Imani ya mababu za Mtume (s.a.w.w.)

Kutoka wikishia

Imani ya mababu za Mtume (Kiarabu: إيمان أجداد النبي (ص)) inaashiria kumuabudu Mungu mmoja baba na mababu wa Mtume (s.a.w.w). Wanachuoni wa Kishia na baadhi ya wanazuoni wa Kisuni wanaamini kwamba, mababu wote wa Mtume (s.a.w.w) walikuwa wakiamini na kumuabudu Mungu mmoja. Kwa mtazamo wa wale wanaoamini imani ya mababu Mtume (s.a.w.w) ni kwamba, Aya na hadithi kadhaa zinaeleza kuwa Mtume (s.a.w.w) alizaliwa kutoka kwa mababa wasiokuwa washirikina, na kwa hiyo hawamtambui Azar ambaye alikuwa mshirikina kuwa ni baba yake Ibrahim.

Umuhimu na Nafasi

Tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) au kuwa washirikina mababu za Mtume (s.a.w.w) ni miongoni mwa masuala ya hitilafu baina ya madhehebu za Kiislamu.[1] Vitabu na makala kadhaa zimeandikwa katika uwanja huu, na sehemu za vitabu zimetengwa kwa ajili ya mjadala huu.[2] Jalaluddin Suyuti (aliyefariki dunia: 911 H) mmoja wa wanazuoni mashuhuri ameandika vitabu kuhusiana na jambo hili.[3]

Je, Mababu Wote wa Mtume Walikuwa Watu wa Tawhidi?

Sheikh Saduq (aliyefariki: 380 Hijiria) anasema kwamba, imani yetu ni kwamba, mababu wa Mtume kuanzia Adam hadi Abdullah wote walikuwa Waislamu (kwa maana ya jumla, au ile maana ya kunyenyekea na kusalimu amri kwa Mwenyezi Mungu).[4] Sheikh Mufid (aliyefariki dunia 413 H) anasema kuwa, watu wote wa haki wamefikia itikadi moja kwamba, mababa wa Mtume mpaka kwa Nabii Adam wote walikuwa watu wa tawhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu na walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu.[5] Alousi (aliyefariki: 1270 H), mmoja wa wafasiri wa Kisuni, amekanusha na kuinasibisha imani hii na kuihesabu kuwa ni mahasusi kwa Shia na anasema kwamba, Fakhr Razi, ambaye anahusisha imani hii na Mashia hajafanya utafiti wa kutosha.[6]

Nasir al-Din Tusi (aliyefariki: 672 H) na Allama Hilli (aliyefariki: 726 Hijiria) miongoni mwa wanateolojia wa Shia pia wanaamini kwamba baba za Mitume wanapaswa kuwa mbali na aina yoyote ya uchafu. Hilo limebainishwa katika kitabu cha Tajrid al-I’tiqad na vitabu vilivyoandikwa kusherehesha kitabu hiki.[7] Pia, Alauddin Qaushachi (aliyefariki: 879 H), mwanateolojia wa madhehebu ya Ash'ari, katika maelezo na ufafanuzi wake wa kitabu cha tajrid al-i'tiqad, amesema kwamba mababu wa Mitume hawapaswi kuchafuliwa na ushirikina.[8]

Hoja za Kuwa Wanatawhidi Mababu za Mtume

Aya za Qur’an Zinabainisha Juu ya Imani ya Mababu za Mtume (s.a.w.w):

