Josho la janaba
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Josho la janaba (Kiarabu: غسل الجنابة) Ni aina ya josho lifanywalo baada ya mtu kupata janaba. Hali ya janaba kama janaba, hua haihitaji wala kupelekea ulazima wa josho la janaba, ila ulazima huu ni kwa ajili ya kutekeleza matendo maalumu ya wajibu, ambayo usafi ni miongoni mwa masharti ya kukubalika kwake, kama vile amali ya ibada ya Sala. Josho la janaba halitafautiani na majosho mengine ya wajibu, bali hutendwa kama yalivyo majosho mengine ya wajibu. Kwa hiyo, laweza kufanywa kwa njia ya taratibu maalumu au kwa kupiga mbizi na kuzama kwenye maji (Irtimas). Katika njia ya taratibu maalumu, kwanza huoshwa kichwa na shingo, kisha upande wa kulia wa mwili, na mwisho upande wa kushoto. Aliye koga janaba huwa hana haja ya kutia udhu kwa ajili ya kufanya ibada zake mbali mbali, hii inamaanisha kwamba; josho la janaba linashika nafasi ya udhu.
Janaba
- Makala Asili: Janaba
Josho la Janaba ni mojawapo ya majosho ya lazima (wajibu) katika dini ya Uislamu.[1] Kikawaida josho hili pamoja na hukumu zake hujadiliwa katika vitabu vya Hadithi,[2] fiqhi,[3]vitabu vya fatwa na miongozo ya amali vya wanazuoni mbali mbali.[4]
Mtu huingia katika hali ya janaba kutokana na kutoka na manii (akiwa usingizini au akiwa macho), pia hali hiyo hupatikana kwa njia ya kujamiiana (hata kama mtu huyo hatatokwa manii), wote wawili waliotenda tendo (mtenda na mtendwa) hilo hupatwa na hali hiyo ya janaba.[5] Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, ni makuruhu kwa mwenye janaba kutekeleza baadhi ya ibada, na pia kuna ibada nyengine ambazo huwa ni haramu kwake kuzitekeleza.[6] Uharamu na umakruhu huo huwa hauondoki isipokuwa kwa kujitakasa kutokana na janaba hilo. Kwa mfano, ni haramu kwa mtu aliye na janaba kufanya mambo yafuatayo; Kusali, kukaa misikitini, kusoma Sura zenye sajda ndani yake, kugusa maneno ya Qur'ani pamoja na majina ya Maimamu.[7] Pia yalio makruhu (yasiyo pendekezwa kuyafanya) ni; Kula na kunywa, kusoma zaidi ya Aya saba za Qur'ani, kugusa jalada (bamba la nje) la Qur'ani, pamoja na kuwa karibu na mtu aliyekaribia kufa.[8] Hata hivyo, baadhi ya mambo haya ambayo ni makuruhu huwa yanaondokana na umakruhu wake kutawadha (kutia udhu).[9]
Je, ni Lazima Kukoga Mara tu Baada ya Kupata Janaba?
