Mazungumzo ya Imamu Reza (a.s) na Suleiman Marwazi

Kutoka wikishia

Mazungumzo ya Imamu Ridha (a.s) na Suleiman Marwazi (Kiarabu: مناظرته الإمام الرضاعليه السلام مع سليمان المروزي) yanaeleza majadiliano ya kina na ya kitaalamu yaliyojiri kati ya Imamu Ridha (a.s) na Suleiman Marwazi, mmoja wa wataalamu wa theolojia kutoka Khorasan. Mazungumzo haya yalihusu dhana ya Badaa (mabadiliko) na matakwa ya Mungu, yaliyo fanyika kwa misingi ya tafakuri na mantiki aminifu juu ya masuala hayo. Mazungumzo na majadiliano haya yaliandaliwa kwa amri ya Khalifa Al-Maamun wa ukoo wa Abbasiyya, ambaye alikusudia kutumia mjadala huu katika kumjaribu Imamu Ridha (a.s). Maelewano yao juu ya mjadala huu, ilikuwa ni kusimamisha hoja kwa kutumia vyanzo vya riwaya za Shi'a.

Mazungumzo kati ya Imamu Ridha (a.s) na Suleiman Marwazi, kama yalivyorekodiwa katika vitabu vya Tawhid na Uyoon Akhbar Al-Ridha vilivyoandikwa na Sheikh Saduq, pamoja na Al-Ihtijaj cha Ahmad Tabarsi, yana umuhimu mkubwa katika mijadala inayohusiana na nyanja za Tawhid. Kulingana na vyanzo hivi vya Hadithi, Imamu Ridha (a.s) aliibuka mshindi dhidi ya Suleiman katika mjadala huu muhimu. Katika mazungumzo hayo, Suleiman alikubaliana na dhana ya badaa, yaani mabadiliko katika maamuzi na matakwa ya Mungu, jambo lililochangia kushindwa kwake katika mjadala huo. Vilevile, Suleiman alijikuta hana majibu ya maswali na changamoto zilizotolewa na Imamu Ridha (a.s) juu ya suala la matakwa na maamuzi ya Mungu, jambo lililodhihirisha ujuzi na weledi wa Imamu Ridha (a.s) katika nyanja mbali mbali za masuala ya kiitikadi.

Mwanzo wa Mazungumzo

Katika muktadha wa majadiliano haya muhimu juu ya itikadi za kidini, Khalifa Maamun wa ukoo wa Abbasiyya, alipokea ziara ya Suleiman Marwazi, mwanazuoni mashuhuri wa fani ya theolojia kutoka Khurasan. Maamun alimjulisha Suleiman kuwa; amepata ugeni wa kutembelewa na Ali bin Musa al-Ridha (a.s) kutoka Hijaz, ambaye ni mwanazuoni na mpenzi wa elimu ya theolojia, na kwamba kwa wakati huyo alikuwa amewasili akiwa katika himaya yake. Maamun akifanya hivyo akitambua uwezo wa Suleiman katika mijadala ya kitheolojia. Kwa hiyo Maamun alimsihi aje siku ya Tarwiyah ili kushiriki katika mazungumzo na Imamu Ridha (a.s). Hata hivyo, Suleiman alieleza wasi wasi wake juu ya uwezo wa Imamu Ridha (a.s) katika kujibu maswali yake, akihofia kumdhalilisha mbele ya familia ya Bani Hashim. Maamun, akisisitiza dhamira yake, alijibu kwa kusema, "Nilikuagiza kufanya hivyo nikitambua nguvu zako katika mijadala ya kidini, na nia yangu pekee ni kumshinda Ali bin Musa al-Ridha walau katika hoja moja tu miongoni mwa hoja zake." Baada ya mazungumzo hayo na Marwazi, Maamun alimkaribisha Imamu Ridha (a.s) kushiriki katika majadiliano hayo, na kwa heshima na busara, Imamu alikubali mwaliko huo. [1]

Misingi ya Mazungumzo

Imamu Ridha (a.s) na Suleiman Marwazi walichagua dhana ya Badaa kuwa ndiyo jiwe la msingi la mjadala wao. Imamu Ridha (a.s) alianza kujenga hoja zake kwa kutoa rejelea Aya kadhaa kutoka Qur'ani, zikiwemo Aya zisemayo: «وَهُوَ الَّذِی یبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ یعِیدُهُ ; Naye ndiye mwanzishaji wa uumbaji, kisha anaurejesha (anaubadili)» (Surat Al-Rum, 30:11), [2] «بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ; Naye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi» (Surat Al-An'am, 6:101), [3] na «وَآخَرُ‌ونَ مُرْ‌جَوْنَ لِأَمْرِ‌ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ; Na wengine wameakhirishwa kwa amri ya Mwenye Ezi Mungu, ima Yeye atawaadhibu au atawasamehe» (Surat Al-Tawba, 9:106). [4] Kupitia Aya hizi, Imamu Ridha (a.s) alihoji namna Suleiman anavyoweza kupinga dhana ya Badaa huku Aya hizi zikiashiria uwepo wa mabadiliko katika maamuzi ya Mungu. Suleiman alihitaji ufafanuzi zaidi juu ya dhana hii, na kwa ufafanuzi wa kina kutoka kwa Imamu Ridha (a.s), aliweza kuelewa na hatimae kukubali hoja za Imamu juu ya dhana ya Bada'. Mazungumzo haya yalidhihirisha hadharani uwezo wa kielimu wa Imamu Ridha (a.s) na uhodari wake wa kutumia Qur'an kuthibitisha na kujenga hoja, sambamba na umuhimu wa kutumia maandiko matakatifu katika kutoa mwongozo wa kuewewa itikadi za Kiislamu. [5]

Baada ya Suleiman kukubali dhana ya Badaa, alianzisha mjadala mpya kuhusu Irada ya Mwenye Ezi Mungu, akijaribu kutaka kuelewa tofauti yake na sifa nyingine za Mungu kama vile kuwa Msikivu (Samii’u), Mwenye Kuona (Basiiru), na Mweza (Qadiiru). Suleiman alisisitiza kuwa Irada ni sehemu ya sifa asilia za Mungu, sawa na sifa nyingine zilizoelewa hapa. Hata hivyo, Imamu Ridha (a.s) alikataa mtazamo huu, akibainisha kwamba kuna tofauti kubwa kati ya irada na sifa nyingine za Mwenye Ezi Mungu. Alieleza kuwa sifa kama Samii'u, Basiiru, na Qadiiru ni sehemu ya asili za Dhati ya Mwenye Ezi Mungu, zilizokuwapo tangu na milele, na hazitegemei matendo fulani katika uwepo wake. Sifa hizi haziwezi kubadilika na zipo hata kabla ya kuumbwa kwa kitu chochote. Kwa upande mwingine, Irada ni sifa inayojidhihirisha pale Mungu anapotaka kuumba au kubadilisha kitu fulani. Hii ina maana kwamba Irada inahusiana moja kwa moja na vitendo vya Mwenye Ezi Mungu, tofauti na sifa nyingine ambazo haziathiriwi moja kwa moja na uwepo wa matendo Yake. Imamu Ridha (a.s) alisisitiza kwamba; hatuwezi kusema kuwa Mwenye Ezi Mungu aliumba au alifanya mabadiliko kwa sababu ni Msikivu (Samii’u), (Basiiru), au Mweza (Qadiiru), bali alifanya hivyo kwa sababu ya matakwa na mapenzi Yake. [6]

