Ayyub bin Nuh bin Darraj al-Nakhai al-Kufi

Kutoka wikishia

Ayyub bin Nuh bin Darraj al-Nakhai al-Kufi (Kiarabu: أّيُّوب بن نُوح بن دَرَّاج النخعي الكوفي) Ni faqihi na mwanahadithi wa upande wa madhehebu ya Shia Ithnaasharia wa karne ya tatu Hijiria. Yeye ni mpoze wa Hadithi aliyepokea Hadithi zake kutoka kwa Imamu Ali Ridha (a.s), Imamu Muhammad Taqi (a.s), Imamu Ali Naqi (a.s), na Imamu Hassan al-Askari (a.s). Ayyub alikuwa ni wakala wa Imamu Ali Naqi (a.s) na Imamu Hassan al-Askari (a.s), naye alikuwa na hadhi maalum mbele ya Maimamu wawili hawa. Watambuzi wa nasaba za wapokezi wa Hadithi wamemuelezea yeye kuwa ni mtu mcha Mungu na mwenye hadhari kubwa katika matendo yake. Baba yake, ambaye ni Nuh bin Darraj, alikuwa ni miongoni mwa masahaba wa Imamu Sadiq (a.s) na Imamu Musa al-Kadhim (a.s), na pia alikuwa ni qadhi wa mji wa Kufa ulioko nchini Iraq. Aidha, inasemekana kwamba Jamil bin Darraj, ambaye ni ami wa Ayyub, alikuwa ni mtu tegemezi na ni wakala, pia ni mmoja wa masahaba wa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s).

Nafasi Yake katika Nasaba za Wapokezi wa Hadithi

Ayyub bin Nuh bin Darraj al-Nakhai al-Kufi, faqihi na mwanahadithi wa madhebu ya Shia Imamiyyah, alizaliwa mjini Kufa katika nchi ya Iraq na maarufu wake ulikuwa ni Abu al-Hussein. [1] Kulingana na wanahistoria wa Shi'a, Ayyub bin Nuh alikuwa ni miongoni mwa masahaba wa Maimamu wanne ambao ni: Imamu Ali Ridha (a.s), Imamu Muhammad Taqi (a.s), Imamu Ali Naqi (a.s), na Imamu Hassan al-Askari (a.s), na Hadithi alikuwa akizipokea kutoka kwa Maimamu wanne hao. [2] Najashi na Kashshi wamemuelezea na kumsifu kwa sifa za aminifu, wakala, na mwenye hadhi maalum mbele ya Imamu Ali Naqi (a.s) na Imamu Hassan al-Askari (a.s). [3] Aidha, kuna rikodi za maandiko maalumu waliokuwa wakiandikiana baina yake na Imamu Ali Naqi (a.s) yaliyorekodiwa. [4] Kulingana na maelezo ya Najashi, ni kwamba; Ahmad bin Muhammad Barqi amesema kuwa kitabu Nawadir ni kazi andishi ya Ayyub bin Nuh. [5] Ayyub amenukuu Hadithi zenye miktadha ya madhui mbali mbali, ikiwa ni pamoja na Hadithi zinazozungumzia thawabu za kuwatembelea Maimamu watukufu. Pia Ayyub bin Nuh amenukuu Hadithi mbali mbali zinzohusiana na masuala ya fiq’hi, kama vile tohara, talaka, sala, ndoa, pamoja na urithi. [6] Kwa mujibu wa maelezo ya Ayatullahi Khui (aliyefariki mwaka 1371 Shamsia), ni kwamba; jina la Ayyub linapatikana ndani ya hadithi 251 akiwa ni miongoni mwa wapokezi wa Hadithi hizo. [7] Najashi, Kashshi, Tusi, na Barqi wote wanamwona yeye kuwa ni mtu mwaminifu asiye na dosari. [8]

Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Hassan al-Askari (a.s), Ayyub imetambuliwa kama ni mmoja wa Peponi. [9] Pia, Najashi amesema kwamba Ayyub bin Nuh alikuwa mtu mcha Mungu mwenye na mwenye hadhari kubwa juu ya matendo maovu. [10]

Mashekh wa Ayyub bin Nuh

Ayyub bin Nuh amepokea Hadithi zake kutoka kwa mashekh (wanazuoni) wafuatao:

Hadithi

Baadhi ya wapokezi ambao wamepokea hadithi kutoka kwa Ayyub bin Nuh ni kama ifuatavyo:

Ukoo wa Ayyub bin Nuh

Familia ya Ayyub bin Nuh ilikuwa ikiishi mjini Kufa nchini Iraq, na ilikuwa na uhusiano wa karibu na kabila la Nakha’i, kiasi ya kwamba hata familia yao wao pia nayo ilijulikana kwa jina la al-Nakha’i au Mawla al-Nakha’I (wafungamanifu wa kabila la al-Nakha’i). [Maelezo 1] [13] Wanahistoria wenye kutafti nasaba za wapokezi wa hadithi za Shi’a wamesema kwamba; baba yake, ambaye ni Nuh bin Darraj, alikuwa qadhi maarufu wa mji wa Kufa ulioko nchini Iraq. Na alikuwa ni miongoni mwa masahaba wa Imamu Swadiq (a.s) na Imamu Musa al-Kadhim (a.s), pia alikuwa akifahamika kwa kuwa na imani thabiti na uimara wa kimadhehebu (yaani alikuwa Shia Ithnaashariyya). [14] Kaburi la Nuh bin Darraj linapatikana karibu na mava ya Karbala, katikati ya mashamba ya mitende kwenye ardhi inayomilikiwa na kabila la Aalu-Mas'ud. [15] Pia, Jamil bin Darraj ambaye ni ami yake, alikuwa ni mashuhuri, naye alijulikana kwa uthabiti wa imani, ambaye pia alikuwa ni wakala na ni miongoni mwa masahaba wa Imam Ja'far al-Sadiq (a.s). [16] Kwa mujibu wa maelezo ya Ali Namazi Shahrudi, aliyelifariki mwaka 1364 Shamsia, katika kitabu chake Mustadrakat ‘Ilmu al-Rijal al-Hadith, ni kwamba; watoto wa Ayyub bin Nuh, yaani Hasan na Muhammad, pamoja na mjukuu wake Ahmad bin Qasim bin Ayyub, walikuwa ni miongoni mwa wapokezi wa Hadithi. [17]

Maelezo

  1. Fungamano hili hujulikana kwa jina la “Dhimanu al-Jarirah” ambalo ni aina ya mkataba wa kidini wa Kiislamu ambapo mmoja wa wahusika huchukua jukumu kutoa himaya na kulipa fidia (diyya) kwa niaba ya upande mwingine, ikiwapo upande huo utafanya jinai inayohusisha malipo ya fidia. Mkataba huu hufanyika kwa sharti la kwamba mhusika aliyekubali dhima hii huwa na haki ya kurithi kutoka kwa yule anayemlinda au aliyemlipia fidia ya jinai.

Rejea

Vyanzo