Nenda kwa yaliyomo

Dua Makarim al-Akhlaq

Kutoka wikishia
Kitabu cha Sahifat al-sajadiyah ambacho ndani yake kunapatikana Dua Makarim al-Akhlaq

Dua ya Makarim al-Akhlaq (Kiarabu: دعاء مكارم الأخلاق): Dua ya tabia njema au dua ya 20 ya al-Sahifa Sajadiyya ni katika dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) ambamo ndani yake anamuomba Mwenyezi Mungu amsaidie kujipamba kwa sifa na tabia njema na kufanya mambo mazuri na wakati huo huo anamuomba msaada Allah amuepushe na mambo machafu ya kimaadili. Maombi ya dua hii yanajumuisha mambo ya kimaadili (Kiakhlaq) katika mihimili miwili ya akhlaq za mtu binafsi na ya jamii. Katika dua hii Imamu Sajjad (a.s) ameashiria vizingiti na mambo yanayomzuia mtu kukwea na njia za kuokoka kwake na shari ya ushawishi wa shetani.

Mwanzoni mwa dua sehemu kubwa ya vipengee vyake kumekaririwa salawat (kumswalia Mtume na Aali zake) na baada ya hapo Mwenyezi Mungu anaombwa ambapo sababu ya kukariri huku imeelezwa na kutambuliwa kuwa ni kuifanya dua ikaribie kujibiwa. Dua ya 20 katika kitabu cha al-Sahifa al-Sajjadiyya kutokana na kuwa ndani yake kuna mafundisho ya kuwajenga (kiroho) wanadamu kwa ajili ya kuchuma maadili mema, kufanya amali njema na mambo yafaayo imetambuliwa kwa jina la Dua ya Makarim al-Akhlaq (Dua ya tabia njema).

Dua ya Makarim al-Akhlaq imetolewa maelezo na ufafanuzi na Muhammad Taqi Falsafi, Misbah Yazdi na Ruhullah Khatami kupitia darsa za akhlaq na kuchapishwa vikiwa vitabu vinavyojitegemea. Kadhalika dua hii imefafanuliwa katika fafanuzi zingine zilizotolewa kuhusiana na al-Sahifa al-Sajjadiyya kama vile Diyar Ashiqan ya Hussein Ansariyan na Riyadh al-Salikin ya Sayyid Ali Khan Madani.

Umuhimu na Nafasi Yake

Dua ya 20 katika kitabu cha al-Sahifa al-Sajjadiyya kutokana na kuwa ina mafundisho ya kuwajenga (kiroho) wanadamu kwa ajili ya kuchuma maadili mema, amali njema na mambo yafaayo imeondokewa kuwa mashuhuri kwa jina la Dua Makarim al-Akhlaq, yaani dua ya tabia njema. [1] Katika dua hii, Imamu Sajjad anataja orodha kubwa ya mambo machafu ya kimaadili na dhambi. Kadhalika anataja orodha ya mambo mema na tabia njema ambazo anamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie ajipambe nazo. [2]

Kutumia Imamu Sajjad (a.s) maneno ya kifasihi na kuteua mafahimu na maneno yanayooana na muhtawa na yaliyomo ndani yake ni miongoni mwa sifa maalumu za dua hii. [3]

Kukaririwa Kumswalia Mtume Mwanzoni mwa Vipengee vya Dua

Kumswalia Mtume Muhammad na Aali zake katika dua ya Makarim al-Akhlaq kumekaririwa mara 20 na kila mara baada ya kumswalia Mtume kumebainishwa matakwa mapya. [4] Kuanza dua kwa kumswalia Mtume kumetambuliwa kuwa ni katika Sunna na ada zilizotoka katika sira na mwenendo wa Maasumina na waliagizia kuwa, kabla ya kumuomba Mwenyezi Mungu na baada ya hapo aswaliwe Mtume na Aali zake. [5] Inaelezwa kuwa, kwa mujibu wa hadithi kumsalia Mtume na matakwa na maombi ambayo yanaambatanishwa nayo na kuombwa Mwenyezi Mungu, huwa na hali nzuri ya kukubaliwa; kwa muktadha huo, Imamu Sajjad (a.s) katika dua hii na katika dua zingine za al-Sahifa al-Sajjadiyya amemswalia sana Mtume (s.a.w.w). [6]

Kwa Nini Mwenyezi Mungu Aombwe Tabia Njema

Ruhullah Khatami mwanzoni mwa kutoa ufafanuzi na maelezo kuhusiana na dua ya Makarim al-Akhlaq (dua ya tabia njema) sambamba na kuuliza swali hili kwamba, vipi inawezekana kuomba tabia njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika hali ambayo, hili ni jambo ambalo mtu mwenyewe anapaswa kulitenda, anapaswa kuchuma tabia njema na kufanya juhudi na bila ya hima na idili hawezi kufikia popote? Anajibu swali hili kwa kusema: Dua si mrithi wa juhudi na kufanya hima; bali huwa ni kinga na himaya ya juhudi za mwanadamu; kwa msingi huo ili kupata na kuchuma tabia njema mbali na kufanya hima mtawalia anahitajia dua pia. Kwa upande mwingine, mikono inaponyanyuliwa kwa ajili ya kuomba dua, aina fulani ya ufundishaji hutiwa ndani ya mtu na kufanya azma na irada yake ya kuchuma na kujipamba na tabia njema kuimarika na kupata nguvu zaidi. [7]

Mafundisho

Mada kuu ya dua ya Makarim al-Akhlaq ni kumuomba Mwenyezi Mungu ampatie mwanadamu nguvu na uwezo wa kuchuma na kujipamba na tabia njema na kufanya mambo mema. [8] Yanayoombwa katika dua hii yanajumuisha maadili katika nyanja za fikra, maneno na vitendo, na yamewasilishwa katika mihimili miwili ya maadili ya mtu binafsi na ya kijamii. [9] Mafundisho ya Dua ya Makarim al-Akhlaq kutoka kwa Imam Sajjad (a.s) yamo katika vipengee na dondoo 30. [10] kwa kuzingatia mgawanyo wa tarjuma na maelezo ya kitabu cha Sayyid Ali Naqi Faizul Islam.