Kwa mujibu wa nadharia na fat'wa za mafaqihi, ni kwamba; Wajibu wa kukoga janaba ni wajibu wa ambukizo (wujubu ghairiyyun)[10] lililosabababishwa au kuambukizwa kutoka katika wajibu wa amali nyengine kabisa; yaani kiuhalisia josho la janaba ni amali pendekezwa na si ya lazima (wajibu),[11] ila kwa kuwa amali ya pili ni amali inayopaswa kutendwa katika hali ya kitohara, hii ndio iliolazimisha kufanyika kwa josho la janaba. Kwa hiyo, amali hii ya kukoga janaba ya lazima kwa ajili ya kutenda amali ambazo usafi ni moja ya sharti za kukubalika kwa amali hizo,[12] ambazo mfano wake ni sala.[13] Pia, kwa mujibu wa fatwa za mafaqihi, josho la janaba ni miongoni mwa wajibu wenye puruzio lililopuruziwa kiwango cha muda wake (iliosabiliwa muda); kwa hiyo wajibu huu wa kukoga janaba unaweza kucheleweshwa hadi wakati wa kutaka kutekeleza amali ya wajibu fulani.[14]
Kwa Mwenye Janaba Usahihi wa Saumu Yake Unategemea Uwepo Tohara ya Kukoga Janaba
- Makala: Kubakia na janaba
Ni wajibu kukoga josho la janaba kwa yule aliyepata janaba hali akiwa katika mwezi wa Ramadhani. Josho hilo linatakiwa kufanywa kabla ya kuingia wakati wa adhana ya alfajiri. Iwapo mtu huyo ataacha kukoga josho hilo kwa makusudi mpaka akingiwa na wakati wa adhana ya alfajiri, hapo saumu yake itakuwa ni batili, na atalazimika kuilipa funga ya siku hiyo (kufanya qadhaa) na pia kutoa kafara (fidia) kwa ajili ya kosa lake hilo.[15]
Namna ya Kukoga Janaba
- Makala Asili: Kuoga Josho
Josho la kukoga janaba hufanyika kama yalivyo majosho mengine ya wajibu; yaani kwa njia ya tartibi (utaratibu maalumu) na irtimasi (kuzamisha mwili mzima kwenye maji).[16] Katika njia ya tartibi, kwanza kabisa kuanzwa kuoshwa shwa kichwa pamoja na shingo yake, kisha upande wa kulia wa mwili na hatimaye upande wa kushoto wa mwili wa mwenye janaba.[17] Katika njia ya irtimasi, mwili wote huzamishwa kwenye maji mara moja; hata hivyo, na ni lazima katika mfumo huu wa irtimasi mwili mzima uwe chini ya maji kwa wakati mmoja. Yaani haitafaa kwenda kuzamisha sehemu moja ya mwili kisha ukasubiri kwa kipindi fulani, halafu ukamalizia sehemu iliobakia.[18]
Adabu za Josho la Janaba
- Iwapo janaba litakuwa limetokana na kutokwa na manii, basi kwa mujibu wa fatwa za mafaqihi, ni vizuri na ni Sunna kukojoa kabla ya kukoga josho la janaba.[19]
- Ni sunna kuosha mikono, kusukutua na kusema Bismillah kabla ya kuanza kukoga, na pia kusoma dua zilizopendekezwa wakati wa kukoga janaba.[20]
Josho la Janaba na Kukidhi Kwake Mahitaji ya Udhu
Kwa mujibu wa fatwa za mafaqihi wa Kishia ni kwamba; Josho la janaba linatosha na hakuna haja ya kutia udhu baada ya kukoga janaba.[21] Hii ina maana kwamba mtu aliye koga josho la janaba huwa hahitaji tena kutia udhu kwa ajili ya kusali au kufanya ibada nyingine zinazohitaji udhu. Wengi miongoni mwa mafaqihi wanaamini kuwa; Haifai mtu kutia udhu baada ya yeye kukoga josho la janaba.[22] Hata hivyo, kulingana na maelezo ya Alama Hilli, ni kwamba; Sheikh Tusi alitoa fatwa tofauti na wanazuoni wengine kwa kupendekeza na kujuzisha kutia udhu baada ya kukoga janaba.[23]
Mafaqihi wamekhitilafiana kuhusiana na kubatilika au kuto batilika kwa josho la janaba, kwenye hali ya mtu kutokwa na hadath ndogo (mambo yanayo batilisha udhu kama kukojoa au kutoa upepo) hali akiwa Hata kama kutakuwa na nadharia ya kukubalika kwa josho hili, ila bado kuna tofauti za maoni kuhusiana na kuwa je josho hilo litakidhi mahitaji ya udhu au la.[24] Kwa mujibu wa fatwa ya Sayyid Muhammad Kadhim Tabatabai Yazdi ni kwamba; Josho lake halitabatilika ila itambidi kutia udhu.[25]
Falsafa ya Josho la Janaba
Kwa mujibu wa Riwaya zilizotajwa katika kitabu cha 'Ilalu al-Sharai'i, ni kwamba; sababu ya kuwajibishwa kukoga janaba, ni kuondoa uchafu na kusafisha mwili kutokana na najisi. hii ni kwa sababu ya kwamba uchafu wa janaba huwa unatoka kwenye mwili mzima, kwa hivyo ni lazima kuuosha mwili mzima.[26] Pia katika tafsiri ya Qur’ani iitwayo Tafsir Nemuneh, imeelezwa kuwa; kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, ni kwamba; mwili wa binadamu una mifumo miwili ya neva (hisia) inadhibiti shughuli za mwili. Wakati wa kufikia kilele cha raha ya ngono (orgasm), uwiano kati ya mifumo hii miwili huwa unatoweka. Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa; kuosha mwili kwa maji kunaweza kurejesha uwiano huo, na kwa kuwa athari ya orgasm inahusisha mwili mzima wa mwanadamu, hivyo basi imeamriwa kwamba baada ya janaba, mtu anatakiwa kuosha mwili mzima.[27]
Rejea
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 493.
