Nenda kwa yaliyomo

Mapambo ya wanawake

Kutoka wikishia

Mapambo au Vipodozi vya Wanawake (Kiarabu: زينة المرأة) ni urembo wa uso, mwili, nywele au kucha za wanawake, ambayo hukumu zake zimetolewa katika sheria. Urembo wa wanawake unaruhusiwa; lakini ni wajibu kwa mume ikiwa ataomba na ni mustahabu kama mume hajaomba hilo. Haijuzu kwa wanawake kujipodoa wakiwa katika Ihramu na wakati wa eda ya kifo cha mume.

Mafakihi wa Shia wanasema kuwa, ni wajibu kwa wanawake kufunika mapambo na urembo wao mbele ya wasio maharimu wao. Inaruhusiwa kulipwa kwa ajili ya kuwaremba na kuwapamba wanawake, ikiwa ni kwa madhumuni ya halali. Si lazima kufunika mapambamo wakati wa kusali; bali, kwa mujibu wa fat’wa ya baadhi ya mafaqihi, ni mustahabu wanawake kujipamba kwa ajili ya Sala.

Utambuzi wa Maana na Nafasi

Kujipamba maana yake ni kujiremba sura kwa kutumia vipodozi au kutoa nywele za ziada za uso au ni kusuka na kusokota nywele au ni kuzipamba kucha. [1]

Kujipamba kunaelezwa katika vitabu vya fiq’hi kwa jina la zinat (pambo); [2] hata hivyo maana hiyo ni jumla zaidi nainajumuisha pia urembo na uzuri mwingine. [3] Katika kamusi za lugha, zinat (pambo) ina maana ya kila ambacho kinatumika kwa ajili ya kujipamba. [4]

Katika hadithi, imeamrishwa na kukokotezwa juu ya kujipamba wanawake [5] Kwa mfano, kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Imam Baqir (a.s), haifai kwa mwanamke kuacha mikono yake bila hina. [6] Kwa mujibu wa riwaya nyingine, moja ya sifa maalumu za mwanamke mwema ni kujipodoa kwa ajili ya mume na kufunika mapambo yake kwa wasio maharimu wake. [7]

Katika vitabu vya fiqhi, mapambo ya wanawake yametajwa katika milango mbalimbali kama vile ya ndoa, [8] Hija, [9] Sala [10] na machumo ya haramu (Tadlis Mashta) – kujipamba mwanamke kwa namna ambayo sura yake ya asili haifahamiki. [11]

Mifano

Katika vitabu vya fiq’h vya Kishia, mambo kama kupaka wanja, kupaka rangi nyusi, [12] kusuka na kuunganisha nywele, [13] kuchora tatoo, [14] rangi ya nguo, [15] kutumia manukato, [16] na kila kitu ambacho kinaifanya sura na mueneo kuwa mzuri, [17] kinatambuliwa kuwa ni pambo na urembo. Kuna hitilafu baina ya wanazuoni wa Fiq’h kuhusiana na kuwa pambo baadhi ya mambo kama kusuka na kuunganisha nywele, [18] na rangi ya nguo. [19]

Kwa mujibu wa Sahib al-Jawahar, mwanafakihi wa Kishia katika karne ya 13 Hijiria anasema kuwa, kitu kuwa ni pambo inategemea desturi na ada; kwa mfano, yeye haitambui rangi ya nguo kama pambo katika zama zake. [20] Sahib Ur’wah (aliaga dunia 1337 Hijiria) faqihi wa Kishia katika karne ya 13 na 14 Hijiria naye amelitambua pambo kwa mujibu wa mtu anayejipamba, zama na sehemu ambayo mtu anaishi kwamba, ni lenye kutofautiana. [21]

Pia, kwa mujibu wa fat’wa ya Sayyid Ali Khamenei, mmoja wa Marajii Taqlidi ni kwamba, kuwa urembo vitu kama vile kuchora tatoo katika nyusi kunategemea ada na mazoea. [22]

Hukumu ya Kifiq’h

Kwa mujibu wa Aya ya 32 ya Surat al-A’raf, mafaqihi wa Shia wanaona kuwa aina yoyote ya mapambo na urembo kama urembo inaruhusiwa; [23] hata hivyo kujipamba na kujipodoa kwa wanawake ni wajibu, mustahab au haramu kwa mujibu wa masharti.

