Kuvunjia heshima matukufu
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Kuvunjia heshima mambo matukufu (Kiarabu: الإساءة للمقدسات) ni kutusi, kudhihaki mtu au kitu ambacho kwa mujibu wa sheria au watu wa sheria kinaheshimiwa na ni kitukufu. Ni haramu kuvunjia heshima mambo matukufu na hilo linahesabiwa kuwa ni katika madhambi makubwa. Katika kuthibitisha kosa na uhalifu wa kuvunjia heshima jambo tukufu hakuna tofauti baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Anuani ya matukufu inajumuisha wakati, sehemu, watu, vitabu na kadhalika; kama vile mwezi wa Ramadhani, Kaaba, Mitume, Maimamu (a.s), dharih (eneo la ndani linalolizunguka kaburi) na Qur’an.
Kiwango cha adhabu ya kuvunjia heshima mambo ambayo ni matukufu kinatofautiana; baadhi ya hayo hupelekea mtu kuwa kafiri na kuritadi (kutoka katika Uislamu) na adhabu ya mfanyaji wa hilo ni kuuawa; kama vile kuvunjia heshima na kudhalilisha au kufanyia mzaha dharura miongoni mwa dharura za dini na madhehebu. Katika baadhi mengine pia hupelea hukumu ya ta’zir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo); kama vile mtu kuzini mchana wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo mbali na kutekelezwa dhidi yake huainishiwa pia adhabu ya ta’zir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo).
Kwa mujibu wa mafakihi, ni harmua kuvunjia heshima na kulaani matukufu ya madhehebu manne ya Ahlu-Sunna. Kadhalika kwa wakitegemea Aya ya 108 ya Surat al-An’am, wanaona kuwa haijuzu kuvunjia heshima mambo ambayo kwa dini na madhehebu ya Mwenyezi Mungu na yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu ni matukufu.
Utambuzi wa maana
Kutukana na kuvunjia heshima vitu vitakatifu ni kubeza na kutukana kila jambo ambalo ni faradhi kuliheshimu kwa mujibu wa sharia na watu wake. [1] Katika kuthibitisha kosa na uhalifu wa kuvunjia heshima jambo tukufu hakuna tofauti baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. [2] Mifano na vielelezo vya kuvunjia heshima matukufu vinajumuisha watu na wasiokuwa watu; watu ni kama vile shakhsia za Kiislamu na wasiokuwa wa Kiislamu ambao kwa mujibu wa Uislamu ni wenye kuheshimika; kama vile Mtume (s.a.w.w), Maimamu (a.s), Kadhija (a.s), [3] Bibi Maryam (a.s) Bibi Hajar; [4] na wengineo wasiokuwa hao kama Mwenyezi Mungu, Qur’an, Kaaba, Misikiti, makaburi ya Mitume na Maimamu na kadhalika. [5]
Nafasi yake Kifikihi
Katika vitabu vya fikihi (sheria), hakuna kosa au uhalifu unaochunguzwa kwa anuani ya kutusi au kuvunjia heshima vitu au mambo matakatifu; lakini mafaqihi, sambamba na kueleza mifano yake, kama vile Sabb al-Nabiy (kumtukana Nabii) [6] kutukana waumini [7] Idha'i (kuudhi) [8] Qadhf (tuhuma ya zinaa au liwati), [9] katika sehemu za tohara, [10] Hija, [11] Makasib muharramah (machumo ya haramu) [12] hudud (adhabu zisizo za kimali), [13] wametoa hukumu ya kuwa haramu kutusi na kuvunjia heshima. [14] Kuhusiana na hili, vitabu vya kanuni za fiqhi pia vimetaja na kubainisha anuani kama: Kuharamishwa kuvunjia heshima mambo matukufu (حُرمَةُ اِهانةِ المُحَّرمات فی الدّین), [15] na Kuharamishwa kuvunjia heshima shaari na kufadhilisha (حُرمةُ الاِهانةِ بالشَّعائر و رُجحانِ تعظیمِها). [16]
Katika vitabu vya hadithi pia kuna hadithi zilizopokewa kuhusiana na masuala maalumu ambayo yanahesabiwa kuwa ni katika matukufu ya dini na ni haramu kuyatusi na kuyavunjia heshima; kama vile kuvunjia heshima Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu (Kaaba) na kumtusi Mtume (s.a.w.w). [17] Katika baadhi ya hadithi, maimamu (a.s) wamewakataza wafuasi wao kutukana vitu vinavyoheshimiwa na kutukuzwa na wengine. [18] Baadhi ya wafasiri pia wametumia kanuni na hukumu kutoka katika Aya ya 108 ya Surah An'am; kama vile kuharamishwa kuwatukana makafiri, ikiwa itasababisha matusi kwa Mwenyezi Mungu, na pia kukataza kuwatukana wasio Waislamu na matukufu yao, ikiwa itapelekea kuwatukana matukufu ya Waislamu. [19] Aya hiyo inasema:
وَ لا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّهَ عَدْواً بِغَيْرِ عِلْمٍ كَذلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلى رَبِّهِمْ مَرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُمْ بِما كانُوا يَعْمَلُونَ
- Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.
