Nenda kwa yaliyomo

Mwislamu

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Amesilimu)
Picha ya Qur'ani, kitabu kitukufu cha Waislamu

Mwislamu (Kiarabu: المسلم) ni mtu ambaye anaamini mafundisho ya dini ya Uislamu na anayafanyia kazi mafundisho hayo. Kwa mtazamo wa mafakihi wa Kishia ni kwamba, mtu anapotamka shahada mbili, basi huthibiti uislamu wake na kwa msingi huo huthibiti kwake hukumu kama kuwa tohara mwili wake, kuheshimiwa mali, roho na heshima yake na kusihi ibada. Kuwa na itikadi na tawhidi, utume na ufufuo (marejeo siku ya kiyama) ni katika itikadi ambazo Waislamu wote wanashirikiana (madhehebu zote zina imani na mambo haya matatu) na Sala, Saumu na Hija ni baadhi ya amali za kiibada ambazo waislamu wanashirikiana. Kwa maana kwamba, waislamu wote itikadi yao ni moja kuhusiana na haya. Wanahistoria wanasema kuwa, Imam Ali ibn Abi Twalib (a.s) na mke wa Mtume Bibi Khadija binti Khuwailidi (a.s) ndio waliokuwa waislamu wa kwanza.

Kituo cha utafiti cha Pew (Pew Research Center) cha Marekani kinasema, hadi kufikia mwaka 2015 idadi ya Waislamu duniani ilikuwa 1,752,620,000 (bilioni 1 milioni 752 na laki sita na elfu ishirini) na Uislamu ulitambuliwa kuwa dini ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani baada ya Ukristo. Kwa mujibu wa tathmini ya kituo hicho cha utafiti, karibu theluthi tatu (62%) ya Waislamu duniani wanaishi katika eneo la Asia na Oceania. Kuwa Muislamu inatumika pia kwa maana ya kusalimu amri mbele ya amri ya Mwenyezi Mungu. Neno Mwislamu (مُسلِم) na yaliyonyambuliwa kutokana nalo, limetumika zaidi katika Qur'an kwa maana ya kusalimu amri mbele ya amri za Mwenyezi Mungu.

Nafasi na Historia

Dini ya Uislamu ilidhihiri mwaka 610 Miladia katika mji wa Makka ulioko katika Peninsula ya Arabia kwa kubaathiwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wafuasi wa dini hiyo wakafahamika kwa jina la Waislamu.[1] Imekuja katika historia ya kwamba, Imam Ali ibn Abi Twalib (a.s) ambaye ni Imamu wa kwanza wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na mke wa Mtume Bibi Khadija binti Khuwailidi (a.s) ndio waliokuwa watu wa kwanza kuiamini dini ya Kiislamu.[2] Ibn Hisham amesema katika kitabu chake cha al-Sirat al-Nabawiyah ya kwamba: Baada ya Imam Ali bin Avi Talib (a.s) na Bibi Khadija (a.s), waliofuata katika kuamini Uislamu na kuingia katika dini hii walikuwa, Zayd ibn Haritha, Abu Bakr ibn Quhafa, Othman ibn Affan, Sa'd ibn Abi Waqqas, Zubayr ibn Awwam, Abdul-Rahman ibn Awf na Twalha ibn Ubaydullah.[3]

Neno Mwislamu au Uislamu limetumika katika baadhi ya hadithi za kifikihi[4] hususan katika milango ya fikihi kama tohara, sala, zaka, swaumu, hija, jihad, biashara, uwakala, wosia, ndoa, kuwinda, kuchinja, kuhuisha wafu, hudud (adhabu zisizo za kimali) na kisasi.[5]

Leksikolojia (Elimu Msamiati)

Muislamu ni mtu au watu ambao wana imani na mafundisho ya dini ya uislamu na wanayafanyia kazi mafundisho hayo.[6] Baadhi pia wamemtambua mtu kuwa ni Mwislamu baada tu ya kuingia kwake katika Uislamu na kusalimu amri mbele ya Mtume Muuhammad (s.a.w.w).[7]

