Kuvuka bahari kwa Wana wa Israeli
Kuvuka bahari kwa Wana wa Israeli: Tukio la kuvuka bahari kwa Wana wa Israeli lilikuwa ni miongoni mwa matukio muhimu na ni muujiza wa kipekee uliowakomboa kutoka katika mateso yaliyokuwa yakiwasulubu walipokuwa nchini Misri. Tukio hili lilijumuisha kupasuka kwa bahari na kuruhusu Wana wa Israeli kuvuka salama, huku Firauna na majeshi yake wakizama katika maji bila ya kupata mwokozi.
Kwa mujibu wa amri ya Mwenye Ezi Mungu, Nabii Musa (a.s) aliwaongoza Wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri wakati wa usiku. Firauna, akiwa na majeshi yake, alifanya juhudi za kuwafuatilia ili kuwazuia na kuwarudisha. Pale Firauna na jeshi lake walipowakaribia Wana wa Israeli, watu walihisi kukosa matumaini wakiwa kati ya bahari upande mmoja na majeshi ya Firauna upande mwingine. Hali hii iliwafanya Wana wa Israeli kumlalamikia Nabii Musa (a.s), wakidhani kwamba hawana njia ya kuokoka.
Baada ya hali hiyo kujiri Mwenyezi Mungu alimpa Nabii Musa (a.s) amri kwa njia ya wahyi kumwagiza kupiga bahari kwa kutumia fimbo yake. Pale Nabii Musa (a.s) alipofanya kama alivyoagizwa, papo hapo bahari ilijigawa sehemu na kufungua njia ya nchi kavu kwa ajili ya Bani Israil. Nabii Musa (a.s) na wafuasi wake waliingia baharini wakipita juu ya ardhi kavu huku maji yakiwa yamesimama pande mbili kama kuta. Mwishowe, Nabii Musa (a.s) na watu wote waliokuwa pamoja naye walivuka bahari salama.
Hata hivyo, Firauna na majeshi yake, walipojaribu kuwafuatilia kwa kupitia njia ileile ya ndani ya bahari, waligharikishwa wote kwa pamoja, na miili yao ikaelea juu ya maji. Huo ukawa ndiyo mwisho na hatima ya Firauna na ukatili wake dhidi wengine.
Wengi wa wafasiri wa Qur’ani wanaamini kuwa; Bahari iliyogawanyika sehemu mbili ilikuwa ni Bahari ya Shamu (Red Sea). Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni, kama vile Tabarsi katika tafsiri yake Majma‘ al-Bayan, wanaamini kuwa tukio hili lilifanyika katika mto Nile badala ya Bahari ya Shamu.
Kukimbia kwa Wana wa Israeli kutoka Nchini Misri na Kufika Baharini
Kwa mujibu wa maelezo yaliyomo katika tafsiri za Qur’ani, Mwenye Ezi Mungu alimwagiza Nabii Musa (a.s) awaongoze Wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri wakati wa usiku, ili kuwaokoa kutokana na mateso na dhulma za Firauna. [1] Agizo hili lilikuwa ni hatua muhimu ya kihistoria ya kuwakomboa Wana wa Israeli kutoka katika utumwa wa muda mrefu wakiwa nchi Misri.
