Kuwakufurisha Ahlu al-Qiblah (Waislamu)

Kutoka wikishia

Kuwakufurisha Ahlu al-Qiblah au kuwakufurisha Waislamu (Kiarabu: التكفير (تكفير أهل القبلة)): Humaanisha kitendo cha kundi fulani la Waislamu kuwahisabu Waislamu wa kundi au mmoja kati yao kuwa ni kafiri. Ambapo natija yake huwa ni kujuzisha kuwaua na kutaifisha mali zao baada ya kuwapachika sifa hiyo ya ukafiri. Mawahabi kutokana na welewe maalumu walionao kuhusiana na dhana ya tawhid, kuzuru makaburi na kutawasali, imepelekea wao kuwakufurisha Waislamu wengine ambao wamekhitalifiana nao kinadharia juu ya dhana tatu hizo.

Wengi miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba mpaka baina ya Uislamu na ukafiri ni kutamka shahada mbili, na wala hawajuzishi kuwakufurisha wafuasi wa madhehebu ya Kiislamu na kuwaita makafiri. Hata hivyo, katika historia ya Uislamu, kumekuwa na Waislamu ambao wamewatuhumu wafuasi wa madhehebu pinzani kuwa ni makafiri. Miongoni mwa matukio yaliorikodiwa kuhusiana na matendo haya ni: Kukufurishwa kwa Imam Ali (a.s) katika tukio la mazungumzo ya kuleta amani baina yake na Muawia katika vita vya Siffin, kulikofanywa na khawarij (waasi ), na kukufurishwa kwa watu wa ridda (اهل رِدّه) wakati wa utawala wa Khalifa wa kwanza (Abu Bakar) ni mifano ya mwanzo iliyo tendeka katika kuwakufurisha Waislamu. Baada ya hapo, mawazo haya katika zama mbali mbali yalijitokeza miongoni mwa wafuasi wa madhehebu tofauti ya Kiislamu, jambo ambalo lilipelekea watu wengi kuuawa chini ya kivuli cha fitna hiyo. Hata hivyo, suala la kukufurishana na kuitana makafiri halikuwa tu ndani ya mzunguko wa madhehebu mbali mbali, bali wakati mwingine hata baadhi ya wanazuoni, wanafalsafa walioko katika dhehebu moja pia walionekana kukufurishana wenyewe kwa wenyewe. Katika fitna iliotokea kuhusiana na suala la uumbwaji wa Qur'ani, wafuasi wa pande zote mbili walikuwa ni wafuasi wa madhehebu ya Kisunni walikuwa wakikufurishana kutokana na tofauti zao za kinadharia. Katika fitna hii, wale walioamini kuwa Qur’ani ni kiumbe cha Mungu, waliwakufurisha walioamini kuwa Qur’ani ni ya tangu ambayo utangu wake ni sawa na utangu wa Mwenye Ezi Mungu, pia hawa waliokufurishwa nao wakawa wanawakufurisha wale walioamini kuwa Qur’ani si ya tangu na tangu bali ni kama viumbe wengine, yaani nayo imeumbwa.

Baada ya kuanzishwa kwa Kundi la Kiwahabi, kukufurishwa kwa Waislamu kumeonekana kuongezeka. Pia, chini ya ushawishi wa mawazo ya Wahhabi na kwa msaada wao, vikundi kama vile ISIS vimeundwa, vikundi ambavyo vianaonekana kushika kasi zaidi katika kuwatuhumu Waislamu kwa ukariri, hasa Waislamu wa mrengo wa Kishia.

Kuna kazi nyingi zilizoandikwa kuhusiana na masuala ya kuwahukumu Waislamu kwa ukafiri, ambazo nyingi zake zimeandikwa kwa lengo la kukosoa mawazo haya. Pia, mikutano kadhaa imefanyika kukosoa itikadi za kuwahumu Waislamu kwa ukafiri na kushikamana na harakati za kigaidi.

