Sala ya Ziara

Kutoka wikishia

Sala ya Ziara(Kiarabu:صلاة الزيارة) ni Swala ambayo ni mustahabu na huswaliwa wakati mtu anapowazuru Maasumina. Imetambuliwa kuwa ni mustahabu kusoma Surat Yasin katika rakaa ya kwanza na Surat Rahman katika rakaa ya pili baada ya Surat al-Fatiha.

Sheikh Abbas Qomi amesema katika kitabu chake cha Mafatihul-Jinan kwamba, mahali bora kabisa kwa ajili ya kuswali Swala ya ziara ya Mtume (s.a.w.w) ni Rawdha ya haram yake (Rawdha ni baina ya mimbari na kaburi la Mtume katika Masjid al-Nabbi mjini Madina) na kwa ajili ya Maasumina wengine eneo bora la kuswali swala ya ziara ni sehemu ya juu kichwani. Kwa mujibu wa fatuwa za Marajii Taqlidi, ni haramu kuswali swala ya ziara katika hali ya kulipa mgongo kaburi kama hatua kufanya kutahesabiwa kuwa ni kumvunjia heshima Maasumu kwa mujibu wa ada na mazoea ya watu.

Katika hadithi hakujabainishwa kuswali swala ya ziara kwa ajili ya mtu ambaye sio Maasumu; kwa muktadha huo kuswali swala kama hii sio sahihi; hata hivyo baada ya ziara mtu anaweza kuswali swala ya mustahabu na kumpa zawadi ya thawabu hizo aliyezikwa mahali hapo.

Namna ya kuswali swala ya ziara

Swala ya ziara ina rakaa mbili na huswali wakati wa kuwazuru Maasumina(a.s).[1] Katika swala ya ziara hakujabainishwa suala la kuusoma sura maalumuu, hata hivyo ni bora kusoma Surat Yassin katika rakaa ya kwanza na Surat al-Rahman katika rakaa ya pili baada ya al-Hamdu.[2] Katika ziara ya Mtume (s.a.w.w) kwa mbali kumenukuliwa kuswali rakaa nne za swala ya ziara (kwa sura ya rakaa mbili mbili).[3] Kuhusiana na ziara kwa Maasumina wengine inawezekana kuswali swala kadhaa za rakaa mbili mbili.[4] Baadhi ya mafakihi wanaamini kuwa, kama ziara inafanyika kando ya kaburi la Maasumu Swala ya ziara huswaliwa baada ya ziara na kama ziara inafanyika kwa mbali, basi Swala ya ziara itangulizwe kabla ya ziara yenyewe.[5]

Mahali bora kabisa pa kuswali swala ya ziara

Sheikh Abbas Qomi amesema katika kitabu chake cha Mafatihul-Jinan kwamba, mahali bora kabisa kwa ajili ya kuswali swala ya ziara ya Mtume (s.a.w.w) ni Rawdha ya haram yake (Rawdha ni baina ya mimbari na kaburi la Mtume katika Masjid al-Nabbi mjini Madina) na kwa ajili ya Maasumina wengine eneo bora la kuswali swala ya ziara ni sehemu ya juu kichwani[6].Kwa mujibu wa fatuwa za Marajii Taqlidi, ni haramu kuswali swala ya ziara katika hali ya kulipa mgongo kaburi kama katika ada na mazoea ya watu hilo linahesabiwa kuwa ni kumvunjia heshima Maasumu[7].

