Nenda kwa yaliyomo

Istihala

Kutoka wikishia

Istihala (Kiarabu: الاستحالة): Dhana ya istihala katika tafsiri ya kifiq-h, inaeleweka kama mchakato maalumu ambapo kitu kisicho safi (ambacho ni najisi) hubadilika na kugeuka kuwa kitu safi chenye utohara kamili. Katika muktadha huu, mafaqihi wanakihisabu kitu hicho (kilicho badilika) kuwa ni miongoni vitoharishaji (vitakatishaji). Kulingana na fat’wa hii, iwapo kitu kisicho safi, kinabadilika kwa njia ya asilia, basi kitakuwa safi na hakitakuwa na matatizo katika matumizi yake. Kwa mfano, ikiwa mbwa anakufa na kugeuka udongo, udongo huo huhisabiwa ni kuwa ni udongo safi. Hali kadhalika, majivu yanayotokana na kuni zisizo safi pia yanachukuliwa kuwa ni majivu safi.

Hata hivyo, kwa maoni ya kifiq-hi, kubadilika kwa ngano kuwa unga au mkate, pamoja na kubadilika kwa maziwa kuwa jibini, hayaingii katika dhana ya “istihala” na hivyo hayaingii katika muktadha wa sheria zinazohusiana na “istihala”. Katika hali hii, mchakato huu wa kubadilika hauathiri hali ya usafi wa kitu kilichobadilika, na hivyo, unachukuliwa kuwa ni mfumo tofauti na “istihala” inayotambulika katika sheria za kifiq-hi.

Ufafanuzi wa Kifiq-hii wa Istihala na Mifano Yake

Dhana ya "istihala" katika fiqhi, inarejelea mchakato maalumu ambapo najisi (kama mbwa) au kitu kilicho najisika kupitia najisi fulani, hubadilika kutoka hali moja kwenda nyengine kupitia mabadiliko ya asilia, na hatimae kuwa safi na chenye tohara kamili. Mabadiliko haya ya asili hufanyika wakati kitu hicho kinavyopitia hatua za kimaumbile ambazo zinabadili hali yake ya awali, kwenda hali nyengine kabisa. Mfano wa wazi wa “istihala”, ni pale kuni inabadilika kuwa jivu au moshi baada ya kuchomwa moto. Katika hali hii, kama kuni hiyo, ilikuwa ni najisi, kwa kuzingatia sheria za fiq-h, pale kuni hiyo inapokuwa jivu au moshi, huhisabiwa kuwa ni safi, usafu huo unatokana na mchakato wake wa mabadiliko ya asili yake. Vile vile, mchakato wa mwili wa mnyama au binadamu aliye kufa na kugeuka udongo, hupelekea ugongo wao kuhisabiwa kuwa ni kitu safi, kufuatia mabadiliko haya. [1]

Kwa hivyo, “istihala” ni mchakato maalumu ambao kwa nadharia za kifiq-hii husababisha kitu kilichobadilika kupata hukumu ya safi baada ya kupitia hatua za mabadiliko yake ya kimaumbile. Kuna mifano mbalimbali ya “istihala” inajadiliwa katika vitabu vya fiq-hi, ili kuelewa mchakato wa mabadiliko ya asili na athari zake katika hali ya usafi. Mifano mingine ya istihala ni pamoja na:

  • Kubadilika kwa Kinyesi kuwa Udongo: Kinyesi kinapopitia mchakato wa kuoza au kuteketea, kinaweza kubadilika kuwa udongo. Katika hali hii, kinyesi, ambacho ni najisi asilia, huchukuliwa kuwa kitu safi baada ya mchakato huu wa mabadiliko yake asilia.
  • Kubadilika kwa Mkojo au Kioevu Kisicho Safi kuwa Mvuke: Mkojo au kioevu kisicho safi kinapopashwa moto na kubadilika kuwa mvuke, hali hii ijulikanayo kama ni istihala, hupelekea mvuke huu kuwa usafi, hii na kwa sababu kioevu kimebadilika kutoka umbile moja asilia na kwenda umbile jengine.
  • Kubadilika kwa Mbegu (Manii) kuwa Kiumbe Hai: Mabadiliko ya mbegu kuwa kiumbe hai, kama vile mmea au mnyama, pia huhisabiwa ni miongoni mwa michakato ya istihala. Mchakato huu unahusisha mabadiliko makubwa kutoka hali ya awali ya mbegu hadi kuwa kiumbe hai.
  • Kubadilika kwa Chakula Kilicho Najisi kuwa Sehemu ya Mwili wa Mnyama Anayeweza Kuliwa

