Nenda kwa yaliyomo

Uzuri na Ubaya

Kutoka wikishia

Uzuri na Ubaya (Kiarabu: الحُسن و القُبح) Ni Suala linalohusiana na masuala ya elimu ya theolojia. Muqtadha wake hujadili kuwa je kiasilia, matendo kama matendo huwa yanasifika kwa sifa ya uzuri au ubaya, au uzuri na ubaya wake hutegemea amri za Mungu tu? Yani, chochote kile ambacho Mungu ameagiza huhisabiwa kuwa ni kizuri kutokana na hilo, na chochote alichokataza huhisabiwa kuwa ni kibaya kutokana na katazo hilo la MUngu. Wanazuoni wa Kiislamu wamechunguza kwa kina suala hili na kulipa uzito mkubwa katika tafiti zao mbali mbali.

Kuna tofauti za kimitazamo miongoni mwa wanafikra wa Kiislamu katika kujadili suala hili muhimu la uzuri na ubaya wa matendo. Wafuasi wa madhehebu ya Shia na Mu'tazila wanaamini kwamba; kwamba ubaya wa matendo hafahamika kupitia ufahamu wa akili, dhana ambayo inajulikana kwa jina la uzuri na ubaya wa kiakili (الحُسن و القُبح العقلیین). Wao wanaona kuwa thamani ya matendo inahusiana na sifa zake za kiasili ambazo hupelekea matendo hayo kusifika kwa sifa za uzuri au ubaya, na kwamba akili ya mwanadamu inaweza kutambua uzuri au ubaya wa baadhi ya matendo fulani bila kusubiri amri za Mungu. Kwa upande mwingine, wafuasi wa Ash’ariyya, wanaamini kuwa uzuri na ubaya hutegemea sheria za Kiungu peke yake. Kwao, kiasili matendo hayana aina ya sifa ya uzuri au ubaya ndani yake; bali kile ambacho Mungu amekiamuru huwa ni kizuri (hassan), na kile ambacho amekataza huwa ni kibaya (qabih).

Pia, mjadala huu kuhusiana na uzuri na ubaya wa matendo umeingia katika fani ya usuli al-fiqh (misingi ya fiqhi). Amabapo wataalamu wa fani hii hujadili suala hili kwa kusema ya kwamba; endapo uzuri na ubaya wa matendo utaweza kuthibitishwa  kiakili, basi hiyo itapelekea akili kuhisabiwa kuwa ni moja ya vyanzo vinne vya kutambua hukumu za kisheria. Nayo ndiyo dhana inayokubaliwa na wanazuoni wa Kishia wa fani ya usuli al-fiqh.

Nafasi ya Suala la Uzuri na Ubaya wa Matendo

Suala la uzuri na ubaya (الحُسن و القُبح), ni moja wapo ya masuala muhimu katika taaluma ya elimu ya fani ya elmu al-kalamu (teolojia ya Kiislamu), na inachukuliwa kuwa ndiyo msingi wa nadharia nyingi ndani ya taaluma hiyo. [1] Wanazuoni wa Kiislamu wamelipa uzito mkubwa suala la uzuri na ubaya wa matende, pamoja kulitafiti kwa tafiti mbali mbali suala hili. [2] Katika maandiko ya kikalamu (kitheolojia), dhana hii inachunguzwa na kutafitiwa sambamba na masuala yanayohuisana na muktadha wa matendo ya Mungu, na hutumika katika kuthibitisha dhana ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu. [3]

Kama alivyoeleza Ja'far Subhani, dhana hii inayohusiana na uzuri na ubaya (matendo), ina umuhimu mkubwa pia katika taaluma nyingine mbali mbali ikiwemo taaluma ya maadili pamoja na taaluma ya usuli al-fiqhi, Katika taaluma ya maadili, kukubali uzuri na ubaya wa matendo kiakili, kunamaanisha kuthibitisha kwamba thamani za maadili (matendo) ni za kudumu, asilia na zisizo badilika. Kutokukubali dhana hiyo, kwa upande mwingine, kunaweza kuashiria kukubali kwamba maadili (matendo), ni miongoni mwa masuala linganishi au tegemezi, yaani hutegemea jinsi mtu anavyo yaona kulingana na itikadi yake, na yanaweza kubadilika kulingana na hali zilivyo. [5]

