Ushahidi wa uwongo

Kutoka wikishia

Ushahidi wa uwongo (Kiarabu: شهادة الزور) ni katika madhambi makubwa na maana yake ni mtu kutoa ushahidi wa jambo fulani ambalo ni kinyume kabisa na uhakika na uhalisia wa jambo. Mafakihi wakitumia Aya za Qur’ani na hadithi mbalimbali wanakitambua kitendo hicho kuwa ni haramu na kwa mujibu wa mtazamo wao, endapo itathibiti ushahidi wa uwongo kupitia kukiri, kutolewa ushahidi (wa kuthibitisha kwamba mhusika alitoa ushahidi wa uwongo) na elimu ya hakimu (kadhi) shahidi muongo atapatiwa adhabu ya Taazir (adhabu ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo). Ikiwa kabla ya hakimu kutekeleza hukumu ikafahamika kwamba, ushahidi ule ulikuwa wa uwongo, hukumu itatenguliwa, lakini kama hilo litathibiti baada ya kutekelezwa hukumu, watu ambao walitoa ushahidi wa uwongo wanapaswa kufidia hasara zilizopatikana (kama fedha, dia na kisasi) dhidi ya aliyehukumiwa.

Ushahidi wa uwongo kwa mujibu wa sheria za adhabu za Kiislamu nchini Iran ni uhalifu na anayetenda kosa hilo anahukumiwa kwenda jela na kulipa pesa taslimu.

Nafasi na umuhimu

Sheikh Tusi (aliyefariki mwaka wa 460 Hijiria) amesema katika kitabu chake cha al-Mabsut kwamba, ushahidi wa uwongo unahesabiwa kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa; [1] pia imesemwa kuwa hakuna dhambi kubwa zaidi baada ya shirki kwa Mwenyezi Mungu kama kutoa ushahidi wa uwongo. [2] Katika fiq’h ya Shia Imamiya, kuna mlango maalumu wenye anuani ya al-Shahadaat ambamo ndani yake hujadiliwa pia hukumu za ushahidi wa uwongo.[3]

Muhammad Muhammadi Ishtihardi (aliyefariki 2005), mwanazuoni na mwandishi wa Kishia, amesema kuwa, kutajwa ushahidi wa uwongo kando ya ibada ya masanamu katika Qur'an [4] kuwa ni ishara na dalili ya uchafu wa ushahidi wa uongo. [5] kadhalika imetajwa katika Qur'an kwamba, kujiepusha na ushahidi wa uwongo ni katika sifa za waja wa Mwingi wa rehma (waja wema na bora wa Mwenyezi Mungu). [6]

Maana

Ushahidi wa uwongo maana yake ni mtu kutoa ushahidi kwa makusudi kwa jambo ambalo halijui au kutoa ushahidi wa uwongo ambao kimsingi ni kinyume kabisa na ukweli na uhalisia wa jambo. [7] Baadhi ya wataalamu wa masuala ya sheria wanaamini kwamba, ushahidi wa uwongo huhesabiwa kuwa uhalifu na kosa na kufuatiliwa kisheria pale unapotolewa mbele ya viongozi rasmi mahakamani. [8]

Sababu za kuharamishwa ushahidi wa Uwongo

Ushahidi wa uwongo umehesabiwa kuwa haramu katika fiq’h ya Kishia na katika kuharamisha hilo kumetegemewa Aya isemayo: ((وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ‌ الزُّور ; na jiepusheni na usemi wa uwongo)).[9] Aya hii imetumiwa kama hoja ya kuthibitisha uharamu wa kusema uwongo. [10] Imamu Khomeini na Sayyid Ali Khamenei wanaamini kwamba, Aya hiyo inaashiria kuharamishwa kusema maneno ya batili ambayo yanajumuisha uwongo, ushahidi wa uwongo na ghinaa. [11]

Baadhi ya wafasiri wametumia pia Aya isemayo: ((وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ ; Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo)) [12] Kwa ajili ya kuwa haramu kutoa ushahidi wa uwongo. [13] Sayyid Hussein Buroujerdi, Marjaa Taqlidi wa Mashia, akitegemea hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) anasema kuwa, kutoa ushahidi wa uwongo ni haramu. Hadithi hiyo inasema: Mtoa ushahidi wa uwongo, moto wa jahanamu huwa wajibu kwake kabla hata hajapiga hatua kutoka katika sehemu aliyokuweko. [14][15] Allama Hilli ametumia hadithi nyingine kutoka kwa Imamu Muhammad Baqir (a.s): Hakuna mtu ambaye akiwa na lengo la kuchukua mali ya Mwislamu anatoa ushahidi wa uwongo isipokuwa, Mwenyezi Mungu badala ya hilo anamuandikia sanadi na waraka wa kuwa kwake mtu wa motoni. [16]