Firauna, baada ya kupokea habari za kuondoka kwao, haraka aliamua chukua hatua ili kukabiliana na suala hilo. Alituma wajumbe wake katika miji mbalimbali ili kuandaa majeshi makubwa kwa lengo la kuwafuatilia na kuwarudisha Wana wa Israeli kwa nguvu. [2] Katika juhudi hizi, Firauna alitumia mbinu za propaganda ili kuwashawishi watu wake kuunga mkono kampeni yake. [3] Aliwaeleza majeshi wake kuwa yenye ni mwenye nguvu na uwezo wa kushinda, huku akiwasifu Wana wa Israeli kama ni kikundi dhaifu, chenye malengo ya kusababisha matatizo katika himaya yake. [4]
Firauna, akiwa ameambatana na majeshi yake, aliwafuatilia Wana wa Israeli kwa lengo la kuwarudisha mjini Misri.[5] Firauna aliwasili eneo walilopo Wana wa Israeli wakati wa kuchomoza jua. Hapo Wana wa Israeli walijikuta wakikabiliwa na hali ngumu: ambapo upande mmoja kulikuwa na bahari, na upande mwingine jeshi la Firauna likiwa linawasogelea kwa kasi. Hali hii ilisababisha hofu kubwa miongoni mwao, wakihisi kwamba wamenaswa bila ya kuwa na njia ya kutoroka. [6]
Hata hivyo, kwa mujibu wa Qur'ani, Nabii Musa (a.s) aliwatuliza kwa maneno ya imani thabiti, akisema: "La hasha! Hakika Mola wangu yu pamoja nami, na hivi karibuni atanionesha njia" (Qur'ani 26:62). [7]
Imeezwa kuwa kauli ya Nabii Musa (a.s) iliyoelezea imani yake thabiti kwa msaada wa Mwenye Ezi Mungu, isemayo: "La hasha! Hakika Mola wangu yu pamoja nami, na hivi karibuni atanionesha njia" (Qur'an 26:62), inahusiana moja kwa moja na ahadi ya Kimungu ya ushindi na kwapa usalama na amani. [8]
Muujiza wa Kugawanyika kwa Bahari na Uokovu wa Wana wa israeli
Kisa chakuokoka kwa Wana wa Israeli na kuangamizwa kwa jeshi la Firauna (Farao) katika bahari ni miongoni mwa visa vilivyo tajwa katika Sura kadhaa za Qur'an. Muujiza huu ulitimia baada ya Mwenye Ezi Mungu kumtuma Nabii Musa (a.s) ili awaokoe Wana Israeli kutoka katika utawala wa dhulma wa Firauna. Kisa hichi kimeelezwa katika Aya mbalimbali za Qur'an, ikiwa ni pamoja na:
- Suratu al-A'raf, Aya ya 136
- Suratu al-Anfal, Aya ya 54
- Suratu al-Isra, Aya ya 103
- Suratu ash-Shu'ara, Aya ya 63 hadi 66
- Suratu az-Zukhruf, Aya ya 55 [9]
Kwa mujibu wa Aya ya 63 ya Suratu ash-Shu'ara, Mwenye Ezi Mungu alimwamuru Nabii Musa (a.s) kutumia fimbo yake na kuigonga bahari kwa fimbo hiyo. [10] Alitakiwa kufanya hivyo ili bahari ichanike nan a kupata njia slama ya nchi kavu itakayowaokoa. Hii ilikuwa sehemu ya muujiza mkubwa wa kimungu ambao ulisababisha bahari kugawanyika, na Wana Israeli walipita salama, huku jeshi la Firauna lilikutana na kifo cha kuzama (kughariki) katika maji. [11]
Baada ya Nabi Musa (a.s) kupiga fimbo yake juu ya maji, muujiza mkubwa ulitokea ambapo bahari ilijitenga na kuacha njia kavu katikati. [12] Kila sehemu iliyojitenga ilionekana kama milima miwili mikubwa ya maji. [13] Hapo Nabii Musa (a.s) Wana wa Israeli wakatembea juu ya ardhi kavu hiyo, [14] huku maji yakiwazunguka kutoka pande mbili. [15] Hatimae Nabii Musa (a.s) na Waisraeli wakavuka salama kupitia njia hiyo, [16] lakini Firauna pamoja na jeshi lake, ambao walikuja kwa lengo la kuwasaka Wana wa Israeli, walijikuta wakiingia kwenye ghadhabu za Mungu. [17] Pale Firauna pamoja na jeshi lake walipokuwa katikati ya njia kavu, maji yalirudi kwa kasi na kuwazunguka, na wote walikufa kwa kuzama katika bahari. [18]
Baadhi ya wafasiri, akiwemo Fadhlu bin Hassan Tabrasi, mfasiri maarufu wa Kishia wa karne ya sita, wamesema kwamba; Baada ya Nabi Musa (a.s) kutumia fimbao yake na kuigonga bahari kupitia fimbo hiyo, muujiza wake ulikuwa ni kufunguka kwa njia kumi na mbili katikati ya maji ya bahari hiyo. Kila njia ikajianisha kwa ajili ya kabila moja ya makabila kumi na mbili ya Bani Israeli, na kila kabila likaweza kuvuka kupitia njia yake maalumu. [19]
