Hotuba ya Fadak

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na khutba ya al-Fadakiyyah (hotuba ya Fadak). Ili kufahamu kuhusiana na kuporwa ardhi ya Fadak, angalia makala ya tukio la Fadak.

Hotuba ya Fadak (Kiarabu: الخطبة الفدكية) (Khutba al-Fadakiyyah) au Khutba Lummah ni hotuba ya Mtukufu Bibi Fatima Zahra (a.s) alioitoa kwenye msikiti wa Mtume baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kulalamikia na kupinga kuchukuliwa na Abu Bakar ardhi ya Fadak. Baada ya Abu Bakr kushika hatamu za ukhalifa, akitumia hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) isemayo kwamba Mitume hawaachi mirathi, alikichukua kijiji cha Fadak ambacho Mtume alimpatia Fatima (a.s) na kunyang'anya Fadak kwa maslahi ya ukhalifa.

Kufuatia kushindwa shtaka lake, Fatima (a.s) alikwenda msikitini na kutoa hotuba iliyokuja kuwa mashuhuri kwa jina la Khutba al-Fadakiyyah (hotuba ya Fadak). Katika hotuba yake hiyo, Bibi Fatima (a.s) alibainisha wazi kwamba, eneo la Fadak ni milki na mali yake. Aidha alibainisha na kutetea haki ya Ukhalifa wa Ali na akawalaumu Waislamu kutokana na kunyamaza kimya.

Khutba ya Fadak ni majimui na mkusanyiko wa mafunzo katika nyanja za kumtambua Mwenyezi Mungu, kutambua ufufuo, Utume, kubaathiwa Mtume (s.a.w.w), adhama ya Qur'ani, falsafa ya sheria na al-Wilaya (uongozi). Maandiko ya khutba ya Fadak imenukuliwa katika vyanzo vya Shia na Ahlu-Sunna. Sayyid Izzudin Husseini Zanjani, Hussein Ali Muntadhari na Mujtaba Tehrani wameandika maelezo na ufafanuzi wa hotuba hii.

Umuhimu na nafasi

Khutba Fadakiyyah (Hotuba ya Fadak) inabainisha misimamo ya kisiasa ya Bi Fatima Zahra (a.s) dhidi ya mfumo uliokuwa ukitawala na kulaumu waporaji wa eneo la Fadak na ukhalifa. [1] Katika khutba hii, imesisitizwa juu ya kujenga umoja katika jamii ya Kiislamu na kuepuka mifarakano na unafiki, chini ya kuukubali Uimamu na Wilaya (uongozi) ya Ahlul-Bayt (a.s). [2] Kutokana na hotuba hii kubeba majimui ya maarifa katika uga wa Tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu, ufufuo, utume, kubaathiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), adhama ya Qur'ani Tukufu, falsafa ya sheria na al-Wilaya [3] imetambulishwa kuwa moja ya turathi za kidini za Fatima (a.s) zenye thamani kubwa. [4]

Vile vile, kwa kuzingatia kwamba, khutba ya Fadakiyyah ni sawa na khutba za Imam Ali (a.s) katika suala la ufasaha na balagha [5] na matumizi ya viashiria vya kimantiki vinavyojulikana sana katika fani ni miongoni mwa sababu zilizoifanya hotuba hii iondekee na kutambuliwa kuwa na umuhimu. [6] Kwa muktadha huo, katika kitabu cha Balaghat al-Nisaa cha Ibn Tayfur hotuba hii imetambulishwa kuwa miongoni mwa hotuba zenye balagha na ufasaha mkubwa. [7]

Hotuba ya Fadak hutumiwa kuthibitisha kuruhusiwa wanawake wa Kiislamu kushiriki katika mikusanyiko ya kisiasa. [8] Ayatullaha Abdullah Javad Amoli, mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia anasema, hotuba mithili ya hotuba ya Fatima inapaswa kufundishwa kama somo rasmi katika Hawza (vyuo vya kidini). [9]

Sababu

Makala kuu: Tukio la Fadak, Fadak na Sisi Manabii haturithiwi

Baada ya kifo cha Mtume, kuliatokea mgogoro kuhusu umiliki wa Fadak. Khalifa Abu Bakr alimpokonya Fatima Fadak na akaitaifisha bustani hiyo kwa manufaa ya ukhalifa. Abu Bakr alidai kwamba, Mitume hawaachi urithi; [10] na kwa msingi huo akaitaifishha na kupora bustani ya Fadak ambayo baada baada ya kuteremka Aya ya 26 ya Surat al-Israa -((وَآتِ ذَا الْقُرْ‌بَیٰ حَقَّهُ؛ ; Na mpe aliye jamaa yako haki yake))- iliyomtaka Mtume (s.a.w.w) atoe haki ya Dhawil-Qurba (watu wa karibu), Mtume alimpa Fadak Fatima (a.s) [12] ambaye ni binti yake na ilikuwa katika milki ya Fatima.[13] na kuifanya mali ya Ukhalifa. [14]

Kwa upande wa pili, Fatima (a.s) aliwaleta Imamu Ali (a.s) na Ummu Ayman kama mashahidi [15] ambapo Mtume kabla ya kuaga dunia, alimpatia ardhi ya Fadak. Kwa mujibu wa baadhi ya nukuu, Abu Bakr akakubali na akaandika waraka ili mtu asije akaichukua tena ardhi hiyo. Wakati Fatima (a.s) alipoondoka katika kikao hicho, Omar bin al-Khattab alichukua waraka huo na kuuchana. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya Ahlu-Sunna, Abu Bakr hakukubaliana na mashahidi wa Fatima alitaka waje wanaume wawili kwa ajili ya kutoa ushahidi. [17]

Wakati Fatima alipoona kwamba madai ya kupigania haki yake ya Fadak, yameshindikana, akiwa pamoja na kundi la wanawake kutoka kwa jamaa zake alikwenda msikitini kutoa hotuba. [18] Kwa mujibu wa ripoti ya Ibn Tayfur katika kitabu chake cha Balaghat al-Nisaa, wakati Fatima alipofika msikitini Abu Bakr na kundi la Muhajirina na Ansari walikuwa wamekaa msikitini. Kukawekwa kizuizi baina ya Fatima na hadhirina. Binti ya Mtume alipotoa sauti ya kwanza ya manung'uniko na maumivu, hadhirina waliangua kilio, kisha akanyamaza kidogo ili watu watulie na kisha ndipo alipotoa hotuba yake. [19] Kutokana na hotuba hii kutolewa kwa ajili ya radiamali dhidi ya tukio la kuporwa Fadak, imeondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Khutba al-Fadakiyyah. [20] Hata hivyo kutokana na kuwa kabla ya kutoa hotuba hiyo, Bibi Fatima aliingia msikitini akiwa na kundi la watu wa familia yake, inatajwa pia kama Khutba Lummah . [21]

Mlolongo wa mapokezi ya hadithi

Majlisi katika Bihar al-Anwar anaamini kwamba khutba hii ni miongoni mwa khutba maarufu ambamo Mashia na Ahlu Sunna wameinakili kwa sanadi na mapokezi mbalimbali. [22] Sheikh Saduq amenukuu sehemu ya hotuba hii katika kitabu chake cha Man La Yahdhruh al-Faqih. [23] Kwa mujibu wa Ayatullah Muntadhari, hati na nyaraka ya zamani zaidi ya khutba hii ni kitabu cha Balaghat al-Nisaa kilichoandikwa na Ahmad Ibn Abi Tahir Marwazi, anayejulikana kama Ibn Tayfur (204-280 AH), mmoja wa wanazuoni wa Kisunni walioishi katika zama za Imam Hadi (a.s) na Imam Hassan Askari (a.s) [24] Ibn Tayfur aliiandika khutba hii kwa riwaya mbili, [25] lakini kwa mujibu wa Sayyid Jafar Shahidi katika nyaraka za baadaye, riwaya na mapokezi yote mawili yalichanganyika pamoja na kunukuliwa kwa sura moja. [26] Kumetajwa zaidi ya nyanzo 16 kuhusiana na Khutba al-Fadakiyyah. [27]

Inaelezwa kwamba Imamu Hassan (a.s), Imamu Hussein (a.s), Zainab (a.s), Imam Baqir (a.s), Imamu Swadiq (a.s), Aisha, Abdullah bin Abbas, n.k. ni miongoni mwa wapokezi wa khutba hii. [28]

Yaliyomo

Khutba al-Fadakiyyah inaanza kwa kumhimidi na kumsifu Mwenyezi Mungu na kisha inakumbusha Utume wa Mtume (s.a.w.w) na baada ya hapo inaashiria ukuruba wa Imam Ali (a.s) na Mtume (s.a.w.w) na kuwa kwake kiongozi baina ya mawalii wa Mwenyezi Mungu na ujasiri na ushujaa wake usio na kifani katika kumlinda na kumhami Mtume (s.a.w.w) na Uislamu. Baada ya hapo, hotuba hii inawalaumu Maswahaba kwa sababu walimfuata shetani baada ya kufa Mtume na unafiki ukadhihiri kati yao na wakaiacha haki.

Katika khutba hii, pia limeashiriwa tukio la unyakuzi wa ukhalifa, na kauli ya Abu Bakr kwamba Mitume hawaachi mirathi na kunatajwa Aya za Qur'ani zinazopinga hilo. Kadhalika katika khutba hii, Fatima (a.s) anamkabidhi Abu Bakr kwenye mahakama ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama na anawahutubia maswahaba wa Mtume kwa nini wananyamaza mbele ya dhulma hizi. Anasema walichokifanya ni kuvunja agano lao na Mtume wa Mwenyezi Mungu, na katika sehemu ya mwisho ya khutba hii, anasema kwamba doa baya na fedheha ya kitendo chao hiki kitadumu milele na hatima yao ni motoni. [29]

Andiko na tarjumi ya Khutba ya Fadak

اَلْحَمْدُللَّـهِ عَلی ما اَنْعَمَ، وَلَهُ الشُّكْرُ عَلى ما اَلْهَمَ، وَالثَّناءُ بِما قَدَّمَ، مِنْ عُمُومِ نِعَمٍ اِبْتَدَاَها، وَسُبُوغِ الاءٍ اَسْداها، وَتَمامِ مِنَنٍ اَوْلاها، جَمَّ عَنِ الْاِحْصاءِ عَدَدُها، وَنَأی عَنِ الْجَزاءِ اَمَدُها، وَتَفاوَتَ عَنِ الْاِدْراكِ اَبَدُها، وَنَدَبَهُمْ لاِسْتِزادَتِها بِالشُّكْرِ لاِتِّصالِها، وَاسْتَحْمَدَ اِلَی الْخَلائِقِ بِاِجْزالِها، وَثَنی بِالنَّدْبِ اِلی اَمْثالِها.