Umuhimu na uzito wa kuwahukumu Waislamu kwa ukafiri

Kuwahukumu Waislamu kwa ukafiri; Ni suala linalofungamana na masuala ya kisheria (kifiqhi) na kitheolojia ambalo limekuwa na uzito mkubwa katika historia ya Uislamu. Kuhukumiwa kwa ukafiri kwa mtu au kikundi cha Waislamu kumesababisha kuhalalisha umwagaji damu na utaifishaji mali za Waislamu hao, na hivyo kusababisha vita, mauaji na watu wengi kukosa mali pa kukaa. [1] Pia, kuwapachika sifa za ukafiri baadhi ya wafuasi wa madhehebu fulani ya Kiislamu kumesababisha uharibifu wa baadhi ya maeneo na majengo yenye heshima na taadhima mbele yao. [2] Mnamo karne za hivi karibuni, kutokana na kuenea kwa mawazo ya kigaidi na kuhukumiwa kwa ukafiri kwa baadhi ya Waislamu kulikosababishwa na udhamini wa viongozi na wafuasi wa mawazo haya. Pia katika kipindi mijadala, mikutano, tafiti na vitabu vingi vimeandinkwa kuhusiana na suala hili la kuwahukumu Waislamu kwa ukafiri.

Ufafanuzi wa dhana na aina za ukafirishaji

Kuhukumiwa kwa ukafiri kunamaanisha kule kumwita au kumpachika Mwislamu jina ukafiri au kuwapa Waislamu sifa ya ukafiri. Ukafiri unaweza kugawanywa katika aina mbili: ukafiri wa kumkufurisha Mwislamu kifiqhi na kiitikadi. Kutumia aina yoyote kati ya aina mbili hizi hupelekea matokeo maalumu dhidi ya yule Mwislamu aliyetuhumiwa kwa sifa hiyo ya ukafiri. Kama tulivyo ashiria ya kwamba mtu anaweza kupewa moja kati sifa mbili za ukafiri ambazo ni:

  • Ukafiri wa kifiqhi au ukafiri wa dhahiri ambao unamaanisha kutoka nje ya dini ya Kiislamu. Kwa hivyo, Mwislamu aliyehukumiwa kuwa ukafiri wa kifiqhi huamiliwa kama anavyo amiliwa kafiri.
  • Ukafiri wa kiitikadi au wa kiundani ambao humaanisha kutoka nje ya imani, sio Uislamu. Kwa hivyo, Mwislamu aliyehukumiwa kuwa ukafiri wa kiitikadi au wa kiundani huamiliwa kama anavyo amiliwa Muislamu, sio kafiri, yaani yeye huamiliwa kama vile anavyo amiliwa mnafiki ambaye kwa kidhahiri ni Mwislamu lakini kiundani hana imani. [6] Kulingana na maelezo ya Imam Khomeini, ni kwamba; Hadithi zinapatikana katika baadhi ya vyanzo vya Shia, ambazo zinaashiria ukafiri wa wapinzani wa madhehebu haya, ikiwa zitakuwa ni zenye kukubalika, zitakuwa zinahusiana na ukafiri wa kiitikadi. [7]

Makatazo juu ya kuwakufurisha Ahlu al-Qibla (Waislamu)

Kwa mujibu wa fat'wa ya wanazuoni wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu, si halali kuwakufurisha Waislamu, bali tendo hili ni miongoni mwa makosa ambayo mtendaji wake yabidi kuadhibiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yake. [8]Kwa mujibu wa itikadi za wanachuoni, mpaka uliopo baina ya kafiri na Muislamu ni kutamka shahada mbili na kuamini siku ya malipo (Kiama). [9]Kwa hivyo, wanachuoni wameepuka kuwakufurisha wafuasi wa madhehebu mbalimbali, hata kama baadhi ya itikadi zao haziko sawa. [10]

Historia ya kukufurishana

Historia ya kukufurishana baina ya Waislamu inarudi katika karne ya kwanza Hijiria, baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w). Katika utawala wa Abu Bakar, kikundi cha Waislamu waliopinga ukhalifa wa Abu Bakar waliitwa makafiri na waritadi, kisha kikundi cha Waislamu kikatoka kwenda kupigana nao. Vita hivi vinajulikana kwa jina la vita vya riddah. [11] Kulingana na maelezo ya Rasul Ja'afariyan, mtafiti wa historia ya Kiislamu (aliye zaliwa mwaka 1343 Shamsia); miongoni mwa watu wa ridda, kulikuwa na watu maarufu, kama vile Malik bin Nuwayra ambao walikuwa ni miongoni mwa Waislamu waliokuwa wakisimamisha sala, ila walikuwa hawakubaliani na ukhalifa wa Abu Bakar, na badala yake walikuwa wakitaka utawala wa Ahlul Bayt wa Mtume (s.a.w.w). [12] Kwa hivyo walikataa kabisa kutoa zaka na kumkabidhi khalifa wa wakati huo, na hilo ndilo lilipelekea wao kuitwa makafiri na waritadi na hatimaye kuuawa. [13]