Neno Mwislamu pamoja na mnyambuliko wake limekuja zaidi ya mara 40 katika Qur'an na lina maana mbili, jumla na makhsusi.[8] Neno muislamu katika Aya nyingi za Qur'an tukufu imetumika kwa maana jumla na upana wa neno na huambiwa mtu ambaye amesalimu amri mbele ya amri ya Mwenyezi Mungu na ambaye ana tawhidi kamili ambayo ndani yake haina aina yoyote ile ya shirki na kuabudu masanamu.[9] Ama katika maana makhsusi huitwa mtu ambaye ni mfuasi na mwenye imani na dini ya Mtume Muhammad(s.a.w.w).[10]

Tofauti ya Muislamu na Muumini

Mafakihi na wanazuoni wametofautisha baina ya muislamu na muumini wakitegemea baadhi ya Aya[11] na hadithi[12]; kwa maana hii kwamba, muumini katika maana jumla huitwa mtu ambaye amesadikisha, amekiri kwa moyo na kukubali kila ambacho kimeletwa na Mtume (s.a.w.w) na kutamka hilo kwa ulimi;[13] hii ni katika hali ambayo, kuwa muislamu kunathibiti kwa kutamka tu kwa ulimi shahada mbili.[14] Muumini katika maana makhsusi kwa mujibu wa mafakihi wa kishia huitwa mtu ambaye ana itikadi na imani juu ya uimamu na uongozi wa maimamu wa waislamu wa madhehebu ya kishia(a.s).[15]

Sifa Maalumu za Muislamu katika Hadithi

Katika baadhi ya hadithi ambazo zina muelekeo na utendaji wa kimaadili, kumetajwa sifa maalumu za muislamu wa kweli.[16] Kwa mfano imekuja katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ikibainisha muislamu wa kweli: muislamu wa kweli ni yule ambaye watu wanasalimika kwa ulimi na mikono yake.[17] Imam Ali ibn Abi Twalib (a.s) amenukuliwa katika hadithi moja akitaja sifa maalumu za muislamu wa kweli kwamba ni: Kutumia akili (kuwa na busara), kulinda heshima, kusema kweli, kusoma Qur'an kwa mazingatio, kufanya urafiki na uadui katika njia ya Mwenyezi Mungu, kutambua uongozi wa Ahlul-Beiti (a.s), kuchunga haki za wengine na kuwa na ujirani mwema na watu.[18]

Misingi ya Kiitikadi

Makala asili: Misingi ya dini

Baadhi ya misingi ya kiitikadi ambayo Waislamu wote wanashirikiana ni:

  • Tawhidi: Msingi mkuu kabisa wa mafundisho ya kiitikadi ya waislamu ni Tawhidi.[19] Waislamu wote wanaamini kwamba, Mwenyezi Mungu ni mmoja, ameumba ulimwengu na hana mshirika.[20]
  • Ufufuo: Ni kuamini kwamba, kutakuweko na suala la kufufuliwa kimwili na kiroho siku ya kiyama na kurejea tena mwanadamu akiwa hai kwa ajili ya hesabu ya amali zake; ambapo watenda mema wataingizwa peponi na kunufaika na neema za kudumu na watenda maovu wataadhibiwa.[21]
  • Utume: Itikadi ya waislamu kuhusiana na utume ni: kwanza, Mtume Muhammad (s.a.w.w) ameteuliwa na kutumwa na Mwenyezi Mungu.[22] Pili, ameshushiwa kitabu cha Qur'an na Mwenyezi Mungu kwa njia ya ufunuo[23] na tatu: Yeye ni Mtume wa mwisho na baada yake hakutakuweko na Mtume mwingine.[24]

Matendo ya Kiibada

Picha ya waislamu wakiwa katika ibada tukufu ya Hija katika masjid al-haram
Makala asili: Matawi ya dini

Miongoni mwa matendo muhimu kabisa ya kiibada ambayo Waislamu wote wanashirikiana ni:

  • Saumu: Ni wajibu kwa kila muislamu kufunga waumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa muda wa mwezi mmoja. Na swaumu maana yake ni kujizuia na mambo yanayobatilisha swaumu (kama kula na kunywa n.k) kuanzia adhana ya asubuhi mpaka aadhana ya magharibi.[28]
  • Hija: Kwenda kuhiji Makka ni wajibu kwa kila muislamu mwenye uwezo na ambaye ametimiza masharti). Wajibu huu ni mara moja tu katika kipindi chote cha umri wa mtu.[29] Ibada ya Hija hufanyika kila mwaka mara moja katika mwezi wa Dhul-Hija (Mfunguo Tatu) katika mji wa Makka na waislamu wengi kutoka katika maeneo mbalimbali ya dunia na hukusanyika huko kwa ajili ya kutekeleza ibada hii muhimu.[30]

