Fadak

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na eneo la Fadak; ili kujua kuhusiana na tukio la Fadak angalia tukio au mkasa wa Fadak.
Mipaka ya eneo la Fadak kaskazini mwa mji wa Madina

Fadak (Kiarabu: فدك) ilikuwa ni ardhi ya bustani yenye rutuba karibu na Khaybar iliyopo umbali wa kilomita 200 kutoka Madina ambapo hapo mwanzo Mayahudi walikuwa wakiishi ndani ya ardhi hiyo. Eneo hili lilikuwa na mashamba mengi, zikiwemo bustani na mashamba ya mitende. Eneo la Fadak liliangukia chini ya udhibiti wa Waislamu bila ya mapigano katika vita vya Khaybar. Baada ya kuteremka Aya ya 26 ya Surat al-Isra -((وَآتِ ذَا الْقُرْ‌بَیٰ حَقَّهُ؛ ; Na mpe aliye jamaa yako haki yake)) - iliyomtaka Mtume (s.a.w.w) atoe haki ya Dhawil-Qurba (watu wa karibu), Mtume alimpa Fadak Fatima (a.s) ambaye ni binti yake.

Baada ya kifo cha Mtume, kukatokea mgogoro kuhusu mmiliki wa mali ya Fadak. Khalifa wa kwanza Abu Bakr aliitaifisha bustani ya Fadak kwa manufaa ya ukhalifa. Kwa upande wa pili; Fatima (a.s) alitoa hotuba ya Fadakiyyah kwa ajili ya kutoa maelezo na kutetea umiliki wake juu ya bustani hiyo.

Katika zama za utawala wa Bani Umayya na Bani Abbas, ardhi ya Fadak ilikuwa pia chini ya umiliki ya makhalifa. Hata hivyo katika zama na duru za baadhi ya watawala wa Bani Umayya na Bani Abbas eneo hilo lilirejeshwa kwa watoto wa Fatima, licha ya kuwa watawala waliokuja baadaye walipokonya tena ardhi hiyo. Fadak ipo katika mkoa wa Hail nchini Saudi Arabia na eneo hili linatambulika kwa jina la "Wadi Fatima" na mitende yake inafahamika kwa jina la "Bustani ya Fatima". Kadhalika kuna msikiti na visima katika eneo hilo ambapo ni mashuhuri kwa jina la "Masjid Fatima" na "Uyun Fatima".

Nafasi ya kijiografia na umuhimu wa kihistoria

Picha ya eneo la bustani ya Fadak

Fadak ilikuwa ni ardhi ya bustani yenye rutuba huko Hijaz [1] umbali wa kilomita 200 kutoka Madina. [2] Mwanzoni mwa Uislamu Mayahudi walikuwa wakiishi ndani ya ardhi hiyo. [3] Eneo la Fadak liliangukia chini ya udhibiti wa Waislamu [4] bila ya mapigano katika vita vya Khaybar. Baada ya kuteremka Aya ya 26 ya Surat al-Israa ((وَآتِ ذَا الْقُرْ‌بَیٰ حَقَّهُ ; Na mpe aliye jamaa yako haki yake)), iliyomtaka Mtume (s.a.w.w) atoe haki ya Dhawil-Qurba (watu wa karibu), Mtume alimpa Fadak Fatima ambaye ni binti yake. [5] Baada ya kifo cha Mtume, kukatokea mgogoro kuhusu mmiliki wa Fadak na kupelekea kuandikwa mengi na wanazuoni wa Kishia na Kisuni kuhusiana na hilo, [6] kama ambavyo kumeandikwa vitabu vya kujitegemea kuhusiana na maudhui hii. [7] Kadhahlika katika duru mbalimbali kuliibuka radiamali kutoka kwa watawala kuhusiana na hili.

