Tashahudi

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.

Tashahudi (Kiarabu: التشهد) ni katika mambo ya wajibu katika Sala katika rakaa ya pili baada ya sijida mbili na katika rakaa ya mwisho baada ya sijida mbili na ndani yake ina matamshi ya kukiri kwamba, Mungu ni Mmoja na kushuuhuudia Utume wa Muhammad (s.a.w.w) na vilevile kumswalia Bwana Mtume na watu wa nyumbani kwake: «اَشْهَدُ اَنْ لا اِلهَ اِلاَّ اللّهُ وَحْدَهُ لا شَریکَ لَهُ وَ اَشْهَدُ اَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَ رَسُولُهُ، اَللّهُمَّ صَلِّ عَلی مُحَمَّدٍ وَ الِ مُحَمَّدٍ ; Nashuhudia kwamba, hapana Mungu ila Allah!Yeye peke Yake, hana mshirika! Na ninashuhudia kwamba, Muhammad ni Mja Wake na Mtume Wake, Ewe Mwenyezi Mungu!, mtakie rehma Muhammad na kizazi cha Muhammad

Tashahudi ni katika vipengee ambavyo sio nguzo na ni kutokana na sababu hiyo ambapo licha ya kuwa kusoma tashahudi ni wajibu lakini kama mtu anayesali atasahau, Sala yake haitabatilika.

Dhikri

Mkao wa kikao cha tashahud (tahiyatu) katika sala

Tashahudi ni katika vipengee vya wajibu katika Sala.[1]. ambayo inaashiria kutamka shahada mbili (Nashuhudia kwamba, hapana Mungu ila Allah! Yeye peke Yake , hana mshirika! Na ninashuhudia kwamba, Muhammad ni Mja Wake na Mtume Wake) na kumsalia na kumtakia rehma Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake katika rakaa ya pili baada ya sijida mbili na katika rakaa ya mwisho baada ya sijida mbili na kabla ya kutoa Salamu ya Sala.[2]

Ali Mishkini, mmoja wa mafakihi wa Kishia anasema: Kwa mujibu wa nadharia mashuhuri vaina ya mafakihi wa Kishia, tamko la tashahudi liko namna hii:

«اَشْهَدُ اَنْ لااِلهَ اِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَریکَ لَهُ وَ اَشْهَدُ اَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَ رَسُولُهُ، اَللّهُمَّ صَلِّ عَلی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ ; Nashuhudia kwamba, hapana Mungu ila Allah!Yeye peke Yake , hana mshirika!, Na ninashuhudia kwamba, Muhammad ni Mja Wake na Mtume Wake, Ewe Mwenyezi Mungu! mtakie rehma Muhammad na kizazi cha Muhammad.[3]

Pamoja na hayo, kiwango cha wajibu cha tashahudi ambacho kimetajwa katika atahari na vitabu vya fikihi vya mafakihi wakubwa kama Allama Hilli na Muhaqiq Karaki ni kifupi nacho ni:

«أشهد أن لا إله إلّا الله و أشهد أن محمدا رسول الله اللهم صل على محمد و آل محمد ; Nashuhudia kwamba, hapana Mungu ila Allah! na ninashuhudia kwamba, Muhammad ni Mtume Wake, Ewe Mwenyezi Mungu! mtakie rehma Muhammad na kizazi cha Muhammad»[4]

Kwa msingi huo Allama Hilli ametilia shaka katika kitabu chake cha al-Nihaya juu ya kuwa wajibu kipengee cha: (وَحْدَهُ لا شَریکَ لَهُ) yaani Yeye peke Yake, hana mshirika.[5].

Hukumu

Baadhi ya hukumu za tashahudi ni:

  • Wakati wa kusoma tashahudi ni sharti kuchunga muwalat (mfuatanisho) kwa maana ya kusoma kwa kufuatanisha (bila kutenganisha), utaratibu, utulivu na kusoma maneno kwa usahihi.[6]
  • Ni mustahabu kwa anayeswali wakati wa kusoma tashahudi aweke mikono yake juu ya mapaja ya miguu yake, abananishe vidole na aangalie mapaja yake.[7]
  • Wakati wa kusoma tashahudi ni mustahabu kufanya tawarruk[8] ambayo ni kuweka mguu wa kushoto chini ya ugoko wa mguu wa kulia na anayeswali akalie paja la mguu wa kushoto.[9]
  • Wakati wa kutekeleza kipengee cha tashahudi ni mustahabu kusoma dhikri ambapo miongoni mwazo ni: (اَلْحَمدُلله) au (بِسْمِ اللهِ و بِاللهِ وَ الْحَمدُ لِلهِ وَ خَیرُ الأسماءِ لِله) [10] Na kusoma baada ya hapo ibara isemayo: وَ تَقَبَّلْ شَفاعَتَهُ وَارْفَعْ دَرَجَتَه ; Na ukubali uombezi wake na uinue daraja yake.[11]

