Nenda kwa yaliyomo

Baraka

Kutoka wikishia

Baraka (Kiarabu: البركة) ni neema na ziada za kheri za Mwenye Ezi Mungu kwa viumbe wake. Neno hili limetumika mara tatu katika Qur'an, na limetumika katika mfumo wa wingi, na hakuna mahala katika Qur’an lilipotumika neno hili kwa mfumo wa umoja. Kwa kuwa katika Qur'an, daima baraka imeonekana kuwemo ndani ya mikono ya Mungu peke yake, kwa hiyo upatikanaji wake hauwezi kuwa nje ya mikono ya Mwenye Ezi Mungu.

Kuna matendo kadhaa ambayo hupelekea kupatikana kwa baraka katika maisha ya mwanadamu, mfano wa hayo ni; kuwa na imani, taqwa, istighfar, dhikr, utiifu kwa Mungu, kutenda haki na kuwa na tabia njema. Matendo haya yametambulika kuwa ni sababu za kuvuta baraka za Mwenye Ezi Mungu, na kwa upande mwingine, baadhi ya matendo ya binadamu, ikiwa ni pamoja na kutenda dhambi na kuto amrisha mema na kutokataza maovu, yamezingatiwa kuwa ni vizuizi vya baraka za Mwenye Ezi Mungu.

Baadhi ya viumbe vya Mungu vimetajwa kuwa ni miongoni mwa madhihiriko ya baraka za Mwenye Ezi Mungu, miongoni mwao ni; Nabii Nuhu (a.s), watu wema katika jamii na Qur'an Tukufu. Na kwa upande wa nyakati ni kama vile; Laylatul Qadr na mwezi wa Ramadhani. Pia kuna maeneo ambayo ni madhihiriko ya baraka za Mola, nayo ni kama vile; Makka, na Madina. Na kwa upande wa matukio ni kama vile mvua na mfano wake.

Welewa wa dhana

Baraka ina maana ya ongezeko la kheri. [1] Allamah Tabatabai akifafanua maana ya neno baraka, amesema kwamba; maana ya baraka ni uwepo wa kheri nyingi katika kitu fulani, kama vile uwepo wa maji kwenye bwawa. [2] Pia kwa maoni yake neno hili ni neno linalobema ndani ya welewa tofauti kulingana matumizi yake, kwa msingi huo, basi, uwepo wa baraka katika kitu fulani ni tofauti na uwepo wake katika kitu chengine. Kwa mfano, baraka katika kizazi ni wingi wa watoto, lakini baraka katika wakati ni upana wa kazi za mwanadamu iliyoweza kutenedeka vyema katika wakati fulani, ambapo kwa wakati mdogo tu huweza kupatikana mafanikio makubwa ndani yake. [3] Kwa hiyo baraka ya wakati, si wingi wa wakati, bali faida kubwa inayo weza kupatikana katika kiwango fulani cha wakati.

Neno baraka katika istilahi za Qur'ani Tukufu, linatumika katika kuashiria neema na wingi wa kheri kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. [4] Kwa msingi huu, baraka za mbinguni zimetafsiriwa kuwa ni wingi wa mvua, na baraka za ardhini zimetafsiriwa kuwani wingi wa mimea na matunda. [5] Neno tabaaraka (تَبَارَكَ) pia linatokana na neno baraka na lina maana ya baraka zisizo na kifani. Neno tabaaraka (تَبَارَكَ) katika Qur'ani Tukufu, aghalabu hutumika kwa ajili ya Mwenye Ezi Mungu, na ni nadra neno hili kutumika kwa asiye kuwa Mwenye Ezi Mungu. [6] Ila visewe vya neno hili vimeonekana kutumika kwa ajili ya wanadamu, matukio na maeneo mahususi. [7]

Neno baraka katika Qur'ani Tukufu limetajwa katika Aya tatu likiwa katika mfumo wa wingi, [8] ambapo baadhi ya wanazuoni wamelifasiri neno hili katika Aya hizo kwa maana ya kuashiria ishara ya wingi wa baraka za Mwenyezi Mungu. [9] Visawe vyengine vya neno hili vimetumika mara 32 ndani ya Qur’ani Tukufu, navyo; baarak (بارک) [10], baarkna (بارکنا) [11], buurik (بورک) [12], mubarakun (مبارک) [13], mubaarakan (مبارکا) [14], "Mubaarakatun" (مبارکة) [15], na tabaarak (تبارک) [16]. Mara zote visawe vya neno bark katika Qur'ani, vimehusishwa na Mwenyezi Mungu; uhusishwaji huu umechukuliwa kama ushahidi ya kwamba ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye mamalaka ya kuleta baraka. [17] Neno baraka pia linapatikana katika Hadithi za Ahlul-Bait (a.s), na linachukuliwa kuwa mojawapo ya majeshi ya akili na kinyume chake ni "maḥqun" [Maelezo 1] inayo chukuliwa kuwa ni miongoni mwa majeshi la ujinga. Hassan Mustafawiy [18] amelifasiri neno "mahqun" kwa maana ya kupungua kwa kitu taratibu au hatua kwa hatua, hadi kumalizika kabisa na kutoweka. [19] Mbali ya neno Baraka kupatikana ndani ya Qur'ani Tukufu na maandishi mabli mbali ya Kiislamu, pia dhana hii inapatikana ndani ya vitabu vyengine vya mbinguni vilivyokuja kabla ya Qur’ani. Miongoni mwa yaliokuja kuhusiana na mada hii katika hivyo ni; Baraka za Mwenye Ezi Mungu kwa manabii wake, na Baraka za manabii na makuhani kwa katika kuwabariki watu wengine. 20] Kuna kiasi cha maneno 400 katika Agano la Kale yanayotokana na mizizi ya neno baraka, pia kuna idadi kadhaa ya maneno hayo ndani ya Agano Jipya, mfano wa maneno ndani ya Maagano hayo mawili ni; baraka, barakha na baraakhaahu, na yote kwa pamoja ni yenye maana ya baraka. [21]