Katika utawala wa Imam Ali (a.s), waasi (Makhawarij) walimtangaza Imam Ali (a.s) kuwa kafiri kwa sababu ya kukubaliana fikra ya Tahkim (kufanyika kwa mazungumzo ya suluhu baina yake na Muawia) iliyobuniwa na Amru Aas. [14] Hiyo ikawa ndiyo sababu ya waokukataa kumuunga mkono katika vita vyake dhidi ya Muawiya bin Abi Sufyan. [15] Baada ya hapo waasi hao walianzisha vita vya Nahrawan dhidi yake. [16]

Pia, kama alivyoripoti Ayatullah Jafar Sobhani, mufti wa Kishia (aliyezaliwa mwaka wa 1909 Shamsia), katika kitabu chake Buhuthu fil Milali wa al-Nihali (بحوث فی الملل و النحل), ya kwamba; katika fitna za mzozo juu ya itikadi ya uumbwaji wa Qur'an, kila mmoja wa wanaounga mkono nadharia ya uumbwaji wa Qur’ani na nadharia ya utangu wa Qur'an, huku wote wakiwa ni kutoka madhehebu ya Sunni, walitangaza wafuasi wa nadharia nyingine kuwa makafiri. [17] Tangu wakati huo, vikundi vya Waislamu binafsi au kundi fulani miongoni mwao limeonekana kuitwa makafiri na watu fulani. Katika karne za hivi karibuni, na baada kuenea kwa mawazo ya Kisalafi na Kiwahabi, Waislamu, hasa Mashia, wameonekana kutangazwa kuwa ni makafiri na wafuasi wenye fikra za Kiwahabi.

Motisha wa vichochezi

Kuwakufurisha Waislamu kumefanyika kupitia vichochezi tofauti, ikiwa ni pamoja na:

