Nenda kwa yaliyomo

Ziyara ya Imam Husein (a.s)

Kutoka wikishia
Kaburi la Imamu Hussein (a.s)

Ziyara ya Imam Husein (a.s) ni kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s), kutoa salamu kwa Imam na kusoma ziyara ya Imam Hussein (a.s) zilizoko katika vitabu mbalimbali.

Ziyara ya Imam Hussein (a.s) ni miongoni mwa matendo yenye fadhila nyingi sana Kwa Mashia. Wanazuoni wa Kishia wamenuku mkusanyiko wa vitabu vya hadithi kuhusiana na thawabu zinazopatikana katika ziyara hii, Ikiwemo fadhila ambazo Mwenyezi Mungu amewapatia Wanaotembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) na dua za Mtume (s.a.w.w) na maimamu kwa ajili yao. Inapendekezwa kufanya ziyara ya Imamu Hussein (a.s) Kwa niaba ya mtu mwengine, na mtu ambae hawezi kufika katika kaburi hili tukufu anaweza kufanya ziyara hii Kwa kusoma ziyara ya Imam Hussein akiwa mbali.

Katika vitabu vya hadithi Kuna adabu nyingi sana ambazo zimesisitizwa Kwa mtu ambae anataka kumtembelea Imamu Husein (a.s). Miongoni mwa adabu hizo ni; Kumtambua Imamu Husein (a.s), kufanya ghusl, kuvaa nguo safi, kumuomba Mwenyezi Mungu ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la imam, na kusoma Ziyara ya imam hussein (a.s). Mnamo tarehe 20 safar ya Kila mwaka (Arbaini ya imam Hussein) wanazuoni mbalimbali kama vile Sheikh Morteza Ansari na Sheikh Jafar Kashif al-Ghitaa walikua wakitembea Kwa miguu kutoka mji wa Najaf kuelekea kaburi la imam Hussein (a.s). Leo hii, matembezi ya Arbaeen ni mojawapo ya mila muhimu ya Mashia na mamilioni ya watu hushiriki katika hilo.

Katika vyanzo vya hadithi vya Mashia, ziyara kama vile ziyara ya warith, ziyara la eneo tukufu na ziyara ya Ashura ni miongo mwa Ziyara zilizopendekezwa kusomwa na mtu amayetembelea kaburi la Imamu Hussein. Vilevile Kunapendekezwa kusoma Ziyara ya Imamu Hussein (a.s) katika siku mbalimbali kama vile siku ya Arafah, siku ya Ashura, Tarehe 15 ya Sha’ban na katika mwezi wa Rajab.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, mtu wa kwanza kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) alikuwa ni Jaber bin Abdullah Ansari. Baadhi ya makhalifa wa Bani Abbas, akiwemo Harun al-rashid na Mutawakkil, walijaribu kuzuia watu kufanya Ziyara ya Imam Hussein (a.s); Kwa upande mwingine, wakati wa utawala wa Al-Buya, Safavie na Qajar, hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuendeleza ujenzi wa Haram ya Imam Hussein (a.s).

Nafasi na Umuhimu

Ziyara ya Imam Hussein (a.s) ni kutembelea kaburi la Imam Hussein,[1]. na kufanya vitendo mbalimbali kama vile kutoa salamu na kusoma Ziyara ya imam Hussein (a.s)[2].

Kwa mujibu wa Hadith mbalimbali zilizopokelewa kutoka Kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w)[3]. na maimamu wa Mashia,[4]. Miongoni mwa matendo bora na yenye fadhila nyingi sana ni kuzuru kaburi la Imamu Hussein (a.s) lililopo katika mji wa Karbala.

Miongoni mwa fadhila za kutembelea kaburi la Imamu Hussein (a.s) zilizotajwa katika vitabu vya hadithi ni: kumzuru Imam Hussein kunamfanya mtu awe karibu zaidi na Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imamu Ali na bibi Fatimah (a.s), Mtume Muhammad (s.a.w.w) na maimamu wote huwaombea dua njema wenye kumzuru Imamu Hussein (a.s).[5].

Historia Fupi

Vyanzo mbalimbali vya Mashia, imenakili kuhusiana na nafasi au Umuhimu wa eneo la Karbala ( alipouwawa imam Hussein ) hata kabla ya Uislamu, [8] Kwa mujibu wa Moja ya hadithi zilizopokelewa, Imam Ali (a.s) alipokuwa akirudi kutoka vita vya siffin alipita eneo la Karbala na kukumbuka tukio la Ashura na kumlilia mwanae Imamu Hussein (a.s). [9]

Kwa mujibu ya wanahistoria, Jabir bin Abdullah Answari Alikua mtu wa kwanza aliyefika Karbala baada ya Imamu Hussein (a.s) kuuwawa shahidi, Baadhi ya watu pia wanamchukulia Ubaidullah bin Har Jafi kama mtu wa kwanza aliyezuru kaburi la Imamu Hussein (a.s) [12].