Hukumu za Kifiqh

Kwa mujibu wa mafakihi wa kishia, kuwa Mwislamu kunathibiti kwa kutamka tu kwa ulimi shahada mbili kwa Kiarabu au tarjume yake.[31] Katika sheria ya Kiislamu, mtu anapokuwa Mwislamu kuna athari ambazo huambatana na hilo na baadhi ya athari hizo ni:

  • Mwili na jasho la mwili wa Mwislamu ni tohara.[32]
  • Roho, mali na heshima yake ni vyenye kupewa hadi na heshima.[33]
  • Ni wajibu kwa muislamu kutahiriwa hata kama atakuwa mtu mzima na mzee.[34]
  • Kuwa muislamu ni sharti la kusihi ibada na matendo ambayo ndani yake ni lazima kuweko ufanyaji wake kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.[35]
  • Haisihi kwa muislamu kufunga ndoa na kafiri ambaye sio Ahlul-Kitab.[36] Haijuzu kwa mwanamke muislamu kufunga ndoa na kafiri hata akiwa ni kafiri ahlul-Kitab.[37]
  • Kafiri hana wilaya (uongozi na usimamizi) na udhibiti kwa muislamu; yaani kwa kuzingatia Qaidah Nafi’i Sabil (Kanuni ya kutofungua mlango wa kutungwa sheria ambayo itamfanya kafiri awe na udhibiti kwa muislamu), Mwenyezi Mungu hatatunga sheria yoyote ile ambayo kwa sababu yake, kuweko na njia ya udhibiti na wilaya wa kafiri kwa muislamu.[38]
  • Kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi wa kishia ni kwamba, mtu ambaye alikuwa muislamu na kisha akaiweka kando dini ya Uislamu na akasema wazi na bayana kwamba, mimi kuanzia sasa sio muislamu, au akakana dharura miongoni mwa dharura za kiislamu au akakana moja ya mambo ambayo waislamu au mashia wanaafikiana kwa kauli moja, atahesabiwa kuwa ni murtadi (ametoka katika Uislamu) na hivyo hukumu za Al-Irtidâd (Kuritadi) zinatekelezwa kwake.[39]

Maeneo Matakatifu ya Waislamu

Baadhi ya maeneo ambayo yanahesabiwa kuwa ni matakatifu kwa Waislamu ni:

  • al-Kaaba ni eneo tukufu zaidi miongoni mwa maeneo ya kidini katika ulimwengu wa Kiislamu. Al-kaaba inapatikana katika mji wa Makka na kibla cha waislamu.[40] Kadhalika Masjdul-Haram unahesabiwa kuwa ni miongoni mwa misikiti muhimu kabisa ya waislamu ambao unapatikana katika maeneo ya al-Kaaba na mazingira yake.[41]
  • Masjid al-Nabbi ni eneo jingine takatifu na la kidini kwa waislamu. Msikiti huu wa Mtume upo katika mji wa Madina huko Saudi Arabia.[42] Historia inasema kuwa, msikiti huu ulijengwa na Mtume (s.a.w.w) akishirikiana na waislamu baada ya kuwasili tu katika mji wa Madina.[43]
  • Masjid al-Aqswa ni kibla cha kwanza cha waislamu. Hili ni eneo jingine la kidini na tukufu kwa waislamu. [46] Msikiti huu unapatikana kusini mashariki mwa mji wa Baytul-Muqaddas. (Palestina).[44]
  • Ghar -e-Hira ni sehemu ya kwanza ambayo Mtume Muhammad alishushiwa wahyi. Pango hili la Hira linahesabiwa kuwa miongoni mwa maeneo matakatifu kwa waislamu.[45]

Idadi

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha Utafiti cha Pew (Pew Research Center) cha Marekani ni kwamba, hadi kufikia mwaka 2015 idadi ya waislamu duniani ilikuwa 1,752,620,000 (bilioni 1 milioni 752 na laki sita na elfu ishirini) [49] na dini ya uislamu ilitambuliwa kuwa dini ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani baada ya ukristo. [50] Kwa mujibu wa tathmini ya kituo hicho cha utafiti, karibu thetluthi tatu (62%) ya waislamu duniani wanaishi katika eneo la Asia na Oceania. [51] Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa ni kituo hicho, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwaka 2015, mataifa 10 duniani ndio yaliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya waislamu duniani. Mataifa hayo kwa mujibu wa jedwali hili hapa chini ni: [52]


