Nenda kwa yaliyomo

Sakaratul Maut

Kutoka wikishia

Sakaratul Maut (Kiarabu: سكرات الموت) ni hali ya uchungu wa kutoka roho ambayo humpata mtu wakati wa kukata roho. Jambo hili limezungumziwa katika Qur'ani kwenye Aya ya 19 ya Surat Qaaf. Kwa mujibu wa Hadithi mbalimbali uchungu wa kutokwa roho ni mgumu mno na watu wote huonja na kupitia tajiriba hiyo wakati wa kifo.

Aidha kwa mujibu wa hadithi mbalimbali, baadhi ya waumini ambao hukata roho au hutokwa na roho kwa ugumu na uchungu, husamehewa dhambi zao. Katika maneno ya Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) kumebainishwa njia mbalimbali za kurahisisha ugumu wa uchungu wa kutoka roho ambapo baadhi ya mambo hayo ni: Kuunga udugu, kuwatendea wema baba na mama, kuwasaidia ndugu wa kidini, kusoma Surat Yasin na Saffat, kumpenda Imamu Ali (a.s) na kukithirisha kuzuru kaburi la Imamu Hussein (a.s).

Utambuzi wa Maana

Sakaratul Mauti (uchungu wa kutoka roho) ni hali ambayo inaelezwa kuwa inafanana na kulewa ambayo humtokea mtu wakati wa kukata roho. Katika hali hii mtu hupoteza uwezo wa kuainisha mambo.[1] Sakarat ni wingi wa sakrah ambayo ina maana ya kulewa, ugumu, uchungu na hali ya kutangatanga.[2] Neno mauti nalo lina maana ya kifo.[3]

Katika Aya na Hadithi

Ndani ya Qur’an na katika Aya ya 19 ya Surat Qaaf, neno «Sakaratul-Maut» limetumika: «وَجاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ذَلِكَ مَا كُنْتَ مِنْهُ تَحِیدُ; Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia».

Katika hadithi pia neno «Sakaratul-Maut»[4] na «Sakaratul-Maut»[5] yametumika. Katika kitabu cha hadithi cha Bihar al-Anwar, kuna sehemu maalumu imetengwa kuzungumzia Sakaratul Maut na kuna hadithi 52 zilizotajwa katika mlango huu.[6] Imenukuliwa katika kitabu cha Tahdhib al-Ahkam cha Sheikh Tusi dua kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ambayo sehemu yake inasema: «Ewe Mola wangu! Naomba unisaidie katika Sakaratul-Maut (uchungu wa kutoka roho)».[7]

Sakaratul Maut ilivyo

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Sheikh Saduq kutoka kwa Imamu Ali (a.s) ni kwamba: Hali mbaya kabisa zinazomkabili mwanadamu ni lahadha tatu: Wakati anapokabiliwa na kifo, wakati anapoamka kutoka kaburini na wakati atakapokutana (kukutana huku sio kwa kimwili na kwa kuona kwa macho) na Mwenyezi Mungu.[8] Katika kitabu cha Payam Qur’an (Ujumbe wa Qur’an) moja kati ya Tafsiri za Qur’an za kimaudhui, kwa kutumia neno «Sakrat al-Maut» imekuja katika Aya ya 19 ya Surat al-Qaaf kwamba, mauti huambatana na uchungu, ugumu na wahka.[9] Kwa mujibu wa kitabu hiki, kwa mujibu wa hadithi mbalimbali hata Mitume na mawalii wa Mwenyezi Mungu pia hawakusalimika na matatizo na machungu ya kutoka roho.[10]

Tofauti ya Uchungu wa Kifo cha Muumini na Kafiri

Imenukuliwa katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ya kwamba, muumini hutokwa na roho kwa wepesi sana, lakini baadhi ya waumini hutokwa na roho kwa taabu na mashaka makubwa na sababu ya hilo ni kutoharishwa na kusafishwa madhambi yao; kama ambavyo mauti ya kafiri ni magumu mno, lakini kutoka roho baadhi ya makafiri huwa rahisi ili kufidia wema na hisani yao walioitenda hapa duniani na huko Akhera watapata adhabu tu.[11]