Mauzi na usumbufu wa utawala wa Banu Umayya Kwa mazuwari wa Imam Hussein, haukuzuia watu kwenda kulitembelea kaburi la Imamu Hussein (a.s) [13] Uqbah bin Amr Sahmi, mwana mashairi wa lugha ya Kiarabu, aliingia Karbala mwishoni mwa karne ya kwanza hijiria kwa ajili ya kumzuru imam Hussein na kuimba mashairi ya maombolezo.[14] Licha ya ukali wa Banu Umayya Kwa ahlulbait, kaburi la Imam Hussein (a.s) halikuharibiwa, lakini baadhi ya makhalifa wa Abbasiyah, akiwemo Harun al-Rashi na Mutawakkil, walichukua hatua za kuharibu kaburi la Imam Hussein (a.s), ili kufuta athari za kaburi hilo na kuzuia watu kuzuru eneo hilo takatifu.[15] Kwa upande mwingine, wakati wa utawala wa Aali-Bueih, Jalairian, Safavid na Qajar, hatua za kimsingi na za kina zilichukuliwa kwa ajili ya maendeleo, ujenzi na upambaji wa kaburi la imam Hussein.[16]

Wanahistoria kama vile Ibn Battuta (aliyefariki 703 AH) alizungumzia kuhusiana na kuzuru kaburi la Imamu Hussein (a.s) na ugawaji wa chakula Kwa mazuwari wa Imamu katika eneo hili tukufu [17] Ibn Sabbagh (aliyefariki 855 AH) pia amesimulia kuhusiana na Ziyara ya idadi kubwa ya watu katika Karne ya 9 hijriya.[18]

Adabu za Ziara

Wapokezi wa hadithi wamepokea hadithi nyingi sana ambazo zimekuja kuelezea kuhusu adabu za Ziara ya Imam Hussein (a.s). Kwa mujibu wa Hadithi hizo, kufahamu uhakika kuhusu Imam Hussein, ikhlasi, kuhudhurisha moyo na kuwa na huzuni, ni miongoni mwa adabu za kiroho za kufanya amali za ziara, na kuoga khusli ,[19] kuvaa nguo safi ,[20] kutumia manukato na mapambo, [21] Kuomba ruhusa kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt Kwa ajili ya kuingia katika Haram ya Imam, [24] na pia kusoma ziara mbalimbali kama vile Ziyarat Jamiu Al-Kabira ni baadhi ya adabu dhahiri. [25]

Kwa mujibu wa riwaya kutoka katika kitabu cha Kamel al-Ziyarat, Imam Swadiq (a.s) aliamuru kuswali rakaa mbili karibu na kaburi la Imam Hussein (a.s),ambapo katika rakaa ya kwanza husomwa Surat al-Hamad na Surat Yasin na katika rakaa ya pili husomwa Surat al-Hamad na Surat al-Rahman [26]

Nyakati Maalum za Ziara

Nyakati maalum za ziara katika Hadithi mbalimbali zilizopokewa na Mashia, inapendekezwa zaidi kusoma ziara ya Imamu Hussein (a.s) katika siku mbalimbali kama vile siku ya Arafah, [27] siku ya Ashura, [28] Tarehe 15 ya Sha’ban, [29] na katika mwezi wa Rajabu.[30]

Kisomo cha Ziyara

Katika vyanzo vya Hadithi vya Mashia, kuna Ziara nyingi sana kwa ajili ya kusoma wakati wa kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) [33] miongoni mwa Ziara hizo ni[34] Ziyara ya warith,[35] Ziyara ya Ashura, [37] Ziyara ya Rajabiyeh, [38] na Ziyara za usiku za Qadr. [39]

Kwenda Ziyara ya Imam Hussein kwa Miguu

Matembezi ya Arobain ya Imamu Hussein (a.s)
Makala Asili: Kwenda Ziyara ya Imam Hussein (a.s) Kwa miguu.

Kuna riwaya mbalimbali kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s) kuhusiana na kwenda kumzuru Imamu Husein (a.s) kwa miguu.[40]

Hadithi mbalimbali zimepokelewa katika vitabu vya Mashia vikisema mwenye kuenda kuzuru kaburi la Imam Hussein kwa miguu husamehewa madhambi yake. Imepokelewa kutoka Kwa Imamu Swadiq (a.s) akisema mwenye kutoka Kwa ajili ya kwenda kutembelea kaburi la Imam Hussein Kwa miguu basi ataandikiwa thawabu Kwa kila hatua ambayo atakayoichukua.[41] Sheikh Tusi amesema katika kitabu cha Tahzeeb Al-Ahkam kwamba zuwari wa imam Hussein anaporudi kutoka kwa Imam kwa miguu, Malaika humwambia Kuhusu neno la Mungu; Anza upya kwani madhambi yako yote uliyafanya yamesamehewa.[42]