Namba Nchi Idadi Asilimia kwa kila nchi
1 Indonesia 219,960,000 watu Asilimia 87/1
2 India 194,810,000 watu Asilimia 14/9
3 Pakistan 184,000,000 watu Asilimia 96/4
4 Bangladesh 144,020,000 watu Asilimia 90/6
5 Nigeria 90,020,000 watu Asilimia 50
6 Misry 83,870,000 watu Asilimia 95/1
7 Iran 77,650,000 watu Asilimia 99/5
8 Uturuki 75,460,000 watu Asilimia 98
9 Algeria 37,210,000 watu Asilimia 97/9
10 Iraq 36,200,000 watu Asilimia 99

Kadhalika kwa mujibu wa kituo hicho cha utafiti, mwaka 2017 Miladia, idadi ya waislamu nchini Marekani ilifikia takribani 3,450,000 ambayo ni sawa na takribani 1.1% ya watu wote nchini Marekani, [53] na katika bara la Ulaya idadi ya Waislamu kuanzia mwaka 2010-2016 Miladia iliongezeka na kufikia 25,800,000 kutoka 19,500,000 (kutoka 3.8% hadi 4.9%). [54]

Makundi

Makundi mawili ya waislamu wa kishia na kisuni yanahesabiwa kuwa makundi makubwa zaidi ya waislamu. Kwa mujibu wa takwimu, waislamu wa madhehebu ya shia wanaunda 10% hadi 13% huku waislamu wa kisuni wakiwa ni 87% hadi 90% ya waislamu wote duniani.[46] Kwa mujibu wa ripoti nyingine, idadi ya mashia inajumuisha (Shia Ithnaasharia, Ismailiya na Zaidiyah) na kwamba, leo ni zaidi ya milioni 300 ambayo ni sawa na 19.1 ya idadi ya waislamu wote duniani na kwamba, wanaunda takribani 4.1% ya watu wote duniani[47].

