Nenda kwa yaliyomo

Mafatihu al-Jinan

Kutoka wikishia

Mafatihu al-Jinan (Kiarabu: مفاتيح الجنان (كتاب)) (maana yake ikiwa ni Funguo za Mabustani ya Peponi) ni kitabu maarufu sana cha dua miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Kitabu hichi kimeandikwa na Sheikh Abbas Qumi (aliye zaliwa mnamo mwaka 1294 na kufariki 1359 Hijiria). Kitabu hiki kinajumuisha ndani yake mkusanyiko wa dua, ziara (sala na salamu za taadhima kwa watu maalumu), matendo maalum ya ibada kwa siku na miezi mbalimbali, na desturi za kidini ambazo zimenukuliwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Maimamu wa Kishia, pamoja na amali zilizo ripotiwa kutoka kwa wanazuoni. Mwandishi wa Mafatihu kwa kiasi kikubwa amenukuu matini ya kitabu hichi kutoka kwenye vitabu vilivyotangulia kabla yake, kama vile; Eqbal kilichoandikwa na Sayyid Ibn Tawus, Misbaah kilichoandikwa na Kaf'ami, na Zadu al-Ma'ad kilichoandikwa na Allamah Majlisi. Maandishi ya dua na ziara kitabuni humo, yameandikwa kwa lugha ya Kiarabu, na mwandishi ametoa maelezo yake kwa lugha ya Kiajemi mwanzoni mwa baadhi ya dua zilizomo kitabuni humo.

Mafatihu kwa mara ya kwanza kabisa kilichapishwa mjini Mashhad mwaka wa 1344 Hijiria na kupata umaarufu haraka mno ndani ya jamii za Mashia. Kitabu hichi ni kitabu kinachopatikana katika nyumba na maeneo matakatifu yote takriban ya Waislamu wa Shia nchini Iran. Mara nyingi kitabu Mafatihu al-Jinana, kimekuwa ndio marejeo kuu na pekee kuhusiana na amali zinazopendekezwa (mustahabu), pamoja na amazli zitendwazo kufuatia matukio na maadhimisho maalumu ya kidini kwa Waislamu wa Shia ulimwenguni kote. Tafsiri maarufu zaidi ya "Mafatihu" kwa Kiajemi, ni ile iliyoandikwa na Mehdi Ilahi Ghomshei. Ayatullah Qommi pia aliongeza matini nyengine katika Mafatih iitwayo Al-Baqiyatu al-Salihat, iliyo jumuisha ndani yake; dua, ziara, na aina kadhaa sala. Mara nyingi ziada hiyo iliyo ongezwa na Ayatullahi Qommi, hupatikana pembeni mwa matini za Mafatihu.

Kuna vitabu vitatu vipya vilivyo andikwa kuhusiana na Mafatihu al-Jinani, viwili kati ya yake ambavyo ni Mafatihu newin na Minhaju al-Hayati viliandikwa kwa na lengo la kutoa hati halali ya nukuu za matini ya kitabu cha Mafatihu al-Jinan, na cha tatu ambacho ni Mafatihu al-Hayati kikiwa na lengo la kukamilisha kitabu Mafatihu al-Jinani. Pia kuna vitabu kadhaa vilivyo andikwa kwa majina mbali mbali kama ni muhtasari wa "Mafatihu al-Jinani".

