Nenda kwa yaliyomo

Ummu Ayman

Kutoka wikishia

Umm Ayman (Kiarabu: أم أيمن) ni mmoja wa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) na mama yake Usama bin Zayd, ambaye Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimtambulisha kama mmoja wa wanawake wa peponi. Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), alikuwa pamoja na Imam Ali (a.s) kwenda kwa Abu Bakar kwa ajili ya kuidai kurejeshwa Fadak na alitoa ushahidi kwamba Mtume (s.a.w.w) alimpa Fatima Zahra (a.s) Fadak.

Ummu Ayman alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kusilimu na kuingia katika Uislamu. Pia alikuwepo katika vita vya Uhud na Khaybar. Katika vita vya Uhud, alikuwa akiwapa maji waliojeruhiwa na pia kuwatibu. Kuna riwaya zilizonukuliwa na Umm Ayman katika vyanzo vya hadithi.

Maisha Yake

Barakah, binti ya Tha'laba bin Amru, mashuhuri kwa jina la Ummu Ayman, alikuwa kanizi wa Kihabeshi[1] na alikuwa akimilikiwa na Abdullah bin Abdul Muttalib, baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w)[2] na kisha akarithiwa na Mtume (s.a.w.w)[3] na baada ya Mtume  kufunga ndoa na Bibi Khadijah,[4] alimwachilia huru.[5]

Pia, baada ya kifo cha Amina, mama yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) huko Abwa, Ummu Ayman alikuwa na jukumu la kumlea na kuwa na Mtume (s.a.w.w) hadi alipoingia Makka[6] na baada ya hapo aliendelea na jukumu hilo mpaka Mtume alipofikisha umri wa kubaleghe.[7].

Kabla ya Uislamu, Ummu Ayman aliolewa Ubayd bin Amru huko Makka na akajifungua mtoto wa kiume aitwaye Ayman, ambaye alikuweko katika jeshi la Uislamuu katika Vita vya Hunayn na kuuawa katika vita hivyo.[8] Baada ya kuaga dunia Ubayd bin Amru, Ummu Ayman aliolewa na Zayd bin Haritha.[9] Osama bin Zayd ni mtoto wa Ummu Ayman na Zayd bin Haritha.[10] Kabla ya Ummu Ayman kuolewa na Zayd bin Hharitha, Mtume (s.a.w.w) aliwahutubu maswahaba zake kwa kuwaambia, mwenye kutaka kuoa mwanamke wa peponi basi na amuoe Ummu Ayman.[11]

Tarehe ya kifo cha Ummu Ayman imetambuliwa kuwa ni miezi mitano au sita baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).[12] Hata hivyo, baadhi wamesema kwamba, alikuwa hai wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na Omar.[13]

Pamoja na Mtume

Ummu Ayman alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kuwa Mwislamu na baadaye alihajiri na kuhamia Madina.[14] Pia, baadhi ya wanahistoria wanamchukulia kuwa miongoni mwa Waislamu waliohajiri kwenda Uhabeshi (Ethiopia ya leo).[15] Jina la Ummu Ayman limetajwa miongoni mwa masahaba wa Mtume.[16]

Ummu Ayman alikuweko katika vita vya Uhud na alikuwa akiwapa maji majeruhi[17] na kuwatibu.[18] Ummu Ayman akiwa pamoja na Ummu Salamah alikuwa mmoja wa wanawake ishirini walioondoka Madina pamoja na Mtume (s.a.w.w) katika vita vya Khaybar[19].

Mtume (s.a.w.w) alikuwa akimpenda sana Ummu Ayman na wakati mwingine alikuwa akimuita mama.[20] Kwa mujibu wa ripoti na nukuuu za kihistoria, Mtume Muhammad (s.a.w.w), alikuwa akikutana na Ummu Ayman katika nyumba yake na baada ya Mtume, Abu Bakr na Omar pia wakifuata ada hiyo ya Mtume walikuwa wakifanya hivyo pia.[21] Katika baadhi ya vyanzo vya hadithi, fadhila za Umm Ayman zimetajwa katika sehemu kando ya kujitegemea [22].

Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), Ummu Ayman alikuwa pamoja na Imam Ali (a.s) kwa ajili ya kwenda kwa Abu Bakar kwa lengo kudai kurejeshwa Fadak na alitoa ushahidi kwamba Mtume (s.a.w.w) alimpa Fatima Zahra (a.s) ardhi ya Fadak.[23] Katika vyanzo vya hadithi vya Ahu-Sunna, kuna hadithi kadhaa za Mtume (s.a.w.w) zilizonukuliwa kutoka kwa Ummu Ayman.[24] Watu kama Anas bin Malik, Abu Yazid Madani na Hanash bin Abdullah Sanani pia wamenukuu na kusimulia hadithi kutoka kwa Ummu Ayman.[25]

Rejea

Vyanzo