Kisa cha Fadak

Kutoka wikishia

Sakata na kisa cha Fadak (Kiarabu: حادثة فدك) kinahusiana na Abu Bakari kumpokonya bibi Fatima (a.s) bustani ya Fadak baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w). Abu Bakar, kupitia kisingizio cha Hadith kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) (ambayo msimulizi wake ni Abu Bakar pekee), alidai kwamba Mitume hawaachi urithi; Ila Fatima akajibu kwamba Mtume (s.a.w.w) alimpa Fadak kabla ya kifo chake na akamleta Imam Ali (a.s) na Ummu Aiman kama ni mashahidi wa kauli yake hiyo. Kwa mujibu wa wanazuoni wa Kishia na baadhi ya wanazuoni wa Kisunni, baada ya kuteremka Aya ya 26 ya Surat al-Isra, iliyomtaka Mtume (s.a.w.w) atoe haki ya Dhawil-Qurba (watu wa karibu), Mtume alimpa Fatimah Fadak.

Katika moja ya nukuu, imeelezwa kwamba Abu Bakar katika moja ya nyaraka, alikubaliana na umiliki wa Fatima juu ya ardhi ya Fadak; Lakini Omar bin Khattab aliichukua nyaraka hiyo kutoka kwa Fatima na kuirarua. Kwa mujibu wa riwaya nyingine, Abu Bakar hakuuwakubali ushahidi wa mashahidi wa Fatima (a.s). Binti ya Mtume (s.a.w.w) alipoona mashtaka yake na mumewe Imam Ali (a.s) hayana matunda, alikwenda Masjid al-Nabi na kutoa hotuba. Katika hotuba hiyo inayojulikana kwa jina la hotuba ya Fadakiyyah, alizungumzia suala la kunyakuliwa kwa ukhalifa na kuita kauli ya Abu Bakar isemayo; "Mitume hawaachi urithi" ni kauli dhidi ya Qur'an na kumwachia Mwenyezi Mungu amhukumie juu ya mashtaka yake Siku ya Kiyama. Baada ya tukio hili, Fatimah (a.s) alikasirishwa sana na Abu Bakar na Omar na akabaki na hasira juu yao mpaka alipokufa kishahidi.

Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w)), bustani ya Fadak iliangukia mikononi mwa makhalifa na wakapokezana mkono kwa mkono miongoni mwao. Bila shaka, baadhi ya makhalifa, akiwemo Omar bin Abdulaziz Amawiy na Maamun Abbasi, waliirjesha Fadak au walitoa mapato kutoka kwayo na kuwapa watoto wa bibi Fatima, ingawaje hatimae makhalifa wa baadae waliirudisha Fadak kwa warithi wake.

Kuna maandishi mengi yalioandikwa kuhusu tukio hili, ambayo baadhi ni kwa Kiarabu na baadhi yake ni kwa lugha ya Kiajemi. Miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kuhusiana na hilo ni; Fadak fi al-Tarikh, cha Sayyied Muhammad Sadri, ambacho kimeandikwa kwa njia ya uchambuzi. Baqir Sadri katika kitabu chake hichi, amefafanua na kuyahisabu madai ya bibi Fatima juu ya Fadak kama ni hatua ya muondoko wa kuanzia harakati za bibi Fatimah (a.s) dhidi ya serikali na ni moja ya hatua zake katika utetezi wake wa Uimamu.

