Nenda kwa yaliyomo

Kupoza Moto kwa ajili Ibrahim

Kutoka wikishia
Picha yenye kuakisi Kutupwa kwa Ibrahim kwenye moto.

Kupoza Moto kwa Ajili ya Ibrahim (Kiarabu: برد النار لإبراهيم) Kulingana na Qur’ani, Ibrahim aliokoka kimiujiza kutokana na moto aliotayarishiwa na Namrud aliyekuwa mfalme wa Babul (Babylon) na waabudio sanamu. Ibrahim alitayarishiwa moto huo kama ni adhabu ya tendo lake la kuyavunja masanamu yao waliokuwa wakiayaabudu.[1] Qur'ani inarejelea tukio hili kuanzia Aya 51 hadi 70 za Surat Anbiya, Aya 85 hadi 98 za Surat Saffaat, na Aya ya 24 ya Surat Ankabut.[2] Kwa mujibu wa Aya 69 ya Surat Anbiya, Mwenye Ezi Mungu aliupa moto amri ya kuwa baridi na salama kwa ajili ya Ibrahim.[3] Wafasiri wa Qur’ani wanaamini kwamba; amri hii kwa moto ilikuwa amri ya kuleta mabadiliko ya kimaumbile kwenye maumbile halisi ya moto huo, ambayo kwa lugha ya kitaalamu huita kwa jina la amru takwiiniy.[4] Wafasiri wameeleza maoni tofauti kuhusiana na jinsi amri hii ya Mungu ilivyotekelezwa hadi moto ukawa baridi kwa ajili ya Ibrahim.[5] Maoni ya wafasiri hao ni kama ifuatavyo:

  • Asili ya moto ilibadilika kabisa kabisa na ikawa ni bustani fulani.[6]
  • Mwenye Ezi Mungu aliweka kizuizi kati ya moto na Ibrahim ili asiungue.[7]
  • Joto liliondolewa kutoka kwenye asili ya maumbile ya moto kwa sababu joto kiasilia si sehemu asili ya moto isiyoweza kutenganishwa nayo.[8]
  • Mwenye Ezi Mungu aliweka sifa maalum kwenye mwili wa Ibrahim ili moto huo usimuathiri, kama vile hali ilivyo kwa miili ya walinzi wa Jahannam.[9]
  • Jambo hili linahusiana na masuala maalumu ya kimiujiza ya Mungu ambayo hatuwezi kuelewa wala kutoa ufafanuzi kikamilifu kuhusiana nalo.[10]

Kwa mujibu wa tafsiri kadhaa za Qur’ani, tukio hili la kuyavunja masanamu lilitokea wakati Ibrahim alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita.[11] Tendo ambalo lilitokea wakati watu walipokuwa nje ya mji kwa ajili ya sherehe za kila mwaka, ambapo Ibrahim alitumia shoka maalumu kwa ajili ya kuyavunja masanamu, kisha akaliweka shoka hilo kwenye sanamu kubwa kubwa zaidi miongoni mwayo.[12] Mtu mmoja aliyekuwa akijua uadui wa Ibrahim dhidi ya sanamu hayo ndiye aliyekuja alifichua jina la mvurugaji wa masanamu hayo. Ibrahim alipelekwa mahakamani na alijaribu kudharau imani za waabudu masanamu hayo kwa kusema kuwa; sanamu kubwa miongoni mwayo ndilo ililo yavunja masanamu hayo, ila waabudio masanamu hayo hawakuamini maneno hayo. Hatimaye, waliamua kumchoma moto kama ni adhabu dhidi yake. Washirikina hao waabudio sanamu waliwahimiza watu kushiriki katika kumchoma Ibrahim na waliona kama ni msaada muhimu kwa ajili ya miungu yao.[13] Wengine waliweka nadhiri ya kuni au kutoa mali zao kwa ajili ya kununua kuni za kumchomea Ibrahim.[14] Moto ulikuwa ni mkubwa mno hadi kukawa hakuna mtu hata mmoja aliyethubutu kumsogeza Ibrahim karibu na moto huo. Katika hali hii, Iblis alitoa wazo la kutumia manjaniki ambayo ni manati (catapult) maalumu. Ibrahim aliwekwa kwenye manati (catapult) na kurushwa kuelekea motoni.[15]

Kwa mujibu wa baadhi ya Riwaya, wakati Ibrahim alipokuwa akirushwa kuelekea motoni, alizungumza na baadhi ya malaika wa Mwenye Ezi Mungu.[16] Malaika waliomba ruhusa kotoka kwa Mweny Ezi Mungu ili kumsaidia, na Mwenye Ezi Mungu akakubali ombi lao hilo, lakini Ibrahim alikataa msaada wao. Hatimae Jibril alimshauri Ibrahim aombe msaada moja kwa moja kutoka kwa Mola wake, lakini Ibrahim alijibu kwamba Mwenye Ezi Mungu yuwajua vyema hali yake ilivyo na hakuhitaji kuomba msaada.[17] Kuna dua mbalimbali zilizo nukuliwa katika baadhi ya Riwaya zilizohusishwa na Ibrahim. miongoni mwazo kama vile: «یا اللَّهُ یا وَاحِدُ یا أَحَدُ یا صَمَدُ یا مَنْ لَمْ یلِدْ وَ لَمْ یولَدْ وَ لَمْ یکنْ لَهُ کفُواً أَحَد ; Ewe Alla, Ewe Mmoja, Ewe wa Pekee, Ewe Asiye na mfano, Ewe ambaye hajazaa wala hazaliwi, na wala hana anayefanana naye». Pia miongoni mwa dua hizo ni dua isemayo: «اللَّهُمَّ إِنِّی أَسْأَلُک بِحَقِّ مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ لَمَّا آمَنْتَنِی فَجَعَلَهَا بَرْداً وَ سَلاماً ; Ewe Mungu, nakuomba kwa haki ya Muhammad na Aali Muhammad, uniokoe kutokana na moto huu.” Hapo Mwenye Ezi Mungu akaufanya moto huo kuwa ni baridi na salama kwa ajili ya Ibrahim».[18]

