Nenda kwa yaliyomo

Mjadala wa Imam Ridha na Mwanazuoni wa Kimajusi (Zoroastrianism)

Kutoka wikishia

Mjadala wa Imam Ridha na Mwanazuoni wa Kimajusi (Zoroastrianism) (Kiarabu: مناظرة الإمام الرضا عليه السلام مع الزرادشتيين) ni mazungumzo ya kielimu kati ya Imamu Ridha (a.s) na Manazuoni wa Kimajusi, juu ya uthibitisho wa unabii wa mitume wa Kiyahudi, Ukristo na Uislamu. Mjadala huu uliojiri baina Imamu Ridha (a.s) na mwanazuoni huyo aliyejulikana kwa jina la Hirbidh, unajulikana kama ni moja ya mazungumzo muhimu ya kidini na kielimu katika Madhehebu ya Shia. Katika mjadala huu, Imamu Ridha (a.s) alitumia hoja zile zile za Hirbidh alizotumia kuthibitisha utume wa mtume wake (Zarathustra), katika kuthibitisha unabii wa Mitume wa dini ya Uyahudi, Ukristo, na Uislamu, ambao ni; Nabii Musa (a.s), Nabii Isa (a.s) na Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mazungumzo haya yalifanyika katika kikao maalum kilichoandaliwa na Khalifa Maamun wa ukoo wa Bani Abbas. Katika kikao hicho, Imamu Ridha (a.s) alijadiliana kwa kina na wataalamu wa dini mbalimbali, wakiwemo; Mayahudi, Wkristo, Wamajusi, na Sabiina (Sabians). Hadithi ya mjadala huu iliandikwa kwa mara ya kwanza na Sheikh Sadouq katika vitabu vyake vya Tawhidi na Uyoun Akhbar al-Ridha, na imekuwa kumbukumbu muhimu katika historia ya mijadala ya kidini. Kisa cha majadilioano hayo kiliripotiwa kwa mara ya kwanza kabisa na Sheikh Saduq katika vitabu vyake viitwavyo Tawhidi na Uyunu Akhbar Al-Ridha.

Kulingana na simulizi za Sheikh Sadouq, Hirbid hakuweza kujibu changamoto na maswali ya Imamu Ridha (a.s) na alilazimika kumaliza mjadala huo mapema.

Muktadha wa Kuundwa kwa Mdahalo na Mada Yake

Mdahalo wa Imamu Ridha (a.s) na Hirbidh Akbar, mwanazuoni wa Kizoroastria, ni mazungumzo mafupi yanayo husiana na ithibati za utume wa Zarathustra, Nabii Musa, Nabii Isa, na Nabii Muhammad (s.a.w). Mdahalo huu uliandaliwa kwa ombi la Khalifa wa Bani Abbas, Maamun. Tokeo hili lilitokea pale Imamu Ridha (a.s) alipokuwa akisafiri kutoka Madina kwenda Marw. Pale imamu akiwa katika matayarisho ya safari hiyo, Maumun aliwaalika wanazuoni wa Kikristo, Kiyahudi, Kizoroastria, na Kisabia kujadiliana naye, majadiliano ambayo yalifanyika ndani ya mji huo wa Marw. [1]

Katika kikao hichi, Jathaliq (kiongozi wa Wakristo), Ras al-Jalut (kiongozi wa Wayahudi), viongozi wa Wasabi’i, na Imran Sabi’i walihudhuria na kushiriki katika mdahalo huo. [2] Hassan bin Muhammad Naufali, mtoa simulizi wa mdahalo huu, anaeleza kwamba; lengo la Ma’amun kuandaa mjadala huo lilikuwa ni kumjaribu Imamu Ridha. [3]

Matini ya Mdahalo

  • Imamu Ridha (a.s): Je, ni ipi hoja yako kuhusu utume wa Zoroaster, ambaye unamchukulia kuwa ni nabii wa haki?
  • Hirbidh: Alituletea mambo ambayo hayajaletwa na yeyote kabla yake. Sisi hatujawahi kumuona kwa nmacho yetu wenyewe, ila tumepokea habari kutoka kwa waliotutangulia kwamba alihalalisha mambo ambayo hakuna mwingine aliye halalisha na kuharamisha mambo ambayo hakuna mwingine aliye haramisha. Kwa hivyo, tumemfuata.
  • Imamu Ridha (a.s): Kwa hivyo, mnamfuata kwa sababu ya habari zilizopokewa kuhusu yeye?
  • Hirbidh: Ndiyo.
  • Imamu Ridha (a.s): Pia kwa nyumma nyengine. Waio tantulia ndio walio waletea habari za manabii wao, wakiwemo Musa, Isa, na Muhammad (s.a.w). Ikiwa hoja yenu ya kukubali utume wa Zoroaster ni mtirirko wa habari zilizopokewa kwa njia ya mutawatir (kupitia wapokeza wa matabaka tofauti), kwa nini basi hamkubali utume wa manabii hao wengine?

