi, Abu al-Qasim. Jami' al-Shattat fi Ajwibah al-Sualat. Mhakiki na mhariri: Murtadha Radhawi. Teheran: Muasasat Keyhan, Chapa ya kwanza, 1413 HS,
- Muhaqiq Hilli, Najmuddin. Shara'i al-Islam fi Masail al-Halal wa al-haram. Mhakiki na mhariri: Baqal, Abdul Hussein Muhammad Ali. Qom: Muasasat Ismailiyan, Chapa ya pili. 1408 HS.
- Muslim bin Hajjaj. Sahih Muslim. Beirut: Dar al-Fikr.
- Najafi, Muhammad Hassan. Jawahir al-Kalam fi Sharh Shara'i al-Islam. Mhakiki na mhariri: Quchani, Abbas, Akhundi, Ali. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, Chapa ya saba, 1404 HS.
- Rashid Ridha, Muhammad. Tafsir al-Manar. Lebanon: Dar al-Ma'rifah, Chapa ya kwanza, 1414 HS.
- Sepah-e Pasdaran-e Inqilab-e Islami. Ma'arif-e Quran. Teheran: Pezhuhekide Tahqiqat-e Islami Sepah-e Pasdaran-e Inqilab-e Islami, Chapa ya nne, 1378 S.
- Safi Golpeighani, Luthfullah. Jami' al-Ahkam. Qom: Intisharat Hazrat-e Ma'sumah, Chapa ya nne, 1417 HS.
- Shah Abdul Adhimi, Hussein. Tafsir Ithna 'Ashari. Teheran: Intisharat Miqat, Chapa ya kwanza. 11363 S.
- Sheikh Hur Alimi, Muhammad bin Hassan. Wasail al-Shiah. Qom: Muasasat Āhlulbait (a.s), Chapa yan kwanza, 1378 HS.
- Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali bin Babawaih. Man La Yahdhuruhu al-Faqih. Mhakiki na mhariri: Ali Akbar, Ghafari. Qom: Daftar Intisharat Islami, Chapa ya pili, 1413 HS.
- Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan. al-Tibyan fi Tafsir al-Quran. Mhakiki: Ahmad Qashir Amili. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi.
- Tabatabai, Muhammad Hussein Tabatabai. al-Mizan fi Tafsir al-Quran. Beirut: 1390-1394/1971-1974.
- Tabrasi, Fadhl bin Hassan. Majma' al-Bayan fi Tafsir al-Quran. Ba muqadime Muhammad Jawad Balaghi. Tehran: Intishar Nashir Khusru, Chapa ya tatu, 1382 S.
- Tirmidzi, Muhammad bin Issa. Sunan al-Tirmidzi. Beirut: Chapa ya Abdul Wahhab Abdul lathif, 1403 HS.