Nenda kwa yaliyomo

Wasio Maharimu

Kutoka wikishia

Itumikapo ibara ya; Asiyekuwa Maharimu ambayo ni kinyume cha neno Maharimu, humaanisha na kuashiria yule mtu anayelazimika kuuhifadhi mwili wake kulingana na sheria za hijabu mbele yako, ambaye pia ni halali kuoana naye.

Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi ni kwamba; haijuzu kuutazama mwili wa mwanamke asiyekuwa Maharimu wako isipokuwa uso na viganja vya mikono hadi vifundoni mwa viganja hivyo. Ni haramu kuutazama uso mpamoja na mikono ya asiyekuwa maharimu wako. Pia ni haramu kusikiliza sauti ya mwanamke asiyekewa maharimu wako, iwapo kufanya hivyo kutapelekea kutenda dhambi (kutamtamanisha). Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi, ni wajibu kwa mwanamke kusitiri mwili wake mzima mbele ya watu wasiokuwa maharimu wake. Bila shaka, wanazuoni wamekhitalifiana katika ulazima wa mwanamke kufunika mviringo wa uso pamoja na mikono yake, kuanzia vidole vya mikono hadi kwenye vifundo vya viganja vyake. Mafaqihi hawaoni kuwa suala hilo ni wajibu kwa mwanamke. Ila haijuzu kwa mwanamke kuangalia mwili wa mwanaume ambaye si maharimu wake.

Ni haramu kugusa mwili wa asiyekuwa maharimu wako, na ni haramu pia kwa watu wawili wasiokuwa na uhusiano wa kimaharimu kukaa faragha peke yao, kwa hofu ya wa wili hao kuingia makosani (kutenda dhambi). Sheria za Kiislamu, zinaruhusu bila ya pingamizi kufunga ndoa wanake na wanaume ambao si maharimu zao. Ila ni lazima ieleweke kuwa; kuna hali maalumu ambazo husbabisha uharamu wa kuowana na baadhi ya wasiokuwa maharimu zetu.


Welewa wa dhana na nafasi yake

Mtu ambaye si maharimu wako anaitwa; "غير محارم" yaani asiye maharimu. Neno "محارم" yaani maharimu humaanisha uwepo wa uhusiano maalumu wa kijamaa baina ya watu wao kwa wao, unaotokana na nasaba (kiukoo), ndoa au kupiti njia ya kunyonya. [1] Istilahi hii inatumika katika milango ya kifiqhi kadhaa; kama vile ndoa, talaka na mipaka ya kisheria (hukumu na kanuni za kisheria). [2]

Aya ya 30 na 31 za Surat Noor, zimeamrishwa kuinamisha macho chini na kutowakodolea macho wasioyekuwa Maharimu zetu. Kuna Hadithi kadhaa zlilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu (a.s) zinazokataza wanawake na mwanamume kufanya mahusiano na wasiokuwa Maharimu. [4] Kwa mujibu wa kauli ya Imam Baqir (a.s); kuzungumza na mtu usiyefungamana naye kiumaharimu, ni kuingia mitegoni mwa Shetani. [5] Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), imeelezwa kuwa; kumkodolea macho asiyekuwa maharimu wako, ni miongoni mwa mishale ya Shetani. [6] Pia kulingana na Hadithi kutoka kwa Imamu Ali (a.s); kusungumza na wanawake wasio maharimu wako, hupelekea kushuka balaa na kukengeuka kwa moyo kutoka katika njia ilio sawa. [7]

Faidh Kashaniy katika kitabu cha Mahajjatu al-Baidhaa [8] na Mulla Mohammad Mahdi Nairaqyi katika kitabu cha Jaami'u al-Saadaat, [9] wamelihisabu suala la mtu kumkodolea macho asiye maharimu wake, kuwa ni kuikufuru neema ya macho tuliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Murtadha Mutahhari, katika kitabu chake Mas-aleye Hijab "مسئله حجاب", ameielezea falsafa ya kutilia mkazo uvaaji wa hijabu na mavazi yanayostahiki kwa wanawake katika Uislamu, kuwa ni kwa ajili ya kudumisha afya ya kimwili na kiali ya wanajamii, amani na utulivu wa jamii, kuimarisha familia, kuinua heshima ya wanawake na kuzuia uchafuzi wa kuwafisidi wanawake. [10]

Sheria za Mahusiano na Wasiokuwa Maharimu

Katika fiqhi ya Kiislamu, kuna sheria maalumu kuhusiana na wasiokuwa maharimu, nazo ni kwamba:


Haramu kumwangalia asiyekuwa maharimu

  • Ni haramu kwa mwanamume kuutizama mwili wa mwanamke asiyekuwa maharimu wake isipokuwa uso na mikono kuanzia kwenye vidole hadi kwenye vifundoni mwa viganja. [11] Ila itakuwa ni haramu kuutazama uso na mikono hiyo hadi vifundoni mwa viganja vyake, iwapo atakuwa na nia kujiburudisha, au iwapo atakhofia kwamba; iwapo atamtizama mwanamke huyo itampelekea kuingia makosani. [12]
  • Ni haramu kwa mwanamke kuutizama mwili wa mwanamume asiyekuwa maharimu wake, isipokuwa zile sehemu tu za mwili wake ambazo aghalabu yake huwa hazistiriwi, kama vile kichwa, mikono na miguu hadi katika miundi. Ila ni lazima ieleweke ya kwamba si halali kwa mwanamke huyo kuuangalia mwili wa mwanammme asiyekuwa maharimu wake, hata katika sehemu zilizotajwa ambazo kikawaida huwa si haramu kuziangalia, iwapo mwangalio huo au mtizamo huo utakuwa una nia ya kujiburudisha. Na pia ni haramu kwake kuuangali mwili huo iwapo atahofia kuwa mtizamo huo utapelekea yeye kuingia makosani. [13]
  • Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi wa Kishia, inajuzu kuutazama uso wa mwanamke ikiwa kuna nia na malengo ya kunga ndoa naye. [14] Baadhi ya mafaqihi pia wanaruhusu kuangalia baadhi ya sehemu za mwili wa mwanamke huyo kama vile; nywele, shingo na sehemu ya kifua chake. Ila kufanya hivyo iwe ni kwa nia ya ndoa, na si kwa nia ya starehe. [15]
  • Hakuna junaa, kuangalia filamu au picha za wanawake ambao hawahishimu miili yao, au kwa lugha nyingine, hawavai hijabu. Ila kuangalia huko kusiwe na nia ya kujiburudisha, na filamu au picha hizo ziwe ni za watu asio wajua. Lakini ikiwa anawajua, basi huku zake itakuwa ni sawa na hukumu za kuwatazama wenye kimwili. [16]
  • Inaruhusiwa kwa daktari kuangalia mwili usio wa maharimu wake ikiwa atalazimika kufanya hivyo kwa ajili matibabu. [17]

Hakuna ubaya wala junaa kuangalia picha za wanawake wasio Waislamu bila hijabu, ikiwa hakutakuwa na nia kujifurahisha na kujiburudisha, au pia iwapo jambo hilo halitapelekea ufisadi na kusababisha uharibifu. [18]


Wajibu wa kusitiri mwili mbele ya asiye Maharimu

Ni wajibu kwa wanawake kusitiri miili yao mbele ya wasiokuwa maharimu zao. [19] Bila shaka, kuna khitilafu kuhusiana na wajibu wa kufunika nyuso na mikono yao kuanzia kwenye ncha za vidole hadi kwenye viganja vyao. Kulingana na nadharia za baadhi ya mafaqihi kama vile; Sheikh Tusi, [21] Sahibu Hadaa-iq, [22] Sheikh Ansari, [23] Sayyid Muhammad Kadhim Yazdiy, [24] Sayyid Muhsin Hakim [25] Imam Khomeini [26] na Sayyied Ali Khamenei, [27] si wajibu kwa wanawake kufunika uso na mikono kutoka kwenye ncha za vidole hadi kwenye vifundo vya mikono. Kwa upande mwengine, kuna mafaqihi kadhaa waliowajibisha na kuona kuwa; ni haramu kwa wanawake kuacha wazi nyoso na mikono yao kuanzia ncha za vidole hadi vifundoni mwa viganja vyao. Baadhi ya wanazuoni wenye mtazamo huuo ni; vile Allama Hilliy ambaye ameashiria suala hilo katika kitabu chake Tadhkira al-Fiqha, [28] Fadhil Miqdad [29] na Sayyied Abdul Ali Sabzewariy. [30] Wote hao wamewajibisha kufunika uso na mikono. Mafaqihi wote wamewafikiana ya kwamba; ikiwa kutakhofiwa mwanamke kutumbukia katika mambo ya haramu, au ikiwa mwanamke atakuwa na nia ya kumtumbukiza mwanamme katika mambo haramu, basi katika hali kama hiyo, itakuwa ni wajibu kwake kufunika uso na mikono yake. [31]


Uharamu wa kugusana na asiye Maharimu

Kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi; hairuhusiwi kugusana na mwili wa asiye maharimu wako, ingawa inajuzu katika hali za dharura kama vile katika hali ya matibabu na kuokoa maisha ya mwanadamu. [32] Pia, hakuna tatizo kugusa mwili wa asiyekuwa maharimu kwa njia ya mavazi au kupitia kizuizi, kama vile kitambaa au soksi, ikiwa kufanya hivyo hakutokuwa na nia ya matamanio na kujistarehesha. [33] Baadhi ya mafaqihi wamejuzisha kupeana mikono na asiyekuwa maharimu, iwapo patatumika kizuizi cha kitambaa au kwa glovu, na ikawa hakukuwepo nia ya mbaya, na endapo pande mbili za wapeanao mikono hapo hawatokamuana mikono katika tendo hilo la kupeana mikono. [34]