Maktaba ya Picha

Rejea

  1. Bahramian, "Islam", juz. 8, uk.395.
  2. Yaqoubi, Tarikh Al-Yaqoubi, Dar Sadir, juz. 2, uk.23.
  3. Kwa mfano, tazama: Ibn Hisham, Al-Sirah al-Nabawiyya, Dar Ihya al-Tarath al-Arabi, juz. 1, uk.262-273.
  4. Kwa mfano, tazama: Kalini, Al-Kafi, 2007, juz. 3, uk. 68-76.
  5. Muasase dairatul-maarif al-fiqh, Farhang fiqh farsi, 1385, juz. 1, uk.511.
  6. Wikis, Daneshnamee aqwamu musalman, 2003, Muqadime, uk. 2
  7. Sayyied Sharafuddin, Ayyin hamzistii musalmanan, 2014, uk.34.
  8. Tabatabai, Al-Mizan, 1393 AH, juz. 18, uk.328-329.
  9. Makarem Shirazi, Tafsir al-Nashon, 1374, juz. 2, uk.703; Mustafavi, Tahaqiq fi klemat al-Qur'an, 1368, juz. 2, uk. 294-295.
  10. Tabatabai, Al-Mizan, 1393 AH, juz. 18, uk.328-329.
  11. Surah al-Hujrat, aya ya 14.
  12. Kwa mfano tazama: Kuleini, Al-Kafi, 2007, juz. 3, uk. 68-76.
  13. Shahid Thani, Masalak al-Afham, 1423 AH, juz. 5, uk.337.
  14. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juz. 65, uk.315.
  15. Shahid Thani, Masalak al-Afham, 1423 AH, juz. 5, uk.338.
  16. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1403 AH, juz. 71, uk. 158-159; Ibn Shuba Harrani, Tohf al-Aqool, 1404 AH, uk. 196-197.
  17. Bukhari, Sahih Bukhari, 1422 AH, juz. 1, uk.11; Kuleini, Al-Kafi, 2007, juz. 3, uk.592.
  18. Ibn Shuba Harrani, Tohf al-Aqool, 1404 AH, uk. 196-197.
  19. Yahya, “Siir mas'ale tawhid dar a'lam islam ta karne haftom hijri”, uk. 196; Swafi, Tajalii tawhid dar nidham imamat, 1392 S, uk.21.
  20. Karimi, Tawhid dar az didegha ayaat va riwayaat, 1379 S, uk. 19-20.
  21. Allamah Majlisi, Haq al-yaqin, Itisharat islamiya, juz. 2, uk.369.
  22. Kwa mfano, tazama: Hilli, Kashf al-Morad, 1430 AH, uk. 485-480; Iji, Sharh al-Mawaqif, 1325 AH, juz. 8, uk. 243-244.
  23. Mutahari, Majmue a'thar, 2008, juz. 26, uk. 127.
  24. Isquii, Nubuwat, 1390, uk. 202-203.
  25. Najafi, Jawahar al-Kalam, 1362, juz. 7, uk.12.
  26. Muhaqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1409 AH, juz. 1, uk. 46.
  27. Muhaqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1409 AH, juz. 1, uk. 46.
  28. Muhaqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1409 AH, juz. 1, uk. 139
  29. Muhaqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1409 AH, juz. 1, uk. 163; Sheikh Ansari, Kitab al-Hajj, Nashr turath Sheikh al-Adhwam Ansari, uk. 6
  30. Muhaqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1409 AH, juz. 1, uk. 174
  31. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 65, uk. 315; Najafi, Jawaharlal Kalam, 1362 S, juz. 41, uk. 630.
  32. Dairatul-maarif fiqh islami, Farhang fiqh farsi, 1385 S, juz. 1, uk. 513.
  33. Muhaqiq Da'mad, Qawaid fiqh, 1406 AH, Juz. 1, uk. 213-214.
  34. Najafi, Jawahar al-Kalam, 1362, juz.31, uk. 263.
  35. Najafi, Jawahar al-Kalam, 1362, juz. 17, uk. 161.
  36. Shahid Thani, al-Rawdhwa al-Bahiya fi Sharh al-Lum'a al-damashqiyyah, 1427 AH, juz. 2, uk. 412.
  37. Najafi, Jawahar al-Kalam, 1362, juz.30, uk. 92.
  38. Husseini, Al-Anawin al-Fiqhiyyah, 1417 AH, juz. 2, uk. 350.
  39. Hashemi, Dar ba'ab takfir wal irtidad, 1400 S, uk.85.
  40. Kurdi Makki, kaabe wa masjid al-haram dar gozar tareh, 1378 S, uk. 11, utangulizi wa kitabu.
  41. Tunai, Farhang haji, 1390 S , uk.885-886.
  42. Muasase farhange honrii mash'ar, Masjid al-Nabi (s.a.w.w), Nashr mash'ar, uk. 3.
  43. Muasase farhange honrii mash'ar, Masjid al-Nabi (s.a.w.w), Nashr mash'ar, uk. 3
  44. Musa Ghosheh, Tareh majmue masjid al-aqswa, 1390 S, uk. 7.
  45. Hamidi, Tareh Urushlem, 1381 S, uk. 183.
  46. Najman Dini wazindegii umumii puyuu, Nakshe jamiyat jahan, 1393 S, uk. 11.
  47. Najman Dini wazindegii umumii puyuu, Nakshe jamiyat jahan, 1393 S, uk. 1

