Kaburi la Abul-Fadhl al-Abbas (as)
Kaburi la Abul-Fadhl al-Abbas (a.s) (Kiarabu: حرم العباس (ع)) ni mahali alipozikwa Abbas bin Ali bin Abi Talib (a.s) katika mji wa Karbala, Iraq. Eneo hili ni miongoni mwa maeneo matakatifu na pia ni maeneo yanayotembelewa na Waislamu wa Kishia ambao huenda hapo kwa ajili ya kufanya ziara. Haram ya Abbas ipo kaskazini mashariki mwa Haram ya Imam Hussein (a.s) na umbali uliopo baina ya Haram mbili hizi unafahamika kama Baina al-Haramein. Historia ya Haram hii inarejea nyuma katika zama za Aal Buweih. Hata hivyo ilipanuliwa na kufanyiwa marekebisho katika zama za Safawi na Qajar. Abul Fadhl a-Abbas ni kaka wa Imamu Hussein (a.s) na aliyekuwa mbeba bendera ya jeshi lake Karbala ambaye aliuawa shahidi Siku ya Ashura mwaka 61 Hijiria katika vita na Jeshi la Omar bin Sa’d.
Hadhrat Abbas
- Makala Asili: Hadhrat Abbas (a.s)
Hadhrat Abbas ni mtoto wa Imam Ali (a.s) na Ummul-Banina. Aliuawa shahidi katika tukio la Karbala mwaka 61 Hijiria. Katika tukio la Karbala, Abbas alikuwa kamanda na mbeba bendera wa jeshi la Imam Hussein (a.s).[1] Abbas ndiye aliyewaletea maji Imamu Hussein pamoja na wafuasi wake. Siku ya Ashura alielekea katika mto Alqama kwa ajili ya kuleta maji na Jeshi la Omar bin Sa’d likamuua shahidi.[2] Alizikwa hapo hapo alipouwa shahidi.[3] Baadaye kaburi lake likajengewa na kuwa sehemu ya kufanyia ziara ambapo hii leo ni mashuhuri kwa jina la Haram ya Hadhrat Abbas. Haram ya Aabbas ipo Karbala umbali wa takribani mita 300 kaskazini mashariki mwa Haram ya Imam Hussein (a.s).[4] Umbali uliopo baina ya Haram mbili hizi unafahamika kama Baina al-Haramein.
Historia
Kuna taarifa chache mno za kihistoria kuhusiana na jengo la kwanza la Haram ya Hadhrat Abbas.[5] Baadhi ya waandishi wanaamini kwamba, historia ya Haram ya Imam Hussein (a.s) na Abul-Fadh al-Abbas haitenganishiki, na kwamba; kila tukio lililoripotiwa kufanyika kwa ajili ya Haram ya Imam Hussein (a.s) kama ujenzi, ukarabati, ubomoaji na upanuzi basi ulihusisha pia Haram ya Abbas.[6] Katika tovuti yenye mfungamano na Haram ya Abbas, kuna historia ya Haram ya Imam Hussein kama vile jengo la kwanza katika zama za Mukhtar al-Thaqafi, kubomolewa katika zama za Harun, kujadidishwa jengo katika zama za Maamun na kubomolewa kwake kwa amri ya Mutawakkil Abbasi mwaka 236 Hijria.[7] Haya ni baadhi ya mambo yaliyotajwa katika tovuti hiyo kuhusiana na Haram ya Abbas.[8]
Baadhi ya waandishi wanasema, historia ya kujengwa jengo la kwanza la Haram ya Abbas inafikia katika karne ya Pili Hijiria.[9] Jengo hili lilibomolewa mwaka 170 Hijria kwa amri ya Harun Rashid.[10] Wametumia hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kama hoja ambapo ndani yake inaashiriwa kuweko kivuli katika kaburi la Hadhrat Abbas.[11]
Kujengwa Jengo la Zama za Aal-Buweih