Baadhi ya wanazuoni wamesisitiza uwezekano wa kutoke tukio la kuchanika kwa bahari katika nyakati mbali mbali kupitia uwezekano wa kimaumbile, kama vile ilivyojiri kupitia muujiza wa Musa (a.s). Yaani wao wanakusudia kusema kwamba; Hili si jambo lipingikalo kiakili wa kijografia. Mfasiri maarufu wa Shia, aitwaye Makarim Shirazi, anaamini kwamba ikiwa tunakubali kuwepo kwa miujiza, basi si lazima kutoa maelezo ya ziada juu ya mfumo wa maumbile nchi kuhusiana na na tukio hilo. Yeye anaamini kuwa hakuna vikwazo kwa Mungu katika kuyaamuru maji ya bahari kukusanyika sehemu fulani kutokana na mvuto wa mwezi (gravity), kisha kwamba baada ya muda fulani, mvuto huo ukaondolewa, hivyo kuwatengenezea njia Wana wa Israeli, ni miongoni mwa miktadha ya nguvu za Kimungu zinazoweza kushinda sheria za asilia za maumbile ya tabia nchi. [20]
Tukio la Kuzama kwa Firauna na Jeshi Lake
Kuzama kwa Firauna na jeshi lake, ni tukio la kihistoria linaloelezwa ndani ya Qur'ani, tukio ambalo lilitokea baada ya Wana wa Israeli kuvuka kupitia njia ya nchi kavu ilioko kati ya maji yaliyogawanyika. Kuzama kwa Firauna kulijiri yeye na jeshi lake walipojaribu kuwasaka kwa kufuata nyuma yao, ambapo baada ya wao kungia ndani ya njia hiyo, maji yalirudi katika hali yake ya kawaida, na kumuacha Firauna pamoja na wafwasi wake kuzama baharini. [21] Miili ya askari wa Firauna ilielea juu ya maji, na Waisraeli waliona tukio hili kwa macho yao. [22] Tukio hili limetajwa na Qur'ani katika Suratu al-Baqarah, Aya ya 50, Aya isemayo: "Na bahari ilipopasuka kwa ajili yenu na tukakuokoeni na tukawazamisha Mafirauna nanyi mkiwa mnaona." (Qur'an, 2:50) [23]
Katika Aya ya 92 ya Surah Yunus, kuna ibara isemayo: “نُنَجِّیکَ بِبَدَنِکَ” "Tutauokowa mwili wako". Ibahii unahusishwa moja kwa moja na Firauna, na ni sehemu muhimu ya maelezo ya kifo chake. [24] Wafasiri mbali mbali maarufu wamesema kwamba; Kipengele hichi kinakusudia mwili wa Firauna. [25] Hii ina maana ya kwamba, baada ya kifo cha Firauna, Mwenye Ezi Mungu ailutoa mwili wake kutoka majini na kuwekwa hadharani mbele ya umma, [26] ili watu wauone mwili huo, [27] na mafuzo juu ya kujihadhari na nguvu za Kimungu. Huo ulikuwa ni muujiza wa Mwenye Ezi Mungu, wenye lengo la kuwaonyesha watu ukweli wa matukio hayo. Wafasiri wengine pia wamesema kwamba; Wengine wamesema kwamba; Neno Badanika / بِبَدَنِکَ haliashirii mwili wake, bali ni vazi lake makhususi la kivita alilokuwa akijilinda nalo. Kwa hiyo mwenye Ezi Mungu alimtoa Firauna kutoka majini yeye pamoja na vazi lake maalum ili ajulikane. Wafasiri fulani wameona hilo lilikuwa ni somo kwa Wana wa Israeli, ambao hawakukubali habari za kifo cha Firauna. [29]
Je ni Mto Nile au Bahari Nyekundu (Red Sea)?
Katika Qur'ani, maji yaliyochanywa kwa ajili ya Wana wa Israeli yanatajwa kwa majina mawili: "Yam" kwa maana ya bari [30] na "Bahr" pia huwa na maana ya bahari [31] au maji makubwa. [33] Mfasiri wa Kishia, Mohammad Jawad Mughniya, anaamini kwamba; Wengi wa wafasiri wa Qur’ani wanaamini kuwa maji yaliyochanya kwa ajili ya Wana wa Israeli na ambayo na aliyozama ndani yake Firauna, ni maji ya Bahari, inajulikana kwa jina la bahari Nyekundu (Red Sea) katika zama zetu za leo. [34] Hata hivyo, baadhi ya wafasiri kama vile Tabarsi katika katika kitabu Majal al-Bayan, wanadhani kwamba neno hili linaweza kumaanisha Mto Nile. [35]
Katika Qur'ani, neno "Yam" pia linapotumika likiashiria maji aliyowekwa Nabii Musa (a.s) ndani yake na mama yake pale alipokuwa mtoto Musa (a.s). Ambapo mama yake alimweka ndani ya sanduku na kulitia sanduku hili ndani ya maji, ambayo yameelezewa kuwa ni maji ya Mto Nile. [36]
Maandiko Kuhusiana na Waisraeli baada ya Kuwekwa Akti Wakiwa Baina ya bahari na jeshi la Firauna