Himidi zote na Sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu kwa zile neema alizotuneemesha, na shukurani zote ni zake kwa yale aliyoyatia ilhamu, na sifa zote na shukrani zote ni Kwake kwa yale aliyoyatoa (kumpa Mwanadamu), nayo ni neema na baraka nyingi alizoziumba, pamoja na zawadi kubwa na pana alizotoa (na kumneemesha kwazo Mwanadamu), na baraka tele zisizohesabika ambazo alitoa (kwa Mwanadamu), na ambazo kamwe haiwezekani kuzihesabu, Na mwisho wake ni zaidi ya malipo, na upeo wake (au mipaka yake na kikomo chake) ni jambo lililopo juu (au nje) ya utambuzi (wa mwanadamu) milele, na aliwaita watu (alitoa wito kwa watu waweze) kuongeza baraka na neema hizo kwa wingi kupitia kushukuru kwao (kushukuru kwa neema ulizopewa ni sababu ya kuongeza na kuzidisha neema hizo), aliwataka watu kumhimidi na kuzidisha shukran (kwa yale anayowaneemesha) ili kupanua kiwango cha neema hizo, na kutokana na kualika kwake watu kuelekea neema hizi, akazizidisha (neema hizo) maradufu.

وَاَشْهَدُ اَنْ لا اِلهَ اِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَريکَ لَهُ، کَلِمَةٌ جَعَلَ الْاِخْلاصَ تَأْويلَها، وَضَمَّنَ الْقُلُوبَ مَوْصُولَها، وَاَنارَ فِي التَّفَکُّرِ مَعْقُولَها، الْمُمْتَنِعُ عَنِ الْاَبْصارِ رُؤْيتُهُ، وَمِنَ الْاَلْسُنِ صِفَتُهُ، وَمِنَ الْاَوْهامِ کَيْفِيتُهُ.

Na ninashuhudia ya kwamba hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, wala hana mshirika, ambapo hili (yaani: Shahada hii ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ni jambo (au ni neno) kubwa lililofanya ikhlasi kuwa ndio tafsiri yake na kuziunganisha nyoyo na jambo hilo, na (pia jambo hilo) limerahisisha fikira na tafakuri kulitambua akilini (kwa maana: Jambo hilo limeifanya fikra ya Mwanadamu kuwa na urahisi wa kufikiri na kulitambua akilini mwake, na sio jambo gumu kufikirika katika fikra za Mwanadamu kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na wa pekee, hana mshirika), (huyo ndiye ) Mwenyezi Mungu ambaye macho ya wanadamu kamwe hayawezi kumuona, na ndimi za wanadamu haziwezi kumuelezea (kwa ukamilifu jinsi alivyo), na dhana (fikra) na mawazo ya wanadamu havina uwezo kamwe wa kumdiriki (na kumfahamu kuwa dhati yake yupo hivi au vile).

اِبْتَدَعَ الْاَشْياءَ لا مِنْ شَيْ‏ءٍ کانَ قَبْلَها، وَاَنْشَاَها بِلاَاحْتِذاءِ اَمْثِلَةٍ اِمْتَثَلَها، کَوَّنَها بِقُدْرَتِهِ وَذَرَأَها بِمَشِيَّتِهِ، مِنْ غَيْرِ حاجَةٍ مِنْهُ اِلى تَکْوينِها، وَ لا فائِدَةٍ لَهُ فی تَصْويرِها، اِلاَّ تَثْبيتاً لِحِکْمَتِهِ وَتَنْبيهاً عَلی طاعَتِهِ، وَاِظْهاراً لِقُدْرَتِهِ وَتَعَبُّداً لِبَرِيَّتِهِ، وَاِعْزازاً لِدَعْوَتِهِ، ثُمَّ جَعَلَ الثَّوابَ عَلی طاعَتِهِ، وَوَضَعَ الْعِقابَ عَلی مَعْصِيَتِهِ، ذِيادَةً لِعِبادِهِ مِنْ نِقْمَتِهِ وَ حِياشَةً لَهُمْ إِلى جَنَّتِهِ.

Ameumba (vitu au) viumbe (kwa mara ya kwanza kabisa) bila kutokana na maada iliyoumbwa na kuwepo kabla ya viumbe (vitu) hivyo, na akaviumba bila ya kufuata (au kuangalizia na kuiga) mfano wowote wa umbo lolote, (bali) aliviumba kwa uwezo wake na kuvianzisha kwa matakwa (irada) yake, bila ya kuwa na haja (yoyote) katika kuvitengeneza (na kuviumba) na bila ya kuwa na manufaa yoyote (yale anayoyategemea) katika kuvianzisha (kwa kuviumba na kuvipa muonekano maalum) na kuvifanya viwepo, isipokuwa (sababu kuu ya kuviumba kwake ni ili) kuithabitisha hekima yake (kwa kuifanya kuwa thabiti na madhubuti) na kuwatanabahisha watu watatambue kuwa wanatakiwa kuwa na utiifu kwake, na kuthibitisha (au kudhihirisha) uwezo wake, na kuwafanya waja wake waweze kujua njia (sahihi) ya ibada (wamuabudu Mola wao), na kuheshimu (au kuthamini) wito wake. Kisha akaweka malipo (thawabu) kwa utiifu wake (kwa wale watakao mtii) na adhabu kwa uasi wake (kwa wale watakao muasi), ili aweze kuwaepusha waja wake na adhabu yake (kali) na kuwaongoza kuelekea kwenye Pepo yake.

وَاَشْهَدُ اَنَّ أبي‏ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، اِخْتارَهُ قَبْلَ اَنْ اَرْسَلَهُ، وَ سَمَّاهُ قَبْلَ اَنْ اِجْتَباهُ، وَاصْطَفاهُ قَبْلَ اَنْ اِبْتَعَثَهُ، اِذ الْخَلائِقُ بِالْغَيْبِ مَکْنُونَةٌ، وَبِسَتْرِ الْاَهاويلِ مَصُونَةٌ، وَ بِنِهايَةِ الْعَدَمِ مَقْرُونَةٌ، عِلْماً مِنَ اللَّهِ تَعالی بِمائِلِ الْاُمُورِ، وَاِحاطَةً بِحَوادِثِ الدُّهُورِ، وَمَعْرِفَةً بِمَواقِعِ الْاُمُورِ.

Na ninashuhudia ya kwamba Baba yangu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake (Mwenyezi Mungu), ambaye Mwenyezi Mungu alimchagua kabla ya kumtuma, na akamwita Nabii kabla ya kumchagua, na alimchagua (na kumteua) kabla ya kumtuma (kuwa Nabii), wakati huo viumbe wote walikuwa katika pazia la ghaibu (hawakuwepo kabisa katika uhai), na walikuwa wamefunikwa na pazia la giza lenye kutisha (kwa maana: Walikuwa gizani tu), na walikuwa kwenye (kilele cha juu kabisa cha kutokuwepo au kwenye) kikomo cha (mwisho kabisa cha) kutokuwepo (a’lamul- adam), aliteuliwa (na kuchaguliwa kuwa Nabii) kwa sababu ya ujuzi na elimu yake aliyokuwa nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) juu ya matokeo ya matendo, Na kutambua kwake matukio ya zama, na utambuzi wake kamili juu ya kutokea kwa majaaliwa ya vitu (au maarifa yake kamili juu ya kutokea kwa hatima ya vitu, au utambuzi wake kamili kuwa vitu vina makadirio – qadari – yake).

اِبْتَعَثَهُ اللَّهُ اِتْماماً لِاَمْرِهِ، وَعَزيمَةً عَلى اِمْضاءِ حُکْمِهِ، وَاِنْفاذاً لِمَقاديرِ رَحْمَتِهِ، فَرَأَى الْاُمَمَ فِرَقاً في اَدْيانِها، عُکَّفاً عَلی نيرانِها، عابِدَةً لِاَوْثانِها، مُنْکِرَةً لِلَّهِ مَعَ عِرْفانِها.

Alimtuma (kuwa Nabii) ili kukamilisha amri yake (au agizo lake s.w.t), na kutia sahihi hukumu yake ya hakika, kwa kuzitekeleza amri (na hukumu) zake, na kutimiza vipimo vya rehema zake, Na aliona (Mtume Muhammad -s.a.w.w-) mataifa (au nyumati mbalimbali) yakiwa katika dini tofauti tofauti, na yakiwa yamejitenga mbele ya moto unaowaka wakiuabudu (kwa maana: Akaona baadhi yao wakiwa wamejitenga wakiabudu moto mbele yao), na wengine wakiabudu masanamu yao ya kuchonga kwa mikono yao, huku wakimkanusha Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanamtambua katika maumbile yao.

فَاَنارَ اللَّهُ بِاَبی‏مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَیْهِ و الِهِ ظُلَمَها، وَ کَشَفَ عَنِ الْقُلُوبِ بُهَمَها، وَ جَلى عَنِ الْاَبْصارِ غُمَمَها، وَ قامَ فِی النَّاسِ بِالْهِدايةِ، فَاَنْقَذَهُمْ مِنَ الْغِوايةِ، وَ بَصَّرَهُمْ مِنَ الْعِمايةِ، وَهَداهُمْ اِلَى الدّينِ الْقَويمِ، وَ دَعاهُمْ إِلَى الطَّريقِ الْمُسْتَقيمِ.

Kwa hiyo, kupitia kwa baba yangu Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu akalitia nuru giza hilo (walilokuwa wametumbukia ndani yake), na akaondoa matatizo ya nyoyo (zao yaliyokuwa yakiwakabili, kutokana na upotevu wao wa kuabudu masanamu yao na vyote visivyokuwa Mwenyezi Mungu), na akaondoa (vikwazo au) vizuizi kwenye macho yao, na akasimama (imara) miongoni mwa watu kwa uwongofu (ili kuwaongoa kuelekea njia sahihi ya Mwenyezi Mungu), na akawaokoa na upotevu (na upotovu), na akawafanya wawe ni wenye kuona kwa kuwaondoa kwenye upofu, na akawaongoza kwenye Dini iliyo madhubuti, na akawalingania kwenye Njia Nyoofu.

ثُمَّ قَبَضَهُ اللَّهُ اِلَیْهِ قَبْضَ رَأْفَةٍ وَ اخْتِیارٍ، وَ رَغْبَةٍ وَ ایثارٍ، فَمُحَمَّدٌ صَلَّى اللَّهُ عَلَیْهِ و الِهِ مِنْ تَعَبِ هذِهِ الدَّارِ فی راحَةٍ، قَدْ حُفَّ بِالْمَلائِکَةِ الْاَبْرارِ وَ رِضْوانِ الرَّبِّ الْغَفَّارِ، وَ مُجاوَرَةِ الْمَلِکِ الْجَبَّارِ، صَلَّى اللَّهُ عَلی أَبی نَبِیِّهِ وَ اَمینِهِ وَ خِیَرَتِهِ مِنَ الْخَلْقِ وَ صَفِیِّهِ، وَ السَّلامُ عَلَیْهِ وَ رَحْمَةُاللَّهِ وَ بَرَکاتُهُ.