Mihimili ya Tabia za Mtu Binafsi

  • Kuomba hatua kamili kabisa ya kiimani, daraja ya juu ya yakini, nia bora kabisa na amali bora kabisa.
  • Imani ni chimbuko na chemchemi ya kheri na tabia zote njema.
  • Nia njema ni chimbuko la amali njema.
  • Matatizo na vikwazo ya kukwea mwanadamu: Kumzingatia na kujishuhughulisha na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, umasikini, tamaa, kiburi, kujiona na kujifaharisha.
  • Njia za kumuokoa mwanadamu: Kutenda amali (njema) kwa ajili ya Siku ya Kiyama, kutumia muda katika njia ya malengo, kulindwa na umasikini, upana wa riziki, kufanya ibada bila ya kujiona na kujionyesha na kufanya mambo ya kheri bila ya masimbulizi.
  • Kuomba unyenyekevu katika hali ya kuwa katika ukubwa na mafanikio.
  • Kuomba umri kwa ajili ya kuutumikia katika njia ya kufanya ibada na uja. [11]
  • Kudumu katika amali: Hidaya na uongofu stahiki, nia imara, kudumu katika ibada na kuwa mbali na shetani.
  • Kuomba kujibiwa dua.
  • Dua ya kufungukiwa katika mali katika kipindi chote cha maisha na upana wa riziki katika masiku ya uzeeni.
  • Kuomba msamaha wa Mwenyezi Mungu mwisoni mwa umri.
  • Kumtaja na kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika maisha yote.
  • Kuomba kinga ya adhabu ya Mwenyezi Mungu.
  • Kuomba hidaya kwa njia bora.
  • Kuomba kutotahiniwa.
  • Kuwa na hali ya wastani katika maisha.
  • Kuomba kujitenga mbali na vinavyopelekea kunyimwa rehma za Mwenyezi Mungu. [12]
  • Mtihani wa Mwenyezi Mungu kwa waja kupitia utajiri.
  • Kuomba baraka katika mali.
  • Kuzifanya nguvu za Mwenyezi Mungu kuwa kimbilio.
  • Kuomba kunufaika na taqwa (uchaji Mungu) na kuzungumza kwa mujibu wa uongofu wa Mwenyezi Mungu. [13]
  • Ugumu na unyonge wa umasikini (kutokuwa na kitu).
  • Kuomba hali ya wastani katika ibada.
  • Kutoacha ibada kwa sababu ya kutafuta riziki. [14]
  • Mabadiliko ya kila kitu ni jambo la Allah.
  • Katika hatari ya kuangamia nafsi.
  • Kuomba kuhusisha mwisho wa maisha na msamaha wa Mwenyezi Mungu.
  • Kufikia na kupata kheri za dunia na akhera kwa kumdhukuru (kumtaja) Mwenyezi Mungu na kumtii Alllah na huba yake. [15]
  • Kuomba njia nyepesi kwa ajili ya huba ya Mwenyezi Mungu.
  • Kuomba jema kutoka kwa Allah duniani na akhera. [16]

Mihimili ya Tabia za Kijamii

  • Dua ya kurekebisha fikra mbaya za wengine: Kubadilisha husuda kuwa mapenzi.
  • Dua kwa ajili ya kuwashinda maadui.
  • Kuomba kunufaika na ladha tamu ya usalama na kinga ya dhulma ya madhalimu. [17]
  • Kujitolea na usamehevu wa kimaadili (kitabia).
  • Kupinga kutaka jaha na ukuu na kupora haki za wengine.
  • Kubainisha sifa za waja wema: Kuenea uadilifu, kuzuia hasira, kuleta upatanishi baina ya watu, kudhihirisha kazi na matendo mazuri ya watu, kufunika aibu, kuwa na hali ya ulaini, unyenyekevu, kuamilia vizuri na wengine, utulivu, tabia njema, kuchunga adabu za kijamii na akhlaq za umma na kadhalika.
  • Kujiepusha na israfu (ubadhirifu).
  • Jibu zuri mbele ya kitendo kibaya.
  • Matokeo ya matukio mabaya ni kuomba msaada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
  • Ushawishi wa kishetani katika moyo na ndimi za watu (kutamani batili, dhana mbaya, husuda, matusi, lugha chafu, ushahidi wa batili, kuharibu heshima ya watu na kadhalika).
  • Kuomba hifadhi ya Mwenyezi Mungu kuhusu kudhulumu na kuona dhulma.
  • Kubainisha uongofu wa Mwenyezi Mungu (uwezo wa kubainisha na taathira yake katika kuwaongoza watu).
  • Kukubali majukumu na kuongoza kwa usahihi.
  • Kubadilisha uadui wa watu wa karibu na kuufanya urafiki.
  • Ushirikiano na wengine katika kuhudumia jamii.
  • Kuwa pamoja na watu na kuwaacha watu wa bidaa. [18]
  • Kuzingatia utukufu na heshima ya watu.
  • Kuomba hifadhi ya heshima na kutokuwa na haja ya watu wabaya na wasiofaa.
  • Kuwa katika orodha ya waongozaji katika kheri.
  • Kuwa na kigezo na ruwaza na kuainisha muelekeo katika kueneza uadilifu.
  • Kuleta utulivu na kupambana na utumiaji mabavu
  • Umuhimu wa ushindani wa kijamii katika kutenda mema.
  • Kuondoa sababu za madhara.
  • Kuacha kutenda wema mahali pasipostahiki.
  • Kuomba nguvu mkabala na dhalimu na uwezo wa kujieleza mbele ya maadui.
  • Kupuuza ulimbikizaji wa mali na utajiri.
  • Kuomba kumswali Mtume Muhammad (saww)na Aal zake kwa njia bora kabisa. [19]

Ufafanuzi

Dua ya Makarim al-Akhlaq imebainishwa kwa sura ya vitabu vya kujitegemea na baadhi ya sherh na fafanuzi hizo ni:

  • Sherh va tafsir Dua Makarem al-Akhaq, mwandishi Muhammad Taqi Falsafi. Kitabu hiki ni majimui ya mawaidha ya kutolea ufafanuzi dua hii ambayo baadaye yalikusanywa na kuchapishwa katika sura ya kitabu. [20]
  • Sherh Dua Makarim al-Akhlaq, mwandishi Muhammad Taqi Misbah Yazdi (majimui ya darsa za akhlaq) za alimu huyu. [21]
  • Nurul Afaq: Ufafanuzi wa Dua ya Makarim al-Akhlaq, mwandishi Sheikh Muhammad Hussein Dhu-Ilm. [22]
  • Aineh Makarim (ufafanuzi wa dua ya Makarim al-Akhlaq ya Imamu Sajjad); Kitabu hiki ni cha juzuu mbili na ni majimui ya darasa za akhlaq za Sayyid Ruhullah Khatami katika kubainisha na kutoa ufafanuzi wa dua ya Makarim al-Akhlaq. [23]

Kadhalika Dua ya Makarim al-Akhlaq imefanyiwa ufafanuzi wakati kitabu chote cha al-Sahifa al-Sajjadiya kilipofafanuliwa na kutolewa sherh. Dua hii imeafafanuliwa katika ufafanuzi wa kitabu cha Sahifa al-Sajjadiya katika kitabu cha Diyar Ashiqan cha Hussein Ansariyan, [24] na vilevile katika kitabu cha Shuhud va Shenakht cha Muhammad-Hassan Mamduhi Kermanshahi [25] na Sherh na tarjuma ya al-Sahifa al-Sajjadiyya ya Sayyid Ahmad Fahri, [26] kwa lugha ya Kifarsi.