Hukumu

Kutoa ushahidi wa uwongo ni katika madhambi ambayo kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu hayajaainishwa adhabu (adhabu isiyo ya kimali), lakini ipo katika adhabu za Taazir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo). [17] Katika hili (kadhia jumla) mafakihi na wanazuoni wa Kishia na Kisunni wameafikiana. Lakini wametofautiana kuhusiana na vipengee vyake. Mafukahaa wa Kishia hawajatofautiana na kuhusiana na kutekelezwa adhabu ya taazir (ambazo mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye jukumu la kuainisha adhabu hizo) sambamba na Tash'hir (kumzunguisha na kumuumbua mhusika baina ya watu); [18] Sheikh Tusi amebainishha wazi jambo hili. [19] Hata hivyo, wanazuoni wa Kisunni wao wametofautiana kuhusiana na jambo hili. [20]

Njia za kuthibitisha

Ushahidi wa uwongo unaweza kuthibitisha kwa njia kadhaa:

  • Kukiri mtu mwenyewe: Mtu ajitokeze na kukiri kwamba, alitoa ushahidi wa uwongo hivyo anabatilisha kauli yake ya awali. [21
  • Ushahidi wa watu wengine: Wajitokeze watu na kutoa ushahidi wakipinga ushahidi uliotolewa na kueleza kuwa unapingana na uhalisia wa mambo. [22
  • Elimu na utambuzi wa kadhi: Kuna wakati pia kadhi akitumia njia mbalimbali anapata uhakika kwamba, ushahidi uliotolewa ni wa uwongo. [23] Kwa mujibu wa Mustafa Muhaqqiq Damad (alizaliwa 1324 Hijiria Shamsia) ni kwamba, elimu ya kadhi katika suala hili ni yenye kutangulizwa mbele ya ushahhidi mwingine. [24]

Matokeo ya kifiq'h na kisheria

Kuna matokeo ambayo yametajwa kuhusiana na ushahidi wa uwongo:

Kubatilishwa hukumu iliyotolewa

Kwa mujibu wa Shahid al-Awwal (aliakufa shahidi 786 Hijiria) katika kitabu cha al-Durus al-Shar'iah ni kwamba, kama itathibitika kabla ya kutekelezwa hukumu kwamba, ushahidi uliotolewa ulikuwa wa uwongo, hukumu ya kadhi inabatilishwa. [25] Kwa mujibu wa kipenge cha 1319 cha sheria za Iran pia, endapo shahidi atabatilisha ushahidi wake au ikafahamika kwamba, alitoa ushahidi usio kweli, ushahidi wake hautazingatiwa. [26]

Kufidia hasara na kisasi

Endapo itathibiti baada ya kutekelezwa hukumu kwamba, ushahidi uliotolewa ulikuwa wa uwongo, mashahidi watabeba dhima ya mali iliyotolewa na aliyehukumiwa [27] na kama aliyehukumiwa alihukumiwa kisasi au dia na hukumu hiyo imeshatekelezwa, mashahidi watahukumiwa kisasi au kutoa dia; [28] kwani mazingira kama haya sababu (kisababishi kikuu) ina nguvu zaidi kuliko aliyetekeleza hukumu. [29]

Kufungwa na kupigwa faini ya fedha

Baadhi ya mafakihi wakitegemea sira ya Imamu Ali (a.s) katika zama za utawala wake, wametoa fat'wa ya kufungwa jela mtoa ushahidi wa uwongo. [30] Kwa mujibu wa kifungu cha 650 cha sheria ya adhabu za Kiislamu ya Iran, mtu ambaye atatoa ushahidi wa uweongo mbele ya maafisa rasmi mahakamani, atahukumiwa kwenda jela [31] na adhabu ya kulipa fidia fedha taslimu. [32] Adhabu hizi ni tofauti na adhabu ambazo zimetajwa katika mlango wa adhabu zisizo za kimali (hudud), kisasi na dia kwa ajili ya aliyetoa ushahidi wa uwongo. [33]

Kutokubaliwa ushahidi wake baada ya hapo

Kwa mujibu wa fat'wa za mafakihi wa Kishia, kadhalika ushahidi wa baadaye wa watu waliotoa ushahidi wa uwongo mahakamani hautakubaliwa tena, isipokuwa kama watatubu na uadilifu wao ukawa umethitika wazi. [33]

