Ayat al-Kursi
Ayat al-Kursi (Kiarabu: آية الكرسي) (Surah Al-Baqarah: 255) ni mkusanyiko wa sifa za utukufu na uzuri wa Mwenyezi Mungu, ambazo zinajumuisha sifa zote mbili za dhati ya Mwenyezi Mungu, kama vile Umoja, uhai, tadibiri na usimamizi wa mambo, elimu na uwezo, na pia inajumuisha sifa za matendo yake, kama vile umiliki wa ulimwengu na maombezi. Kutokana na Aya hii kuwa na ibara ya : (وَسِعَ کُرسِیُّهُ السَّمواتِ و الارضَ ; Elimu yake imeenea mbingu na ardhi), imeondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Ayat al-Kursi. Baadhi ya Aya za 256 na 257 za Surat al-Baqarah nazo zimetambuliwa kuwa miongoni mwa Ayat al-Kursi; hata hivyo baadhi ya wengine wanasema, kwa kuzingatia hadithi na ushahidi tofauti, Ayat al-Kursi ni Aya ya 255 tu ya Surat al-Baqara.
Jina la Aya | Ayat al-kursi |
---|---|
Sura Husika | Baqara |
Namba ya Aya | 255 |
Juzuu | 3 |
Sababu ya Kushuka | Haina |
Mahali pa Kushuka | Madina |
Maudhui | Itikadi |
Mada Yake | Tawhidi, Majina na Sifa za Mungu |
Mengineyo | Aya Kubwa Kabisa katika Qur'ani |
Aya Zinazofungamana Nayo | 256 na 257 Surat Baqara |
Katika vyanzo vya hadithi, zimetajwa sifa maalumu na fadhila nyingi kwa ajili ya Aya hii, zikiwemo zilizonukuliwa katika baadhi ya hadithi ya kwamba, Aya hii inachukuliwa kuwa Aya bora zaidi ya Qur'ani. Inashauriwa kusoma Aya hii daima na katika hali zote, hasa baada ya Sala, baada ya kutia udhu, kabla ya kulala, wakati wa kuondoka nyumbani, wakati wa kukabiliana na hatari na shida, nk. Usomaji wa Aya hii umejumuishwa katika baadhi ya Sala za Sunna kama vile Sala ya usiku ya kwanza kaburini.
Andiko na Tarjumi
Aya ya 255 ya surat al-Baqara kutokana na kuwa na neno al-Kursi iimepewa jina la Ayat al-Kursi. [1] Inaelezwa kuwa, mwanzoni mwa Uislamu na katika zama za Bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) pia, Aya hii ilikuwa mashuhuri kwa jina la Ayat al-Kursi. [2]
Aya yenyewe:
اَللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾ لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾ اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu. Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu.
(Quran: 2: 255-257)
Ni Ayat al-al-Kursi au Ayaat al-Kursi
Lililo mashuhuri baina ya wafasiri wa Kishia ni kwamba, Ayat al-Kursi ni Aya ya 255 tu katika Surat al-Baqara [3] na Aya mbili zinazofuata si katika Aya al-Kursi. [4] Kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Hussein Tehrani ni kuwa, Allama Tabatabai mwandishi wa tafsiri ya Qur’ani ya al-Mizani anaamini kwamba, Ayat al-Kursi ni Aya ya 255 ya Surat al-Baqara na kwamba, inaishia na : (وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ; Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu). [5] Makarim Shirazi mmoja wa wafasiri wa Kishia ametoa ushahidi sita kuhusiana na kuwa, Ayat al-Kursi ni makhsusi kwa Aya ya 255 katika Surat al-Baqara; na miongozi mwa ushahidi huo ni:
- Hadithi zote zilizonukuliwa kuhusiana na fadhila na ubora wa Aya hii zimeitaja Aya hii tu ( ya 255) kuwa ndio Ayat al-Kursi;
- Neno Kursi limekuja tu katika Aya ya 255;
- Imekuja katika baadhi ya hadithi kwamba, Ayat al-Kursi ina maneno 50. [6] Kwa mtazamo wake ni kuwa, hadithi ambazo zinatoa agizo la kusoma Aya mbili zinazofuata, hakujatajwa anuani ya Ayat al-Kursi ndani yake. [7]
Mkabala na nadharia na mtazamo huo mashuhuri, kuna baadhi ambao wakitegemea baadhi ya hadithi wamezitambua aya za 256 na 257 katika Surat al-Baqara kuwa nazo ni sehemu ya ayuat al-Kusri. [9] Hadithi hizo zimetambuliwa kuwa sababu ya kuwa mashuhuri kuunganishwa na Ayat al-Kursi Aya mbili zinazofuata miongoni mwa Mashia. [10] Miongoni mwa hoja zingine za kuunganishwa na Ayat al-Kursi Aya za 256 na 257 za Surat al-Baqara ni mfungamano mkubwa na wa kina wa madhumuni yaliyopo katika Ayat al-Kursi na Aya mbili zinazofuata. [11] Sayyid Muhammad Kadhim Tabatabai Yazdi anasema katika kitabu chake cha al-Ur’wat al-Wuthqa kwamba, kusoma mpaka mwishoni mwa Aya ya 257 yaani mpaka «هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ» katika Sala ya usiku wa kwanza kaburini ni kwa mujibu wa ihtiyat (tahadhari). [12]
Neno al-Kursi
Neno al-Kursi limeelezwa kuwa lina maana kadhaa:
- Kitanda
- Mamlaka ya utawala na usimamizi wa mambo (tadibiri)