  • Aya ya Taqallubaka fi al-Sajidin (Na mageuko yako kati ya wanao sujudu): Fakhrurazi, mmoja wa maulamaa wa Kisuni anasema: Rafidha (Mashia) wanatumia Aya hii pia kwa ajili ya kuthibitisha kwamba, baba na babu za Mtume walikuwa wakimuamini Mungu mmoja.[9] Sheikh Tusi (aliaga dunia: 460 H) akitegemea nukuu ya Ibn Abbas anasema: Makusudio ya Aya ni kuhamisishwa Mtume kutoka katika Sulb (maji yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu) za baba na mababu watoharifu na wasafi mpaka atakapozaliwa.[10] Fadhl bin Hassan Tabarsi (alifariki: 548 H) pia amesema katika tafsiri yake ya Majmaa al-Bayan kwamba: Sajidun (wenye kusujudu) ni sifa ya baba za Mtume (s.a.w.w).[11]
  • Dua ya Nabii Inrahim katika Aya ya 128 katika Surat al-Baqarah: Ibrahim aliomba dua watoto wake wawee Waislamu (wenye kusilimu kwa Mwenyezi Mungu na katika Aya ya 30 ya Surat Zukhruf, dua hii imetambuliwa kuwa imejibiwa. Baba za Mtume wote wanatokana na kizazi cha Ibrahim na Mtume (s.a.w.w) ametambuliwa kuwa ni misdaq (kielelezo) ya Aya hii.[12]

Hadithi Zinazothibitisha Kwamba Mababu za Mtume Walikuwa Wakimuamini Mwenyezi Mungu

Mwandishi wa makala ya «Imani wa Mababu wa Mtume» amezigawa hadithi zinazohusiana na maudhui katika makundi matano:

  • Hadithi ambazo zinabainishwa wazi kabisa juu ya kuwa na imani ya Mungu mmoja baadhi ya mababu za Mtume.
  • Hadithi ambazo zinasema kuwa, Mtume ametoka katika sulb (maji yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu) na matumbo na mafuko ya uzazi yaliyo masafi na toharifu.
  • Hadithi ambazo zinasema, Mtume amewekwa katika kundi na familia bora kabisa.
  • Hadithi ambazo zinamtambua Mtume (s.a.w.w) kwamba, daima yupo katika maji yatokayo katika mifupa ya mgongo na mbavu za Manabii.
  • Hadithi ambazo zinabainisha wazi na bayana kabisa kwamba, maji yatokayo katika mifupa ya mgongo na mbavu aliotokea Mtume yameharamishiwa moto wa jahanamu.[13] Kwa mfano imekuja katika kitabu cha al-Kafi kwamba, ni haramu kuingizwa motoni mgongo na tumbo lililomzaa Mtume na kumsaidia.[14] Kadhalika imenukuliwa kutoka kwa Mtume katika kitabu cha A’mali cha Sheikh Tusi: Tone langu linatoka katika maji yatokayo katika mifupa ya mgongo na mbavu za Adam mpaka kwa babu yangu daima yalikuwa katika mafuko ya uzazi toharifu na katu uchafu wa kijahilia haukuniingia na kunichafua.[15] Hadithi za namna hii zimekuliwa pia katika vyanzo vya Ahlu-Sunna.[16]

Kukubali Wito wa Manabii kwa Kuzingatia Wazee wao Kumpwekekesha Mwenyezi Mungu

Kwa mujibu wa Abul Fattuh Razi, mmoja wa wafasiri wa Kishia ni kwamba, kiakili, mababuwote wa Mitume walikuwa wakimpwekesha Mwenyezi Mungu; kwa sababu Mitume ni lazima wajiepushe na mambo ambayo yanawafanya watu wawachukie wao na da’awa (ulinganiaji) yao, la sivyo kuwepo kwa haya kunasababisha watu wasikubali miito yao.[17] na kujibu ulinganiaji wa Mitume, waseme: Baba zenu pia walikuwa washirikina.[18] Pia Mwenyezi Mungu amewaita washirikina kuwa ni najisi; kwa hiyo, kwa mtazamo wa kiakili, yule aliyetuma kusafisha maovu hatakiwi kuzaliwa mchafu.[19]