Sababu za Baraka katika Utamaduni wa Kiislamu

Katika utamaduni wa Kiislamu, suala la wanadamu kupata baraka linahusishwa moja kwa moja na matendo, tabia, na maneno yao. Qur'an Tukufu pamoja na Hadithi za Maimamu Watakatifu, limeihusisha na matendo kadhaa ya wanadamu, kama vile; imani na taqwa, istighfar, shukurani, utiifu, dhikri ya Mwenyezi Mungu, [22] kutenda haki, [23] kuamka alfajiri, [24] tabia njema, [25] kutoa salamu, [26] kutoa sadaka, [27] kuzingatia usafi, [28] kupunguza gharama za ndoa, [29] kuunga udugu, [30] insafu katika biashara, [31] ukarimu kwa majirani, [32] kuwafariji ndugu wa kidini, [33] na kufunga saumu na kula daku. [34] Yote hayo kwa jumla yanahisabiwa kuwa ni baadhi ya sababu za kushuka kwa baraka.

Imani na Taqwa

Qur'an Tukufu katika Aya ya 96 ya Surat Al-A'raf, imefungamanisha suala la kushuka kwa baraka za mbinguni na ardhini na wingi wa watu wenye imani na taqwa katika ardhi au miji fulani. Kwa mujibu wa tafsiri za Qur'an kuhusu Aya hii, imani na taqwa ya watu wachache, haiwezi kuhakikisha kushuka kwa baraka za mbinguni kwa wote. [35]

Kuomba maghufira

Katika Aya ya 52 ya Surat Huud na Aya ya 10 hadi 13 ya Surat Nuuh, Mwenyezi Mungu anaeleza kwamba kuteremka kwa baraka zake, ikiwa ni pamoja na baraka za mvua, kunategemea, kunategemea kuto wepo kwa vikwazo vinavyo zuia baraka hizo. Kwa vile dhambi ni mojawapo ya vikwazo vya kuteremka kwa baraka, kwa hiyo istighfar za waja ni moja wapo ya njia za kupata rehema ya Mwenyezi Mungu. [36]

Kulingana na Qur'an Tukufu, Mwenyezi Mungu anaongeza neema zake kutokana na shukrani za mwanadamu, na kinyume chake, kuzikifuru neema ni moja wapo ya sababu za kuongezeka kwa adhabu. Imamu Ali (a.s) ameeleza ya kwamba; istighfar ni moja ya njia zinazo pelekea kudumu kwa riziki na rehema za Mwenyezi Mungu. [37]

Vikwazo

Kwa mujibu wa maandiko na utamaduni wa Kiislamu, kuwa na tabia ya matendo na maneno fulani, huzuia mtu kupata baraka za Mungu, na miongoni mwayo; Kutenda dhambi na uasi, kuto amrisha mema na kukataza maovu, na kutomkumbuka Mwenye Ezi Mungu, [39] ni miongoni mwa mambo yanayo zuia kushuka kwa baraka za Mwenye Ezi Mungu, ambayo hata ndani ya Qur’an na Hadithi yametajwa kuwa ni vikwazo vya kupata baraka.

