Elimu ya Ghaibu
Elimu ya Ghaibu (Kiarabu: علم الغيب) ni kuwa na ufahamu wa mambo yaliyofichika na mambo ambayo hayawezi kueleweka kwa hisi. Kwa mujibu wa Aya za Qur’ani Tukufu, wanateolojia wa Shia wamezingatia aina mbili za elimu ya ghaibu: Moja ni elimu ya asili au dhati na inayojitegemea ya ghaibu, ambayo ina maana ya aina ya elimu ya ghaibu ambayo haiwezi kupatikana kutoka kwa mtu mwingine. Aina hii ya elimu ya ghaibu ni makhsusi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana kwamba, ni ya Mwenyezi Mungu tu na asiyekuwa Yeye hawezi kuwa nayo. Nyingine ni ilm mustafad au elimu tegemezi ambayo Mwenyezi Mungu amewapatia baadhi ya waja wake wateule. Wanachuoni wa Shia Imamiyya wanaamini kwamba, suala la Mitume wa Mwenyezi Mungu na Maimamu Maasumu (a.s) kuwa na elimu ya ghaibu kunatokana na aina ya elimu ya ghaibu ambayo ni mustafad au tegemezi ambayo wanaipata kwa idhini na mafunzo ya Mwenyezi Mungu.
Baadhi ya wanavyuoni wa Kiwahabi wakinukuu Aya za Qur’an wanaamini kuwa elimu ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu, na kuhusisha elimu ya ghaibu na asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni sababu ya upotofu na ukafiri. Wanawatuhumu Mashia kwamba, wanaabudu Maimamu kwa sababu ya kuamini kwao Mitume na Maimamu Maasumu wana elimu ya ghaibu. Kwa upande mwengine wanavyuoni wa Shia Imamiyyah wakinukuu Aya nyingine, wamesema Mwenyezi Mungu huwapa elimu ya ghaibu baadhi ya Mitume na waja wake wateule.
Kwa mujibu wa Imamiyyah, elimu ya ghaibu ya Maimamu (a.s) inatoka kwa Mungu, sawa na elimu ya Mtume (s.a.w.w). Wanaamini kwamba elimu ya Mwenyezi Mungu wakati fulani ilifikishwa kwa Maimamu kupitia kwa Mtume, na wakati mwingine wanapata elimu ya ghaibu kupitia kuzungumzishwa kwa njia ya malaika au ilhamu. Kuhusu elimu ya ghaibu ya Maimamu, kuna rai mbili zilizowasilishwa; wanateolojia kadhaa wa Imamiyya wameiwekea mipaka elimu ya ghaibu ya Imamu kwa baadhi ya matukio, na kwa upande mwingine, baadhi ya wengine, wakitegemea baadhi ya hadithi, wanaona kwamba ujuzi na elimu yao inajumuisha mambo yote yaliyotokea au yatakayotokea siku zijazo.
Utambuzi wa Maana na Nafasi
Elimu ya ghaibu huitwa ile elimu ambayo inahusiana na mambo ya siri na yaliyofichikana mambo ambayo hayawezi kueleweka kwa hisia.[1] Neno ghaibu katika lugha lina maana kitu ambacho kimefunikwa na kufichwa kutokana na hisia za nje; mkabala wake ni vitu vinavyoshuhudiwa, ambayo ina maana ya kitu ambacho kinaweza kueleweka kwa hisia.[2] Ghaibu katika katika istilahi ina maana ya kitu ambacho hakiwezi kutambuliwa kwa msaada wa njia za kawaida.[3]
Wakitaja baadhi ya Aya na Hadithi, Shia Imamiyya wanaamini kwamba sio tu Mtume (s.a.w.w), bali pia Maimamu Maasumu (a.s) na pia baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, wana elimu ya ghaibu kwa idhini na neema ya Mwenyezi Mungu.[4] Kuwa na itikadi kama hii, kumewafanya baadhi ya Mawahabi kuwa na mtazamo kwamba, Mashia ni maghulati (watu wanaompa Imamu Ali (a.s) na wanawe sifa za kiungu au za kinabii na kuzidisha au kutia chumvi katika wasifu wao).[5] Suala la elimu ya ghaibu, aina zake, mipaka na ubora wake ni mojawapo ya masuala yaliyojadiliwa na wanateolojia huko nyuma[6] na leo (katika karne ya 15 Hijria) na majibu baadhi ya tuhuma zisizo na msingi za Mawahabi na ukosefu wao wa ufahamu sahihi kuhusiana na suala hili na mambo ambayo yanachunguzwa na kufanyiwa utafiti na wanateolojia wa Shia Imamiya.[7]
Aina za Elimu ya Ghaibu
Elimu ya ghaibu imegawanyika katika aina mbili kutokana na kufungamana na kuhusiana na yule anayeijua:
- Elimu ya Ghaibu ya Dhati na Yenye Kujitegemea:[8] Makusuidio ya elimu hii ni ile ambayo mtu hajasoma elimu hii kutoka kwa mtu.[9] Aina hii ya elimu ya ghaibu haina mpaka na inahusiana na Mwenyezi Mungu tu. Na inaelezwa kwamba, hana mshirika na mwingine katika elimu hii. [10] Sheikh Mufidu amesema katika kitabu chake cha Awail al-Maqalaat kwamba, baadhi ya maghulati na mufawadh (wanaoamini kwamba, Mwenyezi Mungu amemuachia mwanadamu uhuru na mamlaka kamili ya kufanya atakacho) wameinasibisha aina hii ya elimu ya ghaibu kwa Maimamu Maasumu. [11] Yeye anauona mtazamo huu kwamba, ni batili. [12]
- Ilm Ghayb Mustafad au Elimu yenye mfungamano na utegemezi: [13] Hii ni aina ya elimu ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu amewapatia baadhi ya waja wake. [14] Wanachuoni wote wa Imamiyyah wanaamini kwamba elimu ya ghaibu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na Maimamu Maasumu ni ya aina hii, ambayo ni kwa idhini na kwa kufundishwa na Mwenyezi Mungu, na wanapata elimu ya aina hii ya ghaibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.[15]
Ishkali za Elimu ya Ghaibu ya Mtume (s.a.w.w) na Jibu la Mashia
Baadhi ya Mawahabi wanaona elimu ya ghaibu kuwa ni ya Mwenyezi Mungu pekee na wamekanusha elimu ya ghaibu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na hata kwa Mtume (s.a.w.w). [16] Abdul-Aziz bin Baazi, Mufti wa Kiwahabi wa Saudi Arabia amesema kuwa, kuinasibisha elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni sababu ya upotofu na kufuru kwa Mwenyezi Mungu. [17] Wao wametegemea makundi mawili ya Aya za Qur’ani kama hoja kuhusiana na elimu ya ghaibu:
- Aya ambazo ndani yake Mtume (s.a.w.w) alikanusha juu ya kuwa kwake na elimu ya ghaibu;[18] kama kama hii isemayo: «قُلْ لَا أَقُولُ لَکُمْ عِنْدِی خَزَائِنُ اللَّهِ وَ لَا أَعْلَمُ الْغَیْبَ ; Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana». [19]
- Aya ambazo ndani yake zinazungumzia elimu ya ghaibu na kuitaja kuwa ni mahususi kwa Mwenyezi Mungu;[20] kama Aya isemayo: «وَعِنْدَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ; Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu». [21]
Ili kutoa jibu kwa maoni na mtazamo huu, zimetajwa Aya kama vile Aya ya 44 na 179 ya Surat Al-Imran na Aya ya 26 na 27 ya Surat Jinni, ambazo kwa mujibu wake Mwenyezi Mungu amewajaalia baadhi ya Mitume na watumishi wake wateule ujuzi na elimu ya ghaibu. [22]
Vile vile wamesema kuwa, kwa kuangalia Aya za Qur'an inafahamika kuwa Quran imezungumza kuhusu aina mbili za elimu ya ghaibu, yaani elimu ya ghaibu ya asili na inayojitegemea, na elimu ya ghaibu yenye manufaa (mustafad) na tegemezi. Aya zinazozingatia elimu ya ghaibu kuwa ni ya Mwenyezi Mungu pekee, maana na makusudio ya Aya hizo ni elimu ile ile ya dhati na inayojitegemea ambayo ni ya Mungu pekee, na Aya ambazo zinaashiria juu ya kuweko elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ni zile Aya ambazo zinaashiria na kuonyesha elimu ya ghaibu tegemezi na mustafad; yaani ile elimu ambayo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa idhi yake elimu hiyo amepatiwa Mtume (s.a.w.w) na baadhi ya waja wake wateule.[23]
Murtaza Mutahhari, mwanazuoni na Mwanafalsafa wa Kishia amesema kwa ajili ya kukusanya pamoja makundi mawili ya Aya hizi kwamba, elimu ya ghaibu katika istilahi ya Qur'an ina maana kwamba mtu anajua ghaibu kwa maumbile yake na bila ya kujifunza, na kwa hiyo ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua kuhusu ghaibu, na Mtume (s.a.w.w) na waja wengine wateule ni wenye elimu ya ghaibu na wanapokea elimu ya ghaibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.[24]