Mpaka wakati ambapo Mwenyezi Mungu alimwita Kwake, mwito ulioegemezwa juu ya wema, uhuru, kwa kupenda, na kwa kutaka (mwenyewe amchukue kuelekea kwake), na hapo ndipo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipoweza kupata utulivu na raha na kuondokana na mateso (na misukosuko) ya dunia hii, na (wakati huo wa kuitikia wito kuelekea kwa Mola wake) Malaika wema walikuwa karibu yake (wamemzunguka), na akiwa amefunikwa na radhi za Mola wake Msamehevu, na akawa karibu mno na rehema za Mola wake. Basi amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya Baba yangu, Mtume (Mjumbe) wake na Mwaminifu wake, na Mbora wa viumbe vyote na Mteule wake. Na Amani, Rehema na Baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

ثم التفت إلى أهل المجلس وقالت: اَنْتُمْ عِبادَ اللَّهِ نُصُبُ اَمْرِهِ وَ نَهْیِهِ، وَ حَمَلَةُ دینِهِ وَ وَحْیِهِ، وَ اُمَناءُ اللَّهِ عَلى اَنْفُسِکُمْ، وَ بُلَغاؤُهُ اِلَى الْاُمَمِ، زَعیمُ حَقٍّ لَهُ. فیکُمْ، وَ عَهْدٍ قَدَّمَهُ اِلَیْکُمْ، وَ بَقِیَّةٍ اِسْتَخْلَفَها عَلَیْکُمْ: کِتابُ اللَّهِ النَّاطِقُ وَ الْقُرْانُ الصَّادِقُ، و النُّورُ السَّاطِعُ وَ الضِّیاءُ اللاَّمِعُ، بَیِّنَةً بَصائِرُهُ، مُنْکَشِفَةً سَرائِرُهُ، مُنْجَلِیَةً ظَواهِرُهُ، مُغْتَبِطَةً بِهِ اَشْیاعُهُ، قائِداً اِلَى الرِّضْوانِ اِتِّباعُهُ، مُؤَدٍّ اِلَى النَّجاةِ اسْتِماعُهُ.

Kisha Sayyidat Fatima (s.a) akawageukia hadhirina (waliokuwa katika kikao hicho Msikitini na) kusema:

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu!, nyinyi ndio wabeba bendera wa maamrisho na makatazo Yake, na wabebaji wa Dini Yake na wahyi Wake, na waaminiwa wa Mwenyezi Mungu baina yenu nyinyi kwa nyinyi, na wenye kufikisha ujumbe Wake kwa walimwengu wote, Kiongozi wa haki alikuwepo baina yenu, hilo ni agano ambalo lilitumwa kwenu mapema, na ni lenye kubakia daima kwa ajili yenu: Na hicho (yaani: Agano hilo lililotumwa kwenu) ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu chenye kuzungumza, na ni Qur'an yenye kusema ukweli, na ni nuru inayowaka, na miale yenye kung'aa, ambapo kauli zake na hoja zake ziko wazi, (batini yake au) Siri zake za ndani zinakuwa wazi na dhahiri, na dhahiri yake ni ya kuvutia (kwa maana kwamba: Muonekano wake wa dhahiri ni wa kuvutia), Wafuasi wake (wafuasi wa Kitabu hicho) walikuwa ni wenye kuonewa wivu na walimwengu, na kukitii (au kukifuata) Kitabu hicho kunapelekea (mja) kuzifikia radhi za Mwenyezi Mungu, na kukisikiliza kitabu hicho ndiyo njia ya kuelekea kwenye wokovu.

بِهِ تُنالُ حُجَجُ اللَّهِ الْمُنَوَّرَةُ، وَ عَزائِمُهُ الْمُفَسَّرَةُ، وَ مَحارِمُهُ الْمُحَذَّرَةُ، وَ بَیِّناتُهُ الْجالِیَةُ، وَ بَراهینُهُ الْکافِیَةُ، وَ فَضائِلُهُ الْمَنْدُوبَةُ، وَ رُخَصُهُ الْمَوْهُوبَةُ، وَ شَرائِعُهُ الْمَکْتُوبَةُ.

Kwa njia hiyo (kupitia kitabu hicho, yaani: Qur’an), inawezekana kurejelea dalili (na hoja) za Mwenyezi Mungu zenye kung'ara, na wajibu (faradhi) zilizofasiriwa (kubainishwa wazi), na (makatazo yake) miiko yake iliyoharamishwa kufanyika (na kutendeka), na pia bayani zake zilizokuwa dhahiri, na dalili (hoja) zake za kutosha, na fadhila zake zenye kupendeza, na ruhusa zake zilizotolewa, na sheria zake zilizoandikwa na kufaradhishwa.

فَجَعَلَ اللَّهُ الْایمانَ تَطْهیراً لَکُمْ مِنَ الشِّرْکِ، وَ الصَّلاةَ تَنْزیهاً لَکُمْ عَنِ الْکِبْرِ، وَ الزَّکاةَ تَزْکِیَةً لِلنَّفْسِ وَ نِماءً فِی الرِّزْقِ، وَ الصِّیامَ تَثْبیتاً لِلْاِخْلاصِ، وَ الْحَجَّ تَشْییداً لِلدّینِ، وَ الْعَدْلَ تَنْسیقاً لِلْقُلُوبِ، وَ طاعَتَنا نِظاماً لِلْمِلَّةِ، وَ اِما مَتَنا اَماناً لِلْفُرْقَةِ، وَ الْجِهادَ عِزّاً لِلْاِسْلامِ، وَ الصَّبْرَ مَعُونَةً عَلَی اسْتیجابِ الْاَجْرِ.

Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupeni imani ili kukutakaseni na ushirikina, na Sala ili kukutakaseni na kiburi, na zaka ili kuzitakasa nafsi zenu na kuongeza riziki (zenu), na saumu ili kuimarisha ikhlasi, na Hija kwa ajili ya kuimarisha dini, na akafanya uadilifu kwa ajili ya uponyaji wa nyoyo, na utiifu (wenu) kwetu sisi (Ahlul-Bayt) akaufanya kuwa ni wenye kuifanya familia hii iweze kusimamisha nidhamu na utaratibu (sahihi) wa dini, na akaufanya Uimamu wetu uwe ni sababu ya kuondoa mifarakano, na akaifanya Jihad kuwa ni heshima ya Uislamu, na akaifanya subira iwe ni yenye kusaidia kuleta (ujira na) thawabu (kwa mja).

وَ الْاَمْرَ بِالْمَعْرُوفِ مَصْلِحَةً لِلْعامَّةِ، وَ بِرَّ الْوالِدَیْنِ وِقایَةً مِنَ السَّخَطِ، وَ صِلَةَ الْاَرْحامِ مَنْساءً فِی الْعُمْرِ وَ مَنْماةً لِلْعَدَدِ، وَ الْقِصاصَ حِقْناً لِلدِّماءِ، وَ الْوَفاءَ بِالنَّذْرِ تَعْریضاً لِلْمَغْفِرَةِ، وَ تَوْفِیَةَ الْمَکائیلِ وَ الْمَوازینِ تَغْییراً لِلْبَخْسِ. Na kuamrisha mema kwa manufaa ya umma, na kuwafanyia wema wazazi (wawili) kwa ajili ya kuepukana na ghadhabu za Mwenyezi Mungu, na akajaalia kuunda udugu kuwe ni sababu ya kurefusha umri (wa mja), na kuongeza idadi ya watu, na Qisas (kulipiza Kisasi kwa waovu au wauaji kwa dhulma) kuwa ni njia ya kuhifadhi damu (za watu, kwa sababu muuaji akijua akiua naye atauliwa, anajizuia na mauaji yake, na hivyo damu za watu zinakuwa zimehifadhika), na akafanya (kutekeleza na) kutimiza nadhiri iwe ni sababu ya kupatikana kwa msamaha wa Mwenyezi Mungu, na kuwa na umakini katika usahihi wa mizani na utimilifu wa vipimo ili kuondosha uuzaji wa kupunja (na kupunguza katika mizani).

وَ النَّهْىَ عَنْ شُرْبِ الْخَمْرِ تَنْزیهاً عَنِ الرِّجْسِ، وَ اجْتِنابَ الْقَذْفِ حِجاباً عَنِ اللَّعْنَةِ، وَ تَرْکَ السِّرْقَةِ ایجاباً لِلْعِصْمَةِ، وَ حَرَّمَ اللَّهُ الشِّرْکَ اِخْلاصاً لَهُ بِالرُّبوُبِیَّةِ.

Na akajaalia kuharamisha unywaji wa pombe kuwa ni njia ya kutoharika kutokana na uovu (na uchafu), na akaweka utaratibu wa kujiepusha na tuhuma (ya dhulma kwa watu wema na watakatifu) ili iwe ni kizuizi (kwa watu) kutotumbukia katika laana ( na kuwa mbali na rehema) ya Mwenyezi Mungu, na kuacha wizi kuwa ni njia ya utakaso, na akaharamisha ushirikina (shirki) ili watu wawe na ikhlasu katika Tauhidi.

فَاتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقاتِهِ، وَ لا تَمُوتُنَّ اِلاَّ وَ اَنْتُمْ مُسْلِمُونَ، وَ اَطیعُوا اللَّهَ فیما اَمَرَکُمْ بِهِ وَ نَهاکُمْ عَنْهُ، فَاِنَّهُ اِنَّما یَخْشَی اللَّهَ مِنْ عِبادِهِ الْعُلَماءُ.

Basi mcheni Mwenyezi Mungu haki ya kumcha (ipasavyo), wala msiondoke hapa duniani (msife) isipokuwa mkiwa ni Mwislamu. Na mtiini Mwenyezi Mungu katika yale aliyokuamrisheni kwayo na yale aliyokukatazeni kuyatenda, kwani kwa hakika ni wale wenye elimu tu ndio wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu.

ثم قالت:

Kisha akasema:

اَیُّهَا النَّاسُ! اِعْلَمُوا اَنّی فاطِمَةُ وَ اَبی‏مُحَمَّدٌ، اَقُولُ عَوْداً وَ بَدْءاً، وَ لا اَقُولُ ما اَقُولُ غَلَطاً، وَ لا اَفْعَلُ ما اَفْعَلُ شَطَطاً، لَقَدْ جاءَکُمْ رَسُولٌ مِنْ اَنْفُسِکُمْ عَزیزٌ عَلَیْهِ ما عَنِتُّمْ حَریصٌ عَلَیْکُمْ بِالْمُؤْمِنینَ رَؤُوفٌ رَحیمٌ. فَاِنْ تَعْزُوهُ وَتَعْرِفُوهُ تَجِدُوهُ اَبی دُونَ نِسائِکُمْ،وَ اَخَا ابْنِ عَمّی دُونَ رِجالِکُمْ، وَ لَنِعْمَ الْمَعْزِىُّ اِلَیْهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَیْهِ وَ الِهِ. فَبَلَّغَ الرِّسالَةَ صادِعاً بِالنَّذارَةِ، مائِلاً عَنْ مَدْرَجَةِ الْمُشْرِکینَ، ضارِباً ثَبَجَهُمْ، اخِذاً بِاَکْظامِهِمْ، داعِیاً اِلى سَبیلِ رَبِّهِ بِالْحِکْمَةِ و الْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ، یَجُفُّ الْاَصْنامَ وَ یَنْکُثُ الْهامَّ، حَتَّى انْهَزَمَ الْجَمْعُ وَ وَ لَّوُا الدُّبُرَ.