Umuhimu na utambulisho wa Mafatihu al-Jinani

Muhuri wa ukumbusho wa mwaka wa 100 wa kuandikwa Mafatihu al-Jinani

Mafatih al-Jinan ni kitabu kilichoandikwa katika karne ya 14 Hijria na Sheikh Abbas Qumi, ambaye mwanahadithi wa kutoka upande wa madhehebu ya Shia. Kitabu hichi ni moja ya vitabu maarufu na vinavyotumiwa sana katika kutekeleza ibada ya dua na ziara kati ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika karne ya 14 na 15 Hijria. Waislamu wa Shia na hasa wale wanao ishi nchini Iran, hutumia na kutegemea sana kitabu hichi katika shughuli zao za kidini na katika amali zao zinazo husiana na maadhimisho ya matukio mbalimbali ya kidini. "Mafatihu al-Jinani" ni kitabu kinachofuatia Qur'ani kwa idadi ya kuwa na nakala nyingi, [1] na kulingana na Waziri wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, karibu nakala milioni 28 za kitabu hiki zimechapishwa nchini Iran katika kipindi cha miaka 45. [2] Hii ukiachana na matoleo tofauti yaliochapishwa na baadhi ya wachapishaji, ambapo baadhi yake ni sehemu ya baadhi ya matini zilizochaguliwa na kuchapwa chini ya majina kama vile; "Muntakhabe Mafatihu" au "Gozideye Mafatihu". [3] Mnamo mwezi wa Khordad mwaka 1402 Shamsia (2023 Miladi), kulifanyika maadhimisho ya miaka 100 ya kuandikwa kwa "Mafatihu al-Jinani" yalifanyika nchini Iran maadhimisho yaliopata shindikizo lake kutokana na ujumbe maalumu kutoka kwa Ayatullah Makarem Shirazi, [4] mmoja wa viongozi wa kidini wa pili kwa daraja nchini Iran. [5]

Kuhusiana na mwandishi

Makala asili: Sheikh Abbas Qummi

Sheikh Abbas Qummi (aliyefariki mwaka 1359 Hijiria) ndiye mhariri wa "Mafatihu al-Jinani". Yeye ni mwanazuoni maarufu wa fani ya Hadithi, historia, na wahubiri wa kutoka upande wa madhehebu ya Shia. Sheikh Abbas Qummi ameandika vitabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na; Safinat al-Bihar na Muntaha al-Amal. Mwana fani huyu wa elimu ya Hadithi, amezikwa katika mava yenye kaburi la Imam Ali (a.s) huko Najaf nchini Iraq. [6] Mwanawe akitoa maelezo kuhusiana na baba yake, alisema kwamba; baba yake aliandika kitabu hichi cha Mafatihu al-Jinani akiwa katika hali ya udhu (maandalizi ya usafi wa kidini ya kabla ya kufanya baadhi ya ibada). [7] Sheikh Abbas Qumi aliandika kitabu cha Mafatihu kwa nia ya kuboresha kitabu cha Mafatihu al-Jinani. [Maelezo 1] Kitabu Mafatihu al-Jinani kilikuwa ni maarufu wakati huo, ambapo kilikuwa na dua zisizo na marejeo ndani yake. Yeye aliamua kuliandika kitabu hicho, baada ya baadhi kumwomba atenganishe dua zenye hati thibitisho kutoka katika kitabu "Mafatihu al-Jinani" kisha aziambananishe na dua nyingine zenye hati halali na kuzijumuisha katika kitabu kimoja. [8]

Wasifu wake

Mafatih al-Jinan ina jumuiko moja kuu lililogawanyika katika sura tatu, nazo ni: dua, amali za kila mwaka, na ziara. Pia kuna sehemu iliyo ongezwa lijulikanayo kama Mulhakaat (viambatisho) na jengine liitwalo Baqiyatu al-Salihat (mavuno mema yaliyobaki). Maongezeko haya yaliongezwa na mwandishi mwenyewe. Sheikh Abbas Qummi hajaweka marejeo (hati thibitisho) kuhusiana na nukuu za dua na matini ya kitabu hicho, bali ametosheka kwa kuelezea chanzo alichotumia katika kunukuu dua hizo. [9] Baadhi ya dua zilizomo katika Mafatihu hazikunukuliwa kutoka kwa Ma'asumina (watoharifu) bali ni dua zilizo andikwa na baadhi ya wanazuoni, ambapo moja wapo ni ile dua ijulikanayo kwa jina la Adilah. [10]

