Ziyara ya Imam Husein (a.s)

Kutoka wikishia

Ziyara ya Imam Husein (a.s) ni kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s), kutoa salamu kwa Imam na kusoma ziyara ya Imam Hussein (a.s) zilizoko katika vitabu mbalimbali.

Ziyara ya Imam Hussein (a.s) ni miongoni mwa matendo yenye fadhila nyingi sana Kwa Mashia. Wanazuoni wa kishia wamenuku hadithi nyingi kuhusiana na thawabu zinazopatikana katika ziyara hii, Ikiwemo fadhila ambazo Mwenyezi Mungu amewapatia Wanaotembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) na dua za Mtume (s.a.w) na maimamu kwa ajili yao. Inapendekezwa kufanya ziyara ya Imam Hussein (a.s) Kwa niaba ya mtu mwengine, na mtu ambae hawezi kufika katika kaburi hili tukufu anaweza kufanya ziyara hii Kwa kusoma ziyara ya Imam Hussein akiwa mbali.

Katika vitabu vya hadithi Kuna adabu nyingi sana ambazo zimesisitizwa Kwa mtu ambae anataka kumtembelea Imamu Husein (a.s). Miongoni mwa adabu hizo ni; Kumtambua Imamu Husein (a.s), kuoga/kufanya ghusli, kuvaa nguo safi, kumuomba Mwenyezi Mungu ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la imam, na kusoma Ziyara ya imam hussein (a.s). Mnamo tarehe 20 safar ya Kila mwaka (Arbaini ya imam Hussein) wanazuoni mbalimbali kama vile Sheikh Morteza Ansari na Sheikh Jafar Kashif al-Ghitaa walikua wakitembea Kwa miguu kutoka mji wa najaf kuelekea kaburi la imam Hussein (a.s). Leo hii, matembezi ya Arbaeen ni mojawapo ya mila muhimu ya Mashia na mamilioni ya watu hushiriki katika hilo.

Katika vyanzo vya hadithi vya Mashia, ziyara kama vile ziyara ya warith, ziyara la eneo tukufu na ziyara ya Ashura ni miongo mwa Ziyara zilizopendekezwa kusomwa na mtu amayetemelea kaburi la Imamu Hussein. Vilevile Kunapendekezwa kusoma Ziyara ya Imam Hussein (a.s) katika siku mbalimbali kama vile siku ya Arafah, siku ya Ashura, Tarehe 15 ya Sha’ban, na katika mwezi wa Rajab. Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, mtu wa kwanza kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) alikuwa ni Jaber bin Abdullah Ansari. Baadhi ya makhalifa wa Bani Abbas, akiwemo Harun al-rashid na Mutawakkel, walijaribu kuzuia watu kufanya Ziyara ya Imam Hussein (a.s); Kwa upande mwingine, wakati wa utawala wa Al-Buya, Safavid na Qajar, hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuendeleza ujenzi wa kaburi la mtukufu huyunwa daraja.

Umuhimu

Ziyara ya Imam Hussein (a.s) ni kutembelea kaburi la Imam Hussein, [1] na kufanya vitendo mbalimbali kama vile kutoa salamu na kusoma Ziyara ya imam Hussein (a.s) [2]. Kwa mujibu wa Hadith mbalimbali zilizopokelewa kutoka Kwa Mtume Muhammad (s.a.w) [3] na maimamu wa Mashia,[4] miongoni mwa matendo bora na yenye fadhila nyingi sana ni kuzuru kaburi la Imam Hussein (a.s) lililopo katika mji wa Karbala.[1] Miongoni mwa fadhila za kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) zilizotajwa katika vitabu vya hadithi ni : kumzuru Imam Hussein kunamfany mtu awe karibu zaidi na Mtume Muhammad (s.a.w), Imamu Ali na bibi Fatimah (a.s), Mtume Muhammad (s.a.w) na maimamu wote huwaombea Dua njema mazuwari wa imam Hussein (a.s), [5].

Historia fupi

Vyanzo mbalimbali vya Mashia, imenakili kuhusiana na nafasi au Umuhimu wa eneo la Karbala ( alipouwawa imam Hussein ) hata kabla ya Uislamu, [8] Kwa mujibu wa Moja ya hadithi zilizopokelewa, imam Ali (a.s) alipokuwa akirudi kutoka vita vya seffain alipita eneo la Karbala na kukumbuka tukio la Ashura na kumlilia mwanae imam Hussein (a.s). [9] Kwa mujibu ya wanahistoria, Jabir bin Abdullah Answari Alikua mtu wa kwanza aliyefika Karbala baada ya Imamu Husein (a.s) kuuwawa shahidi, Baadhi ya watu pia wanamchukulia Obaidullah bin Har Jafi kama mtu wa kwanza aliyezuru kaburi la imam Hussein (a.s) [12]. Mauzi na usumbufu wa utawala wa Banu Umayya Kwa mazuwari wa imam Hussein, haukuzuia watu kwenda kulitembelea kaburi la Imamu Husein (a.s.) [13] Uqbah bin Amr Sahmi, mwana mashairi wa lugha ya Kiarabu, aliingia Karbala mwishoni mwa karne ya kwanza hijriya kwa ajili ya kumzuru imam Hussein na kuimba mashairi ya maombolezo.[14] Licha ya ukali wa Banu Umayya Kwa ahlulbait, kaburi la imam hussein (a.s) halikuharibiwa, lakini baadhi ya makhalifa wa Abbasiyah, akiwemo Harun al-Rashi na Mutawakkel, walichukua hatua za kuharibu kaburi la Imam Hussein (a.s.), ili kufuta athari za kaburi hilo na kuzuia watu kuzuru eneo hilo takatifu.[15] Kwa upande mwingine, wakati wa utawala wa Al-Buyeh, Jalairian, Safavid na Qajar, hatua za kimsingi na za kina zilichukuliwa kwa ajili ya maendeleo, ujenzi na upambaji wa kaburi la imam Hussein.[16] Wanahistoria kama vile Ibn Battuta (aliyefariki 703 AH) alizungumzia kuhusiana na kuzuru kaburi la Imamu Hussein (a.s.) na ugawaji wa chakula Kwa mazuwari wa imam katika eneo hili tukufu [17] Ibn Sabbagh (aliyefariki 855 AH) pia amesimulia kuhusiana na Ziyara ya idadi kubwa ya watu katika Karne ya 9 hijriya.[18]