Mwaka 371 Hijiria na katika zama na kipindi cha Aal-Buweih kulijengwa jengo juu ya kaburi la Hadhrat Abbas kwa amri ya Azdu al-Dawla al-Daylami.[12]
Kupanuliwa Jengo katika Zama za Safawi
Katika zama za SafaWi Haram ya Hadhrat Abbas ilipanuliwa. Shah Tahmasb mwaka 1032 alitoa amri ya kupambwa kuba la Haram na kaburi la Abul-Fadhl kujengewa dharih. Kadhalika katika zama zake kulijengwa kumbi za Haram.[13]
Ukarabati katika Duru Mbalimbali
Haram ya Hadhrat Abbas ilifanyiwa marekebisho na ukarabati katika duru mbalimbali. Wafalme ambao walifanyia ukarabati Haram ya Imam Hussein (a.s) walifanya hivyo pia kwa Haram ya Hadhrat Abbas.[14] Katika zama za utawala wa Nader Shah kulifanyiwa ukarabati wa kaburi na kumbi la Haram na katika zama za Abdul Majid Khan Mahmoud Othman, Haram hiyo ilifanyiwa ukarabati na katika zama za Qajar kuba lake lilikarabatiwa.[15]
Shambulio la Mawahabi na Kubomolewa Haram
Mwaka 1216 Hijiria, Saud bin Abdul-Aziz alishambulia Karbala. Wanajeshi wake walibomoa Haram ya Hadhrat Abbas na kuchukua mali zake. Baada ya shambulio la Mawahabi, Haram hiyo ikakarabatiwa kwa amri ya Fat'h Ali Shah Qajar.[16] Katika Intifadha ya Shaabaniya mwaka 1411 Hijiria pia, shambulio la vikosi vya chama cha Baath dhidi ya mji wa Karbala ulileta uharibifu pia dhidi ya Haram ya Abbas (a.s).[17]
Usanifu Majengo
Haram ya Hadhrat Abbas ina umbo la mstatili na kaburi lipo katikati ya Haram hiyo. Haram hiyo ni mjumuiko wa dharih (eneo la ndani linalozunguka kaburi) kumbi, uwanda, mnara na kuba.[18] chini ya jengo la Haram kuna korido ambayo njia yake ya kuingilia inaelekea upande wa kaburi la Hadhrat Abbas (a.s).[19] Katika tovuti yenye mfungamano na Haram, ukubwa wa haram hiyo umetajwa kuwa ni mita mraba 10,973.[20]
Dharih (Eneo la ndani linalozunguka kaburi)
Dharih (eneo la ndani linalozunguka kaburi) limejengwa kwa dhahabu na fedha na lipo juu ya kaburi. Kuanzia zama za Safawi, dharih iliwekwa juu ya kaburi la Abbas,[21] na katika zama za baada yake lilikarabatiwa na kubadilishwa. Kwa amri ya Muhammad Shah Qajar mwaka 1236 Hijria kulijengwa dharih ya fedha juu ya kaburi la Abbas.[22] Mwaka 1385 Hijiria kwa himaya na uungaji mkono wa Sayyid Mohsin Hakim dharih ya Haram ikabadilishwa.[23] Dharih hii ilijengwa na kutengenezewa nchini Iran na ndani yake kulitumika kilo 2,000 za fedha na kilo 40 za dhahabu.[24] Mwaka 1395 Hijiria Shamsia pia, dharih ya Haram hiyo ilibadilishwa.[25] Dharih ya sasa imetengenezwa kutoka na dhahabu na fedha na utengenezaji wake uliofanyikia nchini Iraq ulichukua muda wa takribani miaka 5.[26]
Shakhsia Mashuhuri Waliozikwa katika Haram ya Abbas
- Makala Asili: Orodha ya waliozikwa katika Haram ya Hadhrat Abbas
Baadhi ya waliozikwa katika Haram ya Hadhrat Abbas ni:
- Ali bin Zaynul Abidin Parchini Yazdi (aliaga dunia 1333 Hijria), alikuwa alimu wa Kishia na mwandishi wa kitabu cha Ilzam al-Nasib kuhusiana na Imam wa Zama (a.t.f.s).
- Muhammad Rashid Jalabi Swafi.
