Nenda kwa yaliyomo

Kashf al-Murad fi Sharh Tajrid al-I’tiqad (kitabu)

Kutoka wikishia
Kitabu cha Kashful- Murad fi sharh Tajrid Al- I’tiqad

Kitabu cha Kashful- Murad fi sharh Tajrid Al- I’tiqad (Kiarabu: كشف المراد في شرح تجريد الاعتقاد (كتاب)) ni miongoni mwa vitabu vya theolojia (itikadi) vya Madhehebu ya Kishia. Kitabu hiki ambacho ni athari ya Allama Hilli kimeandikwa kwa lugha ya Kkiarabu. Kitabu hiki kinatambulika kuwa ni kitabu cha kwanza kabisa na bora zaidi kilichoandikwa kufafanua kitabu cha (Tajrid al-I’tiqad) ambacho kimeandikwa na Khawaja Nasir al-Din Tusi. Kitabu cha Kashf al-Murad mwanzoni kinabainisha maudhui za kifalsafa kama vile Uwepo na Utambulisho wa mwanzo (dhati asili ya Uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu), na kisha baada ya hapo kinabainisha maudhui kuhusu misingi ya itikadi ya madhehebu ya Shia Imamiya kuanzia Tauhidi mpaka Ufufuo. Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vinavyotumika kufundishia katika vyuo vikuu vya kidini (Hawza) na kuna ufafanuzi mwingi na vitabu vingi vilivyoandikwa kwa ajili ya kufafanua kitabu hiki.

Mwandishi

Makala ya Asili: Allama Hilli

Hassan bin Yusuf bin Mutahhar Hilli (726-648 H) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Allama Hilli, ni miongoni mwa wanazuoni wa fikihi na theolojia wa karne ya nane Hijria[1]. Allama Hilli ameandika vitabu vingi vinavyohusu elimu mbali mbali, miongoni mwa vitabu hivyo ni vitabu vya fikihi, Usuli, Akida, Falsafa na Mantiki [2]. Hali kadhalika miongoni mwa vitabu alivyoandika ni Manahij Al-Yaqin fi Usuli- Din, Kashf al-Murad, Nahjul-Haq na Kashf Al- Swidq, Babu Hadi Ashar, khulasatul- Aq’wal Fi Ma’rifatil- al-Rijal na Jawahir Al-Nadhwid. Alimu huyu anazingatiwa kuwa ni mtu wa kwanza kabisa ambaye aliitwa kwa lakabu ya Ayatullah kutokana na fadhila na elimu yake ya hali ya juu aliyokuwa nayo[3]. Mijadala, midahalo na athari zake, zilimfanya Sultan Muhammad Khudabande kuwa mfuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s) (kuwa mshia). Pia midahalo na athari hizo zilipekea kuenea kwa madhehebu ya Shia ndani ya nchi ya Iran [4].

Sababu ya Kuandika (Kitabu HHiki)

Allama Hilli katika utangulizi wa kitabu chake kiitwacho Kashf al-Murad, amebainisha sababu ya kualifu na kuandika kitabu hiki kwamba ni kufafanua masuala magumu na yenye utata katika kitabu cha Tajrid al-I’tiqad ambacho ni athari ya Khawaja Nasir al-Din Tusi. Kwa mujibu wa kauli yake ni kwamba, licha ya kuwa kitabu cha Tajrid al-I’tiqad kimekusanya na kubainisha mambo mengi ya kiitikadi, lakini kimeandikwa kwa mukhatasari sana. Hilo limepelekea wanafunzi wengi watafutaji wa elimu kutokuwa na uwezo wa kufahamu maana kusudiwa ndani ya kitabu hiki.[5].

Umuhimu wa Kitabu cha Kashf al-Murad

Kashful-Murad ni miongoni mwa vitabu vya kusomeshea vyuo vikuu vya kidini, na wanazuoni wanakipa umuhimu wa aina yake kitabu hiki[6]. Wasomi mbalimbali wanasema kwamba kitabu hiki kina umuhimu na ubora kutokana na sababu mbili, kikilinganishwa na vitabu vingine vilivyotungwa kwa ajili ya kufafanua kitabu cha Tajrid al-I’tiqad: 1) Ni Kitabu cha kwanza kilichotungwa kwa ajili ya kufafanua kitabu cha Tajridul-I'tiqad. 2) Mwandishi wa kitabu hiki ni mwanafunzi wa mtunzi wa kitabu cha Tajrid al-I'tiqad. [7]