Hukumu ya kusikiliza sauti ya mwanamke asiye Maharimu

  • Kwa mujibu wa maoni ya mafaqihi; inajuzu kusikiliza sauti ya mwanamke asiyekuwa maharimu, ikiwa kufanya hivyo hakutakuwa na nia ya kujistarehesha, na iwapo haitokhofiwa kupelekea msikilizaji huyo kutumbukia katika haramu. Kwa lugha nyengine ni kwamba; ni haramu kusikiliza sauti ya mwanamke aseye maharimu kwa nia ya kujistarehesha, au iwapo itahofiwa jambo hilo kumpelekea mtu kuingia katika mambo yalioharamishwa. [35]
  • Kwa maoni ya mafaqihi kama vile Shahidu Al-awwal, ni haram na husababisha sala ya mwanamke kubatilika, iwapo yeye asali kwa sauti inayosikika katika sehemu ambayo atakuwa anajua ya kwamba, katika sehemu hiyo kuna watu wasio maharimu zake, ambao iwapo atasali kwa sauti, basi wao wataweza kusikia sauti yake. [36] Ingawaje Sahib Jawahar amekubaliana na uharamu wa jambo hilo, ila yeye hakubaliana na usemi wa kwamba sala yake pia itabatilika. Hivyo basi, kwa mtazamo wake yeye, jambo hilo ni haramu ila halibatilishi sala. [37]


Hukumu ya kukaa faragha na asiye Maharimu

Kwa mujibu wa fat'wa za baadhi ya mafaqihi; ni haram kufaraghika (kujitenga mbali na watu) na asiyekuwa maharimu [38] Baadhi ya mafaqihi wameharamisha mtu kufaraghika na asiyekuwa maharimu wake na kukaa naye mbali na watu, ikiwa tu jambo hilo litashakiwa kuwapelekea watu hao kuingia makosani na kutenda dhambi. [39] Kwa mujibu wa fat'wa za Ayatullahi Khui (aliyefariki mwaka 1371 Shamsia), ni kwamba; Kule mtu kufaraghika na asiyekuwa maharimu wake, ni moja ya utangulizi wa kuignia matatizoni na kutenda haramu, na kwa kuwa jambo hilo linahisabiwa kuwa ni msingi wa kutenda haru, basi nalo pia litakuwa ni haramu. [40] Kwa mujibu wa maoni na fat'wa za Muhammad Hassan Najafi, mwandishi wa kitabu Jawahiru al-Kalam; ni makuruhu mtu kukaa peke na kufaraghika na asiye maharimu wake. [41]


Kuzungumza na asiye Maharimu

  • Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi; Yajuzu kuzungumza na asiye maharimu ikiwa jambo hilo halina nia ya kujistarehesha au hofu ya kamba jambo huenda likapelekea na kusababisho mambo haramu. [42]
  • Kulingana na maoni ya Mirza Jawad Tabrizi; Ni bora kuachana kabisa na kuepuka kuzungumza na mwanamke, haka kama hakutakuwa na nia ya kujiburudisha au kukhofia kutumbukia makosani. [43]
  • Ni haramu kufanya mawasiliano na asiye maharimu kupitia njia ya SMS, gumzo kwa njia ya kuchati pamoja na barua pepe, iwapo kufanya hivyo kutapelekea kupatikana kwa ufisadi na hatimaye kuingia makosani. [44]


Ruhusa ya kuoana na asiye Maharimu

  • Katika sheria za Kiislamu, inaruhusiwa kufunga ndoa na asiyekuwa maharimu tu, na wala haijuzu mtu kuowana na maharimu wake. [45]
  • Ingawa dada wa mkwe si maharimu wako, ila hairuhusiwi kuowana naye maadamu uko katika ndoa ya nduguye, ila kama akifariki mkeo au ukaachana naye, hapo basi itajuzu kumoa ndugu yake wa kike au dada yake. [46]
  • Ndoa na baadhi ya wasio maharimu inakuwa haramu milele kwa mujibu wa masharti yafuatayo:
  1. Ndoa ya mwanamme juu ya mwanamke ambaye amemtaliki mara tisa. [47]
  2. Ndoa ya mwanamume juu ya mwanamke ambaye ameezini na mama wa mke huyo au binti yake, kabla ya kufunga ndoa na mwanamke huyo. [48]
  3. Ndoa ya mwanamume juu ya mwanamke mwenye mume na mwanamke aliyezini naye huku akiwa katika eda ya talaka ya mumewe wa mwamzo ambaye ameachana naye. [49]
  4. Ndoa ya mwanamume juu mwanamke ambaye mume amewahi kumlawiti mwana wa mke huyo, kaka au baba wa mke huyo kabla ya kuowana naye. [50]

Masuala yanayofungamana