Nafasi ya Fadak na umuhimu wake

""Makala asili: Fadak

Fadak ilikuwa ni ardhi ya bustani yenye rutuba karibu na Khaibar[1] iliopo umbali wa kilomita 200 kutoka Madina[2] ambapo hapo mwanzo Wayahudi walikuwa wakiishi ndani ya ardhi hiyo.[3] Eneo hili lilikuwa na mashamba mengi, zikiwemo bustani na mashamba ya mitende.[4] Baada ya kifo cha Mtume, kukatokea mgogoro kuhusu mmiliki wa mali ya Fadak. Makhali waliitaifisha bustani ya Fadaka kwa manufaa ya ukhalifa. Kwa upande wa pili; Fatima (a.s) alitoa hotuba ya Fadakiyyah kwa ajili ya kutoa bayana na kutetea umiliki wake juu ya bustani hiyo. Mashia wanaamini kwamba Fadak ilinyakuliwa na makhalifa hali wakiwa hawana haki juu ya bustani hiyo, nao wanalihisabu tendohilo kuwa ni alama ya ukandamizaji wa makhalifa dhidi ya bibi Fatima. (a.s)

Tunuko ya Fadak kwa Bibi Fatimah (a.s)

Wakati wa zama za Mtume, ardhi ya Fadak iliangukia mikononi mwa Waislamu bila ya nguvu au mapigano ya kijeshi [16] Kwa hiyo, bwana Mtume (s.a.w.w) akamtunukia ardhi hiyo bibi Fatima (a.s). Wanazuoni wa Kiislamu, wakirejelea Aya ya Fai-u, [Maelezo 1 ] wanaamini na kukubali ya kwamba; mali yoyote ili inayoangukia mikononi mwa Waislamu bila vita au uvamizi wa kijeshi, kuwa ni mali ya Mtume (s.a.w.w) peke yake. [17]

Kwa mujibu wa kauli ya Jafar Subhani, wafasiri wa Shia na kundi la wapokezi wa Hadithi wa Kisunni wamesimulia Hadithi zinazoeleza kwamba; Baada ya kuteremshwa Aya isemayo (وَآتِ ذَا الْقُرْ‌بَیٰ حَقَّهُ ; Na wape haki (ya ulichopata) jamaa wa karibu), [18] Mtume (s.a.w.w) alimtunukia bibi Fatima (a.s) [19] ardhi ya Fadak. Kuna wanachuoni kadhaa wa Kisunni waliosimulia tukio hili, miongoni mwao ni; Jalal al-Din Siyuti katika Al-Darru al-Manthur, [20] Muttaqi Hindi katika Kanzal-Umal, [21] Hakim Hasakani katika Shawahidu Al-Tanzil, [22] Kanduzi katika Yanabi'u al-Mawaddah [23] ] na wengine [24] wasikuwa hao pia wamesimulia tukio la jambo hili.


Uhusiano wa Fadak na Uimamu

Hussein Ali Muntadhari, mujtahid wa upande wa Shia aliyefariki mwaka 1388 Shamsia, anaamini kwamba; Fadak ni nembo ya Uimamu, na kule Mtume (s.a.w.w) kumpa Fatima ardhi hiyo ya Fadak, kulikuwa na lengo la kuanzisha chanzo cha mapato kwa ajili uongozi na serikali ya Maimamu. Pia utaona kwamba; Mtume (s.a.w.w) alimpa alimtunukia Fatima (a.s) na sio Ali (a.s). Bila shaka alifanya hivyo ili wasiweze kuinyakua kwa urahisi. [25] Ili kuthibitisha nadharia hii imenukuliwa Hadithi [26] ambayo kwa mujibu wake; Haruna Abbasi alimtaka Imamu Kadhim (a.s) kubainisha mipaka ya Fadak, ila Imamu Kadhim (a.s) akaihisabu mipaka yote ya serikali ya Abbas [27] na zaidi yake, kuwa ndio mipaka halisi ya Fadak. Hapo Harun alimjibu Imamu Kadhim (a.s) kwa kumwambia; hakuna kitu kilichobakia kwa ajili yetu yaani hakuna ulichotubakishia katika kuanisha kwako mipaka. [28] Pia, katika riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Ummu aiman, ni kwamba; Fatima (a.s) alimwomba Mtume (s.a.w.w) amwachie yeye Fadak, ili ikiwa atakutwa na haja yoyote katika siku zijazo, aweze kutatua haja hiyokupitia Fadak. [29]

