Nenda kwa yaliyomo

Josho la kugusa maiti

Kutoka wikishia

Josho la kujitoharisha kutokana na kumgusa maiti (Kiarabu: غسل مس الميت) Ni utaratibu na mfumo maalumu wa kuoga ambao hunafanywa kutokana na kugusa mwili wa mtu aliyefariki dunia. Josho hili huwa la lazima (wajibu) kwa yule ambaye amekugusa mwili wa maiti mwili wake tayari umesha poa (umeshakuwa bardi) na kabla ya maiti hiyo kuoshwa. Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa madhehebu ya Shia, josho hili ni josho la wajibu kwa atakaye tenda tendo hilo; lakini kwa upande wa wanazuoni wa madhehebu Sunni wamelihisabu josho hili kuwa ni mustahabu. Hukumu hii haingizi ndani yake miili ya Mitume, watu watakatifu (Maasumina) wala miili ya mashahidi.

Kwa mujibu wa maoni maarufu ya wanazuoni wa Shia, tohara ya josho la kugusa maiti hauwezi kuchukua nafasi ya udhu. Pia, kuna maoni mawili juu ya uhalisia wa tendo la kugusa maiti; kwamba jee tendo hili linalosababisha kupatikana kwa hadathi kubwa (حدث اکبر) au husababisha hadath ndogo (حدث اصغر)? Kulingana na maoni ya kwanza, mambo yote ambayo mwenye janaba hatakiwi kuyafanya, itaikuwa haijuzu kwake kuyafanya, kama vile kukaa katika msikiti na kufunga saumu, na atalazimika kukoga josho la kugusa maiti kabala ya kutenda matendo hayo. Lakini kulingana na maoni ya pili, josho la kugusa maiti litakuwa ni wajibu tu kwa ajili ya kutenda amali ambazo zinahitajia wudhuu (hazitendwi bila ya uhu).

Mofolojia na Welewa wa Dhana

Josho la kugusa mwili wa maiti: ni josho la wajibu kwa mtu aliye kugusa mwili wa mtu aliyekufa huku mwli huo ukiwa tayari umesha kuwa baridi.[1] Josho hili limetadiliwa katika vitabu vya fiqhi kwenye milango inayozungumzia masuala ya tohara.[2]

Namna ya kukoga josho la kugusa mwili wa maiti ni sawa na njia ya inayo tumika katika kukoga majosho mengine ambayo ni ya wajibu au mustahabbu (ya sunna), kiufupi ni sawa na kukoga josho la janaba.[3] Josho hili linaweza kufanywa kwa njia mbili: kwa utaratibu wa hatua kwa hatua na kwa kujizamisha kwenye maji (ghuslu al-irtimasi). Katika njia inayo fuata utaratibu; baada ya mtu kutia nia, kwanza huoshwa kichwa na shingo, kisha upande wa kulia kuanzia shingoni hadi vidoleni mwa mguu wa kulia, kisha hufuatia upande wa kushoto kuanzia shingoni hadi vidoleni mwa mguu wa kushoto. Lakini katika ghusl ya kuzama, mwili wote huzama ndani ya maji.[4]

Falsafa ya Kukoga Josho la Kugusa Maiti

Falsafa ya kukoga josho la kugusa mwili wa maiti imeelezewa kwamba; ni kwa ajili ya kuhakikisha utohara wa kimwili na utakaso wa kiroho kwa mtu aliye mgusa maiti. Kulingana na Hadithi iliyo nukuliwa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) ni kwamba; mtu anayeosha maiti ni lazima aoge ili kujitakasa kutokana na uchafu unaotokana na mwili wa maiti. Hii ni kwa sababu wakati roho inapoachana na mwili (anapotoka roho), magonjwa na maambukizi mbali mbali hubakia kwenye mwili wake.[5]

