Ghina'

Kutoka wikishia

Ghina' (Kiarabu: الغِناء) ina maana ya kuimba nyimbo na katika fikihi ya Kiislamu kuna mjadala mkubwa kuhusiana na hukumu ya kisheria ya jambo hili. Wanazuoni wa fikihi wanatoa maana na fasiri tofauti kuhusiana na kuimba. Baadhi wanasema ni kuimba tu kunakoambatana na kughani na kurembesha sauti. Baadhi ya wengine wanaamini kuwa, wimbo wenye maudhui na mambo ya batili ni ile inayoambatana na muziki na unaonasibiana na vikao vya kipuuzi na visivyofaa. Akthari ya wanazuoni wa fikihi wa Kishia katika karne ya 14 na 15 Hijiria wanaamini kwamba, wimbo ambao ni haramu ni ule unaofikiana na maana na fasiri ya pili; lakini baadhi yao pia wanatoa fat'wa ya kuwa haramu kila uimbaji yaani aina yoyote ile ya uimbaji.

Maana ya kifikihi ya ghina

Katika fasihi ya wanazuoni wa elimu ya fikihi, kunaonekana maana na fasiri tofauti ya kuimba nyimbo au wimbo. Baadhi yao wamezingatia tu suala la sauti na kuwa kwake kwamba, ni wimbo. Baadhi yao pia wamezingatia muaudhui na kille kilichomo ndani ya wimbo wenyewe. Kwa mujibu wa nadharia ya baadhi ya wanazuoni kama Allama Hilli, Muhaqqiq Karaki na Shahidi Thani ni kuwa, Ghina' ni kupandisha na kushusa sauti, kuvuta sauti au ndio ile hali ya kughani na kurembesha sauti.[1] Kundi jingine la Maulamaa kama Sheikh Tousi na Feidh Kashani wanaamini kuwa, Ghina' ni wimbo ambao ndani yake kuna maneno ya kibatili kukiambatana na zana ya muimbaji.[2]

Hukumu ya kifikihi ya ghina (kuimba)

Baadhi ya wanazuoni wa elimu ya fikihi wanatambua suala la ghina' na kuimba kwa sura ujumla kuwa ni haramu na hata katika kuwa kwake haramu wanadai kuwa kuna kauli moja iliyofikiwa katika hili; kama Sheikh Tousi, Shahidi Thani, Sahib al-Jawahir, Naraqi na Ayatullah Khui.[3]

Baadhi ya mafakihi wengine hawaafikiani na suala la kuwa haramu dhati na asili ya ghina' na kuimba na wanasema, hilo litakuwa haramu tu pale litakapoambatana na ngoma, au mambo ya kipuuzi na yaliyo ya kifisadi (upuuzi na kitu kisichokuwa na faida); miongoni mwao ni Muhaqqiq Karaki[4], Feidh Kashani[5], Muhaqqiq Sabzawari,[6] Sheikh Ansari[7] na Imamu Khomeini.[8]

Wahakiki wanasema kuwa, sababu ya hitilafu katika hukumu hii inarejea katika kutoa fasiri na maana ya kuimba baina ya mafakihi na wanazuoni wa elimu ya fikihi; kwani baadhi yao wanamini kuwa, kuwa na ngoma, mdundo, mambo ya kipuuzi, yasiyo na maana na ya kupumbaza kwamba, ndio mafuhumu na maana ya ya ghina'. Kwa msingi huo, wanatoa fat'wa ya kuharamisha na baadhi ya wengine ambao wanatenganisha mafuhumu na maana ya kuimba, wanaamini kwamba, kuimba peke yake tu na katika dhati yake sio haramu.[9]

Uimbaji gani ni halali?

Lile kundi la mafakihi ambalo linaamini uharamu katika dhati yake kuimba (ghina) katika baadhi ya sehemu limeondoa hukumu hiyo hapo na wao licha ya kusadikika nyimbo lakini wanaona nyimbo hiyo ni halali; miongoni mwa hayo ni kusoma Qur’ani, dua, kusoma nauha (mashairi na nyimbo za maombolezo), kuimba katika vikao vya harusi na sikukuu; lakini lile kundi ambalo haliamini na kusema uharamu wa kuimba katika dhati yake, linaamini kuwa, kila uimbaji ambao hautaambatana na ngoma, mambo ya kipuuzi na yasiyofaa basi ni halali.[10]

