Nenda kwa yaliyomo

Manaibu Wanne

Kutoka wikishia

Manaibu Wanne au Wawakilishi Wanne au pia Mawakala au Makamu Wanne (Kiarabu: النواب الأربعة): Ibara hii imekuwa ni istilahi maalumu mbele ya Mashia inayoashiria Manaibu Wanne makhususi wa Imamu Mahdi (a.t.f.s). Ibara hii inaashiri Manaibu Wanne waliokuwa wakimwalikisha Imamu Mahdi (a.t.f.s) katika kipindi cha Ghaiba Ndogo ambapo Imamu Mahdi (a.s) alighibu kwa muda wa miaka 70. Katika ughaibu huo mdogo wawakilishi hawa walikuwa ndio kiungo kati ya Mashia na Imamu wao (Mahdi (a.s)), nao walikuwa ni: Othman bin Said, Muhammad bin Othman, Hussein bin Ruuh na Ali bin Muhammad Samuri. Nuwwabu al-Arba'a walikuwa ni miongoni mwa masahaba wenye uzoefu wa muda mrefu na wenye kutegemewa na Maimamu, ambao walitambulika mmoja baada ya mwingine kupitia utambulisho utokao kwa Imamu Zamani (a.t.f.s) (Imamu Mahdi) pamoja na kuarifishwa kupitia wakili (makamu) aliye tangulia kabla yake. Kwa muda wa miaka sabini, watu hawa wanne walishika nafasi ya unaibu wa Imamu, na waliweza kufikisha ujumbe wa Imamu hata katika miji mbali kabisa kupitia mawakala wao katika miji hiyo. Mtandao wa mawakala uliweza kuchukuwa amri za Imamu Mahdi (a.t.f.s) na kuwafikishia Mashia, na kwa upande wa pili pia waliweza kumfikisha Imamu Mahdi (a.t.f.s) dukuduku au masuala mbalimbali yaliokuwa Mashia wake, yakiwemo maswali mbalimbali ya kidini. Moja ya majukumu mengine ya manaibu hao makhususi ilikuwa ni kuondoa shaka juu ya uwepo wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) pamoja na kuficha siri kuhusiana na makazi yake.

Wakala Waalum

Makala Asili: Wakala Maalum

Neno wakala maalum linamaanisha unaibu au wakala makhususi kupitia uteuzi wa Imamu (a.t.f.s) kwa jali ya kuwasiliana na watu katika hali ambapo mawasiliano ya moja kwa moja hayawezekani. Katika hali hii, Imamu huwateua watu fulani kuwa ni makamu wake, ambapo wakala wa kwanza wao lazima atambulishwe kwa watu kupitia Imamu mwenyewe, kisha makamo huyo wa kwanza ndiye anayemtambulisha kwa watu makamu (wakala) atakaye fuatia baada yake. [1]

Manaibu na Kipindi cha Unaibu Wao

Shughuli za Manaibu maalum wa Imamu Zaman (a.t.f.s)(Imamu Mahdi) zilishika hatamu kuanzia mwaka 260 hadi 329 Hijiria, (karibu miaka 70), nacho ni kipindi cha kutokuwepo kwa Imamu Mahdi mbele ya macho ya jamii, kipindi hichi kinajulikana kwa jina la Ughaibu Mdogo. Katika miaka hiyo sabini, watu wanne miongoni mwa Mashia, ambao baadhi yao walikuwa ni masahaba wa Imam wa 10 na Imamu wa 11 na ni miongoni mwa watu mashuhuri, walikamata nafasi ya unaibu wa kumwakilisha Imamu Mahdi (a.t.f.s), nao wakwa ni ni kiungo kati ya Imamu na Mashia mashia wake. Pia katika miaka hiyo, kulikuwa na mawakala maalumu katika miji na ardhi za Kiislamu ambao walio wawakilisha manaibu hao wanne.[2]

