Kuchinjwa Ismail
Kuchinjwa Ismail (Kiarabu: ذبح إسماعيل) ni amri na mtihani ambao Mwenyezi Mungu alimpatia Nabii Ibrahim (a.s). Nabii huyo wa Allah alioteshwa na kupewa amri ya kumchinja na kumtoa dhabihu mwanawe Ismail. Baba na mwana (Ibrahim na Ismail) walikubaliana na amri ya Mwenyezi Mungu; akaanza kufanya hivyo lakini kisu hakikukata, kisha ukatokea mwito kutoka kwa Mwenyezi Mungu; Tukamwita, tukamwambia, Ewe Nabii Ibrahim ndoto yako hiyo. Hivyo ndivyo tunavyowalipa watu wema. Hakika huo ulikuwa mtihani ulio wazi. Tulimkomboa mwanawe kwa kafara kubwa. Akaletwa kondoo dume kutoka peponi na akapatiwa Ibrahim amchinje badala ya mwanawe Ismail. Sunna ya kuchinja katika siku ya Eidul Adh’ha inakumbusha tukio la amri ya kuchinjwa Ismail. Kwa mujibu wa baadhi ya nukuu, kurushwa mawe ya kumpiga shetani (Rami Jamarat) kulifanywa na Nabii Ibrahim katika tukio la amri ya kuchinjwa Ismail.
Kwa mujibu wa Hadithi na mlolongo wa Aya, Waislamu wa Kishia wanamuita Nabii Ismail kwa jina la Dhabihullah; lakini Mayahudi wanamuita Nabii Is’haka kwa lakabu ya Dhabihullah na huku Waislamu wa madhehebu ya Sunni wakiwa wana mitazamo tofauti katika hili.
Ndoto ya Ibrahim (a.s)
Kwa mujibu wa Aya za Qur’an, Nabii Ibrahim (a.s) aliota ndoto ya kwamba, anamchinja mwanawe. [1] Imekuja katika hadithi ya kwamba, ndoto hii ilijikariri mara tatu. [2] Hata hivyo baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba, si jambo lililo mbali kwamba, baada ya ndoto hii bado Nabii Ibrahim akawa na shaka na Mwenyezi Mungu akaondoa shaka yake hiyo kwa Wahyi wa wazi. [3]
Kumchinja Mtoto
Baada ya Nabii Ibrahim kuota ndoto kwamba, anamchinja mwanawe, na ndoto hiyo kujikariri mara tatu, alimsimulia mwanawe na kutaka kujua mtazamo wake. Qur’an tukufu inaeleza mashauriano hayo kwa kusema: Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri [4]
Kwa mujibu wa hadithi zilizonukuliwa katika kitabu cha al-Kafi, baada ya kufikia uamuzi wa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, Ismail alisema: Ewe baba! Nifunike na unifunge miguu yangu. Nabii Ibrahim akamfunika lakini akaapa kwamba, wakati wa kutofunga miguu yake wakati wa kumchinja. [5] Wakati paji la Ismail lilipokuwa ardhini, [6] Ibrahim alitoa kisu na kukiweka katika shingo ya Ismail ili amchinje, lakini Jibril alizuia kisu kukata. Ibrahim alijitahidi kukata shingo ya Ismail mara kadhaa lakini kisu hakikukata. [7] Kisha ukashuka Wahyi: (یا إِبْرَاهِیمُ قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْیا ; Ewe Ibrahim! Umekwisha itimiliza ndoto (umetekeleza amri ya Mwenyezi Mungu). [8] Kisha akaletewa kondoo dume kutoka peponi na akapatiwa Ibrahim akamchinja badala ya mwanawe Ismail. [9]
Qur’an tukufu inautaja mtihani huo wa Nabii Ibrahim namna hii: (إِنَّ هذا لَهُوَ الْبَلاءُ الْمُبینُ ; Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri). [10]
Kwa mujibu wa baadhi ya nukuu, shetani alifanya jitihada nyingi ili kuzuia amri hiyo ya Mwenyezi Mungu isitimizwe. Ili kufikia lengo hili, alifanya juhudi za kumpotosha Nabii Ibrahim, mke wake, na mtoto wake, na hakufanikiwa katika matukio yote matatu. [11] Kwa mujibu wa baadhi ya nukuu, kupigwa mawe shetani na Ibrahim huko Jamarat kulifanyika katika tukio la kuchinjwa Ismail. [12]
- Kadhalika Angalia: Rami al-Jamarat
Mazungumzo ya Nabii Ibrahim na Mzee
Katika baadhi ya hadithi zizliopokewa na Waislamu wa Kishia, kumenukuliwa mazungumzo baina ya Ibrahim na mzee mmoja; Mzee alimwambia Ibrahim: Unataka nini kutoka kwa mtoto huyu? Ibrahim: Ninataka kumchinja. Mzee: Subhanallah! Unataka kumchinja mtoto na kumuua mtoto ambaye hana dhambi yoyote? Ibrahim: Mwenyezi Mungu ameniamrisha nimchinje mtoto huyu. Mzee: Hapana, kimsingi Mwenyezi Mungu wako amekukataza kufanya jambo kama hili na shetani ndiye aliyekujia ndotoni na kukuamrisha jambo hili. Ibrahim: Ole wako! Amri hii imetoka kwa Mwenyezi Mungu. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sitazungumza tena na wewe. Mzee: Ewe Ibrahim! Wewe ni kiongozi ambaye watu wengine wanakufuata. Kama utamchinja mwanao, watu wengine pia watawachinja watoto wao. Ibrahim hakuzungumza naye tena. [14]
Kuchinjwa Ismail au Is’haq
- Makala asili: Dhabihullah