Kadhalika sherh na ufafanuzi wa Dua ya Makarim al-Akhlaq umekuja katika vitabu kama vya Riyadh al-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani, [27] Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajajadiyya cha Muhammad javad Mughniyyah, [28] Riyadh al-Arifina cha Muhammad bin Muhammad Darabi, [29] na Afaaq al-Ruh cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah, [30] kwa kugha ya Kiarabu. Maneno ya dua hii pia yamekuja katika ufafanuzi wa vitabu vya klugha kama Taaliqaat ala al-Sahifa al-Sajjadiya cha Feidh Kashani [31] na sherh na ufafanuzi wa al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Izzuddin al-Jazairi. [32]

Andiko la Dua

Tarjama Andiko la dua
1. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na uifanye imani yangu kuwa imani kamilifu zaidi, na uifanye yakini yangu kuwa yakini iliyo bora kabisa, Na jaalia mwisho mwema wa nia yangu iwe ni nia njema zaidi, na mwisho mwema wa matendo yangu yawe ni matendo mema zaidi.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ بَلِّغْ بِإِیمَانِی أَکمَلَ الْإِیمَانِ، وَ اجْعَلْ یقِینِی أَفْضَلَ الْیقِینِ، وَ انْتَهِ بِنِیتِی إِلَی أَحْسَنِ النِّیاتِ، وَ بِعَمَلِی إِلَی أَحْسَنِ الْأَعْمَالِ
2. Eeh Mwenyezi Mungu! Ninakuomba ifanye nia yangu iwe kamili kwa Neema (na Taufiq) yako (kwa kuifanya iwe ni nia ya ikhlasi na safi kwako), na uiweke yakini yangu katika mzunguko wa siha na afya njema kwa rehema Zako, na urekebishe ufisadi (uovu, na ukosefu) wangu kwa uwezo wako.
اللَّهُمَّ وَفِّرْ بِلُطْفِک نِیتِی، وَ صَحِّحْ بِمَا عِنْدَک یقِینِی، وَ اسْتَصْلِحْ بِقُدْرَتِک مَا فَسَدَ مِنِّی
3. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na unizuie kutokana na kile kinachoweza kunishughulisha (na kunitia wasiwasi) na kunifanya nipoteze umakini wangu kuelekea yeye, na unihusishe (na kunifanya niwe mwenye kutafakari zaidi) katika mambo ambayo utakuja kunihoji juu yake Siku ya Kiyama, na umalizie siku zangu katika malengo uliyoniumbia; na unifanye kuwa tajiri (na mwenye uwezo wa kiuchumi), Na nienezee baraka (na riziki) Zako, na usinifanye kuwa mwenye kuhuzunika kwa yale yaliyopo mikononi mwa huyu na yule, na unifanye niwe mwenye kuheshimika; na uniepushe (na kuninasua kutoka kwenye) uasi na kiburi (mbele ya maamrisho na makatazo yako), na uniweke kwenye mzunguko wa waja wako wema, na nifanye niwe ni mwenye kukuabudu na ibada yangu isibatilike kutokana na kujikweza kwangu, na utiririshe wema na baraka kupitia mkono wangu kwa watu wote, na wala usiiangamize (mikono yangu) kwa sababu ya (kuchafuka kwake kunatokana na) kutoa (sadaka na kufanya wema) kunako ambatana na majigambo na masimango yenye kuudhi, na unijaalie kuwa na maadili mema, na heshima ya daraja ya juu, na uniepushe na kujifakharisha.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اکفِنِی مَا یشْغَلُنِی الِاهْتِمَامُ بِهِ، وَ اسْتَعْمِلْنِی بِمَا تَسْأَلُنِی غَداً عَنْهُ، وَ اسْتَفْرِغْ أَیامِی فِیمَا خَلَقْتَنِی لَهُ، وَ أَغْنِنِی وَ أَوْسِعْ عَلَی فِی رِزْقِک، وَ لَا تَفْتِنِّی بِالنَّظَرِ، وَ أَعِزَّنِی وَ لَا تَبْتَلِینِّی بِالْکبْرِ، وَ عَبِّدْنِی لَک وَ لَا تُفْسِدْ عِبَادَتِی بِالْعُجْبِ، وَ أَجْرِ لِلنَّاسِ عَلَی یدِی الْخَیرَ وَ لَا تَمْحَقْهُ بِالْمَنِّ، وَ هَبْ لِی مَعَالِی الْأَخْلَاقِ، وَ اعْصِمْنِی مِنَ الْفَخْرِ.
4. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na wala usinyanyue na kupandisha zaidi daraja yangu (na cheo changu) kwa watu, isipokuwa ikiwa ni kwa kuniweka kwenye (ile daraja na) kile kiwango ambacho nafsi yangu inastahili kuwa, wala usinionyeshe (na usinipe) heshima (utukufu na izza) ya dhahiri, isipokuwa kwa kunionyesha (na kunijaalia) unyonge (na unyenyekevu) ndani (yangu) kwa kiwango kile kile (cha heshima na utukufu ulionipa).
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ لَا تَرْفَعْنِی فِی النَّاسِ دَرَجَةً إِلَّا حَطَطْتَنِی عِنْدَ نَفْسِی مِثْلَهَا، وَ لَا تُحْدِثْ لِی عِزّاً ظَاهِراً إِلَّا أَحْدَثْتَ لِی ذِلَّةً بَاطِنَةً عِنْدَ نَفْسِی بِقَدَرِهَا
5. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na nifanye nifaidike na (uongofu na) mwongozo unaostahiki ambao sitaubadilisha na njia nyingine, na unijaalie (kuwa katika) njia iliyo sawa (na ya haki) nisije nikakengeuka, na unijaalie nia thabiti ambayo sitakuwa na shaka nayo, na uniweke hai, maadamu maisha yangu (na umri wangu wote) ni katika kukutii wewe, na maisha yangu (yanapogeuka) na kutaka kuwa malisho ya shetani, basi yafunge maisha yangu; kabla ya hasira na ghadhabu zako kunifikia, au hasira yako kubaki kuwa kali na thabiti juu yangu.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ، وَ مَتِّعْنِی بِهُدًی صَالِحٍ لَا أَسْتَبْدِلُ بِهِ، وَ طَرِیقَةِ حَقٍّ لَا أَزِیغُ عَنْهَا، وَ نِیةِ رُشْدٍ لَا أَشُک فِیهَا، وَ عَمِّرْنِی مَا کانَ عُمُرِی بِذْلَةً فِی طَاعَتِک، فَإِذَا کانَ عُمُرِی مَرْتَعاً لِلشَّیطَانِ فَاقْبِضْنِی إِلَیک قَبْلَ أَنْ یسْبِقَ مَقْتُک إِلَی، أَوْ یسْتَحْکمَ غَضَبُک عَلَی
6. Eeh Mwenyezi Mungu! Usiache tabia mbaya (yenye kukemewa) ijikite ndani yangu, isipokuwa umeisahihisha (na kuwa tabia njema), na usiache (kosa au) kasoro yenye kulaumiwa katika uwanja wa maisha yangu, ispokuwa umenifanya niwe ni mwenye kuboresha na kufanya mema. Na wala usiache heshima yoyote ambayo ni nakisi (na yenye upungufu) ndani yangu, isipokuwa umeifanya kuwa (ni heshima) kamili.