Hukumu za Kifikihi
Kuna hukumu ambazo zimetajwa kuhusiana na kuvunjia heshima mambo matukufu; miongozi mwazo ni:
- Ni haramu kuvunjia heshima matukufu ya kidini na ni wajibu kuyatukuza na kuyaheshimu. [20]
- Katika kuvunjia heshima mambo matukufu hakuna tofauti baina ya mambo ya wajibu ya Mwenyezi Mungu na ya mustahabu. [21]
- Mafakihi wanaamini kuwa, katika kuvunjia heshima mambo matukufu, toba ya aliyefanya kitendo hicho haikubaliwi, isipokuwa kwa mtu ambaye ni kafiri ambaye baada ya kuvunjia heshima matukufu akasilimu na kuwa Mwislamu. [22]
- Ikiwa mtu atavunjia heshima mambo ambayo ni matukufu na ya kuheshimiwa katika hali ya hasira na bila ya kukusudia au akadhani kwamba, kile anachokifanya hakihesabiwi kuwa ni kuvunjia heshima matukufu, hatatekelezwa hukumu za kuvunjia heshima mambo matukufu. [23]
Vielelezo na adhabu zake
Adhabu za kutukana vitu na mambo matakatifu ni tofauti. Baadhi ya athari zake ni kupelekea mtu kuwa kafiri na kuritadi (kutoka katika Uislamu) na mfano wa hilo ni kiumtsi na kumvunjia heshima Mwenyezi Mungu, Manabii (a.s) na Maimamu (a.s). Adhabu ya baadhi ni hukumu ya ta’zir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo):
Kuvunjia heshima matukufu kunakopelekea mtu kuwa kafiri na kuritadi
Anuani ya kosa la haddi (adhabu isiyokuwa ya kifedha) katika kuvunjima heshima mambo matakatifu, au kutusi na qadhf (kutoa truhuma ya zinaa au liwati) au kukufuru na kuritadi:
- Kumtukana na kumtusi Mwenyezi Mungu: Mafakihi wanasema kuwa, mtu ambaye anamtusi na kumvunjia heshima Mwenyezi Mungu adhabu nbi kafiru na damu yake ni halali kumwaga (anapaswa kuuawa). [24]
- Kumtusi na kumtukana Nabii: Mtu ambaye atatoa maneno machafu na na kumtusi Mtume Muhammad (s.a.w.w) au akanasibisha kitu na Mtume ambacho kitapelekea kuddhalilishwa Mtume anatambuliwa kuwa damu yake ni halali kumwagwa (Mahdur al-Dam) [25] na hata akitubu toba yake haitamsaidia kuzuia kutekelezwa adhabu hiyo. [26] Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi, katika kumtusi Nabii hakuna tofauti juu ya aliyetenda kosa hilo baina ya Mwislamu na kafiri, mwanaume na mwanamke. [27] Kwa mujibu wa mafakihi wa Kishia ni kuwa, Mitume wengine (28], Fatima Zahra (a.s) [29] na Malaika pia wanajumuishwa katika hukumu hii.
- Kutukana Maimamu (a.s): Kwa mujibu wa itikadi ya mafakihi ni kuwa, kila ambaye atamtusi na kumvunjia heshima Imamu muadilifu kuuawa kwake huwa wajibu. [31]
Katika vitabu vya fikihi kumetajwa baadhi ya vielelezo vya adhabu za kuvunjia heshima matukufu. Kama kutaja mfano kumetumika kuarifisha kuritadi; kwa mfano:
- Kutupa Qur’an katika uchafu kwa kukusudia: [32] mwenye kufanya kosa hili ni murtadi na anapaswa kuuawa. [33]
- Kutia najisi Kaaba au kuiharibu: Mwenye kufanya kosa hili anapaswa kuuawa. [34]
- Kutia najisi dharih (eneo la ndani linaloizunguka kaburi) ya Mtuyme (s.a.w.w) na Maimamu kwa kukusudia. [35]
- Kubeza, [36] kudhlilisha au kudunisha dini: [37] Endapo Mwislamu anafanyia mzaha na kubeza Usul al-Dini (Misingi ya Dini) kama Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) au dharura miongoni mwa dharura za dini kama wajibu wa Sala na Saumu [38] ataritadi na kukufuru [39] na atakuwa ametenda dhambi kubwa. [40] Allama Hilli ametoa hukumu ya kuidhinisha kuuawa mtu aliyefanya mzaha na udunishaji huo. [41]
Kuvunjia heshima matukufu kunakopelekea ta’azir
Hakuna hitilafu baina ya mafakihi kuhusiana na kuhusishwa na adhabu ya ta’azir mtu ambaye amevunjia heshima mambo matakatifu ya watu au dini. [42] Kuhusiana na masuala kama vile kutia najisi kwa makusudui msikiti wa Makka (Masjdul Haram), kumeainishwa kiwango thabiti cha ta’azir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo). [43] Baadhi ya hukumu za ta’zir kuhusiana na mwenye kuvunjia heshima mambo matukufu ni:
- Kaburi la Mtume (s.a.w.w) na Maimamu na Haram zao: Ni haramu kufanya jambno lolote linalopelekea kuvunjiwa heshima, kufanyiwa mzaha na kudhalilishwa makaburi ya Maimamu na Haram zao [44] na mwenye kufanya hivyo huainishiwa ta’zir (ta’zir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo). [45]
- Katika fikihi ya Kiislamu, kutokea na kufanyika uhalifu na kosa katika baadhi ya nyakati kama siku ya Ijumaa, mwezi wa Ramadhani na maeneo yanaheshimiwa na kutukuzwa na Waislamu kama misikiti, huwa na taathira katika katika hatua ya mtawala wa Kiislamu kuainisha adhabu dhidi ya mhalifu huyo. [46] Kwa mfano kama mtu katika nyakati hizi atafanya zinaa, mbali na kutekelezwa adhabu ya zinaa dhidi yake kutokana na kosa lka kuvunjia heshima mambo matukufu hustahiki adhabu ambaye ataainishiwa na mtawala wa Kiislamu. [47]
- Misikiti: Miongoni mwa vielelezo vya kuvunjia heshima mirikiri ni kuutia najisi kwa makusudi. [48]
- Kila kitu ambacho kwa mujibu wa sheria za Kiislamu ni wajibu kuheshimiwa; kama vile vitabu vya hadithi na fikihi [49], turba ya Imamu Hussein (a.s) na kila ambacho kimechukuliwa kutoka katika kaburi la Imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya tabaruku na shifaa na kila ambacho kimetoka katika makaburi ya Maimamu (a.s); kama turba (udongo) ya kaburi [50[ na suhula zake. [51]
Kuvunjia heshima matukufu ya madhehebu
Kwa mujibu wa fat’wa ya mafaqihi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia ni haramu kumtusi Bibi Aisha, kuwalaani Masahaba na mambo mengine matakatifu ya madhehebu nne za Kisunni. Na Wanatambua kuwa, kitendo hiki khiyana na usaliti kwa Uislamu na ni kutoa huduma kwa makundi ya makafiri na washirikina. [52]
Katika muktadha huu, katika kitabu cha: Kuharamishwa Kuwatusi na Kuwakufurisha Waislamu kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kishia kuna fatwa za Marajii Taqlidi 33 wa Kishia, kuhusiana na kuwa haramu kutukana matukufu ya madhehebu za Kiislamu na kukufurisha Waislamu. [53]
Kuvunjia heshima makundi na dini zisizokuwa za Kiislamu
Kwa mujibu wa mafaqihi, haijuzu kutukana vitu vitakatifu na vya heshima kwa makundi na dini nyingine (hata masanamu na miungu ya makafiri). [54] Sababu ya hukumu hii ni Aya ya 108 katika Surat al-An’am na baadhi ya hadithi. [55] Sababu ya kukatazwa kuvunjia heshima mambo matakatifu ni kukabiliana na kutochukuliwa hatua kama hiyo hiyo; [56] kwani kuvunjia heshima matakatifu yao itakuwa sababu ya wao kuvunjia heshima na kutusi matukufu ya Waislamu, [57] na kuharamishwa kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu ni jambo ambalo Maulamaa wameafikiana na kukubaliana kwa kauli moja. [58]
Allama Tabatabai, mfasiri wa Qur’an tukufu anasema katika kitabu chake cha Tafsir al-Mizan kwamba, hukumu hii ni katika adabu za kidini ambapo kama itachungwa na kuheshimiwa, matukufu yote katika mataifa mbaklimbali yatapata kinga na kubakia salama. [59]
Kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwa kisingizio cha uhuru wa kusema
- Makala asili: Charlie Hebo (jarida) na Salman Rushdie
Baadhi ya nchi zikitumia kisingizio cha haki ya uhuru wa kujieleza na kusema, [6] zinaruhusu aina yoyote ya dharau, matusi na kuvunjiwa heshima matukufu ya wengine (kuchomwa moto Quran au kuchora katuni mbaya za Mitume), na kukataza kuvunjia heshima matukufu ya wengine au ulazima wa kuheshimiwa kwake kunahesabiwa kuwa ni kubinya uhuru wa kusea na kutoa maoni. Katika kukabiliana na kutoa jibu la hili, imesemwa kwamba uhuru wa kusema unaheshimiwa pale ambapo haudhuru na kutoa pigo kwa haki na uhuru wa wengine; kwa sababu moja ya uhuru muhimu na haki za binadamu ni haki ya kuchagua dini. [61] Lakini cha ajabu ni kwamba, mataifa hayo hayo yanayoruhusu kuvunjiwa heshima matukufu ya dini hasa ya Uislamu kama kuchorwa katuni za kumvnjia heshima Mtme Muhammad (saww) na kuchomwa moto Qur’amni tukufu yamezuia na kupiga marufuku maoni ya kukosoa kile kinachodaiwa kuwa mauaji ya kimbari ya Mayahudi katika Vita vya Pili vya Dunia yanayojulikana kama Holocaust.
Rejea
Vyanzo