Kunyang'anywa kwa Fadak na kesi ya Fatima

Fadak iliendelea kuwa mikononi mwa bibi Fatima (a.s) hadi kifo cha Mtume (s.a.w.w), na ndani yake mlikuwa na walifanya kazi kadhaa wakiiendesha na kushighulikia bustani hiyo kwa niaba ya bibi Fatima. Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), na Abu Bakar kuingia madarakani, yeye alitanga kuwa bustani hiyo si milki inayomilikiwa na mtu yeyote, kisha akaitaifisha kwa manufaa ya ukhalifa. [31] Milki ya Fadak iliendelea kushikiliwa kimabavu, na hata utawa wa Omar bin Khattab [32] uliposhika hatamu za uongozi, pia milki hiyo haikurudi kwenye familia ya bwana Mtume (s.a.w.w), Utawala wa Othman pia nao haukuirudisha milki hiyo kwa wamiliki wake halali. [33]

Mashtaka ya bibi Fatima

Baada ya kutekwa kwa Fadak, Fatima (a.s) alidai haki yake hiyo kutoka kwa Abu Bakar. Abu Bakar naye alijibu kwa kusema kuwa: Amemsikia Mtume (s.a.w.w) akisema kwamba; baada yake mali yake itabaki kuwa ni urithi na mali ya Waislamu. [34] Fatima (a.s) akajibu: "Baba yangu ndiye aliyenipa mali hii." Abu Bakar akamtaka Fatima (a.s) alete mashahidi wa kuthibitisha madai yake. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya historia; Ali (a.s) na Ummu Aiman walisimama upande wa bibi Fatima na kuitoa ushahidi wa kuunga mkono madai yake [35], na kwa mujibu wa kauli za waandishi wengine, Ummu Aiman na mmoja wa wafuasi wa Mtume (s.a.w.w) [36], na kwa mujibu wa baadhi ya maandishi, Imam Ali (a.s), Ummu Aiman na Hassanein ndio [37] waliokuwa mashahidi, na Abu Bakar akakubaliana na ushahidi wao kisha akaandika waraka ili azuie mtu yeyote asiiguse Fadak. Wakati Fatimah (a.s) alipotoka nje ya mkusanyiko, Omar bin Khattab alichukua waraka huo ulioandikwa na Abu Bakar na kuurarua [38] Ila kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya Kisunni, Abu Bakar hakuwakubali mashahidi wa Fatima na badala yake akataka watu wengine wawili waje kutoa ushahidi. [39] Ibn Abi al-Hadid Mu'tazili anasema: Nilimuuliza Ibn Farqi, mwalimu wa shule ya magharibi ya Baghdad, je, Fatima alikuwa anasema ukweli juu ya madai yake? Ibn Faraqi akasema ndio. Nikauliza ni kwa nini basi Abu Bakar hakumrudisha Fadak? Akajibu; kama angefanya hivyo, bsi siku ya pili yake angekwenda kumdai ukhalifa kwa mumewe, na Abu Bakar asingeweza kulikataa dai lake. Kwa sababu tayari ameshakubaliana na ushahidi wake kuhusu Fadak bila ya kutaka ushahidi mwengine.” Ibn Abi al-Hadid ameendelea kwa kusema: “Hata kama Ibn Farqi alisema hivyo kwa mzaha, ial maneno yake yalikuwa sahihi”. [40]

Katika Kitabu cha Al-Ikhtasas, ikitegemewa Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), ni kwamba; Suala kuharibika kwa mimba ya Muhsin limehusisha moja kwa moja na tukio la bibi Fatima la kudai haki yake ya Fadak. Ila katika vyanzo vya historia, suala la kuharibika mimba ya Muhsin limehusishwa na tukio la uvamizi dhidi ya nyumba ya bibi Fatima (a.s). [42]

