Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:TawakkalMS8/2

Kutoka wikishia

Imamu Sadiq

Imamu Hadi (a.s)

Ghadir

Matini ya Barua kwa Kiarabu na Tafsiri ya Kiswahili

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

من کتاب له(ع) لشريح بن الحارث قاضيه

رُوِيَ أَنَّ شُرَيْحَ بْنَ الْحَارِثِ قَاضِيَ أَمِيرِالْمُؤْمِنِينَ (علیه السلام) اشْتَرَى عَلَى عَهْدِهِ دَاراً بِثَمَانِينَ دِينَاراً فَبَلَغَهُ ذَلِكَ

فَاسْتَدْعَى شُرَيْحاً، وَ قَالَ لَهُ: بَلَغَنِي أَنَّكَ ابْتَعْتَ دَاراً بِثَمَانِينَ دِينَاراً وَ كَتَبْتَ لَهَا كِتَاباً وَ أَشْهَدْتَ فِيهِ شُهُوداً فَقَالَ لَهُ شُرَيْحٌ قَدْ كَانَ ذَلِكَ يَا أَمِيرَالْمُؤْمِنِينَ(ع)

قَالَ فَنَظَرَ إِلَيْهِ نَظَرَ الْمُغْضَبِ ثُمَّ قَالَ لَهُ: يَا شُرَيْحُ أَمَا إِنَّهُ سَيَأْتِيكَ مَنْ لَا يَنْظُرُ فِي كِتَابِكَ وَ لَا يَسْأَلُكَ عَنْ بَيِّنَتِكَ، حَتَّى يُخْرِجَكَ مِنْهَا شَاخِصاً وَ يُسْلِمَكَ إِلَى قَبْرِكَ خَالِصاً.

فَانْظُرْ يَا شُرَيْحُ لَا تَكُونُ ابْتَعْتَ هَذِهِ الدَّارَ مِنْ غَيْرِ مَالِكَ أَوْ نَقَدْتَ الثَّمَنَ مِنْ غَيْرِ حَلَالِكَ؛ فَإِذَا أَنْتَ قَدْ خَسِرْتَ دَارَ الدُّنْيَا وَ دَارَ الْآخِرَةِ

أَمَا إِنَّكَ لَوْ كُنْتَ أَتَيْتَنِي عِنْدَ شِرَائِكَ مَا اشْتَرَيْتَ لَكَتَبْتُ لَكَ كِتَاباً عَلَى هَذِهِ النُّسْخَةِ، فَلَمْ تَرْغَبْ فِي شِرَاءِ هَذِهِ الدَّارِ [بِالدِّرْهَمِ] بِدِرْهَمٍ فَمَا فَوْقُ.

وَ النُّسْخَةُ هَذِهِ هَذَا مَا اشْتَرَى عَبْدٌ ذَلِيلٌ مِنْ مَيِّتٍ قَدْ أُزْعِجَ لِلرَّحِيلِ اشْتَرَى مِنْهُ دَاراً مِنْ دَارِ الْغُرُورِ مِنْ جَانِبِ الْفَانِينَ وَ خِطَّةِ الْهَالِكِينَ

وَ تَجْمَعُ هَذِهِ الدَّارَ حُدُودٌ أَرْبَعَةٌ الْحَدُّ الْأَوَّلُ يَنْتَهِي إِلَى دَوَاعِي الْآفَاتِ وَ الْحَدُّ الثَّانِي يَنْتَهِي إِلَى دَوَاعِي الْمُصِيبَاتِ وَ الْحَدُّ الثَّالِثُ يَنْتَهِي إِلَى الْهَوَى الْمُرْدِي وَ الْحَدُّ الرَّابِعُ يَنْتَهِي إِلَى الشَّيْطَانِ الْمُغْوِي وَ فِيهِ يُشْرَعُ بَابُ هَذِهِ الدَّارِ