Kutilia Shaka Imani ya Wazazi Mtume kwa Kutegemea Tukio la Azar na Hadithi

Fakhr Razi (aliyefariki: 606 H), mmoja wa wanateolojia wa madhehebu ya Ash’ari, yeye hakubali na mtazamo wa kwamba, mababu wote wa Mtume walikuwa wakimuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na anaichukulia imani hiyo kuwa ni ya Kishia.[20] Ibn Taymiyyah (aliyekufa: 728 H), kiongozi wa Usalafi, pia anamchukulia baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni kafiri katika kitabu chake Al-Maj’ma al-Fatawi.[21]Rashidridha (aliyefariki: 1935) pia anaamini kwamba, imani juu ya utakaso na utoharifu wa baba za Mitume ni kinyume na muonekano wa kidhahiri wa Qur'an na hadithi sahihi.[22] Akitegemea hadithi ambazo madhumuni yake ni kwamba babake Mtume alikuwa kafiri na ni mtu wa motoni, anasema kwamba inawezekana mababa wa Mitume walikuwa ni washirikina.[23] Wapinzani wa itikadi ya kwamba, mababu wa Mtume walikuwa wakimuani Mwenyezi Mungu na kumpwekesha kadhalika wanaamini kuwa, kwa kuzingatia kwamba, Azar, baba yake Nabii Ibrahim, alikuwa muabudu masanamu, basi mababu wote wa Mtume (s.a.w.w) hawakuwa watu wa tawhidi.[24]

Katika upande wa pili, wale wanaoamini kwamba, baba za Mitume walikuwa watu wa tawhidi, hawamtambua Azar kuwa ni baba yake Ibrahim, bali wanaamini kwamba, alikuwa ni mlezi wake au ami yake.[25] Kwa mujibu wa Allama Tabatabai (aliyefariki: 1402 H), mwandishi wa Tafsir al–Mizan: Babake Ibrahim alikuwa mtu mwingine ghairi ya Azar; kwa sababu akiwa katika uzee Ibrahim alimuombea maghufira kwa Mwenyezi Mungu baba yake.[26]

Maudhui Yanayo Fungamana

Rejea

  1. Madani Bajistani, «Iman Ajdad Rasul Khudah», uk. 162.
  2. Madani Bajistani, «Iman Ajdad Rasul Khudah», uk. 188.
  3. Madani Bajistani, «Iman Ajdad Rasul Khudah», uk. 166.
  4. Sheikh Saduq, Al-Itiqadat, 1413 AH, uk. 110.
  5. Sheikh Mufid, Tas-hih Itiqadat al-Imamiyah, 1413 AH, uk. 139.
  6. Alusi, Ruhu al-Ma'ani, 1415 AH, juz. 4, uk. 184.
  7. Allamah Hilli, Kashf al-Murad, 1422 AH, uk. 472.
  8. Qaushaji, Sharh Tajrid al-Aqaid, Manshurat Radhi, uk. 359.
  9. Fakhr Razi, Mafatih al-Ghaib, 1420 AH, juz. 24, uk. 537
  10. Sheikh Tusi, al-Tabayan, Dar Ahya al-Tarath al-Arabi, juz. 8, uk. 68.
  11. Tabarsi, Majma al-Bayan, 1415 AH, juz. 7, uk. 356.
  12. Madani Bajistani, «Imani Ajdad Rasul Khuda», uk. 170-171.
  13. Madani Bajistani, «Imani Ajdad Rasul Khuda», uk. 175-176.
  14. Kulein, Al-Kafi, 1407 AH, Juz. 21, uk. 446.
  15. Sheikh Tusi, al-Amali, 1414 AH, uk. 500, 1095 H.
  16. Tabarani, al-Mu'jam al-Kabir, 1415 AH, juz ya 11, uk. 362, Al-Halabi, Al-Sira Al-Halabiyyah, 2006 M, juz ya 1, uk. 44; Al-Haythami, Majma al-Zawaed, 1414 AH, juz. 7, uk. 86.
  17. Abulfatuh Razi, Raudh al-Janan, 1376 S, juz. 7, uk. 340.
  18. Abulfatuh Razi, Raudh al-Janan, 1376 S, juz. 7, uk. 340.
  19. Abulfatuh Razi, Raudh al-Janan, 1376 S, juz. 7, uk. 340.
  20. Tazama Fakhr Razi, Mafatih al-Ghaib, 1420 AH, juz. 13, uk. 31-34.
  21. Ibn Taymiyyah, Majmu al-Fatawa, 1416 AH, Juz. 1, uk. 144.
  22. Rashid Ridha, Al-Manar, 1990 M, juz. 7, uk. 451-454.
  23. Rashid Ridha, Al-Manar, 1990 M, juz. 7, uk. 451.
  24. Rashid Ridha, Al-Manar, 1990 M, juz. 7, uk. 449.
  25. Tabatabai, Al-Mizan, 1371 S, juz. 7, uk. 164-165
  26. Surat Ibrahim, Aya ya 41.