  • Naibu wa kwanza wa Imam Zaman (a.t.f.s) alikuwa ni Othman bin Said Amri (aliyefariki kabla ya mwaka 267 Hijiria). Imeelezwa katika Hadithi kwamba; Imam Askari (a.s) alimuonyesha mwanawe (Imamu Mahdi (a.t.f.s)) kwa masahaba zake arobaini, na akawaambia wamtii Othman bin Said katika kipindi chote ambacho Imamu wa kumi na mbili (Imamu Mahdi (a.t.f.s)) atakuwa hayupo machoni mwa jamii (atakuwa katika Ughaibu Mdogo). [3] Hata Imam Zamani alipo kutana na watu wa mji wa Qom aliashiria suala la unaibu wa Othman bin Said na kuwataka wao wamrejee yeye katika masuala mbali mbali [4] Othman bin Said alikuwa ni naibu makhususi wa Imam Zaman hadi mwisho wa maisha yake, kipindi kilicho hukua takribani muda wa kama miaka 6.
  • Muhammad bin Othman bin Said Amri (aliyefariki 305 Hijiria), ambaye ni mtoto wa makamu (naibu) wa kwanza, ni makamu wa pili maalum wa Imamu Zamani (a.t.f.s). Alipofariki naibu wa kwanza, Imamu Zamani (a.t.f.s) alimwandikia barua mwana wa Muhammad bin Othman baada kimfariji kutoka na kifo cha baba yake, alimweka kuwa ni mrithi wa nafasi ya unaibu iliyokuwa ikishikiliwa na baba yake wakati wa uhai wake.[5] Kabla ya hapo, Imam Hassan Askari (a.s.) pia naye alikuwa amemteua Muhammad bin Othman kama mrithi wa mwanawe (Imamu Mahdi) (a.t.f.s). [6] Muhammad bin Othman Amari alishika nafasi ya unaibu wa Imamu Mahdi (a.s) kwa takriban miaka arubaini. [7]
  • Hussein ibnu Ruh al-Nawbakhti (aliyefariki mwaka 326 Hijiria), ni naibu wa tatu wa Imam Mahdi (a.t.f.s), alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiaminiwa mbele ya Muhammad bin Othman na watu walio karibu naye huko Baghdad. Katika siku za mwisho wa maisha yake, Muhammad bin Othman alimtambulisha Hussein bin Ruh Nawbakhti kama ni mrithi wake kwa amri ya Imam Zaman (a.t.f.s). [8] Yeye manzoni alikuwa na nafasi na heshima maalum katika serikali ya ukoo wa Bani Abbas. Lakini baadaye aliingia kwenye matatizo hadi akaishi maisha ya siri kwa muda fulani, kisha akafungwa jela miaka mitano. [9] Yeye alishika nafsi ya unaibu wa Imam Zamani (a.t.f.s) kwa takriban miaka 21.
  • Naibu wa nne wa Imam Zaman (a.t.f.s) alikuwa ni Ali bin Muhammad Samuri (aliyefariki mwaka 329 Hijiria), yeye alishika wadhifa wa unaibu kwa muda wa miaka mitatu (kuanzia mwaka 326 hadi 329 Hijiria). Kipindi cha unaibu wa Samuri kiliambatana na udhibiti mkali na ukandamizaji wa serikali, jambo ambalo lilimzuia kufanya shughuli kwa mapana katika mtandao wa mawakala. [10] Taarifa ya Imamu Zamani (a.t.f.s) kwa Ali bin Muhammad Samri akimwarifu habari za kifo chake na kumalizika wa kipindi cha unaibu wake, ilikuwa ndio mwisho wa kumalizika kwa muhula wa Ughaibu mdogo na ndio mwanzo wa kuanza kwa kipindi cha Ughaibu mkubwa. Matukio haya ya mwisho ni mojawapo ya matukio muhimu zaidi katika maisha ya naibu wa mwisho. [11]

Barua ya Imamu Asri (Imamu Mahdi) kwa Samuri

“Mungu awalipe jaza njema ndugu zako katika kifo chako. Utakufa ndani ya siku sita. Kwa hiyo malizia kazi yako na usimteue yeyote yule kushika nafasi ya unaibu baada yako; Kwa sababu tayari zama za Ughaibu wa Pili zimeanza na zitadumu kwa muda mrefu, hadi Mwenyezi Mungu anipe idhini ya kudhiri, jambo ambalo halitatokea mpaka nyoyo (za watu) zilalame kutokana na ukatili, na ulimwengu kujaa dhulma, ambapo watatokea watu watakao waendea wafuasi wangu (Mashia) na kudai kwamba wameonana nami. Ila elewa ya kwamba; yeyote anayedai kuniona kabla ya kusimama kwa Sufani na kusikika ukelele kutoka mbinguni, mtu huyo mzushi na mwongo."[1]