اللَّهُمَّ لَا تَدَعْ خَصْلَةً تُعَابُ مِنِّی إِلَّا أَصْلَحْتَهَا، وَ لَا عَائِبَةً أُوَنَّبُ بِهَا إِلَّا حَسَّنْتَهَا، وَ لَا أُکرُومَةً فِی نَاقِصَةً إِلَّا أَتْمَمْتَهَا
7. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na unibadilishie chuki ya watu wa ulimwengu juu yangu kuwa upendo, na husuda ya watu waovu (na wapotovu) dhidi yangu kuwa mapenzi (na mawadda), na dhana mbaya na kashfa dhidi ya watu wema kuwa yakini, na uadui wa ndugu na jamaa kuwa urafiki. (mwema), na upinzani wa ndugu na jamaa kuwa tabia njema, na kuwaacha ndugu na jamaa peke yao na wanyonge kwa kuwapa msaada, na urafiki wa wadanganyifu kuwa urafiki halisi na wa kweli, na kuwakataa majirani (kwa kuwatendea ya dhulma na mabaya) kuwa ni kuwatendea wema na ukarimu, na uchungu wa kuwaogopa madhalimu kuwa utamu wa amani na usalama.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ، وَ أَبْدِلْنِی مِنْ بِغْضَةِ أَهْلِ الشَّنَآنِ الْمَحَبَّةَ، وَ مِنْ حَسَدِ أَهْلِ الْبَغْی الْمَوَدَّةَ، وَ مِنْ ظِنَّةِ أَهْلِ الصَّلَاحِ الثِّقَةَ، وَ مِنْ عَدَاوَةِ الْأَدْنَینَ الْوَلَایةَ، وَ مِنْ عُقُوقِ ذَوِی الْأَرْحَامِ الْمَبَرَّةَ، وَ مِنْ خِذْلَانِ الْأَقْرَبِینَ النُّصْرَةَ، وَ مِنْ حُبِّ الْمُدَارِینَ تَصْحِیحَ الْمِقَةِ، وَ مِنْ رَدِّ الْمُلَابِسِینَ کرَمَ الْعِشْرَةِ، وَ مِنْ مَرَارَةِ خَوْفِ الظَّالِمِینَ حَلَاوَةَ الْأَمَنَةِ
8. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na nijaalie nimshinde yule anayenidhulumu, na nijalie ulimi fasaha wa kumshinda yule anayebishana nami, na nijaalie nguvu ya ushindi juu ya yule aliye na uadui dhidi yangu, nifanye niwe mshindi dhidi ya yule anayenihadaa, na nipe nguvu dhidi ya anayenidhulumu, na niwe na nguvu ya kuwakanusha wanaonikosea kwa kunitukana (kunikosea adabu) na kunisengenya, na nipe salama kutokana mkono wa yule anayenitisha, na nijaalie niwe ni mwenye kufaulu katika kumtii yule anaye niongoza kwenye njia iliyo sawa, na nijaalie niwe ni mwenye kufanikiwa kufuata mwongozo wa yule anayeniongoza kuelekea kwenye njia iliyo ya haki na sawa.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ لِی یداً عَلَی مَنْ ظَلَمَنِی، وَ لِسَاناً عَلَی مَنْ خَاصَمَنِی، وَ ظَفَراً بِمَنْ عَانَدَنِی، وَ هَبْ لِی مَکراً عَلَی مَنْ کایدَنِی، وَ قُدْرَةً عَلَی مَنِ اضْطَهَدَنِی، وَ تَکذِیباً لِمَنْ قَصَبَنِی، وَ سَلَامَةً مِمَّنْ تَوَعَّدَنِی، وَ وَفِّقْنِی لِطَاعَةِ مَنْ سَدَّدَنِی، وَ مُتَابَعَةِ مَنْ أَرْشَدَنِی
9. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, Na unithabitishe na kuniimarisha katika mambo haya ninayokuomba: Kusimama imara juu ya aliye nisaliti (na kunifanyia hiana) kupitia silaha ya (kumpa) ushauri mzuri na (kumtendea) wema; na kumzawadia mtu ambaye ameniepuka, kwa (kunifanya niwe ni mwenye kumtendea) wema na mema; na kumlipa yule aliyeninyima zawadi yake, ukarimu na msamaha, na nisiwe ni mwenye kulipiza kisasi kwa mtu aliyeachana nami, ispokuwa nimlipe kwa kumtendea heshima zaidi na (kujenga pamoja naye) uhusiano mwema; na kutokukubaliana kwangu na mtu aliyenichoma kisu kwa nyuma (aliye nisengenya na kuniteta) kuwe katika sura ya kuwa na kumbukumbu nzuri; (kwa yale mazuri aliyonitendea hapo awali na) kushukuru kwa mema (yake juu yangu) na kupuuza mabaya (yake).
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ سَدِّدْنِی لِأَنْ أُعَارِضَ مَنْ غَشَّنِی بِالنُّصْحِ، وَ أَجْزِی مَنْ هَجَرَنِی بِالْبِرِّ، وَ أُثِیبَ مَنْ حَرَمَنِی بِالْبَذْلِ، وَ أُکافِی مَنْ قَطَعَنِی بِالصِّلَةِ، وَ أُخَالِفَ مَنِ اغْتَابَنِی إِلَی حُسْنِ الذِّکرِ، وَ أَنْ أَشْکرَ الْحَسَنَةَ، وَ أُغْضِی عَنِ السَّیئَةِ
10. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na unifanye kuwa pambo la (watu wema) wanaostahiki, na nivishe pambo la Wacha Mungu, ambalo ni pambo la wastahiki na wema katika mambo haya: Kueneza uadilifu, Kutuliza hasira, kuzima moto wa fitna, kuwakusanya waliotawanyika, kurekebisha (na kusuluhisha) watu, kufichua matendo mema ya watu, kusitiri (aibu na) makosa ya watu, upole, unyenyekevu, tabia njema, amani, utu, maadili mema, kusonga mbele kuelekea wema, kuchagua wema na ihsani, kuacha lawama, kufanya wema kwa wasiostahiki, kusema ukweli hata kama ni jambo zito (na mchungu). Niyahesabu (na niyachukulie) maneno na matendo yangu mema kuwa ni kidogo, hata kama yatakuwa ni mengi; na niyahesabu (na kuyachukulia) maneno yangu na tabia zangu mbaya kuwa ni mambo makubwa sana, hata kama yatakuwa ni kidogo; na ukamilishe mambo yote haya kwa kunifanya niwe mwenye kuendelea kukutii Ewe Mola wangu na nishikamane na Waislamu na niachane na wazushi (watu wa bid’a) na wanaotumia dhana za uwongo katika dini.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ حَلِّنِی بِحِلْیةِ الصَّالِحِینَ، وَ أَلْبِسْنِی زِینَةَ الْمُتَّقِینَ، فِی بَسْطِ الْعَدْلِ، وَ کظْمِ الغَیظِ، وَ إِطْفَاءِ النَّائِرَةِ، وَ ضَمِّ أَهْلِ الْفُرْقَةِ، وَ إِصْلَاحِ ذَاتِ الْبَینِ، وَ إِفْشَاءِ الْعَارِفَةِ، وَ سَتْرِ الْعَائِبَةِ، وَ لِینِ الْعَرِیکةِ، وَ خَفْضِ الْجَنَاحِ، وَ حُسْنِ السِّیرَةِ، وَ سُکونِ الرِّیحِ، وَ طِیبِ الْمُخَالَقَةِ، وَ السَّبْقِ إِلَی الْفَضِیلَةِ، وَ إِیثَارِ التَّفَضُّلِ، وَ تَرْک التَّعْییرِ، وَ الْإِفْضَالِ عَلَی غَیرِ الْمُسْتَحِقِّ، وَ الْقَوْلِ بِالْحَقِّ وَ إِنْ عَزَّ، وَ اسْتِقْلَالِ الْخَیرِ وَ إِنْ کثُرَ مِنْ قَوْلِی وَ فِعْلِی، وَ اسْتِکثَارِ الشَّرِّ وَ إِنْ قَلَّ مِنْ قَوْلِی وَ فِعْلِی، وَ أَکمِلْ ذَلِک لِی بِدَوَامِ الطَّاعَةِ، وَ لُزُومِ الْجَمَاعَةِ، وَ رَفْضِ أَهْلِ الْبِدَعِ، وَ مُسْتَعْمِلِ الرَّأْی الْمُخْتَرَعِ
11. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na uniwekee siku ya ukarimu zaidi nitakapokuwa mzee; na unipe nguvu (zinazotokana na) nguvu zako ambazo ndio nguvu imara zaidi, pindi nitapochoka na kukosa msaada; wala usinitie (katika balaa la kuwa na) udhaifu na uvivu (na uchovu) katika kukuabudu; na wala usinitie upofu wa kutokuijua njia yako; na wala usinifanye niwe mwenye kuachana na urafiki wako; na usinifanye kuwa karibu na mtu ambaye amejitenga na wewe, na usinitenge na mtu aliye karibu na nawe.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ أَوْسَعَ رِزْقِک عَلَی إِذَا کبِرْتُ، وَ أَقْوَی قُوَّتِک فِی إِذَا نَصِبْتُ، وَ لَا تَبْتَلِینِّی بِالْکسَلِ عَنْ عِبَادَتِک، وَ لَا الْعَمَی عَنْ سَبِیلِک، وَ لَا بِالتَّعَرُّضِ لِخِلَافِ مَحَبَّتِک، وَ لَا مُجَامَعَةِ مَنْ تَفَرَّقَ عَنْک، وَ لَا مُفَارَقَةِ مَنِ اجْتَمَعَ إِلَیک
12. Eeh Mwenyezi Mungu! Nijalie niwashambulie maadui kwa msaada wako inapobidi, na itakapobidi na kulazimu basi nikuombe wewe, na wakati wa unyonge na umaskini, nikugeukie wewe (na kukutegemea); Wala usinijaribu kwa mambo haya: Kuomba msaada kwa (kumkimbilia na kumtegemea) asiyekuwa wewe, ninapohitaji na kukosa namna; nisiwe mwenye unyenyekevu wa kunyenyekea mbele ya asiyekuwa wewe, ninaposhikwa (au ninapokumbwa na) shida; nisiwe mwenye kulia na kukimbilia katika mlango wa asiyekuwa wewe, ninapopata hofu kwa sababu ya mambo haya, nisistahiki kudhalilika na kunyimwa neema na baraka zako na kupuuzwa na wewe; Ewe Mwingi wa ukarimu kuliko wakarimu wote.
اللَّهُمَّ اجْعَلْنِی أَصُولُ بِک عِنْدَ الضَّرُورَةِ، وَ أَسْأَلُک عِنْدَ الْحَاجَةِ، وَ أَتَضَرَّعُ إِلَیک عِنْدَ الْمَسْکنَةِ، وَ لَا تَفْتِنِّی بِالاسْتِعَانَةِ بِغَیرِک إِذَا اضْطُرِرْتُ، وَ لَا بِالْخُضُوعِ لِسُؤَالِ غَیرِک إِذَا افْتَقَرْتُ، وَ لَا بِالتَّضَرُّعِ إِلَی مَنْ دُونَک إِذَا رَهِبْتُ، فَأَسْتَحِقَّ بِذَلِک خِذْلَانَک وَ مَنْعَک وَ إِعْرَاضَک، یا أَرْحَمَ الرَّاحِمِینَ
13. Eeh Mwenyezi Mungu! Nijalie kuhusu kile ambacho shetani anakiweka (na kukitupia) moyoni mwangu ambacho ni katika tamaa ya batili, dhana mbaya, wivu na husuda, (yote hayo na mengine) niwe ni mwenye kuyakumbuka na kuyaepuka kwa adhama yako (na utukufu wako), na niwe ni mwenye tafakuri juu ya uwezo wako, na niwe mwenye kufanya mipango mizuri na uamuzi sahihi dhidi ya adui yako; na kamwe usipitishe hata neno moja chafu kwenye ulimi wangu (kiasi kwamba neno hilo chafu na lisilostahili likasikika likitamkwa na ulimi wangu), au kulaani na kukashifu heshima ya watu, au kutoa ushahidi wa uongo, au kumteta na kumsengenya Muumini asiyekuwepo (kwa sasa), au kumtukana Muumini aliyepo, na mambo yote yanayofanana na haya, kiasi kwamba ulimi wangu (katika hayo) uwe ni wenye kutamka sifa njema na kukuhimidi na kukushukuru, na kuzidisha zaidi katika kukusifu kwa sifa zako tukufu, na kukusujudia katika kukutukuza, na kukushukuru kwa neema na baraka zako, na kuzikiri hisani zako, na (kutafakari kwa) kuzihesabu neema zako (juu yangu).
اللَّهُمَّ اجْعَلْ مَا یلْقِی الشَّیطَانُ فِی رُوعِی مِنَ التَّمَنِّی وَ التَّظَنِّی وَ الْحَسَدِ ذِکراً لِعَظَمَتِک، وَ تَفَکراً فِی قُدْرَتِک، وَ تَدْبِیراً عَلَی عَدُوِّک، وَ مَا أَجْرَی عَلَی لِسَانِی مِنْ لَفْظَةِ فُحْشٍ أَوْ هُجْرٍ أَوْ شَتْمِ عِرْضٍ أَوْ شَهَادَةِ بَاطِلٍ أَوِ اغْتِیابِ مُؤْمِنٍ غَائِبٍ أَوْ سَبِّ حَاضِرٍ وَ مَا أَشْبَهَ ذَلِک نُطْقاً بِالْحَمْدِ لَک، وَ إِغْرَاقاً فِی الثَّنَاءِ عَلَیک، وَ ذَهَاباً فِی تَمْجِیدِک، وَ شُکراً لِنِعْمَتِک، وَ اعْتِرَافاً بِإِحْسَانِک، وَ إِحْصَاءً لِمِنَنِک
14. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na wala usijalie niwe mwenye kudhulumiwa, hali ya kuwa unao uwezo mkubwa wa kuniondolea dhulma hiyo, wala usinifanye niwe mwenye kumdhulumu mwingine, hali ya kuwa unao uwezo mkubwa wa kunizuia; Na wala usinifanye niwe ni mwenye kupotea hali ya kuwa Wewe ni Mwenye Nguvu zaidi katika uwongofu wangu; na usinifanye kuwa masikini (nisiyekuwa na kitu, mikono mitupu), hali ya kuwa riziki zangu katika maisha yangu nazitegemea kutoka kwako, na ujaalie nisiwe mwenye kufanya maasi na kuvuka mipaka (kwa sababu ya mali zangu nilizokuwa nazo), hali ya kuwa uwezo wangu wa kimali unatoka kwako.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ لَا أُظْلَمَنَّ وَ أَنْتَ مُطِیقٌ لِلدَّفْعِ عَنِّی، وَ لَا أَظْلِمَنَّ وَ أَنْتَ الْقَادِرُ عَلَی الْقَبْضِ مِنِّی، وَ لَا أَضِلَّنَّ وَ قَدْ أَمْکنَتْک هِدَایتِی، وَ لَا أَفْتَقِرَنَّ وَ مِنْ عِنْدِک وُسْعِی، وَ لَا أَطْغَینَّ وَ مِنْ عِنْدِک وُجْدِی
15. Eeh Mwenyezi Mungu! Nimekuja nikielekea katika upande wa maghfira yako, na nimegeukia msamaha wako, na nimetamani kusamehe kwako (na kuyafuta makossa yangu), na nimetumainia (ihsani na) wema wako; na sina chochote cha kunifanya niwe mwenye kustahili msamaha wako, wala matendo (mema ya kutosha na) ya kunifanya niwe mwenye kustahili msamaha wako; na baada ya kujihukumu, nilifikia katika hitimisho (na natija hii) kwamba hakuna lolote ispokuwa wema wako (na ihsani yako) kwangu; basi Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake, na nifanyie wema na ihsani.
اللَّهُمَّ إِلَی مَغْفِرَتِک وَفَدْتُ، وَ إِلَی عَفْوِک قَصَدْتُ، وَ إِلَی تَجَاوُزِک اشْتَقْتُ، وَ بِفَضْلِک وَثِقْتُ، وَ لَیسَ عِنْدِی مَا یوجِبُ لِی مَغْفِرَتَک، وَ لَا فِی عَمَلِی مَا أَسْتَحِقُّ بِهِ عَفْوَک، وَ مَا لِی بَعْدَ أَنْ حَکمْتُ عَلَی نَفْسِی إِلَّا فَضْلُک، فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ تَفَضَّلْ عَلَی
