Dhabihullah

Kutoka wikishia

Dhabihullah (Kiarabu: ذَبیح‌ُ الله) ni lakabu ya Ismail mtoto wa Nabii Ibrahim (a.s) ambaye Mwenyezi Mungu alitoa amri achinjwe na baba yake. Qur’an Tukufu imesimulia mkasa na tukio la kuchinjwa, lakini haijataja jina la kichinjwa (dhabihu). Waislamu wa madhehebu ya Shia wanamuita Nabii Ismail kwa jina la Dhabihullah; lakini Mayahudi wanamuita Nabii Is’haq kwa lakabu ya Dhabihullah na huku Waislamu wa madhehebu ya sunni wakiwa wana mitazamo tofauti katika hili ya kwamba, Dhabihullah ni Ismail au ni Is’haq.

Mkasa wa kuchinjwa

Makala asili: Kuchinjwa Ismail

Dhabihullah ina maana ya kutolewa muhanga au kuchinjwa na kukatwa kichwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Dhabihullah ni lakabu ya mmoja wa watoto wa Nabii Ibrahim ambapo Nabii huyo wa Allah alitakiwa na Mwenyezi Mungu amchinje na kumtoa muhanga katika njia ya Allah. [1] Kwa mujibu wa Qur’an Tukufu, Nabii Ibrahim aliota ndoto kwamba, anamchinja mwanawe, alimsimulia mwanawe na kutaka kujua mtazamo wake ambapo Ismail alisema, Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa. Baada ya wawili hao kusalimu amri mbele ya takwa la Mwenyezi Mungu, Ibrahim alimchukua mwanawe mpaka machinjioni na kumlaza ili amchinje. Katika hali hii ukaja wito kutoka mbinguni: Ewe Ibrahim! Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri. Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. [2] Kwa mujibu wa hadithi, kwa amri ya Mwenyezi Mungu Jibril alizuia kisu kukata. Kisha akaletewa kondoo dume kutoka peponi na akapatiwa Ibrahim akamchinja badala ya mwanawe Ismail. [3] Eid al-Adh’ha au Eid Qurban (idi ya kuchinja) ni moja ya sikukuu kubwa zaidi za Waislamu. Sunna ya kuchinja katika sikukuu hii ni ukumbusho wa tukio la kuchinjwa Ismail. [4] Kuchinja katika lugha ina maana ya kukata kichwa. [5]

Dhabihu ni lakabu ya nani?

Qur’an Tukufu imesimulia mkasa na tukio la kuchinjwa, lakini haijataja jina la dhabihu (kichinjwa). [6] Hii kwamba, Dhabihullah ni lakabu ya nani kati ya watoto wa Ibrahim, kuna mitazamo miwili; baadhi wanaona kuwa hiyo ni lakabu ya Ismail huku wengine wakitambua lakabu hiyo kuwa ni ya Is’haq. Allama Majlisi ameleta hadithi na riwaya zote mbili katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar. [7]

Ismail

Wafasiri wa madhehebu ya shia wakitegemea Aya za 101-103 katika Surat Safat wanaamini kuwa, Mwenyezi Mungu alitoa bishara kwa Ibrahim ya kuzaliwa Is’haq [8] baada ya bishara ya kuzaliwa Ismail na tukio la kuchinjwa. [9] [10] Ayatullah Makarim Shirazi anasema, watu ambao wanamtambua Is’haq kuwa ni Dhabihullah wanazitambua bishara mbili za Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim katika Qur’an kwamba, zinahusiana na Is’haq; bishara ya kwanza inahusiana na kuzaliwa na bishara ya pili wanaihusisha na Utume wake. Kwa mtazamo wake ni kuwa, Aya zilizotajwa ziko wazi kabisa bishara husika inahusiana na watoto wawili. [11] Kadhalika Allama Tabatabai anaamini kuwa, siyaq (mtiririko) na uwazi wa Aya hizi zinaashiria kuwa, Ismail ndiye Dhabihullah. [12]

Aidha katika baadhi ya hadithi, Ismail amearifishwa na kutambulishwa kuwa ni Dhabihullah. Miongoni mwazo ni hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ambayo amejiita yeye kuwa ni Ibn Dhabihein mtoto wa madhabihu wawili. [13] Kadhalika katika Dua al-Mashlul ambayo inanasibishwa kwa Imamu Ali (a.s) [14] na hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s), [15] na Imamu Ridha (a.s) [16], Ismail ametambulishwa kuwa ni Dhabihullah. Katika Ziyarat Ufaylah (Ziara makhsusi ya Imam Hussein (a.s) katika nusu ya Rajab) Imam Hussein anasalimiwa hivi kwa anuani ya mrithi wa Ismail ambaye ni Dhabihullah. [17]

«السَّلامُ عَلَیک یا وارِثَ إسماعیلَ ذَبیحِ اللّه»

Amani iwe juu yako ewe mrithi wa Ismail Dhabihullah.