Nyongeza kwa Mafatihi

Sheikh Abbas ili kuzuia wazushi wasije kuweka ongezeko jengine kwenye kitabu chake; aliamuwa kutangaza laana ya Mwenye Ezi Mungu, Mtume wake pamoja na Ma'imamu wa Ahlul Bayt (a.s) kwa mtu yeyote atakaye engeza kitu chochote kile kwenye kitabu cha Mafatihu al-Jinani. [11] Hata hivyo baadaye, baadhi ya wachapishaji wa Mafatihu waliongeza sehemu nyengine kitabuni humo, iliyopewa jina la Mulhakaat Dovvom Mafatihu, yaani nyongeza ya pili ya Mafatih. Sehemu hii inajumuisha dua ya baada ya Sala ya Imam Hussein (a.s) na Imam Jawad (a.s) na Hadithi ya Kisaa. [12] Baadhi ya wachapishaji pia wameongeza sehemu mbili kwenye mlango wenye dua za Baqiyatu al-Salihatu. Kwa hiyo, mkusanyiko wa Mafatih al-Jinan katika umbile jipya hilo, imekuwa na sehemu sita, ambapo tatu zimeandikwa na Sheikh Abbas Qumi, ambazo ni: sehemu ya msingi ya Mafatih, Mulhakaat Mafatihu, na Baqiyatu al-Salihat, pamoja na sehemu tatu zilizo ongezwa baadaye, ambazo ni: Mulhakaat Dovvom Mafatihu, Mulhakaat Awwal Baqiyatu al-Salihat, na Mulhakaat Dovvom Baqiyatu al-Salihat. [13]

Muundo na maudhui zake

Kawaida, mwanzoni mwa kitabu cha Mafatihu al-Jinani, kuna sura kadhaa za refu na fupi za Qur'an, ambazo huwekwa kabla ya kuingia katika maudhui zilizomo kitabuni humu. [Maelezo 2]. Maudhui za Mafatihu al-Jinani zimepangwa na kugawanywa katika milango kadhaa kama ifuatavyo:

Mlango wa kwanza: Dua

Mlango huu unajumuisha maudhui kama vile:

Taaqibaati (amali za baada ya sala za wajibu): amali za usiku na mchana, na ibada za siku za wiki. Sala maarufu na maalumu: Kama vile Sala ya Mtume (s.a.w.w), na Sala ya Amir al-Muuminina (a.s), Sala ya bibi Fatimah (a.s), Sala ya Ja'afar Tayyar, na Ziara za Maimamu katika siku za wiki. Dua na Munaajaati (Maombi ya kujipendekeza): Miongoni mwa dua na maombi yilizomo ndani yake ni; Munajaatii Khamsatu ‘Ashara kutoka kwa Imam Sajjad (a.s), Munajaati Imam Ali ambayo ni maombi yake katika Msikiti wa Kufa, Dua al-Samaati, Dua Kumail, Jushan Sagheer na Jushan Kabir, Dua Makarimul Akhlaq, na zingine nyinginezo.

Mlango wa Pili: Ibada za Kila Mwaka

Malango huu umeandaliwa ili kufafanua amali zilizopendekezwa kutendwa katika mwaka mzima wa Kiislamu. Maudhui ya sehemu hii huanza na matendo yapaswayo kutendwa ndani ya mwezi wa Rajabu, kisha amali za mwezi wa Jamadi al-Thani, na kisha kumalizikia na amali za Nowruz (Mwaka Kogwa) na miezi ya Kirumi. Maudhui zinazo fuata katika mlango huu ni: Manaajaati Sha'abaniyya, dua ya Abu Hamzah Thumali, Dua Iftitaah na dua maarufu ya Sahar, amali za Laylatul Qadr katika mwezi wa Ramadhani na dua ya Imamu Hussein siku ya Arafa katika mwezi wa Dhul-Hijjah. Hizi baadhi ya maudhui maarufu zaidi katika mlango huu wa "Mafatih al-Jinan".

Mlango wa tatu: Ziara (taadhima ya sala na salamu)

Mlango huu unaanza kwa ufunguzi wa maelezo juu ya adabu za safari ya ziarah pamoja na namna ya kuomba ruhusa ya kuingia katika maeneo mtakatifu. Ziarah ya kwanza katika mlango huu, ni ziarah ya bwana Mtume (s.a.w.w), baada yake ni ziarah ya bibi Fatima (a.s), kisha ni ziarah za Maimamu waliozikwa katika mava ya Baqii. Mbali na ziara za Maimamu kumi na mbili, mlango huu pia unajumuisha ndani yake ziarah za mawalii kadhaa ambao ni watoto na wajukuu Maimamu pamoja na baadhi ya wachamungu maarufu na wanazuoni wa Kishia, kama vile; ziarah ya Hamzah bin Abdulmuttalib, Muslim bin Aqil, Fatima bint Asad, mashahidi wa Vita vya Uhud, Salman al-Farsi, na wengineo. Pia mlango huu unajumuisha ibada zinazofanyika katika miskiti maarufu, kama vile Msikiti wa Kufa, na Msikiti wa Sa'da.