Enyi watu! Jueni (na tambueni) kuwa mimi ni Fatimah na Baba yangu ni Muhammad, niliyoyasema hapo mwanzo, ninayasema pia mwishoni, maneno yangu hayakuwa mabaya (hayakuwa na makosa) na wala hayana dhuluma ndani yake, amekujieni Mtume Muhammad (s.a.w.w) akitoka miongoni mwenu, akiwa ni mwenye kujali mateso yenu na mwenye kukuhurumieni, na ni mpole na mwenye huruma kwa Waumini.Kwa hiyo mkimjua, basi kwa hakika mtajua kwamba alikuwa ni Baba yangu na sio (Baba wa) wanawake wenu, na ni ndugu ya mtoto wa Ami yangu na sio (Ami ya yeyote miongoni mwa) wanaume wenu, ni uzuri ulioje na ni heshima kubwa iliyoje kuwa mimi nina uhusiano huu pamoja naye (Amani ya iwe juu yake na Aali zake). Alitekeleza kazi yake (Alifikisha ujumbe wake) na kuonya, alijitenga na kuwa mbali na shimo la washirikina, akawapiga kwa upanga wake, akayashika makoo yao, na akawalingania kuelekea katika njia ya Mola wake Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, akayaangamiza masanamu yao, na akavivunja mbali vichwa vya wale waliokuwa na vinyongo (madhalimu), mpaka (kundi lao) wakatawanyika na kukimbia kutoka katika uwanja wa mapambano.

حَتَّى تَفَرََّى اللَّیْلُ عَنْ صُبْحِهِ، وَ اَسْفَرَ الْحَقُّ عَنْ مَحْضِهِ، و نَطَقَ زَعیمُ‏الدّینِ، وَ خَرَسَتْ شَقاشِقُ الشَّیاطینِ، وَ طاحَ وَ شیظُ النِّفاقِ، وَ انْحَلَّتْ عُقَدُ الْکُفْرِ وَ الشَّقاقِ، وَ فُهْتُمْ بِکَلِمَةِ الْاِخْلاصِ فی نَفَرٍ مِنَ الْبیضِ الْخِماصِ.

Mpaka asubuhi angavu ikatoka kwenye pazia la usiku, na Haki ikaondoa pazia usoni mwake, mtawala wa dini akazungumza, na mayowe ya mashetani yakanyamazishwa, mwiba wa unafiki ukaondolewa kwenye njia, na mafundo ya ukafiri na mgawanyiko yakafunguka, na midomo yenu ikafunguka kwa neno ikhlasi, katikati ya kundi (la watu) ambalo matumbo yao yalikuwa yameshikamana na migongo yao.

وَ کُنْتُمْ عَلى شَفا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ، مُذْقَةَ الشَّارِبِ، وَ نُهْزَةَ الطَّامِعِ، وَ قُبْسَةَ الْعِجْلانِ، وَ مَوْطِی‏ءَ الْاَقْدامِ، تَشْرَبُونَ الطَّرْقَ، وَ تَقْتاتُونَ الْقِدَّ، اَذِلَّةً خاسِئینَ، تَخافُونَ اَنْ یَتَخَطَّفَکُمُ النَّاسُ مِنْ حَوْلِکُمْ، فَاَنْقَذَکُمُ اللَّهُ تَبارَکَ وَ تَعالی بِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَیْهِ وَ الِهِ بَعْدَ اللَّتَیَّا وَ الَّتی، وَ بَعْدَ اَنْ مُنِیَ بِبُهَمِ الرِّجالِ، وَ ذُؤْبانِ الْعَرَبِ، وَ مَرَدَةِ اَهْلِ الْکِتابِ. کُلَّما اَوْقَدُوا ناراً لِلْحَرْبِ اَطْفَأَهَا اللَّهُ، اَوْ نَجَمَ قَرْنُ الشَّیْطانِ، اَوْ فَغَرَتْ فاغِرَةٌ مِنَ الْمُشْرِکینَ، قَذَفَ اَخاهُ فی لَهَواتِها، فَلا یَنْکَفِی‏ءُ حَتَّى یَطَأَ جِناحَها بِأَخْمَصِهِ، وَ یَخْمِدَ لَهَبَها بِسَیْفِهِ، مَکْدُوداً فی ذاتِ اللَّهِ، مُجْتَهِداً فی اَمْرِ اللَّهِ، قَریباً مِنْ رَسُولِ‏اللَّهِ، سَیِّداً فی اَوْلِیاءِ اللَّهِ، مُشَمِّراً ناصِحاً مُجِدّاً کادِحاً، لا تَأْخُذُهُ فِی اللَّهِ لَوْمَةَ لائِمٍ. وَ اَنْتُمَ فی رَفاهِیَّةٍ مِنَ الْعَیْشِ، و ادِعُونَ فاکِهُونَ آمِنُونَ، تَتَرَبَّصُونَ بِنَا الدَّوائِرَ، وَ تَتَوَکَّفُونَ الْاَخْبارَ، وَ تَنْکُصُونَ عِنْدَ النِّزالِ، وَ تَفِرُّونَ مِنَ الْقِتالِ.

Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto, na mlikuwa kama fundo la maji, na mlikuwa kwenye hatari ya tamaa ya wenye pupa (na tamaa), na mlikuwa kama moto unaowaka na kuzimika mara moja (moja kwa moja), na mlikuwa sehemu ya kukanyagwa na watembea kwa miguu, mlikuwa mnakunywa maji yaliyochafuliwa na Ngamia, na mlikitumia magome ya miti kama chakula, mlidharauliwa na kukataliwa, na mlikuwa mkiogopa kutekwa (na kunyakuliwa) na watu waliokuwa karibu nanyi, mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu alipokuokoeni kupitia Mtume Muhammad (s.a.w.w) baada ya kudumu kwenu katika hali ngumu kama hizo, na baada ya kuteseka kwenu vya kutosha mkiwa mikononi mwa wale mbwa mwitu wenye nguvu wa kiarabu (Waarabu Madhalimu) na waasi wa Ahlul- Kitābi. Kila walipowasha moto wa vita, Mwenyezi Mungu aliuzima (moto hu), au kila Shetani alipoinua kichwa chake au joka la washirikina kila lilipokuwa likifungua kinywa chake, Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikimtupa ndugu yake ndani yake (na anafanya kazi ya kukisambaratisha kinywa hicho), na hakurudi (ndugu yake) mpaka alipovivunja vichwa vyao (washirikina hao) na kuvitupa chini na kuuzima moto wao kwa maji ya upanga wake, mpaka alichakaa (na kutaabika) kutokana na kujitahidi kwake katika njia ya Mwenyezi Mungu, alikijitahidi katika (jambo au) amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), na akiwa karibu na Mtume (Mjumbe) wa Mwenyezi Mungu, akiwa ni Bwana (Sayyid) wa mawalii wa Mwenyezi Mungu, akiwa amefunga mkanda kiunoni, na alikuwa mshauri (mwenye kutoa ushauri na nasaha), mwenye bidii na juhudi, na kamwe hakuogopa kukemea katika njia ya Mwenyezi Mungu(s.w.t). Na hii ilikuwa ni kwa wakati ule ambao nyinyi mlikuwa mkiishi kwa raha na starehe, mkifurahia kwenye kitalu salama, na mlikuwa mkitungojea tupate mateso (shida na misukosuko), mkiwa katika hali ya kusikilizia habari (kunako ni mabaya yepi yatutokee), huku mkirudi nyuma wakati wa kampeni za mapambano, na kukimbia wakati wa vita.

فَلَمَّا اِختارَ اللَّهُ لِنَبِیِّهِ دارَ اَنْبِیائِهِ وَ مَأْوى اَصْفِیائِهِ، ظَهَرَ فیکُمْ حَسْکَةُ النِّفاقِ، وَ سَمَلَ جِلْبابُ الدّینِ، وَ نَطَقَ کاظِمُ الْغاوینَ، وَ نَبَغَ خامِلُ الْاَقَلّینَ، وَ هَدَرَ فَنیقُ الْمُبْطِلینَ، فَخَطَرَ فی عَرَصاتِکُمْ، وَ اَطْلَعَ الشَّیْطانُ رَأْسَهُ مِنْ مَغْرَزِهِ، هاتِفاً بِکُمْ، فَأَلْفاکُمْ لِدَعْوَتِهِ مُسْتَجیبینَ، وَ لِلْغِرَّةِ فیهِ مُلاحِظینَ، ثُمَّ اسْتَنْهَضَکُمْ فَوَجَدَکُمْ خِفافاً، وَ اَحْمَشَکُمْ فَاَلْفاکُمْ غِضاباً، فَوَسَمْتُمْ غَیْرَ اِبِلِکُمْ، وَ وَرَدْتُمْ غَیْرَ مَشْرَبِکُمْ.

Na wakati huo pindi Mwenyezi Mungu alipomchagulia (na kumteulia) Nabii wake nyumba ya Manabii wake, na (kaburi au) makazi ya wateule wake, ishara za unafiki wenu zilionekana kwenu, na likaondolewa pazia la dini, ua ukimya wa wapotevu umevunjika (kwa maana: Wapotevu wakawa na nguvu tena na kuongea – kusambaza – upotevu wao watakavyo), na watu wa daraja ya chini (waovu) wakawa na adhama na heshima, na Ngamia wa watu wa batili akatoa sauti, na akaja majumbani mwenu, na Shetani akatoa kichwa chake katika maficho yake, na akakuiteni, na akakushuhudieni mkiitikia wito wake, na mkawa tayari kudanganywa, kisha akakuombeni muinuke (akakuaamsheni), na akakuoneni mkifanya hivyo kwa urahisi, alikukasirisheni, na akakuoneni mkiwa ni wenye kukasirika na wenye ghadhabu, basi hapo mkawaashiria Ngamia wa watu wengine, na mkaingia kwenye maji yasiyokuwa sehemu yenu.

هذا، وَ الْعَهْدُ قَریبٌ، وَالْکَلْمُ رَحیبٌ، وَ الْجُرْحُ لَمَّا یَنْدَمِلُ، وَ الرَّسُولُ لَمَّا یُقْبَرُ، اِبْتِداراً زَعَمْتُمْ خَوْفَ الْفِتْنَةِ، اَلا فِی الْفِتْنَةِ سَقَطُوا، وَ اِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحیطَةٌ بِالْکافِرینَ. فَهَیْهاتَ مِنْکُمْ، وَ کَیْفَ بِکُمْ، وَ اَنَّى تُؤْفَکُونَ، وَ کِتابُ اللَّهِ بَیْنَ اَظْهُرِکُمْ، اُمُورُهُ ظاهِرَةٌ، وَ اَحْکامُهُ زاهِرَةٌ، وَ اَعْلامُهُ باهِرَةٌ، و زَواجِرُهُ لائِحَةٌ، وَ اَوامِرُهُ واضِحَةٌ، وَ قَدْ خَلَّفْتُمُوهُ وَراءَ ظُهُورِکُمْ، أَرَغْبَةً عَنْهُ تُریدُونَ؟ اَمْ بِغَیْرِهِ تَحْکُمُونَ؟ بِئْسَ لِلظَّالمینَ بَدَلاً، وَ مَنْ یَبْتَغِ غَیْرَ الْاِسْلامِ دیناً فَلَنْ یُقْبَلَ مِنْهُ، وَ هُوَ فِی الْاخِرَةِ مِنَ الْخاسِرینِ.

