Maqam Mahmuwd

Kutoka wikishia

Maqam Mahmuud (Kiarabu: مقام محمود) maana yake ni cheo cha juu zaidi, ambacho Mwenyezi Mungu alimpa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) kwa sababu ya Kuswali swala za usiku na Kukesha kwa ajili ya kufanya ibada. Wafasiri wameelezea madhumuni ya aya ya 79 katika Suratul Al- Israa ya kwamba cheo hichi ni heshima ya uombezi wa Mtume (s.a.w.w) kwa wafuasi wake.

Neno maombezi (الشفاعة) maana yake ni usaidizi (wa kuomba msaada kwa mtu aliyeaminika na kukamilika mbele ya Mwenyezi Mungu kwa madhumuni ya mhalifu kusamehewa makosa yake au kutimiziwa haja ya maombi yake) Ni kana kwamba mtu anayemuomba muombezi haoni nguvu zake peke yake kuwa zinatosha kufikia lengo lake; Kwahiyo, anaongeza uwezo wa muombezi na msaidizi ndani yake ili kufikia kusudi lake.

Baadhi ya wafasiri wameichukulia Maqam Mahmoud kuwa ina maana ya utukufu wa Mtume (s.a.w.w) juu ya viumbe vyote na ukaribu wake wa mwisho kwa Mwenyezi Mungu, ambao bila shaka unajumuisha pia nafasi ya uombezi. Kwa mujibu wa Ziyara ya Ashura, imeelezewa Imamu Hussein (a.s) pia ana cheo hichi cha Maqam Mahmuud.

Aya ya 79 ya Suratul Al- Israa

Umekuja msamiati huu wa (Maqam Mahmuud) katika aya ya 79 ya Surat al-Israa, nayo ni; ((وَ مِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسىَ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحمُوداً ; Na amka usiku kwa ibada,ni ziada ya sunna haswa kwako wewe, huenda Mola wako mlezi akakunyanyua cheo kinacho sifika)).

Cheo kitukufu zaidi(maqam mahmuu) kwa Mtume (s.a.w.w)

Wanavyuoni na wafasiri wa Kiislamu wameichukulia Maqam Mahmud kuwa ni nafasi na cheo kitukufu cha juu zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amempa Mtume (s.a.w.w)[1] kwa sababu ya kuswali swala za usiku(Tahjud) na kukesha kwa ajili ya ibada .

Kuna kauli za wanazuoni Kuhusu maana ya Maqam Mahmuud zikiwa zinaashiria maana sawa na cheo cha uombezi(shafaa)[2]

  • Nafasi ya Uombezi: Wafasiri wengi wa Shia [3] na Sunni [4] kwa kuzingatia hadithi zilizopokelewa katika kipengele hiki wanahesabia ya kwamba Maqam Mahmuud ndio cheo cha uombezi(shafaa), na miongoni mwa hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w), ambazo zinachukulia Maqam Mahmud iliyokuja katika Aya ya 79 ya Surat Al-Israa kuwa ni kama nafasi ya uombezi(shafaa) katika umma wake [5]. Au katika hadithi nyingine iliyopokelewa kutoka kwa Imam Baqir(a.s) na Imam Swadiq(a.s) zinaweka wazi ya kuwa Maqam Mahmuud ndio cheo cha uombezi [6]. Pia kuna baadhi ya wafasiri wameelezea juu ya cheo hichi cha Maqam Mahmuud kuwa ni uombezi mkubwa(Shafaa) [7].
Sayyid Muhammad Husein Tehrani anasema kuwa (Maqam Mahmud) ni ukamilifu na sifa zote alizopewa Mtume (s.a.w.w). bila masharti, na akaendelea kuthibitisha kuwa; Mtume Muhammad(s.a.w) amepewa cheo hicho cha uombezi wa shafaa kwa jumla, kwa hivyo mitume wengine pia wanaombewa naye.
  • Usimamizi wa viumbe: Kundi la wafasiri wanaichukulia Maqam Mahmoud ya Mtume(s.a.w.w) kuwa ni usimamizi wa viumbe vyote, na ndio cheo au nafasi anayowafanyia watu maombezi [8].
  • Kima cha juu zaidi cha ukaribu kwa Mwenyezi Mungu: Imeelezwa katika tafsiri ya Al-Amthal kwamba kuna uwezekano Maqam Mahmuud ni ule ukaribu wa juu zaidi na Muumba, na ndio ambayo inakuwa moja ya athari zake ni uombezi mkubwa(shafaa) [9].

Cheo kitukufu zaidi(maqam mahmuud) kwa Maimamu(a.s.)

