Adhabu ya Kaburi
Adhabu ya kaburi (Kiarabu: عذاب القبر) ni shinikizo la mateso na dhiki anayopata mtu akiwa katika ulimwengu wa kaburini (ulimwengu wa Barzakh) baada ya kifo chake. Kulingana na Hadithi; kufitinisha, kutojali kuhusu usafi na tohara kutokana na uchafu (najisi), tabia za maudhi kwa mwanaume dhidi ya mkewe, mtu kutokuwa na adabu (kutokuwa na tabia njema) na familia yake na kudharau Sala, ni baadhi ya sababu zinazo sababisha adhabu ya kaburi. Kwa upande wa pili; Kumtembelea Imamu Hussein (kuzuru kaburi lake) (a.s), kubahatika kuzikwa kwenye mji wa Najaf, kuwapenda Ahlul Bayt wa Mtume (s.a.w.w), kufa kati ya nyakati za Alasiri ya siku Alhamisi hadi Alasiri ya siku ya Ijumaa, n.k., zimehesabiwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayosaidia katika kuondoa adhabu ya kaburi.
Ukiachana na Dhiraaru bin Omar, ambaye ni mwanafunzi wa Wasil bin ‘Ataa, Waislamu wote walio bakia wanaamini suala la kuwepo kwa adhabu ya kaburi. Wanazuoni wa fani ya theolojia wametumia Aya ya 11 ya Surat Ghafir kama ni ithibati na ushahidi kuwepo kwa suala la adhabu ya kaburi. Ila kuna khitilafu za maoni kuhusu suala la kwamba je, ni ule mwili mkamilifu (ulioboreshwa baada ya mauti ambao ni mwili wa Kibarzakh) ndiwo utakao adhibiwa au ni mwili huu huu wa duniani? Kuhusu hili wanazuoni wengi wa kitheolojia wanaamini kwamba; adhabu ya kaburi inahusiana na mwili wa Kibarzakh, mwili ambao umeboreshwa kulingana na hali ya ulimwengu huo ulivyo.
Muhammad bin Ismail al-Bukhari, mmoja wa wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Sunni, katika kitabu chake kiitwacho ‘Sahih al-Bukhari’, amenukuu Hadithi kutoka kwa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) isemayo kwamba; maiti huadhibiwa kutokana na kilio cha jamaa zake wanao mlilia kaburini kwake. Kulingana na maelezo ya Yahya bin Sharaf Nawawi, mfasiri wa Sahih Muslim, ni kwamba; wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Sunni wameitafsiri hadithi hii na kuipatia maana nyengine, kinyume na maana Dhahiri ya Hadithi hii. Ameelezea akisema kuwa; wao wamelazimika kufanya hivyo kwa sababu, kuadhibiwa kwa maiti kutokana na kuliliwa jamaa zao walio hai, hakuendani na bayana za Aya ya 18 ya Surat Fatir, ambayo inasema kwamba; hakuna mtu atakaye beba mzigo wa mwingine. Pia, kulingana na maelezo ya bibi Aisha, Hadithi hii haijapokewa kwa usahihi kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), yaani kumepita mchanganyiko wa kuto kuelewa maneno ya bwana Mtume (s.a.w.w).