Hoja ya Abu Bakar juu ya Mitume kutowarithiwa

Makala asili: Sisi Manabii Haturithishi

Imepokewa ya kwamba; Abu Bakar katika kujibu mashtaka ya bibi Fatima, alimwambia: “Nimemsikia Mtume (s.a.w.w) akisema: “Sisi (mitume) hatuachi mirathi na kilichobakia kwetu ni sadaka.” [43] Bibi Fatima akatoa bayana katika madai yake kwa kuashiria baadhi ya aya za Qur’an Tukufu ambayo zinazothibithisha watu kuwarithi Mitume waliopita, [44] na kuichukulia kauli ya Abu Bakar; kuwa inapingana na Aya wazi za Qur'an. [45] Wanazuoni wa Kishia wamesema kwamba; hakuna Sahaba yeyote aliyenukuu maneno hayo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) isipokuwa Abu Bakar. [46]

Imepokewa ya kwamba Othman aliposhika nafasi ya ukhalifa, Aisha na Hafsa walimwendea na kumtaka awape tena kile ambacho baba zao (makhalifa wa kwanza na wa pili) walikuwa wamewapa; Lakini Othman akawajibu kwa kusema, Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitawapa kitu kama hicho... Je! hamkuwa ninyi wawili ndio mlioshuhudia mbele ya baba zenu ya kwamba... Mitume hawaachi urithi. Siku moja mlishuhudia hivyo na siku nyengine mnakuja kuomba urithi wa Mtume (s.a.w.w)? [47]

Hotuba ya Fadakiyyah

Makala asili: Hotuba ya Fadakiyyah

Baada ya mashtaka ya bibi Fatima (a.s) dhidi ya utaifishaji wa Abu Bakar kutofaulu, Fatima alikwenda kwenye msikiti wa Mtume na kuwasomea masahaba hotuba. Katika hotuba hii, ijulikananayo kwa jina la hotuba ya Fadakiyyah [48], Fatimah (a.s) alizungumzia suala unyakuzi wa ukhalifa na akakanusha kauli ya Abu Bakar isemayo kwamba; Mitume hawarithiwi. Aliuliza ni msingi gani wa sheria unaomzuia yeye kumrithi baba yake?Je, kuna Aya ya Qur'an inayosema hivyo?! Kisha akamkabidhi Mola wake amhukumie Siku ya Kiyama. Yeye aliwauliza masahaba wa Mtume (s.a.w.w) ni kwa nini walinyamaza mbele ya dhulma hizo. Fatimah (a.s) alisema kwamba; waliyoyafanya (Abu Bakr na walio karibu naye) ni kuvunja kiapo chao, na mwisho wa khutba, kasema; matendo yao yatabaki kuwa ni fedheha ya milele na mwishowe ni motoni. [49]

Kutoridhika kwa Fatima hadi mwisho wa Mmisha yake

Kwa mujibu wa Hadith iliopokewa katika Sahih Bukhari, ambayo imenukuliwa kutoka katika vitabu vya Sihah Ahl al-Sunnat, ni kwamba; Baada ya tukio la Fadak bibi Fatima (a.s) aliwakasirikia Abu Bakar na Omar, na aliendelea na ghadhabu hizo hadi siku aliofariki kishahidi. [50] Pia kuna Hadithi nyinge zenye madhumuni kama hayo kutoka katika vitabu vyengine vya Kisunni. [51] Isimuliwa kwamba; Kuna wakati fulani Abu Bakar na Omar waliamua kukutana na bibi Fatima (a.s) ili kuondoa hisia ya sintofahamu na kumridhisha moyo wake, ila Fatima alikataa. Baada ya wao kumuingiza kati Imamu Ali (a.s), na kumtaka awaombee ruhusa ya kukutana naye, hapo ndipo walipoweza kukutana naye. Katika mkutano wao huo, bibi Fatima (a.s) aliikumbuka Hadithi ya Bidh-'ah inayohusiana na hadhi na nafasi yake, na akaendelea hali ya kutoridhika nao. [52]

Radiamali ya Imam Ali (a.s)