Qur’an Tukufu imeashiria tukio la kuchinjwa Ismail tu: Ibrahim akasema, Ewe mwanangu! [15] ama hii kwamba, mtoto huyu alikuwa ni Ismail au Is’haq kuna tofauti za kimitazamo. Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kwamba, Ismail ndiye dhabihullah [16] na wakiwa na lengo la kuthibitisha madai yao wanatumia Aya ya 112 ya Surat Saffat ambayo inatoa bishara ya kuzaliwa Is’haq baada ya kuzaliwa Ismail na huku tukio la kuchinjwa Ismail likiwa linasimuliwa katika Aya za 100-107 mbali na ukweli kwamba katika suala la Is’haq, habari njema ya Utume wake ilitolewa, yaani, lazima aishi na kutimiza kazi ya Utume, na hili haliafikiani na suala la kuchinja sivyo. [17] Pia kuna hadithi za Maasumina zilizonukuliwa ambazo zinamtambulisha Ismail kuwa ni dhabihu. [18]
Waislamu wa Kisunni wametofautiana kuhusiana na dhabihu. [19] Baadhi yao wakitegemea baadhi ya hadithi [20] wanatambua lakabu ya dhabihu kuwa ni ya Is’haq. [21] Katika kitabu cha Tafsir Nemooneh, kuna hadithi zinazotumiwa na kundi hili kama hoja yao ambazo zimetambuliwa kuwa ni Israiliyat na imeelezwa kuwa kuna uwezekano hadithi hizi zikawa zimebuniwa na Mayahudi. [22] Baadhi ya Masuni wengine wakitegemea kundi la hadithi zingine wanamtambua Ismail kuwa ni dhabihu. [23] Fakhrurazi na Ibn Ashur wamesema kuwa, uwezekano Ismail akawa ni dhabihu. [24]
Sunna ya Kuchinja
- Makala Asili: Eid al-Adh’ha
Eid al-Adh’ha au Eid Qurban (idi ya kuchinja) ni moja ya sikukuu kubwa zaidi za Waislamu. Sunna ya kuchinja katika sikukuu hii ni ukumbusho wa tukio la kuchinjwa Ismail. [25] Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, wanyama wote wanaochinjwa katika ardhi ya Mina siku ya Eid al-Adha ni fidia ya Ismail. [26]
Murtadha Mutahhari, mwandishi wa Kishia, anaamini kwamba, ukweli ni kuwa, Mwenyezi Mungu hakuwa akitaka Ismail achinjwe, kwa sababu halikuwa jambo muhimu au sifa maalumu kwa baba kumuua mwanawe kwa mikono yake mwenyewe, lakini ilikuwa ni mila na Sunna ambayo hapo kabla watu walikuwa wakiuwa na Ibrahim alipaswa kufuata mila hii... Na kama Ibrahimu angepinga kumchinja mwanawe, watu wangesema kwamba Ibrahim anaogopa kumtoa kafara mwanawe (kumfanya dhabihu), lakini Ibrahim alipofikia hatua ya kuwa tayari mia kwa mia kumchinja mwanawe kwa mikono yake mwenyewe, ikaja amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kubatilishwa milele dhabihu ya mwanadamu na badala yake kutokea dhabihu ya kondoo. [27]
Kuchinjwa Mtoto katika Torati
Torati inasimulia kisa cha kuchinjwa kwa mtoto kama ifuatavyo: Ilikuwa ni baada ya matukio hayo ndipo Mwenyezi Mungu alipomtia mtihani Abraham (Ibrahim) na kumwambia: Sasa mchukue mwanao, mwanao wa pekee umpendaye, Isaka (Is’haq). Nenda katika nchi ya Moria, huko, juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia, umchinje na kumtoa sadaka.[28]
Lakini wakati Ibrahim alipoamua kumtoa mwanawe dhabihu na kunyoosha kisu kuelekea kwa mtoto ili kukata kichwa cha mwanawe, malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita kutoka mbinguni na kumwambia: Usinyooshe mkono wako kwa kijana huyo na usimfanye chochote, kwa sababu sasa najua ya kuwa unamcha Mungu. Kwa sababu hukuninyima mwanao wa pekee.” [29] Hatimaye, Mungu akatuma kondoo dume na Ibrahim akamtoa dhabihu badala ya mtoto. [30]
Rejea
Vyanzo
- The Qur'an.
- The Bible.
- Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar. Mafātīḥ al-ghayb. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
- Ibn Abī l-Ḥātam, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Edited by Asʿad Muḥammad al-Ṭayyib. Third edition. Riyadh: Maktabat Nazār Muṣṭafā al-Bāz, 1419 AH.
- Ibn 'Ashur, Muhammad b. Tahir. Al-Tahrir wa al-tanwir. n.p., n.p., n.d.
- Kulaynī, Muaḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Fourth edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1374 Sh.
- Māzandarānī, Muḥammad Hādī b. Muḥammad Ṣāliḥ al-. Sharḥ furūʿ al-Kāfī. Edited by Muḥammad Jawād Maḥmūdī. Qom: Dār al-Ḥadīth li-l-Ṭibāʿa wa l-Nashr, 1429 AH.
- Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Ṭayyib Mūsawī Jazāʾrī. Qom: Dār al-Kitāb, 1404 AH.
- Qurtubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1364 Sh.
- Sayyid Quṭb. Fī ẓilāl al-Qurʾān. Beirut & Cairo: Dār al-Shurūq, 1412 AH.