Hukumu ya Kusahau Tashahudi

Kwa mujibu wa fat’wa ya Marajii Taqlidi ni kuwa, endapo mtu anayesali atasahau tashahudi na kisha akakumbuka kabla ya kutekeleza kipengee cha rukuu ya rakaa inayofuata, anapaswa kukaa mara moja na kusoma tashahudi na kisha kuendelea na Sala.[12] Kwa mujibu wa fat’wa ya Sayyid Muhammad Ridha Golpaygani, Sayyid Abul-Qassim al-Khui, Mirza Jawad Tabrizi na Lutfullah Safi Golpaygani ni kuwa, katika hali kama hii anayesali anapaswa kutekeleza sijida mbili za kusahau baada ya kukamilisha Sala yake.[13] Ikiwa mwenye kusali yupo katika rukuu au baada ya hapo, kisha akalumbuka kwamba, hakusoma tashahudi ya rakaa ya kabla, anapaswa baada ya kukamilisha Sala atekeleze tashahudi ya kadhwaa (ya kulipa) na kwa mujibu wa Tahadhari ya Wajibu atekeleze sijida mbili za kusahau kwa ajili ya tashahudi aliyoisahau.[14].

Rejea

  1. Allamah al-Hilli, Nihayat al-Ahkam, juz. 1, uk. 499, 1419 H.
  2. Mishkini, Mustalahat al-Fiqh, uk. 145-146, 1419.
  3. Mishkini, Mustalahat al-Fiqh, uk. 146, 1419.
  4. Allamah al-Hilli, Nihayat al-Ahkam, juz. 1, uk. 499, 1419 H; al-Muhaqqiq al-Karki, Jami' al-Maqasid, juz. 2, uk. 318, 1414 H.
  5. Allamah al-Hilli, Nihayat al-Ahkam, juz. 1, uk. 499, 1419 H.
  6. Mishkini, Mustalahat al-Fiqh, uk. 146, 1419.
  7. Shahid al-Awal, al-Durus, juz. 1, uk. 182, 1417 H.
  8. Shahid al-Awal, al-Durus, juz. 1, uk. 182; Muhaqqiq al-Karki, Rasail al-Muhaqqiq al-Karki, juz. 1, uk. 112, 1409 H.
  9. Muhaqqiq al-Karki, Rasail al-Muhaqqiq al-Karki, juz. 1, uk. 112, 1409 H.
  10. Al-Shahid al-Awal, al-Durus, juz. 1, uk. 182, 1417 H.
  11. Imam Khomaini, Taudhih al-Masail, uk. 239, 1424. 1424 H, Mas-alah Nambari. 1061
  12. Imam Khomaini, Taudhih al-Masail (muhashsha) juz. 1, uk. 597, 1424 H, Mas-alah. 1102.
  13. Imam Khomaini, Taudhih al-Masail (muhashsha) juz. 1, uk. 597, 1424 H, Mas-alah. 1102.
  14. Imam Khomaini, Taudhih al-Masail (muhashsha) juz. 1, uk. 597, 1424 H, Mas-alah. 1102.

Vyanzo

  • Imam Khomaini, Sayid Ruhullah. Taudhih al-Masail (Muhashsha). Tas-hihi: Sayid Muhammad Hussein bani Hashim Khomaini. Qom: Daftar Intesharat Islam Vabaste be Jamiah Mudarrisin Hauzah Ilmiah Qom, 1424 H.
  • Al-Shahid al-Awal, Muhammad bin Makki. Al-Durus al-Shar'iyah fi Fiqh al-Imamiyah. Qom: Qom: Daftar Intesharat Islam Vabaste be Jamiah Mudarrisin Hauzah Ilmiah Qom, 1417 H.
  • Allamah al-Hilli, Hussan bin Yusuf. Nihayat al-Ahkam fi Ma'rifat al-Ahkam. Qom: Muasese Al al-Bait alaihimussalam, 1419 H.
  • Al-Muhaqqiq al-Karki, Ali bin Husain. Jami' al-Maqasid fi Syarh al-Qawa'id. Qom: Muasese Al al-Bait alaihimussalam, 1414 H.
  • Mishkini, Mirza Ali. Mustalahat al-Fiqh wa Mu'dhamu 'Anawinihi al-Maudhu'iyah. Qom: al-Hadi, 1419 H / 1377 S.