Sehemu refu zaidi ya sura hii imetawaliwa na ziarah ya Imamu Hussein (a.s). Ziarah maarufu za Imamu Hussein (a.s) zilizoko katika mlango huu ni kama vile; Ziaratu Ashura, Ziaratu al-Arba'iin, na Ziaratu al-Warith. Pia katika mlango huu kuna idadi ya amali zinazo husiana na Imamu Zamani (Mahdi) (a.f), ambazo ni; Dua ya Nudba, Dua ya Ahad, na Ziaratu Jamiatu al-Kubra. Baada ya ziara za Imamu Mahdi (a.f), pia kuna ziarah nyengine kadhaa ndani yake ambazo ni; Ziara za Manabii, Ziara ya bibi Fatima Ma’asumah (a.s), na Ziara ya Walii Abd al-Azim al-Hasani. Maudhui ya mwisho katika mlango huu, ambayo ndiyo sehemu ya mwisho ya toleo (chapa) la mwanzo la “Mafatihu al-Jinani”, ni mada inayohusiana na ziara za makaburi ya waumini na dua zinazohusiana na amali hiyo.

Viambato vya ziada vya Mafatih al-Jinan

Sheikh Abbas Qommi katika toleo la pili la Mafatihu al-Jinani aliweka sehemu nyongeza yenye jina la Mulhaqaatu (viambato), katika kitabu hicho. [14] Sehemu hii ina vifungu nane ambavyo kwa mujibu wa mawazo ya mwandishi; aliamini kuwa watu walikuwa na haja nyongeza hizo. Vifungu hivi nane ni kama ifuatavyo:

Baqiyatu al-Salihat

Baqiyatu al-Salihat ni kitabu kilichoandikwa na Sheikh Abbas Qommi ambaye mwenyewe alikiandika na kukiambatanisha na Mafatihu al-Jinani, ikiwa ni kama maelezo fafanuzi ya pembeni mwa kitabu. Kulingana na maelezo ya Sheikh Abbas Qommi, sehemu hii ilikamilishwa siku ya Ijumaa, tarehe 19 Muharram, mwaka 1345 Hijiria. [16] Katika matoleo mbalimbali ya "Mafatih al-Jinan," kitabu hichi kilichapwa sambamba kikiwa kimeambatanishwa pamoja na “Mafatihu”. Kitabu hichi kina sehemu sita pamoja na viambato vya ziada, sehemu sita hizo ni:

  1. Sura ya kwanza: Maelezo juu ya amali na adhkaar kuhusu maisha ya kila siku, dua za nyakati tofauti za siku nzima na jinsi ya kusali Sala za Usiku (Salatu al-Laili).
  2. Sura ya pili: Mafundisho ya baadhi ya Sala zilizopendekezwa; ambazo ni Sala ya zawadi kwa Ma'asumiin, Sala ya Usiku wa Mazishi, Sala za kuomba haja, Sala za kuomba wokovu, na Sala za siku za wiki. Sheikh Abbas Qommi pia ameeleza aina tofauti za Istikhara na jinsi ya kuomba mwongozo katika sura hii ya pili ya kitabu hichi.
  3. Sura ya tatu: Dua na kinga kwa ajili ya maumivu na magonjwa, ambapo dua za kuponya maumivu na magonjwa mbalimbali zimeelezwa ndani yake.
  4. Sura ya nne: Dua zilizochaguliwa kutoka kitabu cha al-Kafi. Dua zaidi katika sehemu hii zinahusiana na kutatua matatizo kama vile; uhaba wa riziki na mahitaji ya kidunia.
  5. Sura ya tano: Orodha ya dua fupi na Aya za kinga zilizochaguliwa kutoka kitabu cha Muhaj al-Da’awaat na Al-Mujtanaa. Katika sehemu hii, kuna dua (herizi au kinga) za kujikinga na majanga, na pia ndani yake mna sala na dua kadhaa zinazohusiana na kipato cha riziki.
  6. Sura ya sita: Maelezo na ufafanuzi juu ya sifa za baadhi ya Surah na Aya za Qur'ani, pamoja na nyiradi, baadhi ya dua na mada kadhaa mbalimbali. Katika surah ii pia kumetajwa faida za baadhi ya Aya za Qur'ani na Surah zinazotumika katika kutatua matatizo ya kila siku, dua kwa ajili ya kuwaona watu fulani ndotoni, dua kwa ajili ya kutalii vitabu, sharti za aqiqi (kichinjwa kama ni kafara ya mtoto aliye zaliwa) na istikhara (kumwoba Mungu ushauri) kupitia Qur’ani.
  7. Hitimisho: Maelezo kwa ufupi kuhusiana na hukumu za maiti