Leo hii, matembezi ya Arbaeen ni miongoni mwa mila ya Mashia ambayo hufanywa kila mwaka wakati wa maombolezo ya Arbaini ya Hussein . Tamaduni hii, inayohudhuriwa na mamilioni ya watu, inachukuliwa kuwa msafara au mkusanyiko mkubwa zaidi ulimwenguni.[43]

Kufanya Ziyaza Ukiwa Mbali

Inapendekezwa kwa mtu ambaye hana uwezo wa kufika karbala Kufanya ziyara ya Imamu Hussein (a.s) akiwa mbali. [41] Katika aina hii ya Ziyara, inapendekezwa kuoga au kufanya khusli ya Ziyara, kuvaa nguo safi, na pia kusoma ziyara katika sehemu kama vile paa ya nyumba au jangwani.[42] Pia inajuzu kusoma Sala ya Ziara, kabla au baada yake. Imepokelewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) akisemu mtu mwenye kufanya khusli ya Ziyara akiwa nyumbani kwake kisha akamtolea salamu Imamu Hussein (a.s) basi huandikiwa thawabu ya sawa na mtu ambaye amemzuru Imam katika kaburi lake. [44]

Rejea

  1. Dibache bar Ziarat, uk. 9-11, 1394 S, Kargar, Haqiqat Ziarat, Uk. 7, 1391 S.
  2. Dibache bar Ziarat, Uk. 9-11, 1394 S, Kargar, Haqiqat Ziarat, uk. 7, 1391 S.
  3. Tazama: Jami' Ziarat al-Ma'sumin, juz. 3, uk. 39-69, 1389 S.
  4. Tazama: Jami' Ziarat al-Ma'sumin, juz. 3, uk. 36-39, 1389 S.
  5. Najafi Yazdi, Asrar Ashura, juz. 2, uk. 103-105, 1377 S.

Vyanzo

  • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1419 AH.
  • Al-Hādī, Jaʿfar. Ahammīyat wa falsafa-yi zīyārat-i marqad-i Ḥusaynī. Faslnāma-yi Farhang-i Zīyārat. No 19, 20. Summer and Fall 1393 Sh.
  • ʿAlawī, Sayyid ʿAdil. Faḍīlat-i pīyādarawī barā-yi zīyārat-i maṣūmīn. Translated by Ḥusayn Shahristānī. Faslnāma-yi Farhang-i Zīyārat. No 19, 20. Summer and Fall 1393 Sh.
  • Dībācha-ie bar zīyārat: Pasukh bi shubahāt-i wahhābīyat az dīdgāh-i dānishmandān-i Shīʿa wa Ahl-i Sunnat. Qom: Intishārāt-i Payām-i Imām al-Hādī (a), 1394 Sh.
  • Farhang-i fiqh muṭābiq-i madhhab-i Ahl-i Bayt. Edited and authored by Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif Fiqh-i Islāmī, 1389 Sh.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tafṣīl wasāʾil al-Shīʿa ilā taḥṣīl masā'il al-sharī'a. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1416 AH.
  • Ibn Qūlawayh, Jaʿfar b. Muḥammad. Kāmil al-zīyārāt. Edited by Jawād Qayyūmī. Qom: Nashr al-Fiqāha, 1424 AH.
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Al-Luhūf ʿalā qatlay al-ṭufūf. TQom: Anwār al-Hudā, 1417 AH.
  • Kārgar, Rahīm. Ḥaqīqat-i zīyārat. Mashhad: Āstān-i Quds-i Raḍawī, 1391 Sh.
  • Jāmiʿ zīyārāt al-maʿṣumīn. Muʾassisat al-Imām al-Hādī (a). Qom: Payām-i Imām al-Hādī (a), 1389 Sh.
  • Kilīddār, ʿAbd al-Jawād. Tārīkh-i Karbalā wa hāʾir Ḥusaynī. Translated by Muslim Ṣāḥibī. Tehran: Mashʿar, 1389 Sh.
  • Muḥammadī Reyshahrī, Muḥammad. Dānishnāmah-yi Imām Ḥusayn (a) bar pāya-yi Qurʾān, ḥadīth wa tārīkh. Translated by ʿAbd al-Hādī Masʿūdī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1430 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Beirut: Muʾassisa al-Wafā, 1403 AH.
  • Muhaddithī, Javād. Farhang-i Āshūrā. Qom: Nashr-i Maʿrūf, 1374 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Kitāb al-Mazār. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Najafī Yazdī, Sayyid Muḥammad. Asrār-i āshūrā. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1373 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Qom: Dār al-Thiqāfa, 1414 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Beirut: Dar al-Turāth, 1967.
  • Zāriʿ Khurmīzī, Muḥammad Riḍā. ʿArbaʿīnhā-yi khunīn; nigāhi bi barkhī az hamalāt-i khūnīn bi marāsim-i arbaʿīn-i Ḥusaynī dar dura-yi muʿaṣir. Faṣlnama-yi zīyārat, No 19, 20. Summer and Fall 1394 Sh.