Nenda kwa yaliyomo

Jawahir al-Kalam (kitabu)

Kutoka wikishia
Jawahir al-Kalam fi sharh shara’i al-Islam

Jawahir al-Kalam fi sharh shara’i al-Islam au Jawahir al-Kalam (Kiarabu: جواهر الكلام أو جواهر الكلام في شرح شرائع الإسلام) ni kitabu kilichoandikwa na Muhammad Hassan al-Najafi (1202-1266 AH). Kitabu hiki kinatoa sharh na ufafanuzi wa kitabu cha Shara’i al-Islam kilichoandikwa na Muhaqqiq al-Hilli. Miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa sifa maalumu za kitabu hiki ni kuwa kamili kozi ya fikihi, tathmini, uchambuzi, kujengea hoja, kutoa mitazamo tofauti tofauti ya kifikihi katika kila mas’ala na lugha na fasihi nyepesi iliyotumika humo. Kumeandikwa risala na vitabu kadhaa vya kukifafanua kitabu hiki cha Jawahir al-Kalam.

Miongoni mwa mitazamo makhsusi na maalumu ya Najafi katika kitabu hiki ambayo tunaweza kuiashiria ni: Sio lazima kwa kadhi kufikia daraja ya ijtihadi, inajuzu mwanaume kusikiliza sauti ya mwanamke (kinyume na mtazamo mashuhuri) na kuwa na wigo mpana mamlaka ya mtawala wa kisheria wa Kiislamu (fakihi aliyetimiza masharti). Kwa mara ya kwanza kitabu hiki kilichapishwa katika zama za uhai wa mwandishi kikiwa katika muundo wa lithografia.

Nafasi ya Kitabu

Jawahar al-Kalam fi Sharh Shari'i al-Islam ni mojawapo ya vitabu vyenye maelezo ya kina ya Fiqh Istidilal (fikihi ya utoaji hoja) ya Shia kilichoandikwa na Muhammad Hassan al-Najafi, mmoja wa Mujtahidi na Marajii Taqlid wa karne ya 13 Hijria. [1] Agha Bozorg Tehrani anasema kuwa, Jawahar al-Kalam ni kitabu cha kina kinachoshughulikia fiqhi kuanzia mwanzo hadi mwisho. [2] Vile vile ameeleza kuwa ni kitabu chenye uchanganuzi sana, [3] chenye hoja na sahihi. [4] Mohsen Amin amemnukuu Sheikh Ansari katika kitabu cha A’yan al-Shia kwamba, vitabu viwili Jawahir na Wasail pamoja na baadhi ya maandishi ya wanasheria ni ya kutangulizwa na vinatosha kwa ajili ya ijtihadi. [5] Amin amekitambua kitabu cha Jawahir al-Kalam kwamba, daima kilikuwa tegemeo la Mamujitahidina na wanafunzi wa masomo ya dini. [6] Murtadha Mutahhari amekitaja kitabu cha Jawahir al-Kalam kwamba, ni ensaiklopidia ya Maarifa ya Fikihi ya Shia [7] ambacho hadi sasa hakuna fakihi ambaye hana haja nacho. [8] Ayatullah Khomeini, Marjaa Taqlidi wa karne ya 14 na Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kubuni neno la Fiqh ya Jawahir [9], alikuwa akizishauri Hawza kufanya fiqhi ya Jawahiri kuwa msingi wa masomo yao ya sheria (Fikihi) [10] na kuiimarisha [11] na alikuwa akiona kuwa haijuzu kuikhalifu. [12].

Sababu ya Kukiandika

Najafi ameandika katika utangulizi wa Jawahir; kwa kuzingatia kuwa, kitabu cha Shara’i al-Islam ni jumuishi, makini, sahihi na kilikuwa kigezo cha mafaqihi, aliamua kuandika maelezo kuhusu kitabu hiki ili kufichua mambo yake muhimu na yenye manufaa yaliyofichika, kuripoti makosa ya wafasiri wake, na kwa kueleza vyema yaliyomo na kutaja mitazamo mbalimbali ya kifiqhi na hoja zao. [13] Muhammad Harz al-Din (1273-1365 AH) ameandika katika Ma'arif al-Rijal kwamba, awali Sahib Jawahir hakukusudia kuandika ufafanuzi juu ya Shara’i; bali alitaka tu kuandika maoni ya mafaqihi juu ya masuala ya kifiqhi kwa matumizi binafsi; Lakini wanafunzi wake walipata nakala zake na huu ukawa ndio msingi na mwanzo wa kuandikwa kitabu hiki. [14] Kwa mujibu wa Sahib al-Jawahir mwenyewe, kitabu cha Jawahir kilimalizika usiku wa Jumanne, tarehe 23 Mwezi wa Ramadhani kuanzia masiku ya Qadr katika mwaka 1254 Hijiria. [15]