Mjadala huu uliendelea kwa maswali ya kina kutoka kwa Imamu Ridha (a.s), ambaye kwa ustadi aliweka changamoto mbele ya Suleiman kwa kumuuliza maswali ambayo yalizidi kumweka katika hali ngumu. Kadri mjadala ulivyoendelea, Suleiman alizidi kupoteza mwelekeo hadi kufikia hatua ambapo hakuweza kutoa majibu sahihi. Hatimaye, alipokutana na swali la mwisho kutoka kwa Imamu Ridha (a.s), Suleiman alinyamaza kimya, akishindwa kujibu, na hivyo kumaliza mjadala huo kwa kutoweza kujitetea. [7]

Matokeo ya Mjadala

Katika mjadala huu, kulingana na vyanzo vya Hadithi, Suleiman alikumbana na changamoto kubwa mbele ya hoja za Imamu Ridha (a.s). Kwa mfano, mwishoni mwa mjadala wa dhana ya Badaa (mabadiliko ya maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu), Suleiman alikubali mtazamo wa Imamu na alikiri kuwa hatapinga tena na nadharia hiyo. [8] Pia katika majadiliano kuhusiana na sifa za Mwenye Ezi Mungu, Suleiman alijibu kwa namna iliyomletea mashaka na dhihaka, huku akipata lawama kutoka kwa Maamun. [9] Suleiman alijaribu kujibu maswali ya Imamuu kwa njia yenye mikinzano isiyokuwa na uwazi ndani yake. Imamu Ridha (a.s) alimuuliza maswali yenye magumu, kulikomfanya Suleiman kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha, nabadala yake akawa anatoa jawabu tatanishi, hasa katika suala la mwisho lililoulizwa na Imamu Ridha (a.s). [10] Kwa hivyo, mjadala huo ulimalizika kwa Suleiman kushindwa kutoa majibu sahihi, huku Imamu Ridha (a.s) akithibitisha uwezo wake wa kipekee katika majadiliano na kuimarisha ukweli wa mafundisho ya Kiislamu kwa njia ya kitaalamu na yenye busara. [11]

Vyanzo

Vyanzo vya kihistoria vinavyohusiana na mjadala huu ni: Vitabu viwili vya Sheikh Saduq: Tawhid [12] (vilivyoandikwa kati ya mwaka wa 305 na 381 AH) na Uyoun Akhbar al-Ridha [13] (vilivyoandikwa kati ya mwaka wa 305 na 381 AH), Kitabu cha Ahmed ibn Ali Tabarsi: Al-Ihtijaj (aliyeishi katika karne ya sita AH) [14], Kitabu cha Bihar al-Anwar:[15] Taarifa za Hadithi zinatokana na vitabu vya Sheikh Saduq, Tawhid Saduq na Uyoun Akhbar al-Ridha. [16]

Matini na Tafsiri ya Mjadala

Suleiman al-Marwazi, mwanatheolojia kutoka Khorasan, alifika kwa Khalifa al-Maamun, ambapo alikubaliwa na kupokelewa kwa heshima. Khalifa al-Maamun alimuambia kwamba binamu yake, Ali bin Musa al-Ridha (a.s), amemtembelea kutoka Hijaz na kwamba yeye na wafuasi wake ni wapenzi wa masuala au fani ya theolojia. Khalifa alimuomba Suleiman aje siku ya Tarwiyah ili kujadili na Imamu al-Ridha (a.s) juu ya masuala ya imani na theolojia. Hata hivyo, Suleiman alijibu kwa kusema, "Ewe Amirul-Muuminina, mimi sipende ya kumjadili mtu kama yeye hadharani mbele ya jopo la familia ya Banu Hashim. Hali ambayo itasababisha kupoteza hadhi yake mbele ya watu, na si sawa kumweka mtu kama yeye katika hali ya kudhalilishwa.

Khalifa al-Maamun akamwambia: Nimekuchagua wewe na kukuleta hapa kwa sababu nina imani na uwezo wako katika uwanja wa majadiliano na mashindano. Lengo langu lilikuwa ni kuona jinsi utakavyoweza kumshinda Ali bin Musa angalau katika hoja moja miongoni mwa hoja zake. Suleiman alijibu: Basi, ni vyema andaa kikao na unikunishe mimi na Imamu al-Rida (a.s), nawe uwepo kikaoni humo kama shahidi.

Maamun akamtuma mtu aende kwa Imamu na kumwambia: Kuna mtu mmoja amekeja kututembela nyumbani kwetu kutoka mji wa Marw, ambaye ni mmoja wa bingwa katika wa Khurasan katika fani ya theolojia na hana mpizani katika uwanja huo. Ikiwa huna pingamizi, tafadhali njoo nyumbani. Imamu akainuka kwa ajili ya kutia wudhu na akatuambia: nyinyi tangulieni. Wakati huo Imran Saabi’I pia alikuwa pamoja nasi. Tukaongoza hadi mlangoni mwa chumba cha Maamun. Yasir na Khalid wakanishika mkono na kuniongoza hadi ndani. Baada kutoa salam, Maamun alisema akiniuliza: Ndugu yangu Abu al-Hassan yuko wapi? Mwenye Ezi Mungu amuhifadhi.

Nilkamjibu kwa kumwambia, Tulipokuja huku, tulimwacha yeye akijiandaa kuvaa nguo. Na akatutaka sisi tutangulie kabla yake, nikaongeza, Ewe Amirul-Muuminina, rafiki yako Imran mwenye mapenzi nawe pia yuko nje anasubiri idhini yako. Maamun akauliza, Imran yupi? Nikamwambia, Ni Imran Sabi'i ambaye wewe ulimsaidia kuingia katika Uislamu. Maamun akamwambia, Aingie ndani. Imran akaingia, na Maamun alimkaribisha kwa heshima na kumweka mahali panapo stahiki. Kisha Maamun akasema, Ewe Imran, hukufa na Mungu amekuwe mpaka ukawa mmoja wa Bani Hashim! Imran akajibu, Ninamshukuru Mwenye Ezi Mungu aliye nipa heshima kupitia kwako, ewe Amir. Maamun akasema, Ewe Imran, huyu unaye muona hapa ni Suleiman Marwazi, mwanatheolojia kutoka Khurasan. Imran akajibu, Ewe Amirul-Muuminina, mwanazuoni huyu ndiye mtaalamu wa pekee katika Khurasan kuhusiana na majadiliano ya kitheolojia, naye ni miongoni mwa wenye kanusha dhana ya Badaa'.