Fakhr al-Razi katika tafsiri yake iitwayo Tafsiru al-Kabir alijibu maswali kadhaa kuhusiana na dadisi juu ya ufafanuzi wa tukio la kuchomwa kwa Ibrahim. Moja ya maswali hayo ni kwamba: Je, ni kweli kuwa; kama Mweye Ezi Mungu asingeuamuru "mto huo kuwa salama" baada ya kuaamuru moto huo kuwa baridi, basi Ibrahim angekumbwa na baridi? Akijibu swali hili alisema: hali ya ubaridi wa moto iliktokana na amri ya Mungu, na haingewezekana kwamba Mungu atoe amri ya baridi hatari na kisha aizimue na kuiweka sawa na kuirekebisha ili istawi kulingana na hali ya Ibrahim.[19]

Rejea

  1. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 13, uk. 433-446.
  2. Makarim Shirazi, Tarjume Qur'an, uk. 326, 327, 399 na 449.
  3. Makarim Shirazi, Tarjume Qur'an, uk. 327.
  4. Tabatabai, al-Mīzān, juz. 14, uk. 303; Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 13, uk. 446.
  5. Sajjadi Zade, Naqd Wa Barresi Tafsir Aye Sard Shudan Atash Bar Ibrahim (a.s), majalah Amuzeha-e Qur'an, juz. 25, uk. 158.
  6. Tayyib, Atyab al-Bayān, juz. 9, uk. 208.
  7. Tusi, At-Tibyān, juz. 7, uk. 263.
  8. Iraqi, Al-Qur'ān wa Al-'Aql, juz. 3, uk. 327; Tusi, At-Tibyān, juz. 7, uk. 263.
  9. Fakhrur Razi, Tafsīr al-Kabīr, juz. 22, uk. 159.
  10. Fadhlullah, Min Wahy al-Qur'ān, juz. 15, uk. 241.
  11. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 13, uk. 436.
  12. Tabrasi, Majma' al-Bayān Fī Tafsīr al-Qur'ān, juz. 7, uk. 84, 83; Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 13, uk. 436 & 437.
  13. Makarim Shirazi, Tarjume Qur'an, uk. 327.
  14. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 13, uk. 444; Tabrasi, Majma' al-Bayān Fī Tafsīr al-Qur'ān, juz. 7, uk. 87.
  15. Tabrasi, Majma' al-Bayān Fī Tafsīr al-Qur'ān, juz. 7, uk. 85-87; Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 13, uk. 436 & 444.
  16. Majlisi, Bihār al-Anwār, juz. 12, uk. 24; Tabrasi, al-Ihtijāj, juz. 1, uk. 48.
  17. Majlisi, Bihār al-Anwār, juz. 68, uk. 155.
  18. Majlisi, Bihār al-Anwār, juz. 12, uk. 24; Tabrasi, al-Ihtijāj, juz. 1, uk. 48.
  19. Fakhur Razi, Tafsīr al-Kabīr, juz. 2, uk. 159 & 160.

Vyanzo

  • Sajjadi Zade, Sayyid Ali & Mustafa Mirzai, «Naqd wa Barresi Tafsir Aye Sard Shudan Atash Bar Ibrahim (a.s)», Dofasliname Amuzehaye Qur'ani, No. 25, 1396 S.
  • Fadhlullah, Muhammad Hussein, Min Wahy al-Qur'ān, Lebanon, Dar al-Milak, Chapa ya kwanza, 1419 H.
  • Fakhrur Razi, Muhammad bin Umar, Tafsīr al-Kabīr, Beirut, Dar Ihya' at-Turath al-Arabi, Chapa ya tatu, 1420 H.
  • Iraqi, Sayyid Nuruddin, Al-Qur'ān Wa al-'Aql, Qom, Bunyad Farhang Islami Haj Muhammad Husein KusHanpur, 1362 HS/1983.
  • Majlisi, Muhammad Taqi, Bihār al-Anwār, Beirut, Dar Ihya' at-TuratH al-Arabi, 1403 H.
  • Makarim SHirazi, Nashir, Tafsir Nemune, Tehran, Dar al-Kutub al-Islamiyah, Chapa ya kumi, 1371 HS/1992.
  • Makarim Shirazi, Nashir, Tarjume Qur'an, Qom, Daftar Mutala'at Tarikh wa Ma'arif Islami, Chapa ya pili, 1373 HS/1994.
  • Tabatabi, Muhammad Hussein, Al-Mīzān Fī tafsīr al-Qur'ān, Beirut, Muasase al-A'lami Li al-Matbu'at. Chapa ya pili, 1390 H.
  • Tabrasi, Ahmad bin Ali, Al-Ihtijāj 'Alā Ahl al-Lijāj, Mashhad, Nashr Murtadha, 1403 H.
  • Tabrasi, Fadhl bin Hassan, Majma' al-Bayān Fī Tafsīr al-Qur'ān, Iran, Nashir Khusru, Chapa ya tatu, 1372 HS/1993.
  • Tayyib, Abdul Hussein, Atyab al-Bayān Fī Tafsīr al-Qur'ān, Tehran, Islam, Chapa ya pili, 1369 HS/1990.
  • Tusi, Muhammad bin Hassan, At-Tibyān Fī Tafsīr al-Qur'ān, Beirut, Dar Ihya' at-Turath al-Arabi, Chapa ya kwanza.