Kwa mujibu wa Hadithi iliyosimuliwa katika Bihar al-Anwar; Baada ya kunyakuliwa kwa Fadak, Imam Ali (a.s) alikwenda msikitini na kumlaumu Abu Bakar kutokana na kumnyima Fatimah haki yake aliyopewa na Mtume (s.a.w.w). Abu Bakr alimtaka Ali alete shahidi wa haki juu ya haki hiyo, Imam Ali (a.s) kwa upande wake alimjibu kwa kumwambia; Ikiwa kitu fulani kiko mkononi mwa mtu, kisha kukatokea mtu mwingine ambaye adai kitu hicho, basi kisheria mdai huyo (mtu huyo wa pili) ndiye anayetakiwa alete ushahidi (ushahidi na shahidi) na sio Fatima, ambaye tayari Fadak ilikuwa mkononi mwake. [53] Imamu Ali (a.s) akiendelea kumjibu alisoma Aya ya utakaso na akachukua ungamo kutoka kwa Abu Bakar ya kwamba Aya hii iliteremka kuthibitisha hadhi ya Imamu Ali na familia yake (a.s). Kisha akamuuliza utafanyaje iwapo watakuja mashahidi wawili watakaodai kwamba Fatima amefanya uasherati? Abu Bakar akasema, "Nitamhukumu Fatima kisheria." Imamu (a.s) akamjibu kwa kusema: “Wewe umeuthamini ushahidi wa wanadamu kuliko ushahidi wa Mwenyezi Mungu, na ukifanya hivyo utakuwa kafiri.” [54] Katika kitabu cha Ihtijaaju cha Tabrasi, kumenukuliwa barua kutoka kwa Imam Ali (a.s) iliyomwandikia Abu Bakar, ambamo ndani alitumia lugha ya vitisho dhidi ya unyakuzi wa ukhalifa pamoja na bustani ya Fadak. [55]

Hata katika zama za ukhalifa wa Imamu Ali (a.s), Fadak ilikuwa mikononi mwa wapinzani. Ingawa Imam Ali (a.s) alikichukulia kitendo cha makhalifa waliopita kuwa ni unyakuzi, ila hukumu ya jambo hilo alimwachia Mungu.” [56] Kuna riwaya kadhaa katika vyanzo vya Hadithi kuhusu kwa nini Imam Ali (a.s) hakujaribu kurudisha tena Fadak mikononi mwa wamiliki wake halali. Miongoni mwa mambo yaliotajwa kuhusiana na hilo ni kwamba; Ni ili kauli ya Imamu Ali (a.s) mwenyewe alioisema katika hotuba yake, isemayo: "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu lau ningeiamuru Fadak irudi kwa warithi wa Fatima (a.s), [Maelezo 2], watu wangetawanyika (wangeliniacha mkono) na kuondoka kutoka karibu yangu. [57] Pia katika Hadithi ya Imamu Sadiq (a.s) imeelezwa ya kwamba; Imam Ali (a.s.) alifuata nyayo za Mtume (s.a.w.w) katika suala hili. Kwa sababu katika siku ya kutekwa kwa mji wa Makka, Mtume (s.a.w.w) hakuichukua tena ile nyumba aliyofosiwa kwa dhulma. [58]

Katika barua ya Imam Ali (a.s) kwa Othman bin Hanif, akielezea kisa cha Fadak maamuzi aliochukuliwa juu yake, aliandika akisema: “Chini ya mbingu hii, mali pekee iliyokuwa mikononi mwetu ilikuwa ni Fadak, ila kuna watu waliotufanyia ubahili juu yake, na watu wengine wakawa wakarimu katika kufumbia macho tukio hilo. Kadhi aliye bora ni Mola Mlezi, na itanisaidia nini mimi nikimiliki Fadak, na nitapungukiwa na nini nisipokuwa na Fadak, na kesho pahala pa mtu ni kaburi? [59]