Hassan Hassanzade Amoli ambaye ni msahihishaji wa kitabu hiki anasema kwamba, Tajrid al- I’tiqad ni miongoni mwa kiini cha vitabu vya theolojia na cha mwanzo miongoni mwa vitabu hivyo. Na Kashful- Murad ni kitabu cha kwanza bora kilichoandikwa kufafanua kitabu hicho cha Tajrid al-Itiqad. [8] Na yeye amenukuu kutoka kwa Fadhil Kushchi kwamba: Kama kitabu cha Kashful-Murad kisingekuwepo, (basi) kitabu cha Tajridul-Itiqad kisinge fahamika ipasavyo. Naye Agha BozorgTehrani mwandishi wa kitabu cha Al-Dhariah amenukuu kutoka kwa Shamsu-Din Isfahani mmoja wa wafafanuzi wa tajridul- I’tiqad na kuandika ya kwamba: Kama kitabu cha Kashful-Murad kisingelikuwepo, hakuna mtu ambaye angeliweza kufafanua kitabu cha Tajrid al-I’tiqad.

Muundo na Yaliyomo Ndani ya Kitabu

Kitabu cha Kashful-Murad, kimejadili na kuelezea maudhui ya Kifalsafa tu, kama vile Uwepo na Kutokuwepo ( Uju’d na Adam) na Dhati ya Uju’d, na kinazungumzia pia maudhui ya kitheolojia na kiitikadi kuanzia Tauhid mpaka Ufufuo. Kitabu hiki kimetungwa kikiwa na vipengele sita, ambapo kila kipengele kimepewa jina kwa makusudio ya maudhui maalumu. Baadhi ya vipengele vimekusanya milango kadhaa na chini ya kila mlango kumetajwa mas'ala tofauti:

  1. Mambo jumla: Mlango huu umekusanya maudhui tatu: Ujud wa Adam (Uwepo na Kutokuwepo), Mahiyyat (Dhati) na yanayohusiana, Ella wa Ma’lul ( Sababu na kisababishwa).
  2. Kuthibitisha Muumbaji: Maudhui hii ina vipengele vitatu: Ujud au Uwepo wa Muumba, Sifa za Muumba, Vitendo au matendo ya Muumba.
  3. Utume: Katika kipengele hiki kumezungumziwa masuala saba; miongoni mwa hayo ni: Udharura wa kubaathiwa, udharura wa umaasumu (kwa Mitume wa Allah) , njia ya kujua ukweli wa Mtume na Utume wa Bwana Mtume Muhammad (a.s.w.w).
  4. Uimamu: Katika kipengele hiki kumezungumziwa masuala tisa;
  5. mfano! Wajibu wa kuteuliwa Imam (wa kila zama), udharura wa Umaasumu kwa Imam, udharura wa Imam kuwa mbora zaidi ya wote, udharura wa kuwepo Nass (andiko/hoja nakili) inayothibitisha kwamba Imam ameteuliwa, kustahiki Uimamu Ali (a.s) mara tu baada ya kuaga dunia Mtume Muhammad (a.s.w.w), ubora wa Imam Ali (a.s) juu ya maswahaba wote na Uimamu wa Maimamu wote kumi na mbili.
  6. Ufufuo na Kiyama: Kipengele hiki kinajumuisha masuala sita ambayo baadhi ya hayo ni: Uwezekano wa (kuwepo) Akhera, Kiyama na Ufufuo (kimwili na kiroho), kubatilika (kwa thawabu za matendo mema kutokana na athari ya madhambi) na baadhi ya Waislamu kukufurisha Waislamu wengine, shafaa na uombezi, toba na adhabu ya kaburi [11].