Elimu ya Ghaibu ya Maimamu
- Makala kuu: Elimu ya Maimamu
Kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyyah ni kwamba, elimu ya ghaibu ya Maimamu (a.s) ni sawa na elimu ya Mtume (s.a.w.w) ambayo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.[25] Wanaamini kwamba, elimu ya Mwenyezi Mungu wakati mwingine ilifikishwa kwa Maimamu kupitia Mtume; kwa muktadha huo, Mtume (s.a.w.w) aliipokea elimu hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akamfundisha Imam Ali (a.s) na Imam Ali (a.s) alimfundisha Imamu Hassan (a.s) na vivyo hivyo kila Imamu alimfundisha Imamu aliyefuata mpaka Imamu wa mwisho, yaani Imam Mahdi(a.t.f.s).[26]
Wakati mwingine, elimu ya Mwenyezi Mungu humfikia Imamu (a.s) kupitia njia nyinginezo.[27] Kwa mfano, kwa kuzingatia baadhi ya riwaya katika vyanzo vya hadithi vya Waislamu wa madhehebuu ya Shia, Jibril alimwambia Bibi Fatima (a.s) habari za matukio yajayo na akaziandika katika Mus'haf Fatima. [28] Pia, kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, Imamu (a.s) anaweza kupata elimu ya ghaibu kupitia kuzungumzishwa na malaika [29] au wahyi.[30]
Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, Imamu ndiye mrithi wa elimu ya Mitume[31] na mtunza hazina wa elimu ya Mwenyezi Mungu [32]. Mashia wanategemea baadhi ya hadithi, ikiwemo hadithi ya Mji wa Elimu, ambayo ndani yake Mtume (s.a.w.w) alijitambulisha kuwa ni mji wa elimu na Imam Ali (a.s) ni mlango wake.[33]
Kuhusu kiwango cha elimu ya ghaibu ya Imamu, baadhi ya wanateolojia wa Kishia wanaamini kwamba, elimu yao ina mipaka kuhusiana na mambo maalumu.[34] Sheikh Mufidu hakuzingatia suala la elimu ya ghaibu ya Imam kuwa ni sifa ya lazima na sharti la Uimamu wao. Alisema kwamba Maimamu (a.s) wanafahamishwa na wana elimu ya baadhi ya dhamira na makusudio ya watu na elimu na ufahamu wa baadhi ya mambo ambayo hayajatokea bado.[35] Wengine, wakitegemea baadhi ya hadithi,[36] wanaamini kwamba elimu ya Maimamu inajumuisha mambo yote yaliyotokea au yatakayotokea duniani.[37]
Elimu ya Ghaibu ya Mitume Wengine
Kwa mujibu wa Aya ya 26 na 27 ya Surat al-Jinni ni kuwa, Mwenyezi Mungu akitaka anaweza kumpatia elimu ya ghaibu yeyote kati ya Mitume Wake.[38] Kadhalika kwa mujibu wa baadhi ya Aya za Qur'ani, baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu walikuwa na elimu ya ghaibu katika baadhi ya mambo na wakitoa habari kuhusiana na mambo hayo:
- Kwa mujibu wa Aya ya 81 ya Surat Hud, Nabii Lut alifahamishwa kuhusu wakati wa adhabu na baadhi ya Malaika wa Mwenyezi Mungu kabla ya watu wake kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu[39] na huu ni mfano mmojawapo wa kujua mambo ya ghaibu au elimu ya ghaibu.[40]
- Kwa mujibu wa Aya hii: «{[Arabic|وَ أُنَبِّئُکُمْ بِمَا تَأْکُلُونَ وَ مَا تَدَّخِرُونَ فِی بُیُوتِکُمْ}} ; na ninakwambieni kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu». [41] Uwezo wa Nabii Issa (a.s) wa kufahamu na kujua siri za watu zilizofichikana na kufahamu mambo na siri za ghaibu, ni moja ya miujuza na ishara za kuwa kwake Mtume wa haki kwa ajili ya kaumu yake. [42]
- Kwa mujibu wa Aya ya 45 ya Surat Aal Imran, Mwenyezi Mungu kupitia Malaika, alimpa bishara Bibi Maryam ya kuzaliwa mwanawe Issa.[43]
- Kwa mujibu wa Aya hii: «تِلْکَ مِنْ أَنْبَاءِ الْغَیْبِ نُوحِیهَا إِلَیْکَ ; Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia».[44] Wakati Mwenyezi Mungu anapodhihirisha historia ya watu wa Nuh kwa Mtume (saww) ndani ya Qur'an na kumjulisha yeye na watu wake kuhusu hali yao, anasema kuwa: Hizi ni katika khabari za ghaibu alizofunuliwa na kuteremshiwa.[45]