Thamani ya eneo la Fadak

Wakati wa kudhihiri Uislamu, eneo la Fadak lilikuwa bustani yenye mitende mingi. [9] Ibn Abil Hadid Mu'tazili (aliaga dunia: 656 Hijiria) amenukuu kutoka kwa mmoja wa Maulamaa wa Kishia kwamba, thamani ya mitende katika eneo la Fadak ilikuwa ikilingana na mitende ya mji wa Kufa katika zama hizo ambao ulikuwa moja ya miji tajiri katika kustafidi na mitende mingi. [10] Kwa mujibu wa Mayahudi mpaka katika kipindi cha Khalifa wa pili walikuwa wakiishi katika eneo la Fadak; lakini akawalazimisha kuondoka katika eneo hilo. [11] Imenukuliwa ya kwamba, wakati Omar bin al-Khattab alipowafukuza Mayahudi kutoka Hijaz aliwalipa dirihamu 50,000 ikiwa ni nusu ya thamani ya Fadak. [12] Imekuja katika vyanzo mbalimbali ya kwamba, kipato cha mwaka cha Fadak katika zama za Mtume (s.a.w.w) kinakadiriwa kuwa kilikuwa dinari 24,000 [13] mpaka 70,000. [14]

Udhibiti wa Waislamu kwa Fadak

Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufanikiwa kulikomboa eneo la Khaybar na ngome zake katika vita vya Khaybar, Mayahudi waliokuwa wakikaa katika ngome na mashamba ya Fadak walituma wajumbe kwa Mtume (s.a.w.w) na wakaridhiria mapatano. Ilikubaliwa kwamba, nusu ya ardhi hiyo iwe mali yao. Kwa msingi huo, Fadak ikawa imeungikia katika milki na udhibiti wa Waislamu bila ya vita na kutuma jeshi. [26] Kwa mujibu wa Aya ya 7 ya Surat al-Hashr mali ambazo zimepatikana bila ya vita zinafahamika kwa jina la Fay na Mtume (s.a.w.w) ana mamlaka nazo na anaweza kuwapatia watu kwa mujibu anavyoona yeye. [27] Kwa mujibu wa nukuu za vyanzo vya Kishia [28] na Ahlu-Sunna [29] kwa kushuka Aya ya 26 ya Surat al-Israa ((وَآتِ ذَا الْقُرْ‌بَیٰ حَقَّهُ؛ ; Na mpe aliye jamaa yako haki yake)) iliyomtaka Mtume (s.a.w.w) atoe haki ya Dhawil-Qurba (watu wa karibu), Mtume alimpa Fadak Fatima (a.s) ambaye ni binti yake. [30]

Mizozo kuhusu umiliki wa Fadak

Makala asili: Tukio la Fadak na Sisi Manabii Haturithiwi

Baada ya kifo cha Mtume, kukatokea mgogoro kuhusu umiliki wa Fadak. Khalifa Abu Bakr alimpokonya Fatima Fadak na akaitaifisha bustani hiyo kwa manufaa ya ukhalifa. [31] Hoja ya Abu Bakr ilikuwa kwamba, Mitume hawarithi na wala hawarithiwi na alidai kwamba, alisikia hilo kutoka kwa Mtume(s.a.w.w). [32]

Kwa upande wa pili, Fatima (a.s) alitoa hotuba ya Fadakiyyah kwa ajili ya kuweka wazi na kutetea umiliki wake juu ya bustani hiyo ambapo alisema kuwa, maneno hayo ya Abu Bakr yanapingana na Qur'an [33] na akawamleta Imamu Ali (a.s) na Ummu Ayman kama mashahidi ambapo Mtume kabla ya kuaga kwake dunia, alimpatia ardhi ya Fadak. [34] Abu Bakr akakubali na akaandika waraka ili mtu asije akaichukua tena ardhi hiyo. Wakati Fatima (a.s) alipoondoka katika kikao hicho, Omar bin al-Khattab alichukua waraka huo na kuuchana. [35]

Kufuatia kushindwa kwa shauri la Imam Ali (a.s), Fatima (a.s) alikwenda msikitini na kutoa hotuba iliyokuja kuwa mashuhuri kwa jina la Hotuba ya Fadakiyah.[36]

Katika zama za utawala wa Bani Umayya na Bani Abbas, ardhi ya Fadak ilikuwa pia chini ya miliki ya makhalifa. Hata hivyo katika zama na duru za baadhi ya watawala wa Bani Umayya na Bani Abbas kama Omar bin Abdul-Aziz Umawi, [37] Saffah, [38] na Maamun Abbasi [39] eneo hilo lilirejeshwa kwa watoto wa Fatima, licha ya kuwa watawala waliokuja baadaye walipokonya tena ardhi hiyo. Mutawakkil Abbasi, (alitawala: 232-247 Hijiria), alitoa amri ya kurejeshwa Fadak katika hali yake ya kabla ya amri hiyo ya Maamun. [40]