Hatua na Kazi Mbalimbali

Hatua zote zilizochukuliwa na manaibu maalum (Manaibu Wanne) zilitekelezwa chini ya amri ya Imamu Zamani (a.t.f.s) [12] Shughuli hizo zinaweza kugawika kama ifuatavyo:

Utendaji kwa Njia ya Siri

Kutokana kifo cha kishahidi cha Imamu Askari na kutokuwepo Imamu wa kumi na mbili, Nawwabu al-Arba'a (Manaibu Wanne) walikuwa ndio wenye mamlaka ya kushughulikia masuala mbalimbali ya Shia. Kwa vile zama hizo zilizmbatana na zama zenye hali ngumu katika utawala wa Bani Abbas, hivyo basi suala la kufanya taqiyyah (kujificha imani na itikadi) lilishika kasi mno katika zama hizo, hasa katika kipindi cha makamu (naibu) wa pili, wa tatu na wa nne [13] [14] Kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha ukandamizaji wa hali ya juu kabisa, hadi kufikia hatua ambayo Hussein bin Ruuh kwa muda fulani aliishia kuishi maisha ya siri, kisha akatiwa kifungoni kwa muda wa miaka mitano. Matokeo ya msimamo huu yalipelekea Mashia wa Maimamu kuhifadhi uwepo wao katikati utawala wa Bani Abbas na kujiweka kama watu wachache rasmi na wanaotambulika na serikali ya Bani Abbas na wafuasi wao ambao ni Sunni ushawishi mkubwa huko Baghdad. Kubakia kwao serikali hali wakiwa na daraja ya juu kabisa taaluma mbalimbali, kuliilazimisha serikali na wafuasi wake kuwatumia Mashia hao na kuishi nao kwa salama na amani. [15]

Mahusiano na Utawala wa Kikhalifa

Moja ya sera maalum za kisiasa ambazo baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Shia na hasa Mawawakili Maalum wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) katika kipindi hicho, ambao pia waliungwa mkono na Maimamu watakatifu, ulikuwa ni kujipenyeza ndani ya utawala wa Bani Abbasi na hata kuchukua nafasi ya uwaizari ndani ya utawala huo. [16] Hussein bin Ruhu Nawbakhti mwanzoni mwa uwakilishi (unaibu) wake wakati wa ukhalifa wa Muqtadir Abbasi, aliweza kupata heshima katika utawala huo. Yeye alibahatika kupata heshima hiyo kupitia ushawishi wa familia ya Nawbakhti na familia ya Ibn Furat, ambao alikuwa ni Mashia walioshika nafasi uwaziri ndani ya ukhalifa wa Muqtadir Abbasi, jamabo ambalo lilimfanya yeye kuwa na ushawishi na heshima kubwa katika utawala wa Bani Abbasi. [17] [18]

Kupambana na Magulati

Suala la kufanya ghuluwwu (kumpa mja siza za kiungu) lilikuwa ni mojawapo ya masuala muhimu na hatari katika enzi ya Wawakilishi Wanne, kiasi kwamba hata baadhi ya watoto wa Maimamu, kama vile Ja'afar mwana wa Imamu Hadi (a.s), aliyeitwa Ja'afar Kaddhabu, waliandamana na Maghulati [Maelezo 1] yeye pamoja na baadhi ya wanasiasa wa madhehebu ya Shia. [19] Mojawapo ya majukumu ya wawakilishi wanne ilikuwa kuwafedhehesha wale wote wenye madai ya uongo na kuwafikishia Mashia ujumbe wa Imamu wa Zama (a.t.f.s) juu ya laana na na kujitenga na watu hawo. [20] Kwa mfano, Muhammad ibn Nasiir, mwanzilishi wa madhehebu ya Naasiriyyah, alikuwa ni mmoja wa Maghulati aliyekuwa akiamini uungu Maimamu (a.s) na alikuwa akisambaza dhana ya uhalali wa ndoa baina ya maharimu wenyewe kwa wenyewe. Muhammad ibn Othman alimlaani na kufarakana naye. [21]