Adabu za Ziyara

Mwanahadithi wamepokea Hadithi nyingi sana ambazo zimejaribu kueelezea kuhusiana na adabu ya Ziyara ya Imam Hussein(a.s), Kwa mujibu wa hadithi hizi, kujua ukweli kuhusiana na Imam Hussein, ikhlasi, uwepo wa moyo na huzuni ni miongoni mwa adabu za kibatwini za ziyara, na kuoga/kufanya khusli ,[19] kuvaa nguo safi ,[20] kutumia manukato na mapambo, [21] Kuomba ruhusa kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (s.a.w) na Ahlul-Bayt Kwa ajili ya kuingia katika Haram ya imam, [23] na pia kusoma Ziyara mbali mbali kama vile Ziyarat Jamia Al-Kabira ni baadhi ya adabu zahiri. [24] Kwa mujibu wa riwaya kutoka katika kitabu cha Kamel al-Ziyarat, Imam Sadiq (a.s) aliamuru kuswali rakaa mbili karibu na kaburi la Imam Hussein (a.s),ambapo katika rakaa ya kwanza husomwa Suratul Hamad na Yasin na katika rakat ya pili husomwa Suratul Hamad na al-Rahman [25] Nyakati maalum za Ziyara Katika hadithi mbalimbali zilizopokelewa na Mashia, imependekezwa zaidi kusoma ziyara ya Imam Hussein (a.s) katika siku mbalimbali kama vile siku ya Arafah, [26] siku ya Ashura, [27] Tarehe 15 ya Sha’ban, [28] na katika mwezi wa Rajab.[29]

Kisomo Cha Ziyara

Katika vyanzo vya Hadithi vya Mashia, kuna Ziyara nyingi sana kwa ajili ya kusoma wakati wa kutembelea kaburi la Imam Hussein (a.s) [30] miongoni mwa Ziyara hizo ni Ziyara ya warith,[32] Ziyara ya Ashura, [34] Ziyara ya Rajabiyeh, [35] na Ziyara za usiku za Qadr. [36]

Kwenda Ziyara ya Imam Hussein kwa miguu

Makala kuu: kwenda Ziyara ya Imam Hussein (a.s) Kwa miguu. Kuna Riwaya mbalimbali kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s) kuhusiana na kwenda kumzuru Imamu Husein (a.s) kwa miguu.[37] Hadithi mbalimbali zimepokelewa katika vitabu vya Mashia vikisema mwenye kuenda kuzuru kaburi la Imam Hussein kwa miguu husamehewa madhambi yake. Imepokelewa kutoka Kwa imam swadiq (a.s) akisema mwenye kutoka Kwa ajili ya kwenda kutembelea kaburi la Imam Hussein Kwa miguu basi ataandikiwa dhawabu Kwa kila hatua ambayo atakayoichukua.[38] Sheikh Tusi amesema katika kitabu cha Tahzeeb Al-Ahkam kwamba zuwari wa imam Hussein anaporudi kutoka kwa Imam kwa miguu, Malaika humwambia. Kuhusu neno la Mungu; Anza upya kwani madhambi yako yote uliyafanya yamesamehewa.[39] Leo hii, matembezi ya Arbaeen ni miongoni mwa mila ya Mashia ambayo hufanywa kila mwaka wakati wa maombolezo ya Arbaini ya Hosseini . Tamaduni hii, inayohudhuriwa na mamilioni ya watu, inachukuliwa kuwa msafara au mkusanyiko mkubwa zaidi ulimwenguni.[40]

Kufanya ziyaza ukiwa mbali

Inapendekezwa kwa mtu ambaye hana uwezo wa kufika karbala Kufanya ziyara ya Imamu Husein (a.s.) akiwa mbali. [41] Katika aina hii ya Ziyara, inapendekezwa kuoga/kufanya khusli ya Ziyara, kuvaa nguo safi, na pia kusoma ziyara katika sehemu kama vile paa ya nyumba au jangwani.[42] Pia inajuzu kusoma Sala ya Ziarat, kabla au baada yake. Imepokelewa kutoka kwa imam swadiq (a.s) akisemu mtu mwenye kufanya khusli ya Ziyara akiwa nyumbani kwake kisha akamtolea salamu imam hussein basi huandikiwa thawabu ya sawa na mtu ambaye amemzuru imam katika kaburi lake. [44]