Mahali alipozikwa Bibi Fatima (a.s)

Kutoka wikishia
Makala hii inazungumzia mahli alipozikwa Bibi Fatma (a.s). Kama unataka kujua kuhusiana na matukio yanayohusiana na hili angalia makala ya kusindikizwa na kuzikwa Bibi Fatma (a.s) na kufa shahidi Bibi Fatma (a.s).

Mahali alipozikwa Fatma (a.s) (Kiarabu: موقع قبر السيدة فاطمة (ع)) ni sehemu isiyojulikana ambapo imejaaliwa na inadhaniwa kuwa, huenda akawa amezikwa katika nyumba yake, Rawdhat al-Nabi, Baqi na nyumba ya Aqil (iliyokuwa karibu na makaburi ya Baqi’i). Kuzikwa katika Nyumba ya Fatima (a.s) inajulikana kama rai maarufu baina ya wanachuoni wa Shia; ingawa Sheikh Tusi anaamini kwamba wengi wa wanazuoni wa Kishia wanaona kuzikwa katika Rawdhah al-Nabi kuwa ndio rai yenye ni nguvu zaidi. Kwa mujibu wa Allama Majlisi, kwa mujibu wa imani ya Kishia, Rawdha inajumuisha pia nyumba ya Fatima (a.s). Ni kwa sababu hii ndio maana, watafiti wengine wamezingatia na kutanguliza rai na mtazamo wa Rawdha mbele ya kauli ya nyumba.

Sayyid Jafar Murtadha Amili ambaye ni mwanahistoria anasema kuwa, haiwezekani kubainisha kwa uhakika eneo na mahali lilipo kaburi la Bibi Fatima (a.s). Kwa mujibu wa Sheikh Tusi na Amin al-Islam Tabarsi, ni bora kumtembelea na kumzuru Hazrat Fatimah (a.s) katika sehemu zote tatu: Rawdhah al-Nabi, Nyumba ya Fatima (a.s) na Baqi’i.

Shia wanaamini kwamba sababu ya kutojulikana lilipo kaburi la Fatimah (a.s) ni kwamba, alizikwa kwa siri, jambo ambalo lilikuwa ni kwa wasia wa Fatima mwenyewe. Kwa mujibu wao, Fatima (a.s) aliusia kwamba, hataki watu waliomdhulumu Fadak, waliomuudhi na kupora ukhalifa wausalie mwili wake na kuhudhuria mazishi yake. Kwahiyo, alitaka mazishi yake yafanyike kwa siri, na mahali pa kaburi lake pia pawe ni sehemu ya siri na pasipojulikana.

Wanachuoni wengi wa Kisunni wanalichukulia kaburi la Hadhrat Fatima (a.s) kuwa lipo katika makaburi ya Maimamu Baqi'i. Baadhi ya wahakiki wa Kishia wanaamini kuwa, nia na msukumo wa kutoa rai hii ni kupunguza shinikizo la kiitikadi la wafuasi wa Ushia kuhusiana na kuwa siri na kutojulikana lilipo kaburi la Fatima (a.s).

Kumeandikwa athari mbalimbali kuhusu mahali alipozikwa Hazrat Fatima (a.s) kama vile kitabu "Marqad Sayyidat al-Nisaa Fatima al-Shahidah al-Zahra (a.s), Fi ayyi Makani na Ayna Qabru Fatima.

Umuhimu wa sehemu ya kuzikwa

Suala la eneo na mahali alipozikwa Bibi Fatima (a.s) limeingia katika vitabu vya teolojia ya Shia na usiri wake umetumika kumlaumu Abu Bakr Khalifa wa Kwanza. [1] Waislamu wa madhehebu ya Shia wanalitambua suala la kutofahamika mahali alipozikwa Bibi Fatima (a.s) kuwa ni uthibitisho wa kuchukizwa kwa Fatima na Abu Bakr na Umar na wanapinga unyakuzi wa ukhalifa na ardhi ya Fadak. [2] Kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Hussein Jalali (aliyefariki dunia 2020), Fatima aliusia azikwe kwa siri ili mambo ya kifo chake isisahaulike katika historia sababu ya kifo chake. [3]

Suala la kutofahamika na kuwa siri sehemu alipozikwa Bibi Fatima limeakisiwa katika tungo za mashairi pia. [4] Mfano wa hilo ni tunzo na beti za mashairi za Sayyid Muhammad Hussein Shahriyar, mshairi wa Kiirani. [5]

Maeneo dhaniwa

Maulamaa wa Kishia wametaja baadhi ya maeneo ambayo wanasema, kuna uwezekano Bibi Fatima akawa amezikwa katika mojawapo ya maeneo hayo. [6] Wameitambua raia ya kuzikwa Fatma katika nyumba yake kuwa ni mashuhuri; [7] ingawa Sheikh Tusi anaamini kwamba wengi wa wanazuoni wa Kishia wanaona kuzikwa katika Rawdhah al-Nabi kuwa ndio rai yenye ni nguvu zaidi. [8] Kuna dhana zingine pia zilizotajwa katika vyanzo vya Kishia ikiwemo Baqi’i [9] na nyumba ya Aqeel (iliyokuwa karibu na makaburi ya Baqi’i).