Vyanzo

  • Ibn Shuba Harrani, Abu Muhammad Hasan bin Ali, Tohf al-Aqool, Qom, Al-Nashar al-Islami Foundation, 1404 AH.
  • Ibn Hisham, Abd al-Malik Ibn Hisham, Al-Sirah al-Nabawiya, Beirut, Dar Ihya al-Tarath al-Arabi, Bita.
  • Chama cha Dini ya Pew na Maisha ya Umma, Ramani ya Idadi ya Watu Duniani, iliyotafsiriwa na Mahmoud Taghizadeh Davari, Qom, Sayansi ya Shia, 2014.
  • Iji, Azad al-Din, Sharh al-Maqsih, Qom, chapa ya kwanza, 1325 AH.
  • Biabani Eskoui, Mohammad, Nebubot, Tehran, Naba Publications, 1390.
  • Tonei, Mojtabi, Kamusi ya Hajj, Qom, Machapisho ya Mashoor, 1390.
  • Bahramian, Ali, "Islam", Big Islamic Encyclopaedia, Tehran, Center of Big Islamic Encyclopedia, 1381.
  • Hosseini, Seyed Mir Abdul Fattah, Al-Anawin al-Fiqhiyyah, Qom, Al-Nashar al-Islami Foundation, chapa ya pili, 1417 AH.
  • Sayyied Sharafuddin, Abdul Hossein, Dini ya Kuishi Pamoja kwa Waislamu, Qom, Nyumba ya Uchapishaji ya Habib, 2014.
  • Shahidi Thani, Zain al-Din bin Ali, al-Rawda al-Bahiya fi Sharh al-Lama' al-Damashqiya, Qom, Dar al-Tafsir, chapa ya 7, 1427 AH.
  • Shahid Thani, Zain al-Din bin Ali, Masalak al-Afham, Qom, Taasisi ya Al-Maarif al-Islamiya, 1423 AH.
  • Sheikh Ansari, Morteza, Kitab al-Hajj, Qom, Tarath al-Sheikh al-Azam Ansari, Bita.
  • Safi, Lotfollah, Udhihirisho wa Tauhidi katika Mfumo wa Uimamu, Qom, Ofisi ya Kuhariri na Uchapishaji ya Hazrat Ayatollah Mkuu Ayatollah Safi Golpayegani, 1392.
  • Tabatabaei, Mohammad Hossein, Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an, Beirut, Al-Alami Institute for Press, chapa ya tatu, 1393 AH.
  • Allamah Majlisi, Mohammad Baqer, Bihar al-Anwar, Beirut, Dar Ahya Trahat Arabi, 1403 AH.
  • Allamah Majlisi, Mohammad Baqer, Haq Al-Yekin, Qom, Islamia Publications, Beta.
  • Allamah Hali, Kashf al-Murad fi Sharh Tajrid al-Itqad, Taasisi ya Al-Nashar al-Islami, 1430 AH.
  • Kordi Makki, Mohammad Taher, Kaaba na Msikiti wa Al-Haram katika kifungu cha historia, Tehran, Mashaar Publishing House, chapa ya pili, 1378.
  • Karimi, Jafar, Tauhidi kwa mtazamo wa Aya na Hadith (2), Tehran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, 1379.
  • Kilini, Muhammad bin Yaqub, Al-Kafi, Qom, Dar Al-Hadith, chapa ya kwanza, 1387.
  • Mohaghegh Damad, Seyyed Mostafi, Jurisprudence, Islamic Sciences Publishing Center, toleo la 12, 1406 AH.
  • Mohaghegh Hali, Jafar bin Al-Hassan, Sharia' al-Islam, Tehran, Esteghlal Publications, chapa ya pili, 1409 AH.
  • Mustafavi, Hassan, Tahaqiq fi kalamat al-Qur'an, Tehran, Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu, toleo la kwanza, 1368.
  • Motahari, Morteza, mkusanyiko wa kazi, Qom, Sadra Publishing House, 2008.
  • Makarem Shirazi, Nasser, Tafsir al-Nashon, Tehran, Dar al-Katb al-Islamiya, 1374.
  • Taasisi ya Ensaiklopidia ya Kiislamu ya Fiqh, Taasisi ya Sheria ya Kiajemi, Qom, Taasisi ya Ensaiklopidia ya Kiislamu ya Fiqh, 1385.
  • Najafi, Mohammad Hassan, Javaher Al-Kalam, Beirut, Ufufuo wa Urithi wa Kiarabu, toleo la 7, 1362.
  • Weeks, Richard, Encyclopaedia of Muslim Nations, iliyotafsiriwa na Masoume Ebrahimi na Peyman Mateen, Tehran, Amir Kabir Publishing House, 2003.
  • Hashemi, Seyyed Sadra, katika suala la takfir na uasi, Tehran, Negah Masares, chapa ya kwanza, 1400.
  • Yahya, Osman bin Ismail, "Mkondo wa suala la tauhidi katika ulimwengu wa Kiislamu hadi karne ya 7 Hijria", iliyotafsiriwa na Alireza Zakavati Karagzlou, katika jarida la Maarif, namba 16 na 17, Aprili na Novemba 1368.
  • Yaqoubi, Ahmed bin Abi Yaqoob, Historia ya Eliyaqoubi, Beirut, Dar Sader, toleo la kwanza, BTA.