Maamun akasema: Kwa nini hujafanya mjadala naye? Imran akajibu: Hilo ilitegemea makubalioano yake yeye mwenyewe. Tukiwa katika mazungumzo hayo, mara Imamu Ridha (a.s.) aliingia na kuuliza: Mlikuwa mnazungumzia nini? Imran akasema: Ewe mwana wa Mtume, huyu unaye muona hapa ni Sulaiman Marwazi. Sulaiman akamwambia Imran: Je, hivi wewe unakubaliana na maoni ya Abu al-Hassan kuhusu Badaa? Imran akajibu: Ndiyo, lakini kwa sharti kwamba atoe madhubuti itakayo niwezesha kushinda katika majadiliano dhidi ya wenye mawazo kama yangu. Maamun akasema: Ewe Abu al-Hassan, una maoni gani kuhusu kile wanacho kizungumzsa na kukhitilafiana nacho? Imamu Ridha (a.s) akasema: "Ewe Sulaiman, ni kwa jinsi gani huwezi kukubaliana na dhana ya Badaa hali ya kwamba Mwenye Ezi Mungu katika Qur’an anasema: أَ وَ لا یذْکرُ الْإِنْسانُ أَنَّا خَلَقْناهُ مِنْ قَبْلُ وَ لَمْ یکُ شَیئاً Je, mwanadamu hakumbuki (hawi namazingatio) kwamba hakika sisi tulimuumba hapo mwanzo, hali ya kwamba yey hakuwa kitu chochote? (Qur'an, Suratu Maryam, Aya 67). Na pia anasema: وَ هُوَ الَّذِی یبْدَؤُا الْخَلْقَ ثُمَّ یعِیدُهُ ; Naye ndiye anayeanzisha uumbaji kisha anaruudisha (tena) (Qur'an, Surat Ar-Rum, Aya 27). Na pia anasema: بَدِیعُ السَّماواتِ وَ الْأَرْضِ ; Mwanzilishi wa mbingu na ardhi (Qur'an, Suratu Al-Baqarah, Aya 117). Na tena anasema: یزِیدُ فِی الْخَلْقِ ما یشاءُ ; Anazidisha katika uumbaji kwa anavyotaka (Qur'an, Surat Fatir, aya 1). Na anasema: بَدَأَ خَلْقَ الْإِنْسانِ مِنْ طِینٍ ; Alianza uumbaji wa mwanadamu kupia udongo (Qur'an, Surat As-Sajdah, aya 7). Na pia anasema: وَ آخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّهِ إِمَّا یعَذِّبُهُمْ وَ إِمَّا یتُوبُ عَلَیهِمْ ; Na wengine wanasubiri amri (matakwa) ya Mwenye Ezi Mungu; ima atawaadhi au atawasamehe (makossa yao) (Qur'an, Surat At-Tawbah, aya 106). Na pia anasema: وَ ما یعَمَّرُ مِنْ مُعَمَّرٍ وَ لا ینْقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِی کتابٍ ; Hakuna arefushiwaye wala apunguziwaye umri wake isipokuwa hilo limo (limeandikwa) katika Kitabu (Qur'an, Surat Fatir, aya 11). Baada ya hayo, Sulaiman akauliza: Je, kuna Riwaya yoyote uliyo ipokea kutoka kwa baba zako kuhusiana na hili?

mam al-Ridha (a.s.) akasema: Ndiyo, nimepokea Riwaya kutoka kwa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s) isemayo kwamba: Mwenye Ezi Mungu ana elimu mbili: moja iko katika hazina ya siri zake, na hakuna mwingine aijuaye isipokuwa Mwenye Ezi Mungu peke yake, na elimu ihisanayo na dhana ya 'badaa' ipo katika hazina yake hiyo ya siri zake; na elimu ya pili ni ile ambayo Mwenye Ezi Mungu amewafundisha na kuwafunulia Malaika, Mitume wake, pamoja na wanazuoni kutoka familia ya Mtume wetu."

Suleiman akajibu: Ningependa kuona ushahidi wa jambo hili kutoka katika Kitabu cha Mwenye Ezi Mungu. Imamu al-Ridha (a.s) akamjibu: Mwenye Ezi Mungu anasema kumwambia Mtume wake: فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَما أَنْتَ بِمَلُومٍ ; Kwa hiyo, epukana (achana) wao; wewe simwenye kulaumiwa (Qur'an, Surat Adh-Dhariyat, Aya 54). Hii inaonyesha kwamba hapo mwanzoMwenye Ezi Mungu alikusudia kuangamiza watu hao. Kisha alibadilisha maamuzi yake na kusema: ذَکِّرْ فَإِنَّ الذِّکرى‏ تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِینَ‏ ; Naonya (kumbusha); na bila shaka ukumbusho huwafaa waumini (Qur'an, Surat Adh-Dhariyat, aya 55).

Suleiman alisema: Tafadhali, endelea, maisha yangu yawe ni fidia kwako (niko chini ya miguu yako). Imamu akajibu: Baba yangu, kwa kupitia baba zao, wamesimulia Hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) kwamba: Mwenye Ezi Mungu Mtukufu alimfunulia mmoja wa manabii wake akimuamuru kumpelekea ujumbe mfalme fulani, ya kwamba; ifikapo muda fulani, Mwenye Ezi Mungu ataichukua roho yake. Nabii huyo akaenda kwa mfalme huyo na kumjulisha kuhusu jambo hilo. Baada ya kusikia habari hii, mfalme alianza kuomba na kumsihi Mwenye Ezi Mungu kwa unyenyekevu mkubwa, hata akafikia kuporomoka kutoka kutoka kwenye kiti chake cha enzi. Mfalme huyo alijitahidi kumuomba Mwenye Ezi Mungu akisema: Ewe Mwenye Ezi Mungu! Nakuomba unipe muda zaidi hadi mwanangu akue na aweze kuchukua majukumu yangu. Mwenye Ezi Mungu akamshushia Wahyi nabii huyo kwa mara nyengine, akisema: Nenda kwa mfalme na umjulishe kuwa nimekiakhirisha kifo chake na kumuongezea miaka kumi na tano katika maisha yake. Nabii huyo akasema kumwambia Mola wake: Ewe Mwenye Ezi Mungu, bila shaka Wewe unajua wazi kuwa katu mimi sijawahi kusema uongo. Hapo Mwenye Ezi Mungu Mtukufu akamwambia: 'Wewe ni mtumishi wangu na kazi yako ni kutekeleza amri zangu. Hivyo basi peleka ujumbe huu kwake. Hakuna mtu hata mmoja mwenye haki ya kuhoji maamuzi ya Mwenye Ezi Mungu.

Alipomaliza kusema hayo, Imamu alimgeukia Suleiman na kusema: Ninadhani fikra zako juu ya jambo hili kama zilivyo fikra za Wayahudi? Suleiman akajibu: Ninamuomba Mwenye Ezi Mungu aniepushe na mawazo kama hayo. Kwani Wayahudi wanasemaje kuhusiana na hili? Imamu akasema: Wayahudi wanasema: یدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ ; Mkono wa Mwenyezi Mungu umekunja (Mungu ana mkono wa buli) (Qur'an, Surat Al-Ma'idah, Aya 64). Wanamaanisha kuwa tayari Mwenye Ezi Mungu amesha kamilisha kazi yake, na haumbi tena kiumbe kipya. Ila Mwenye Ezi Mungu aliwajibu kwa kusema: غُلَّتْ أَیدِیهِمْ وَ لُعِنُوا بِما قالُوا ; Mikono yao ndiyo iliyokunjwa, na wamelaaniwa kutokana na kauli zao (mbovu). (Qur'an, Surat Al-Ma'idah, Aya 64).

Kadhalika, kundi fulani liliwahi kuja kwa baba yangu (Musa bin Ja'far) (a.s) na kumuuliza, kuhusina na dhana ya Badaa. Baba yangu aliwajibu akiwaambia: Kwa nini watu wanakanusha Badaa na pia wanakataa uwezekano wa Mwenye Ezi Mungu anaweza kuahirisha maamuzi yake juu ya watu fulani?