Ufafanuzi wa Mofolojia na Nafasi ya Adhabu ya Kaburi
Adhabu ya kaburi ni mateso na shida zinazomwandama mwanadamu baada ya kifo chake hali akiwa katika maisha ya ulimwengu wa Barzakh. Ulimwengu wa kaburi ni ulimwengu ujulikanao kwa jina la Barzakh, ambao huanza baada ya kumalizika maisha ya duniani, na hudumu hadi siku ya Kiyama. [1] Kuna mifano kadhaa katika Hadithi iliyotajwa kuhusiana na adhabu ya kaburi, miongoni mwayo ni; joto la moto, shinikizo la kufinya na ardhi, kutufunwa na wadudu, na kupata khofu ilio furutu ada. [2]
Kulingana maelezo ya Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), iliyo nukuliwa katika kitabu Man laa Yahdhurhu al-Faqih, ni kwamba; adhabu ya kaburi inamhusu kila mtu miongoni mwa wafu, bila ya kutofautisha baina ya yule aliye kufa na kuzikwa na yule aliye kufa na kubaki bila ya kuzikwa. [3] Pia kwa msingi wa Hadithi nyingine iliyo nukuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) katika kitabu Bihar al-Anwar, ni kwamba; watu wengi miongoni mwa wanadamu watapata shinikizo la adhabu ya kaburi. [4]
Katika dua na maombi yaliyo nukuliwa kutoka kwa Maimamu watoharifu, kuna ibara kadhaa zinazoashiria naombi yao ya kumtaka Mwenye Ezi Mungu awaepushie ukali adhabu ya kaburi. [5] Kwa mfano, Mtume (s.a.w.w) alipomzika binti yake (Ruqayyah), aliomba Mwenye Ezi Mungu amwepushie adhabu ya kaburi lake. [6] Au mfano mwengine, ni kabla ya kumzika bibi Fatima bint Asad, alilala kaburini kwa bibi Fatima binti Asad ili amtimizie ahadi aliyompa, ya kumtaka Mwenyezi Mungu amlinde kutokana na shinikizo la adhabu ya kaburi. [Maelezo 1] [7] Pia bibi Fatima (s.a) katika wosia wake, alimtaka Imamu Ali (a.s) abaki kwenye kaburi lake na amsomee Qur’ani pamoja na dua baada ya kuzikwa kwake.[8]
Katika vitabu vya rikodi za hadithi, hadithi zote zinazohusiana na masuala ya kaburi zimekusanywa katika sura (mlango) maalumu. Mkusanyaji wa Hadithi za, Sheikh Muhammad Baqir Majlisi, katika kitabu chake kiitwacho Bahar-ul-Anwar, amenukuu Hadithi 128 kuhusiana na masuala ya kaburi katika sura moja iliyopewa jina la (أحوال البرزخ و القبر و عذابه و سؤاله و سائر ما يتعلق بذلك ; Hali au mambo yanayo husiana na ulimwengu wa Barzakh, kaburi pamoja na adhabu yake). [9]
Sababu za Adhabu ya Kaburi
Kulingana na Hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s) katika kitabu kiitwacho ’Ilalu al-Sharaai’u, kuna sababu kadhaa zinazo sababisha adhabu ya kaburi. Baadhi ya sababu hizi ni:
- Kufitinisha watu
- Kutokuwa na uangalifu juu ya usafi na kutojali najisi
- Mume kujitenga na mkewe [10]
Sheikh Abbas Qummi, akiashria Hadithi hiyo, ameeleza kuwa adhabu kuu za kaburi zinahusiana na mambo haya matatu. [11] Mambo mengine ambayo husababisha adhabu ya kaburi ni pamoja na:
- Tabia mbaya: Kulingana na Hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w), ni kwamba sababu ya adhabu ya kaburi aliyopata Saad bin Muadh ilisababishwa na tabia mbaya dhidi ya familia yake. [12]
- Kudharau sala: Kulingana na Hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha "Al-Mawa'idhu al-‘Adadiyyah" cha Ali Mishkini, ni kwamba; uzembe katika kutekeleza ibada ya sala husababisha kubanwa na kufinywa na kaburi.[13]
- Kupoteza na kuto jali neema za Mungu:[14] Kulingana na moja ya Hadithi, ni kwamba; adhabu ya kaburi kwa Mwislamu ni kafara ya neema ambazo amezipoteza katika uhai wake. [15]
Pia, kulingana na Hadithi kadhaa, ni kwamba; kusengenya,[16] kuto shikamana na uongozi wa Maimamu Maasumu (a.s),[17] kutosaidia wanaodhukumiwa, [18] na kusali bila udhu[19] ni miongoni mwa mambo yanayo sababisha adhabu ya kaburi. Katika kitabu cha Jami' al-Sawa'id, imeelezwa kwamba; mtu aliyekosa radhi za mamaye hupata tabu zaidi wakati wa kifo chake (katika sakarati al-Maut) na pia hupata adhabu kubwa zaidi ya kaburi baada ya kufa kwake. [20]