Sayyid Jafar Mortadha Amili ambaye ni mwanahistoria anasema kuwa, ni muhali kubainisha kwa uhakika eneo na mahali lilipo kaburi la Bibi Fatima (a.s). [11] Kwa mujibu wa Sheikh Tusi [12] na Amin al-Islam Tabarsi [13], ni bora kumtembelea na kumzuru Bibi Fatima (a.s) katika sehemu zote tatu: Rawdhah al-Nabi, Nyumba ya Fatima (a.s) na Baqi’i. [14] Sayyid Ibn Tawus ameitaja sehemu ya ziara katika kitabu cha Misbah al-Zair kuwa ni Rawdhat al-Nabi [15] lakini katika kitabu cha Iqbal kimetajwa chumba cha Mtume (s.a.w.w). [16]

Nyumba ya Fatima (a.s)

Kadhalika angalia: Nyumba ya mtukufu Bibi Fatima (a.s)

Rai mashuhuri baina ya wanazuoni wa Kishia ni kuwa, Bibi Fatma alizikwa katika nyumba yake. [17] Sheikh Saqud, [18] Ibn Idris Hilli, [19] Ibn Tawus, [20] Allama Majlisi [21] na Sayyid Muhsin Amin [22] wameitambua nadharia hiyo kuwa yenye nguvu zaidi kuliko dhana na rai zingine. Hoja yao ni hadithi [23] iliyopokewa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) ambayo kwa mujibu wake, Bibi Fatima amezikwa katika nyumba yake na kufuatia upanuzi uliofanywa na Bani Umayya kwa msikiti wa Mtume (Masjid al-Nabi), kaburi hilo kwa sasa lipo ndani ya msikiti huo. [24]

Baadhi ya wanazuoni wa Kishia wanasema kuwa, hadithi ambayo Imamu Ali (a.s) anamtambulisha Fatima kama “uliyezikwa kando ya Mtume”, [25] kwamba, inaunga mkono dhana na nadharia ya kwamba, Fatima amezikwa katika nyumba yake; kwani sehemu ya karibu zaidi kutoka alipozikwa Mtume (s.a.w.w) ilikuwa nyumba ya Fatima (a.s). [26] Kuona fakhari kuzikwa kando ya Mtume (s.a.w.w) ni uthibitisho mwingine wa raia hii kama alivyousia Imam Hassan pia ya kwamba, kama itawezekana azikwe jirani na Mtume (s.a.w.w). [27]

Baadhi ya wahakiki wa Kishia wanasema kuwa, dhana na uwezekano wa kuzikwa Bibi Fatima katika nyuma yake uunakinzana na hadithi kutoka kwa Imamu Ali (a.s) zinazozungumzia kwamba, aliutoa mwili wa Fatima ndani ya nyumba kwa ajili ya usindikizaji na mazishi. [28] Katika kujibu hilo imeelezwa kuwa, usindikizaji wa jeneza haukuwa na uhalisia, [29], bali hilo na mengineyo yalifanyika ili kuwafanya watu wasitambue kaburi halisi la Fatima lilipo. [30] Mmoja wa wahakiki wa Kishia anaamini kwamba, usindikizaji huo wa jeneza ulifanyika katika nyumba nyingine ya Ali na Fatima iliyokuwa kaburi la Baqi’i kuelekea katika nyumba nyingine ya Fatima (a.s). [31] Anaamini kwamba, matukio ya baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w) likiwemo la kuhujumiwa na kuvamiwa nyumba ya Fatima (a.s) yalifanyika katika nyumba ambayo ipo jirani na Baqi’i. [32]

Rawdhat al-Nabi

Kadhalika angalia: Rawdhat al-Nabi

Katika kitabu chake Al-Muqna'a Sheikh Mufid anaona uwezekano wa Fatima (a.s) kuzikwa katika Rawdhat al-Nabi kuwa ni sahihi [33] na Sheikh Tusi, mwanachuoni wa Kishia, amezingatia kauli ya kuzikwa kwa Fatima (a.s) katika Rawdha kama itikadi ya wanavyuoni wengi wa Kishia. [34] Rawdhat al-Nabi mi umbali kati ya mimbari na kaburi la Mtume (s.a.w.w) katika Masjid al-Nabi, ambapo Mtume alipaita kuwa Rawdha (tafsiri: ardhi ya kijani kibichi [35]) ni katika eneo miongoni mwa maeneo ya peponi. [36] Kwa mujibu wa hadithi iliyoko katika kitabu cha Maani al-Akhbar, Mtume (s.a.w.w) alitaja sababu ya eneo hilo kuwa Rawdha kwamba, ni kuzikwa hapo Bibi Fatima (a.s). [37]

