Nenda kwa yaliyomo

Haki ya Mwenyezi Mungu

Kutoka wikishia

Ḥaqq Allāh (Kiarabu: حق الله) au Haki za Mwenyezi Mungu ni zile haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwa maana ya kwamba; kuna haki ambazo watu wanapaswa kumfanyia Mwenyezi Mungu, na mkabala wake; ni haki za watu baina yao, wanazo paswa kutimiziana wenyewe kwa wenyewe. Kwa maana kwamba, kila mja ana haki kwa mwenzake. Mkabala na haki za Kimwenyezi Mungu, kuna taklifu na mambo ya wajibu kama vile Sala na Saumu ambazo ziko katika mabega ya waja, na waja wa Mwenyezi Mungu wanapaswa kuzitekeleza na wasipofanya hivyo, toba yao na kadhaa huwa ni wajib kwao.

Katika hukumu za mahakama za Kiislamu, kuna tofauti kati ya Haq Allah (haki ya Mwenyezi Mungu) na Haq al-Nas (haki za watu); miongoni mwazo: Hakimu anaweza kumzuia mkosaji kuungama katika kesi za haki ya Mwenyezi Mungu, kama vile uzinzi; lakini katika haki za watu kama kesi ya wizi, hawezi kufanya hivyo. Wamesema: Tofauti baina ya haki za Mwenyezi Mungu na haki za watu zinatokana na kuwa katika dini ya Kiislamu imeamrishwa kufanya wepesi katika haki za Mwenyezi Mungu na kuwa makini na uangalifu katika haki za watu.

Utambuzi wa Maana

Katika Uislamu, haki zinagawanywa katika sehemu mbili, haki za Mwenyezi Mungu na haki za watu. [1] Maana ya haki za Mwenyezi Mungu ni haki za Mungu juu ya mwanadamu; na mkabala wake ni haki za watu juu ya mtu mwingine. [2] Bila shaka haki za Mwenyezi Mungu ni pamoja na amri na makatazo yote ya Mwenyezi Mungu [3] na ni pamoja na haki za watu. [4] Lakini neno na istilahi hii inanapotumika mkabala na haki za watu, basi katika hali hii huhusiana na na zile haki tu ambazo si haki za watu na hakuna awezaye kuziondoa. [5]

Kwa mtazamo wa kisheria, uhalifu wowote unaosababisha uvunjifu wa utulivu na kutoa pigo kwa maslahi ya kijamii na haki za umma, adhabu yake inachukuliwa kuwa ni Haq Allah (haki ya Mwenyezi Mungu. [6]

Baadhi ya mafaqihi wamezigawanya haki za Mwenyezi Mungu katika makundi mawili: Haki halisi na safi za Mwenyezi Mungu: kama vile adhabu ya uzinzi, liwati na unywaji pombe; na haki zisizo halisi na safi za Mwenyezi Mungu, yaani; haki ambazo, pamoja na haki za Mwenyezi Mungu, pia kuna haki za watu ndani yake; kama vile: Adhabu ya wizi ambayo hukumu yake ni ya kukatwa mkono . [7]

Sala [8] na sheria zote za kimahakama isipokuwa adhabu inayo husiana na tuhuma ya zinaa na liwati ni haki ya Mungu nayo ni ya kundi la kwanza, [9] na sheria kama vile Ta'zir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo) [10] na adhabu ya tuhuma ya zinaa na liwati [11] ni katika kundi la pili.

Nafasi

Katika Aya na hadithi mbalimbali imesisitizwa juu ya kuzingatia haki za Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa Allama Tabataba'i, katika aya ya 42 hadi 45 ya Surat al-Mudathirr, ambapo kutoswali na kutowalisha masikini kunazingatiwa kuwa ni sababu ya kuingia motoni, Sala inaashiria haki za Mwenyezi Mungu na kulisha masikini inahusu haki za watu. [12] Vile vile amesema haki zote za Kiungu mukhtasari wake ni katika kujifunza dini na kuitekeleza. [13] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), ambayo inajulikana kama Risala ya Haki, haki za Mwenyezi Mungu zimetajwa kuwa ndiyo haki kubwa kuliko zote. [14]

Katika vyanzo vya kifiqhi, Haqullah (haki ya Mwenyezi Mungu) imetajwa katika sehemu ya sheria za mahakama. Pia imezingatiwa katika sheria za haki za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kulingana na maoni ya Kamisheni ya Masuala ya Fat’wa ya Baraza Kuu la Kimahakama la Iran, daima upande wa haki ya Kiungu na kuwa jumla uhalifu hutangulizwa mbele ya kipengele cha haki zake za watu. [15]

Tofauti Yake na Haki za Watu

Wanazuoni wametaja baadhi ya tofauti baina ya Haki za Mwenyezi Mungu na Haki za watu. Baadhi yazo ni kama zifuatazo:

  • Kuthibiti haki ya Mungu mbele ya hakimu ni vigumu zaidi kuliko kuthibiti haki ya watu. Kwa sababu haki ya Mwenyezi Mungu haithibiti kwa shahidi mwanamume mmoja na mashahidi wawili wanawake, au shahidi mmoja mwanamume na kiapo, au kwa ushahidi wa wanawake peke yao. Lakini baadhi ya haki za watu zinaweza kuthibitishwa kwa ushahidi huu. [16]
  • Utekelezaji wa hukumu katika Haqullah hautegemei matakwa ya mtu yeyote; Tofauti na Haq al-Nas, ambayo inahitaji ombi la mwenye haki.[17]
  • Katika Haqullah, tofauti na Haqul-Nas, hakimu anaweza kumzuia mhalifu kukiri na kuungama. [18]
  • Katika Haqullah, mtu asiyekuwepo hahukumiwi na kuwepo kwa mtuhumiwa ni muhimu na jambo la dharura. [19] Suala hili limeelezwa katika Kifungu cha 290 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Iran. [20]
  • Katika haki ya Mungu, msamaha wa mtu ambaye uhalifu ulitendwa dhidi yake hilo halipelekei kufutika na kuondoka kwa haki husika; hii ni katika hali ambayo, baadhi ya mifano ya Haq al-Nas inaweza kusamehewa au kuhamishwa.[21]
  • Baadhi ya haki za Mwenyezi Mungu huondoka kupitia njia ya kutubia, lakini haki za watu haziondoki hata kwa toba. [22]
  • Haki ya Mwenyezi Mungu inategemea urahisi na tahafifu, lakini haki ya watu imejengeka juu ya msingi wa umakini na tahadhari.[23] Inasemekana kwamba, baadhi ya mafaqihi wanatambua kwamba, tofauti kati ya haki ya Mungu na haki ya watu katika hukumu za mahakama chimbuko lake ni hili. [24]

Kufidia Haki ya Mungu

Haki ya Mungu inalazimu wajibu na majukumu ambayo mwanadamu lazima atekeleze kwa ajili ya Mungu. [25] Ikiwa hatatekeleza majukumu hayo, ni lazima afidie; Ufidiaji wa baadhi ya haki hizi ni kwa njia ya toba. [26] Ufidiaji wa baadhi ya haki zingine za Mwenyezi Mungu, kama vile Sala na Saumu, mbali na kufanya toba, mhusika anapaswa pia kulipa kadhaa. [27]

Rejea

Vyanzo

  • Abdu al-Rahman, Mahmud, Mu'jam al-Mustalahat wa al-Alfadz al-Fiqhiyah.
  • Akhundi, Muhammad, Ayine Dadrasiye Keifari. Teheran: 1368 S
  • Allamah Tabatabai, Sayyid Muhammad Hussein, Al-Mizan fi Tafsir al-Quran, Qom: Kantor Penerbit Islami Jamiah Mudarrisin, Hawzah Ilmiah Qom, 1417 H
  • 'Amili, Yasin Issa, Al-Istilahat al-Fiqhiyah fi al-Rasail al-Ilmiah, Beirut: Dar al-Balaghah, 1413 H
  • Ardabili, Ahmad bin Muhammad, Zubdah al-Bayan fi Ahkam al-Quran, Editor Muhammad Baqir Bahbudi, Teheran: Perpustakaan al-Ja'faryah li Ihya al-Atsar al-Ja'fariyah, tanpa tahun
  • Baheshti, Ahamd, Haq wa Taklif, Kitab Naqd, no. 1, 1375 S
  • Bani Hashimi, Khomaini, Sayyid Muhammad Hassan, Taudhih al-Masail Maraji Sesuai dengan Fatwa-Fatwa 16 orang dari para Maraji' Agung, Qom: Kantor Penerbit Islami, cet. 1, 1392 S
  • Ibnu Shu'bah Harani, Hassan bin Ali, Tuhaf al-'Uqul, Editor Ali Akbar Ghifari, Qom: Jamiah Mudarrisin, 1404 H
  • Muhaqqiq Damad, Sayyid Musthafa,Qawaid Fiqh', Teheran: Markas Publikasi Ulum Islami, 1406 H
  • Muntadhiri, Hussein Ali, Dirasat fi Wilayah al-Fiqhiyah wa Fiqh al-Daulah al-Islamiah, Qom: Tafakur, 1409 H
  • Murqayi, Sayyid Taha, Haqqullah wa Haq al-nas. Ensiklopedia Jahan Islam
  • Musawi Ardabili, Sayyid Abdul Karim, Fiqh al-Qadha, Qom: 1423 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam fi Syarh Shara'i al-Ilam, Riset: Abas Qucani dan Ali Akhundi, Beirut: Dar Ihya al-Turath al-'Arabi, 1404 H
  • Shiri, Abas, Suqut-e Mujazat dar Huquq-e Keifariye Islam va Iran, Teheran: Markas Penerbitan Jihad Universiyas Shahid Baheshti, 1372 S
  • Shahid Awal, Muhammad bin Makki, Al-Qawaid wa al-Fawaid. Riset Sayyid Abdul Hadi Hakim, Najaf: 1400 H (Ofsit, Qom, toko buku Mufid)
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Al-Mabsuth fi Fiqh al-Imamiah. Editor: Sayyid Muhammad Taqi Kashfi, Teheran: Perpustakaan al-Murtadhawiyah li Ihya al-Athar al-Ja'fariyah, 1387 H