Sababu Zinazopelekea Kupunguziwa Adhabu ya Kaburi
Katika vitabu vya Hadithi, kuna mambo kadhaa yaliotajwa, ambayo huwa ni sababu ya kuepukana au kupata angalau takhfifu ya shinikizo la adhabu ya kaburi, baadhi yake ni kama ifuatavyo:
- Upendo kwa Ahlul Bayt (a.s): Kulingana na Hadithi fulani iliyopokelewa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) katika kitabu kiitwacho Bahar-ul-Anwar, ni kwamba; upendo wa kumpenda bwana Mtume na Ahlul Bayt wake (a.s), hupelekea mtu kufaidika katika sehemu saba, moja wapo ikiwa ni kaburini.[21]
- Kusali sala za sunna maalum: Kwa misingi wa baadhi ya Hadithi zilizonukuliwa na Sayyid bin Tawus katika kitabu chake kiitwacho Iqbalu- al-A'mal kutoka kwa Ma'asumina (Maimamu watoharifu), ni kwamba; kusali sala maalum zilizo suniwa katika miezi ya Rajab na Shaban, hupelekea mja kuondolewa adhabu ya kaburi.[22]
- Kuzikwa katika mji wa Najaf: Kulingana na kauli ya Hassan bin Muhammad Dailami katika kitabu cha Irshadu-l-Qulub akinukuu maelezo ya Hadithi, amesema kwamba; mojawapo ya sifa za udongo wa Najaf ni kwamba, kuzikwa katika udongo huo hupelekea mtu kuepukana na adhabu ya kaburi na kuto kabiliwa na maswali ya Malaika maarufu wanao wanao wakabili maiti makaburini mwao, waitwao Munkar na Nakir.[23]
- Kusoma Qur'ani: Katika vyanzo vya Hadithi, kuna Hadithi kuhusu faida za Sura maalumu, ambazo kwa mujibu wa Hadithi hizo, ni kwamba; iwapo mtu atadumisha kuzisoma Sura hizo za Qur'ani, hupelekea kuondolewa adhabu ya kaburi; miongoni mwazo ni Sura ni Surat Zukhruf na surat Nisaa, ambazo yabidi mtu kudumisha kusoma Sura hizo kila Ijumaa, [24] na Sura nyengine ni Surat Takathur, ambayo yatakiwa mtu kudumisha kuisoma Sura hiyo kila wakati wa kulala.[25]
- Kuweka majiti mawili mabichi kaburini karibu na maiti: Kwa misingi ya Hadithi ilioko katika kitabu cha Hadithi kiitwacho al-Kafi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), ni kwamba; falsafa ya kuweka majiti mawili mbichi (moja ubavuni mwa kuli na la pili ubavuni mwa kushoto) pembeni mwa maiti, ni kuondolewa adhabu ya kaburi. [26]Pia, kwa misingi ya Hadithi nyingine, ni kwamba; baada ya kumzika maiti, yatakiwa kumwagilia maji juu ya kaburi lake, kwa msingi wa Hadithi hiyo ni kwamba, kumwagilia maji juu ya kaburi la maiti baada ya kuzikwa, husababisha kuondolewa kwa adhabu ya kaburi.[27]
Baadhi ya mambo mengine ambayo, kulingana na Hadithi, husababisha kuondolewa au kupunguzwa kwa adhabu ya kaburi, ni kama ifuatavyo:
- Kimtembelea Imam Hussein (a.s), yaani kuzuru kaburi lake (a.s).[28]
- Kurukuu rakaa kamilifu katika sala.[29]
- Kusali sala za usiku.[30]
- Kufunga saumu siku nne za mwezi wa Rajab.[31]
- Kufariki dunia baina ya muhula uliopo kati ya alasiri ya siku ya Alhamisi hadi alasiri ya siku Ijumaa.[32]
- Kupatana na kuishi na mumewe asiye na adabu au aliye maskini.[33]
- Kusamehe mume mahari.[34]
- Amali njema za mtoto wa maiti atendazo kwa ajili ya maiti huyo baada ya kifo, au hata amali nyengine njema atendazo katika maisha ya kila siku. Kiufupi kuwa na mtoto mwema hupelekea kupunguziwa au kuondolewa kwa adhabu za kaburi kwa wazee wa mtoto huyo.[35]
Kwa mujibu wa maoni ya Imam Khomeini yaliomo katika kitabu chake Sherhe Chehel Hadith, kiwango cha muda wa kudumu kwa adhabu ya kaburi na adhabu ya ulimwengu wa Barzakh, ni sawa na kiwango cha mapenzi kupenda dunia na kushikamana nayo. Kwa msingi huu basi, kadiri ya mapenzi ya dunia ya mja yatakavyopungua, atapata afueni zaidi katiak ulimwengu wake wa Barzakh, na kaburi la mja litakuwa na wasaa na nuru zaidi kwa ajili yake.[36]
Je, kilio cha Jamaa za Marehemu Kinaweza Kumsababishia Adhabu ya Kaburi?