  • Kutokuelewa na kuwa na tafsiri zisizo sawa juu mafundisho ya kidini: Kwa mfano, Makhawariji walipinga maamuzi ya kuchukuwa hatua za kufanya mazungumzo ya amani kati ya Ali (a.s) na Muawia katika vita vya Siffin, jambo ambalo lilipelekea kumchukulia Imam Ali (a.s) kuwa kafiri. Wao lifikia uamuzi huo kutokana na ufahamu maalumu waliokuwa nao juu ya tafsiri ya Aya isemayo: ((لَا حُكْمَ إِلَّا لِله ; Hakuna hukumu (inayostahiki kufuatwa) ila ya Mwenyezi Mungu peke yake)). [18] Mawahabi pia nao wanawahukumu wengi miongoni mwa Waislamu kuwa ni makafiri, hasa Mashia, hii inatokana ule welewa wao juu ya mafunzo ya tawhidi, dhana ya shirki, kuzuru makaburi, kutafuta baraka kutoka wa watu watukufu, na tawassul (kutawasali). [19] Muhammad bin Abdul-Wahhab, mwanzilishi wa Uwahabi (aliyafariki mwaka 1206 Hijiria), anaona kuwa damu ya wenye imani kama hizo ni halali na amejuzisha kuuawa kwao. Msimamo wa Muhammad bin Abdul-Wahhab ni mkali zaidi kwa Mashia, na kwa mtazamo wake Mashia moja kwa moja ni makafiri. [20]
  • Nadharia za kiitikadi: Makhawaji waliamini kwamba mtu yeyote aliyefanya dhambi kubwa ni kafiri. [21] Mtazamo wao huo umetegemea kwenye Aya isemayo: ((وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ; Na wowote wale wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenye Ezi Mungu, basi hao ndio makafiri)). [22] [23] Lakini kwa mtazamo wa Waislamu walio wengi, ni kwamba; kufanya dhambi kubwa hakuwezi kumtoa mtu katika dini ya Kiislamu, bali kinamtoa katika imani yake. Kwa hivyo, mtu anayefanya dhambi kubwa anakuwa fasiki, na haipelekei yeye kuwa kafiri. [24] Katika fina juu ya dhana ya uumbwaji wa Qur'ani, Abû 'Alî al-Ash'ari [25] na Ahmad ibn Hanbal [26] walidai kuwa wale wanaoamini kwamba Qur'ani imeubwa ni makafiri, huku Mu'tazilah nao wakidai kwamba wale wanaoamini kwamba Qur'ani ni haikuumbwa (ya tangu na tangu) ni makafiri. [27] Katika Hadithi za Shia, Maghulati (watu ambao walizidisha na kutia chumvi katika kuwasifu Maimamu Maasumina), na wanao amini imani ya tafwiidh (itikadi ya kwamba, matendo ya mwanadamu ni matendo yake mwenyewe yasio na aina yoyote ile fumano baina yake na Mola wake) wamehukumiwa na kuitwa makafiri. [28]
  • Ukichwamchungwa, usugu na ugabuzi wa kimadhehebu: Kwa mujibu wa ripoti za kihistoria, katika baadhi ya vipindi, wafuasi wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu wamekuwa wakiwakufurisha wafuasi wa madhehebu mengine. Kwa mfano, katika karne ya nane Hijiria, wafuasi wa madhehebu ya Sunni waliwakufurisha wasuasi wa madhehebu ya Hanbali kutokana na matendo ya Ibn Taymiyyah (ambaye ni mmoja wa wanazuoni wao), na kwa upande mwingine, Ibn Haatim al-Hanbali aliwakufurisha Waislamu wote (isipokuwa Mawahabali tu). [29]Pia, unyanyasaji huu wa kuitana makafiri umeonekeana kutokea kwa wafuasi wa Sunni dhidi ya Mashia na kinyume chake pia (Mashia dhidi ya Masunni). Ibn Jibreen, mufti wa Kiwahabi, amewahisabu Mashia kuwa ni makafiri kwa kuwahusisha na imani mbali mbali, kama vile; kupotosha Qur'ani, kuwachukulia wengi wa Maswahaba kuwa ni makafiri, kuwachukulia Waislamu wa Kisunni kuwa ni najisi, na kumtukuza Ali (a.s) pamoja na watoto wake, kwa kwapa sifa zilizopindukia mipaka. [30] Hata hivyo, Mashia hawana imani kama hizo. [31] Na karibu wanazuoni wote wa Shia na Sunni wanaamini kwamba; wafuasi wa madhehebu mengine si makafiri [31], na kwamba ikiwa kitu kama katika vyanzo fulani, hiyo itakuwa na maana ya ukafiri wa kitikadi. [32]
  • Maudhui za kifalsafa na kiirfani (usufi wa Kishia): Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wameonekana kuwakufurisha wanaflsafa na wanairfani. Kwa mfano, Al-Ghazali katika kitabu chake Tahāfut al-Falāsifah, aliwaona wanafalsafa kuwa ni makafiri. [33] Pia, kulingana maelezo ya Sayyid Muhammad Bāqir Khānsārī (aliyafariki mwka 1313 Hijiria), kikundi cha wanazuoni kifiqhi walimwona Mulla Sadrā kuwa ni kafiri kwa sababu ya maneno yake ambayo hayakuendana na dhahiri sheria za dini. [34]

Pia, fitina za serikali ili kubaki madarakani na njama za maadui wa Uislamu zimeonekana kuwa miongoni mwa mazingira na sababu nyingine za kuenea kwa wazo la kuhuwakumu Waislamu wengine kuwa ni mnafiki. [35]

Matokeo ya kukufurishana

Kukufurishwa kwa Waislamu kumepelekea kupatikana kwa matokeo mengi, ikiwa ni pamoja na:

  • Mauaji ya Waislamu: Katika historia ya Uislamu, Waislamu wengi wameuawa baada ya kukufurishwa kwao.
  • Uharibifu wa majengo ya kihistoria yakiwemo makaburi na majengo ya kidini: Mawahabi wameharibu majengo mbali mbali ya kihistoria, yakiwemo makaburi na majengo mengine ya kidini yanayoheshimiwa na Waislamu, kama vile Haramu za Maimamu. Wamefanya hivyo kwa kisingizio cha kupigana na shirki.
  • Kuakisi vibaya sura ya Uislamu na kuipa sura kikatili ulimwenguni: Vitendo vya makundi ya kigaidi kwa jina la Uislamu vimefanya wapinzani wa Uislamu wauone Uislamu kuwa ni dini ya kikatili. [36]

Pia miongoni mwa athari za kukufurishana, ni kuasi kwa kutumia silaha dhidi ya serikali za Kiislamu na kuzidhoofisha. Kuzua fitna na kuziparaganisha serikali za Kiislamu, kuhalalisha mali za wanawake wa Kiislamu wanaotekwa na wapiganaji wa kigaidi, ni baadhi ya matokeo mengine ya kukufurishana Waislamu wenyewe kwa wenyewe. [37]