Njia za Kupunguza Uchungu wa Kutoka Roho

Katika baadhi ya hadithi, kumetajwa baadhi ya mambo ambayo yanapelekea kupunguza uchungu wa kutoka roho. Kwa mfano, Sheikh Kulayni amenukuu hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) ambayo inasema: Mwenye kumvisha nguo ndugu yake katika dini, inakuwa ni wajibu kwa Mwenyezi Mungu kumvalisha nguo ya peponi na kumrahisishia uchungu wa kutoka roho.[12]

Mambo mengine ambayo kwa mujibu wa hadithi yametajwa kuwa ni sababu ya kupungua uchungu wa kutoka roho ni: Kuunga udugu,[13] kuwatendea wema baba na mama,[14] kufunga Saum ya Ramadhani,[15] kusoma Surat Yassin,[16] kufunga Saumu mwezi wa Rajab,[17] kumpenda Imamu Ali (a.s)[18] na kwenda kuzuru kaburi la Imamu Hussein (a.s).[19] Muhammad Mahdi Naraqi anasema katika kitabu cha Jamiu al-Sadat: Kwa mujibu wa hadithi, mtu ambaye mama yake hatokuwa radhi naye, atakabiliwa na uchungu zaidi wa kutoka roho na adhabu ya kaburi.[20]

Kupunguza Uchungu wa Kutoka Roho kwa Mtu Anayekata Roho

Sahib al-Jawahir, mmoja wa mafakihi wa Kishia anasema: kwa mujibu wa hadithi, ni mustahabu kumuweka mtu anayekata roho mahali ambapo alikuwa akiswalia. Kufanya hivi kunampunguzia uchungu wa kutoka roho.[21] Muhaqiq Karaki pia akitumia kama hoja hadithi kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) anasema, ni mustahabu kumsomea Surat al-Saffat mtu anayekata roho.[22] Kwa mujibu wa hadithi hii, kama Surat al-Saffat itasomwa upande wa mto wa mtu anayekata roho, Mwenyezi Mungu humchukua haraka na kwa wepesi mtu huyo.[23] katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ni kwamba, kumsomea Surat Yassin mtu anayekata roho, kunamrahisishia kifo.[24]

Masuala Yanayo Fungamana

Rejea

  1. Tabatabai, al-Mīzān, juz. 18, uk. 348; Warām, Majmū'at Warām, juz. 1, uk. 26.
  2. Kamusi ya Dakhuda, Chini ya neno Sakarat (سكرة).
  3. Kamusi ya Dakhuda, Chini ya neno Mauti (موت).
  4. Kaf-'ami, al-Baladu al-Amīn, uk. 105; Sheikh Tusi, Misbāh al-Mutahajjid, juz. 2, uk. 443.
  5. Sheikh Tusi, Tahdhīb al-Ahkām, juz. 3, uk. 93.
  6. Tazama: Majlisi, Bihār al-Anwār, 1403 AH, juz. 6, uk. 145-173.
  7. Sheikh Tusi, Tahdhīb al-Ahkām, 1407 AH, juz. 3, uk. 93.
  8. Sheikh Saduq, al-Khisāl, juz. 1, uk. 119.
  9. Makarim Shirazi & Wenzake, Payam Qur'an, juz. 5, uk. 431.
  10. Makarim Shirazi & Wenzake, Payam Qur'an, juz. 5, uk. 431.
  11. Sheikh Saduq, 'Uyūn Akhbār ar-Ridhā, juz. 1, uk. 274-275.
  12. Kulaini, al-Kāfī, juz. 2, uk. 204.
  13. Sheikh Saduq, al-Āmālī, uk. 208.
  14. Sheikh Tusi, al-Āmālī, uk. 432.
  15. Sheikh Saduq, Man Lā Yahdhuruhu al-Faqīh, juz. 2, uk. 74.
  16. Sheikh Saduq, Thawāb al-A'māl, uk. 111-112.
  17. Sheikh Saduq, Fadhā'il al-Ashhur Athalathat, 1396 AH, uk. 12.
  18. Sheikh Saduq, Fadhā'il as-Shī'ah, uk. 4.
  19. Ibn Qaulawih, Kāmil az-Ziyārāt, uk. 150.
  20. Narraqi, Jāmi' as-Sa'ādāt, juz. 2, uk. 273.
  21. Najafi, Jawāhir al-Kalām, juz. 4, uk. 18.
  22. Muhaqqiq Karaki, Jāmi' al-Maqāsid, juz. 1, uk. 353.
  23. Kulaini, al-Kāfī, juz. 3, uk. 126.
  24. Muhaddith Nuri, Mustadrak al-Wasā'il, juz. 2, uk. 136.