Katika vyanzo vya Hadithi vya Ahlu-Sunna, kuna Hadithi inayohusishwa na Mtume (s.a.w.w) inasemayo kwamba; maiti huadhibiwa kaburini kwake kutokana na kilio cha jamaa zake. [37] Wasimulizi wa Hadithi hii ni Khalifa wa Pili na Abdullahi bin Umar, ila mujibu wa maelezo ya bibi Aisha, ni kwamba; wapokezi hawa hawakuisajili Hadithi hiyo kwa usahihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w); [38] kwani Mtume (s.a.w.w) alisema: "Maiti huadhibiwa kwa dhambi zake akiwa kaburini mwake, ambapo wakati huo huo jamaa zake nao pia huwa wanamlilia maiti huyo." [39] Kulingana na maelezo ya Nawawi, mfasiri wa Sahih Muslim, ni kwamba wanazuoni wa madhehebu ya Ahl-Sunnah wamekhitilafiana katika kuifsiri hadithi hiyo; wengine wamesema kwamba, Hadithi hii inahusiana na maiti ambao wameweka wosia wa kutaka kuliliwa baada ya kifo chao, huku wengine wakisema kwamba, suala la kuadhibiwa kwa maiti kutokana na matendo ya watu walio hai haiendani na Aya isemayo: (وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ; Na wala Mtu hatabeba mzigo (dhambi) wa mtu mwingine).[40].[41]
Je, Adhabu ya Kaburi Inahusiana na Mwili wa Duniani au wa Barzakh?
Kuna tofauti za maoni na dharia kuhusu mwili ambao utaadhibiwa kupiti adhabu ya kaburi. Swali muhimu ni kwamba je, adhabu ya kaburi inahusiana na mwili wa kidunia au mwili wa kiroho (mwili wa ulimwengu wa Barzakh)? Inasemekana kwamba; kulingana na imani maarufu ya wasomi na wanafalsafa, roho ya mwanadamu baada ya kifo huhamia kwenye mwili mwengine ambao ni wa kiroho. Mwili huu ni kama mwili wa kidunia, isipokuwa tofauti yake ni kwamba mwili huu huwa hauna nyenzo za kimaada zinazoweza kuhisika kwa hisia za kidunia, ambapo mwili huu huwa hauna wingi wala uzito.[42] Hata hivyo, inaaminika kuwa Sayyid Murtadha na Sadidu al-Ddin Hamsi Razi, miongoni mwa wanafalsafa wa madhehebu ya Shia, wanaamini kwamba; baada ya kifo, roho hurudi kwenye mwili huu wa kidunia na shinikizo la adhabu ya kaburi huhisiwa na mwili huu huu wa kidunia.[43] Kulingana na kauli ya Abdulrazzaq Lahiji, ni kwamba; wale wanaoamini kwamba baada ya mja kufariki, roho yake nayo huwa imekamilisha safari yake, yaani roho nayo hufariki kwa kufariki kwa mwili, wao wanaoamini kwamba adhabu ya kaburi inahusiana na mwili, lakini wale wanaoamini uendelevu wa maisha ya roho baada ya kufariki kwa mja, wao wanaamini kwamba baada ya kifo mja, roho hurudi kwenye mwili wake wa kidunia na adhabu ya kaburi ima huhusiana na roho ya mja huyo, au kwamba adhabu hiyo huhisiwa na roho pamoja na mwili wake.[44]
Kulingana na mailezo ya Abu al-Hasan al-Ash'ari, mwanzilishi wa madhehebu ya Ash'ari, ni kwamba; Waislamu wamekhitalifiana kinadharia juu ya suala adhabu ya kaburi. Yeye aliamini kwamba, Waislamu wengi wanaamini juu ya uwepo wa adhabu ya kaburi, akifafanua amesema kwamba; miongoni mwa walio amini itikadi ya kuwepo kwa adhabu ya kaburi ni wafuasi wa madhehebu ya Mu'tazila na Khawarij.