اشْتَرَى هَذَا الْمُغْتَرُّ بِالْأَمَلِ مِنْ هَذَا الْمُزْعَجِ بِالْأَجَلِ هَذِهِ الدَّارَ بِالْخُرُوجِ مِنْ عِزِّ الْقَنَاعَةِ وَ الدُّخُولِ فِي ذُلِّ الطَّلَبِ وَ الضَّرَاعَةِ فَمَا أَدْرَكَ هَذَا الْمُشْتَرِي فِيمَا اشْتَرَى مِنْهُ مِنْ دَرَكٍ فَعَلَى مُبَلْبِلِ أَجْسَامِ الْمُلُوكِ وَ سَالِبِ نُفُوسِ الْجَبَابِرَةِ وَ مُزِيلِ مُلْكِ الْفَرَاعِنَةِ مِثْلِ كِسْرَى وَ قَيْصَرَ وَ تُبَّعٍ وَ حِمْيَرَ

وَ مَنْ جَمَعَ الْمَالَ عَلَى الْمَالِ فَأَكْثَرَ وَ مَنْ بَنَى وَ شَيَّدَ وَ زَخْرَفَ وَ نَجَّدَ وَ ادَّخَرَ وَ اعْتَقَدَ وَ نَظَرَ بِزَعْمِهِ لِلْوَلَدِ إِشْخَاصُهُمْ جَمِيعاً إِلَى مَوْقِفِ الْعَرْضِ وَ الْحِسَابِ وَ مَوْضِعِ الثَّوَابِ وَ الْعِقَاب

إِذَا وَقَعَ الْأَمْرُ بِفَصْلِ الْقَضَاءِ «وَ خَسِرَ هُنالِكَ الْمُبْطِلُونَ»

شَهِدَ عَلَى ذَلِكَ الْعَقْلُ إِذَا خَرَجَ مِنْ أَسْرِ الْهَوَى وَ سَلِمَ مِنْ عَلَائِقِ الدُّنْيَا