- Makao ya uongozi na mamalaka na usimamizi wa mambo
- Imeelezwa kuwa, makusudio ya Kursi katika Ayat al-Kursi ni utawala, mamlaka, satwa na tadibiri ya Mwenyezi Mungu. [14]
Katika hadithi mbalimbali zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu (a.s) Kursi imefasiriwa kwa maana ya elimu ya Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ni kuwa: Kursi ni elimu makhsusi ya Mwenyezi Mungu ambayo hakumfahamisha Mtume yeyote miongoni mwa Mitume na wajumbe wake. [16]
Maudhui Yake
Ayat al-Kursi (Surah Al-Baqarah: 255) ni majimui na mkusanyiko wa sifa za utukufu na uzuri wa Mwenyezi Mungu na kwamba, ndani ya aya hii kumezungumziwa jina la Mwenyezi Mungu na sifa zake mara 16 na ni kutokana na sababu hii Aya hii inaitwa kuwa nara na ujumbe wa Tawhidi. [18] Ayat al-Kursi inajumuisha pia sifa za dhati ya Mwenyezi Mungu, kama vile umoja, uhai, tadibiri na usimamizi wa mambo (mamlaka), elimu na uwezo, na pia inajumuisha sifa za matendo yake, kama vile umiliki wa ulimwengu na maombezi. [19]
Wafasiri wa Qur’ani wameandika chini ya Aya hii masuala mbalimbali kuhusiana na uhai wa Mwenyezi Mungu hasa kuhusiana na al-Hayy, al-Qayyum na al-Kursi, mfungamano na utegemezi wa ulimwengu wote kwa Mwenyezi Mungu na makusudio ya Kursi na arshi ya Mwenyezi Mungu. [20]
Fadhila na Sifa Maalumu
SAyyid MUhammad Hussein Tabatabai, katika Tafsir al-Mizan, amezingatia adhama ya Ayat al-Kursi kwamba, ni kwa sababu inajumuisha mafundisho ya kina kuhusu tauhidi safi na mamlaka na usimamizi kamili wa Mwenyezi Mungu. [21]
Kuhusiana na fadhila ya Ayat al-Kursi, Mtume (s.a.w.w) amesema kwamba: Ayat al-Kursi ni ni bwana na kiongozi wa Aya na bora miongoni mwazo na ina kila kheri ya dunia na akhera. [22] Katika riwaya nyingine imepokewa kuwa ni kiongozi wa maneno ni Qur’ani, na kiongozi wa Qur’an ni Sura Al-Baqarah, na kiongozi wa Sura Al-Baqarah ni Aya Al-Kursi. [23]
Aya hii imekuwa ikitukuzwa mno miongoni mwa Waislamu na sababu yake ni kwamba, ina maarifa yote na mafundisho ya Uislamu kwa mujibu wa Tawhidi. Katika ayat al-Kursi Tawhidi imebainishwa kwa kwa sura jumla na mukhtasari.
Kuhusu sifa za kusoma Ayat al-Kursi, riwaya nyingi zimenukuliwa kwa upande wa Shia [25] na Sunni [26]. Imepokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) kwamba yeyote atakayeisoma Aya hii mara moja, Mwenyezi Mungu atamwondolea mabalaa na masaibu elfu moja duniani, ambayo mepesi yake ni umasikini, na mambo magumu elfu moja huko Akhera, ambalo rahisi kuliko yote ni adhabu ya kaburi. [27]
Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s), ikiwa mtu atasoma Ayat al-Kursi wakati ana maumivu ya macho na ana moyoni mwake ana nia kwamba atapona, Mungu akipenda, atapona. [28] Katika imani ya umma, wakati mwingine wakati wa kusoma aya Al-Kursi watu huweka mikono yao juu ya macho yao, kwa hakika kitendo hiki hakina hoja na ushahidi; lakini Kaf’ami amenukuu kisa katika kuunga mkono kitendo hiki katika kitabu cha Junnah al-Aman -e al-Waqiyyah kutoka Sayyid Ibn Tawoos [29]
Wakati wa Kuisoma
Kwa mujibu wa hadithi, [30] imependekezwa na kukokotezwa kusoma Ayat al-Kursi wakati wowote, hasa baada ya kuswali, kabla ya kulala, wakati wa kuondoka nyumbani, wakati wa kukabiliana na hatari na shida, wakati wa kupanda kipando, ili kuzuia kijicho, kwa ajili ya afya na kadhalika. [31] Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwamba kama ukiijua Aya hii ni nini au kilichomo ndani yake, hutaiacha kwa hali yoyote. [32] Mafakihi pia wanasema ni mustahabu kusoma Ayat al-Kursi katika hali kama vile baada ya kutia udhu, juu ya anayekata roho, baada ya Sala za faradhi, wakati wa kulala, wakati wa safari na kadhalika.[33] Imekuja pia kuhusu kusoma Aya hii katika baadhi ya Sala za Sunna kama vile Swala ya Ghadir na Sala ya usiku wa kwanza kaburini (Salat al-Wahsh). [34]
Bibliografia
Maulamaa wengi wameandika kwa sura ya kujitegemea kuhusiana na tafsiri ya Aya hii; miongoni mwao ni: Abdul-Razaq al-Kashani, Shamsuddin al-Khafri na Mulla Sadra chini ya anuani ya Tafsir Ayat al-Kursi. Kadhalika Muhammad Taqi falsafi ameandika kitabu kiitwacho "Ayat al-Kursi", Payam Aseman Tawhed (Ayat al-Kursi, ujumbe wa mbinguni wa Tawhidi).
Rejea
Vyanzo
{[End}}