Vyanzo vya vitabu

Baadhi ya vyanzo vilivyo tumiwa na Sheikh Abbas Qommi katika uandishi wa Mafatihu al-Jinani alivyo vitaja katika kitabu hicho ni kama ifuatavyo:

  1. Ithbat al-Hudaati kilichoandikwa na Sheikh Harru al-Amili.
  2. Al-Ihtijaaju kilichoandikwa na Ahmad bin Ali Tabarsi.
  3. Al-Ikhtiyaru kilichoandikwa na Ibn Baqi.
  4. Arba'atu Ayyami kilichoandikwa na Mirdaamad.
  5. Al-Azriyyah maarufu kwa jina la "Ha'iyyah" kilichoandikwa na Sheikh Kadhim Azri.
  6. Alam al-Waraa kilichoandikwa na Sheikh Tabarsi.
  7. Al-Iqbalu kilichoandikwa na Sayyid bin Taawus.
  8. Al-Amali kilichoandikwa na Sheikh Tusi.
  9. Al-Amanu kilichoandikwa na Sayyid bin Tawus.
  10. Bihar al-Anwari kilichoandikwa na Allamah Majlisi.
  11. Balad al-Amini kilichoandikwa na Kaf’ami.

Sheikh Abbas Qommi pia ametaja vyanzo vingine kadhaa katika Mafatihu kama vile Tarikh ‘Alamu Aarayi Abbasi, kilichoandikwa na Mirza Iskandar Beg Munshi, Tuhfat al-Za'ir kilichoandikwa na Allamah Majlisi, Tahdhib al-Ahkami cha Sheikh Tusi, Jami'u al-Akhbari (mwandishi asiyejulikana), na Jamal al-Usbuu’i kilichoandikwa na Sayyid bin Tawus. [17]

Uchapishaji na Tafsiri

Mafatihu Nevin

Sheikh Abbas Qommi aliandika na kuchapisha Mafatihu al-Jinani kwa mara ya kwanza kabisa mnamo mwaka 1344 Hijiria huko Mashhad Iran. [18] Kitabu hichi pia kimesanifiwa na wasanii wakubwa wa hati kupitia fonti (herufi) za kuvutia za Nasakh na Nastaliq, miongoni mwa wasanii hao ni kama vile; Taher Khoshnevis, [19] Misbahzadeh, [20] Mirza Ahmad Zanjani, [21] na Mohammad Reza Afshari [22]. Kitabu cha Mafatihu al-Jinani kimechapishwa katika matoleo tofauti, pia katika vipimo (ukubwa) na sura tofauti. Kutokana na ukubwa wa kitabu hichi, baadhi ya wachapishaji wamechagua baadhi tu ya sehemu za maudhui na kuchapisha kwa jina la Muntakhabu al-Mafatihu au Goziideye Mafatihu.