Vyanzo

  • Qur'an
  • Dakhuda, Ali Akbar, Lughat-name Dakhuda. Muasase Lughat-name Dakhuda, 1341 HS/1963.
  • Ibn Qaulawih, Ja'far bin Muhammad, Kāmil az-Ziyāraāt, Mhakiki: Abdul Husain Amini, Najaf: Dar al-Murtadhawiyah, Chapa ya kwanza, 1356 HS/1978.
  • Kaf-'ami, Ibrahim bin Ali, Al-Baladu al-Amin wa A'ud-Dar al-Hasīn, Beirut: Muasase al-A'lami Li al-Matbu'at, Chapa ya kwanza, 1418 H.
  • Kulaini, Muhammad bin Ya'qub, Al-Kāfī, Mhakiki: Ali AKbar Ghaffari & Muhammad Akhudi, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, Chapa ya nne, 1407 H.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Bihār al-Anwār al-Jāmi'ah Li Durar Akhbār al-A'immah al-Athār, Beirut: Dar at-Turath al-'Arabi, Chapa ya pili, 1403 H.
  • Makarim Shirazi, Nashir & Wenzake, Payam Qur'an, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, 1377 HS/1999.
  • Muhaddith Nuri, Mirza Hussein, Mustadrak al-Wasā'il wa Mustanbat al-Masā'il. Mhakiki: Muasase Āhlul-Bait (a.s), Beirut, Chapa ya kwanza, 1408 H.
  • Muhaqqiq Karaki, Ali bin Hussein, Jāmi' al-Maqāsid Fī Sharh al-Qawā'id, Qom: Muasase Āhlul-Bait (a.s), Chapa ya pili, 1414 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawāhir al-kalām Fī Sharh Sharā'i' al-Islām, Mhariri: Abbas Quchani & Ali Akhundi, Beirut, Dar Ihya' at-Turath al-Arabi, Chapa ya saba, 1404 H.
  • Narraqi, Muhammad Mahdi, Jāmi' as-Sa'ādāt, Mhariri: Muhammad Kalantir, Beirut: Muasase al-A'lami, Chapa ya kwanza, 1383 HS/2005.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, 'Uyūn Akhbār ar-Ridhā, Mhakiki & Mhariri: Mahdi Lajurdi, Tehran, Nashr Jahan, Chapa ya kwanza, 1378 HS/2000.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Al-Khisāl, Mhakiki: Ali AKbar Ghaffari, Qom: Jami'e Mudarrisim. Chapa ya kwanza, 1362 HS/1984.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Al-Āmālī, Tehran, Ketabchi, Chapa ya nane, 1376 HS/1998.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Fadhā'il al-Ashhur at-Thalāthah, Mhakiki: Ghulam Ridha Irfaniyan Yazdi, Qom: Kitab Furushi Dawari, Chapa ya kwanza, 1396 HS/2018.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Fadhā'il as-Shī'ah, Tehran, A'lami, Chapa ya kwanza.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Man Lā Yahdhuruhu al-Faqīh, Mhakiki & Mhariri: Ali AKbar Ghaffari. Qom: Daftar Intisharat Islami Wabaste Be Jami'e Mudarrisin Hauze Ilmiyye Qom, Chapa ya pili, 1413 H.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Thawāb al-A'māl wa 'Iqāb al-A'māl, Qom, Dar as-Sharif ar-Ridha, Chapa ya pili, 1406 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Al-Āmālī, Mhariri: Muasase al-Biitha, Qom, Dar at-Thaqafah, Chapa ya kwanza, 1414 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Misbāh al-Mutahajjid wa Silāh al-Muta'abbid, Beirut: Muasase Fiqh as-Shi'ah, Chapa ya kwanza, 1411 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Tahdhīb al-Ahkām, Tehran, Dar al-Kutub al-Islamiyyah, Chapa ya nne, 1407 H.
  • Waram bin Abi Faras, Mas'ud bin Issa, Majmū'at Warām, Qom, Maktabat Faqih, Chapa ya kwanza, 1410 H.