Kuibuka ugomvi

Katika karne ya 13 Hijiria kulitokea mzozo na ugomvi kwa jina la "ugomvi wa juu ya kichwa na nyuma ya kichwa au ugomvi wa sehemu ya kuswalia. Wafuasi wa kundi la Shekhiyah wakati wa kuswali swala katika haram za Maimamu, walikuwa wakisimama kuswali kwa namna ambayo kaburi la Imam linakuwa baina yao na baina ya kibla. Kwa hatua yao hii wakaondokea kuwa mashuhuri kwa jina la "nyuma ya kichwa" na wakatuhumiwa kwamba, wamelifanya kaburi kuwa kibla. Mkabala wao, Mashia ambao walikuwa wakikihesabu kitendo hicho kuwa ni ughulati (Maghulati ni watu ambao walmechupa mipaka kuhusiana na shakhsia ya Maimamu maasumina) walikuwa wakiswali kwa makusudi katika eneo na mbele la kichwani katika kaburi la Maasumu (upande wa kulia wa kaburi la Imam). Kwa msingi huo, nao wakaondokea kufahamika kwa jina la "juu ya kichwa".[8]

Swala ya ziara ya watoto wa maimamu

Katika hadithi hakujabainishwa kuswali Swala ya ziara kwa ajili ya mtu ambaye sio Maasumu; kwa muktadha huo kuswali Swala kama hii sio sahihi; hata hivyo baada ya ziara mtu anaweza kuswali Swala ya mustahabu na kumpa zawadi ya thawabu hizo aliyezikwa mahali husika.

Swala ya ziara ya niaba

Ziara na swala ya ziara ya mustahabu inawezekana mtu akawaswalia walio hai na walioaga dunia.[9] Kadhalika inawezekana kufanya ziara na kuswali Swala ya ziara kwa niaba ya watu wote (kwa sura jumla) au kwa kila mtu mmoja mmoja.[10] Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, thawabu za amali ya mustahabu ambayo mtu anaifanya kwa ajili ya wengine, huandikwa kwa ajili ya mtu mwenyewe mwenye kufanya amali hiyo na kwa ajili ya mtu aliyemfanyia kwa niaba; bila ya kupunguzwa hata kidogo ujira na malipo ya mwenye kuitekeleza.[11]

Rejea

  1. Sheikh Abbas Qummi, Mafatih al-Jinan, Adab Ziarat, uk. 429.
  2. Sheikh Abbas Qomi, Mafatih Al-Jinan, 1387 Shamsii, Mada((Adabu ziyara)), uk. 430.
  3. Sheikh Abbas Qomi, Mafatih Al-Jinan, 1387 Shamsii, Mada((Ziyara ya bwana Mtume)), uk. 447.
  4. Sheikh Abbas Qomi, Mafatih Al-Jinan, 1387 Shamsii, Mada((Ziyaratul-hujaj jahirah dar ruzee jumue)), uk. 447.
  5. Alawi Amuli, “Kutanguliza ziyarat ya swala katika Ziyarat kutoka mbali,” uk. 339-345
  6. Mafatihul-Jinan, Adabu ziyara, Adabu ya kumi nasaba, Chapa ya mush'ar, uk. 447
  7. Imam Khomeini, Taudhihat al-masail, 1392 Shamsii, juz. 1, uk.629-633
  8. Haireinia “madhehebu ya sheikhiya”, Wabehghae shianews, 18 Farvardin 1391 Shamsii, Diedeh shud dar 9 Ardibehesht 1397 Shamsii
  9. Imam Khomeini, Taudhihat al-masail, 1392 Shamsii, juz. 1, uk.1049-1051
  10. Sheikh Abbas Qomi, Mafatih Al-Jinan, 1387 Shamsii, Mada((Adabu ziyara kwa niaba)), uk. 803.
  11. Sheikh Abbas Qomi, Mafatih Al-Jinan, 1387 Shamsii, Mada((Adabu ziyara kwa niaba)), uk. 804

Vyanzo

  • Syekh Abbas Qummi. Mafātih al-Jinān, Tehran, Mash’ar, Chapa ya kwanza, 1387 Shamsii
  • Allamah Majlisi, Muhammad Baqir. Bihār al-Anwār, Teheran, Dar al-Kutub al-Islamiyah.
  • Imam Khomeini, Taudhihatul-masail, Marajii mutwabiq ba fat'wa shunz'dah nafar az marajii muadham taqlid, Tandhim Sayyied Muhammad Hassan Bani-hashimi Khomein, Qom, Daftar Intisharat Islami, Chapa ya kwanza, 1392 Shamsii.