Vyanzo

  • Abulfatuh Razi, Hussein bin Ali, Raudh al-Janan Wa Ruh al-Jinan fi Tafsir al-Qur'an, Mhariri Yahaqi, Mohammad Jaafar Yahaqi, Buniyad pezhuhesh-haye Islami Astan Quds Radhwi, Mashhad muqaddas, 1376 S.
  • Alusi, Sayyed Mahmoud, Ruh al-Ma'ani fi Tafsir al-Qur'an al-'Adheem, Mhakiki: Ali Abd al-Bari Atiyah, Beirut, Dar al-Kitab al-Alamiya, 1415 AH.
  • Ibn Taymiyyah, Ahmad bin Abd al-Halim, Majmu al-Fatawa, Tahqiq: Abd al-Rahman bin Muhammad bin Qasim, Madina, Majma al-Mulk Fahd, 1416 AH.
  • Al-Halabi Al-Shafa'i, Ali Ibn Ibrahim, Al-Sira Al-Halabiyyah, Mhakiki: Abdullah Muhammad Al-Khalili, Beirut, Dar Al-Katb Al-Alamiya, 2006 M.
  • Rashidridha, Muhammad, Tafsir al-Manar, Misri, Al-Haiat Al-Misriyya Al-Katab, 1990 M.
  • Sheikh Saduqi, Muhammad bin Ali, Al-Itiqadat, Qom, Al-Mutamar al-Alami Li Sheikh Al-Mufid, 1413 AH.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, al-Amali, Qom, Dar al-Thaqafah, 1414 AH.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, al-Tabyan fi Tafsir al-Qur'an, Mhakiki: Ahmad Qasayr Ameli, Beirut, Dar Ahya Al-Tarath al-Arabi, Bita.
  • Tabarani, Abu al-Qasim, al-Mu'jam al-Kabir,Mhakiki: Hamdi bin Abdul Majid al-Salafi, Cairo, Maktaba Ibn Taymiyyah, 1415 AH.
  • Sheikh Mufid, Muhammad bin Muhammad, Mhariri Itiqadat Imamiyyah, Qom, Al-Mutamar al-Alami Li Sheikh Al-Mufid, 1413 AH.
  • Tabatabai, Sayyed Mohammad Hussein, Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an, Qom, Muasese Matbuati Ismailiyun, 1371 S.
  • Tabarsi, Fadhl bin Hassan, Majma al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an, Beirut, Muasese Al-Alami Lil-Matbuat, 1415 AH.
  • Allameh Hilli, Hasan bin Yusuf, Kashf al-Murad fi Sharh Tajrid al-Itiqad, Mhariri: Hasan Hassanzadeh Amoli, Qom, Al-Nashar al-Islami, Chapa ya 9, 1422 AH.
  • Fakhr Razi, Muhammad bin Omar, Mafatih al-Ghaib, Beirut, Dar Ahya al-Tarath al-Arabi, 1420 AH.
  • Qushchi, Aladdin, Sharh Tajrid Al-Aqaid, Qom, Manshurat Radhi-Bidar-Azizi, Bita.
  • Kulein, Muhammad bin Yaqub, al-Kafi, Tehran, Dar al-Kitab al-Islamiya, 1407 AH.
  • Madani Bajstani, Sayyed Mahmud, «Iman Ajdad Rasul Khuda», Miqat Hajj Quarterly, No. 44, Summer 2013.
  • Al-Haythami, Ali Ibn Abi Bakr, Majma al-Zawaed Wa Manbaa Al-Fawaed, Mhakiki: Hossam al-Din Qudsi, Cairo, Maktaba Al-Qudsi, 1414 AH.