Kujipamba Ambako ni Wajibu

Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi wa Kishia, ni wajibu kwa mwanamke kujipamba kwa ajili ya mumewe, ikiwa mume ataomba hilo. [24] Sababu na hoja ya hilo imetambuliwa kuwa ni wajibu wa kumtii mume na kutekeleza haki yake. [25]

Kujipamba Ambako ni Mustahabu

Kwa mujibu wa mafaqihi, ni kuwa, endapo mke atajipamba bila ya kutakiwa na mumewe kufanya hivyo, basi jambo hilo litakuwa ni mustahabu. [26]

Kujipamba mwanamke pia katika kipindi cha eda ya talaka rejea nako kumetambuliwa kuwa ni mustahabu [27] na hekima yake, kulingana na simulizi, ni kumvutia mume na kumfanya arejee katika maisha. [28]

Kujipamba Ambako ni Haramu

Kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi wa Kishia, haijuzu kwa wanawake kujipodoa na kujipamba wakiwa katika Ihramu [29] na wakati wa eda ya kifo cha mume. [30]

Mafakihi kama Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka 413 Hijiria) na Sahib al-Jawahar (aliyefariki dunia mwaka 1266 Hijiria) wameona kuwa ni haramu kujipamba kwa wanawake kwa ajili ya kuwavutia wasio maharimu. [31] Kujipamba kwa ajili ya kumdanganya mchumba pia kwa mujibu wa fat’wa mashuhuri ya mafakihi ni haramu. [32]

Mapambo Hafifu

Kwa mujibu wa Fatwa ya Nassir Makarim Shirazi, Marjaa Taqlidi, inajuzu kujipamba mviringo wa uso, mikono mpaka katika kifundo cha mkono, ikiwa ni hafifu sana na haisababishi ufisadi. [33] Kwa mujibu wa Sayyid Ali Khamenei, Marjaa Taqlidi ni kwamba, ni wajibu kufunika urembo na mapambano ambayo ni hafifu mbele ya mtu asiye maharibu wa mwanamke, kama kwa mujibu ada na mazoea hilo litahesabiwa kuwa ni mapambo na urembo. [34] Kwa mujibu wa Jafar Sobhani, Marjaa wa Taqlid, pia ni wajibu kufunika kile kinachochukuliwa kuwa ni mapambo. [35] Muhammad Sadiq Rouhani, haijuzu kuweka mapambo na urembo wa kawaida kama utamchochea na kumsisimua asiyekuwa maharimu. [36]

Sayyid Ali Sistani, [37] Sayyid Abul-Qasem Khui na Mirza Jawad Tabrizi [38] miongoni mwa Marajii Taqlid wameona kuwa ni wajibu kufunika mapambo na urembo mbele ya macho ya asiye maharimu, hata kama ni kidogo.

Hukumu Zenye Kuhusiana

Baadhi ya hukumu zinazohusiana na mapambo ya wanawake ni:

Kipato cha Kazi ya Kupamba

Inajuzu kuchukua ujira kwa ajili ya kupamba kama hilo litakuwa ni jambo la halali (kama kumpamba mke kwa ajili ya mumewe). [39] Kwa mujibu wa fat’wa ya Sayyid Ali Khamenei, mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia ni kwamba, haijuzu kumpamba mwanamke kwa lengo la kumsaidia kufanya haramu (kama vile kumuonyesha kwa asiyekuwa maharimu wake). Kwa mujibu wa fat’wa yake, haijuzu kupamba nywele na kujifananisha na makundi potofu na ni haramu kuchukua ujira kwa ajili ya kazi kama hiyo.

Kutia Udhu na Mapambo

Kwa mujibu wa fat'wa ya Marajii Taqlidi, vipodozi vilivyo na mnato ni kizuizi cha udhu na pia ni lazima viondolewe kabla ya kutia udhu. [41] Vipodozi ambavyo vina rangi tu na havina uchafu/mnato [42] au vimewekwa chini ya ngozi havizuii udhu na udhu huwa sahihi kwa kuwepo hivyo. [43]

Wakati wa kusali, si lazima kufunika vipodozi vya uso,[44] mapambo na nywele ambazo zimeunganishwa kwenye nywele za mwanamke kutoka nywele, (kama asiyekuwa maharimu haoni); [45] Baadhi ya wafasiri wametumia Aya ya 31. ya Surat Al-A'raf kwamba ni mustahabu kwa wanaume na wanawake kujipamba wakati wa kuswali. [47]

Kuonyesha Mapambo kwa Wengine

Kadhalika angalia: Majishauwo

Katika Aya isemayo: (...وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا ; wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa...) (Surat Nur-31) ambayo ni mashuhuri kwa jina la Aya ya kuonyesha uzuri na urembo, [48] wanawake wamekatazwa kuonyesha uzuri na mapambo yao kwa watu wasio maharimu wao. Kwa mujibu wa fa’twa ya mafakihi wa Kishia na wakitumia Aya hii kama hoja ni kwamba, ni wajibu kufunika mapambo mbele ya mtu asiye maharimu. [49] Katika vitabu vya fiq’h hatua ya mwanamke kuonyesha mapambo na uzuri wake kwa mwanaume asiye maharimu wake imetajwa kuwa ni majishauwo.[50]

Kadhalika katika hadithi mbalimbali, mwanamke kuonyesha mapambo yake kwa mwanaume asiye maharimu ni jambo ambalo limekemewa. [51] Katika hadithi iliyokuja katika kitabu cha Tahdhib al-Ahkam, imeelezwa kuwa moja ya masharti ya kukubaliwa ushahidi wa mwanamke ni mwanamke huyo kutoonyesha mapambo yake ya kike na kujionyesha (majishauwo) katika kikao cha wanaume. [52]

Masuala Yanayo Fungamana