Suleiman akauliza: Aya inayosema: إِنَّا أَنْزَلْناهُ فِی لَیلَةِ الْقَدْرِ ; Hakika sisi tumeiteremsha (Qur’an) ndani ya usiki wa Lailatul-Qadr (ushiku wenye cheo) inaashiria nini? (Qur'an, Surat Al-Qadr, aya 1) Imamu akamjibu kwa kumwambia: Ewe Suleiman, Mwenyezi Mungu huweka mipango na matukio yote ya mwaka mzima ujao ndani ya usiku wa Laylatul-Qadr, ikiwa ni pamoja na vifo na uhai, mema na mabaya, riziki pamo na hatima ya kila mmoja. Kila kinachoamuliwa ndani ya usiku huo ni lazima kitokee bila pingamizi. Suleiman akasema: Sasa nimeelewa, maisha yangu yawe munga kwako (nipo chini ya miguu yako), tafadhali endelea. Imamu akaendelea kwa kusema: Ewe Suleiman, baadhi ya mambo yako mikononi mwa Mwenye Ezi Mungu na utendekaji wake hutegemea maamuzi na mapenzi yake. Hukitanguliza akitakacho na hukichelewesha akitakacho. Mwenye Ezi Mungu pia ana mamlaka kamili ya kufuta au kuthibitisha chochote akitakacho. Ewe Suleiman, Imamu Ali (a.s) alisema: Kuna aina mbili za Elimu ya Mwenye Ezi Mungu: Elimu aliyowafunulia malaika na mitume wake, nayo ni ile elimu inayo husiana na masuala ambayo tayari yameshakuwa na muhuri juu yake, ambayo hayarudi nyuma kwenye utokeaji wake. Na ya pili, ni ile elimu ilioko kwenye hazina ya siri za Mwenye Ezi Mungu, ambayo hakuna aijuaye ispokuwa Yeye peke yake. Matokeo yanayo husiana na elimu ya pili ya Mwenye Ezi Mungu ndiyo yanaweza kuharakishwa, kucheleweshwa, kufutwa, au kuthibitishwa kulingana na matakwa na mapenzi Yake.

Suleiman alimwambia Maamun: Ewe Amirul-Mu'minina, kuanzia leo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, sitakataa wala kupingana tena dhana ya Badaa wala sitaihisabu kuwa ni miongoni mwa dhana za uongo. Maamun akajibu kwa kumwambia: Una fursa ya kumuuliza Abul Hassan chochote kile ukitakacho, lakini kwa sharti kwamba uzingatie kwa makini na uwe na insafu katika majadiliano haya. Hapo Suleiman alimgeukia Imamu (a.s) na kusema: Ewe Bwana wangu, je, unaniruhusu kuuliza swali? Imamu akamjibu: Uliza lolote ulitakalo. Suleiman akauliza kwa kusema: Una Maoni gani kuhusiana na mtu anaye iweka Irada (Matakwa ya Mungu) sambamba na maana ya majina na sifa nyengine za Mwenye Ezi Mungu kama vile; Hayyun (Mwenye uhai), Samiun (Msikivu), Basirun (Mwenye kuona), na Qadir (Mweza)? Imamu akajibu: Kikawaida nyinyi (wanatheolojia), huwa mnasema kwamba vitu na viumbe vimeumbwa vikiwa na tofauti, na tafauti hizo zinatokana na matakwa ya Mwenye Ezi Mungu, na wala hamsemi kwamba; viumbe hivyo vinatofautiana kutokana na kwamba Yeye ni Samiun au Basirun. Hii inaonesha kwamba Irada (matakwa ya Mungu) ni tofauti na majina na sifa za Samiun, Basirun na Qadirun.

Suleiman akauliza kwa kusema: Je, tokea mwazno Mwenye Ezi Mungu alikuwa na Irada (matakwa), yaani, tokea tangu na tangu Yeye alikuwa na sifa hiyo ya Irada? Imamu akamjibu akimwambia: Ewe Suleiman, je, kwa mtazamo wako Irada yake ni tofauti na Yeye mwenyewe? Suleiman akasema: Ndio. Imamu akaendelea: Ikiwa ndio hivyo, basi unakiri kwamba kuna kitu chengine ambacho kilikuwepo pamoja na Yeye tangu na tangu! Suleiman akakana kwa kusema: Hapana, siamini kwamba kuna kitu chengine kilicho kuwa pamoja naye. Imamu akamuuliza: Je, Irada yake ni jambo jipya? Suleiman akajibu: Hapana, si jambo jipya. Hapo Maamun, alimkemea Suleiman, kwa kumwambia: Unampopoa mtu kama huyu kwa jawazi zisizokuwa na msingi!? Hebu kuwa na insafu; hivi huoni kwamba wanazuoni wenzako wamekaa hapa kukusikiliza?" Kisha akaongeza akisema: Ewe Abul Hassan, endelea na mjadala wa naye katika mjadala wa kitheolojia, bila shaka yeye ni mwanazuoni wa Khorasan! Hapo Imamu alirudia swali lakeakisema: Ewe Suleiman, bila shaka Irada ni jambo jipya, kwa sababu kitu ambacho hakikuwepo tangu mwanzo, kitakuwa ni jambo jipya. Na kama si jambo jipya, basi ni la tangu na tangu. Suleiman akasema: Matakwa yake yanatokana na Yeye mwenyewe, kama vile sifa za; kusikia, kuona, na sifa ya elimu, zinavyotokana na Yeye mwenyewe. Imamu akamwuliza: Je, Yeye mwenyewe amejiwekea matakwa? Suleiman akasema: Hapana. Imamu akahitimisha: Kwa hiyo, Muridu (Mwenye matakwa) si sawa na Samiun (Msikivu) na Basirun (Mwenye kuona).

Suleiman akasema: Mwenyezi Mungu amejipangia mwenyewe, kama vile anavyosikia sauti yake mwenyewe, anaiona nafsi yake mwenyewe, na ana ufahamu wa nafsi yake yeye mwenyewe. Imamu alimwuliza: Kujipangia mwenyewe kunamaanisha nini? Je, inamaanisha kwamba alitaka kitu fulani kuwepo? Je yeye alitaka kuwa hai, msikivu, mwenye kuona, au mwenye uwezo? Suleiman alijibu: Ndiyo. Imamu akauliza tena: Je, hivi alifikia hali hiyo kwa mapenzi na matakwa yake mwenyewe? Suleiman akasema: Hapana. Imamu akahitimisha akisema: Kwa hiyo, kusema kwamba alijipangia (alitaka kwa matakwa au kwa Irada yake) kuwa hai, msikivu, na mwenye kuona kutakuwa hakuna maana yoyote; kwa sababu uhai, kusikia, na kuona kwake vitakuwa havikutokana na matakwa (Irada) yake mwenyewe.

Suleiman akasema: Hapana, bila shaka ni kwa matakwa na mapenzi yake mwenyewe. Alipojibu kwa kauli hiyo, Maamun na wale waliokuwepo pamoja naye wakaangua kicheko, na Imamu Ridha (a.s) naye pia alitabasamu na kusema: Msimpe uzito mwanatheolojia wa Khorasan, wala msimuudhi. Kisha Imamu akaendelea: Ewe Suleiman, kwa mujibu wa imani yako, unadai kwamba Mwenye Ezi Mungu alibadilika kutoka hali moja kwenda nyingine, na hii ni moja ya mambo ambayo hayafai kumhusisha nayo Mwenye Ezi Mungu. Suleiman akabaki kimya na kutulia tuli bila kutikisika.