[45] Hata hivyo, Ibn Abi al-Hadid amenukuu kutoka kwenye kitabu cha Qadhi al-Qudhat kiitwacho “Tabaqat al-Mu'tazila” ya kwamba; sababu iliyopelekea watu kunasibisha itikadi ya kuto kuamini uwepo wa adhabu ya kabiri, inatokana na Imani ya Dharar bin Umar, ambaye ni mwanafunzi wa Wasil bin ‘Ataa, ya kuto waamini uwepo wa adhabu ya kaburi, jambo ambalo limepelekea watu kuamini kwamba wafuasi wote wa madhehebu ya Wa-Mu'tazila wanapingana na imani hiyo, hali ya kwamba wafuasi wa madhehebu ya Mu'tazila wanaamini uwepo wa adhabu ya kaburi. Kwa hiyo ni idadi ndogo tu kati yao ambao hawana uhakika wa kuwepo kwa adhabu ya kaburi, ila wengi wao wanaamini juu ya imani hiyo, haidhuru kwamba wao wainasibisha adhabu hiyo ya kaburi kwenye roho sio mwili. [46]
Ithibati Kutoka katika Qur’ani
Kulingana na kile alichokinukuu Allama Majlisi kutoka kwa Sheikh Bahai, ameeleza ya kwamba; ithibati na kielelezo muhimu kilicho tumika katika vitabu vya fani ya akida, katika kusimamisha hoja juu suala la uwepo wa adhabu ya kaburi, ni ile Aya isemayo: (قالُوا رَبَّنا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَ أَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ ; Wakasema (wtasema wakiwa mbele ya Mola wao), "Ewe Mola wetu Mlezi! Umetuua mara mbili na ukatuhuisha mara mbili). [47] Kupitia Aya hii wanazuoni wamesema kwamba; kifo cha kwanza kilicho zungumziwa katka Aya hii, ni kile kifo cha hapa duniani, na kifo cha pili ni kile cha kaburini (kinachotokea katika ulimwenguwa Barzakh), na kwamba; ufufuo wa kwanza ni ule unaotokea kaburini, na ufufuo wa pili ni ule wa siku ya kiyama. [48]Kulingana na maelezo ya Allama Majlisi, ni kwamba; baadhi ya wafasiri kama vile Abdullah bin Omar Baidhawi na Fadhil bin Hassan Tabarsi katika Al-Jawami'i al-Jaami, wamefasiri vifo viwili vilivyo tajwa katika Aya hii wakisema kwamba; ni kifo cha kabla ya mja kuingia katika umbile la manii (mbegu), na kifo cha pili ni kile kufariki kwa mwanadamu, ama maisha mawili (aina mbili za ufufuo) ni yale maisha ya mbegu (manii) na maisha ya kukufuliwa siku ya Kiyama. [49] Pia Allama Majlisi ameyahusisha maoni ya mwanzo kwa kwa Fakhru al-Razi na kwa Fadhil bin Hassan Tabarsi katika kitabu chake Mujmau al-Bayan. [50]
Allama Majlisi kuhusiana na "maisha ya kidhalili" yaliotajwa katika Aya isemayo: (وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ ; Na yeyote ataye puuza ukumbusho wangu, bila shaka yeye atapata maisha ya yasio na utulivu (maisha ya mashaka), na tutamfufua Siku ya Qiyama hali akiwa kipofu). [51] Amesema kuwa; makusudio ya maisha hayo ni adhabu ya kaburi. [52]
Pia katika Mujmal al-Bayan (tafsiri ya Qur’ani iliyoandikwa katika karne ya 6 Hijiria) imenukuliwa ndani yake kutoka kwa baadhi ya wafasiri ya kwamba; moja ya adhabu mbili zilizo tajwa katika Aya isemayo: (سَنُعَذِّبُهُمْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ ; Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa…)[53] ni ile adhabu ya kaburini, na adabu ya pili ni ile ya siku ya Kiyama. [54] Kulingana na maoni ya Allama Tabatabai mfasiri wa Qur’ani kutoka upande wa madhehebu ya Shia (aliyofariki mwaka 1360 Shamsia), akizungumzia Aya isemayo: (لنَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ ; Moto hupelekewa kwao asubuhi na jioni, na siku saa itakaposimama (Kiama), itangaziwe kwamba uingizeni ukoo wa Firauni katika adhabu kali zaidi).[55] Amesema kwamba; Aya hii inaashiria kuwa Firauna na ukoo wake, hukabiliwa na adhabu ya moto mara mbili kwa siku katika ulimwengu wa kaburini mwao (Barzakh), na hatimae wataishia katika adhabu ya moto wa Jahannam ifikapo siku ya Kiama.[56]