Motisha wa kutaifisha na kuidai Fadak

Sayyied Mohammad Baqir Sadr katika kitabu chake Fadak fi al-Tarikh anaamini ya kwamba; suala la mashtaka na kuidai Fadak halikuwa suala la kibinafsi au mzozo wa kugombania dunia, bali ni aina ya kutangaza na konesha upinzani dhidi ya mamlaka ya wakati huo na ni alama ya kupingana na kufelisha uhalali wa serikali, yaani ni kupingana na maamuzi ya Saqifah. [60] ) Kudai haki ya Fadak ni hatua msingi ya bibi Fatima ya kusimama dhidi ya serikali, na ni moja ya hatua yake katika kutetea suala la Uimamu na utawala halali. [61]

Sayyied Jafar Shahidiy, mwanahistoria aliyefariki mwaka 1386 Shamsia, anaamini kwamba; lengo la Fatima (a.s) katika kudai Fadak lilikuwa ni kuhuisha na kuzindua upya Sunna za Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kusimamisha uadilifu. Bibi Fatima alikuwa na wasiwasi juu ya kurudi tena kwa maadili ya kijahili na ufakhari wa kikabila uliokuwa ukiinyemelea jamii ya Kiislamu. [62]

Kwa mujibu wa maelezo ya Ayatullah Makarim Shirazi, mmoja wa wanazuoni wa Kishia wenye mamalaka ya kutoa fatwa, ni kweamba; Makhalifa waliitaifisha Fadak ili kisiwe ni chanzo cha kiuchumi kitakachomwinua na kumpa nguvu Imamu Ali (a.s) na familia yake. [63] Akithibitisha suala hilo, Ayatullah Makarim Shirazi amenukuu riwaya kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) [64] isemayo kwamba; baada ya Abu Bakar kushika nafasi ya ukhalifa, Omar alimtaka achukue khums, fai-u (mali zinazokuwa zikimilikiwa na Ahlul Al-Bait) pamoja na Fadak kutoka kwa Ali na familia yake, kwani wafuasi wake watakapoona katika hali hiyo (ya mkono mtupu), watamtoroka Ali (a.s) na kuwelekea kwa Abu Bakar. [65]

Kurudishwa kwa Fadak mikononi mwa watoto wa Fatima

Hata katika zama za Bani Umayya na Bani Abbas, Fadak iliendelea kubaki mikononi mwa Makhalifa, katika baadhi ya vipindi fulani tu Fadak ilirejea kwenye mikono ya watoto wa Fatima, baadhi ya vipindi hivyo ni:

  1. Kipindi cha Ukhalifa wa Omar bin Abdul Aziiz Amawiy. [66]
  2. Enzi za Safahu Abbasiy. [67]
  3. Enzi za Mahdi Abbasiy. [68] Bila shaka, kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, Imam Kadhim (a.s) alidai Fadak kutoka kwa Mahdi Abbasi, lakini Mahdi Abbasi alikataa kuirejesha. [69]
  4. Enzi za ukhalifa wa Maamun Abbasiy .[70]

Baada ya Mamun, kupitia amri ya Mutawakkil Abbasiy, Fadak ikarudi tena kwenye hali yake ya kabla ya amri hiyo ya Mamun. [71] Kulingana na maelezo ya Majlisi Kuupai katika kitabu chake "Fadak az Ghasbe taa Takhrib", vitabu vingi vya kihistoria havikutaja matukio na hali ya Fadak ilivyokuwa baada ya uongozi wa Mutawakkil. [72] Di'ibil Khozaiy (aliyefariki mwaka 246 Hijiria) baada ya kurudisha Fadak kwa watoto wa Fatimah (a.s) alitoa shairi, ambalo ubeti wake wa kwanza unasema hivi:

اَصْبَحَ وَجْهُ الزَّمانِ قَدْ ضَحِکاً * بِرَدَّ مَأْموُنُ هاشِمَ فَدَکاً



Kicheko cha furaha kimedhihiri kwenye uso wa wakati
kwani Maamuni kwa Bani Hashimu kairudisha Fadaki.[73]

