Nenda kwa yaliyomo

Mjadala wa Imam Ridha(a.s) kuhusu Tawhiid

Kutoka wikishia

Mjadala wa Imam Ridha (a.s) kuhusu Tawhiyd (Kiarabu: مناظرة الإمام الرضا عليه السلام عن التوحيد) ni hadithi ambayo Imamu Ridha (a.s) anazungumzia kuwepo kwa Mwenyezi Mungu pamoja na mtu anayekana kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Katika hadithi hii, Imamu Ridha (a.s) aliwasilisha hoja (dalili) tatu za kuwepo kwa Mungu na akajibu hoja za wale wanaokanusha kuwepo kwa Mwenyeezi Mungu.

Taarifa Fupi ya Mjadala huo

Katika mjadala huu wa Imamu Ridha (a.s) anajadiliana na mtu ambaye anakanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu [1] na yeye Imam Ridha (a.s) anathibitisha kuwepo kwa Mola mmoja ambaye ndiye anayepaswa kuabudiwa. Mwanzoni mwa mazungumzo, Imam Ridha anaibua na kutowa hoja kuhusu mantiki ya kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Mtu anayekataa na kupinga uwepo wa Mungu hajibu swali hili na huibua matatizo na hoja mbalimbali akijaribu kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu. Pamoja na Imam Ridha kujibu hoja zake, Imam Ridha pia anawasilisha hoja nyingine mbili za kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. [2] hatimae, mtu huyu anaamini kuwepo kwa Mungu mwishoni. [3]

nHoja za Imam Ridha Juu ya Kuwepo kwa Mwenyezi Mungu

Katika mjadala huu, Imam Ridha (a.s) aliwasilisha hoja tatu kuhusiana na kuwepo kwa Mwenyezi Mungu: moja mwanzoni mwa mjadala na nyingine mbili, miongoni mwa maswali na majibu yanayoibuliwa kati yake na mtu aliyekanusha kuwepo kwa Mungu. Hoja hizi tatu ni kama zifuatazo:

  • Ikiwa hakuna Mwenyeezi Mungu, baada ya kifo, (siku ya Kiama) hadhi ya makafiri na waumini itakuwa sawa; Lakini ikiwa kuna Mungu, makafiri watakwenda motoni na waumini watakwenda Peponi.[4]
  • Kwa kuzingatia mwili wetu wenyewe, tunaona kwamba hatuwezi kuongeza au kupunguza kiungo chochote kutoka kwake. Na kila kiungo kinafanya kazi yake kulingana na Mwenyeezi Mungu alivyotuumba, hivyo ni nani mwenye uwezo au nguvu wa kumuumba binaadamu?
  • Tukiangalia vitu vyote alivyoumba Mwenyeezi Mungu, na kila kimoja akakiweka katika sehemu yake na kukiamrisha kufanya kazi yake hizo zote ni ishara tosha zinazothibitisha kuwepo kwa Mwenyeezii Mungu. Kwa mfano natutupilie macho mzunguko wa mbingu, kuonekana kwa mawingu na upepo, mwendo wa jua, mwezi, na nyota, na ishara nyinginezo za ajabu na zenye nguvu, huonyesha kwamba kuna mtu aliyeumba vitu hivi.[6]

Matatizo ya Mkanushaji Aliyepinga Kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na Majibu ya Imamu Ridha (a.s)

Katika mjadala wa Imamu Ridha (a.s) kuhusu Tawhiyd, mtu ambaye anakanusha kuwepo kwa Mungu, baada ya kila hoja ya Imam Ridha (a.s) juu ya kuwepo kwa Mungu, anaibua hoja ambayo Imam Ridha (a.s) anaijibu kwa njia hiyo hiyo. Miongoni mwa mambo mengine, anauliza: Ikiwa Mungu yuko, yukoje? mungu yuko wapi tangu lini? Ikiwa yupo, kwa nini haonekani? Pia ni tatizo kwamba ikiwa Mungu anasikia na kuona, ni muhimu kwake kuwa na masikio na macho.[7]

.[۹] Imam Reza anajibu, kwamba Mwenyeezi Mungu ndiye muumba wa ubora (jinsi) na mahali. Kwa hiyo, si mahali popote na ubora hauingii katika kuwepo kwake. Wala haijawahi kuwa na wakati ambapo haukuwepo. Kwa hiyo, haiwezekani kusema ni lini Mungu aliumbwa. Sababu kwa nini Mungu hawezi kuonekana ni kwamba, kwanza, kuna tofauti kati ya muumba na aliyeumbwa, na pili, Mungu ni mkuu kuliko kuonekana kwa macho au kueleweka kwa akili na fikra.[8]

Kusikia na kuona kwa Mungu si sawa na kuona na kusikia kwa viumbe vinavyohitaji masikio na macho; Bali ndio maana wanamwita Mwenyezi Mungu kuwa ni Mwenye kusikia, ambaye anasikia kila sauti mbinguni na ardhini, ikiwa ni ndogo au kubwa. Ndio maana wanamwita mwonaji mwenye kuona kila kitu; Hata nyayo za mchwa mweusi kwenye jiwe jeusi usiku. [9]

Rejea

Vyanzo



.