Imepokewa katika baadhi ya ziara kutoka kwa Imam Ali(a.s) [10], Imam Hussein(a.s), [11] na Imam al-Ridha(a.s) [12] walikuwa na cheo cha Maqam Mahmuud, na imetajwa katika ziara ya Ashura: “Basi mimi namuomba Mwenyezi Mungu... anijaalie niwe pamoja nanyi katika dunia na Akhera na aniwekee mbele ya haki katika dunia na Akhera na ninamuomba anijaalie nifikie cheo cha Maqam Mahmuud mlichonacho kwa Mwenyezi Mungu [13]

Mfasiri wa Kishia, Nasser Makarem Al-Shirazi kataja: Ijapokuwa mwenye kuhutubia katika Aya ya 79 ya Surat Al-Isra ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani za Allah ziwe juu yake na familia yake), hukumu inaweza kujumlishwa kwa waumini ambao wanaisoma Qur-an na wanasimamisha Swala za usiku, na watakuwa karibu na Mwenyezi Mungu kwa kadiri ya imani na matendo yao na wataombea wengine [14].

Rejea

  1. Tousi, Tibyan, Darul-ihyaa turathul-arabi,juzuu ya 6, kurasa ya 510-511; Tabrasi, Majmau al-bayan, toleo la mwaka 1372, juzuu ya 6, kurasa ya 671; Al-faidh al-kaashan, Tafsiri swafi, toleo la mwaka 1415 hijria, juzuu ya 3, kurasa ya 210; Al-bahran, Al-burhan, toleo la mwaka shamsia 1416 hijria, juzuu ya 3, kurasa ya 569; Al-iyash, Tafsiri al-iyash, toleo la mwaka 1380 shamsia, juzuu ya 2, kurasa ya 314; Tabatabai, Tafsiri al-mizan, toleo la mwaka 1377 shamsia, juzuu ya 1, kurasa ya 178,; Makarimu Shiraz, Tafsiri al-amthal, juzuu ya 9, kurasa ya 94; Jawad Amuli, Tafsiri Tasnim, toleo la mwaka 1378 shamsia, juzuu ya 4, kurasa ya 285; Shibru, Tafsiri al-quran al-karim, toleo la mwaka 1412 Qamaria, kurasa ya 286; Fakhru Razi, Mafatih al-aib, toleo la mwaka 1420 Qamaria, juzuu ya 21, kurasa ya 386-387; Al-Qurtubi, Yaumu al-faziu al-akbar, Maktabatul-Quran, kurasa ya 155
  2. Tabrasi, Maajmau al-bayan, toleo la mwaka 1372 shamsia, juzuu ya 6, kurasa ya 670; Tabrasi, Jawamiu al-jamiu, juzuu ya 2, kurasa ya 341
  3. Tousi, Tibyan, Darul-ihyai turathu al-arab, juzuu ya 6, kurasa ya 512, toleo la mwaka 1372 shamsia, juzuu ya 6, kurasa ya 671; Al-faidh al-kaashan, Tafsir swafi, toleo lamwaka 1415 hijria,juzuu ya 3, kurasa ya 211-212; Al-bahran, Al-burhan, toleo la mwaka 1416 hijria, juzuu ya 3, kurasa ya 570-574; Al-iyaash, Tafsir al-iyaash, toleo la mwaka 1380 shamsia, juzuu ya 2, kurasa ya 314; Tabatabai, Tafsir al-mizan, toleo la mwaka 1377 shamsia, juzuu ya 1, kurasa ya 178; Makarem Shiraz, Tafsir al-amthal, juzuu ya 9, kurasa ya 94; Jawad Amuli, Tafsir tasnim, toleo la mwaka 1378 shamsia, juzuu ya 4, kurasa ya 285, Shibr, Tafsir al-Quran al-karim, toleo la mwka 1412 Qamaria, kurasa ya 286
  4. Fakhru Razi, Mafatihu al-aib, toleo la mwaka 1420hijria, juzuu ya 21, kurasa ya 381,; Al-Qurtubi, Yaum al-faziu al-akbar, Maktabatul-Quran, kurasa ya 155
  5. Ibnu Hambal, Musnad Ibnu Hambal, Darul-sadri, juzuu ya 2, kurasa ya 441
  6. Ayaash, Tafsir al-ayaash, toleo la mwaka 1380 shamsia, juzuu ya 2, kurasa ya 314
  7. Tabatabai, Tafsir al-mizan, toleo la mwaka 1377 shamsia, juzuu ya 1, kurasa ya 178; Makarem Shiraz, Tafsir al-amthal, juzuu ya 9, kurasa ya 94; Jawad Amuli, Tafsir tasnim, toleo la mwaka 1378 shamsia, juzuu ya 4, kurasa ya 285
  8. Tabrasi, Majmau al-bayan, toleo la mwaka 1372, juzuu ya 6, kurasa ya 671,; Ibnu Arabi, Al-futuhat al-makkia, Taasisi ya ahlulbayt, juzuu ya 4, kurasa ya 57; Al-arusi, al-hauyizi, Tafsir al-thaqalein, toleo la mwaka 1407 hijria, juzuu ya 3, kurasa ya 206
  9. Makarem Shiraz, Tafsir al-amthal, juzuu ya 9,kurasa ya 94
  10. Al-majlis, Tahdhib al-ahkam, toleo la mwka 1407 hijria, juzuu ya 6, kurasa ya 30
  11. Al-majlis, Biharu al-anuar, toleo la mwaka 1403 hijria, juzuu ya 101, kurasa ya 292
  12. Suduq, Man la yahdhuruhu al-faqih, toleo la mwaka 1413 hijria, juzuu ya 2, kurasa ya 605; Al-majlis, Tahdhib al-ahkam, toleo la mwaka 1407 hijria, juzuu ya 6, kurasa ya 88
  13. Al-maljis, Biharu al-anuar, toleo la mwaka 1403, juzuu ya 101, kurasa ya 292
  14. Makarem Shiraz, Tafsir al-amthal, juzuu ya 9, kurasa ya 94

