Istilamu Al-Hajar

Kutoka wikishia
Istilamu Al-Hajar

Istilamu Al-Hajar (Kiarabu: اِستِلام الحَجَر), Istilahi ya Istilamu Al-Hajar inarejelea kitendo cha kugusa Jiwe Jeusi na kulibusu kwa nia ya kutafuta baraka. Kitendo hichi cha kugusa na kubusu jiwe hilo ni miongoni mwa matendo yaliyo sisitizwa katika vyanzo vya Hadithi za Shia pamoja na Sunni, huku wanazuoni wakiamini kuwa ni miongoni mwa yaliyo pendekezwa (sunna). Moja ya Hadithi zinazopokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), inaeleza kwamba; falsafa ya kitendo hiki ni kushuhudia kwa Jiwe hilo Jeusi Siku ya Kiyama juu ushikamanivu wa imani ya mtu katika kumuamini Mwenye Ezi Mungu. Ruhusa ya kugusa na kubusu Jiwe Jeusi “Hajaru al-Aswad”, inachukuliwa kama ni idhini ithibitishayo uhalali wa katafuta baraka kutoka katika vitu maalumu vinavyosadikiwa kuwa na hadhi maalumu mbile ya Mwenye Ezi Mungu.

Istilahi ya Istilamu Al-Hajar

Kilugha ibara ya "istilamu al-Hajar" inarejelea kitendo cha kugusa Jiwe Jeusi (Hajar al-Aswad) na kulibusu kwa nia ya kutafuta baraka.[1] Kifiqhi ibara hii huwa na maana zaidi ya moja, ikiwemo kugusa Jiwe Jeusi, kugusa Kaaba pamoja na arkanu al-Kaaba ambazo ni pembe nne za Kaaba (pembe ya mashariki, magharibi, kaskazini na kusini). [2] Maana hasa ya "istilamu al-Hajar" ni kugusa Jiwe Jeusi kwa njia ya kupangusa au kupitisha mkono wako juu yake au kulibusu jiwe hilo. [3]

Hajaru Al-Aswad

Makala asili: Hajaru Al-Aswad

Hajaru Al-Aswad ni jiwe takatifu mbele ya Waislamu, nalo lipo kwenye pembe (kona) ya mashariki Kaaba iliomo ndani ya msikiti mtukufu wa Makka. [4] Jiwe hili ni lenye rangi nyeusi inayo elemea kwenye wekundu. [5] Jiwe hili ni lenye historia refu mno, ambalo hata kabla ya Usilamu pia lilikuwa ni jiwe lenye heshima maalumu mbele ya jamii mbali mbali zilizotanguli kabla yetu [6] Hakuna ishara ya moja kwa moja kuhusiana na jiwe hili ndani ya Aya mbali mbali za Qur'ani, [7] ila kwa mujibu wa moja ya Riwaya kutoka kwa Imamu Ali (a.s), ni kwamba; “Hajaru Al-Aswad” ni moja ya Aya za wazi zilizotajwa katika Aya izungumziayo Aya za Mungu zilizomo ndani ya mji wa Makka. [9]

Hukumu za Fiq-hi Juu ya Kugusa Hajaru Al-Aswad

Hadithi zilizomo katika vyanzo vya Shia na Sunni, vinasisitizo juu ya umuhimu wa kugusa na kulibusu Jiwe Jeusi (Hajar al-Aswad). [10] Kulingana na Hadithi zilizomo ndani ya vitabu vya Wasa'il al-Shia na Sahih Bukhari, Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na tabia ya kugusa na kulibusu Jiwe Jeusi wakati akiwa katika ibada zake za kutufu. [11] Aidha, kwa mujibu wa moja ripoti za Kulayni, Imamu Swadiq (a.s) aliwahimiza Waislamu kugusa na kulibusu Jiwe Jeusi wakati wa kutufu kwao. [12]

Moja ya mambo yaliyotajwa Hadithi kuhusiniana na amali ya kugusa na kubusu Jiwe Jeusi, ni kusoma dua wakati wa kuligusa au kulibusi jiwe hilo. Kulingana na Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), iwapo mtu hataweza kulibusu Hajaru Al-Aswad kutokana na msongomano wa watu, basi yatosha kuligusa tu jiwe hilo. Na kama mtu hataweza kulifiki kutokana na msongomano uliopo, basi yatosha kuliashiria na kusoma dua maalumu isomwayo wakati wa kugusa Hajaru Al-Aswad. [13] Mashia pamoja na Masunni wato kwa pamoja wamelihisabu tenda la kugusa Hajaru Al-Aswad, kama ni miongoni mwa matendo ya sunna, fatwa hii imejiri kulingana na Hadithi tulizo ziashiria kuhusiana na amali hiyo. [14] Miongoni mwa mifano ya fatwa za wanazuoni mbali mbali, inapatikana katika fafanuzi za matendo ya sunna za kutufu zilizo elezewa na Muhaqqiq Hilli, ambapo kugusa na kubusu Hajaru Al-Aswad, ni moja ya amali za mustahabu zilizo orodheshwa na Muhaqqiq Hilli katika fafanuzi hizo. [15]