Bibliografia (Seti ya Orodha ya Vitabu Inayo Husiana na Maudhui Hii)
Kuna vitabu kadhaa ambavyo ndani yake mna mada kuhusiana na adhabu ya kaburi, miongoni mwavyo ni: Manazilu al-Akhirah cha Sheikh Abbas Qomi, ‘Uruuji Ruuh cha Muhammad Shuja'i na Insan az Marge taa Barzakh cha Neematullah Salehi Hajji Aabady. Pia, vitabu kuna waandishi kadhaa walioandika vitabu vilivyo kusanya ndani yake masuala yanayo husiana na mada hii peke yake, ambavyo baadhi yake ni kama ifuatavyo:
- Utafiti wa Qur'ani na Hadithi Kuhusu Mateso ya Kaburi (تحقیقی قرآنی و روایی درباره عذاب قبر , kitabu kilicho andikwa na Mehdi Farbudi, kiilichochapishwa mwaka wa 1386 Shamsia, na pia kimechapishwa kwa mara nyengine chini kwa jina la Mateso ya Kaburi (عذابهای قبر : pia kimekuja kuchapiashwa tena chini ya jina la Utafiti wa Qur'ani na Hadithi Kuhusu Ulimwengu wa Kaburi (تحقیقی قرآنی و روایی درباره عالم قبر)[57]
- Ulimwengu wa Kaburi / Siri Kubwa (عالم قبر/ راز بزرگ), kilichoandikwa na Jaber Ridhwaniy. [58]
Maudhui Yanayo Husiana
Maelezo
- ↑ (ذَكَرْتُ ضَغْطَةَ الْقَبْرِ فَقَالَتْ وَا ضَعْفَاهْ فَضَمِنْتُ لَهَا أَنْ يَكْفِيَهَا اللهُ ذَلِكَ فَكَفَّنْتُهَا بِقَمِيصِي وَ اضْطَجَعْتُ فِي قَبْرِهَا لِذَلِكَ ; Mtume (s.a.w.w) amesema: ‘Nilizungumzia adhabu ya kaburi, naye (Fatima binti Asad) akasema: ‘Mimi ni dhaifu mno.’ Nikamuahidi kupata shufaa ya Mungu juu ya adhabu hiyo, nikamkafini kwa kanzu yangu, kasha nikalala kwenye kaburi lake ili kumwepushia adhabu ya kaburi).
Rejea
- ↑ Allameh Tabatabai, Al-Mizan, 1417 AH, juzuu ya 15, uk.68; Ardabili, insha za kifalsafa, 2005, gombo la 3, ukurasa wa 240-239.
- ↑ Qami, Manazel al-Akhara, Al-Nashar al-Islami Foundation, uk. 149-137.
- ↑ Sheikh Sadouq, Man La Yahdrah al-Faqih, 1367, juzuu ya 1, uk.279.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 261.
- ↑ Kwa mfano, angalia: Kilini, Al-Kafi, 1407 AH, Juz. 2, uk. Ibn Tawoos, Iqbal al-Amal, 1409 AH, Juz. 1, uk. 338, 439.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 261.
- ↑ Klini, Usul Kafi, juzuu ya 1, uk.454.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 79, uk. 27.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 202-282.
- ↑ Sheikh Sadouq, Al-Al-Sharia, 1385, juzuu ya 1, uk.310.
- ↑ Qami, Manazel Al-Akhreh, Est. Al-Nashar al-Islami, uk. 138.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 261.
- ↑ Mishkini, Tahrir al-Mo'az al-Salmiyyah, 2002, uk. 232-233.
- ↑ Sheikh Sadouq, Sheria za Sheria, 1385, juzuu ya 1, uk.309.
- ↑ Sheikh Sadouq, Al-Amali, 1376, uk.50.
- ↑ Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 245.
- ↑ Angalia: Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1407 AH, juzuu ya 6, uk.262.
- ↑ Sheikh Sadouq, Man La Yahdrah al-Faqih, Juz. 1, 1413 AH, uk. 58.