Athari zilizobakia za Fadak

Fadak ipo katika mkoa wa Hail nchini Saudi Arabia. Katika eneo hilo kuna mji uliaonzisha unaofahamika kwa jina la "al-Hait". Eneo la Fadak linatambulika kwa jina la "Wadi Fatima" na mitende yake inafahamika kwa jina la "Bustani ya Fatima". Kadhalika kuna msikiti na visima katika eneo hilo ambapo ni mashuhuri kwa jina la "Masjid Fatima" na "Uyun Fatima". [42] Nyumba na minara ya eneo hilo yamebomolewa na akthari ya mitende yake imekauka. [43] Mwaka 1387 Hijiria Shamsia, Akbar Hashemi Rafsanjani mmoja wa maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika zama hizo akiwa ameandamana na wajumbe wake alitembelea eneo hilo. [44]

Monografia

Baadhi ya vitabu vilivyoandikwa kuhusiana na Fadak ni:

  • Fadak wal-awali au al-Khawait al-Shia fil Kitab wal-Sunna wal-tarikh wal adab, mwandishi Sayyid Muhammad Baqir Husseini Jalali (alizaliwa (1324 Hijria Shamsia). Katika kitabu hiki, mwandishhi anabainisha historia ya Fadak, nafasi yake ya kijiografia, tukio la Fadak na masuala ya kihadithi na kiteolojia kuhusiana na kadhia hiyo. [45] Kitabu hiki mwaka 1385 Hijiria Shamsia kiliteuliwa kuwa kitabu bora cha mwaka cha Wilaya. [46]
  • Fadak az Ghasb ta takhrib, mwandishi Ghulamhussein Majlisi Kupai. Kitabu hiki kilichapishwa mwaka 1388 kikiwa na kurasa 290. [47] Pamoja na mambo mengine kitabu hiki kinaeleza kuhusu ripoti ya safari ya Akbar Hashemi Rafsanjani mmoja wa maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika zama hizo akiwa ameandamana na ujumbe wake alipotembelea eneo hilo. [48]

Vyanzo

  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Futūḥ al-buldān. Edited by Ṣalāḥ al-Dīn al-Munjid. Cairo: Maktabat al-Nahḍa al-Miṣrīyya, 1956.
  • Balādī, ʿĀtiq b. Ghayth al-. Muʿjam maʿālim al-ḥijāz. [n.p]: Dār Mecca – Muʾassisat al-Rayān, 1431 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Ḥamawī, Yāqūt b. ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-buldān. Second edition. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1995.
  • Ḥusaynī Jalālī, Sayyid Muḥammad Bāqir. Fadak wa l-ʿawālī. Qom: Kungira-yi Mīrāth-i ʿIlmī wa Maʿnawī-yi Ḥaḍrat-i Fātima, 1384 Sh.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārikh madinat Damascus. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Āthār-i Islāmi-yi Mecca wa Medina. Third edition. Tehran: Mashʿar, 1384 Sh.
  • Jawharī al-Baṣrī, Aḥmad b. ʿAbd al-ʿAzīz al-. Al-Saqīfa wa Fadak. Edited by Muḥammad Hādī Amīnī. Tehran: Maktabat al-Niynawā al-Ḥadītha, 1401 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Translated by Jawād Muṣtafawī. Tehran: Kitābfurūshī-yi ʿIlmīyya al-Islāmīyya, 1369 Sh.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Imtāʿ al-asmāʿ. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1420 AH.
  • Marjānī, ʿAbd Allāh b. ʿAbd al-Malik al-. Bahjat al-nufūs wa l-asrār fī tārīkh dār hijrat al-nabīyy al-mukhtār. Beirut: Dār al-gharb al-Islāmī, 2002.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Muqniʿa. Second edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1410 AH.
  • Quṭb al-Rāwandī, Saʿīd b. Hibat Allāh. Al-Kharāʾij wa l-jarāʾiḥ. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Mahdī, 1409 AH.
  • Shahīdī, Sayyid Jaʿfar. Zindigānī-yi Fātimā-yi Zahrā (a). Tehran: Daftar-i Nashr-i Farhang-i Islamī, 1376 Sh.
  • Subḥānī, Jaʿfar. 1346 Sh. "Ḥawādith-i sāl-i haftum-i hijrat: Sarguzasht-i fadak". Maktab-i Islām 4:14-18.
  • Suyūtī, Jalāl al-Dīn al-. Al-Durr al-manthūr. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Ṭabāṭabāyī, Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1417 AH.