من کتاب له(ع) لشريح بن الحارث قاضيه
Miongoni mwa barua zake (a.s) kwenda kwa Shuraih bin al-Harith, hakimu wa mji wa Kufa.
رُوِيَ أَنَّ شُرَيْحَ بْنَ الْحَارِثِ قَاضِيَ أَمِيرِالْمُؤْمِنِينَ (علیه السلام) اشْتَرَى عَلَى عَهْدِهِ دَاراً بِثَمَانِينَ دِينَاراً فَبَلَغَهُ ذَلِكَ
Imesimuliwa kwamba Shuraih bin al-Harith, hakimu mteule wa zama za Amir al-Mu'minin (a.s), alinunua nyumba katika zama za utawala wa Amir al-Mu'minin, nyumba ambayo ilimgharimu kiasi cha dinari themanini. Habari hiyo ikamfikia Imamu Ali (a.s), hivyo akamwita Shuraih na kuhudhurisha mbele yake.
فَاسْتَدْعَى شُرَيْحاً، وَ قَالَ لَهُ: بَلَغَنِي أَنَّكَ ابْتَعْتَ دَاراً بِثَمَانِينَ دِينَاراً وَ كَتَبْتَ لَهَا كِتَاباً وَ أَشْهَدْتَ فِيهِ شُهُوداً فَقَالَ لَهُ شُرَيْحٌ قَدْ كَانَ ذَلِكَ يَا أَمِيرَالْمُؤْمِنِينَ(ع)
Alipofika mbele yake alimwambia: "Nimepata habari ya kwamba; umenunua nyumba kwa dinari themanini, na ukaandika waraka wa kujimilikisha na kushuhudisha mashahidi katika umiliki huo?" Shuraih akamwambia: "Ni kweli nemefanya hivyo, Ee Amir al-Mu'minina.
قَالَ فَنَظَرَ إِلَيْهِ نَظَرَ الْمُغْضَبِ ثُمَّ قَالَ لَهُ: يَا شُرَيْحُ أَمَا إِنَّهُ سَيَأْتِيكَ مَنْ لَا يَنْظُرُ فِي كِتَابِكَ وَ لَا يَسْأَلُكَ عَنْ بَيِّنَتِكَ، حَتَّى يُخْرِجَكَ مِنْهَا شَاخِصاً وَ يُسْلِمَكَ إِلَى قَبْرِكَ خَالِصاً.
Msimulizi anasema; Hapo Imamu Ali (a.s) kamtazama kwa mtazamo wa hasira, kisha akamwambia: "Ewe Shuraih! Hakika muda si mrefu atakujia yule (Malaika wa mauti) ambaye hatakuwa na haja ya kutazama waraka wako, wala hakuuliza juu ya ushahidi wako, na hakuacha mpaka akutoe kutoka nyumbani humo ukiwa uchi na akukabidhishe kaburi kwako ukiwa mikono mitupu.
فَانْظُرْ يَا شُرَيْحُ لَا تَكُونُ ابْتَعْتَ هَذِهِ الدَّارَ مِنْ غَيْرِ مَالِكَ أَوْ نَقَدْتَ الثَّمَنَ مِنْ غَيْرِ حَلَالِكَ؛ فَإِذَا أَنْتَ قَدْ خَسِرْتَ دَارَ الدُّنْيَا وَ دَارَ الْآخِرَةِ
Basi kuwa makini, ewe Shuraih! Usiwe umenunua nyumba hii kutoka kwa asiyekuwa mmiliki wake, au umelipa thamani yake kutoka kwa kisichokuwa halali yako; Kwani katika hali hiyo, utakuwa umekula khasara duniani na Akhera.
أَمَا إِنَّكَ لَوْ كُنْتَ أَتَيْتَنِي عِنْدَ شِرَائِكَ مَا اشْتَرَيْتَ لَكَتَبْتُ لَكَ كِتَاباً عَلَى هَذِهِ النُّسْخَةِ، فَلَمْ تَرْغَبْ فِي شِرَاءِ هَذِهِ الدَّارِ [بِالدِّرْهَمِ] بِدِرْهَمٍ فَمَا فَوْقُ.
Bila shaka, lau ungenijia wakati wa manunuzi yako ya hicho ulichokinunua, basi ningekuandikia hati yenye nasaha kama hizi, hivyo usingetamani kununua nyumba hii kwa dirhamu moja, seuze zaidi ya dirhamu moja.
وَ النُّسْخَةُ هَذِهِ هَذَا مَا اشْتَرَى عَبْدٌ ذَلِيلٌ مِنْ مَيِّتٍ قَدْ أُزْعِجَ لِلرَّحِيلِ اشْتَرَى مِنْهُ دَاراً مِنْ دَارِ الْغُرُورِ مِنْ جَانِبِ الْفَانِينَ وَ خِطَّةِ الْهَالِكِينَ
Na hati hii ni kwamba; Hichi ndicho alichonunua mja dhalili kutoka kwa maiti ambaye tayari ameshaharakishwa kwa ajili safari (mauti), amenunua kutoka kwake nyumba miongoni mwa nyumba danganyifu, kutoka kwa wale wanaotoweka na wanaofariki.