- ↑ Sheikh Sadouq, Man La Yahdrah al-Faqih, Juz. 1, 1413 AH, uk. 58, Sababu za Sheria, 1385, juzuu ya 1, uk. 309.
- ↑ Naraghi, Jame Al-Saadat, 2003, juzuu ya 2, uk.263.
- ↑ Allameh Majlesi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 7, uk. 248.
- ↑ Kwa mfano, ona: Seyyed Ibn Tavus, Iqbal al-Amal, 1409 AH, Juzuu ya 2, uk. 664, 629, 656, 665, 683, 723.
- ↑ Dilmi, Irshad al-Qulob, 1412 AH, juzuu ya 2, uk.439.
- ↑ Qami, Safina Al-Bahar, 1378, juzuu ya 2, uk.397.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 89, uk.336.
- ↑ Kilini, Al-Kafi, 1407 AH, juzuu ya 3, uk.103.
- ↑ Kilini, Al-Kafi, 1407 AH, juzuu ya 3, uk.200.
- ↑ Ibn Qolwieh, Kamel al-Ziyarat, 1356, uk. 142-143.
- ↑ Kilini, Al-Kafi, 1407 AH, juzuu ya 3, uk.321.
- ↑ Qami, Safina Al-Bahar, 1378, juzuu ya 2, uk.397.
- ↑ Ibn Tawoos, Iqbal al-Amal, 1409 AH, juzuu ya 2, uk.651.
- ↑ Sheikh Sadouq, Man La Yahdrah al-Faqih, 1367, juzuu ya 1, uk.83.
- ↑ Meshkini, Mu'aaz al-Salmiyyah, 2002, uk 75.
- ↑ Meshkini, Mu'aaz al-Salmiyyah, 2002, uk 75.
- ↑ Kilini, Al-Kafi, 1407 AH, juzuu ya 6, uk.3-4.
- ↑ Imam Khomeini, Ufafanuzi wa Hadithi Arobaini, 1380, uk. 124.
- ↑ Bukhari, Sahih Al-Bukhari, 1422 A.H., Juz.2, uk.80, Sura ya “Nachukia kifo cha marehemu”, 1291-1292 AH.
- ↑ Navi, al-Manhaj Sahih Sahih Muslim bin al-Hajjaj, 1392 AH, juz.6, uk.228.
- ↑ Navi, al-Manhaj Sahih Sahih Muslim bin al-Hajjaj, 1392 AH, juz.6, uk.228.
- ↑ Surah An'am, aya ya 164.
- ↑ Navi, al-Manhaj Sahih Sahih Muslim bin al-Hajjaj, 1392, juz.6, uk.228.
- ↑ Malairi, "Nadharia za Mwili wa Barzakhi - Uhakiki na Uhakiki", uk. 109-115.
- ↑ Malairi, "Nadharia za Mwili wa Barzakhi - Uhakiki na Uhakiki", uk. 113-115.
- ↑ Lahiji, Gohar Murad, 1383, uk. 649-650.
- ↑ Ash'ari, Al-Islamiyin insha, 1400 AH, uk. 430.
- ↑ Ibn Abi al-Hadid, Ufafanuzi wa Nahj al-Balaghah, 1404 AH, juz.6, uk.273.
- ↑ Surah Ghafar, aya ya 11.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 211.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk.214.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 214.
- ↑ Surah Taha, aya ya 124.
- ↑ Allameh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juzuu ya 6, uk. 215.
- ↑ Surah Towba, aya ya 101.
- ↑ Tabarsi, Majma al-Bayan, 1372, juzuu ya 5, uk.100.
- ↑ Surah Ghafar, aya ya 46.
- ↑ Tabatabaei, Al-Mizan, 1417 AH, Juz. 17, uk.335.
- ↑ «عالم قبر»، سایت بازار کتاب.
- ↑ «عالم قبر، راز بزرگ»، سایت کتابخانه ملی.
Vyanzo
- Quran.
- Ardabili, Seyyed Abdul Ghani, Visomo vya Falsafa, Tehran, Taasisi ya Uhariri na Uchapishaji ya Imam Khomeini, 1385.
- Ibn Abi al-Hadid, Abdul Hamid bin Hibatullah, Ufafanuzi wa Nahj al-Balaghah, kilichohaririwa na Muhammad Abul Fazl, Qom, Shule ya Ayatollah Murashi Najafi, 1404 AH.