Amin al-Islam Tabarsi, mfasiri na mwanateolojia wa karne ya 6 Hijiria, [38] na Ibn Shahrashub, mfasiri na mwanateolojia wa karne ya 6 Hijiria, [39] wameuhesabu uwezekano wa mitazamo miwili ya kuzikwa katika nyumba na Rawdha kuwa ipo karibu zaidi na ukweli. Sheikh Tusi alizingatia uwezekano wa mitazamo hii miwili kuwa inakaribiana [40] na Allama Majlisi aliiona mitazamo hiyo miwili kwamba, inawezekana kuijumuisha; kwa sababu kwa mujibu wa imani ya Waislamu wa Kishia, Rawdha inajumuisha pia nyumba ya Fatima (a.s) [41] Ni kwa sababu hii, baadhi ya wanachuoni wameichukulia kauli na rai ya Rawdha kuwa inathibitisha na kuunga mkono kauli na mtazamo wa kuzikwa katika nyumba yake. [42]

Makaburi ya Baqi’i

Kwa mujibu wa Bahau al-Din Irbili mwandishi wa historia wa Kishia wa karne ya 7 Hijiria ni kuwa, ni mashuhuri baina ya watu na wanahistoria kwamba, Fatima amezikwa Baqi’i. Ametaja pia hadithi zinazounga mkono nadharia hii. Hata hivyo hajaainishwa sehemu maalumu katika makaburi ya Baqi’i. [43]

Sheikh Tusi [44] na Amin al-Islam Tabarsi [45] wameuona uwezekano huo kuwa ni jambo lililo mbali. Kwa mujibu wa riwaya iliyomo ndani ya kitabu Al-Kafi, Fatima (as) hakuzikwa Baqi’i. [46] Kwa mujibu wa riwaya hii, Imam Hassan (a.s.) alimuusia Imamu Hussein kwa kumwambia: “Baada ya kufa kwangu shahidi nipeleke katika kaburi la Mtume (saww) ili nikajadidishe baia na kiapo cha utiifu. Kisha nirudishe kwenye kaburi la mama yangu na unichukue kutoka huko hadi Baqi'i.[47]

Nyumba ya Aqil

Kadhalika angalia: Majengo na Baqi’i na makaburi ya Maimamu wa Kishia

Katika kitabu cha Misbah al-Anwar Allama Majlisi ametaja hadithi inayoeleza kwamba, Bibi Fatma amezikwa katika nyumba ya Aqeel. [48] Nyumba ya Aqeel bin Abi Twaib ilikuwa nje ya makaburi ya Baqi’i ingawa ni jirani na makaburi hayo [49] na baada ya kuzikwa hapo Abbas bin Abdul-Muttalib na Maimamu Wanne ikaondoka katika hali ya makazi na kuwa eneo la watu kufanya ziara [50] na kwa kupanuliwa Baqi’i ikaunganishwa nalo. [51]

Muhammad Hussein Farahani mshairi na mwandishi wa kipindi cha utawala wa Qajar nchini Iran ametoa ripoti katika kitabu chake cha simulizi za safari baina ya miaka ya 1302 na 1303 Hijria Shamsia juu ya uwepo wa kaburi katika eneo la Baqi’i ambalo lilikuwa likinasibishwa na Fatima na Shia na Sunni walikuwa wakifanya ziara hapo. [52]

Mtazamo mashuhuri baina ya Maulamaa wa Kisuni ni kwamba, kaburi la Bibi Fatima linapatikana katika ardhi ya Baqi’i mahali walipozikwa Maimamu. [53] Moja ya hoja zao za kuthibitisha hilo ni wasia wa Imamu Hassan wa kutaka kuzikwa kando ya mama yake yaani Fatima (a.s). [54] Mkabala na mtazamo huo, Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kwamba kwa mujibu wa hadithi [55] ni kwamba: Fatima aliyezikwa Baqi’i ni Fatima binti Assad mama wa Imamu Ali bin Abi Talib (a.s). [56] Muhammad Sadiq Najmi mhakiki wa Kishia anaamini kwamba, waandishi wa Kisuni walifanya hima na juhudi za kutambulisha kaburi la Fatima (a.s) kuwa lipo katika haram ya Maimamu waliozikwa Baqi’i ili ni kupunguza shinikizo la kiitikadi la wafuasi wa Ushia kuhusiana na kuwa siri na kutojulikana lilipo kaburi la Fatima (a.s). [57]