- Sayyid Kadhim Bahbahani.
- Hussein Halawi.[27]
- Sayyid Muhsin Seyyid Muhammad Ali Aal Ta'meh.
- Abdul Jawad Kelidar.
- Sayyid Muhammad bin Mohsin Zanjani (aliaga dunia 1355 Hijria).
- Sayyid Abdallah Kashmiri.
- Sheikh Mulla Ali Yazdi mashuhuri kwa jina la Sibawayh.
- Sheikh Kadhim al-Har.[28]
Rejea
- ↑ Ibnu Shahr Ashub, Manāqib Āli Abi Talib, juz. 4, uk. 108.
- ↑ Ibnu Shahr Ashub, Manāqib Āli Abi Talib, 1379 H, juz. 4, uk. 108; Qurashi, Hayat al-Imam al-Husain as, juz. 3, uk. 265-268.
- ↑ Ma'aruf Hassani, Sirah al-Aimmah al-Ithna-Ashar (a.s), juz. 3, uk. 97; Zujaji Kashani, Saqaye Karbala, uk. 135.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 261.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 261.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 261.
- ↑ Tabari, Tarikh al-Umam wa al-Muluk, juz. 9, uk. 185.
- ↑ [https://alkafeel.net/history/ Marahil Binai wa Imar wa Tat-wir al-Itba al-Abbasiyyah al-Muqadassah.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 72.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 74.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 72.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 263.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 263.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 261.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 263-264.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, uk. 263.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Intifadhat Shaabaniya Fi Karbala, 1433 AH, uk. 47.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 262.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 303.
- ↑ [https://alkafeel.net/description/ Wasfu al-Itba al-Muqadassah
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 263.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 263.
- ↑ Tazama: Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 262.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 265-267.
- ↑ Dharih Jadid Hadhrat Abbas (a.s) Rasman Iftitah Shud, aTovuti ya Shafaqna.
- ↑ A'az Marhale Qalmizani Dharih Jadid Hadhrat Abbas (a.s), Khabarigozari Fars.
- ↑ Alu-Ta'ameh, Tarikh Marqad al-Hussein wa al-Abbas, 1416 AH, uk. 271.
- ↑ Muqaddas, Ihsan, Rahnama-e Amākin Ziarati wa Siyahati Dar Iraq, 238-239.
Vyanzo
- Ibnu Shahr Ashub, Muhammad bin Ali, Manāqib Āli Abi Talib, Qom: Allamah, 1379 H.
- Alu Shabib, Sayyid Tahsin, Marqad al-Imam al-Hussein (a.s) Qom: Dar al-Taba'ah, 1421 H.
- Alu Ta'ameh, Salman Hadi, al-Intifadha al-Sha'baniyyah Fi Karbala, Qom: Kitabkhaneh Takhassusi Tarikh Islam wa Iran, 1433 H.
- Tabari, Muhammad bin Jarir, Tarikh al-Umam wa al-Muluk, Mhariri: Muhammad Abul Fadhl Ibrahim. Beirut: Dar al-Turath, 1378 H/1967.
- Qurashi, Baqir Sharif, Hayat al-Imam al-Hussein (a.s), Qom: Madrasat Ilmiah Irwani, 1413 H.
- Alu-Ta'ameh, Salman Hadi, Tarikh Marqa al-Hussein wa al-Abbas, Beirut: Muassasah al-A'lami lil Mathbu'at, 1416 H/ 1996 .
- Ma'aruf Hassani, Hashim, Sirah al-Aimmah al-Ithna Ashar (a.s), Najaf: al-Maktabah al-Haidariyyah, 1382 H.
- Majalah Akhbar Shi'iyan, no. 57, Murdad 1389 HS.
- Muqaddas, Ihsan, Rahnama-e Amākin Ziarati wa Siyahati Dar Iraq, Tehran: Mash'ar, 1388 HS.
- Sheikh Mufid, Muhammad bin Muhammad, Kitab al-Mazar, Mhariri: Muhammad Baqir Abthahi, konggoreh Jahani Hezareh Sheikh Mufid, 1413 H.