- Ibn Tawoos, Ali Ibn Musa, Iqbal al-Amal, Tehran, Darlaktub al-Islamiya, 1409 AH.
- Ibn Qolwieh, Jafar bin Muhammad, Kamel al-Ziyarat, iliyosahihishwa na Abdul Hossein Amini, Najaf, Dar al-Mortazawieh, 1356.
- Ash'ari, Abul Hasan, Insha za Waislamu na Mifarakano ya Waislamu, Ujerumani-Wiesbaden, Franz Steiner, 1400 AD.
- Imam Khomeini, Seyyed Ruhollah, Ufafanuzi wa Hadithi Arobaini, Qom, Taasisi ya Uhariri na Uchapishaji ya Imam Khomeini, 1380.
- Bukhari, Muhammad bin Ismail, Sahih al-Bukhari, utafiti wa Muhammad Zuhair bin Nasser al-Nasser, Dar al-Tooq, 1422 AH.
- Dilmi, Hasan bin Muhammad, Irshad al-Qulub al-Sawab, Qom, Al-Sharif al-Razi, Qom, 1412 AH.
- Sheikh Sadouq, Mohammad Bin Ali, Al-Amali, Tehran, Kitabchi, 1376.
- Sheikh Sadouq, Muhammad Bin Ali, Man Lay Hazara Al-Faqih, Tehran, Sadouq Publishing House, 1367.
- Sheikh Sadouq, Muhammad bin Ali, Al-Ala al-Shar'ee, Qom, Duka la Vitabu la Davari, 1385/1966 AD.
- Tabarsi, Hasan bin Fazl, Makarem al-Akhlaq, Qom, Al-Sharif al-Razi, 1412 AH/1370 AH.
- Tabarsi, Fazl bin Hassan, Majma al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an, Utangulizi wa Mohammad Javad Balaghi, Tehran, Nasser Khosro Publications, 1372.
- Tusi, Muhammad bin Hasan, al-Mali, kilichohaririwa na: Taasisi ya Al-Baath, Qom, Darul Al-Taqwa, Qom, 1414 AH.
- Qomi, Sheikh Abbas, Safina Al-Bahar na Madina Al-Hakim na Al-Athar, Qom, Ofisi ya Machapisho ya Kiislamu, 1378.
- Qami, Sheikh Abbas, Manazel al-Akhlarah, Manazel al-Akhlarah wal-Maltalib al-Fakhra, utafiti na Seyyed Yassin Mousavi, Al-Nashar al-Islami Foundation.
- "Alam Ghabr, Siri Kubwa", tovuti ya Maktaba ya Kitaifa, tarehe ya kutembelea: Oktoba 10, 2019.
- "Alam Qabr", tovuti ya soko la vitabu, tarehe ya kutembelea: Oktoba 10, 2019.
- Allameh Tabatabai, Seyyed Mohammad Hossein, Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an, Qom, Al-Nashar al-Islami School, 1417 AH.
- Kilini, Muhammad bin Yaqub, Kafi, Tehran, Dar al-Katb al-Islamiyya, 1407 AH.
- Lahiji, Abdul Razzaq, Gohar Murad, Utangulizi wa Zainul Abdin Ghorbani, Tehran, Sayeh 2003.
- Majlesi, Muhammad Baqir bin Muhammad Taqi, Bihar al-Anwar, iliyohaririwa na kundi la wanazuoni, Beirut, Darahiya al-Tarath al-Arabi, 1403 AH.
- Mishkini Ardabili, Ali, Tahrir al-Mo'az al-Salmiyyah, Qom, Al-Hadi Publications, 2013.
- ملایری، موسی، «نظریههای بدن برزخی-بررسی و نقد»، پژوهش دینی، شماره۲۱، زمستان ۱۳۸۹ش.
- Naraghi, Mohammad Mahdi, Jame al-Saadat, Qom, Taasisi ya Wanahabari ya Irani, 2013.
- Nuri, Mirzahosein, Mostadrak al-Wasail, Qom, Taasisi ya Al-Al-Bait ya Lahia al-Tarath, 1407 AH.
- Nawi, Yahya bin Sharaf, al-Manhaj fi Sharh Sahih Muslim bin al-Hajjaj, Beirut, Darhiya al-Nirath al-Arabi, 1392 AH.