Maudhui

Kitabu cha Jawahir al-Kalam kina muundo sawa na Sharia'i al-Islam; maudhui zake zimegawanywa katika sehemu kuu nne za ibada, [16] mikataba, [17] Iqaat (mkataba wa upande mmoja ambao unatimia tu kwa kauli ya pendekezo na hakuna haja ya qabul (kukubali) [18] na hukumu [19]. Kitabu cha Jawahir kinaanza maudhui ya tohara na mjadala kuhusu maana ya kitabu na neno tohara na kuhitimisha kwa maudhui ya dia katika fremu ya masuala matano. Madhumuni ya masuala yanayohusiana na hukumu ya dia ya Mwislamu kwa asiyekuwa Mwislamu na kinyume chake. [20]

Sifa Maalumu

  • Kozi kamili ya fikihi. [21]
  • Katika kunukuu hadithi, aghalabu hakujatajwa vyanzo na mlolongo wa mapokezi yake. Hadithi zimetajwa tu kwa anuani kama vile Sahihein, yenye itibari, hasanu, ya kuaminika, mursala na dhaifu. [23]
  • Katika hadithi ndefu aghalabu kumetajwa kipande na sehemu inayohitaji. [24]
  • Kutoa mitazamo tofauti ya mafakihi. [25]

Ukosoaji

Katika baadhi ya matukio, sanadi na mapokezi ya hadithi yameripotiwa kimakosa au hadithi moja imechanganywa na hadithi nyingine, pamoja na ibara kadhaa za kifiqhi zimedhaniwa kuwa mi hadithi zinazodhaniwa kuwa ni hadithi, au katika baadhi ya matukio mrejesho wa mwandishi kwenye yaliyotangulia au ya baadaye ya kitabu hiki si sahihi. Sababu ya makosa haya ni nukuu ya hadithi kwa njia isiyo ya moja kwa moja na mitazamo ya wanachuoni. [26]

Mitazamo Maalumu ya Kifiq’h na Kiusul

  • Kutokuwa lazima suala la ijtihadi kwa ajili ya kadhi. [27]
  • Kujuzu mwanaume kusikia sauti ya mwanamke (kinyume na mtazamo mashuhuri). [28]
  • Kutotosha muatat (muamala ambao ndani yake mnunuzi na muuzaji wanaweza kufanya muamala wao bila ya kuweko mkataba maalumu) katika muamala. [29]
  • Kuwa na wigo mpana mamlaka ya mtawala wa kisheria wa Kiislamu (Hakim Shari’). [30]

Mbali na maoni ya kifiqhi, baadhi ya mitazamo ya usul ya Najafi imejumuishwa katika kitabu cha Jawahir, ambayo kutokana na kupotea kwa kitabu chake cha Usul, hilo limepelekea wasomaji kufahamu mitazamo yake katika uga huo. Miongoni mwao ni upinzani wake mkubwa dhidi ya umakini wa kifalsafa na kiakili katika kunyambua hukumu. [31] Pia alitilia maanani sana umashuhuri wa kifatwa; ni kwa sababu hii, maoni yake mengi katika Jawahir yanawiana na makubaliano ya wanazuoni au mitazamo maarufu ya Shia. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana, baadhi ya mafaqihi wamemwita «ulimi maarufu» (msemaji wa maoni maarufu). [32]

Maelezo na Dondoo

  • Al-Insaf fi tahqiqi Masail al-Khilaf min Jawahir al-Kalam; mwandishi: Muhammad Taha Najf Tabrizi aliaga dunia (1323 AH).
  • Bahr al-Jawahir; mwandishi Ali bin Muhammad Baqir Burujani kwa lugha ya Kifarsi (kitabu hiuki kiliandikwa mwanzoni mwa karne ya 14 Hijria).
  • Al-Hidayah ila al-Maram min Mubhamat Jawahir al-Kalam; kimeandikwa na Sayyid Muhammad Baqir Musawi Hamadani. [33]

Sayyid Hussein Burujerdi, Sayyid Adul-Ali bin Jafar Khunsari, Sayyid Abdallah Bahbahani, Mulla Ali Kani na Zaynul-Abidin Mazandarani wameandika maelezo na dondoo kuhusiana na kitabu hiki. [34]

Nakala na Uchapishaji

Agha Bozorg Tehran anasema, nakala asili ya Jawahir al-Kalam ilisahihishwa na Sahib al-Jawahir mwenyewe. [39] Nakala hii ina juzuu 44 ndogo na ingali inapatikana hadi leo. [40] Baadhi ya nakala zilizoandikwa kwa mkono pia zinapatikana katika maktaba za Najaf, Qom, Tehran, Mash’had na Hamadan. [41] Nakala ya kwanza ya kitabu hiki ilichapishwa 1264 Hijria katika zama za uhai wa mwandishi wake kwa muundo wa lithografia.

  • Chapisho kubwa katika mijadala 15 (Beirut 1992).
  • Chapisho la Taasisi ya Uchapishaji ya Kiislamu kwa sura ta uhakiki. [42]

Bibliografia

  • Ashenai ba Fiqh Javaheri, mwandishi Abdallah Omidfard. Mwaka 1385 Hijria Shamsia kitabu hiki kilichapishwa na Taasisi ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Qum.

Rejea

Vyanzo