16. Eeh Mwenyezi Mungu! Nipe uwongofu, na unitie moyo wa Ucha Mungu, na nipe taufiq (na mafanikio) ya kuwa katika njia safi zaidi, na niwe mwenye kujishughulisha na mambo yanayopendeza zaidi.
اللَّهُمَّ وَ أَنْطِقْنِی بِالْهُدَی، وَ أَلْهِمْنِی التَّقْوَی، وَ وَفِّقْنِی لِلَّتِی هِی أَزْکی، وَ اسْتَعْمِلْنِی بِمَا هُوَ أَرْضَی
17. Eeh Mwenyezi Mungu! Nipeleke (na unielekeze) kwenye njia iliyo kuwa bora zaidi, na unijaalie (niwe na) uthabiti zaidi katika Dini yako Tukufu, na nifariki na kuwa hai nikiwa ni mwenye kushikamana na kudumu katika msingi wake.
اللَّهُمَّ اسْلُک بی‌الطَّرِیقَةَ الْمُثْلَی، وَ اجْعَلْنِی عَلَی مِلَّتِک أَمُوتُ وَ أَحْیا'
18. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, Na unipe kiasi (cha kunitosha kiuchumi) katika mambo yote ya maisha, na unijaalie niwe miongoni mwa watu sahihi na wema, na niwe miongoni mwa kundi la wale ulio waongoza kuelekea kwenye kheri, na niwe miongoni mwa waja wako wema wanao stahiki (kutokana na kutenda kwao matendo sahihi na yanayostahili). Na unijaalie uokovu (na kufuzu) Siku ya Kiyama, na niwe salama (siku hiyo) nisitumbukie kwenye kinamasi cha adhabu.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ مَتِّعْنِی بِالاقْتِصَادِ، وَ اجْعَلْنِی مِنْ أَهْلِ السَّدَادِ، وَ مِنْ أَدِلَّةِ الرَّشَادِ، وَ مِنْ صَالِحِ الْعِبَادِ، وَ ارْزُقْنِی فَوْزَ الْمَعَادِ، وَ سلَامَةَ الْمِرْصَادِ
19. Eeh Mwenyezi Mungu! Pokea kutoka katika nafsi yangu kwa ajili yako kile kitakacho ikomboa na kuikoa nafsi yangu, na (pokea) kwa ajili ya nafsi yangu, kutoka katika nafsi yangu, yale yanayoirekebisha (na kuisahihisha nafsi yangu), kwa hakika! Nafsi yangu iko katika hatari ya kuangamia, isipokuwa ikiwa Wewe utakuwa ni Mwenye kuihifadhi.
اللَّهُمَّ خُذْ لِنَفْسِک مِنْ نَفْسِی مَا یخَلِّصُهَا، وَ أَبْقِ لِنَفْسِی مِنْ نَفْسِی مَا یصْلِحُهَا، فَإِنَّ نَفْسِی هَالِکةٌ أَوْ تَعْصِمَهَا
20. Eeh Mwenyezi Mungu! Nitakapokuwa na huzuni, Wewe ndiye kimbilio langu na chanzo cha furaha yangu, na kama (watu) wakininyima (na wakanifungia) mlango wowote, basi Wewe ndiye mahali pangu pa kuendea (na kukimbilia); na nitakapokuwa chini ya shinikizo, shida na matatizo, Wewe ndiye ambaye nitakuomba msaada, na chochote nitakachokipoteza (na kukikosa), badala yake iko kwako; na kila kitu kitakachoharibika, basi sahihisho lake (dawa yake, na ufumbuzi wake uko) mbele yako, na chochote unachokichukia (na kisichostahili), (taufiq ya) ubadilishaji wake (usahihishaji wake) iko mikoni mwako. Eeeh Mola wangu! Nipe uwongofu kabla ya maafa kunipata kwenye upande wa afya na ustawi; na unibariki kwa nguvu ya mali (na uwezo wa kiuchumi) kabla sijaomba, na unibariki uwongofu kabla sijapotea (kwa upotovu), na uniepushe na kuwatesa na kuwatia katika dhiki, shida na taabu waja wako, na unijaalie Salama na Amani Siku ya Kiyama, na unipe uwongofu mwema na mzuri.
اللَّهُمَّ أَنْتَ عُدَّتِی إِنْ حَزِنْتُ، وَ أَنْتَ مُنْتَجَعِی إِنْ حُرِمْتُ، وَ بِک اسْتِغَاثَتِی إِنْ کرِثْتُ، وَ عِنْدَک مِمَّا فَاتَ خَلَفٌ، وَ لِمَا فَسَدَ صَلَاحٌ، وَ فِیمَا أَنْکرْتَ تَغْییرٌ، فَامْنُنْ عَلَی قَبْلَ الْبَلَاءِ بِالْعَافِیةِ، وَ قَبْلَ الْطَّلَبِ بِالْجِدَةِ، وَ قَبْلَ الضَّلَالِ بِالرَّشَادِ، وَ اکفِنِی مَئُونَةَ مَعَرَّةِ الْعِبَادِ، وَ هَبْ لِی أَمْنَ یوْمِ الْمَعَادِ، وَ امْنَحْنِی حُسْنَ الْإِرْشَادِ
21. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, Na uniondolee shari na mabaya kwa huruma yako (na baraka Zako), na unilee kwa Neema zako, na unisahihishe kwa ukuu wako (na utukufu wako), na unitendee wema wako (na ihsani yako), na unikinge kwenye kivuli chako, na unifunike kwa vazi la radhi zako. Na pindi mambo yatakapo kuwa hayaeleweki na kuwa magumu kwangu, basi niongoze katika njia ya mafanikio zaidi, na matendo yatakaponitia shaka (na wasiwasi), na nibariki (kwa kunielekeza) kwa yale (matendo) yaliyokuwa safi na bora kabisa, na pindi dini zitakapo tofautiana (na kuhitilafiana), basi niwafikishe kwa kunidumisha na kunithabitisha zaidi katika ile Dini (ya haki) inayopendwa zaidi (na iliyo sahihi na yenye kuridhiwa).
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ ادْرَأْ عَنِّی بِلُطْفِک، وَ اغْذُنِی بِنِعْمَتِک، وَ أَصْلِحْنِی بِکرَمِک، وَ دَاوِنِی بِصُنْعِک، وَ أَظِلَّنِی فِی ذَرَاک، وَ جَلِّلْنِی رِضَاک، وَ وَفِّقْنِی إِذَا اشْتَکلَتْ عَلَی الْأُمُورُ لِأَهْدَاهَا، وَ إِذَا تَشَابَهَتِ الْأَعْمَالُ لِأَزْکاهَا، وَ إِذَا تَنَاقَضَتِ الْمِلَلُ لِأَرْضَاهَا اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ ادْرَأْ عَنِّی بِلُطْفِک، وَ اغْذُنِی بِنِعْمَتِک، وَ أَصْلِحْنِی بِکرَمِک، وَ دَاوِنِی بِصُنْعِک، وَ أَظِلَّنِی فِی ذَرَاک، وَ جَلِّلْنِی رِضَاک، وَ وَفِّقْنِی إِذَا اشْتَکلَتْ عَلَی الْأُمُورُ لِأَهْدَاهَا، وَ إِذَا تَشَابَهَتِ الْأَعْمَالُ لِأَزْکاهَا، وَ إِذَا تَنَاقَضَتِ الْمِلَلُ لِأَرْضَاهَا
22. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na uiletee nafsi yangu taji la utukufu wako, na uniweke chini ya uangalizi mzuri (na ulezi mwema) kwa kunipandisha katika daraja ya juu (katika wilayat-uongozi- hiyo na uangalizi huo wa kimalezi), na unipe (uwongofu na) mwongozo sahihi, na usinijaribu (kwa kunipa mitihani) kwa wingi katika mambo ya kimaisha, na unipe amani njema, na usiyafanye maisha yangu kuwa magumu na magumu, na wala usiyarudishe maombi yangu (na dua yangu bila majibu), usinirejeshee uchungu na aibu, kwa hakika mimi sina pingamizi lolote kwako katika imani (na itikadi) yangu, na sikushirikishi na chochote (wala kukufananisha na yeyote).