Hii ilikuwa wakati ule ambapo muda mwingi ulikuwa haujapita, na pengo la jeraha lilikuwa bado ni pana, na jeraha lilikuwa bado halijapona, na wakati huo Mtume (s.a.w.w) alikuwa bado hajazikwa kaburini, mlitoa udhuru (wenu) kuwa mnaogopa fitna, fahamuni kuwa nyinyi (hivi sasa) mmo katika fitna, na kwa hakika Jahannamu imewazunguka makafiri. Ilikuwa haiwezekani kwenu kufanya hivi, na vipi mliweza kufanya hivyo, na mlikuwa mkielekea wapi, wakati Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinakukabilini (kipo mbele yenu), mambo yake yako wazi, na hukumu zake ni zenye kung'ara, na dalili za uwongofu wake zinaonekana (bayana), na makatazo yake yako wazi, na amri zake ziko wazi, lakini nyinyi kitabu hiki mmekiweka nyuma yenu, Je, mnapenda kughafilika na kutojali lolote kuhusu Kitabu hicho? Au mnataka kuhukumu kwa kitabu kisichokuwa Qur’an?. Hakika haya ni mabaya mno kwa madhalimu, na mwenye kutaka (kufuata) dini isiyokuwa Uislamu hatakubaliwa, naye na atakuwa miongoni mwa wenye hasara Akhera.

ثُمَّ لَمْ تَلْبَثُوا اِلى رَیْثَ اَنْ تَسْکُنَ نَفْرَتَها، وَ یَسْلَسَ قِیادَها، ثُمَّ اَخَذْتُمْ تُورُونَ وَ قْدَتَها، وَ تُهَیِّجُونَ جَمْرَتَها، وَ تَسْتَجیبُونَ لِهِتافِ الشَّیْطانِ الْغَوِىِّ، وَ اِطْفاءِ اَنْوارِالدّینِ الْجَلِیِّ، وَ اِهْمالِ سُنَنِ النَّبِیِّ الصَّفِیِّ، تُسِرُّونَ حَسْواً فِی ارْتِغاءٍ، وَ تَمْشُونَ لِاَهْلِهِ وَ وَلَدِهِ فِی الْخَمَرِ وَ الضَّرَّاءِ، وَ نَصْبِرُ مِنْکُمْ عَلى مِثْلِ حَزِّ الْمَدى، وَ وَخْزِالسنان‏فى‏الحشا. وَ اَنْتُمُ الانَ تَزَْعُمُونَ اَنْ لا اِرْثَ لَنا أَفَحُکْمَ الْجاهِلِیَّةِ تَبْغُونَ، وَ مَنْ اَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُکْماً لِقَومٍ یُوقِنُونَ، أَفَلا تَعْلَمُونَ؟ بَلى، قَدْ تَجَلَّى لَکُمْ کَالشَّمْسِ الضَّاحِیَةِ أَنّی اِبْنَتُهُ. اَیُّهَا الْمُسْلِمُونَ! أَاُغْلَبُ عَلى اِرْثی؟ یَابْنَ اَبی‏قُحافَةَ! اَفی کِتابِ اللَّهِ تَرِثُ اَباکَ وَ لا اَرِثُ اَبی؟ لَقَدْ جِئْتَ شَیْئاً فَرِیّاً، اَفَعَلى عَمْدٍ تَرَکْتُمْ کِتابَ اللَّهِ وَ نَبَذْتُمُوهُ وَراءَ ظُهُورِکُمْ، إذْ یَقُولُ «وَ وَرِثَ سُلَیْمانُ داوُدَ» (1) وَ قالَ فیما اقْتَصَّ مِنْ خَبَرِ زَکَرِیَّا اِذْ قالَ: «فَهَبْ لی مِنْ لَدُنْکَ وَلِیّاً یَرِثُنی وَ یَرِثُ مِنْ الِ‏یَعْقُوبَ»، (2) وَ قالَ: «وَ اوُلُوا الْاَرْحامِ بَعْضُهُمْ اَوْلی ببَعْضٍ فی کِتابِ اللَّهِ»، (3) وَ قالَ «یُوصیکُمُ اللَّهُ فی اَوْلادِکُمْ لِلذَّکَرِ مِثْلُ حَظِّ الْاُنْثَیَیْنِ»، (4) وَ قالَ «اِنْ تَرَکَ خَیْراً الْوَصِیَّةَ لِلْوالِدَیْنِ وَالْاَقْرَبَیْنِ بِالْمَعْرُوفِ حَقّاً عَلَى الْمُتَّقینَ». (5)

Kisha hamkukawia kwa muda wa kutosha ili moyo huu uliovunjika uweze kutulia, na ikawa rahisi kuuvuta, mkawasha njiti na kupepea moto ili kuuwasha, na kuitikia mwito wa shetani. Na mlikuwa tayari kuzizima nuru za Dini ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa wazi, na kuharibu (kuzipoteza kabisa) Sunna za Nabii mteule, kwa kisingizio (kwa kujifanya) kuwa mnakula, mnakula povu la maziwa lililofichwa chini ya midomo, na mlikuwa mkijificha nyuma ya vilima na miti kwa ajili ya familia yake na watoto wake, nasi ilitubidi tungojee (tuwe na uvumilivu kunako) mambo (yenu) haya, ambayo ni (machungu mno na mzito) kama vile kupigwa panga na kuchomwa na mkuki na ukapenya katikati ya tumbo. Na sasa mnafikiri kwamba hakuna urithi kwa ajili yetu, je, mnataka hukumu ya kijahiliyya?, na ni hukumu gani iliyo juu zaidi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa watu wa yakini?!. Je, hamjui hilo?, hali yakuwa hilo liko wazi kwenu kama vile uwazi wa jua linalowaka, ya kwamba mimi ni binti yake (huyo Mtume Muhammad s.a.w.w).

Enyi Waislamu! Je, inafaa kuninyang'anya urithi wa Baba yangu?, ewe mwana wa Abi Quhafa!, je, hili lipo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwamba wewe uwe na haki ya urithi kutoka kwa baba yako na mimi ninyimwe urithi wa Baba yangu?!. Kwa hakika umeleta kitu kipya na kibaya, je, ni kwa makusudi mnakiacha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukiweka nyuma ya migongo yenu?!. Je, Qur’an si imesema: “Na Suleiman akarithi kutoka kwa Daudi”{1}, na kuhusu hadithi ya Zakaria aliposema: “Mola nipe mtoto ili anirithi mimi na ukoo wa Yaaqub”{2}, Na akasema (s.w.t): "Na jamaa (ndugu) wa tumbo wanastahiki (ni aula) wao kwa wao (wenyewe kwa wenyewe) kuliko wengine" {3}, na akasema: “Mwenyezi Mungu anawausia juu ya watoto wenu; fungu la Mwanaume ni kama fungu la wanawake wawili” {4}, na akasema: “Mmeandikiwa mmoja wenu anapofikiwa na mauti, kama akiacha mali, kuwausia kitu wazazi wawili na akraba kwa namna nzuri (inayokubalika), na haya (hukumu hii) ni haki kwa Wacha Mungu”{5}.

وَ زَعَمْتُمْ اَنْ لا حَظْوَةَ لی، وَ لا اَرِثُ مِنْ اَبی، وَ لا رَحِمَ بَیْنَنا، اَفَخَصَّکُمُ اللَّهُ بِایَةٍ اَخْرَجَ اَبی مِنْها؟ اَمْ هَلْ تَقُولُونَ: اِنَّ اَهْلَ مِلَّتَیْنِ لا یَتَوارَثانِ؟ اَوَ لَسْتُ اَنَا وَ اَبی مِنْ اَهْلِ مِلَّةٍ واحِدَةٍ؟ اَمْ اَنْتُمْ اَعْلَمُ بِخُصُوصِ الْقُرْانِ وَ عُمُومِهِ مِنْ اَبی وَابْنِ عَمّی؟ فَدُونَکَها مَخْطُومَةً مَرْحُولَةً تَلْقاکَ یَوْمَ حَشْرِکَ. فَنِعْمَ الْحَکَمُ اللَّهُ، وَ الزَّعیمُ مُحَمَّدٌ، وَ الْمَوْعِدُ الْقِیامَةُ، وَ عِنْدَ السَّاعَةِ یَخْسِرُ الْمُبْطِلُونَ، وَ لا یَنْفَعُکُمْ اِذْ تَنْدِمُونَ، وَ لِکُلِّ نَبَأٍ مُسْتَقَرٌّ، وَ لَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَنْ یَأْتیهِ عَذابٌ یُخْزیهِ، وَ یَحِلُّ عَلَیْهِ عَذابٌ مُقیمٌ.

Na mnafikiri (mnadhani) kwamba mimi sina maslahi (na hadhi yoyote ya kuridhi), na sina sehemu yoyote ya urithi kwa Baba yangu, na hakuna udugu kati yetu, au Mwenyezi Mungu amekuteremshia Aya iliyomtoa baba yangu?!, Au mnasema kuwa: Watu wa dini mbili hawarithiana?!, Je, mimi na Baba yangu sio watu wa dini moja?!, au nyinyi ni wajuzi zaidi wa Qur’an mnajua Aamu na Khasu ya Qur’an kuliko Baba yangu na Mtoto wa Binamu yangu?!, Sasa wewe na huyu Ngamia, Ngamia aliyefungwa na kuachiliwa, mshike na umchukue, atakutana nawe Siku ya Kiyama. Ni uzuri ulioje kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mwamuzi (Hakimu) bora, na maombi mema na ya kheri ni ya Mtume Muhammad, na ni ahadi nzuri iliyoje ya (uwepo wa) Siku ya Kiyama, na katika saa hiyo na Siku hiyo watu wa batili watateseka mno, na majuto (siku hiyo) hayatakunufaisheni (kwa lolote), na kila habari ina mahali pake, kisha mtajua juu ya kichwa cha nani itashuka adhabu yenye kufedhehesha, na adhabu ya milele inayojumuisha.