Monografia (Vitabu makhususi juu ya maudhui hii)

  • Fadak fi al-Tarikh "فَدَک فِی التّاریخ ": cha Mohammad Baqir Sadri. Ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, ambacho kinashughulikia mkabala wa uchanganuzi juu ya tukio la Fadak. Kitabu hichi kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiajemi kwa jina la "Fadak Dar Taarikh" «فدک در تاریخ».
  • Fadak wa al-Awali au al-Hawa-it al-Sab-'ah fi al-Kitabi wa Sunnah wa al-Tarikh wa Al-Adab "فدک و العوالی او الحوائط السبعة فی الکتاب و السنة و التاریخ و الأدب": cha Sayyid Mohammad Baqir Hosseiniy Jalaliy (aliyezaliwa mwaka 1324 Shamsia). Katika kitabu hichi, kimetafiti historia ya Fadak, eneo lake la kijiografia, kisa cah Fadak pamoja na Hadithi na mada za kitheolojia zinazohusiana na Fadak. [75] Kitabu hichi kilichaguliwa kama kitabu bora cha mwaka wa 1385 Shamsia. [76]
  • Al-Saqifah wa Al-Fadak " السقیفة و الفدک": cha Abu Bakar Ahmad bin Abdulaziz Jauhariy Basriy, kilichohakikiwa na Mohammad Hadi Aminiy, Chapa ya Tehran, ya Maktabatu Al-Nainawi Al-Hadithah, ya mwaka 1401 Hijiria.
  • Fadak Dar Faraze wa Nashib "فدک در فراز و نشیب": Ni utafiti juu ya suala la Fadak katika kumjibu mwanazuoni wa Kisunni: Kilichoandikwa na Ali Hosseini Milani, Chapa ya Qum, ya Al-Haqaaiq, ya mwaka 1386 Shamsia.
  • Fadak wa Baaztabhaye Taarikhiy wa Siasiy "فدک و بازتاب‌های تاریخی و سیاسی آن": Cha Ali Akbar Hasaniy, chapa ya Qom, ya Kongamano la Hizare Sheikh Mofid la mwaka 1372 Shamsia.

Rejea

  1. Baladi, Ma'ajm Ma'alim al-Hijaz, 1431 H, juz. 2, uk. 206 na 205 na juz. 7, uk. 23; Sobhani, "Hawadith saal haftom hijirat: Saregozashte Fadak", uk. 14.
  2. Tazama: Yaqut Hamui, Majam Al-Buldan, 1995 H, juz. 4, uk. 238.
  3. Tabari, Tarikh al-Umam wal-Muluk, 1387 H, juz. 3, uk. 15.
  4. Tazama: Fakhr Razi, Mafatih al-Ghaib, 1420 H, juz. 29, uk. 506; Tabatabai, Al-Mizan, 1417 H, juz. 19, uk. 203.

