Takriri au Ridha Ma'asumu

Kutoka wikishia

Taqriir al-Ma'asum (Kiarabu: تقرير المعصوم), Neno hili linaponasibishwa na Ma'asum (a.s),huwa na maana ya yeye kuona kauli, tabia au tendo likitendeka mbele yake, naye akawa hakulikaripia yaani kalinyamazia kimya. Ambapo kunyamaza kwake huchukuliwa kuwa yeye ameridhika na jambo hilo, nayo huwa ni dalili ya uhalali wa tendo hilo. Taqriri, kauli pamoja na matendo ya Ma'asumu, huhisabiwa ni Sunna katika dini ya Kiislam. Sunna ni moja kati ya vyanzo vinne vya sheria za dini ya Kiislamu.Kwa mtazamo wa Kishia, taqriri ya Ma'asumu ni sawa na taqriri ya bwana Mtume s.a.w.w), miongoni mwa taqriri hizo, ni taqriri ya bibi Fatima (a.s) pamoja na taqriri za Maimamu 12 wa Kishia (a.s).

Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa fani ya usuli al-fiqhi, taqriir za Ma'asumu huzingatiwa kuwa ni dalili ya kisheria kupitia misngi na sharti maalumu. Miongoni miongoni mwa sharti hizo, ni kule Ma'asumu kulishuhudia tendo hilo, na kule yeye kuwa na uwezo wa kutoa maoni yake juu ya tendo hilo. Hoja madhubuti ya uhalali wa kushikama na taqriri, kumeegemea kwenye msingi usemao kuwa; Ma'asumu ana wajibu wa kulikataza ovu litendwalo mbele yake, na kutofanya hivyo kunaendana kinyuma na utukufu pamoja na wadhifa wake wa kisheria.

Utafiti wa kilugha

Ibara inayosomeka kwa lugha ya Kiarabu; «تقرير المعصوم» yenye maana "kunyamaza kimya kwa Ma'asumu" maana yake ni ukimya wa Ma'asumu (a.s) mbele ya kauli na tabia au tendo lililotendeka mbele yake. [1] Katika fani ya usuli al-fiqhi, taqriri ya Ma'asumu haiwezi kuwa na mashiko isipokuwa iwe imeambatana na masharti maalumu. [2] Msingi unaoifanya taqriri kuwa ni hoja na dalili ya uhalali juu ya tendo hilo, unatokana na msingi usemao kuwa; Imamu anawajibu na ni lazima kwake kulikemea tendo ovu litendwalo mbele yake, na iwapo mtendaji wa tendo hilo atakuwa hana habari juu ya ubaya wa tendo hilo, basi ni wadhifa wa Ma'asumu kumuongoza katika njia ilio sawa. [3]

Kwa mfano iwapo mtu atatawadha mbele ya Ma'asumu aina fulani ya udhu, na ma'asumu akaliona tendo hilo na asiseme kitu, basi ukimya wake huo unaitwa taqriri ya maasumu, na inachukuliwa kuwa ni dalili ya uhalali wa udhu huo. [5]

Aina za Taqriri (Ridha)

Katika baadhi ya vitabu vya fani ya usuli al-fiqhi, taqriri - juu ya kitendo ambacho kimenyamaziwa - imegawanyika katika aina mbili: Tariri juu ya tendo fulani na taqriri juu ya kauli fuani. [15] Na wengine wameongeza aina nyingine ya tatu ya taqriri, nayo ni taqriri juu itikadi fulani. [16] Aina hii ya tatu ni kwamba; Kwa mfano mtu mwenye imani maalum kuhusu masuala kama vile Mungu, ufufuo, na mengine kama hayo, awe amekuja mbele ya Ma'asumu, kisha Ma'asumu awe hakuzungumza chochote kile kuhusiana na imani yake hiyo. [17]

Masharti ya uhalali wa hoja ya Taqriri

Wataalamu wa fani ya usuli Al-fiqhi, huchukulia ukimya wa Ma'asumu mbele ya tabia, kauli au tendo fulani, kuwa ni thibitisho la uhalali wa mambo hayo, chini ya masharti yafuatayo:

  • Ma'asumu awe amefahamu na kuona mambo hayo yakitendeka mbele yake. [18]
  • Ma'asumu awe na uhuru na uwezo wa kudhihirisha maoni na mtazamo wake juu ya mambo hayo. Kwa mfano, mtu ambaye amefanya tabia mbele ya Ma'asumu, asiwe ameondoka mara tu baada ya kutenda tabia hiyo. [19]
  • Kusiwe na kikwazo kwa Ma;'asumu katika uhuru wa kutoa maoni yake. Kwa mfano, Imamu asiwe amelazimika kukaa kimya kutokana na khofu ya kuhatarisha maisha yake au maisha ya wafuasi wake. [20]
  • Kabla ya kimya hicho, Ma'asumu asiwe amewahi hakusema neno fulani katika kulikataza jambo hilo katika zama zilizopita. [21]