Katika fani ya usuli al-fiqhi, suala hili hujadiliwa katika mlango unaohusiana na muktadha wa yanayolazimiana na kiakili (Mulaazimaat ‘Aqliyah مُلازمات عقلیه), ambapo kuthibitishwa kwa uzuri na ubaya wa matendo kiakili, kunapelekea akili kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya kutambua hukumu za kisheria (za kifi-hi). [6]

Mada ya uzuri na ubaya wa matendo, imejadiliwa kwa undani katika vitabu vya fani ya elmu al-kalamu (theolojia ya Kiislamu), [7] vikiwemo vtabu vya usuli al-fiq-hi vya upande wa madhehebu ya Shia pamoja na Sunni. [8]

Swali Kuu Kuhusiana na Uzuri na Ubaya wa Matendo

Mjadala wa uzuri (husn) na ubaya (qubh) wa matendo, unahusiana na msingi au kipimo asili cha wa kupimia uzuri au ubaya wa matendo mbali mbali. Swali kuu ni kwamba: Je, hivi matendo yana uzuri na ubaya wa kweli na wa kiasili ndani yake, au dhana hizi ni za mlinganisho, au kwa lugha nyengine; ni dhana linganishi na tegemezi tu, na kwamba kila kinachoamriwa na Mwenye Ezi Mungu huwa ni kizuri (hasan), huku kila kinachokatazwa na Mwenye Ezi Mungu kikichukuliwa kuwa kibaya (qabih)? [9]

Wafwasi wa mtazamo wa mwanzo, usemao kwamba; uzuri na ubaya wa matendo unahusiana moja kwa mona na sifa asili na za kweli juu ya matendo, wamepelekea dhana hii kutambuliwa kwa jina la uzuri na ubaya wa kiakili au wa kiasili (husn wa qubh al-'aqliyyain au al-dhatiyyain). Ama jina maarufu la mtazamo wa pili kuhusiana na dhana hii, usemao kwamba; uzuri au ubaya wa matendo mbali mbali hutegemea tu amri za kisheria, ni; uzuri na ubaya wa kisheria wa matendo (husn wa qubh shari'iyyaini). [10]

Tofauti za Maoni Kuhusu Uzuri na Ubaya wa Matendo

Wanazuoni wa Kiislamu wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya iwapo uzuri (husn) na ubaya (qubh) ni wa kiakili au wa kisheria. Katika hili: Wafuasi wa madhehebu ya Kishia [11] na madhehebu ya Mu'tazila [12] wanakubaliana kuwa uzuri na ubaya wa matendo unahusiana na sifa aslia za matendo, ambao kiistilahi huitwa; uzuri na ubaya wa kiakili au wa kiasili (husn wa qubh al-'aqliyyain au al-dhatiyyain). Ash'ariyya [13], kwa upande mwingine, wanaamini kuwa uzuri na ubaya si sifa asilia bali sifa hizo zinatokana na sheria. ambapo kiistihahi nadhari huitwa; uzuri na ubaya wa kisheria wa matendo (husn wa qubh shari'iyyaini).