Kutenda dhambi na kutotii

Suala la kutenda dhambi na kutotii amri za Allah, yamehisabiwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayoondoa baraka katika kwa mali, umri, na maisha ya mwanadamu. Wafasiri wa Qur’ani Tukufu, katika tafsiri ya Aya ya 96 ya Surat A’raf, wamesema kwamba; hatima ya watendaji dhambi na wanaowakanusha manabii, kuachana na adhabu kali ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiama, watu wao hunyimwa baraka za mbinguni pamoja na za ardhini duniani humu. [40]

Miongoni mwa amali zilizozingatiwa kuwa ni miongoni mwa amali zinazopelekea mwanadamu kunyimwa baraka ni pamoja na: kuacha sala, [41] kupunja katika mauzo mauzo yake, [42] kuto toa zaka, [43] ubadhirifu (israfu), [44] usaliti, [45] wizi, kunywa vileo, umalaya [46] na kuapa kwa uwongo katika shughuli za kibiashara. [47]

Kuto amrisha mema na kukataza maovu

Kuto amrisha ya mema na kukataza maovu ni mojawapo ya vizuizi vya kuteremka baraka. Kulingana na Hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kwamba; baraka za Mwenyezi Mungu zitaendelea kwa muda mrefu iwapo tu watu waaamrisha mema na kukataza maovu, na watasaidiana katika mambo kheri. Lakini ikiwa wataacha kufanya hivyo, Mwenye Ezi Mungu atawazuilia baraka zake. [48]

Mifano hai ya baraka

Kulingana na Aya za Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu amewafanya baadhi ya viumbe wake kuwa ni mifano hai na ishara za baraka zake; miongoni mwa mifano hiyo hai ni; baadhi ya manabii na waumini wema, Qur'ani Tukufu, baadhi ya nyakati, baadhi ya maeneo, na pia baadhi madhihiriko ya mambo maalumu katika ulimwengu huu wa kimaada. Kati ya baraka za Qur'ani Tukufu, [49] ni mwongozo unaopatikana ndani yake. [50]

Mitume na watu wengine waliobarikiwa katika Qur'an ni pamoja na Nuhu (a.s) na masahaba zake katika alio kuwa pamoja nao katika jahazi, Ibrahim na kizazi chake, Isma'il na Isaka, Mussa (a.s), Isa (a.s), Mtume Muhammad (s.a.w.w) na waumini pamoja na wema. [55]

Baadhi ya maeneo yenye baka yaliotajwa ndani ya Qur’ani, ni kama vile Makka, Sham, [58] Baitu al-Muqaddas na Wadi al-Tuur.

Usiku wa Qadr nao pia ni usiku wenye baraka, kwani ndani yake, dua huwa ni zenye kutakabaliwa, pia Mola husamehe dhambi za waja wake (iwapo watatubia ndani ya usiku huo), pia Qur’ani imeteremshwa ndani ya usiku huo. Baadhi ya matokeo ya asili yanayo tokea katika ulimwengu wa kimaada pia nayo ni matokeo ya baraka, miongoni mwayo ni; kama vile mvua, ambayo katika Qur'an yameitwa "maji yenye baraka". [63]

Maelezo

  1.  الْبَرَكَةُ وَ ضِدَّهَا الْمَحْقَ‌

Rejea

Vyanzo

  • Dihkhudā, ʿAlī Akbar. Amthāl wa ḥikam. Tehran: Amīr Kabīr, 1383 Sh.
  • Fakhr al-Dīn al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUamr al-. Mafātīḥ al-ghayb. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Ibn Ḥanbal, Aḥmad. Musnad. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1416 AH.
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Falāḥ al-sāʾil wa najāḥ al-masāʾil. Qom: Būstān-i kitāb, 1406 AH.
  • Karīmī, Maḥmūd. 1381 Sh. "Barkat." Dāʾirat al-Maʿārif Buzurg-i Islāmī 11:744-745.
  • Kūfī al-Ahwāzī, Ḥusayn b. Saʿīd al-. Al-Zuhd. Edited by Ghulāmriḍā ʿIrfānīyān Yazdī. Qom: al-Maṭbaʿa al-ʿIlmīyya, 1409 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Laythī al-Wāsiṭī, ʿAlī b. Muḥammad al-. ʿUyūn al-ḥikam wa l-mawāʿiẓ. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1376 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1371 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. al-Muqniʿa. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Muṣṭafawī, Ḥasan. Al-Taḥqīq fī kalimāt al-Qurʾān. Tehran: Wizārat-i Farhang wa Irshād-i Islāmī, 1368 Sh.
  • Nasafī, Muḥammad b. Muḥammad Riḍā. Tafsīr kanz al-daqāʾiq wa baḥr al-gharāʾib. Edited by Ḥusayn Dargāhī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād, 1368 Sh.
  • Qidamī, Ghulāmriḍā. 1382 Sh. "Barkat: piydāyish, pāydārī wa fuzūnī khayr dar padīdahā az sūy-i khudāwand." Dāʾirat al-Maʿārif Qurʾān-i Karīm 5:484-486.
  • Qurṭubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Tehran: Nāṣir Khusru, 1364 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿIlal al-sharāʾiʿ. Qom: Kitābfurūshī Dāwarī, 1385 Sh.
  • Ṭabarī, Mūhammad b. Jarīr al-. Jāmiʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1412 AH.
  • Ṭabāṭabāyī, Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān. Tehran: Nāṣir Khusru, 1372 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Aḥmad Ḥabīb al-ʿĀmilī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1383 AH.