- ↑ Tazama: Hurr Amili, Wasail al-Shia, Muasase Ahlul-bayt, juz. 2, uk. 273 na kuendelea.
- ↑ Tazama: Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 521.
- ↑ Bani Hashimi Khomeini, Tawdhih al-Masail al-Masal, 1381, juz. 1, uk. 208.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 496-499.
- ↑ Tazama: Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 507.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 5097-509.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 520.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwa al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 520.
- ↑ Najafi, Jawahar al-Kalam, 1362 S, juz. 1, uk. 46.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwat al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 521.
- ↑ Muasase Dairat al-Maarif Fiqh Islami, Farang Fiqh Mutabaq Madhhab Ahlul-bayt (a.s), 1387 S, juz. 5, uk. 558.
- ↑ Tazama: Tabatabai Yazdi, Al-Urwat al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 521.
- ↑ Tazama: Ibn Idris, Mausuat Ibn Idris al-Hilli, 1387 S, juz. 7, uk. 111.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwat al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 3, uk. 563.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwat al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 522-523.
- ↑ Hakim, Mustamsk al-Urwah, 1968, juz. 3, uk. 79.
- ↑ Hakim, Mustamsk al-Urwah, 1968, juz. 3, uk. 85-86.
- ↑ Najafi, Jawahar al-Kalam, 1362 S, juz. 3, uk. 108.
- ↑ Tabatabai Yazdi, Al-Urwat al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 522-523.
- ↑ Sheikh Tusi, Al-Khilaf, Muasase Nashr Islami, juz. 1, uk. 131; Najafi, Jawahar al-Kalam, 1363 S, juz. 3, uk. 240.
- ↑ Najafi, Jawahar al-Kalam, 1363 S, juz. 3, uk. 240.
- ↑ Allamah Hilli, Mukhtalaf Shia, 1412 AH, juz. 1, uk. 340.
- ↑ Tazama: Tabatabai Yazdi, al-UrwaT al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 547.
- ↑ Tabatabai Yazdi, al-UrwaT al-Wuthqa, 1417 AH, juz. 1, uk. 547.
- ↑ Saduq, Ilalu al-Shara'i, Maktabat Haydariya wa Mutabaatiha Fi Najaf, juz. 1, uk. 281.
- ↑ Makarim Shirazi, Tafsir Namune, 1374 S, juz. 4, uk. 292-294.
Vyanzo
- Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf, Mukhtalaf al-Shiah Fi Ahkām al-Shari'ah, Mhakiki: Markaz al-Abhath wa al-Dirasat al-Islamiyah, Qom, Daftar Tablighat Islami, Chapa ya kwanza, 1412 H.
- Bahrani, Yusuf, Al-Hadaiq al-Nadhirah Fi Ahkam al-Itrah al-Tahirah, Mhakiki: Ali Akhundi, Qom, Nashr Islami, 1986.
- Hakim, Sayyid Muhsin, Mustamsak al-'Urwatul Wuthqa, Najaf, 1968.
- Najafi, Muhammad Hassan Najafi, Jawāhir al-Kalam fi Sharh Sharāi' al-Islam, Beirut, Dar Ahya al-Turath al-Arabi, Chapa ya saba.
- Sheikh Tusi, Muhammad bin al-Hassan, Al-Mabsut Fi Fiqh al-Imamiyah, Mhakiki: Muhammad Baqir Bahbudi. Tehran, Maktabat al-Murtadhawiyah.
- Yazdi, Sayyid Muhammad Kadhim, Al-'Urwat al-Wuthqah, Qom, Darul Tafsir, Ismailiyan, Chapa ya tano, 1419 H.