Misingi Mikuu ya Kimadhehebu

Kutoka wikishia

Jambo la lazima na la dharura (muhimu) kimadhehebu ni hukumu na itikadi ambazo wafuasi wa madhehebu fulani wanalitambua hilo kuwa ni sehemu ya madhehebu na dini yao. Kwa mujibu wa nadharia na mtazamo wa Maulamaa wengi wa dini ni kwamba, kukana jambo la lazima na la dharura katika madhehebu kunamtoa mtu katika madhehebu husika lakini hakumtoi katika dini. Miongoni mwa mambo ya dharura na ya lazima ya madhehebu ya Shia Imamiya ni kuamini Uimamu wa Maimamu 12 na kwamba, ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Utambuzi wa istilahi

Dharuri maana yake ni jambo la lazima na lisilo na shaka na limetumika katika istilahi tatu za kifiq’h: Dharuri dini (jambo la lazima kidini), dharuri madh’habi (jambo la lazima kimadhehebu) na dharuri Fiq’h (jambo la lazima kifikihi). [1]

Jambo la lazima (dharura) kidini

Makala kuu: Jambo la lazima kidini

Jambo la dharura na la lazima kidini( dini ya Uislamu) ni hukumu na itikadi ambazo makundi na madhehebu ya Kiislamu yanazitambua kwa uwazi kabisa kwamba, ni sehemu ya dini kama vile kufufuliwa siku ya Kiyama na Sala kuwa ni wajibu. Kukana jambo la lazima katika dini kimsingi ni kuyaona maneno ya Mwenyezi Mungu au Mtume (s.a.w.w) kwamba, ni urongo na hilo ni moja ya mambo yanayomfanya mtu aritadi na kutoka katika Uislamu.

Jambo la lazima kimadhehebu

Jambo la lazima na la dharura (muhimu) kimadhehebu ni hukumu na itikadi ambazo wafuasi wa madhehebu fulani wanalitambua hilo kuwa ni sehemu ya madhehebu na dini yao. Kwa kuzingatia kwamba, wafuasi wa kila madhehebu wanatambua kuwa madhehebu yao ni ya haki na dini ya kweli, mafakihi kama Sabih al-Jawahir anaamini kwamba, jambo la lazima la madhehebu kwa watu hawa ni mithili ya dharura na lazima ya kidini. [2] Jambo la lazima kifiq’hi

Jambo la lazima kifiq’h limebainishwa katika aina aina mbili: [3]

1. Mambo ambayo mafakihi wote wamefikia ijmaa na wanayakubali. 2. Mambo ambayo ni nguzo ya fiq’h na fiq’h haiwezi kupatikana bila hayo.

Mifano Miongoni mwa mambo ya dharura na ya lazima kimadhehebu kwa upande wa dhehebu la Shia Imamiya ni kuamini Uimamu na kwamba, Maimamu ni Maasumu (hawatendi dhambi). [4] Miongoni mwa dharura na mambo mengine ya lazima ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ambayo tunaweza kuashiria hapa ni: Kuamini kwamba, "Hayya 'Alaa Khair Al-Amal' (Fanyeni haraka na hima kuelekea kwenye amali bora) ni sehemu ya adhana na kwamba, ndoa ya Muta’a (muda) ni halali. [5]

Hukumu ya kifiq’h ya kukana jambo la lazima kimadhehebu

Akthari ya mafakihi wanaamini kwamba, kutokubali na kukana moja ya dharura na jambo la lazima katika madhehebu ya Shia, kunamfanya mtu atoke katika madhehebu hii. [6] Kwa maana kwamba, kwa mfano endapo atakana kwamba, mutaa sio ndoa ya halali, hawezi kubakia kuwa Shia. Mkabala na wao kuna mafakihi kama Sahib Hadaiq yeye anaamini kwamba, kukana jambo la lazima katika madhehebu kunamfanya mhusika kuritadi na kutoka katika dini; [7] baadhi ya wengine mithili ya Sahib al-Jawahir anaamini kwamba, kukana jambo la dharura na la lazima katika madhehebu kwa mtu ambaye anayakubali madhehebu husika ni mithili ya kukana dharura ya dini na hilo linamfanya aritadi na kutoka katika Uislamu. [8] Baadhi ya wengine (mithili ya Seyyid Abdul-A’la al-Sabziwari) wanaamini kwamba, kukana jambo la lazima na la dharura katika madhehebu humtoa mtu katika dini pale tu mtu atakapokana risala (Utume) au tawhidi. [9][10].