Vyanzo

  • ʿAmilī, Jaʿfar Murtida, al-Şaḥīḥ min sīrat al-nabī al-aʿzam, Qum: Dār al-Ḥadīth, 1426 AH.
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Sayyid Hāshim Rasūlī Maḥallātī. Tehran: Maktabat al-ʿIlmīyya al-Islāmīyya, [n.d].
  • Balādīyy, ʿĀtiq b. Ghayth al-. Muʿjam maʿālim al-Ḥijāz. Mecca: Muʾassisat al-Rayyan, 1431 AH.
  • Bilādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Futūḥ al-buldān. Beirut: Dār wa Maktabat al-Hilāl, 1988.
  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Edited by Muḥammad Zahīr b. Nāṣir. Beirut: Dār Ṭawq al-Nijāt, 1422 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Ḥākim al-Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh b. Aḥmad al-. Shawāhid al-tanzīl. [n.p]: Muʾassisat al-Nashr, [n.d].
  • Ḥalabī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Al-Sīrā al-Ḥalabīyya. Edited by ʿAbd Allāh Muḥammad Khalīlī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1971.
  • Ḥalabī, Taqī b. Najm al-. Taqrīb al-maʿārif. Edited by Fāris Ḥasūn. Qom: al-Hādī, 1404 AH.
  • Ḥawawī, Yāqūt b. ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-buldān. Second edition. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1955.
  • Ḥusseinī Jalālī, Muḥammad Bāqir al-. Fadak wa l-ʿawālī. Mashhad: Kungiray-i Mīrāth-i ʿIlmī wa Maʿnawī-yi Ḥaḍrat-i Zahrā, 1426 AH.
  • Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balāgha. Edited by Muḥammad Abū-l-Faḍl Ibrāhīm. Qom: Kitābkhāna-yi Āyatollāh Maʿashī al-Najafī, 1404 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīna Dimashq. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Ibn Qutayba, ʿAbd Allāh b. Muslim. Al-Imāma wa l-sīyāsa. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Āḍwāʾ, 1410 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Qom: Raḍī, 1421 AH.
  • Khazzāz al-Rāzī, ʿAlī b. Muḥammad al-. Kifāyat al-athar fī l-naṣ ʿalā l-aʾimma. Edited by ʿAbd al-Laṭīf Ḥusaynī Kūhkamarī. Qom: Bīdār, 1401 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Translated to Farsi by Jawād Muṣtafawī. Tehran: al-ʿIlmīyya al Islāmīyya, 1369 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Translated to Farsi by Kamaraʾī. Qom: Uswa, 1375 Sh.
  • Majlisī Kūpāʾī, Ghulām Ḥusayn. Fadak az ghaṣb tā takhrīb. Qom: Dalīl-i Mā, 1388 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Edited by Shaykh ʿAbd al-Zahrā ʿAlawī. Beirut: Dār al-Riḍā, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Imtāʿ al-asmāʾ bi-mā li-l-nabīyy min al-aḥwāl wa l-amwāl wa l-ḥafda wa matāʿ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1420 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Ikhtiṣāṣ. Edited by ʿAlī Akbar al-Ghaffārī. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmī, [n.d].
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Muqniʿa. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmī, 1410 AH.
  • Muslim b. al-Ḥajjāj. Ṣaḥīḥ Muslim. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Muttaqī al-Hindī, ʿAlī b. Ḥisām al-. Kanz al-ʿummāl. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, [n.d].
  • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Qom: Muʾassisat Dār al-Kitāb, 1404 AH.
  • Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm al-. Yanābīʿ al-mawadda. Qom: Dār al-Uswa, 1422 AH.
  • Qurʾān.
  • Ṣadr, Muḥammad Bāqir al-. Fadak fī al-tārīkh. Edited by ʿAbd al-Jabbār Sharāra. Qom: Markaz al-Ghadīr li-l-Dirāsāt al-Islāmīyya, [n.d].
  • Shahīdī, Sayyid Jaʿfar al-. Zindigānī-yi Fātima-yi Zahrā. Tehran: Nashr-i Farhang-i Islāmī, 1362 Sh.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Furūgh-i wilāyat. Sixth edition. Qom: Muʾassisat Imām al-Ṣādiq. 1380 Sh.
  • Suyūṭī, Jalāl al-Dīn al-. Al-Durr al-manthūr. Beirut: Dār al-Maʿrifa li-l-Ṭibāʿa wa l-Nashr, [n.d].
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Al-Mustarshid fī imāmat ʿAlī b. Abī Ṭālib. Edited by Aḥmad Maḥmūdī. Qom: Kūshānpūr, 1415 Ah.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abū l-Faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dār al-Turāth, [n.d].
  • Ṭabāṭabāyī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmī, 1417 AH.
  • Ṭabrisī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Al-Iḥtijāj ʿalā ahl al-lijāj. Edited by Muḥammad Bāqir al-Khurāsānī. Mashhad: Nashr-i Murtaḍā, 1403 AH.
  • Ṭabrasī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Nāṣir Khusru, 1372 Sh.