وَ تَجْمَعُ هَذِهِ الدَّارَ حُدُودٌ أَرْبَعَةٌ الْحَدُّ الْأَوَّلُ يَنْتَهِي إِلَى دَوَاعِي الْآفَاتِ وَ الْحَدُّ الثَّانِي يَنْتَهِي إِلَى دَوَاعِي الْمُصِيبَاتِ وَ الْحَدُّ الثَّالِثُ يَنْتَهِي إِلَى الْهَوَى الْمُرْدِي وَ الْحَدُّ الرَّابِعُ يَنْتَهِي إِلَى الشَّيْطَانِ الْمُغْوِي وَ فِيهِ يُشْرَعُ بَابُ هَذِهِ الدَّارِ
Na nyumba hii imekushana ndani yake mipaka minne: Mpaka wa kwanza unaishia kwenye vichocheo vya majanga, na mpaka wa pili unaishia kwenye vichocheo vya misiba, na mpaka wa tatu unaishia kwenye tamaa iangamizayo, na mpaka wa nne unaishia kwenye mamlaka ya Shetani adanganyaye, na huo ndiwo mlango mlango wa kuingilia nyumba hii.
اشْتَرَى هَذَا الْمُغْتَرُّ بِالْأَمَلِ مِنْ هَذَا الْمُزْعَجِ بِالْأَجَلِ هَذِهِ الدَّارَ بِالْخُرُوجِ مِنْ عِزِّ الْقَنَاعَةِ وَ الدُّخُولِ فِي ذُلِّ الطَّلَبِ وَ الضَّرَاعَةِ فَمَا أَدْرَكَ هَذَا الْمُشْتَرِي فِيمَا اشْتَرَى مِنْهُ مِنْ دَرَكٍ فَعَلَى مُبَلْبِلِ أَجْسَامِ الْمُلُوكِ وَ سَالِبِ نُفُوسِ الْجَبَابِرَةِ وَ مُزِيلِ مُلْكِ الْفَرَاعِنَةِ مِثْلِ كِسْرَى وَ قَيْصَرَ وَ تُبَّعٍ وَ حِمْيَرَ
Mdanganwa huyu aliyedanganywa na matumaini, amenunua nyumba hii kutoka kwa yule aliyeharakiswha kuielekea ajali (kifo), ameinunua kwa thamani ya kutoka katika heshima ya kutosheka (kuridhika) na kuingia katika udhalili (unyonge) wa kuomba na kunyenyekea. Basi chochote kile kitakachomsibu mnunuzi huyu kutokana na kile alichonunua kutoka kwa muuzaji huyo, basi ni kazi ya yule anayetikisa miili ya wafalme, na kunyakua roho za majabari, na kuondoa ufalme wa mafarao, kama vile Kisra, Kaisari, Tubba', na Himyar.
وَ مَنْ جَمَعَ الْمَالَ عَلَى الْمَالِ فَأَكْثَرَ وَ مَنْ بَنَى وَ شَيَّدَ وَ زَخْرَفَ وَ نَجَّدَ وَ ادَّخَرَ وَ اعْتَقَدَ وَ نَظَرَ بِزَعْمِهِ لِلْوَلَدِ إِشْخَاصُهُمْ جَمِيعاً إِلَى مَوْقِفِ الْعَرْضِ وَ الْحِسَابِ وَ مَوْضِعِ الثَّوَابِ وَ الْعِقَاب
Na yeyote yule aliyekusanya mali juu ya mali kupita kiasi, na yeyote yule aliyejenga na akainua na kuimarisha kisha akapamba kwa mapambo ya nje na ya ndani, na akahifadhi (akarimbika) na kuamini (akajenga matumaini) na akajenga mtazamo wa kuwekeza, kwa madai yake, kwa ajili ya mtoto (au watoto wake), Malaika wa mauti amewaondoa wote na kuwaongoza kwenye uwanja wa kuonyeshwa na kuhisabiwa, na (kuwahudhurisha) mahali pa thawabu na adhabu.
إِذَا وَقَعَ الْأَمْرُ بِفَصْلِ الْقَضَاءِ «وَ خَسِرَ هُنالِكَ الْمُبْطِلُونَ»
Pale itakapotoka amri ya kuhitimishwa kwa hukumu, "Na huo nido wakati watakapokula kahasara wale wanaotenda batili.
شَهِدَ عَلَى ذَلِكَ الْعَقْلُ إِذَا خَرَجَ مِنْ أَسْرِ الْهَوَى وَ سَلِمَ مِنْ عَلَائِقِ الدُّنْيَا
Akili inathibitisha hayo, pale akili hiyo itakapokuwa imejiondoa katika kifungo cha tamaa na kuwa huru kutokana na pingamizi za kidunia.

🌞
🔄