Ufafanuzi, Maelezo na Tarjuma

Kwa mapokezi ya kitabu cha utambuzi wa kitabu kuhusu Tajrid al-I‘tiqad ni kwamba, kumeandikwa ufafanuzi na maelezo mengi kuhusiana na kitabu cha Kashful-Murad. Miongoni mwa ufafanuzi huo ni kama ifuatavyo:

  • Hashiya Sayyied Abul-Qasim bin Hussein Radhwawi Qomi Ha'iri Lahuri Naqawi (aliyefariki 1324 H).
  • Hashiya (Maelezo ya) Mirza Abdul-Razzaq bin Ali Ridhwa Muhadith Hamadani (aliyefariki 1381 H).
  • Al-Ta'liqat ala Kashfil-Murad , kilichoandikwa na Hassan Hasanzade Amoli.
  • Tawdhwihul-Murad fi sharh Kashf al-murad, kilichoandikwa na Sayyied Hashim Husseini Tehrani (aliyefariki 1412 H).
  • Hashiya (Maelezo ya) Sayyied Muhammad Hashim Rawdhwati.
  • Ta'liqa 'ala sharh al-Tajrid al-Allama kilichoandikwa na Hafiz Bashir Najafi ( aliyezaliwa 1361 H).
  • Ta'liqah 'ala Kashf al-murad fi sharh al-Tajrid, kilichoandikwa na Ibrahim Musawi Abhari Zanjani (aliyezaliwa 1344 H).
  • Tarjuma wa Sharh Kashf al-Murad kwa lugha ya Kifars, kilichoandikwa na Abul-Hassan Sha'rani (aliyezaliwa 1393 H).
  • Sharh Kashf al-Murad kilichoandikwa kwa lugha ya kifarsi na Ali Muhammadi (aliyezaliwa 1377 H)[12].

Nakala na Usambazaji

Kitabu cha Kashful-Murad kina nakala kadhaa zilizoandikwa kwa mkono ambazo baadhi ya hizo ziliandikwa wakati wa uhai wake mwenyewe Allama Hilli na zingine ziliandikwa muda kidogo baada ya kufariki na kuaga kwake dunia[13]. Miongoni mwa hizo, kuna chapa na toleo la mwaka 713 H, ambacho kiliandikwa katika zama za uhai wake.[14] Halikadhalika kuna chapa iliyoandikwa mwaka 754 H, na mwandishi wa kitabu hicho akamsomea Fakhrul-Muhaqiqin ambaye ni mtoto wa Allama Hilli.[15] Hakika nakala ya kitabu hiki ingali inahifadhiwa katika maktaba ya Haram ya Imam Ridha (a.s) [16].

Halikadhalika kitabu cha Kashful-Murad kimechapishwa nchini Iran, Lebanon na India pia[17]. Miongoni mwa matoleo ni yale yaliyosambazwa na Jami’at- Mudarrisin ya Hawza Qom kilichopo katika mji wa Qom mnamo mwa 1407 H. Kitabu hiki kilifanyiwa masahihisho na kuongezewa nukta na maelezo na Ayatullah Hassan Hassanzade Amoli na kusambazwa kikiwa na kurasa 646.[18]

Rejea

Vyanzo

  • Afandī Iṣfahānī, ʿAbd Allāh. Riyāḍ al-ʿulamāʾ wa ḥiyāḍ al-fuḍalāʾ. Edited by Aḥmad Ḥusaynī Ashkwarī. Qom: Khayyām, 1401 AH.
  • Āqā Buzurg al-Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-shīʿa. Edited by ʿAlī Naqī Munzawī and Aḥmad Munzawī. Beirut: 1403 AH.
  • Khāligīyān, Faḍl Allāh. Az ʿAllāma Ḥillī tā Abu l-Ḥassan Shaʿrānī; muqāyasa-i bayn-i shurūḥ-i tajrīd al-iʿtiqād. Rushd-i āmūzish-i maʿārif-i Islāmī 76 (1389).
  • Khāwnsārī, Muḥammad Bāqir. Rawḍāt al-jannāt fī aḥwāl al-ʿulamā wa al-sādāt. Qom: Ismāʿīlīyān, 1390.
  • Ṣadrāyī Khoeī wa Marʿashī Najafī, ʿAlī wa Sayyid Maḥmūd. Kitābshināsī tajrīd al-iʿtiqād. 1st dition. Qom: Kitābkhāna-yi Ayatullāh Marʿashī Najafī, 1382 Sh.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Kashf al-murād fī sharḥ tajrīd al-iʿtiqād. Edited by Ḥasan Ḥasanzāda Āmulī. 7th edition. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1417 AH.
  • Mulawī, Muḥammad ʿAlī. Ayatullāh. Dāʾirat al-maʿārif-i buzurg-i Islāmī. Tehran: Markaz-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Buzurg-i Islāmī, 1374 Sh.