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ تَوِّجْنِی بِالْکفَایةِ، وَ سُمْنِی حُسْنَ الْوِلَایةِ، وَ هَبْ لِی صِدْقَ الْهِدَایةِ، وَ لَا تَفْتِنِّی بِالسَّعَةِ، وَ امْنَحْنِی حُسْنَ الدَّعَةِ، وَ لَا تَجْعَلْ عَیشِی کدّاً کدّاً، وَ لَا تَرُدَّ دُعَائِی عَلَی رَدّاً، فَإِنِّی لَا أَجْعَلُ لَک ضِدّاً، وَ لَا أَدْعُو مَعَک نِدّاً
23. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na unizuie nisiwe na ubadhirifu, na uihifadhi riziki yangu kutokana na hasara na uharibifu, na unizidishie mali yangu kwa kuzidisha baraka ndani yake, na uniongoze kwenye njia ya uwongofu kwa kufanya wema na kheri zaidi katika yale ninayotoa katika mali hiyo.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ امْنَعْنِی مِنَ السَّرَفِ، وَ حَصِّنْ رِزْقِی مِنَ التَّلَفِ، وَ وَفِّرْ مَلَکتِی بِالْبَرَکةِ فِیهِ، وَ أَصِبْ بی‌سَبِیلَ الْهِدَایةِ لِلْبِرِّ فِیمَا أُنْفِقُ مِنْهُ.
24. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na uniepushe na ugumu wa biashara, na unipe riziki yangu kutoka pale nisipotazamia (wala kupatarajia); ili nisiache kukuabudu kwa sababu ya kuwa bize njiani kutafuta riziki, Na uniepushe na kubeba mzigo mzito wa kutokuwa na afya (na kukumbana na hali isiyo ya kawaida) na ugumu wa biashara (niwapo katika harakati za kutafuta riziki).
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اکفِنِی مَئُونَةَ الِاکتِسَابِ، وَ ارْزُقْنِی مِنْ غَیرِ احْتِسَابٍ، فَلَا أَشْتَغِلَ عَنْ عِبَادَتِک بِالطَّلَبِ، وَ لَا أَحْتَمِلَ إِصْرَ تَبِعَاتِ الْمَکسَبِ
25. Eeh Mwenyezi Mungu! Ninakuomba kwa uwezo wako, unipe kile ninachokitafuta na kukiomba kutoka kwako, na ninakuomba kwa utukufu wako, unipe hifadhi kwa kile ninachokiogopa.
اللَّهُمَّ فَأَطْلِبْنِی بِقُدْرَتِک مَا أَطْلُبُ، وَ أَجِرْنِی بِعِزَّتِک مِمَّا أَرْهَبُ
26. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na ulinde heshima yangu kwa kunijaalia nguvu ya mali (na uwezo wa kiuchumi), na usijaalie hadhi yangu, (utukufu wangu), na heshima yangu kutumbukia katika umasikini na kuwa na hali duni ya chini, ili nisiwakimbilie kuwaomba riziki wale (wanaokula na) kutegemea riziki kutoka kwako, na kuiomba msaada (na sadaka) miili ile ya viumbe wako waovu na watu wa shari, ili nisije kunasa na kulazimika kumshukuru (na kumnyenyekea) yule aliyenipa, na kutumbukia katika (mtihani wa kutoa) lawama dhidi ya yule aliyeacha kunipa, hali ya kuwa Wewe ndiye wa pekee Mwenye usimamizi wa kutoa (Neema, Baraka na) riziki kwangu au kuzuia, na sio wao. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ صُنْ وَجْهِی بِالْیسَارِ، وَ لَا تَبْتَذِلْ جَاهِی بِالْإِقْتَارِ فَأَسْتَرْزِقَ أَهْلَ رِزْقِک، وَ أَسْتَعْطِی شِرَارَ خَلْقِک، فَأَفْتَتِنَ بِحَمْدِ مَنْ أَعْطَانِی، و أُبْتَلَی بِذَمِّ مَنْ مَنَعَنِی، وَ أَنْتَ مِنْ دُونِهِمْ وَلِی الْإِعْطَاءِ وَ الْمَنْعِ
27. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na nijaalie swiha na afya njema itakayotumika katika ibada, na raha na tafrija ambayo itakuwa na manufaa kwangu katika anga ya zuhdi, na elimu na maarifa yatakayo tumika katika matendo mema na amali njema, na Ucha Mungu utakaoniweka mbali na utendaji mbaya katika kila kitu kupita kiasi (imma kwa kutenda haraka kupita kiasi au kwa kutenda polepole kupita kiasi).
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ ارْزُقْنِی صِحَّةً فِی عِبَادَةٍ، وَ فَرَاغاً فِی زَهَادَةٍ، وَ عِلْماً فِی اسْتِعْمَالٍ، وَ وَرَعاً فِی إِجْمَالٍ
28. Eeh Mwenyezi Mungu! Maliza (na hitimisha) maisha yangu kwa msamaha (na maghfira yako), na utimize matakwa yangu katika kutarajia rehema zako, na unisahilishie njia yangu iwe nyepesi na laini ili niweze kuzifikia radhi zako, na katika hali zote, yafanye matendo yangu kuwa mazuri na mema.
اللَّهُمَّ اخْتِمْ بِعَفْوِک أَجَلِی، وَ حَقِّقْ فِی رَجَاءِ رَحْمَتِک أَمَلِی، وَ سَهِّلْ إِلَی بُلُوغِ رِضَاک سُبُلِی، وَ حَسِّنْ فِی جَمِیعِ أَحْوَالِی عَمَلِی
29. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, na uniamshe kutoka katika wakati wa usingizi mzito wa kutokuwa na habari na wewe (na kutokufanya dhikri na kukutaja na kukuabudu), na nijaalie katika zile siku za muhula niwe mwenye utiifu kwako, na nitengenezee njia rahisi kuelekea upendo wako, na kwa sababu hiyo (ya kutafuta upendo wako na radhi zako), nitimizie kheri za Duniani na Akhera.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ نَبِّهْنِی لِذِکرِک فِی أَوْقَاتِ الْغَفْلَةِ، وَ اسْتَعْمِلْنِی بِطَاعَتِک فِی أَیامِ الْمُهْلَةِ، وَ انْهَجْ لِی إِلَی مَحَبَّتِک سَبِیلًا سَهْلَةً، أَکمِلْ لِی بِهَا خَیرَ الدُّنْیا وَ الْآخِرَةِ
30. Eeh Mwenyezi Mungu! Mswalie Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad, kama vile salamu bora zaidi ulizomswalia mmoja wa waja wako kabla yake, na ambazo unamswalia mmoja wa viumbe wako baada yake, na unijaalie kheri ya Duniani na Akhera, na unilinde na kunihifadhi na adhabu ya Moto wa Jahanamu kwa Rehema zako.
اللَّهُمَّ وَ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، کأَفْضَلِ مَا صَلَّیتَ عَلَی أَحَدٍ مِنْ خَلْقِک قَبْلَهُ، وَ أَنْتَ مُصَلٍّ عَلَی أَحَدٍ بَعْدَهُ، وَ «آتِنا فِی الدُّنْیا حَسَنَةً وَ فِی الْآخِرَةِ حَسَنَةً»، وَ قِنِی بِرَحْمَتِک «عَذابَ النَّارِ