Hukumu za Kifiqhi

Kwa mujibu wa maoni ya wanachuoni wengi wa Shia, josho la kujitohariasha kutokana na kugusa mwili wa maiti ni wajibu kwa mwenye kugusa mwili wa maiiti hali mwili huo ukiwa tayari umeshapoa.[6] Miongoni mwa wanazuoni wa Shia, inasemekana kwamba Sayyid Murtadha (aliye ishi baina yam waka 355 na 436 Hijiria), yeye haoni kuwa josho hilo ni wajibu, bali kufanya hivyo ni mustahabu (sunna) kwa mujibu wa mtazamo wake.[7] Pia, kulingana na maelezo ya Allama Hilli (aliye ishi kati yam waka 648 na 726 Hijiria), ni kwamba; wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Sunni hawaoni kuwa ni wajibu mtu kuoga josho la mwili wa maiti kwa yule aliye gusa mwili huo.[8] Kwa maoni ya wengi wao, ni kwamba; josho la kugusa mwili wa maiti ni mustahabbu (sunna).[9]

Kwa mujibu wa fat'wa za wanachuoni wa Shia, kugusa mwili wa binadamu aliyekufa, katika hali ambayo mwili huo utakuwa tayari umeshapoa na kabla ya kukoshwa kwake, husababisha kupatikana kwa wajibu wa josho la kugusa mwili wamaiti. Kwa hiyo, kuugusa mwili wa maiti baada ya kukoshwa kwa maiti huyo hakusababishi mtu kukabiliwa na wajibu wa kukoga josho la kugusa mwili wa maiti.[10]

Miili Iliyo Vuliwa na Kuwekwa Nje ya Hukumu ya Josho la Gusa Maiti

Kulingana na maoni ya wanazuoni wa Shia, kuna miili michache ilivyo vuliwa na kuwekwa nje katika hukumu hii, miongoni mwayo ni:

  • Mwili wa Maasumu
  • Shahidi aliye uawa vitani
  • Mwili wa mtu ambaye ameoga josho la maiti kabla ya kuuliwa (kutokana makossa fulani).[11] Ila baadhi ya wanazuoni wengine walio kadiria kuwa; kuna uwezekano kwamba kugusa mwili wa shahidi pia kunasababisha kuwajibikiwa na josho la kugusa maiti.[12]

Hukumu Zinazo Husiana na Kugusa Maiti

  • Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi, ni kwamba; josho la kugusa maiti haliwezi kuchukua nafasi ya udhu. Kwa hivyo, kwa ajili ya kusali, mbali na kukoga josho la kugusa maiti, ni lazima pia mtu kutia udhu kwa ajili ya kutekeleza ibada ya sala.[13] Hata hivyo, kwa mujibu wa fat'wa ya Ayatullah Sistani, tohara ya josho la kugusa maiti linatosha, na hakuna haja ya kutia udhu kwa ajili ya sala, na huku yake ni sawa na hukumu ya josho la janaba.[14]
  • Kwa mujibu wa fat'wa za wengi miongoni mwa wanazuoni ni kwamba; tendo la kugusa kiungo kilicho katwa au kumeguka kutoka kwenye mwili wa binadamu, ambacho kina mfupa ndani yake, husababisha mtu kuwajibika kukoga josho la kugusa maiti.[15] Kwa upande mwingine, Ayatollah Sistani anaamini kwamba kiungo kilicho katwa au kilicho meguka kutoka katika mwili wa binadamu, hata kama kitakuwa na mfupa na nyama, hakipelekei mtu kuwajibikiwa na josho la kugusa maiti.[16]
  • Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya wanachuoni, josho la kugusa maiti ni lazima tu kwa amali ambazo zinahitaji udhu; kama vile sala na kugusa mandishi ya Qur'an. Wanazuoni wengine wanaamini kwamba kugusa maiti husababisha hadith kubwa (حدث اکبر). Kwa hivyo, kujitoharisha kupitia josho la kugusa maiti ni muhimu kwa ajili ya shughuli zote ambazo husurutishwa kuzifanya baada ya kuwa na tohara ya kimwili, kama vile sala, kutufu, kufunga na kukaa msikitini.[17] Kutoka kwa Wahid al-Bahbahani amenukuliwa akisema kwamba; maoni ya pili ndio maarufu zaidi kati ya wanazuoni.[18] Hata hivyo, wengi miongoni mwa wanazuoni wa kisasa wanakubaliana na maoni ya kwanza.[19]