Shalmaghani alikuwa ni mmoja wa wawakilishi (naibu) wa Maimamu ambaye, licha ya cheo chake alichokuwa nacho katika kipindi cha Hussein ibn Ruuh, kwa sababu za tamaa alitumia nafasi yake vibaya na akaporomokea kwenye ughalati. Hussein Ibnu Ruuh alimfukuza na akatoa amri ya kumlaani iliyo idhiniwa kutoka kwa Imamu wa Zamani (a.t.f.s) juu yake. [22]

Kuondoa Shaka Juu ya Uwepo wa Imamu Mahdi (a.t.f.s)

Kulingana na maelezo ya Sheikh Tusi, kulikuwa na mzozo kati ya Ibn Abi Ghanim Qazwini na kundi la Shia kuhusu ukweli kwamba Imamu Askari (a.s) alikuwa na mtoto au la. Kwa hivyo, Mashia walimwandikia Imamu Mahdi (a.t.f.s) barua na kumwomba aumalize mzozo huo. Imamu alijibu kwa kusisitiza kwamba Mungu hajafuta dini yake baada ya Imamu wa Kumi na Moja, na kwamba katu yeye hajakata uhusiano (fungamano) kati yake na waja wake, fungamano hilo litaendelea hadi Siku ya Kiyama. [23]

Pia kuna barua nyingine iliyo toka kwa Imamu Mahdi (a.t.f.s) ambayo imenukuliwa katika moja ya Hadithi. Imamu Mahdi (a.t.f.s) alitoa barua hii wakati Ja'far Kaddhabu alipodai kuwa yeye ndiye mrithi wa Imamu Askari (a.s). Katika barua hii, Imamu Zamani (a.t.f.s) alizungumzia suala la uongozi wa Maimamu, maarifa na kutokuwa na umaasumu wao. Alibainisha kuwa Ja'far elimu ya hakujua ya halali wala ya haramu, wala hakuwa uwezo kutofautisha kati ya haki na batili, na kadhalika. Imamu katika barua yake hiyo, aliuliza ni jinsi Ja'far aliweza kudai uongozi hali akiwa hali kama hiyo. [24]

Mtandao wa Mawakala

Shaka ya Muhammad bin Ibrahim bin Mahziyari, ambaye baba yake alikuwa ni mmoja wa wawakilishi wa Imamu wa Kumi na Moja (a.s), ilitoweka na kumalizika moja kwa moja, baada ya barua hiyo iliyotoka kwa Imamu wa Mahdi (a.t.f.s). [25] Pia kuna barua nyengine kutoka kwa Imamu Mahdi (a.t.f.s) ambayo inaonyesha kwamba Imamu, mbali na Imamu kuthibitisha uwepo wake na kufuta shak wasiwasi dhidi ya uwepo wake, pia ndani ya baru hiyo alijibu maswali kadhaa yanayo husiana na fiqhi. [26]

Kuanzia zama za Imamu Kadhim (a.s), kulikuwa na kawaida ya kuteua wawakilishi tofauti wa kuendesha mambo ya sehemu tofauti na kuunda uhusiano kati ya Mashia na Maimamu (a.s). Baada ya kuanza kwa zama za Ughaibu, mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wawakilishi na Imamu Mahdi (a.t.f.s) yalikatika, na msingi wa mawasiliano baina ya Mashia na Imamu wao ulikuwa ukitegemea Makili Wanne wakuu walioteuliwa na Imamu wa Kumi na Mbili. Mawakili hao walituma mali walizokuwa wakizikusanya kutoka kwa watu na kuzifikisha kwa kwa Wakili Mkuu huko Baghdad kupitia njia tofauti, naye alitumia mali hizo kulingana na maagizo ya Imamu katika matukio yaliyoainishwa kutumika mali hizo. [27]

Kulikuwa na mawakili katika miji kadhaa ya Wailamu waliokuwa wakiwawakilisha Maimamu katika miji hiyo, ambao khabari zao kwa namna fulani zimetufikia kupitia katika vyanzo vya hadithi. Baadhi ya miji ilikuwa na wawakilishi ndani yake ni kama vile; Ahwaz, Samarraa, Misri, Hijazi, Yemen, na pia katika mikoa ya Iran kama vile Khorasani, Rey, na Qom. [27]