Fat'wa za mafaqihi wa karne ya 14 na 15

Akthari ya wanazuoni wa fikihi wa karne ya 14 na 15 Hijria kama Ayatullah Khamenei, Ayatullah Tabrizi, Ayatullah Fadhil Lankarani na Ayatullah Makarem Shirazi wametofautisha baina ya ghina' (kuimba) na muziki) na wametambua ghina' kwamba, ni kuimba kwa sauti ya kuvutia inayonasibiana na vikao vya starehe na mambo ya kipuuzi na yasiyofaa au burudani za ufuska na mambo machafu na yasiyofaa na kwamba, muziki ni kupiga ngoma au gitaa ambako kunanasibiana na vikao vya burudani za ufuska na mambo machafu na yasiyofaa. Kwa msingi huo kufanya hayo au kusikiliza wanatambua kuwa ni haramu.[11]

Kwa msingi huu, wengi wao wanautambua wimbo ambao hauafikiani na vikao vya ufuska na mambo machafu kuwa ni halali. Ayatullah Tabrizi ametoa fat'wa inayosema kuwa, kwa mujibu wa tahadhari ya wajibu kuna haja ya kujiepusha na kila aina ya nyimbo ambayo inaimbwa kwa kuremba na kuvuta sauti hata kama madhumini ya wimbo huo si ya kibatili.[12] Kadhalika Ayatullah Swafi Golpaygani anatambua mutlaki ya wimbo na muziki kuwa ni haramu.[13]

Athari za kujitegemea kuhusu ghina

Kitabu cha Ghina va Musiqi (kilichapishwa 1377 Hijria Shamsia), kinaeleza kuwa, kuanzia zama za utawala wa Safavi (moja ya tawala za Kishia nchini Iran) kutokana na kuenea sana mtindo wa simai (muziki unaoipigwa kwa nai na matari katika hafla za dini ya Kiislamu) ambao ilikuwa ikiambatana na nyimbo na muziki, suala la nyimbo na kuimba lilizingatiwa na kufuatiliwa na mafakihi na kukaandikwa vitabu vya kujitegemea katika uga huu. Katika kitabu hiki, kumetajwa idadi kadhaa ya vitabu ingawa havipatikana hii leo. Kuanzia zama za utawala wa Safavi mpaka kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (yaliyotokea 1979 kwa uongozi wa Imamu Ruhullah Khomeini), kulibainishwa vitabu 49.[14] Baadhi yake vitabu hivyo ni:

Kitabu cha kiada kuhusu muziki na kuimba

Kuna matini iliyosambazwa ya darsa ya Kharij ya Fikihi (masomo ya juu kabisa ya fikihi) ya Ayatullah Khamenei kuhusiana na muziki na nyimbo kwa anuani ya Darsname Ghinaa va musiqi (Kitabu cha Kiada cha Muziki na Kuimba). Katika kitabu hiki zimetumika takribani hadithi 100 kama nyaraka na ushahidi wa kubainisha maana na fasiri ya kuimba na muziki ambao ni haramu. Kwa mtazamo wa Ayatullah Khamenei ni kwamba, kuimba kwenyewe tu na katika dhati yake sio haramu, bali kigezo cha uharamu wake ni kuwa kwake na jambo la kipuuzi na kupotosha na kumtoa mtu katika njia ya Mwenyezi Mungu.[15] Kitabu hiki kilichapishwa na kusambazwa 1398 Hijiria Shamsia kwa lugha ya Kifarsi kikiwa na kurasa 560.[16]

Rejea

  1. Allamah Hilli, Qawaid al-Ahkam, 1413 H, juz. 3, uk. 459 ; Muhaqqiq Karaki, Jami' al-Maqasid, 1414 H, juz. 4, uk. 23 ; Shahid Thani, al-Raudhah al-Bahiyah, 1410 H, juz. 3, uk. 212.
  2. Sheikh Tousi, Istibshar, 1390 Q, juz. 3, uk. 69 ; Faidh Kashani, Waafi, 1406 H, juz. 17, uk. 218.
  3. Yusufi Maqdam, Pazuhesh dar Ghina', 1391 S, uk. 19-20.
  4. Muhaqqiq Karaki, Jami' al-Maqashid, 1414 H, juz. 4, uk. 23.
  5. Faidh Kasyani, Wafi, 1406 H, juz. 17, uk. 218.
  6. Muhaqqiq sabzawari, Kifayah al-Ahkam, 1423 H, juz. 1, uk. 432-433.
  7. Sheikh Anshari, Makasib Muharramah, 1411 H, juz. 1, uk. 141-145.
  8. Khomeini, Makasib Muharramah, 1415 H, juz. 1, uk. 299.
  9. Yusufi Maqdam, Pazuhesh dar Ghina, 1391 S, uk. 22-31 ; Qazi Zadeh, Gina' az Didgahe Islam, uk. 337-341: Sayyied Karimi, Naqd va Barresiye Taarife Maujud dar Mauzue Ghina, uk. 117-120
  10. Nuri, Musiqi va Ghina' az Didgah-e Eslam, 1385 S, uk. 239-269 ; Izadifard, Pazuhesyi-e Tahlili-e Piramu-e Mabani-e Fiqhi-e Ghina' va Musiqi, uk. 74.
  11. Mahmudi, Masail-e Jadid az Didgah-e Ulama va Maraji'-e Taqlid, 1385 S, juz. 1, uk. 48-54.
  12. Mahmudi, Masail-e Jadid az Didgah-e Ulama va Maraji'-e Taqlid, 1385 S, juz. 1, uk. 48-54.
  13. Mahmudi, Masail-e Jadid az Didgah-e Ulama va Maraji'-e Taqlid, 1385 S, juz. 3, uk. 80.
  14. Mukhtari, va Shadiqi, Ghina' va Musiqi, 1377 S, juz. 3 uk. 2039-2041.
  15. Khamenei, Ghina', 1398 S, uk. 452.
  16. Ghina', Muqaddameh (prolog), 1398 S.