Kuundwa kwa vikundi vya kukufurishana

Katika karne tulionayo hivi sasa, Mawahabi pamoja na vikundi kama vile ISIS vilivyoundwa chini ya ushawishi na usaidizi wao, vimekuwa vikiwakufurisha Waislamu kuwaita makafiri, kuwaua na kuchukua mali zao. [38] Wao hutumia Aya zilizoteremshwa kuhusiana na washirikina na makafiri na kwapachika nazo Waislamu. [39] Wameonekana kufanya hivyo hali ya kwamba wanazuoni wa Kiislamu wamepinga kitendo hichi, wakisema kwamba; kinachopelekea mtu fulani kutoka katika Uislamu ni kule kukanusha kwake itikadi kuu za kidini tu, yaani kama vile; kukataa utume na Upweke wa Mwenye Ezi Mungu, ndicho kinachoweza kumfanya Muislamu kuwa kafiri. [40] Pia kukataa kwake misingi hiyo iwe ni njia ya makusudi na ikawa haikuwezekana kufasiriwa kwa maana nyengine. [41]

Mkutano wa kimataifa

Mnamo mwaka wa 2014, mkutano uliofanyika chini ya jina la Mkutano wa Kimataifa wa Harakati za Kihafidhina na Kukufurishana kulingana na Mtazamo wa Wanazuoni wa Kiislamu ulifanyika chini ya usimamizi wa Ayatullahi Makarem Shirazi, mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu, huko Qom Iran. Wanazuoni wa Shia na Sunni kutoka nchi 80 za ulimwenguni walihudhuria mkutano huo. [42] Nakala 830 za Makala zilizotumwa katika mkutano huo zimechapishwa katika juzuu 10 chini kwa jina la “Majmue Maqaalaat Kongere Jihaani Jarayanhae Ifrati wa Takfiiri” yaani: Mkusanyiko wa Makala za Mkutano wa Kimataifa wa Harakati za Kihafidhina na Kukufurishana. Pia, Sekretarieti ya Kudumu ya mkutano huu imechapisha vitabu 40 kwa lugha tofauti na kuanzisha jarida la "Umoja wa Umma wa Kiislamu" kwa lugha za Kifarsi na Kiarabu. [43]

Bibliografia (seti ya vitabu kuhusiana na mada hii)

Kuna kazi nyingi zilizoandikwa katika kukosoa na kutafiti fikra za kukufurishana. Katika "Kitabu cha Bibliografia ya Ukufurishaji", kuna karibu ya kazi 528 kwa lugha ya Kiarabu na Kiajemi zilizo wasilishwa ndani yake, kati ya hizo kazi 235 ni kwa mfumo wa vitabu, kazi 240 ni makala, kazi 49 ni tasnifu, na kazi 4 ni majarida maalum. [44]

  • Kitabu (آراء علماء المسلمین و فتاواهم فی تحریم تکفیر اتباع المذاهب الاسلامیّه), yaani: Maoni ya Wanazuoni wa Kiislamu na Fatwa zao Katika Kuharamisha Kuwakufurisha Wafuasi wa Madhehebu ya Kiislamu Kitabu hichi ni kazi ya Sheikh Fuad Kadhim Miqdadi, mwanzilishi wa Darul-Taqrib ya Iraq. Katika kitabu hichi, kimekusanya na kutafiti ndani yake fatwa na maoni ya wanazuoni wa Kishia na Kisunni katika kukataza suala la kuwakufurisha wafuasi wa madhehebu ya Kiislamu. Kitabu hichi kilichapisha na Taasisi ya Majma’a al-Thaqlaini al-‘Alamiy ya Tehran mnamo mwaka 1428 Hijiria. [45]
  • Kitabu (الاسلام و العنف قراءة فی ظاهرة التکفیر), yaani: Uislamu na Unyanyasaji Uchambuzi wa Tukio la Kukafirishana, Kitabu hichi ni kazi ya Hussein Ahmad al-Khushani ambacho kinachunguza suala la unyanyasaji na ukafirishaji katika Uislamu. Pia kimetafiti ndani yake vigezo vya kukafirisha, asili, aina zake, na sifa za wakafirishaji. Kitabu hiki kilitafsiriwa kwa lugha ya Kifarsi kwa jina la “Islam wa Khushunat”: Negahe Nou be Pediideh takfir” mnamo mwaka 2011. [46]

Maudhui zinazo fungamana