Chakula najisi kinachotumiwa na mnyama na kisha kubadilika kuwa sehemu ya mwili wa mnyama anayekubalika kuliwa, kinachukuliwa kuwa ni miongoni mwa michakato wa istihala. Hii inamaanisha kwamba chakula hicho, licha ya kwamba hapo wali kilikwa najisi, ila kwa kuwa tayari kimeshakuwa ni sehemu ya mwili wa mnyama, basi nyama yake huwa ni halali kifiq-hi. [2]

Kubadilika kwa Sifa za Kitu na Kutawanyika kwa Vipande Vyake: Mchakato wa istihala Katika fiq-hi, haujumuishi mabadiliko ya sifa za kitu fulani au hali ya kutawanyika kwa vipande vyake. Mabadiliko haya ya sifa hizi au mtawanyiko wake, hayahesabiki kama ni moja ya aina za istihala. Hii ni kwa sababu istihala inahitaji mabadiliko ya kimaumbile ambayo hubadilisha asili ya kitu kutoka hali moja asilia na kwenda kwenye asili nyengine, kama jiwe kuwa chokaa. Kwa mfano: Kubadilika kwa Ngano kuwa Unga au Mkate, ngano inapobadilika kuwa unga au mkate, mchakato huu unahusisha na mabadiliko ya muundo lakini hauathiri hali ya usafi wa ngano hiyo. Hii si miongoni mwa istihala, kwa sababu ngano bado ipo katika asili yake, na mabadiliko haya yanahusisha tu mabadiliko ya muundo wake. Kubadilika kwa Maziwa kuwa Jibini, maziwa yanapobadilika kuwa jibini, hapa pia kuna mabadiliko ya kimaumbile lakini siyo mchakato wa istihala. Maziwa hubadilika kuwa jibini kupitia mchakato wa matengenezo maalumu, na maziwa ya awali yanaendelea kuwa na hali yake ya asilia haka kama tanabadilika kutoka kioevu na kuwa jibini. [3]

Utoharishi Kupitia Istihala

Kulingana na fat’wa za mafaqihi, istihala inachukuliwa kama ni moja ya njia au nyenzo toharishi. [4] Nyenzo toharishi (mutahhirat) ni njia au vitu vinavyomsaidia mtu kuondoa najisi na kuleta hali ya usafi. [5]

Tofauti Kati ya Istihala na Inqilab

Makala Asili: Inqilab (Ya kifiq'hi)

Dhana ya "istihala" na "inqilab" katika fiqh, hufasiriwa kwa maana ya mchakato wa mabadiliko ya vitu, ila kuna tofauti muhimu baina dhana mbili hizi ambazo zinahitaji maelezo ya ziada ili kueleweka vizuri. Istihala inamaanisha mchakato kubadilika kwa kitu najisi na kwena kitu chengine kilicho safi kupitia mabadiliko muhimu katika asili yake. Mchakato huu unahusisha mabadiliko ya kimaumbile ambayo hubadilisha hali ya kitu kutoka hali ya unajisi kwenda kwenye kitu chengine chenye asili ya utohara. Mfano wa istihala ni pale kinyesi kinapobadilika kuwa udongo au moshi. Inqilab, kwa upande mwingine, inarejelea mchakato maalum ambapo kinywaji cha pombe hubadilika kuwa siki. [6] Hapa, pombe inabadilika kuwa siki kupitia mchakato wa fermenti, lakini asili ya kitu kinachoingia katika mchakato huu, ni kile kile kinywaji kilichokuwa ni pombe, ambacho bado kinabaki kuwa ni kitu kimoja kinachobadilika kuwa kitu chengine bila kubadilisha hali yake ya asili kwa njia ya mabadiliko ya kimaumbile (mfumo wake wa maji). Kuna mitazamo tofauti miongoni mwa mafakihi kuhusiana na uhusiano kati ya istihala na inqilab, mitazamo hiyo ni kama ifuatavyo: Mitazamo ya Kwanza: Baadhi ya mafakihi wanaona kuwa inqilab ni moja ya aina za istihala. Kwa mtazamo huu, mchakato wa inqilab, ambapo pombe hubadilika kuwa siki, huchukuliwa kama ni miongoni mwa matokeo ya istihala, kwa sababu inahusisha mabadiliko ya hali ya kitu kutoka kuwa kinywaji cha pombe hadi kuwa siki. [7] Mitazamo ya Pili: Wengine wanalihisabu tokeo la inqilab kama ni tokeo la kujitegemea lililo tengana na istihala. Kwa mtazamo huu, inqilab inachukuliwa kuwa ni mchakato wa pekee ambao haujumuishi mchakato wa istihala. Katika mtazamo huu, inqilab ni mchakato unaoendelea bila kubadilisha hali yake ya asili ya kitu fulani katika muktadha wa sheria za fiq-hi, na ni tofauti na istihala ambayo inahitaji mabadiliko ya kimaumbile. [8] Kwa hivyo, tofauti kati ya istihala na inqilab inategemea jinsi mafakihi wanavyoelewa na kuuhisabu mchakato wa mabadiliko wa mawili hayo sheria za fiqh.