Ingawa mawahabi wa kisalafi hawakubaliana na uhalali wa wa kushikana kumbusu vitu vitakatifu mbali mbali, na kuviona vitendo kama ni vitendo shirki, [16] ila wao wanaunga mkono amali ya “istilamu al-Hajar”, pamoja na kumbusu Jiwe Jeusi. [17] Hii inathibitisha kwamba, licha ya mitazamo yao kali dhidi ya vitendo vya kuomba baraka kwa kutumia vitu, bado wanatambua umuhimu wa baadhi ya vitendo hivyo kama ni sehemu ya ibada ya Kiislamu. Istilamu al-Hajar ni mojawapo ya vielelezo vinavyotumiwa kuthibitisha uhalali wa kutafuta baraka na kuhishimu vitu vitakatifu. [18]

Kuhusiana na hali ya kuwepo kwa msongamano wa watu wakati wa kutufu, Fat’wa za mafaqihi zinaeleza wazi kwamba endapo idadi ya watu itakuwa ni kubwa kiasi cha kusababisha wanaume na wanawake kugusana miili yao, hapo hapatakuwa na haja ya “istilamu al-Hajar”, bali katika hali hiyo haitajuzu mtu kwenda kugusa jiwe hilo jeusi. Hii ni kwa sababu ya kuheshimu mipaka ya maadili ya Kiislamu ambayo inazingatia kujiepusha na hali yoyote inayoweza kusababisha mikanganyiko au machafuko ya kimaadili katika mazingira ya ibada. Hivyo, licha ya umuhimu wa “istilamu al-Hajar”, ila bado mipaka ya kimaadili inaendelea kupewa kipau mbele katika ibada hiyo. [19]

Falsafa ya Kugusa Hajaru Al-Aswad

Ukaririfu wa Ahadi za Waja kwa Mola Wao

Katika kitabu cha Al-Kafi, kuna moja ya Hadithi inayoelezea na kubainisha falsafa ya kugusa na kubusu Jiwe Jeusi. Kwa mujibu wa habari zilizo nukuliwa na Kulayni, Imamu Swadiq (a.s), alipokuwa akitoa maji bu juu ya moja ya maswali juu ya sababu na falsafa ya kugusa na kubusu jiwe hilo, alifafanua kwa kusema kwamba: "Kugusa Jiwe Jeusi kunarejelea lile tukio la Mwenye Ezi Mungu kuweka ahadi na viumbe vyake, ambapo Aliliteremsha Jiwe Jeusi kutoka Peponi na kuliagiza lihifadhi ahadi za waja wa Mwenye Ezi Mungu ndani yake. Hivyo, kila mtu anayelinda ahadi yake kwa uaminifu, Jiwe Jeusi litatoa ushahidi kwa niaba yake kwamba hakuvunja ahadi hiyo na alibaki mwaminifu kwayo." [20]

Kwa maana hiyo; kugusa na kubusu Jiwe Jeusi, kunawakilisha uwepo wa kati ya mja na ahadi hiyo iliyowekwa na Mola Muumba kwa viumbe vyake. Kwa kugusa Jiwe Jeusi, ni kumbukumbu inayo wanakumbushwa ahadi zao, na kuwafanfa wajitahidi kuishi kwa mujibu wa maadili na kanuni za Kiislamu, wakitarajia ushuhuda wa Jiwe Jeusi kuwa ithibati ya uaminifu wao mbele ya Mwenye Ezi Mungu katika Siku ya Mwisho.

Ushuhuda wa Hajaru Al-Asawad Siku ya Kiama

Imam Ali (a.s) alisema: «Mwenyezi Mungu atalifufu Jiwe hili Siku ya Kiyama, ambapo litakuwa na ulimi na midomo wa kusema, na litatoa ushuhuda kwa wale waliohifadhi ahadi yao. Jiwe hili ni sawa na mkono wa kuume wa Mwenye Ezi Mungu, ambao viumbe wake hutia hurudia ahadi za kumtii Mola wao kwa kuweka mkono wao juu ya mkono huo». [21]

Rejea

Vyanzo