Rejea

Vyanzo

  • Anṣārīyān, Ḥusayn. Dīyār-i Āshiqān: tafsīr-i jāmiʿ al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Tehran: Payām-i Āzādī, 1372 Sh.
  • Dārābī, Muḥammad b. Muḥammad. Rīyāḍ al-ʿārifīn fī sharḥ al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Edited by Ḥusayn Dargāhī. Tehran: Nashr-i Uswa, 1379 Sh.
  • Dhūʾilm, Muḥammad Ḥusayn. Nūr al-āfāq; sharḥ duʿā-yi makārim al-akhlāq. Tehran: Intishārāt-i ʿAlī Akbar Aʿlamī, 1370 Sh.
  • Falsafī, Muḥammad Taqī. Sharḥ wa tafsīr duʿā-yi makārim al-akhlāq. [n.p]. Daftar-i Nashr-i Farhang-i Islāmī, 1370 Sh.
  • Faḍl Allāh, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Āfāq al-rūḥ. Beirut: Dār al-Mālik, 1420 AH.
  • Fihrī, Sayyid Aḥmad. Sharḥ wa tarjuma-yi Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Tehran: Nashr-i Uswa, 1388 Sh.
  • Fayḍ al-Kāshānī, Muḥammad b. al-Murtaḍā al-. Taʿlīqāt ʿalā l-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Tehran: Muʾassisat al-Buḥūth wa l-Taḥqīqāt al-Thiqāfīyya, 1407 AH.
  • Jazāʾirī, ʿIzz al-Dīn. Sharḥ al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1402 AH.
  • Khātamī, Rūḥ Allāh. Āʾīna-yi makārim. Tehran: Nashr-i Zulāl, 1368 Sh.
  • Khalajī, Muḥammad Taqī. Asrār-i khāmūshān. Qom: Partuw Khurshīd, 1383 Sh.
  • Madanī Shīrāzī, Sayyid ʿAlīkhān. Rīyāḍ al-sālikīn fī sharḥ al-Ṣaḥīfa Sayyid al-Sājjidīn. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1435 AH.
  • Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Fī zilāl al-Ṣaḥīfa al-Sajjādīyya. Qom: Dār al-Kitāb al-Islāmī, 1428 AH.
  • Mamdūḥī Kirmanshāhī, Ḥasan. Shuhūd wa shinākht; tarjuma wa sharḥ Ṣaḥīfa-yi Sajjādīyya. Qom: Būstān-i Kitāb, 1388 SH.
  • Misbāḥ Yazdī, Muḥammad Taqī. Lessons of Makārim al-Akhlāq. The website of Ayatullah Misbah Yazdi.
  • Peywandī, Qāsim and Ibn al-Rasūl, Zahrā and Sayyid Muḥammad Riḍā and Khāqānī, Muḥammad. Sabkshināsī duʿā-yi makārim al-akhlāq. ʿUlūm-i ḥadīth, No 73, 1393 Sh.
  • The official website of grand Ayatullah Makarim Shirazi (Persian)