Katika vyanzo vya Sunni, kuna uwezekano mwingine umetajwa wa mahali alipozikwa Fatima (a.s). Baadhi yao ni kama ifuatavyo: Nyumba yake, [58] Rawdhat al-Nabi, [59] pembe ya nje ya nyumba ya Aqil bin Abi Talib [60] na Bait al-Ahzan. [61]

Kwa nini kaburi lisitambulike

Kadhalika angalia: Wasia wa Bibi Fatima (a.s) na kusindikizwa na kuzikwa Bibi Fatima (a.s)

Maulamaa wa Kishia wanaamini kwamba, sababu ya Bibi Fatima kuwa ni jambo la siri na kutofahamika lilipo kutokana na kuzikwa kwa siri ni wasia wake. [62] Fatima (a.s) aliusia kwamba, hataki watu waliomdhulumu Fadak, waliomuudhi na kupora ukhalifa wausalie mwili wake na kuhudhuria mazishi yake. Kwa hiyo, alitaka mazishi yake yafanyike kwa siri, na mahali pa kaburi lake pia pawe ni sehemu ya siri na pasipojulikana. [63] Kwa mujibu wa Sheikh Mufid [64] na mwandishi wa kitabu cha Dalail al-Aimah, [65] Fatima aliusia kwamba, kaburi liwe siri na lisifahamike. Imamu Ali (a.s) alimzika kwa siri usiku Bibi Fatima [66] na baada ya kuzikwa tu, Imamu Ali (a.s) alitawanya athari za kaburi hilo, ili kaburi hilo lisijulikane. [67] Kisha baada ya hapo akayafanya makaburi 40 [68] na wengine wanasema makaburi saba [69] ili kaburi la Fatima lisifahamike. Imekuja katika baadhi ya vyanzo vya Ushia Omar bin al-Khattab alichukua uamuzi wa kufukua makaburi ili amswalie Sala ya maiti Bibi Fatima; lakini alilazimika kuachana na uamuzi huo baada ya tishio la Imamu Ali (a.s). [70] Inaelezwa kuwa, hakuna kaburi ambalo limenasibishwa na Fatima kwa sura ya kuwa na uhakika wa mia kwa mia. [71] Kadhi Nurullah Shushtari [72] na Sayyid Muhammad Shirazi [73] mmoja wa Maulamaa wa Kishia ni kuwa, siku ya kufahamika na kueleweka kaburi la Bibi Fatima (a.s) ni baada ya kudhihiri Imamu Mahdi (a.t.f.s) na Imamu Mahdi ndiye atakayefichua hilo; hata hivyo hakutaja sababu ya hilo. Ali bin Abdallah Samhudi mwandishi wa Ahlu Sunna (aliaga dunia 911 Hijria) anasema kuwa, moja ya sababu za kuwa siri kaburi la Bibi Fatima (a.s) ni kutoenea na kuzoeleka suala la kuimarishwa makaburi kwa matofali na chokaa mwanzoni mwa Uislamu. [74] Amekosoa hoja hii; kwa sababu kuna makaburi ya masahaba na kaumu zingine za Mtume (s.a.w.w) yanafahaamika na kueleweka. [75]

Monografia

Baadhi ya vitabu ambavyo vimeandikwa vikiwa na maudhui ya kuzikwa Bibi Fatima (a.s) ni:

  • Marqad Sayyidat al-Nisa' Fatimat al-Shahidat al-Zahra (a.s) fi ayy makan? (Kaburi na Bibi Fatima liko wapi?); kimeandikwa na Hashim Naji Musawi Jazairi. Kitabu hiki kimekusanya hadithi zilizopokewa na Mashia kuhusiana na sababu ya kuwa siri na kufichwa kaburi la Bibi Fatima (a.s) na uwezekano wa maeneo ambayo huenda ndipo alipozikwa Bibi Fatima (a.s). [76] Kitabu hiki kilisambazwa 1395 Hijiria Shamsia. [77]
  • Aina Qabr Fatima (a.s)? Mwandishi: Hussein Radhi. Kitabu hiki kimetajwa maeneo ambayo kuna uwezekano Bibi Fatima akawa amezikwa katika mojawapo ya maeneo hayo na kutambua rai ya kuzikwa nyumbani kwake Bibi Fatima kuwa ndio sahihi. [78] Kitabu hiki kilichapishwa Beirut, Lebanon 1432 Hijiria. [79]

Kadhalika kuna vitabu vingine kama “Qabr Madaram Kojast”, (kaburi la mama yangu liko wapi?), Dar Justejui mazar bi neshan madaram Zahra (a.s), “Katika kutafuta eneo la ziara lisilo la utambulisho la mama yangu Fatima”, Mwandishi: Ummul al-Muhsin [80] na “Razi Sadaf: Qabr Makhfi Bibi Fatima kwa mtazamo wa kisiasa na Kiirfani”, mwandishi Mehrdad na Uways Karami katika maudhui hii. [81].