Kuficha Siri Juu ya Imamu Mahdi (a.t.f.s)

Kuficha siri za Imamu Mahdi (a.t.f.s) ilikuwa mojawapo ya majukumu muhimu ya Manaibu maalum. Kulingana na taarifa za kihistoria na Hadithi, Imamu alikuwa akiishi Iraq, Makka na Madina, na aliishi kwa njia ambayo Wakili Mkuu angeweza kukutana naye bila pingamizi. [29] Wakati Hussein bin Ruuh Nobakhti alipofikia cheo cha Unaibu wa Imamu, Abu Sahli Nawbakhti alisema kuhusiana na nafasi na hadhi ya Ibn Ruuh kwamba: "Kama ningejua nina pajua fika mahali pa Imamu aliyeghibu kama vile Abual-Qasim anavyo pajua, pengine ningefichua mbele ya adui katika wakati mgumu wa mjadala; hali ya kwamba Abual-Qasim -kwa uaminifu wake alionao- amemficha Imamu chini ya joho lake, hatamwonesha mtu yeyote, hata wamkate vipande vipande kwa mkasi."[30]"

Ingawaje wawakilishi (manaibu) maalum walisisitiza juu ya uwepo wa Imamu wa Kumi na Mbili, lakini waliwataka Mashia wasisitize kujua mahala alipo Imamu wa zama zao. Walifanya hivyo mawakili hao ili kulinda usalama wake (a.t.f.s). [31]

Kujibu Maswali ya Kifiqhi na Kiitikadi

Manaibu Wanne waliwasilisha maswali ya kifiqhi na kisheria ya Mashia kwa Imamu Mahdi (a.t.f.s) na baada ya kupokea majibu kutoka kwake, waliwafikisha majibu hayo kwa watu. Shughuli hii haikuhusiana na masuala ya kisheria tu, bali mawakala walishiriki katika vikao mbalimbali vya majadiliano ili kutatua matatizo ya kielimu yanayo husiana na ya imani kwa ajili kuongoza umma wote kwa ujumla. [32] Hati ya Isaka bin Ya'qub [33] na pia hati ya Muhammad bin Ja'far Asadi [34] ambazo zinajumuisha masuala muhimu ya kijamii, kifiqhi na sheria na ushiriki wa Hussein bin Ruh katika majadiliano ya kielimu na akida zinaonesha wazi shughuli na jitihada za Mawakala Wanne katika masuala haya. [35]

Ziara ya Manaibu Wanne (Matini ya Sala na Salamu)

Sayyid bin Taawuus katika kitabu chake Misbaah al-Ziyarah, ametaja ziara (matini ya sala na salamu) ambayo inaweza kusomwa kwa ajili ya kila mmoja miongoni mwa mawakala wanne wa Imamu Mahdi (a.t.f.s). Anaamini kwamba maandishi ya ziara hiyo yamehusishwa na baba ya Hussein bin Ruuh Nobakhti. [36] [Maelezo 2]

Pia, Allama Majlisi katika katika kitabu chake Biharu al-Anwari, amenukuu ziara kwa ajili Othmani bin Said na akasema kwamba matini ya ziara hiyo ameiona katika moja ya nyaraka za zamani kutoka kwa mmoja wa wanazuoni wa Kishia.[37] [Maelezo 3]

Kazi Zilizo Andikwa Kuhusiana Mada hii Makhusudi

Kitabu kiitwacho “Pazuuhesh Peraamun Zindegaani Nuwwabe Khaasse Imam Zaman (a.t.f.s)” Mahdi (a.t.f.s)" kilicho andikwa na Ali Ghafarzadeh. Ni kazi ya kujitegemea juu ya nyanja wa kwafahamu Mawakala Wanne. Ayatullahi Ja'afar Subhani ndiye aliye andika utangulizi wa kitabu hicho, ambacho kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Taasisi ya Uchapishaji ya Nubuugh mwaka 1375 Shamsia. [38]