Vyanzo

  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf. Qawa'id al-Ahkam fi Ma'rifat al-Halal wa al-Haram. Riset dan Editor: Sekelompok Penelaah Daftar Intisharat Islami. Qom: Daftar Intisharat Islami wabaste be Jame'e Mudarisin Hauzah Ilmiah Qom, Bustan Kitab, 1413 H.
  • Fadhli, Abdul Hadi dan Muhammad Hadi Ma'rifat. Baresi-e Fiqhi Padide-e Ghina' Mahiyat va Hukm-e An. Terjemah: Mujtaba Ilahi khurasan. Qom: Muasasah Bustan Ketab, 1385 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad Muhsin. Al-Wafi. Riset dan Editor: Dhiya'uddin Husaini Isfahani. Isfahan: Ketab Khune-e Imam Amirul Mukminin Ali as, 1406 H.
  • Izadi Fard, Ali Akbar dan Hussien Kaviyar. Pazuhesyi-e Tahlili-e Piramun-e Mabani-e Fiqhie Ghina' va Musiqi. Jurnal Kawesyha-e Dini, no. 6, musim gugur dan musim dingin, 1390 S.
  • Khamenei, sayyied Ali. Ghina'. Teheran: Intisyhrramah. Teheran: Muasasah Tanzhim va Nahr Asar-e Imam Khomeini. No. 2, musim Panas 1393 S.
  • Muhaqiq Sabzawari, Muhammad Bagir bin Muhammad Mu'min. Kifayah al-Ahkam. Qom: Daftar Intisharat Islami Vabaste be Jame'-e Mudarisin Hauzah Ilmiyah Qom, 1423 H.
  • Muhaqiq Karaki, Ali bin Hussein. Jami' al-Maqasid fi Sharh al-Qawaid. Qom: Muasasah Al al-Bait as, 1414 H.
  • Mahmudi, Sayyied Muhsin. Masail al-Jadid az Didghah-e Ulama va Maraji'-e Taqlid. Varamin: Intisharat Ilmi-e Farhanghi Shahib Zaman, 1385 S.
  • Nuri, Muhammad Ismail. Musiqi va Ghina' az Didghah-e Quran Islam. Qom: Bustan Kitab, 1385 S.
  • Sayyied Karami, Sayyied Abbas. Naqd va Baresi-e Ta'arif-e Maujud dar Maudhu'-e Ghina'. Faslname-e Ilahiyat-e Hunar. no. 2, Musim Panas 1410 H.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Al-Raudhah al-Bahiyah fi Sharh al-Lum'ah al-Damasqiyah. Qom: Toko Buku Davari, 1410 H.
  • Qadhizade, Kazhim. Ghina' az Didghah-e Islam. Fashlname Kavishi-e Nu dar Fiqh. no. 4 dan 5, Musim Panas dan Musim Semi, 1374 S.
  • Sheikh Anshari, Murtadha. Al-makasib al-Muharramah wa al-Bai' wa al-Khiyarat. Qom: Manshrat Dar al-Dzakhair, 1411 H.
  • Sheikh Tousi, Muhammad bin Hassan. Al-Istibshar fima Ikhtalafa min al-Akhbar. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1390 H.
  • Shadiqi, Muhsin va Ridha Mukhtari. Ghina' va Musiqi. Qom: Daftar Tabligat-e Islami Hauzah Ilmiah Qom, 1377 S.
  • Yusufi Muqadam, Muhammad Shadiq. Pazuhesygah-e Ulum va Farhang-e Islami, 1391 S.