Tafsiri zake

Maelezo aliyo weka Sheikh Abbas Qommi kwa lugha ya Kifarsi mwanzo wa kila dua, ziara au amali katika kitabu hicho ni ufafanuzi wa dua, ziara na amali hizo. Lakini maandishi asili ya dua, amali na ziara zilzozomo ndani yake, zimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu, ambazo baadae zimekuja kuhaririwa na baadhi ya wafsiri katika lugha ya Kifarsi. Tafsiri maarufu na nyepesi zaidi ya Mafatihu, ni tafsiri ya Mahdi Elahi Ghomshei. Kuna Tafsiri nyingine kadhaa zilizo chapishwa na wafasiri wengine, ikiwa ni pamoja na; tafsiri ya Sayyid Hashem Rasouli Mahallati, [23] Hussein Ostadwali, [24] Muhammad Baqir Kamarei, na wengineo.

Tarehe 9 Juni 2023 (10 Dhu al-Qa'idah 1444 Hijria), kulifanyika mkutano kusherehekea miaka mia moja ya kuandika kwa “Mafatihu”. [25] Katika mkutano huu, lilizinduliwa toleo jipya la kitabu hicho, ambalo limezingatia nakala ilioandikwa kupiti hati za mkono wa Tahir Khoshnevis na kusahihishwa na Sheikh Abbas Qommi. Ndani ya toleo hili mna maelezo kuhusiana na tofauti za nakala, ambapo maelezo yameelezwa ya chini maandishi asili yalioko katika kitabu hicho. Dua zake zimepangwa kwa mtindo wa vipengele, huku kila kipengele kikiwa na namba maalumu. Pia, alama za uandishi kama vile mkato, koma, na nyenginezo zimezingatiwa ndani yake. [26]

Pia Mafatihu imefasiriwa kwa lugha nyingine tofauti kama vile; Kiingereza (kwa kiasi cha tafsiri nne), Kifaransa, Kituruki, Kifarsi, na Kihispania. [27]

Uchambuzi

Kitabu cha Mafituh al-hayyat kilichoandikwa na Muhammadi Yusuf

Uchambuzi wa maudhui pamoja na baadhi ya madai ya Sheikh Abbas Qommi katika kitabu cha Mafatihul Janani umekosolewa na wanazuoni. Kwa mfano, shairi lake maarufu liitwalo Zinda Deli Dar Safe Afsordegane (Moyo ulio hai katika safu ya walio kata tamaa) lilioandikwa na Jami, [28] amablo limehusishwa na Nidhami. [29] Pia, Sayyid Nasir Makarim Shirazi katika utangulizi wa kitabu Mafatihu Nevin (Mafatihul Jannah Mpya) alielezea sababu kadhaa ambazo zilizopelekea kufanya marekebisho makubwa katika kitabu hicho, ikiwa ni pamoja na kurekebisha mapungufu, kuongeza hati za ushahidi na vyanzo vya dua na ziara, kuzingatia mazingira ya nyakati na mahali, na kuondoa mambo ambayo ni chanzo cha machocheo kwa watu waovu. [30]

Vitabu vinavyohusiana

Mafatihu Nevin

Mafatihu Nevin (Mafatihu al-Jinani Mpya): Ni kitabu kilichoandikwa na Nasir Makarim Shirazi. Kitabu hichi kilikusanywa na kuchapishwa kwa lengo la kutoa hati halali za nukuu za matini, kuthibitisha, na kukamilisha kitabu cha “Mafatihu al-Janani”. [31] Ayatullah Makarim, anaamini kwamba; msukumo wake wa kuchapisha kitabu hichi ni kuzingatia kuchunga na kuzingatia wakati na zama, pia kuondoa mambo ambayo yamesababisha malalamiko, ukosoaji na kuzua maswali mbali mbali. [32] Kulingana na mwandishi, kuongezwa kwa utangulizi kwa kila sehemu ya dua na ziara, kutaja vyanzo na ushahidi na ithibati za dua na ziara ya chini yake, kuondoa baadhi ya amali zinazojirudia mara kwa mara, kuondoa mambo yenye kauli dhaifu, kuzingatia usahihi wa maudhui ya dua na ziara na kuto tosheka tu na usahihi wa hati katika uchaguzi wao katika uandishi wa kitabu hicho, ni sifa za kazi hii. [33]