Imamu Ridha (a.s) akamgeukia Suleiman na kumwambia: Ewe Suleiman, nina swali langu moja nataka unijibu. Suleiman akajibu kwa heshima: Uliza tu, roho yangu iwe nifidia kwako (nipo chini ya miguu yako). Imamu akauliza: Niambie, je, wewena marafiki zako mnashiriki katika mijadala ya kitheolojia kwa kuzingatia maarifa na uelewa wenu, au kwa kuzingatia yale msiyoyajua wala kuyafahamu? Suleiman akajibu: "Bila shaka, tunajadili kwa kuzingatia yale tunayoyajua na kuyaelewa. Imamu akasema: Basi, jambo ambalo linaeleweka kwa kila mtu ni kwamba; mpenda na mwenye matakwa (mtenda au subject) ni tofauti na tendo (kitenzi au verb) lenyewe la kutaka, na pia ni lazima mpenda (mtaka) jambo awepo kabla ya tendo lenyewe kufanyika. Pia mtendaji ni lazima awe ni tofauti na kitendo chake. Hivyo, kauli yenu isemayo kuwa; matakwa na kutaka ni kitu kimoja! Inapingana na mantiki hii. Suleiman akasema: "Ewe bwana wangu roho yangu iwe ni fidia kwako (nipo chini ya miguu yako), suala hili halitegemei tu welewa na maarifa ya watu wa kawaida.

Imamu akamwambia: Hivyo basi, bila kuwa na maarifa ya kina au taarifa za uhakika, mmsijivishe joho la elimu, kisha mkadai kuwa Irada (matakwa ya Mungu) ni sawa na Samiun (kusikia) na Basirun (kuona). Bila shaka imani yenu, haijasImamua juu ya misingi ya akili au elimu sahihi. Suleiman akabaki kimya, bila kujibu kitu. Imamu akaendelea na hoja zake kwa kumuuliza akimwambia: Ewe Suleiman, je, Mwenye Ezi Mungu ana elimu juu ya kila kitu kilichomo Peponi na motoni? Suleiman akakiri kisha akasema: Ndiyo, bila shaka atakuwa na elimu navyo. Imamu akamuuliza tena: Je, na yale mambo yatakayoteka ambavyo ni viumbe vya baadae, vilivyomu katika elimu ya Mwenye Eiz Mungu, je navyo vitatokea?" Suleiman akajibu: Ndiyo. Imamu akauliza: Sasa, iwapo kila kitu kitakuwa tayari kimesha umbwa na hakutakuwa na chochote kilichosalia, je, Mungu bado anaweza kuongeza au kuondoa baadhi yake?

Suleiman akasema: “Bilas haka Mwenye Ezi ataleta viumbe wengine”. Imamu Akamwambia: “Kulingana na maelezo yako haya, hii itamaanisha kwamba; Mwenye Ezi Mungu, huongeza kitu chengine zaidi ya vile vya mwanzo, jambo ambalo litamaanisha kwamba, Yeye ameoneza jambo ambalo hapo mwanzo halikuwepo ndani ya elimu Yake. Kwa lugha nyengine ni kwamba; kuna kitu kitakachokuja ambacho hakikiwemo ndani ya elimu Yake, kwa sababu tulikwisha sema kwamba; yale yote yatakayokuja baadae ambayo yamo ndani ya elimu Yake, tayari yamesha umbwa na yamesha kuwepo, nawala hakuna chengine kilichobaki nje yake.” Suleima akasema: “Mimi ni fidia kwako (nipo chini ya miguu yako), bila shaka viumbe vijavyo havina mwisho”. Imamu akamjibu: “Hivyo basi kwa mtazamo wako; Elimu ya Mwenye Ezi haija vizunguka vile vyote vilivyomo Peponi na Motoni, kwa sababu viumbe hivyo havina mwisho, kwa hiyo Yeye atakuwa hana elimu ya kile ambacho bado hakijatokea. Bilas haka Mwenye Ezi ametakasiaka na yumbali mno na wasifu (ujinga) kama huo”. Suleiman akasema: “Kwa hakika mimi nimesema kuwa Yeye hana elemu juu ya yaliomo Peponi na Motoni, kwa kuwa Yeye mwenyewe amevisifu viliwili hivyo kwa sifa ya ‘khulud’ (maisha yasio na mwisho), nasi tukahisi tabu kuviwekea kiwango na kikomo maalumu”. Imamu al-Ridha (a.s) akasema: “Elimu yake juu ya viwili hivyo, si kizuizi kinacho sababisha vitu hivyo kuwa na kikomo, kwa sababu Yeye anaweza kuwa na elimu navyo kiwa akavipa engezeko jengine juu yake, kisha akajaalia engezeko hilo kuwa ni endelevu, kama Mwenye Ezi Mungu asemavyo katika Qu’rani: كُلَّما نَضِجَتْ جُلُودُهُمْ بَدَّلْناهُمْ جُلُوداً غَيْرَها لِيَذُوقُوا الْعَذابَ‏ ; Kila ngozi zao zinapobabuka tunawabadilishia ngozi nyengine ili waonje adhabu (ipaswavyo). Surat Al-Nisaa Aya ya 56. Pia kuhusiana na watu wa Peponi anasema: “عَطاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ ; Neema isiyo na mwisho”. Pia Mwenye Ezi Mungu anasema: “وَ فاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ لا مَقْطُوعَةٍ وَ لا مَمْنُوعَةٍ ; Na matunda (kwa ajili ya watu wa Peponi), hayana mwisho na hayana umarufu (wa kutatumia)”. Hivyo Mwenye Ezi ni mwenye elimu nayo, na wala Yeye haya hayapi ukomo katika uwepo na uendelevu wake, je hivi hujaona yaliwayo na yanyewayo na watu wa Peponi, hivi nafasi yake haichukuliwi na vyakula na vinywaji vyengine?” Suleman akajibu: “Ndio, (bila shaka nafasi yake huchukuliwa na vyakula na vinyaji nyengina na kufanya vitu hivyo visiwe na mwisho),” Imamuu akamwambia: “Je hivi vitu hivyo vinaweza kumalizika hali ya kwamba nafasi yake huchukuliwa na vitu vyengine?” Suleima akasema: “Hapana”. Imamu akamwambia: “Hivyo basi ikiwa kitu fulani kitaondoka kisha papo hapo nafasi yake ikakamatwa na kitu kifananacho, bila shaka kitu  hicho kitaenelea bila kuwa na mwisho”. Suleima akasema: “Bila shaka katika hali hiyo kutakuwa hakuna kiengezekacho, kwa hiyo hakutakuwa na ziada watakayoipata, hii ina maana ya kwamba Mungu hatawaongezea kitu”. Imamu akasema: “Imamu Ridha (a.s) akaendelea kusema: "Ikiwa hali itakuwa hivyo, kila kitu kitafikia mwisho wake. Elewa basi ewe Suleiman ya kwamba; imani kwma hii inapingana na dhana ya kudumu kwa Pepo na Moto, na ni kinyume na mafunzo ya Qur'an. Mwenye Ezi Mungu Mtukufu katika Qur’ani anasema: لَهُمْ ما يَشاؤُنَ فِيها وَ لَدَيْنا مَزِيدٌ ; Wao watapata wanachotaka ndani yake, na nyongeza yao ipo mikononi mwetu (Qur'an, Surat Qaf, Aya ya 35). Pia anasema: عَطاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ ; Ni zawadi (neema) isiyokatika (Qur'an, Surat Huud, Aya ya 108), na anasema tena: وَ ما هُمْ مِنْها بِمُخْرَجِينَ‏ ; Na wala wao hawatatolewa humo (Qur'an, Surat Al-Hijr, Aya ya 48). Vilevile anasema: خالِدِينَ فِيها أَبَداً ; Wao watadumu humo milele (Qur'an, Surat Al-Bayyinah, Aya ya 8), na anasema: وَ فاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ لا مَقْطُوعَةٍ وَ لا مَمْنُوعَةٍ ; Na matunda mengi, yasiyokatika wala kuwa na umarufuku (wa kuyatumia) (Qur'an, Surat Al-Waqi'ah, Aya ya 32 hadi 33).