Rejea

  1. Rejea kitabu Kamal al-Din wa Tammam Al-Naimah cha Sheikh Saduqu, chapa ya mwaka 1395 Hijiria, juz. 2, uk.516.

Maelezo

  1. Kundi lilipotoka lenye kumpa kiumbe au Imamu sifa za kiungu
  2. السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا فُلَانَ بْنَ فُلَانٍ (نام یکی از نواب را بگوید) أَشْهَدُ أَنَّكَ بَابُ الْوَلِيِّ أَدَّيْتَ عَنْهُ وَ أَدَّيْتَ إِلَيْهِ مَا خَالَفْتَهُ وَ لَا خَالَفْتَ عَلَيْهِ قُمْتَ خَاصّاً وَ انْصَرَفْتَ سَابِقاً جِئْتُكَ عَارِفاً بِالْحَقِّ الَّذِي أَنْتَ عَلَيْهِ وَ أَنَّكَ مَا خُنْتَ فِي التَّأْدِيَةِ وَ السِّفَارَةِ السَّلَامُ عَلَيْكَ مِنْ بَابٍ مَا أَوْسَعَكَ وَ مِنْ سَفِيرٍ مَا آمَنَكَ وَ مِنْ ثِقَةٍ مَا أَمْكَنَكَ أَشْهَدُ أَنَّ اللَّهَ اخْتَصَّكَ بِنُورِهِ حَتَّى عَايَنْتَ الشَّخْصَ فَأَدَّيْتَ عَنْهُ وَ أَدَّيْتَ إِلَيْهِ ثُمَّ تَرْجِعُ فَتَبْتَدِئُ بِالسَّلَامِ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ ص إِلَى صَاحِبِ الزَّمَانِ وَ تَقُولُ بَعْدَ ذَلِكَ جِئْتُكَ مُخْلِصاً بِتَوْحِيدِ اللَّهِ وَ مُوَالاةِ أَوْلِيَائِهِ وَ الْبَرَاءَةِ مِنْ أَعْدَائِهِمْ وَ مِنَ الَّذِينَ خَالَفُوكَ يَا حُجَّةَ الْمَوْلَى وَ بِكَ اللَّهُمَّ تَوَجُّهِي وَ بِهِمْ إِلَيْكَ تَوَسُّلِي ثُمَّ تَدْعُو وَ تَسْأَلُ اللَّهَ مَا تُحِبُّ تَجِبُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَعَالَى‏ ; Amani iwe juu yako, ewe [jina la naibu litajwe hapa]. Ninashuhudia kwamba wewe ni mlango wa Walii, uliye tekeleza kwa niaba yake kazi zake na ukatimiza yalio wajibu juu yako kwa ajili yake, bila hukubadilisha kitu kinyume na alivyo kuamrisha na hukwenda kinyume na matakwa yake. Ulisimama kaka ni naibu makhususi na ukaondoka mapema (umemtangulia katika kufariki). Nimekujia hali nikiitambua haki uliyo nayo, na kwamba hukufanya khiana katika utekelezaji na uwakilishi. Amani iwe juu yako, wewe ni mlango mpana ulioje, na mwakilishi mwaminifu ulioje! Na mkweli ulioje. Ninashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu amekuteua kwa nuru yake hadi ukamwona mtu huyu mtukufu (Imamu Mahdi), kisha ukatekeleza kwa niaba yake na ukatekeleza yaliokuwajibikia kwake. Kisha utaanza kumsalimia (sala na salamu) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kisha Imamu Mahdi (a.t.f.s) kisha baada ya hapo utasema: "Nimekuja kwako nikiwa ni mpwekeshaji na mwenye ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu na mwenye kuwaunga mkono na kuwakubali mawalii wake na kuukubali uongozi wao na kujitenga na maadui zao na wale waliopingana nawe. Ewe hoja (dalili na kielelezo, yaani naibu) ya walii wa Mungu (Imamu Mahdi), na kwako, Ewe Mwenyezi Mungu, mwelekeo wangu uko kwako wewe, na kwao (kwa jaha ya mawalii hawa) ninaomba msaada kwako. Kisha unaomba na kumuomba Mwenyezi Mungu kile unachopenda, kitatimizwa Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda."