Vyanzo

  • Ibn Hanbal, Ahmad, Musnad, Beirut, Dar Sadir, [Bita].
  • Ibn Arabi, Mohyi al-Din, Futuhat Makkiyyah, Qom, Ahlul-Al-Bayt (A.S.) Al-ah-yai Turath [Bita].
  • Bahrani, Seyyed Hashim, Al-Burhan Fi Tafsir al-Qur'an, Tehran, Ba'ath Foundation, 1416 AH.
  • Jawadi Amuli, Abdullah, Tafsir Tasnim, Qom, Esra Publishing Center, 1378.
  • Shabr, Seyyed Abdullah, Tafsir al-Qur'an al-Karim, Beirut, Darul-Balagha litabaati wanashr (Dar al-Balagha kwa uchapishaji) 1412 AH.
  • Saduq, Muhammad bin Ali bin Babaweyh, Man la yahdhuru al-Faqih, tahkiki (utafiti wa) Ali Akbar Ghafari, Qom, Ofisi ya Machapisho ya Kiislamu, toleo la pili, 1413 AH.
  • Tabatabai, Seyyed Mohammad Hossein, Tafsir al-Mizan, Qom, Ofisi ya Machapisho ya Kiislamu, 1377.
  • Tabarsi, Fazl bin Hasan, Tafsir al-Jawami’i al-Jamei’i, Tehran, Chuo Kikuu cha Tehran chini ya uongozi wa vyuo vya elimu ya dini vya Qom, 1377.
  • Tabarsi, Fazl bin Hasan, Majma al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an, Tehran, Nasser Khusruw Publications, 1372.
  • Tusi, Muhammad bin Hassan, al-Tabyan fi Tafsir al-Qur'an, Beirut, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, [Bita].
  • Tusi, Muhammad bin Hassan, Tahzeeb al-Ahkam, iliyofanyiwa utafiti na Hasan Musavi Khurasan, Tehran, Dar al-Kitab al-Islamiya, chapa ya 4, 1407 AH.
  • A’rusi Huwayzi, Abd Ali bin Jumaa, Tafsir Nuur al-Thaqalayni, Qom, Ismailian Publications, 1415 AH.
  • A’yashi, Mohammad Bin Masoud, Kitab al-Tafsir, Tehran, Ilmia Printing House, 1380 AH.
  • Fakhr Razi, Muhammad bin Omar, Mafaatih al-Ghaib, Beirut, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, 1420 AH.
  • Faiz Kashani, Mola Muhsin, Tafsir Al-Safi, Tehran, Sadr Publications, 1415 AH.
  • Qurtubi, Muhammad bin Ahmad Al-Ansari, Yum al-Faza’a al-Akbar, mtafiti: Muhammad Ebrahim Salim, Misr, al-Tabar wa al-Nashar Maktaba al-Qur’an, [Bita].
  • Majlisi, Mohammad Baqir, Bihar al-Anwar Akhbar al-Aima al-At-har, Beirut, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, 1403 AH.
  • Makarem Shirazi, Nasser, na wengine, Tafsir al-Namune, Qom, Dar al-Kitab al-Islamiya, 1370.