Hapo Suleiman akabaki kimya bila ya kuwasilisha jawabu yoyote.

Imamu Ridha (a.s) akamgeukia Suleiman na kumwambia: Ewe Suleiman, unaweza kuniambia kama Irada (matakwa ya Mungu) ni kitendo au si kitendo? Suleiman akajibu: "Ndiyo, bila shaka ni kitendo. Imamu akamjibu kwa kusema: Ikiwa ni hivyo, basi Irada ya Mwenye Ezi Mungu, itakuwa ni jambo jipya ambalo halikuwepo hapo mwanzo, hii ni kwa sababu kila kitendo ni tukio jipya lijalo ambalo hualikuwepo. Suleiman akajaribu kujitetea kwa kusema: Hapana, Irada si kitendo. Imamu akasema: Basi, kwa mujibu wa kauli hiyo, wewe utakuwa unaamini kuwa kuna kitu kilocho kuwepa pamoja na Mwenye Ezi Mungu ambacho kimekuwepo pamoja na Yeye tangu na tangu.

Suleiman alisema: Irada ni uanzilishi (uumbaji). Imamu akamwambia: Ewe Suleiman, huu ndio ule ule mtazamo wa bwana Dhirar na wenzake mlioukosoa, usemao kwamba; kila kitu alichoumba Mwenyezi Mungu katika mbingu, ardhi, baharini au kwenye nchi kavu—iwe ni mbwa, nguruwe, tumbili, binadamu, au kiumbe chochote—ni Irada ya Mwenye Ezi Mungu. Na kwamba Irada ya Mwenye Ezi Mungu ina uhai (inaishi), inakufa, inakwenda, inakula, inakunywa, inaoa na kuolewa, inapata ladha, inafanya dhuluma, inafanya machafu, inakufuru na kumshirikisha Mungu. Hivyo, yapaswa kujitenga na imani kama hiyo na kukosoa msImamuo huu wa kupotosha.

Suleiman akasema: Kwa mtazamo wangu Irada ni sawa na sifa za; usikivu, kuona, na kuwa na elimu. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Umerudia tena maoni yako ya awali! Hebu kanza niambie, kuhusiana na sifa za usikivu, kuona, na elimu, je, sifa hizi ni viumbe? Suleiman akajibu: Hapana, si vitu vilivyo umbwa. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Kama ni hivyo, sasa ni kwa nini basi wakatiki mwenngi huwa inaifuta sifa ya Irada kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu? Yaani wakati mwingine mnasema Mwenye Ezi Mungu si ametaka, na wakati mwingine huwa mnasema Mwenye Ezi Mungu hakutaka, hali ya kwamba mnaamini kuwa matakwa si kitendo cha Mwenye Ezi Mungu. Suleiman akasema: Hii ni sawa na tunavyosema wakati mwingine kuwa Yeye alijua, na wakati mwingine hakujua.

Imamu Ridha (a.s) akamjibu: Hiyo si sawa, kwa sababu kukanusha uwepo wa kimejulikana hakufanani na kukanusha elimu yenyewe. Lakini kukanusha litakiwalo ni sawa na kukanusha matakwa yenyewe. Ikiwa kitu hakikutakiwa, basi hapo huwa hapana matakwa. Kwa hivyo, elimu inaweza kubaki thabiti hata kama lijulikanalao likawa halipo. Hii ni kama uwezo wa kuona; mtu anaweza kuwa na uwezo wa kuona hata kama hakuna kitu cha kuonekana. Vivyo hivyo, elimu inaweza kubaki thabiti hata kama jambo linalojulikana likawa halipo kabisa kabisa.

Suleiman alijibu akisema, Irada (mapenzi au matakwa ya Mungu) ni kitu kilichoumbwa. Imamu Ridha (a.s) akamjibu, Ikiwa Irada ni kitu kilichoumbwa, basi ni itakuwa ni jambo jipya ambalo halikuwepo hapo mwanzo, na hivyo haiwezi kulinganishwa na sifa za kusikia na kuona, ambazo ni asili ambazo ni za enzi na ezi na hazikuumbwa bali zikukuwepo tangu nba tangu. Ila wewe unasisitiza kuwa Irada ni kitu kilichoumbwa. Suleiman akaeleza zaidi kwa kusema: Irada ni mojawapo ya sifa zake za milele (tangu na tangu) na haijawahi kuondoka. Imamu akamjibu, Kama ni hivyo, basi inamaanisha kuwa ubinadamu wenyewe haujawahi kuondoka, kwa kuwa sifa zake za milele hazijawahi kubadilika. Suleiman akapinga, Hapana, kwa sababu Yeye hajaitengeneza sifa hiyo. Imamu Ridha (a.s) akamalizia kwa kumwambai, Ewe Khurasani, una mitelezo mingi mno! Je, kwani si kila kitu huwepo (huumbwa) kwa matakwa na amri ya Mungu?

Suleiman akajibu: Hapana. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Ikiwa jambo hilo (ubinadamu) halikutokana na matakwa yake, maamuzi yake, amri zake, wala ushirikiano wake, basi ni vipi linaweza kuwepo? Bila shaku Mungu hayupo katika hali hiyo ya upungufu. Suleiman akabaki bila majibu.

Kisha Imamu Ridha (a.s) akaendelea: Je, unaweza kunieleza kuhusu kauli ya Mwenye Ezi Mungu Mtukufu isemayo: وَ إِذا أَرَدْنا أَنْ نُهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنا مُتْرَفِيها فَفَسَقُوا فِيها ; Na tunapotaka kuuangamiza mji fulani, tunawaamuru wale wakuu na walioneemeshwa ndani yake, na kisha wao hukiuka mipaka ndani yake... (Qur'an 17:16). Hii inaashiria kwamba Mungu huzalisha irada mpya, au sivyo?" Suleiman akajibu: Ndiyo. Imamu akasema: Ikiwa ni hivyo, na kwamba Irada imekuja kama ni jambo jipya, basi kauli yako kwamba Irada ni sehemu ya Mungu au ni moja ya sifa zake za asili, itakwa si sahihi. Kwa sababu Mungu hawezi kujizalisha yeye mwenyewe, wala kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine. Mungu ametukuka na hayo na yumbali na mapungufu kama hayo.

Suleiman akajibu: Hapo Mwenye Ezi Mungu hakuwa akimaanisha kuwa Yeye anazalisha irada mpya. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Ikiwa hivyo, alikusudia nini? Suleiman akajibu: Alikusudia kutenda kitendo fulani. Imamu Ridha (a.s) akasema: Ole wako! Umekuwa ukirudiarudia suala hili mara kwa mara. Nimesha kwambia kwamba Irada ni jambo lililozaliwa kwa sababu kutenda jambo ni kuleta jambo jipya. Suleiman akasema: Basi, Irada itakuwa haina na maana. Imamu Ridha (a.s) akasema: Kwa hivyo, Yeye mwenye amekujulisheni kuwa Yeye ni mwenye sifa ya Irada, ambayo haina maana yoyote ile, kulingana na maelezo yako. Ikiwa Irada haina maana ya sifa ya tangu na tangu wala sifa ya hivi sasa, basi kauli yenu kwamba Mwenyezi Mungu (swt) yuwaendelea kuwa na matakwa, itakuwa ni kauli batili isiyo na maana yoyote ndani yake.