Kwa mujibu wa wanateolojia wa Kishia na Mu'tazila ni kwamba; Kiasili matendo hugawika katika makundi mawili; mazuri (hasan) na mabaya (qabih) bila ya kuzingatia hukumu za Mungu. Wao wanasema kuwa; akili ya mwanadamu inaweza kutambua uzuri au ubaya wa baadhi ya matendo bila y ahata kusubiri maelezo ya kisheria. [14]

Ash'ariyya wanashikilia mtazamo usemao kuwa; Uzuri na ubaya wa matendo hutegemea na hueleweka kupitia sheria za Mungu tu. [15] Kwa mujibu wa mtazamo huu, matendo hayana asili wa sifa yoyote ile ya uzuri au ubaya ndani yake. Kwa hiyo kitu chochote ambacho Mungu amekiagiza huwa ni kizuri (hasan), na chochote kile alichokikataza huhisabika kuwa ni kibaya (qabih). Hivyo bila mwongozo wa kisheria, hakuna kitakachoweza kutambuliwa kuwa kizuri au kibaya. [16]

Asili na Chimbuko Lake

Inasemekana kwamba; tokea zama za kabla ya kukuja kwa Uislamu, kulikuwa na mijadala kuhusiana na uzuri na ubaya wa matendo, iliyokuwa ikiendelea katika dini nyingine, [17] na pia lililkuwa ni suala linalotafitiwa na baadhi ya wanafikra pamoja na wanafalsafa wa Kigiriki. [18] Hata hivyo, Waislamu walilipa umuhimu zaidi suala hili katika tafiti zao mbali mbali. [19] Mjadala wa uzuri na ubaya wa matendo, ulianza kujitokeza kama suala lenye dhana rasmi katika karne ya pili Hijria, ambalo lilikuwa ni tunda lililozailwa kupitia juhudi za Madhehebu ya Mu‘tazila. [20] Baada ya hapo, Ash‘ariyya, ambao walipinga dhana ya uzuri na ubaya wa matendo kiakili, walijitosa kwenye mjadala huu na kuanzisha hoja juu ya uzuri na ubaya wa kisheria. [21]

Hoja za Wanaounga Mkono Uzuri na Ubaya wa Kiakili

Baadhi ya hoja za wanazuoni wa Kishia za kuthibitisha dhana ya uzuri na ubaya wa kiakili ni kama ifuatavyo:

  • Uzuri na ubaya wa kiakili ni jambo la dhahiri na ni asili ya kimaumbile, Akili ya mwanadamu bila kutegemea sheria za kidini inaweza kuhukumu juu ya uzuri wa wema na ubaya wa dhuluma. Kwa mfano, tunaelewa kwa uhakika na yakini kamaili ya kwamba; kuwtendea wema wengine, ni jambo zuri, na huwa tunamsifu mtendaji wake. Vivyo hivyo, tunahukumu kwamba kufanya uovu ni jambo baya, na tunamkemea mfanyaji wake. [22]
  • Kutegemea akili ili kuelewa uzuri na ubaya, Ikiwa akili haiwezi kuelewa uzuri na ubaya wa matendo, basi hata kupitia sheria za dini hatuwezi kuelewa suala hilo. Kwa mfano, ikiwa akili haifahamu kwamba kusema uongo ni jambo baya, basi inaweza kufikiri kuwa Mwenye Ezi Mungu anaweza kusema uongo. Katika hali hii, hata kama Mungu atasema kuwa jambo fulani ni zuri au baya, hatutapata uhakika wa kweli kuhusiana na jambo hilo. [23]
  • Thibitisho la haki ya dini ya Mungu, Ikiwa uzurina ubaya wa matendo hauwezi kueleweka kupitia akili, basi haiwezekani kuthibitisha ukweli wa dini ya Mwenye Ezi Mungu. Katika hali hiyo, kutakuwa hakuna baya kwa Mungu kuwawezesha wale ambo si manabii kuja na miujiza fulani. Hii inamaanisha kuwa; sisi hatuwezi kuthibitisha unabii wa nabii yeyote yule kupitia miujiza yake, na kwa hivyo, haitawezekana kuthibitisha dini yoyote ile, na kudai kuwa dini fulani ni dini ya haki itokayo kwa Mungu mwenyewe. [24]

Hoja za Wanaounga Mkono Uzuri na Ubaya wa Kisheria

Baadhi ya hoja zilizotolewa na Ash‘ariyya kuthibitisha kwamba uzuri na ubaya wa matendo ni wa kisheria (hutegemea mgongo wa sheria), ni kama ifuatavyo:

  • Kutokuwepo kwa ubaya wa uongo kwa hali zote, Ikiwa kusema uongo ni jambo baya kiasili (bila kutegemea sheria za dini), hiyo itamaanisha kuwa kila uongo ni mbaya. Hata hivyo, yaeleweka dhahiri kwamba si kila uongo ni mbaya. Kwa mfano, kusema uongo ili kuokoa maisha ya nabii hakuchukuliwi kuwa ni jambo baya. [25]
  • Mfano wa dhamira ya kutenda kosa la jinai, fikiria kwamba; kuna mtu fulani aliye ahidi kumuua mwingine kesho yake. Iwapo mtu huyo atafanya mauaji hayo, kitendo hicho kitahisabiwa kuwa ni kitendo kibaya, lakini ikiwa hatatekeleza dhamira hiyo, basi huyo atakuwa ametoa ahadi ya uongo, ambayo kwa msingi wetu na kwa msigi wa wale wanaounga mkono uzuri na ubaya wa kiakili, kila uongo huhisabiwa kuwa ni mbaya. Kwa kuwa sote tunakubaliana kuwa si sawa kwa mtu huyo kutekeleza mauaji hayo, hii inathibitisha kwamba; si kweli kwamba kila uongo huwa ni mbaya. [26]
  • Madai ya kuwajibika kwa Mungu, wale wanaounga mkono uzuri na ubaya wa matendo wa kiakili, wanadai kwamba Mwenye Ezi Mungu analazimika au anawajibika kutofanya matendo mabaya. Kwa mfano, wao wanasema kuwa; iwapo mwanadamu atamshukuru Mungu, basi ni wajibu kwa Mwenye Ezi Mungu kumpa thawabu mtu huyo. ila ni jambo la dhahiri na la wazi kabisa, kwamba haiwezikani jambo lolote lile kuwa ni wajibu kutendwa na Mwenye Ezi Mungu, kwa kuwa kila wajibu huhitaji mlazimisha wa wajibu huo na kuufanya uwe ni jambo la lazima, ila hakuna kiumbe yeyote yule aliye juu ya Mwenye Ezi Mungu, ambaye anaweza kumlazimisha au kumuwajibisha Mungu kufanya jambo fulani kwa lazima. [27]

Biliografia (Orodha ya Vitabu Kuhusiana na Mada Husika)

Wanazuoni wa Kishia na Kisunni wamejadili suala la uzuri na ubaya wa matendo katika maandiko yao ya kielimu ya itikadi [28] na misingi ya fiqhi [29]. Hata hivyo, maandiko huru pia yameandikwa kuhusu mada hii. Baadhi ya maandiko hayo ni kama ifuatavyo:

  • Husne wa Qubhe Aqli au Payeh-haye Akhlaqe Jawidan Uzuri na Ubaya wa Kiakili au Misingi ya Maadili ya Milele, kilichoandikwa na Ja‘afar Subhani.
  • Husne wa Qubhe Zati wa Aqli az Manzar-e Danishmandane Islami, "Uzuri na Ubaya wa Asili na Kiakili kwa Mtazamo wa Wanazuoni wa Kiislamu, kazi ya Hadi Wahdani-Far.
  • Qaedeye Kalamiy Husnu va Qubhe Aqli Kanuni ya Kitheolojia ya Uzuri na Ubaya wa Matendo Kiakili. Kitabu kilichoandikwa na Reza Berenjkar na Mehdi Nusratian.
  • Husne wa Qubhe Zati wa Aqli az Manzare Riwayate Islami Uzuri na Ubaya wa Asili na Kiakili kwa Mtazamo wa Hadithi za Kiislamu, kitabu kilichoandikwa na Hadi Wahdanifar na Zakiya-Beigum Husseini.

Mada Zinazo Fungamana

Rejea

Vyanzo