  3. السَّلَامُ عَلَیک أَیهَا الْعَبْدُ الصَّالِحُ النَّاصِحُ لِلَّهِ وَ لِرَسُولِهِ وَ لِأَوْلِیائِهِ الْمُجِدُّ فِی خِدْمَةِ مُلُوک الْخَلَائِقِ أُمَنَاءِ اللَّهِ وَ أَصْفِیائِهِ السَّلَامُ عَلَیک أَیهَا الْبَابُ الْأَعْظَمُ وَ الصِّرَاطُ الْأَقْوَمُ وَ الْوَلِی الْأَکرَمُ السَّلَامُ عَلَیک أَیهَا الْمُتَوَّجُ بِالْأَنْوَارِ الْإِمَامِیةِ الْمُتَسَرْبِلُ بِالْجَلَابِیبِ الْمَهْدِیةِ الْمَخْصُوصُ بِالْأَسْرَارِ الْأَحْمَدِیةِ وَ الشُّهُبِ الْعَلَوِیةِ وَ الْمَوَالِیدِ الْفَاطِمِیةِ السَّلَامُ عَلَیک یا قُرَّةَ الْعُیونِ وَ السِّرَّ الْمَکنُونَ السَّلَامُ عَلَیک یا فَرَجَ الْقُلُوبِ وَ نِهَایةَ الْمَطْلُوبِ السَّلَامُ عَلَیک یا شَمْسَ الْمُؤْمِنِینَ وَ رُکنَ الْأَشْیاعِ الْمُنْقَطِعِینَ السَّلَامُ عَلَی وَلِی الْأَیتَامِ وَ عَمِیدِ الْجَحَاجِحَةِ الْکرَامِ السَّلَامُ عَلَی الْوَسِیلَةِ إِلَی سِرِّ اللَّهِ فِی الْخَلَائِقِ وَ خَلِیفَةِ وَلِی اللَّهِ الْفَاتِقِ الرَّاتِقِ السَّلَامُ عَلَیک یا نَائِبَ قُوَّامِ الْإِسْلَامِ وَ بَهَاءِ الْأَیامِ وَ حُجَّةَ اللَّهِ الْمَلِک الْعَلَّامِ عَلَی الْخَاصِّ وَ الْعَامِّ الْفَارُوقَ بَینَ الْحَلَالِ وَ الْحَرَامِ وَ النُّورَ الزَّاهِرَ وَ الْمَجْدَ الْبَاهِرَ فِی کلِّ مَوْقِفٍ وَ مَقَامٍ السَّلَامُ عَلَیک یا وَلِی بَقِیةِ الْأَنْبِیاءِ وَ خِیرَةَ إِلَهِ السَّمَاءِ الْمُخْتَصَّ بِأَعْلَی مَرَاتِبِ الْمَلِک الْعَظِیمِ الْمُنْجِی مِنْ مَتَالِفِ الْعَطَبِ الْعَمِیمِ ذی [ذَا اللِّوَاءِ الْمَنْصُورِ وَ الْعَلَمِ الْمَنْشُورِ وَ الْعِلْمِ الْمَسْتُورِ الْمَحَجَّةَ الْعُظْمَی وَ الْحُجَّةَ الْکبْرَی سُلَالَةَ الْمُقَدَّسِینَ وَ ذُرِّیةَ الْمُرْسَلِینَ وَ ابْنَ خَاتِمِ النَّبِیینَ وَ بَهْجَةَ الْعَابِدِینَ وَ رُکنَ الْمُوَحِّدِینَ وَ وَارِثَ الْخِیرَةِ الطَّاهِرِینَ صَلَّی اللَّهُ عَلَیهِمْ صَلَاةً لَا تَنْفَدُ وَ إِنْ نَفِدَ الدَّهْرُ وَ لَا تَحُولُ وَ إِنْ حَالَ الزَّمَنُ وَ الْعَصْرُ اللَّهُمَّ إِنِّی أُقَدِّمُ بَینَ یدَی سُؤَالِی الِاعْتِرَافَ لَک بِالْوَحْدَانِیةِ وَ لِمُحَمَّدٍ بِالنُّبُوَّةِ وَ لِعَلِی بِالْإِمَامَةِ وَ لِذُرِّیتِهِمَا بِالْعِصْمَةِ وَ فَرْضِ الطَّاعَةِ وَ بِهَذَا الْوَلِی الرَّشِیدِ وَ الْمَوْلَی السَّدِیدِ أَبِی مُحَمَّدٍ عُثْمَانَ بْنِ سَعِیدٍ أَتَوَسَّلُ إِلَی اللَّهِ بِالشَّفَاعَةِ إِلَیهِ لِیشْفَعَ إِلَی شُفَعَائِهِ وَ أَهْلِ مَوَدَّتِهِ وَ خُلَصَائِهِ أَنْ یسْتَنْقِذُونِی مِنْ مَکارِهِ الدُّنْیا وَ الْآخِرَةِ اللَّهُمَّ إِنِّی أَتَوَسَّلُ إِلَیک بِعَبْدِک عُثْمَانَ بْنِ سَعِیدٍ وَ أُقَدِّمُهُ بَینَ یدَی حَوَائِجِی أَنْ تُصَلِّی عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ وَ شِیعَتِهِ وَ أَوْلِیائِهِ وَ أَنْ تَغْفِرَ لِی الْحُوبَ وَ الْخَطَایا وَ تَسْتُرَ عَلَی الزَّلَلَ وَ السَّیئَاتِ وَ تَرْزُقَنِی السَّلَامَةَ مِنَ الرَّزَایا فَکنْ لِی یا وَلِی اللَّهِ شَافِعاً نَافِعاً وَ رُکناً مَنِیعاً دَافِعاً فَقَدْ أَلْقَیتُ إِلَیک بِالْآمَالِ وَ وَثِقْتُ مِنْک بِتَخْفِیفِ الْأَثْقَالِ وَ قَرَعْتُ بِک یا سَیدِی بَابَ الْحَاجَةِ وَ رَجَوْتُ مِنْک جَمِیلَ سِفَارَتِک وَ حُصُولَ الْفَلَاحِ بِمَقَامِ غِیاثٍ أَعْتَمِدُ عَلَیهِ وَ أَقْصِدُ إِلَیهِ وَ أَطْرَحُ نَفْسِی بَینَ یدَیهِ وَ السَّلَامُ عَلَیک وَ رَحْمَةُ اللَّهِ وَ بَرَکاتُهُ ثُمَّ صَلِّ صَلَاةَ الزِّیارَةِ وَ أَهْدِهَا لَهُ وَ لِشُرَکائِهِ فِی النِّیابَةِ صَلَّی اللَّهُ عَلَیهِمْ أَجْمَعِینَ ثُمَّ وَدِّعْهُ مُسْتَقْبِلًا لَهُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَعَالَی.