Suleiman akajibu: Nilivyosema hivyo, nilikuwa nikimaanisha kwamba Irada ni kitendo cha Mwenye Ezi Mungu (swt) ambacho hakijabadilika. Imamu Ridha (a.s) akamjibu: Je, hujui kwamba kitu kisichobadilika hakiwezi kuwa na sifa za; mtendwa, mtangu, na kiumbe mpya kwa wakati mmoja? Hapo, Suleiman akabaji ya kuwa na majibu ya maswali haya. Imamu Ridha (a.s) akaongeza: Hakuna shida, endelea na maswali yako. Suleiman akasema: Nilisema kwamba; Irada ni sifa ya Mwenye Ezi Mungu. Imamu Ridha (a.s) akasema: Unarudiarudia kusema kwamba; Irada ni sifa ya Mwenye Ezi Mungu, sasa je sifa hii ni jambo lililozaliwa au ni la milele (tangu na tangu)? Suleiman akajibu: Ni jambo lililozaliwa. Imamu Ridha (a.s) akasema: Allahu Akbar. Kwa hiyo Irada ni kitu kilichokuja baadae, hata kama kitu hicho ni miongoni mwa sifa za Mwenye Ezi Mungu za tangu na tangu, ila Yeye yuwaweza kubaki bila ya kuwa na matakwa ya kitu fulani. Imamu akaendelea kusema: “Lile lililokuwa la tangu haliwezi kuwa ni mtendwa.” Suleiman akasema: Vitu haviwezi kuhisabiwa kuwa Irada, na Mwenye Ezi Mungu hakuwa na matakwa ya kutaka kitu chochote." Imamu Ridha (a.s) akajibu: Ewe Suleiman, umeingiwa na wasiwasi. Imamu Ridha (a.s.) akamwambia: Je, hivi Mwenye Ezi Mungu ameumba kitu ambacho hakukitaka kukiumba? Bila shaka hali hii itakuwa inaashiria kuwa; Mwenye Ezi Mungu hajui kile anachokifanya, hali ya kwamba Mwenye Ezi Mungu ametukuka na sifa kaka hizi. Suleiman akajibu: "Ewe bwana wangu, mimi nilisema kwamba Irada ni sawa na kusikia, kuona, na elimu.

Ma'mun alisema: Ole wako, Suleiman! Hivi ni mara ngapi utarudia makosa hayo hayo? Acha kushikilia jambo hili hebu elekeze nguvu zako kwenye mambo mengine, kwani katu hutawezi kutoa majibu sahihi juu ya suala hili. Imamu Ridha (a.s) akamjibu: Acha tu, ewe Amirul-Mu'minin. Usimkatishie mjadala wake; kwani atachukulia hilo kama ni uthibitisho wa mtazamo wake. Endelea, Suleiman.

Suleiman akasema: Nilisema kwamba; matakwa (Irada) ni sawa na kusikia, kuona, na elimu. Imamu akajibu: Haina shida. Niambie, je, matakwa yana maana moja au yana maana nyingi? Suleiman akajibu: Yana maana moja. Imamu akasema: Hivyo basi, ikiwa matakwa yote yatakuwa na maana sawa, basi matakwa ya kusImamua yatakuwa sawa na matakwa ya kukaa, na matakwa ya maisha yatakuwa sawa na matakwa ya kifo. Kwa hiyo ikiwa matakwa ya Mwenye Ezi Mungu yatakuwa na maana moja, hivyo basi hakutakuwa matakwai ya Mungu yatakayokuwa na umuhimu zaidi kuliko mengine, na hakuna yatakayokuwa tofauti na mengine; yote yatakuwa ni sawa." Suleiman akajibu: Maana zake zinatofautiana. Imamu akasema: "Sawa ni vyema, hebu niambie basi, je, ‘Murid’ (mtakaji) ni sawa na ‘Irada’ (matakwa) au ni kitu chengine?

Suleiman akasema: Bali Yeye ambaye ni Muridu (Mtakaji) ndio Irada yenyewe. Imamu akamwambia: Kwa hiyo, kulingana na mtazamo wane, mptaka (mwenye Irada) ni kitu chengine, kwa sababu Yeye ndiye Irada yenyewe. Suleiman akasema: Ewe bwana wangu! Irada (matakwa) si sawa na mtakatji. Imamu akasema: Kwa hivyo, Irada ni jambo lililozaliwa baadae, vinginevyo ingemaanisha kuwa; hapo tangu kulikuwa na kitu chengine kilichopo pamoja na Mwenye Ezi Mungu. Fikiria kwa makini na endelea na maswali yako. Suleiman, akionekana kujiondoa katika kauli yake ya awali, akasema: Hapana, bali Irada ni moja tu kati ya majina ya Mwenye Ezi Mungu. Imamu akamuuliza: Je, Mwenye Ezi Mungu Mwenyewe amejipa jina hili?"

Suleiman akasema: Hapana, Hajajiita Mwenyewe kwa jina hilo. Imamu Ridha (a.s) akasema: Kwa hivyo, huna haki ya kumwita kwa jina ambalo Hajajiita Mwenyewe. Suleiman akajibu: Lakini Amejielezea Mwenyewe kama Yeye ni Mpenda (Mwenye Irada). Imamu Ridha (a.s) akasema: Kujielezea Mwenyewe kama Mpenda (mtakaji) haimaanishi kwamba Yeye ni Irada, na wala si sawa na kusema kwamba Irada ni moja wapo ya majina Yake.

Suleiman akajibu kwa kusema: "Kwa sababu Irada Yake ni elimu Yake. Imamu Ridha (a.s) akasema: Ewe usiyejua (Ewe juha)! Ikiwa Yeye analijua jambo fulani, hiyo humaanisha amelitaka. Suleiman akajibu: Ndiyo. Imamu Ridha (a.s) akaendelea: "Basi, kama Hakulitaka, si itakuwa Hakulijua? Suleiman akajibu: Ndiyo. Imamu Ridha (a.s) akauliza: "Umeyatoa wapi hayo, na una shahidi gani kwamba Irada Yake ni elimu Yake? Wakati ambapo Anaweza kujua kile ambacho Hakitaki kamwe. Na ushahidi wa hili ni kauli ya Mwenye Ezi Mungu isemayo:وَ لَئِنْ شِئْنا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنا إِلَيْكَ‏ ; Na kama tungelitaka, tungeondoa yale tuliyo kufunulia. Hii inaonesha kwa Yeye anajua jinsi ya kuondoa, lakini kamwe Hataondoa."