Sayyid Abu al-Qasim al-Khui (1278-1371 H.Sh.), mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu katika fiq-hi, anaeleza kwamba; inqilab ni aina ya istihala. Al-Khui anafafanua kwamba katika mchakato wa inqilab, kama inavyotokea wakati kinywaji cha pombe kinapobadilika kuwa siki, asili ya kinywaji hicho hubadilika kabisa kabisa. Kwa mujibu wa maoni ya kawaida ya wanajamii na sheria za fiq-h-, mabadiliko haya ya pombe kuwa siki, yanazingatiwa kuwa ni miongoni mwa istihala kwa sababu, ule ulevi au pombe, huadilika moja kwa moja kutoka kwenye asili ya pombe kwenda kwenye asili ya siki. [9] Kwa hivyo, kwa mtazamo wa al-Khoei, inqilab siyo mchakato wa kipekee wa kujitegemea, bali ni sehemu ya istihala, kwa kuwa yote yanahusisha mabadiliko ya asili ambayo yanabadilisha hali ya kitu kutoka hali moja kwenda hali nyengine.

Hukumu za Istihala

Kulingana na maelezo yaliyopo kwenye vitabu vya fiqh, baadhi ya hukumu zinazohusiana na istihala ni kama ifuatavyo:

  • Kitu Kilicho Najisi Kinapobadilika Hali Yake Asilia: Kulingana na sheria za fiq-hi, ikiwa maada asili najisi au kilicho najisika kitabadilika asili yake na kwena kwenye asili ya kitu chengine kabisa, kitu hicho kitachukuliwa kuwa safi. Mabadiliko haya yanajumuisha kubadilika kwa hali ya kitu hicho kabisa kabisa, kama vile kinyesi kinapobadilika kuwa udongo au moshi.
  • Majivu ya Kuni Zilizo Najisi: Ikiwa kuni zilizochafuka na kuwa najisi, zitaungua na kuwa jivu, jivu hilo litakuwa ni tohara. Hii ni kwa sababu mchakato wa uunguaji umesababisha mabadiliko ya kiasili ambayo yamebadilisha hali ya awali ya kuni hizo, na hivyo jivu hilo huhisabiwa kuwa safi na tohara.
  • Mbwa Aliyebadilika Kuwa Chumvi: Ikiwa mbwa aliyekufa ataanguka katika bonde la chumvi na mwili wake ukabadilika kuwa chumvi, mujibu wa sheria za fiq-hi chumvi hiyo itachukuliwa kuwa safi na toharifu. Mabadiliko haya ya kiasili yanayofanyika katika mwili wa mbwa ni moja ya mifano ya istihala, ndio maana chumvi hiyo ikachukuliwa kuwa safi.
  • Ngano iliyo Najisi Inapobadilishwa kuwa Unga au Mkate: Ikiwa ngano iliyo najisi itasagwa kuwa unga au kuokwa kuwa mkate, unga au mkate huo hautachukuliwa kuwa safi na toharifu. Hii ni kwa sababu mchakato wa kusaga au kuoka hauleti mabadiliko ya kiasili yanayoweza kutafsiriwa kama ni istihala. Kwa hivyo, unga au mkate huo utaendelea kuchukuliwa kuwa ni najisi.
  • Vyungu Vilivyotengenezwa na Udongo Ulio Najisi: Vyungu vilivyotengenezwa kwa udongo uliochafuka kwa najisi, vitabaki kuwa najisi, kwa sababu mchakato wa kutengeneza vyungu haubadilishi hali ya udongo huo kiasili. Hali hii inaonyesha kuwa mchakato wa kutengeneza vyungu siyo istihala.
  • Kitu Kilicho Najisi na Hakuna Uhakika wa Istihala: Ikiwa kuna kitu kilicho najisi na hakuna uhakika wa kama kimepitia mchakato wa istihala au la, kitu hicho kitachukuliwa kuwa najisi mpaka ithibitishwe kuwa kimebadilika na kuwa safi. Hii inamaanisha kwamba, katika hali ya shaka, hukumu itatolewa kulingana na hali ya awali ya kitu hicho, yaani, kitu hicho kitachukuliwa kuwa najisi mpaka pale ambapo istihala itapoweza kuthibitishwa. [10]

Hukumu hizi zinaonyesha umuhimu wa mchakato wa mabadiliko ya kiasili katika kubaini usafi wa vitu mbalimbali katika sheria za fiq-hi. Pia zinaonyesha jinsi sheria hizi zinavyotumika katika hali mbalimbali za maisha ya kila siku, kuhakikisha kuwa usafi unazingatiwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.

Rejea

Vyanzo