Baadhi ya waandishi wameyatambua matukio ya kuhajiri Hajar na kuzaliwa Ismail kwamba, yana uhusiano na tukio la kuchinjwa na kwamba, kuchinjwa Ismail ni kamilisho la hayo. [18] Sheikh Saduq sambamba na kuashiria hitilafu za hadithi anamtambua Ismail kuwa ndiye Dhabihullah na kisha anasema: Kwa kuzingatia kuwa, Is’haq alizaliwa baada ya mkasa na tukio la kuchinja, alikuwa akitamani lau angekuwa yeye yule mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimuamrisha baba yake amchinje; lakini kama ilivyokuwa kwa Ismail naye alisalimu amri mbele ya amri ya Mwenyezi Mungu na akawa ni mwenye subira na akafikia daraja ya Ismail katika thawabu. [19]

Baadhi ya wafasiri wa Ahlu-Sunna wakitegemea baadhi ya hadithi wanamtambua Ismail kuwa ni Dhabihullah. Kauli hiyo imenasibishwa na Abu Hurairah, Amir bin Wathilah, Abdallah ibn Omar, Ibn Abbas, Said ibn Musayyib, Yusuf ibn Mehran, Rabiu ibn Anas na kadhalika. [20] Kadhalika Fakhru Razi na Ibn Ashur wamesema kuna uwezekano dhabihu akawa ni Ismail. [21]

Is’haq

Baadhi ya wafasiri wa Ahlu-Sunna wanaitambua lakabu ya Dhabihullah kuwa ni ya Is’haq. Kauli hii imenasibishwa na watu kama Omar ibn al-Khattab, Saeed bin Zubayr, Ka’ab al-aKhbar, Qatadah, Zuhari, Tabari na Malik ibn Anas. [22] Ayatullah Makarim Shirazi anasema, hadithi ambazo zinamtambulisha Is’haq kuwa ni Dhabihullah zimeathirika na Israiliyat na anasema, kuna uwezekano hadithi hizi zimetungwa na Mayahudi. [23]

Kadhalika katika torati, Is’haq ametambulishwa kuwa ni Dhabihullah. [24] Hata hivyo wakati mwingine dhabihu ametabulishwa kuwa mtoto pekee wa Ibrahim (as). [25]

Ibn Dhabihein

Katika baadhi ya hadithi ni kuwa, kutokana na Abdul-Muttalib kuweka nadhiri ya kumchinja mtoto wake mmoja na kumtoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, Abdallah bin Abdul-Muttalib anafahamika kama dhabihu na Mtume (s.a.w.w) anajulikana kama Ibn Dhabihein (Mtoto wa madhabihu wawili). [26]

Vyanzo

  • Dihkhudā, ʿAlī Akbar. Farhang-i lughat. Tehran: Muʾassisa-yi Lughatnāma-yi Dihkhudā, 1341 Sh.
  • Fakhr al-Dīn al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Ibn ʿĀshūr, Muḥammad b. Ṭāhir. Al-Taḥrīr wa l-tanwīr. Beirut: Muʾassisat al-Tārīkh, 1420 AH.
  • Kafʿamī, Ibrāhīm b. ʿAlī al-. al-Miṣbāḥ. Qom: Dār al-Raḍī, 1405 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1374 Sh.
  • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Mūsawī Jazāʾirī. Third edition. Qom: Dār al-Kitab, 1404 AH.
  • Qurṭubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusru, 1364 Sh.
  • Ṣādiqī Tihrānī, Muḥammad. Al-Balāgh fī tafsīr al-Qurʾān bi-l-Qurʾān. Qom: Muʾallif, 1419 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Mahdī Lājiwardī. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Sayyid Quṭb, Muḥammad. Fī ẓilāl al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Shurūq, 1408 AH.
  • Ṭabāṭabāyī, Mūhammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Fifth edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1417 AH.

{{End]]