ثم رمت بطرفها نحو الانصار، فقالت:

یا مَعْشَرَ النَّقیبَةِ وَ اَعْضادَ الْمِلَّةِ وَ حَضَنَةَ الْاِسْلامِ! ما هذِهِ الْغَمیزَةُ فی حَقّی وَ السِّنَةُ عَنْ ظُلامَتی؟ اَما کانَ رَسُولُ‏اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَیْهِ وَ الِهِ اَبی یَقُولُ: «اَلْمَرْءُ یُحْفَظُ فی وُلْدِهِ»، سَرْعانَ ما اَحْدَثْتُمْ وَ عَجْلانَ ذا اِهالَةٍ، وَ لَکُمْ طاقَةٌ بِما اُحاوِلُ، وَ قُوَّةٌ عَلى ما اَطْلُبُ وَ اُزاوِلُ.اَتَقُولُونَ ماتَ مُحَمَّدٌ؟ فَخَطْبٌ جَلیلٌ اِسْتَوْسَعَ وَ هْنُهُ، وَاسْتَنْهَرَ فَتْقُهُ، وَ انْفَتَقَ رَتْقُهُ، وَ اُظْلِمَتِ الْاَرْضُ لِغَیْبَتِهِ، وَ کُسِفَتِ الشَّمْسُ وَ الْقَمَرُ وَ انْتَثَرَتِ النُّجُومُ لِمُصیبَتِهِ، وَ اَکْدَتِ الْامالُ، وَ خَشَعَتِ الْجِبالُ، وَ اُضیعَ الْحَریمُ، وَ اُزیلَتِ الْحُرْمَةُ عِنْدَ مَماتِهِ.فَتِلْکَ وَاللَّهِ النَّازِلَةُ الْکُبْرى وَ الْمُصیبَةُ الْعُظْمى، لامِثْلُها نازِلَةٌ، وَ لا بائِقَةٌ عاجِلَةٌ اُعْلِنَ بِها، کِتابُ اللَّهِ جَلَّ ثَناؤُهُ فی اَفْنِیَتِکُمْ، وَ فی مُمْساکُمْ وَ مُصْبِحِکُمْ، یَهْتِفُ فی اَفْنِیَتِکُمْ هُتافاً وَ صُراخاً وَ تِلاوَةً وَ اَلْحاناً، وَ لَقَبْلَهُ ما حَلَّ بِاَنْبِیاءِ اللَّهِ وَ رُسُلِهِ، حُکْمٌ فَصْلٌ وَ قَضاءٌ حَتْمٌ.«وَ ما مُحَمَّدٌ اِلاَّ رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ اَفَاِنْ ماتَ اَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلى اَعْقابِکُمْ وَ مَنْ یَنْقَلِبْ عَلى عَقِبَیْهِ، فَلَنْ یَضُرَّ اللَّهَ شَیْئاً وَ سَیَجْزِى اللَّهُ شَیْئاً وَ سَیَجْزِى اللَّهُ الشَّاکِرینَ». (6) Kisha (Sayyidat Fatima s.a) akawageukia Ansari na kusema:

Enyi kundi la watukufu, na enyi mikono (silaha) ya umma, enyi watetezi wa Uislamu, kwa nini (mnaonyesha) udhaifu huu na kupuuzwa (huku) kuhusiana na haki yangu, na kupuuzwa huku kwa uadilifu wangu?!, Je, Baba yangu Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakusema: “Hadhi ya kila mtu imehifadhiwa kwa watoto wake?!, ni haraka iliyoje kwenu nyinyi kufanya vitendo hivi?, na ni kwa haraka iliyoje mbuzi huyu mwembamba, maji yanadondoka na kutoka kinywani na puani mwake?!, hali ya kuwa mkiwa na nguvu na uwezo juu ya kile tunachojaribu (kukipigania na) kukifikia, na nguvu ya kuniunga mkono katika madai yangu (katika hitajio langu hili) na nia yangu mnayo, au mnataka kusema kuwa Muhammad (Rehema na Amani ziwe juu yake na Aali zake) amekufa?!, na kwamba “Huu ni msiba mkubwa, na mwisho wa siku pengo lake ni kubwa, nyufa zake ni nyingi, na mishono yake imepasuka, na ardhi ikawa giza kabisa kwa kutokuwepo kwake, na nyota kutokuwa na utulivu, na ndoto zimegeuka na kuwa kukata tamaa, na milima kuanguka, na utakatifu kukanyagwa, na hakuna heshima iliyoachwa kwa mtu yeyote baada ya kifo chake"?!. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba msiba huo ni ni mzito zaidi na mkubwa zaidi, na kwamba hakuna msiba kama huo, na maafa ya vita katika ulimwengu huu kamwe hayafikii msingi wake, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kimelifunua hilo (na kuliweka wazi), Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho mnakisoma majumbani mwenu, na katika mikusanyiko yenu ya usiku na mchana, na kwa utulivu na kwa sauti kubwa, na kwa kisomo cha tartili na kuimba, hakika huu ni msiba ambao uliwapata Manabii na Mitume hapo kabla, kwa hakika Hukumu ni ya hakika (lazima itakuwa), na ni hukumu ya uhakika, Mwenyezi Mungu amesema: “Muhammad ni Nabii ambaye Manabii wengine walikufa (walipita) kabla yake, basi akifa (Muhammad) au akiuawa nyinyi mtarejea (nyuma kwenye visigino vyenu - mtarejea kwenye ukafiri wenu), na mwenye kurudi nyuma hatamdhuru Mwenyezi Mungu (kwa lolote), na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru"{6}.

ایهاً بَنی‏قیلَةَ! ءَ اُهْضَمُ تُراثَ اَبی وَ اَنْتُمْ بِمَرْأى مِنّی وَ مَسْمَعٍ وَ مُنْتَدى وَ مَجْمَعٍ، تَلْبَسُکُمُ الدَّعْوَةُ وَ تَشْمَلُکُمُ الْخُبْرَةُ، وَ اَنْتُمْ ذَوُو الْعَدَدِ وَ الْعُدَّةِ وَ الْاَداةِ وَ الْقُوَّةِ، وَ عِنْدَکُمُ السِّلاحُ وَ الْجُنَّةُ، تُوافیکُمُ الدَّعْوَةُ فَلا تُجیبُونَ، وَ تَأْتیکُمُ الصَّرْخَةُ فَلا تُغیثُونَ، وَ اَنْتُمْ مَوْصُوفُونَ بِالْکِفاحِ، مَعْرُوفُونَ بِالْخَیْرِ وَ الصَّلاحِ، وَ النُّخْبَةُ الَّتی انْتُخِبَتْ، وَ الْخِیَرَةُ الَّتِی اخْتیرَتْ لَنا اَهْلَ الْبَیْتِ. Enyi Bani Qiyla – ni kundi la Ansari – je, nidhulumiwe kuhusiana na mirathi ya Baba yangu na nyinyi mnaniona na mnasikia maneno yangu?!, Nanyi mna chama cha kijamii, nyote mlisikia wito wangu na mnajua kabisa kuhusu hali yangu, na mna watu na hifadhi, na mna zana (mbalimbali za kijeshi) na nguvu, mnazo silaha, na ngao, sauti ya wito wangu imewafikia, lakini hamjibu!, na mmesikia kilio cha wito wangu, lakini hamkuitikia kilio change!, hali ya kuwa nyinyi mnajulikana kwa ushujaa, na mnasifika kwa kheri na wema wenu, na nyinyi ndio mliochaguliwa, na ni wateule mlioteuliwa kwa ajili yetu Ahlul-Bayt!

قاتَلْتُمُ الْعَرَبَ، وَ تَحَمَّلْتُمُ الْکَدَّ وَ التَّعَبَ، وَ ناطَحْتُمُ الْاُمَمَ، وَ کافَحْتُمُ الْبُهَمَ، لا نَبْرَحُ اَوْ تَبْرَحُونَ، نَأْمُرُکُمْ فَتَأْتَمِرُونَ، حَتَّى اِذا دارَتْ بِنا رَحَى الْاِسْلامِ، وَ دَرَّ حَلَبُ الْاَیَّامِ، وَ خَضَعَتْ نُعْرَةُ الشِّرْکِ، وَ سَکَنَتْ فَوْرَةُ الْاِفْکِ، وَ خَمَدَتْ نیرانُ الْکُفْرِ، وَ هَدَأَتْ دَعْوَةُ الْهَرَجِ، وَ اسْتَوْسَقَ نِظامُ الدّینِ، فَاَنَّى حِزْتُمْ بَعْدَ الْبَیانِ، وَاَسْرَرْتُمْ بَعْدَ الْاِعْلانِ، وَ نَکَصْتُمْ بَعْدَ الْاِقْدامِ، وَاَشْرَکْتُمْ بَعْدَ الْایمانِ؟ بُؤْساً لِقَوْمٍ نَکَثُوا اَیْمانَهُمْ مِنْ بَعْدِ عَهْدِهِمْ، وَ هَمُّوا بِاِخْراجِ الرَّسُولِ وَ هُمْ بَدَؤُکُمْ اَوَّلَ مَرَّةٍ، اَتَخْشَوْنَهُمْ فَاللَّهُ اَحَقُّ اَنْ تَخْشَوْهُ اِنْ کُنْتُمْ مُؤمِنینَ.اَلا، وَ قَدْ أَرى اَنْ قَدْ اَخْلَدْتُمْ اِلَى الْخَفْضِ، وَ اَبْعَدْتُمْ مَنْ هُوَ اَحَقُّ بِالْبَسْطِ وَ الْقَبْضِ، وَ خَلَوْتُمْ بِالدَّعَةِ، وَ نَجَوْتُمْ بِالضّیقِ مِنَ السَّعَةِ، فَمَجَجْتُمْ ما وَعَبْتُمْ، وَ دَسَعْتُمُ الَّذى تَسَوَّغْتُمْ، فَاِنْ تَکْفُرُوا اَنْتُمْ وَ مَنْ فِی الْاَرْضِ جَمیعاً فَاِنَّ اللَّهَ لَغَنِیٌّ حَمیدٌ.اَلا، وَ قَدْ قُلْتُ ما قُلْتُ هذا عَلى مَعْرِفَةٍ مِنّی بِالْخِذْلَةِ الَّتی خامَرْتُکُمْ، وَ الْغَدْرَةِ الَّتِی اسْتَشْعَرَتْها قُلُوبُکُمْ، وَ لکِنَّها فَیْضَةُ النَّفْسِ، وَ نَفْثَةُ الْغَیْظِ، وَ حَوَزُ الْقَناةِ، وَ بَثَّةُ الصَّدْرِ، وَ تَقْدِمَةُ الْحُجَّةِ، فَدُونَکُمُوها فَاحْتَقِبُوها دَبِرَةَ الظَّهْرِ، نَقِبَةَ الْخُفِّ، باقِیَةَ الْعارِ، مَوْسُومَةً بِغَضَبِ الْجَبَّارِ وَ شَنارِ الْاَبَدِ، مَوْصُولَةً بِنارِ اللَّهِ الْمُوقَدَةِ الَّتی تَطَّلِعُ عَلَى الْاَفْئِدَةِ.فَبِعَیْنِ اللَّهِ ما تَفْعَلُونَ، وَ سَیَعْلَمُ الَّذینَ ظَلَمُوا اَىَّ مُنْقَلَبٍ یَنْقَلِبُونَ،وَ اَنَا اِبْنَةُ نَذیرٍ لَکُمْ بَیْنَ یَدَىْ عَذابٌ شَدیدٌ، فَاعْمَلُوا اِنَّا عامِلُونَ، وَ انْتَظِرُوا اِنَّا مُنْتَظِرُونَ. فأجابها أبوبکر عبداللَّه بن عثمان، وقال:

Mlipigana na Waarabu na mkastahimili matatizo (shida na tabu), na mlipigana na mataifa na mkapigana na wapiganaji mashujaa, daima mmekuwa ni makamanda nanyi ni watu watiifu (mnatutii tunapowaamuru), mpaka Uislamu ukasambaa na kuenea Asia, na (matiti ya zama yakatoa maziwa au) kifua cha zama kikaja kukamuliwa maziwa, na kelele za ushirikina (shirki) zikanyamazishwa, na chungu cha (tamaa) ubakhili na kashfa (tuhuma) kikaacha kuchemka, na moto wa ukafiri ulizimika na mwito (au wito) wa machafuko ukatulia, na (nidhamu au) mfumo wa dini ukawiana kabisa, basi ni kwa nini mnatahayari (na kubabaika) baada ya kukiri kwenu na kuwa imani?!, na baada ya kujidhihirisha kwenu mnarudi tena kujificha?!, na baada ya kupiga hatua mbele, mnarudi nyuma, kisha mkaamini ushirikina (mkarudi kwenye shirki). Ole wao kundi (la wale watu) lililovunja mapatano baada ya kuyafanya, na wakataka kumfukuza na kumuondoa Mtume, ijapokuwa ni wao walioanzisha vita, je, mnawaogopa hao na hali Mwenyezi Mungu Ndiye anayestahiki zaidi kumuogopa?!, ikiwa kweli nyinyi ni Muumini?!. Tambueni!, Mimi ninaona kuwa mmeweka mioyo yenu kwenye urahisi wa milele, na mmemkataa yule aliyestahili kutawala (kuongoza), mmestaafu kwa urahisi, na mmefikia uhuru wake kutoka kwa wembamba wa maisha, matokeo yake, mlichokuwa mmekihifadhi kilitoka kupitia kinywani mwenu, na kile mlichokimeza kikarudishwa (mkakitema), basi jueni kwamba ikiwa nyinyi na wote waliomo duniani mtakuwa makafiri, Mwenyezi Mungu Ndiye Mkuu anayehitajiwa na kila mtu na kusifiwa (na kuhimidiwa) na wote. Fahamuni kuwa (hiki) nilichokisema nimekisema kwa ufahamu kamili, kwa ulegevu uliotokea katika maadili yenu, na ukosefu wa uaminifu na hila uliotokea mioyoni mwenu, lakini haya ni mchemko wa moyo wa huzuni, na kumwagika kwa hasira na ghadhabu, na (ni) kile kisichoweza kuvumiliwa, na ni kuchemka kwa kifua change, na ni usemi wa kuweka wazi hoja na dalili, basi uchukueni ukhalifa, lakini jueni kwamba kuna jeraha kwenye mgongo wa Ngamia huyu wa Ukhalifa, na mguu wake una tundu na malengelenge, na aibu na fedheha yake imebakia, na ni dalili ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na fedheha ya milele, na umeunganishwa na moto uwakao wa Mwenyezi Mungu unaozingira nyoyo, unakichofanya kiko mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu. Na walio dhulumu watajua ni mahali gani watarejea, na mimi ni Binti wa aliye kujulisheni kunako adhabu chungu ya Mwenyezi Mungu iliyo mbele yenu, kwa hiyo, fanya chochote unachotaka kufanya, na sisi tutafanya kazi yetu, na subiri (uone kitakachokuja kukutokea) nasi pia tubaki tukiwa ni wenye kusubiri. Abu Bakr bin Abdullah ibn Othman (Ibn Abi Quḥāfa) akamjibu (Sayyidat Fatima –s.a–) kwa kusema:

یا بِنْتَ رَسُولِاللَّـهِ! لَقَدْ كانَ اَبُوكِ بِالْمُؤمِنینَ عَطُوفاً كَریماً، رَؤُوفاً رَحیماً، وَ عَلَی الْكافِرینَ عَذاباً اَلیماً وَ عِقاباً عَظیماً، اِنْ عَزَوْناهُ وَجَدْناهُ اَباكِ دُونَ النِّساءِ، وَ اَخا اِلْفِكِ دُونَ الْاَخِلاَّءِ، اثَرَهُ عَلی كُلِّ حَمیمٍ وَ ساعَدَهُ فی كُلِّ اَمْرٍ جَسیمِ، لایحِبُّكُمْ اِلاَّ سَعیدٌ، وَ لایبْغِضُكُمْ اِلاَّ شَقِی بَعیدٌ. فَاَنْتُمْ عِتْرَةُ رَسُولِاللَّـهِ الطَّیبُونَ، الْخِیرَةُ الْمُنْتَجَبُونَ، عَلَی الْخَیرِ اَدِلَّتُنا وَ اِلَی الْجَنَّةِ مَسالِكُنا، وَاَنْتِ یا خِیرَةَ النِّساءِ وَ ابْنَةَ خَیرِ الْاَنْبِیاءِ، صادِقَةٌ فی قَوْلِكِ، سابِقَةٌ فی وُفُورِ عَقْلِكِ، غَیرَ مَرْدُودَةٍ عَنْ حَقِّكِ، وَ لامَصْدُودَةٍ عَنْ صِدْقِكِ. وَ اللَّـهِ ما عَدَوْتُ رَأْی رَسُولِاللَّـهِ، وَ لاعَمِلْتُ اِلاَّ بِاِذْنِهِ، وَ الرَّائِدُ لایكْذِبُ اَهْلَهُ، وَ اِنّی اُشْهِدُ اللَّـهَ وَ كَفی بِهِ شَهیداً، اَنّی سَمِعْتُ رَسُولَاللَّـهِ یقُولُ: «نَحْنُ مَعاشِرَ الْاَنْبِیاءِ لانُوَرِّثُ ذَهَباً وَ لافِضَّةًّ، وَ لاداراً وَ لاعِقاراً، وَ اِنَّما نُوَرِّثُ الْكِتابَ وَ الْحِكْمَةَ وَ الْعِلْمَ وَ النُّبُوَّةَ، وَ ما كانَ لَنا مِنْ طُعْمَةٍ فَلِوَلِی الْاَمْرِ بَعْدَنا اَنْ یحْكُمَ فیهِ بِحُكْمِهِ». Ewe Binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba yako alikuwa mwema na mkarimu, mpole na mwenye huruma kwa waumini, na mwenye adhabu kali na kubwa kwa makafiri. Tukiutazama ukoo wake, tunamkuta yeye ni Baba yako na si baba kwa wanawake zetu, na miongoni mwa marafiki tunamkuta akiwa ni kaka wa mume wako (na si kaka wa wanaume wetu), ambaye alimfanya (mume wako) kuwa bora kuliko rafiki yeyote, na pia alimsaidia Mtume (s.a.w.w) katika kila kazi kubwa, hawakupendeni ila wale wenye furaha, na hawakuchukieni ispokuwa madhalimu tu na maadui zenu. Basi kwa hakika nyinyi ni jamaa wa karibu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), nyinyi ni watoharifu na wateule wa dunia, na mnatuongoza kuelekea kwenye kheri, na mnatuongoza kuelekea Peponi. Na wewe ni Mwanamke bora kuliko wanawake wote, na ni binti wa Nabii bora zaidi kuliko Manabii wote, wewe ni mkweli na mwaminifu katika mazungumzo yako (katika yale uyasemayo), kwa wenye hekima wewe upo mbele yao (umewatangulia kwa akili na hekima), na hutozuiliwa kamwe haki yako, na hakutakuwa na kizuizi chochote cha kuzuia hotuba (au kauli) yako ya ukweli. Na Wallahi sijachukua hatua yoyote inayokwenda kinyume na uamuzi wa Mtume(s.a.w.w), na wala sikufanya nilivyofanya ispokuwa ni kwa idhini yake, na kiongozi wa watu hawadanganyi. Na ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu ambaye ndiye shahidi bora kabisa, kuwa hakika mimi nilimsikia Mtume akisema: “Sisi kundi la Manabii haturithishi dinari, dirham, nyumba wala mashamba, bali tunarithisha vitabu, hekima, elimu na unabii, ama kile tunachokiacha, kinabakia katika udhibiti wa waliyul amri baada yetu, ambaye anaweza kutoa hukumu yoyote juu yake aitakayo”.

وَ قَدْ جَعَلْنا ما حاوَلْتِهِ فِی الْكِراعِ وَ السِّلاحِ، یقاتِلُ بِهَا الْمُسْلِمُونَ وَ یجاهِدُونَ الْكُفَّارَ، وَ یجالِدُونَ الْمَرَدَةَ الْفُجَّارَ، وَذلِكَ بِاِجْماعِ الْمُسْلِمینَ، لَمْ اَنْفَرِدْ بِهِ وَحْدی، وَ لَمْ اَسْتَبِدْ بِما كانَ الرَّأْي عِنْدي، وَ هذِهِ حالی وَمالي، هِی لَكِ وَ بَینَ یدَیكِ، لاتَزْوی عَنْكِ وَ لانَدَّخِرُ دُونَكِ، وَ اَنَّكِ، وَ اَنْتِ سَیدَةُ اُمَّةِ اَبیكِ وَ الشَّجَرَةُ الطَّیبَةُ لِبَنیكِ، لایدْفَعُ مالَكِ مِنْ فَضْلِكِ، وَ لایوضَعُ فی فَرْعِكِ وَ اَصْلِكِ، حُكْمُكِ نافِذٌ فیما مَلَّكَتْ یدای، فَهَلْ‌ترین اَنْ اُخالِفَ فی ذاكَ اَباكِ (صَلَّی اللَّـهُ عَلَیهِ وَ الِهِ وَسَلَّمَ).

