Haritha bin Nu'man

Kutoka wikishia

Haritha bin Nu'man (Kiarabu: حارثة بن النعمان) (aliaga dunia: 50 Hijiria) ni mmoja wa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali bin Abi Talib (a.s). Haritha bin Nu'man alishiriki katika Vita vya Badr, Uhud na Hunayn kama ambavyo alishiriki pia katika vita vya utawala wa Imamu Ali (a.s). Haritha alitoa zawadi nyumba yake kwa Mtume (s.a.w.w) ili aishi humo na wake zake. Kadhalika alitoa zawadi nyumba kwa Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kuishi Imamu Ali na Fatima (a.s). Haritha alifanikiwa kumuona mara mbili Malaika Jibril katika sura ya Dihyah al-Kalbi na akamsalimia. Kuna hadithi zilizopikewa na Haritha kutoka kwa Mtume ambazo zimenukuliwa katika vyanzo na vitabu vya hadithi.

Daraja

Haritha bin Nu'man alikuwa mmoja wa masahaba wa Bwana Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali bin Abi Talib (a.s). [2] Haritha bin Nu'man akiwa pamoja na Mtume (s.a.w.w) alishiriki katika Vita vya Badr, [3] Uhud, Hunayn na vita vingine.[4] Sheikh Tusi anasema, Haritha bin Nu'man alishiriki katika vita vya zama za utawala wa Imamu Ali (a.s) akiwa upande wa Imamu Ali (a.s). [5]

Haritha ni miongoni mwa masahaba wanaotambulika kwamba, katika Vita vya Hunayn baada ya baadhi ya Waislamu kukimbia vita kutokana na hujuma na shambulio la washirika yeye alibakia kando ya Mtume (s.a.w.w) na kumhami. [6]

Nafasi yake katika uga wa hadithi

Harithi alikuwa mmoja wa wapokezi wa hadithi [7] ambaye inaelezwa kuwa, hadithi alizopokea zimekuja katika vitabu vya hadithi ambavyo vimejumuisha maudhui zote (Jawami' Riwai), vitabu vya wasifu wa wapokezi wa hadithi na vyanzo vya kihistoria kama Musnad Ahmad bin Hanbal, kitabu al-Maghazi, al-Mu'talif wa al-Mukhtalif. [8] Wapokezi wa hadithi kama Abdallah bin Abbas, Abdallah bin Amir Rabi'ah na Tha'labah bin Abi Malik wamepokea hadithi za Mtume (s.a.w.w) kupitia kwake. [9]

Kumuona Jibril

Katika vitabu vya wasifu wa masahaba, Haritha anatajwa kuwa mmoja wa masahaba waliokuwa na fadhila na daraja kubwa. [10] Kwa mujibu wa SheIkh Tusi, Haritha alifanikiwa kumuona mara mbili Malaika Jibril katika sura ya Dihyah al-Kalbi na akamsalimia. [11] Kadhalika Ibn Abdul-Barr ameandika katika kitabu chake cha al-Isti’ab kwamba: Kutokana na Haritha kumsaidia na kumheshimu mama yake aliondokea kuwa mashuhuri kwa wema. [12]

Kutoa nyumba zake na kumpatia Mtume (s.a.w.w)

Haritha anahesabiwa kuwa mtu wa kwanza aliyempa Mtume nyumba zake kama zawadi huko Madina. [13] Kwa mujibu wa Ibn Saad, mwanahistoria wa karne ya 3 Hijiria, vyumba vya Haritha vilikuwa karibu na vyumba vya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). [14] Kila mara Mtume (s.a.w.w) alipofunga ndoa na kuoa mke mwingine, Haritha alikuwa akihama kutoka chumba kimoja hadi kingine, na kwa njia hii alimpa Mtume (s.a.w.w) nyumba zake zote ili aishi na wake zake. [15] Miongoni mwazo ilikuwa ni nyumba ya kwanza ya Maria, [16] na pia nyumba ambayo Mtume alimpa Safiya ambapo, Aisha na wanawake wa Ansari walikuwa wakienda kwenye nyumba hiyo kumuona. [17] Mtume (s.a.w.w) alimuombea dua Haritha kutokana na kutoa nyumba zake kwa Mtume (s.a.w.w) na Muhajirina [18].

Kutoa zawadi nyumba kwa ajili ya kuishi Ali na Fatima (a.s)

Makala kuu: Nyumba ya Bibi Fatima (a.s)

Mwanahistoria wa Kisunni Ibn Saad (aliyefariki dunia: 230 AH) ameandika katika kitabu chake cha Tabaqat al-Kubra akinukuu kutoka kwa Imam Baqir (a.s) kwamba, Imam Ali (a.s) baada ya kumuoa Fatima (a.s), alitayarisha nyumba ambayo ilikuwa mbali kidogo na nyumba ya Mtume. Mtume (s.a.w.w) alisema kwamba anataka binti yake aishi karibu na nyumba yake. Fatima (a.s) alimuomba Mtume (s.a.w.w) aongee na Haritha ili waweze kuishi katika nyumba yake. [19] Mtume (s.a.w.w) alisema kwamba aliona haya kumwambia Haritha kuhusu hili; kwa sababu tayari Haritha alimpa baadhi ya nyumba zake, na kwa sababu yake, alihama kutoka chumba kimoja hadi kingine. [20] Haritha alipata habari ya jambo hilo na akatoa nyumba yake na kumpa zawadi Mtume (s.a.w.w). [21] Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya waislamu wa madhehebu ya Shia, baada ya Ali na Fatima (a.s) kuoana waliishi katika nyumba ambayo Haritha alimpa Mtume (s.a.w.w) kama zawadi. [22]

Ibn Shabbah (aliyefariki: 262 AH) mwanahistoria wa Kisunni amesema kwamba, nyumba ya Haritha ilikuwa karibu na nyumba ya Abu Ayyub Ansari na ikawa mali ya Imamu Sadiq (a.s) na ikawa makazi yake. [23] Nyumba hii ilibomolewa katika mpango wa maendeleo wa mwaka 1365 Hijiria Shamsia. [24]

Nasaba na kuaga kwake dunia

Haritha ni mtoto wa Nu’man bin Naf’i au ibn Naq’i [25] al-Ansari al-Khazraj [26] na Ja’dah binti Ubaid bin Tha’labah.[27] Lakabu yake ni Aba Abdillah [28] na anatokana na kabila la Bani Najjar na alikuwa akiishi Madina [ 29] [30]. Kutokana na kushiriki kwake katika katika Vita vya Badr, katika baadhi ya vyanzo, ametajwa pia kama Haritha bin Nu'man Ansari Badri. [31] Inasemekana kwamba Muhammad bin Abdul-Rahman bin Abdullah bin Haritha, anayejulikana kama. Abu Al-Rajal, ni mmoja wa wajukuu zake. [32]

Ibn Hibban (aliyefariki: 354 AH), mwandishi wa Kisunni wa wasifu wa wapokezi wa hadithi, amesema akitegemea hadithi moja kwamba, Haritha aliuawa shahidi katika Vita vya Badr; [33] lakini baadhi wamekataa rai ya Ibn Hibban kutokana na kuwepo kwa Haritha katika vita vingine vya zama za Mtume (s.a.w.w). [34] Kwa mujibu wa riwaya ya Ibn Saad (aliyefariki: 230 Hijiria), wanahistoria wametosheka tu na kusema kuwa, Haritha alikufa wakati wa ukhalifa wa Muawiyah. [35] Hata hivyo, Dhahabi (aliaga dunia: 748) ametambua mwaka wa kufa Haritha kuwa ni wa 50 Hijria. [36]