Vyanzo

  • The Holy Qurān.
  • Anwārī, Ḥasan. Farhang-i buzurg-i sukhan. Tehran: Intishārāt-i Sukhan, 1390 Sh.
  • Bujnūrdī, Sayyid Muḥammūd. "Qawāʿid fiqhiyya". Tehran: Muʾassisa ʿUrūj, 1401 AH.
  • Burūjirdī, Ḥusayn. Jāmiʿ aḥādīth al-Shīʿa. Tehran: Intishārāt-i Farhang-i Sabz, 1386 Sh.
  • Bihbūdī, Bahrām and Majīd Dādkhāh. Wākāwī-yi fiqhī ḥuqūqī-yi masʾūliyyat-i kayfarī-yi shahādat-i kidhb. Ārāʾ Journal. Period 3, No 4, 1399 Sh.
  • Dayyāniī, ʿAbd al-Rasūl. Qānūn-i Mujāzāt-i Islāmī-yi muʿrab. Tehran: Intishārāt-i Mīzān, 1399 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Hidāyat al-umma ʾilā ahkām al-aʾimma. Mashhad: Bunyād-i Pazhūhishha-yi Āstān-i Quds-i Raḍawī, 1412 AH.
  • Ḥalabī, Abū l-Ṣalāḥ. Al-Kāfī fī al-fiqh. Isfahan: Maktaba Imām Amīr al-Muʾminīn (a), 1403 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Taḥrīr al-aḥkām al-sharʿiyya ʿalā madhhab al-imāmiyya. Qom: Muʾassisat Imām al-Ṣādiq, 1420 AH.
  • Hāshimī Shāhrūdī, Maḥmūd. Mawsūʿa al-fiqh al-islāmī al-muqārin. Qom: Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh-i al-Islāmī, 1423 AH.
  • Fāḍil Lankarānī, Muḥammad. Tafṣīl al-sharīʿa (al-qaḍāyā wa al-shahādāt). Qom: Markaz-i Fiqh-i al-aʾimma al-Aṭhār, 1409 AH.
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿArab. Beirut: Dār Ṣādir, 1414 AH.
  • Imām Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Al-Makāsib al-muḥarrama (Mawsūʿat al-Imām al-Khomeinī 13 and 14). Tehran: Muʾassisa-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeini, 1434 AH.
  • Ibn al-Barrāj, al-Ṭarābulusī. Al-Muhadhdhab. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1406 AH.
  • Khāmeneʾī, Sayyid ʿAlī. Ghināʾ wa mūsīqī. Tehran: Intishārāt-i Inqilāb-i Islāmī (Nashr-i Fiqh Rūz),1398 Sh.
  • Khoeī, Sayyid Abū l-Qāsim al. Mabānī-yi Takmila al-Minhāj (Musūʿa). Qom: Muʾassisa-yi Iḥyā-yi Āthār-i Āyatullāh Khoeī, 1422 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1407 AH.
  • Kamālān, Sayyid Mahdī. Handbooki-i kārburdī qawānīn wa muqarrarā Ḥuqūqī. Tehran: Intishārāt-i Kamālān.
  • Māzandarānī, Muḥammad Sāliḥ b. Ahmad. Sharḥ uṣūl kāfī. Edited by Abdu l-Ḥassan Shaʿrānī. Tehran: Maktaba al-Islāmīyya, 1382 AH.
  • Muḥaqqiq Dāmād, Musṭafā. Qawāʿid-i fiqh (Bakhsh-i qaḍāyī). Tehran: Markaz-i Nashr-i ʿUlūm-i Islāmī, 1381 Sh.
  • Murtāḍī, Aḥmad, Musawī Ruknī, ʿAlī Aṣghar and others. Barrasī-yi maʿnāshinākhtī-yi shahādat-i Zūr wa ḍarūrat-i muʿarrifī-yi ʿumūmī-yi ān dar fiqh-i madhāhib-i khamsa. Faṣlnāma-yi Pajūhish-hā-yi fiqh wa ḥuqūq-i Islāmī 35, (1393 Sh).
  • Marʿashī Shūshtarī, Sayyid Muḥammad Ḥasan. Dīdgāh-hā-yi nū dar ḥuqūq. Tehran: Nashr-i Mīzān, 1427 AH.
  • Muʿāwinat-i Riyāsat-i Jumhūrī. Qānūn-i Mujāzāt-i Islāmī. Tehran: Muʿāwinat-i Tadwin, Tanqiḥ wa Intishār- qawānīn wa Muqarrāt, 1392 Sh.
  • Muḥammadī Ishtihārdī, Muḥammad. Wīzhagī-hā-yi ʿIbād al-Raḥmān parhīz-i shadīd az guwāhī-yi durūgh wa shirkat dar majālis-i gunāh. Pāsdār-i Islām Magazine 229, (1379 Sh).
  • Mūsawī Gulpāyigānī, Sayyid Muḥammad Riḍā. Kitāb al-shāhādat. Qom: Jinab-i Muqarr-i Kitāb, 1405 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Sarakhsī, Muḥammad b. Aḥmad. Al-Mabsūṭ. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1414 AH.
  • Shāmlū Aḥmadī, Muḥammad Ḥusayn. Farhang-i iṣṭilāhāt wa ʿanāwīn-i jazāyī. Isfahan: Intishārāt-i Dādyār, 1380 Sh.
  • Shahīd al-Awwal, Muḥammad b. Makkī. Al-Durūs al-sharʿīyya fī fiqh al-imāmiyya. Qom: 1417 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh al-Islāmī, 1382 Sh.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1st edition, 1415 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥaasn al-. Al-Khilāf. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1407 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Mabsūṭ fī fiqh al-imāmīyya. Tehran: al-Maktaba al-Murtaḍawīyya li Iḥyāʾ al-Āthār al-Jaʿfarīyya, 1387 AH.