Minhaju al-Hayati fi al-Ad’iyati wa al-Ziaaraati

Mafatihu al-hayyat

Kitabu hichi ni kazi ya Muhammad Hadi Yusufi Gharawi, ambacho kimechapishwa na Majma’a Jihani Ahlu al-Bait. Kitabu hichi kimefanya kazi ya kinachunguza uhalali wa hati za dua na ziara zinazopatikana katika kitabu cha Mafatihu al-Jinani [۳۴] Pia kitabu hichi kimefanya kazi ya kupeta na kunyoosha hati halali za dua na ziara za Mafatihu al-Jinani na kuondoa baadhi ya dua na ziara, kisha kuweka dua na ziara mbadala ndani. Kazi nyengi muhimu iliofanya katika kitabu hichi, ni kuweka vyanzo sahihi vya dua na ziara pamoja na marejeleo ya vyanzo vya kihistoria katika baadhi ya matukio kuhusiana na matini za Mafatihu al-Jinani. [۳۵]

Mafatiihu al-Hayati

Kitabu hiki kiliandikwa na kikundi cha watafiti, chini ya usimamizi wa Abdullahi Jawadi Amuli. Yeye amekihisabu kitabu hichi kuwa ni juzu ya pili ya kitabu Mafatihu al-Jinani. Pia yeye amesema kuwa; lengo hasa la kuandika kitabu hicho, ni kutoa mafunzo kwa watu namna ya kuishi maisha ya Kiislamu. [36] Watafiti wa kitabu hichi wamejitahidi kuandika kulingana na zama hali halisi ya ulimwengu wa hivi sasa ulivyo, hizi ndio sifa muhimu zinazokipamba na kukipa shani kitabu hichi. [37]

Maelezo

  1. Kulingana na maelezo ya Sayyid Yahya, Imamu Mkuu wa mji wa Mashhad, mwandishi wa kitabu hichi ni Sheikh Asadullah Tehrani Hairi (aliyafariki mwaka wa 1933 Miladia huko Mashhad). Naye alikuwa ni mwanafunzi wa Sheikh Murtadha Ansari naye alipata bahati ya kuishi umri mrefu (miaka 120). Katika kitabu kiitwacho Fawaidu Riḍhawiyyah, imeelezwa kwamba; yawezekana kuwa yeye alikuwa ni mkazi wa Borujerd na kazi yake ilikuwa ni kuhubiri dini, pia ni maarufu kwa uaminifu wake. (Rejea kitabu cha Agha Bozorge, Tehrani, al-Dharīʿah, juzuu ya 21, ukurasa wa 324). Katika kitabu cha Fawaidha Riḍawiyyah cha Sheikh Abbas Qommi, chini ya jina Asadullah bin Abdullah al-Borujerdi, hakuna maelezo yoyote yale kuhusiana na Mafatihu al-Jinani.
  2. Katika matoleo na machapisho tofauti ya kitabu hicho, Sura za Qur’ani zilizomo kitabuni humo, zinaweza kutofautiana. Kwa ujumla, Sura kama vile; Yasin, Al-Rahman, Waaqiah, Ankabut na Nuur ni Sura zinapendekezwa kusomwa katika nyakati tofauti, ikiwa ni pamoja na usiku wa kuamkia Laylatul-Qadr

Rejea

Vyanzo

  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Mafātīḥ-i nuwīn. Qom: Intishārāt-i Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib, 1390 Sh.
  • Qummī, ʿAbbās. Mafātīḥ al-jinān. Translāted to Farsi by Ḥusayn Anṣārīyān. Qom: Dār al-ʿIrfān, 1388 Sh.
  • Sulṭānī, Muḥammad ʿAlī. 1389 Sh. "Ishāra bi pāriʾī az manābiʿ Mafātīḥ al-jinān." Kungira-yi Buzurgdāsht-i Muḥaddith-i Qummī.
  • Ṭāliʿī, ʿAbd al-Ḥusayn. 1389 Sh. "Sālshumār-i ḥayāt wa āthār-i muḥaddith-i Qummī." Kungira-yi Buzurgdāsht-i Muḥaddith-i Qummī.