Maudhui Yanayo Fungamana

Rejea

  1. Ali Shia, «Ahkam Mayit Dar Fiqh Madzahib Islami», uk. 57.
  2. Tazama: Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 2, uk. 12.
  3. Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 2, uk. 10.
  4. Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 1, uk. 522-524.
  5. Sheikh Saduq, Ilalu al-Shara'i, juz. 1, uk. 300, hadithi ya 3.
  6. Amili, Miftah al-Karamah, juz.n4, uk. 312.
  7. Amili, Miftah al-Karamah, juz.n4, uk. 313.
  8. Allamah Hilli, Tadhkirat al-Fuqaha', juz. 4, uk. 134.
  9. Sheikh Tusi, al-Khilaf, juz. 1, uk. 223.
  10. Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 2, uk. 3.
  11. Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 5, uk. 307.
  12. Tabrizi Ghuruwa, al-Tanqih, juz. 8, uk. 294-298.
  13. Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 2, uk. 9-10.
  14. Sistani, Taudhih al-Masail, uk. 103, Suala la 518.
  15. Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 2, uk. 5.
  16. Sistani, Minhaj al-Salihin, juz. 1, uk. 116.
  17. Tazama: Tabatabai Yazdi, al-Urwat al-Wuthqa, juz. 2, uk. 11; Amili, Miftah al-Karamah, juz. 4, uk. 314-317.
  18. Amili, Miftah al-Karamah, juz. 4, uk. 314.
  19. Tazama: Bani Hashimi, Taudhih al-Masail Maraji' juz. 1, uk. 393-394.

Vyanzo

  • ʿĀmilī, Sayyid Jawād, Miftāḥ al-kirāma fī sharḥ qawā'id al-ʿallāma, Mhariri: Muḥammad Bāqir Khāliṣī, Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1419 AH.
  • ʿAlī shiʿah,ʿAlī, Aḥkām-i mayyit dar fiqh-i madhāhib-i islāmī, Muṭāliʿat Taqrībī Madhāhib-i Islāmī, No. 3, winter 1391 Sh.
  • Banī Hāshimī Khomeinī, Sayyid Muḥammad Ḥassan, Tawḍīḥ al-masāʾil-i marajiʿ, Tehran, Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1392 Sh.
  • Gharawī Tabrīzī, Alī, Al-Tanqīḥ fī sharh-i ʿurwat al-wuthqā; taqrīrāt-i dars-i Aytullāh al-Khoeī, Chapa ya pili, Qom: 1411 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥassan bin Yūsuf al-. Tadhkirat al-fuqahāʾ, Qom, Muʾassisa-i Āl al-Bayt, 1414 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām, Mhariri: ʿAbbās Gūchānī, Chapa ya saba, Beirut, Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1362 Sh.
  • Sīstānī, Sayyid ʿAlī, Tawḍīḥ al-masāʾil, [n.p], [n.d].
  • Sīstānī, Sayyid ʿAlī, Minhāj al-ṣāliḥīn, Qom, Daftar Nashr Ḥaḍrat Aytullāh Sīstānī, 1417 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad bin ʿAlī al-. ʿIlal al-sharāʾiʿ. Qom: Intishārāt-i Dāwarī, 1385 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad bin al-Ḥassan al-. Al-Khilāf, Mhariri: ʿAlī Khurāsānī et.al. Qom, Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1407 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī Yazdī, Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwat al-wuthqā, Mhariri: Aḥmad Muḥsinī Sabziwārī, Chapa ya kwanza, Qom, Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1419 AH.