Vyanzo

  • Ibn Tawus, Misbah al-za'ir. Qom: Al al-Bayt, 1375 sh.
  • Ahmadi, Muhammad Husayn, Nuwwab arba'a wa shakhsiyyat-i ijtima'i anan. Simay-i Tarikh, Num. 4, 1390 sh.
  • Ja'fariyan, Rasul, Hayat-i fikri wa siyasi imaman Shi'a. Qom: Ansariyan, 1381 sh.
  • Saduq, Muhammad b. Ali al-, Kamal al-din wa tamam al-ni'ma. Tehran: Islamiyya, 1395
  • Ghaffarzadi, Ali, Zindigani nuwwab-i khass-i imam zaman. Qom: Intisharat-i Nubugh, 1379
  • Sadr, al-Sayyid Muhammad al-, Tarikh al-ghayba. Beirut: Dar al-Ta'aruf, 1412
  • Jabbari, Muhammad Rida, Sazman-i wikalat wa naqsh-i an dar 'asr-i a'imma. Qom: Mu'assisa Amuzishi Pazhuhishi Imam Khomeini, 1382
  • Tusi, Muhammad b. al-Hasan al-, Al-Ghayba. Qom: Dar al-Ma'arif al-Islamiyya, 1411
  • Kulayni, Muhammad b. Ya'qub al-, Al-Kafi. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyya, 1388
  • Majlisi, Muhammad Baqir al-, Bihar al-anwar li durar akhbar al-a'imma al-athar. Tehran: Al-Islamiyya, 1363
  • Husayn, Jasim, Tarikh-i siyasi ghaybat-i imam-i dawazdahum. Tehran: Amir Kabir, 1385