Mufassalat

Kutoka wikishia

Mufassalat (Kiarabu: المفصلات) (Sura pambanifu): Ni Sura fupi zilizoko mwishoni mwa Qur'ani (kwenye juzuu ya ‘Amma), ambazo humazilia kwa Suratu al-Nas. Hata hivyo, kuna maoni tofauti kuhusiana na mwanzo wa Sura hizo. Mufassalat zimegawanywa makundi matatu kulingana na idadi ya Aya ya Sura hizo: Tiwal (zilizo refu), Ausat (za wastani) na Qisar (fupi). Moja ya sifa ya Sura hizi za Mufassalat, ni kwamba mna Aya chache za Mansukh (zilizoondolewa hukumu zake) zinazopatikana ndani yake. Kwa hivyo, wakati mwengine Sura hizi hujulikana kwa jina la Muhkamat (zilizo wazi). Sura hizi pia zinajulikana kama Riyadhu al-Quran (bustani za Qu’ani).

Asili ya Kuitwa Mufassalat

Katika istilahi za wanazuoni, Mufassalat ni jina linalorejelea Sura fupi zilizopo mwishoni mwa Quran, ambazo zinatenganishwa kila moja baina yake kupitia ibara ya Bismillahi al-Rahmani al-Rahim. [1] Pia wakati mwengine Sura hizi huitwa Muhkamat (zilizo wazi). Sababu hasa ya kupewa jina la Muhakamat, inatokana na uchache wa Aya za Mansukh (zilizoondolewa) zinazo patikana ndani yake. Katika moja ya Hadithi, pale Ibn Abbas alipoulizwa kuhusiana na Muhkamat, alijibu kwa kusema kwamba; Muhkamat ni Mufassalat. [2] Pia katika baadhi ya Hadithi, Sura hizi za Mufassalat zimetajwa kwa jina la Riyadh al-Quran. [3]

Na ni vyema kuelewa kwamba; Sura nyingi za Mufassalat ni za Makkiyya (zilizoshuka Makka). [4]

Nafasi ya Mufassalat Kati ya Sura za Quran

Istilahi ya Mufassalat pia inapatikana katika baadhi ya hadithi zinazo husishwa na bwana Mtume (s.a.w.w); katika Hadithi hizi, Bwana Mtume (s.a.w.w) amesemwa “Mimi sikupewa Taurati na badala yake nimepewa Mi-iin «مئین» (yaani Sura refu zenye idadi ya Aya 100), na badala ya Injili, nikapewa Sura za Mathani, kisha badala ya Zaburi, nikapewa Sura za Mufassalat ambazo idadi yake ni Sura 68”. [5] Kulingana na Hadithi nyingine, ni kwamba; Mwenyezi Mungu amempa Mtume wake (s.a.w.w) ubora wa kuwapindukia manabii wengine kupitia Sura hizi za Mufassalat. [6]

Aina za Mufassalat

Sura za Mufassalat kulingana na idadi ya Aya zake zimegawika makundi matatu yafuatayo:

Mufassalat Tiwal Hujurat, Qaf, Dhariyat, Tur, Najm, Qamar, Rahman, Waqia, Hadid, Mujadala, Hashr, Mumtahina, Saff, Jumu'a, Munafiqun, Taghabun, Talaq, Tahrim, Mulk, Qalam, Haqqah, Ma'arij, Nuh, Jinn, Muzzammil, Mudathir, Qiyamah, Insan, Mursalat, Naba, Nazi'at, Abasa, Takwir, Infitar, Mutaffifin, Inshiqaq, na Buruj.
Mufassalat Ausat Tariq, A'la, Ghashiyah, Fajr, Balad, Shams, Layl, Duha, Sharh, Tin, Alaq, Qadr, na Bayyinah.
Mufassalat Qisar Zalzalah, Adiyat, Qari'ah, Takathur, Asr, Humazah, Fil, Quraish, Ma'un, Kawthar, Kafirun, Nasr, Masad, Ikhlas, Falaq, na Nas. [7]

Tofauti za Maoni Kuhusiana na Sura ya Kwanza ya Mufassalat

Sura ya mwisho katika kundi la Mufassalat bila kuwepo tofauti baina ya Wialamu, ni Suratu al-Nas, ila kuna maoni kumi na mbili kuhusiana na Sura ya kwanza ya kundi la Mufassalat. Kila mmoja kati ya wanazuoni wametaja Sura tofauti kama ndiyo Sura ya mwanzo ya kundi la Mufassala, Sura hizo ni kama ifuatavyo; As-Saffat, Al-Jathiya, Muhammad, Al-Fath, Al-Hujurat, Qaf, Ar-Rahman, As-Saff, Al-Furqan, Al-Insan, Al-A'la na Ad-Duha. [8]

Rejea

Vyanzo