Hirbidh hakuja na jibu ya swali hili, na badala yake akaamua kumaliza mazungumzo. [4] [Maelezo 1]

Vyanzo vya Hadithi

Kwa mara ya kwanza kabisa, matini ya mdahalo huu yamepatikana katika vitabu vya Tawhidi [5] na Uyunu Akhbar Al-Ridha, [6] vilivyoandikwa na Sheikh Saduq (aliye ishi kati ya 305 na 381 Hijria). Kiasha baadae, Ahmad bin Ali Tabarsi (aliyeishi katika karne ya sita Hijria) akaja kunukuu ripoti hiyo katika kitabu chake Ihtijaj. [7] Pia, Hadithi hii inapatokana katika Bihar al-Anwar, ila ni kunukuu iliyo nukuliwa kutoka kwenye vitabu viwili hivyo vya Sheikh Saduq. [8]

Uhalali wa Sanad (Hati) ya Hadithi

Wataalamu wa fani ya rijali (nasaba za wapekezi wa Hadithi), wana mitazamo tofauti kuhusiana na mlolongo wa wapokezi wa Hadithi hii. Baadhi yao wanawahesabu wapokezi wote wa mlolongo huo kuwa ni waaminifu, huku wengine wakiwahesabu baadhi yao kuwa si waaminifu. [9] Zaidi ya hayo, sanad ya Hadithi hii ni mursal, yaani baadhi ya watu katika mnyororo wa wapokezi wake hawajatajwa kwa majina kamili. Kwa hivyo, hadithi hii inachukuliwa kuwa dhaifu kwa upande wa kisanad. [10] Hata hivyo, baadhi ya watu wanaamini kwamba Hadithi hii ni dhaifu lakini inakubalika na kuingia maanani, yaani licha ya kuwa na udhaifu katika sanad, ila ina hadhi ya kufuatwa, kwa sababu msomi mashuhuri kama vile Sheikh Saduq ndiye aliye inukuu, naye alikuwa akinukuu tu Hadithi alizokuwa na uhakika nazo kwamba zimetoka kwa Maasumina. [11]

Mada Zinazo Husiana

Maelezo

  1. ثُمَّ دَعَا (ع) بِالْهِرْبِذِ الْأَکبَرِ فَقَالَ لَهُ الرِّضَا (ع) أَخْبِرْنِی عَنْ زَرْدَهُشْتَ الَّذِی تَزْعُمُ أَنَّهُ نَبِی مَا حُجَّتُک عَلَی نُبُوَّتِهِ قَالَ إِنَّهُ أَتَی بِمَا لَمْ یأْتِنَا أَحَدٌ قَبْلَهُ وَ لَمْ نَشْهَدْهُ وَ لَکنَّ الْأَخْبَارَ مِنْ أَسْلَافِنَا وَرَدَتْ عَلَینَا بِأَنَّهُ أَحَلَّ لَنَا مَا لَمْ یحِلَّهُ غَیرُهُ فَاتَّبَعْنَاهُ قَالَ أَفَلَیسَ إِنَّمَا أَتَتْکمُ الْأَخْبَارُ فَاتَّبَعْتُمُوهُ قَالَ بَلَی قَالَ فَکذَلِک سَائِرُ الْأُمَمِ السَّالِفَةِ أَتَتْهُمُ الْأَخْبَارُ بِمَا أَتَی بِهِ النَّبِیونَ وَ أَتَی بِهِ مُوسَی وَ عِیسَی وَ مُحَمَّدٌ فَمَا عُذْرُکمْ فِی تَرْک الْإِقْرَارِ لَهُمْ إِذْ کنْتُمْ إِنَّمَا أَقْرَرْتُمْ بِزَرْدَهُشْتَ مِنْ قِبَلِ الْأَخْبَارِ الْمُتَوَاتِرَةِ بِأَنَّهُ جَاءَ بِمَا لَمْ یجِئْ بِهِ غَیرُهُ فَانْقَطَعَ الْهِرْبِذُ مَکانَه (شیخ صدوق، توحید، ۱۳۹۸ق، ص۴۱۹؛ شیخ صدوق، عیون اخبار الرضا، ۱۳۷۸ق، ج۱، ص۱۶۷-۱۶۸).

Rejea

Vyanzo