Wanyama halali

Kutoka wikishia

Mnyama ya halali ni mnyama ambaye nyama yake inaruhusiwa kuliwa kwa mujibu wa sheria ya fiqhi. Katika kila aina zote tatu za wanyama wa nchi kavu, wanyama wa majini pamoja na ndege, kuna wanyama ambao nyama zao ni halali kuliwa. Moja ya sharti zinazoifanya nyama ya mnyama fulani kuwa ni halali, ni kuchinjwa kihalali kwa mnyama huyo. Hata hivyo kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi, ni haramu kula baadhi ya sehemu za mnyama huyo, hata kama mnyama huyo atakuwa amechinjwa kihalali. Sehemu ambazo ni haramu kuzila ni; damu, wengu, uume wa mnyama pamoja na korodani.

Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi, hairuhusiwi kutumia ngozi ya wanyama wa halali wenye sifa ya kuwa na damu inayofoka -wakati wa kuchinjwa-, ambao wamekufa wenyewe au wameuliwa au labda hwakuchinjwa kisheria.

Welewa wa dhana

Kifiqhi wanyama wamegawanywa katika sehemu mbili; Wanyama wenye nyama halali na wanyama wenye nyama haramu. [1] Nyama ambao nyama zao ni halali, ni wale ambao ni ruhusa kula nyama zao pamoja sehemu halali za mwili wao baada ya kuchinjwa kihalali. [2] Sheria kuhusiana na nyama za wanyama halali, zimejadiliwa katika vitabu vya fiqhi ndani ya milango maalumu inayojadili yanayohusiana na tohara, sala, kuwinda (viwindwa) pamoja na msuala yanayohusiana na sheria za uchinjaji. [6]

Nyama za wanyama halali

Kwa mujibu wa fiqhi ya Shia, miongoni mwa aina tatu za wanyama wa nchi kavu, wanyama wa baharini na ndege, wanyama wafuatao ni halali nyama zao kuliwa:

  • Wanyama halali wa nchi kavu wenye miguu minne; Ng'ombe, kondoo, mbuzi, paa, kulungu, swala, kulungu, pundamilia, na mbuzi wa milimani. Wote hao ni halali kuliwa, hata punda, farasi, chotara anayetokana na punda na farasi pamoja na pundamilia. Ila ni chukizo (makuruhu) kula nyama za wanyama wa kundi hili la mwisho, yaani: farsi, punda, pundamilia, pamoja na chotara wa punda na farasi. [8]
  • Wanyama wa baharini; Samaki wenye magamba, uduvi na kamba wadogowadogo ni halali kula, wailobakia miongoni mwa wanyama wa majini ni haramu. [9]
  • Ndege: Ndege ambao wana moja ya sifa nne zifuatazo ni halali kula; Ndege wenye kifuko kidogo cha chakula (crop), kifiko hicho ni sehemu iliyopanuliwa yenye ukuta mwembamba wa njia ya chakula inayotumika kuhifadhi chakula kabla ya kusagwa. Kuna wanyama kadhaa wenye mfumo wa kama huo, wakiwemo baadhi ya ndege. Sifa ya pili ni kuwa na firigisi (gizzard/ventriculus). Sifa ya tatu ni kuwa na mwiba nyuma ya mguu. Sifa ya nne ni kupigambawa mfululizo, [10] kama vili kuku, bata mzinga, ndege wadogo waodo, njiwa, bata, kware na mbuni, [11] Pia Nyama ya Hud-hud, kibumbamshale [12] pia ni halali ila ni chukizo (makuruhu). [13]

Sehemu na viungo haramu vya wanyama halali

Mafaqihi wamezihisabu sehemu na viungo kadhaa vya wanyama halali kuwa ni haramu, ingawaje wanyama hao ni halali kuliwa. [14] Sehemu hizo haramu ni kama vile damu, wengu, sehemu za siri za kiume na pamoja na korodani za wanyama hao. [15]

Hukumu ya kutumia ngozi katika ibada

Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi, ni haramu kutumia ngozi za wanyama walio halali kuliwa nyama zao, ambao wana sifa ya damu ifokayo au kuchupa pale wachinjwapo, iwapo wanyama hao watakuwa wamekufa wenyewe, wameuliwa au hawakuchinjwa kwa chinjo la kisheria. Hivyo basi haijuzu kutumia ngozi zao katika sala. Ila ikiwa imetoka katika soko la Waislamu, kutoka na dhana ya kwamba ya kwamba katika masoko ya Waislamu huuzwa vitu halali, dhana ambayo pia inamaanisha ngozi hizo zinatokana na wanyama waliochinjwa kihalali. Na wala si wajibu kwa mnunuzi wa mwingine kufanya uchunguzi na kudadisi uhalali wa machinjo ya wanyama hao. [16]

Mitazamo kuhusiana na machinjo ya wanyama halali

Nchini Iran na baadhi ya nchi nyingine za Kiislamu, ili kuthibitisha ubora wa nyama halali kwa ajili ya kuliwa, wataalamu wa kuchinja na kuwinda wanyama halali husimamia mchakato mzima wa kuwinda na kuchinja wanyama halali. [17] Pia nchini Iran, sheria ya usimamizi wa kisheria kuhusiana na uwindaji na uchinjaji, iliidhinishwa na Baraza la Kiislamu mwaka wa 1387 Ashamsia. [18]

Vyanzo

  • Bani Hashimi Khomeini, Muhammad Hassan. Taudhīh al-Masā'il Maraje'. No. 88. Site Portal Anhar. Diakses tanggal 13 Februari 2018.
  • Ejra-e Qanun-e Zebh-e Shar'i Dar 57 Kesywar-e Eslami. Site Hakime Mehr. Diakses tanggal 13 Februari 2018.
  • Khomeini, Ruhullah Musawi. Resale-e Taudhīh al-Masā'il. Riset Muslim Qalipur Gilani. Cet 1, 1426 H.
  • Khomeini, Ruhullah Musawi. Tahrīr al-Wasīlah. Penerjemah Ali Salami. Qom: Daftar-e Entesyarat-e Eslami Wabaste Be Jame'e-e Mudarrisin Hauze Ilmiyye-e Qom. Cet 21, 1425 H.
  • Muassese-e Dayirah al-Ma'arif Feqh-e Farsi. Farhangg-e Feqh Mutabeq-e Mazhab-e Ahl-e Beit (a.s), Qom: Muassese-e Dayirah al-Ma'arif al-Islami, 1387 HS/2009.
  • Najafi, Muhammad Hassan. Jawāhir al-Kalām Fī Syarh Syarā'i' al-Islām. Editor Abbas Quchani/Ali Akhundi. Beirut: Dar Ihya' at-Turats al-'Arabi. Cet 7, 1401 H.
  • Qanun-e Nezarat-e Syar'i Bar Zebh Wa Sheid. Site Majlis.ir. Diakses tanggal 13 Februari 2018.
  • Sabzawari, Abdul Ali. Muhadzzab al-Ahkām Fī Bayān al-Halāl wa al-Harām. Qom: Dar at-Tafsir, 1413 H.