Na tumeweka unachokitaka (na kukidai) kuwa ni mahsusi kwa ajili ya kununua farasi na silaha, ili Waislamu wapigane (na adui kupitia silaha hizo na farasi) na kufanya jihadi dhidi ya makafiri, na wapigane na waasi na watu waovu, na uamuzi huu ulikubaliwa na Waislamu wote, na sikufanya (sikuamua) hivi peke yangu, na sikufanya (hivyi) kiholela kwa kufuata rai yangu na maoni yangu binafsi. Na hii ndiyo hali yangu na na ndio mali yangu, na ipo kwa ajili yako na katika umiliki wako, na haikuzuiliwa kwako, na haizuiliwa kwako, na haihifadhiwi kwa ajili ya mtu mwingine, na kwa hakika wewe ni Mwanamke bora Zaidi kuliko wanawake wote wa umma wa Baba yako, nawe ni mti wenye matunda na ulio safi kwa ajili ya watoto wako, fadhila zako kamwe hazijakataliwa, na matawi yako na mashina yako hayakatwi, hekima yako ina ufanisi katika kile ninachomiliki mimi, je, unataka nifanye kinyume na maneno ya Baba yako (s.a.w.w) katika jambo hili?!. فقالت:

سُبْحانَ اللَّـهِ، ما كانَ اَبی رَسُولُاللَّـهِ عَنْ كِتابِ اللَّـهِ صادِفاً، وَ لالِاَحْكامِهِ مُخالِفاً، بَلْ كانَ یتْبَعُ اَثَرَهُ، وَ یقْفُو سُوَرَهُ، اَفَتَجْمَعُونَ اِلَی الْغَدْرِ اِعْتِلالاً عَلَیهِ بِالزُّورِ، وَ هذا بَعْدَ وَفاتِهِ شَبیهٌ بِما بُغِی لَهُ مِنَ الْغَوائِلِ فی حَیاتِهِ، هذا كِتابُ اللَّـهِ حُكْماً عَدْلاً وَ ناطِقاً فَصْلاً، یقُولُ: «یرِثُنی وَ یرِثُ مِنْ الِیعْقُوبَ»، وَ یقُولُ: «وَ وَرِثَ سُلَیمانُ داوُدَ». بَینَ عَزَّ وَ جَلَّ فیما وَزَّعَ مِنَ الْاَقْساطِ، وَ شَرَعَ مِنَ الْفَرائِضِ وَالْمیراثِ، وَ اَباحَ مِنْ حَظِّ الذَّكَرانِ وَ الْاِناثِ، ما اَزاحَ بِهِ عِلَّةَ الْمُبْطِلینَ وَ اَزالَ التَّظَنّی وَ الشُّبَهاتِ فِی الْغابِرینَ، كَلاَّ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ اَنْفُسُكُمْ اَمْراً، فَصَبْرٌ جَمیلٌ وَ اللَّـهُ الْمُسْتَعانُ عَلی ما تَصِفُونَ.

Fatima (a.s) akasema:

Subhanallah (ametakasika Mwenyezi Mungu)!, Baba yangu, Mtume Muhammad(s.a.w.w), kamwe hakukiacha (nyuma) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na wala hakupingana na maamrisho yake, bali alikifuata na kuzifanyia kazi Aya zake, je, mnataka kumtuhumu (Baba yangu) kwa nguvu na kwa hila na hadaa?!, na kazi hii (jambo hili) baada ya kifo chake ni sawa na ile mitego iliyotegwa dhidi yake wakati wa uhai wake, na hiki ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambaye ni Hakimu Muadilifu, na (kitabu hiki ni) msemaji anaye farikisha (na kutenganisha) baina ya haki na batili, anasema Mwenyezi Mungu (kwamba):- Zakaria alisema: “Ewe Mwenyeezi Mungu!, nipe (niruzuku) mtoto atakayerithi mimi na ukoo wa Yakoub”. Na anasema: "Suleiman alimrithi Daudi." Na Mwenyezi Mungu ametoa maelezo ya kutosha katika mafunga aliyoyaweka, na kiasi alichopanga (ndani ya Qur’an) kuhusiana na mirathi, na manufaa aliyowawekea Wanaume na Wanawake (wanayoweza kufaidika nayo katika Mirathi), ambapo amevifanya visingizio vya uwongo vya watu wa batili, dhana na mashaka viwe ni vyenye kutoweka mpaka Siku ya Kiyama, si hivyo tu, lakini pia hisia zenu za kinyama zimeweka njia mbele ya miguu yenu, na mimi sina budi ila kuwa na subira, na Mwenyezi Mungu ni Msaidizi wetu katika kile mnachokifanya.

فقال أبوبكر:

صَدَقَ اللَّـهُ وَ رَسُولُهُ وَ صَدَقَتْ اِبْنَتُهُ، مَعْدِنُ الْحِكْمَةِ، وَ مَوْطِنُ الْهُدی وَ الرَّحْمَةِ، وَ رُكْنُ الدّینِ، وَ عَینُ الْحُجَّةِ، لااَبْعَدُ صَوابَكِ وَ لااُنْكِرُ خِطابَكِ، هؤُلاءِ الْمُسْلِمُونَ بَینی وَ بَینَكِ قَلَّدُونی ما تَقَلَّدْتُ، وَ بِاتِّفاقٍ مِنْهُمْ اَخَذْتُ ما اَخَذْتُ، غَیرَ مَكابِرٍ وَ لامُسْتَبِدٍّ وَ لامُسْتَأْثِرٍ، وَ هُمْ بِذلِكَ شُهُودٌ.

Abu Bakr akasema:

Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli, na Bintiye ambaye ndiye chimbuko la hekima na mahala pa uongofu na rehema, na nguzo ya dini na chanzo cha hoja na dalili, anasema kweli, siutupilii mbali (siupuuzi) ukweli wako na wala sikatai hotuba yako, hawa Waislamu ndio wanaohukumu baina yangu na wewe, na walinikabidhi serikali hii, na nikakubali cheo hiki kutokana na uamuzi wao (wenyewe na maafikiano yao), si (kukubali majukumu hayo yaliyotokana na maamuzi ya waislamu) kwa na kiburi wala kwa dhuluma, na wala sikujichukulia chochote kwa rai yangu binafsi, na wote ni mashahidi.

فالتفت فاطمة علیهاالسلام الی النساء، و قالت: مَعاشِرَ الْمُسْلِمینَ الْمُسْرِعَةِ اِلی قیلِ الْباطِلِ، الْمُغْضِیةِ عَلَی الْفِعْلِ الْقَبیحِ الْخاسِرِ، اَفَلاتَتَدَبَّرُونَ الْقُرْانَ اَمْ عَلی قُلُوبٍ اَقْفالُها، كَلاَّ بَلْ رانَ عَلی قُلُوبِكُمْ ما اَسَأْتُمْ مِنْ اَعْمالِكُمْ، فَاَخَذَ بِسَمْعِكُمْ وَ اَبْصارِكُمْ، وَ لَبِئْسَ ما تَأَوَّلْتُمْ، وَ ساءَ ما بِهِ اَشَرْتُمْ، وَ شَرَّ ما مِنْهُ اِعْتَضْتُمْ، لَتَجِدَنَّ وَ اللَّـهِ مَحْمِلَهُ ثَقیلاً، وَ غِبَّهُ وَ بیلاً، اِذا كُشِفَ لَكُمُ الْغِطاءُ، وَ بانَ ما وَرائَهُ الضَّرَّاءُ، وَ بَدا لَكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ ما لَمْ تَكُونُوا تَحْتَسِبُونَ، وَ خَسِرَ هُنالِكَ الْمُبْطِلُونَ.

Kisha Hadhrat Fatima (s.a) akawageukia watu na kusema:

Enyi Waislamu! Mnaofanya haraka ya kusikiliza maneno ya batili na yasiyokuwa na faida, na mnaopuuza maovu (yanayotendeka mbele yenu), hivi hamfikiri na kuwa natadaburi na Qur’an, au nyoyo zenu zimefungwa (na zimepigwa chapa)?!, Si hivyo, bali matendo yenu maovu yametia giza nyoyoni mwenu, na yakaziba masikio na macho yenu, na mkazifasiri Aya za Qur’ani kwa tafsiri (na Taawili) mbaya sana, na mkaiashiria (mkaitumia Qur’an kuelekea) njia mbaya, na mkaibadilisha na kitu kibaya (kwa maana: Mmeshikamana na kitu kibaya badala ya Qur’an). Wallahi huu mzigo ni mzito kwenu kuubeba, na mwisho wake umejaa majanga na mabalaa (kwenu), pindi pazia zitakapo ondolewa na hasara yake ikadhihirika kwenu, na yakakubainikieni yale ambayo hamkuwa mkiyazingatia, basi hapo ndipo watu wa batili watakapokuwa ni wenye kukhasirika.

ثم عطفت علی قبر النبی صلی اللَّـه علیه و آله، و قالت:

Kisha Sayyidat Fatima(s.a) akaelekea katika kaburi la Mtume(s.a.w.w), akagusa kaburi lake na kusema:

قَدْ كانَ بَعْدَكَ اَنْباءٌ وَهَنْبَثَةٌ

      لَوْ كُنْتَ شاهِدَها لَمْ تَكْثِرِ الْخُطَبُ 

اِنَّا فَقَدْ ناكَ فَقْدَ الْاَرْضِ وابِلَها

    وَ اخْتَلَّ قَوْمُكَ فَاشْهَدْهُمْ وَ لاتَغِبُ

وَ كُلُّ اَهْلٍ لَهُ قُرْبی وَ مَنْزِلَةٌ

     عِنْدَ الْاِلهِ عَلَی الْاَدْنَینِ مُقْتَرِبُ

اَبْدَتْ رِجالٌ لَنا نَجْوی صُدُورِهِمُ

      لمَّا مَضَیتَ وَ حالَتْ دُونَكَ التُّرَبُ

تَجَهَّمَتْنا رِجالٌ وَ اسْتُخِفَّ بِنا

       لَمَّا فُقِدْتَ وَ كُلُّ الْاِرْثِ مُغْتَصَبُ

وَ كُنْتَ بَدْراً وَ نُوراً یسْتَضاءُ بِهِ

    عَلَیكَ تُنْزِلُ مِنْ ذِیالْعِزَّةِ الْكُتُبُ

وَ كانَ جِبْریلُ بِالْایاتِ یؤْنِسُنا

      فَقَدْ فُقِدْتَ وَ كُلُّ الْخَیرِ مُحْتَجَبُ

فَلَیتَ قَبْلَكَ كانَ الْمَوْتُ صادِفُنا

    لَمَّا مَضَیتَ وَ حالَتْ دُونَكَ الْكُتُبُ[30] 

• Baada yako, kumekuwepo na habari na masuala (mbalimbali) ambayo yasingekuwa makubwa kama ungekuwepo (ukawa ni mwenye kuyashuhudia).

• Tumekupoteza kama nchi iliyonyimwa mvua na watu wako wametawanyika (na kugawanyika na kufarikiana), njoo uone jinsi walivyopotea.

• Kila familia inayo heshima na hadhi machoni pa Mwenyezi Mungu, na inaheshimiwa pia machoni mwa wageni, isipokuwa sisi.

• Mara tu ulipotoka, na udongo ukakufukia, baadhi ya wanaume katika jamii yako walifichua siri za vifuani mwao.

• Baada yako, watu wengine walituacha na kutudharau (au kututelekeza), na urithi wetu ukaibiwa (wakauchukua kwa nguvu).

• Na ulikuwa mwezi kumi na nne usiku, nawe ukawa taa itoayo nuru, ambapo vitabu viliteremshiwa (kwako) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

• Jibril (a.s) alikuwa Mfariji wetu kupitia Ishara (Aya) za Mwenyezi Mungu, na baada yako kila kitu kizuri kilifunikwa.

• Laiti tungelikufa kabla yako, ulipoondoka basi na vumbi likakuficha chini yake.

Rejea

Vyanzo