Suleiman akasema: Kwa sababu tayari Amekamilisha jambo hilo, hivyo hakuna chengine atakacho ongeza ndani yake. Imamu Ridha (a.s) akasema: Huu ni mtazamo wa Wayahudi! Ikiwa hivyo, vipi Mwenye Ezi Mungu amesema: ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ; Niombeni, Nitajibu maombi yenu? Suleiman akajibu: Alikusudia kuwa Yeye ana uwezo wa kufanya hivyo. Imamu akamwuliza: Je, Anaahidi jambo ambalo Hatotekeleza? Na kwa nini amesema: يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ ما يَشاءُ  ; Anaongeza katika uumbaji Atakavyo, na tena Mwenye Ezi Mungu Mtukufu amesema: يَمْحُوا اللَّهُ ما يَشاءُ وَ يُثْبِتُ وَ عِنْدَهُ أُمُّ الْكِتابِ ; Mwenyezi Mungu hufuta Atakavyo na kuthibitisha (Atakavyo), na kitabu (hatamu au funguo) asili kiko anacho Yeye? Vipi maelezo ya Aya hizi yanaweza kulingana na kauli ya kwamba Yeye amesha maliza kuumba na hakuna jingine liwezalo punguka au kuzidi?"

Hapo Suleima akakaa kimya bila kutoa jawabu.

Imamu Ridha (a.s) akamwuliza kwa kumwambia: Ewe Suleiman, je, Mwenye Ezi Mungu ana habari za kuja kwa mwanadamu atakayeishi, huku akiwa Yeye hataki kabisa kumuumba mwanadamu huyo? Na je, Anajua kwamba kuna mwanadamu atakaye kufa leo, wakati ambapo Yeye hataki kabisa mwanadamu huyo afe leo? Suleiman akajibu: Ndio. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Sasa je, Yeye Ana elimu ya yale yatakayotokea kwa matakwa Yake, au yale yatakayo tokea bila ya matakwa Yake? Suleiman akajibu: Anajua kwamba yote mawili yatatokea. Imamu Ridha (a.s) akauliza: Ikiwa ni hivyo, je, Anajua kwamba kuna mwanadamu ambaye ni hai na mfu, aliyesImamua na aliyekaa, kipofu na mwenye kuona kwa wakati mmoja? Hali hii ni jambo lisilowezekana. Suleiman akasema: Roho yango iwe ni muhanga kwako (nipo chini ya miguu yako), bila shaka Yeye ana alemu ya moja kati ya viwili hivyo. Imamu akasema: Sawa, lakini je, kipi kitakachotokea, ni kile alichotaka kitokee au kile ambacho hakutaka kitokee?

Suleiman akasema: Kile alichotaka kutokea. Hapo Imamu Ridha (a.s), Maamun, na wafuasi wa madhehebu mbali mbali waliangua kicheko. Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Umekosea, na umepuuza kauli yako idemayo kwamba; Yeye Anajua kuwa kuna mwanadamu ataye kufa leo hali ya kwamba Yeye hataki mwanadamu huyo afe leo, na kwamba Yeye huumba kiumbe wakati Yeye mwenyewe hataki kuumba kiumbe hicho. Ikiwa ni hivyo, basi nyinyi hamtakiwi muamini kwamba Yeye ana elimu juu ya kile ambacho Yeye hakutaka kitokee. bali Yeye ana elimu ya kile tu anachotaka kitokee.

Suleiman akajibu: Kauli yangu ni kwamba Irada si Yeye mwenyewe, wala si kitu chengine chochote. Imamu Ridha (a.s) akasema: Ewe mjinga, unaposema kwamba; Irada (matakwa) si Yeye mwenyewe, hapo utakuwa unaiweka Irada kuwa kitu chengine (na kujenga uwili kati ya Mungu na kitu chengine). Na unaposema kwamba si kitu chengine, unaifanya (Irada hiyo) kuwa ni Yeye mwenyewe.

Suleiman alisema: "Yeye anajua jinsi ya kutengeneza (kuumba) kitu fulani. Imamu Ridha (a.s) akasema: Bila shaka. Suleman akaendelea: “Basi hilo jambo tosha linalo thibitisha uwepo wa kitu hicho”. Imamu akasema: "Unachanganyw amabo; kwa sababu mtu anaweza kuwa na ujuzi mzuri wa ujenzi bila yeye kujenga kitu fulani, mshoni mzuri bila kushona, na kawa ni mzuri katika kutengeneza vitu, bila kutengeneza kitu.

Imamu Ridha (a.s) akaendelea akimwambia: Ewe Suleiman, hivi Mwenye Ezi Munge Yeye mwenyewe anajua kwamba; Yeye ni Mmoja, na hakuna kitu chengine pamoja naye? Suleiman akajibu: Ndio. Imamu Ridha (a.s) akasema: Je, kujua kwake huko kunaweza kuwa ni ithibati ya kuwepo kitu chengine pamoja naye?" Suleiman akajibu: "Yeye hajijui kuwa ni Mmoja pweke bila kuwepo kitu chengine pamoja naye.

Imamu Ridha (a.s) akasema: Je, wewe unajua kuwa Yeye yupo katika hali hiyo? Suleiman akajibu: Ndio. Imamu Ridha (a.s) akasema: Basi, wewe, Ewe Suleiman, ni mwenye kuelewa zaidi kuliko Yeye. Suleiman akasema: "Masuala haya ni muhali. Imamu Ridha (a.s) akasema: Kwa mtazamo wako wewe, ni muhali Yeye kuwa ni Mmoja bila kitu chengine kuwa pamoja Naye, na kwamba Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, Mwenye hekima, na Mwenye uwezo, yote hayo ni muhali kwako?

Imamu Ridha (a.s) akamwambia: Kwa nini basi Mwenyezi Mungu yuwasema kwamba; Yeye ni Mmoja, Mhai, Mwenye kusikia, Mwenye kuona, Mwenye hekima, Mwenye uwezo, Mwenye elimu, na Mjuzi, hali ya kwamba (kwa maelezo yako), Yeye hana hana elimu juu ya hayo? Kauli yako hii, ni kupinga kauli yako mwenyewe na kuyakana maelezo yako. Mwenyezi Mungu ni Adhimu na ametakasika na mapungufu hayo. Kisha Imamu Ridha (a.s) akaendelea: Basi, ni jinsi gani Yeye awe na matakwa ya kuumba kitu ambacho Yeye mwenyewe hajui namna ya uumbikaji wa kitu hicho? Na kama mumba hajui jinsi ya kuumba kitu kabla ya kukiumba, basi yeye ni mchanganyikiwa asiyejua atendalo. Bila shaka Mwenye Ezi Mungu ametakasika na mapungufu kama hayo.

Suleiman alisema: Irada ni nguvu (uwezo). Imamu Ridha (a.s) akamjibu kwa kusema: Mwenye Ezi Mungu (s.w.t) ana uwezo wa juu ya kila kitu, hata juu ya yale ambayo Yeye hayataki, na hii ni hakika isiyokatalika; kwani Mwenye Ezi Mungu amesema: وَ لَئِنْ شِئْنا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنا إِلَيْكَ ; Na tungelitaka, basi tungeyaondoa yale tuliokwisha kukufunulia. (Israa, 86). Na kama sifa ya Irada ingekuwa ni sawa na sifa ya nguvu, basi Aya hii ingekuwa na maana ya kwamba; Mwenye Ezi Mungu alitaka kuchukua maamuzi ya kuondoa nguvu (uwezo) zake, kwani Yeye ni mwenye uwezo.

Hapo Suleiman alishindwa kutoa jibu. Maamun alisema: Ewe Suleiman, Yeye ndiye mwenye elimu kubwa zaidi miongoni mwa watu wa ukoo wa Hashim. Kisha, walihudhuria malumbano hayo wakaondoka. [18]

Mada Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo